Wakati wa kupanda miti kwenye milima ni huu ambapo mvua zinanyesha

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,673
22,264
Baada ya janga lililotokea Hanang inaelekea tumelichukulia kuwa limekwisha, ninapenda kuwashauri viongozi wote nchini kuwa vilima byote ambako mvua zinanyesha huu ndio wakati wa kupanda miti.

Viongozi wetu wamekuwa na mtindo wa kiweka siku ya kupanda miti hasa wakati hakuna mvua na matokea hiyo miti ilikufa.

Mkoa wa Morogoro uchukue hatua ya kupanda miti kwenye milima inayouzunguruka mji wa Morogoro kwani milima hiyo hivi sasa iko wazi kutokana na tabia ya wakazi kuchoma moto kwenye milima hiyo.

Mkoa wa Kilimanjaro, huu mkoa unahitaji juhudi za ziada hata kama kutumia JKT na wengineyo.

Maeneo mengi hivi sasa yako wazi na ndiyo chanzo cha theruji kwenye mlima Kilimanjaro kuyeyuka kutokana na joto linalozalishwa maeneo ya chini ya mlima ambayo ni Rombo, Himo, Moshi, Hai na mengineyo.

Mkoa wa Arusha, huu mkoa unahitaji kupandwa miti maeneo mengi yenye vilima ambavyo viko wazi, kwa ujumla wakati wa kupanda miti ni huu.
 
Pandeni miti

Siyo kutwa mnakatika mauno tu

Sjui misondo zuchu na maujinga mengine

Ova
 
Wakazi wa Morogoro wao kwa miaka mingi wamekuwa wakikata na kuchoma mapori kwenye mlima unaouinamia mji wa Morogoro! Kila siku usiku mioto huonekana kwenye milima wala hakuna anayejali.
 
Back
Top Bottom