Single Mother ananilazimisha kulipa ada ya mwanaye

Single Mother ananilazimisha kulipa ada ya mwanaye

Kazi yangu ni bodaboda, na nilijuana na huyu single maza kupitia kazi yangu hii, maana yeye anafanya kazi bar hivyo uwa anatoka usiku sana, basi akachukua namba yangu ikawa kila usiku anapiga simu nimfate mda wa kutoka kazinina mazoea yakaanzia hapo.

Baba mtoto wake ni dereva wa halmashauri fulani huko mkoani, na anampenda sana huyu dada, kiufupi baba mtoto anaonekana alikuwa na malengo na huyu single maza, hata kuhudumia alikuwa anahudumia kwa uwezo wake aliyojaliwa.

Sasa huyo baba mtoto baada ya kugundua mimi Nina mahusiano na huyu single maza wake, amekata mawasiliano kabisa na huyu single maza yaani hatoi hata Mia, siyo kodi, chakula wala Ada ya mtoto.

Nimejahidi kuwa nasaidia kuhusu chakula na kumchangia kodi(tukaanza kuishi wote) nasaidia pia mahitaji mengine madogo madogo, kwa bodaboda yangu nimekuwa nikimpeleka kazini na kumrudisha usiku wa manane bure kabisa,, ila mambo yamekuwa magumu ananitaka nilipe na Ada ya mtoto wake sasa.

Nimemwambia amshirikishe baba wa mtoto wake, anakataa anasema hataki msaada wowote kutoka kwa baba mtoto, kwamba ananipenda mimi kwasasa hivyo mimi ndiyoo nimsaidie hiyo hela ya Ada.

Kipato chake yeye ni 300000 kwa mwezi
Nyumba tunayokaa 100000 kwa mwezi
Dada wa kazi 50000
Mtoto wao anasoma private Ada 250000 kila robo muhula hivyo kwa mwaka milioni,
School bus 50000 kila mwezi

Hapo chakula bado na mahitaj mengine,

Kuhusu mimi kipato changu ni 15000 kwa siku nikitoa mafuta na hela ya tajiri,

Wakuuu hivi natoboa kweli hapaaaaaa

Baba wa mtoto kasusaaa kabisa
All in all, hutoboi nakwambia hutoboi...ndio kisa cha sisi wanaume kufa mapema
 
Ukikubali kufanya huo ujinga siku za mbele utakuja kujilaumu zaidi ukijua kuwa hao wote baba na mama mtoto walikaa meza moja wakakubaliana wakukamue mpaka uharo,shtuka mjini shule huo ni mchongo wameupanga wote wawili,sema kingine watu mna roho ngumu aisee kuishi na baamedi kama mpenzi wako wa kudumu mimi mkurya na roho yangu ngumu lakini sijafikia hiyo hatua🙌🙌
 
😃 😀 😄 😁
 
Back
Top Bottom