DOKEZO Sinza kila nyumba ni kama JALALA. Walioshinda zabuni ya kuondoa taka/uchafu ni kama wameshindwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Wakazi wa Sinza tunawaomba uongozi wa juu kuchukua hatuola stahiki kwa uongozi ulipo sasa kuanzia ngazi ya Diwani kuja hadi serikali za mitaa kwakuwa wameshindwa kusimamia zoezi la uzoaji taka majumbani kwa ukamilifu.

Tangu mwezi wa 11 mwishoni 2023 hadi leo kuna maeneo mfano Sinza c uchafu haujachikuliwa, kila nyumba ina jalala la uchafu.

Za chini kabisa zinanyetisha kuwa kuna mgongano wa kimaslahi baina ya Diwani na wenyeviti wa serikali za mitaa, zinaongeza kuwa mnufaikaji toka kwa alieshinda tenda ya kuzoa taka ni diwani hivyo wenyeviti wa serikali za mitaa wanamkwamisha mzabuni kiaina.

Mzabuni wa awali aliyekuwa anafanya vizuri ktk uondoaji wa taka kwa wakati alikuwa upande wa wenye viti wa serikali za mitaa.

Serikali tusaidieni kipindupindu muda wowote kinaweza kuamka na kugharimu maisha ya watu na Taifa kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom