Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Jiwe la kubusu ni hivi, ili kutoka pale barango kwenda karanga lazima mpite mlimani, na mkiwa pale barango mlima unauona uleeeee, mkifika pale mlimani njia ni nyembamba sana, sasa kuna sehemu kuna jiwe kubwa ili kupita hapo lazima ulikumbatie hilo jiwe na unapita upande upande lakini mbaya zaidi chini kuna korongo so ukikosea step kidogo tu unaweza kujikuta uko korongoni, so mnapita mmoja mmoja na kwa uangalifu mkubwa. Nakumbuka kundi letu tulikuwa zaidi ya watu 30 tulitumia almost 2hrs kuvuka hapo....na slogan ya mlimani ni Pole Pole....no hurry

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaaa hapo jiwe la kubusu sie makamanda enzi hizo nikiwa mgumu kuna kinjia unapita juu kwa juu unaparamia miamba sababu foleni ya pale ukute ndio high season utakaa zaidi ya masaa...
 
naomba kujua endapo mtu mmoja amepandia machame na mwingine mlangu je, hiz njia kunasehem zinakutana?
Hapana hizi route hazikutani, ila kwa anayepandia machame or lemosho akifika karanga au barafu camp kuna vijinjia anaweza pita akatokea kibo hut ambayo ndio last sleeping point ya route ya marangu na rongai, hizo njia wanatumia sana wale cleaners wa park or wagumu wanaoenda deliver supply...
Route zinazokutana ni machame na lemosho mnakutana barranco camp, au marangu na rongai mnakutana kibo hut or school hut
 
By that time ilikua 15 to 20 k per day mkiwa na bahati unaweza pata tip ya 5 au 10 mpaka 30dollars mda mwingine no tip at all.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna safari moja sitoisahau ya siku 10 kuzunguka mlima lemosho route tulikuwa na wabrazili mwisho wa siku tunashuka hawaelewi chochote kuhusu tip, dadeki ile siku kila mgumu alitukana kikwao...
 
Interesting.....

-Ningependa kujua kuna njia ngapi(Routes) za kufika Kilele cha mlima kilimanjaro?

-Mwanzoni tulifundishwa Kibo na Mawenzi ndio vilele vya mlima kilimanjaro ila kwenye hii thread nimeona vilele zaidi ya 10 na kingine naambiwa Uhuru peak,Je Uhuru ndio Kibo au Mawenzi?

-Inachukua siku ngapi kwa kupanda hadi kufika kilele cha mlima k/njaro? Kwa Routes zote.

-Tupeni faida/changamoto za routes zote za kufika kwenye peaks.

-Gharama za kufika huko either personal au kutumia agents.

-Vitu gani vya kuzingatia ukitaka kwenda huko gears/facilities.

-Hali ya kiafya,je inatakiwa uwe katika situation gani ya kiafya ili usipate makandokando ya kufika peak,maana wamezungumzia afya general iwe nzuri,kwahiyo watu wenye HIV,pressure,kisukari etc hawewezi kuruhusiwa kwenda?
 
Back
Top Bottom