Simulizi ya kweli: Mpaka kieleweke

Simulizi ya kweli: Mpaka kieleweke

Story: Mpaka Kieleweke
Mtunzi: Nira Saire
SEHEMU YA 14

Ilipoishia..
Mnaro akasitisha zoezi lake, akafumbua macho na kunitizama, kisha akatizama ambapo moshi ule ulitengeneza mlango nami nikajikuta nikitupia macho yangu kuangalia mlango ule wa moshi, mlango ule ulionekana kuanz kupungua ukubwa kwa kasi.. "KIMBIAAAAAAAA, PITA HAPO UENDEEEE" alipiga kelele Mnaro nami nikakimbia mbio zangu zote, nikiwa nimebakiz hatua chache nikaona kama sitoiwahi kasi ile hivyo nikaamua kujirusha kupenya kwenye mlango ule kabla haujafunga....

Endelea..
Nikafanikiwa kuwahi, nikatua na kugeuka nyuma lakini sikumuona Mnaro, hata mazingira yalikuwa ni tofauti na ambayo nilikuwemo kabla, moja kwa moja nikagundua kuwa nilikuwa nimeingia Muifufu tayari. Kitu cha kushangaza ni kuwa sikuwa na nguo yoyote mwilini mwangu. Ikanibidi kuzunguka hovyo ndani ya pori lile kutafuta chochote cha kuvaa lakini sikupata kitu zaidi ya majani ya mgomba ambayo niliyaunganisha kwa kamba nilizotengeneza kutoka mgomba pia, kisha nikavaa kujisitiri halafu nikatembea kufuata maelekezo ya Mnaro ndani ya pori lile.
Ilinichukua kama saa zima mpaka kuanza kuona mji kwa mbali nikiwa ndani ya pori lile, nikawa makini zaidi na kugundua kuwa nilikuwa katikati ya miti ile iliyojipanga kwa mstari, nikatembea kuelekea nnje ya pori mpaka nilipoifikia mti ule wa mwisho upande wa kulia na kwenda kuweka mkufu ule ambao nilielekezwa kuuacha kwaajili ya Sauda ili atambue uwepo wangu ndani ya Muifufu, kisha nikaingia ndani ya mji ule bila hata ya kujua pa kuanzia.
Nilitembea nikirandaranda bila kuwa na pakwenda mwisho nikakuta gogo kubwa nyuma ya jumba lililojengwa kwa mawe, nikaamua kukaa hapo nikisubiri kupambazuke vizuri kwa maana kulikuwa na kagiza bado, tofauti na siku ambayo niliingia Muifufu kupitia nyumbani kwa Mnaro ambapo niliondoka kule ikiwa usiku lakini Muifufu kulikuwa mchana, leo kote palikuwa na giza.
Nikakaa pale mpaka nikajikuta nimepitiwa na usingizi.

Nilishituliwa na mlio wa mkali kama honi ya meli, nikaamka na kuona watu wakikimbia kuelekea huko ambako sauti hiyo ilitokea. Kulikuwa kumepambazuka tayari hivyo niliweza kuona kila kitu kwa ufasaha kabisa. Nikatamani kujua nini kilikuwa kinaendelea huko hivyo na mimi nikaungana na wakimbiaji wale kufuata mlio ule ambao nadhani ulikuwa ukilizwa kwa makusudi ya kuita watu.
Jambo ambalo nililugundua nikiwa katika kuwahi huko ni kuwa mimi nilikuwa tofauti na watu wote kutokana na kuvaa kwangu majani ya migomba, wenyeji wa eneo lile wangi walijifunga kaniki huku juu wakiwa hawakuvaa kitu, wengine walijifunga ngozi za wanyama mbalimbali lakini wengine ambao walikuwa na wachache tu walikuwa uchi.. uchi kabisa wa mnyama.
Nikaamua kuwa ni bora kufanana na wenyeji, vinginevyo ningeonekana mara moja kuwa mimi nilikuwa mgeni na sikujua madhara yangekuwa yapi kama ningeonekana mgeni.
Njia pekee ambayo ilikuwa rahisi kwenye kujifananisha na wenyeji wale ilikuwa kuwa uchi.. kuwa uchi hakuhitaji kuwa na chochote, ni suala la kuvua tu majani yale ya mgomba, niliwaza na kujiweka kujitoa polepole miongoni mwa wakimbiaji wale ambao bila shaka hakuna hata mmoja ambaye aliutambua uwepo wangu pale kwani hakuna ambaye alikuwa makini kwa mwingine.
Nikasimama na kuvua majani yale kisha safari ya ikaendelea nikijichanganya na ambao walitokea nyuma yangu, baadhi yao walikuwa uchi kama mimi hivyo kuniongeze ujasiri wa kuwa katika hali ile ya uchi hadharani jambo ambalo halikuwahi kutokea kabla maishani mwangu.
Tulikwenda mpka kufika kwenye uwanja mkubwa sana mbele ya jumba kubwa mno na la kifahari, jumba lile bado lingekuwa la thamani hata kama lingekuwa ndani ya dunia yetu hii yenye kila aina ya majengo. Katikati ya uwanja ule kulikuwa na mzee akiwa amekaa kwenye kiti akizungukwa na wasichana warembo kama nane hivi, pembeni yake alikuwa amesimama mwanaume wa kama miaka 40 hivi ambaye alikuwa mkubwa sana wa umbo na alikuwa na misuli ya ukakamavu hasa, mtu yule alikuwa mweusi tiii! Ngozi yake ambayo ilionekana kama ambayo imepakwa mafuta mengi sana ilikuwa ikin`gaa sana.
Watu wakaendelea kimiminika pale mpaka kukawa na kundi kubwa sana ambalo ilikuwa ngumu kuamini kuwa lote lilitokea ndani ya kamji kale kadogo.
Baada ya utulivu wa hekaheka za watu kupatikana, bwana yule mweusi sana akasimama na kuanza kuzungumza "wakazi wote wa Muifufu naomba mnisikilize kwa makini sana! Alfajiri ya leo kuna mtu kutola duniani ameingia Muifufu, mtu huyo ambaye mpaka sasa hatujamjua ameingia bila ruhusa wala taarifa kwa uongozi wetu na hatujui amewezaje kuingia wala hatujui ana lengo gani! Sasa tunataka kumpata mtu huyo ili kujua kilichomleta pamoja na kumuadhibu kwa kuingia kwake bila ruhusa, hivyo tunataka watu wote muwepo hapa! Kama kuna mtu kabaki nyumbani, awe mzee ama mtoto, mzima ama mgonjwa lazima aje hapa!. Tunatoa dakika kumi tu wote waliobaki nyumbani waje hapa". Mara baada ya kusema maneno yale minong`ono ya hapa na pale ikasikika huku baadhi ya watu wakikimbia, nadhani kurudi makwao kuwaleta ambao wamebakia nyumbani.
"Itakuwa ni msaliti Mnaro amerudi" aliongea mzee mmoja ambaye alikuwa karibu na mimi akijaribu kukisia juu ya hali ambayo ilikuwa inaendelea.. "hapana, Mnaro hawezi kurudi hapa kwa maana anajua fika kama akikanyaga tu ndani ya Muifufu basi mkuu Magugi atajua" alijibu mzee mwingine ambaye ndiye aliekuwa akiambiwa jambo ambalo mzee yule wa awali aliliafiki.
Baada ya dakika zile kumi kuisha bwana yule aliamuru watu wote wasimame na kuwataka kila mtu kuhakikisha mkono wake wa kushoto unashikana na mtu ambaye anamjua na ni mkazi wa Muifufu huku mkono wa kulia pia ukishikwa na mtu mwingine mwenye sifa kama hizo na zoezi hilo likaanza mara moja!.
Namimi nikawa katika harakati kujaribu kushikana mkono na mtu yeyote lakini hakuna ambaye alikuwa akiukubali mkono wangu, nikaona kundi lile likiendelea kuungana kwa kushikana mikono kutoka mtu mmoja kwenda mwingine lakini mimi niliendelea kuwa mpingwaji kwa kila ambaye nilijaribu kumpa mkono wangu, hapo nikaelewa nini hasa lilikuwa lengo la mchezo ule, nimimi nilikuwa natafutwa hapa, baada ya kubaki pekeyangu kundi lote likiwa limeungana basi moja kwa moja watajua kuwa mimi ndiye ambaye sina ambaye ananijua hivyo ndiye ambaye nimeingi kutokea duniani alfajiri ya siku hiyo.
Niliingiwa na uoga wa hali ya juu nikikimbia huku na huko kujaribu kupata wa kiushika mkono wangu lakini hakuwepo mtu wa aina hiyo na sasa nikona tayari nn likuwa nimeumbuka na kukamatwa masaa machache tu baada ya kufanikiwa kuingia Muifufu nikiwa hata sijamuona mke wangu, roho iliniuma sana.
Wazo ambalo lilinijia ghafla ni kukimbia kuondoka eneo lile ili nisikutwe na ambacho kinaelekea kunikuta, lakini lilikuwa ni jambo la kutisha vilevile kwa maana nilijua watu walikuwa makini kuangalia nani anabaki akiwa hakushikwa mikono na kama nitakimbia bila shaka nitaonekana na kukimbizwa ndani ya eneo lile ambalo wao walilijua zaidi mimi nikiwa mgeni tu, lakini hakukuwa na namna nyingine hivyo nikavuta pumzi nyingi na kujiandaa nikiangalia ambapo palikuwa na nafasi nzuri ya kutorokea ili nitimue mbio, lakini nikahisi mkono wangu wa kulia ukishikwa na mkono mlaini wa mtu ambaye alikuwa nyuma yangu nilishtuka nikiona kama ilikuwa ndoto, no kageuka na kukutana na sura ya mwanamke mrembo sana akawa ameachia tabasamu zuri sana!.
Mwanamke yule ambaye alikuwa ni chotara wa Muafrika na Muarabu akakunjua kiganja chake cha mkono wa kulia na kunionesha kitu...
Ulikuwa ni ule mkufu ambao nilielekezwa na Mnaro kuuacha kwaajili ya Sauda. Ahsante Mungu, Sauda wakati muafaka! Bila uwepo wake hapa kila kitu kilikuwa kinaharibikia hapa!, Niliwaza nikiwa na furaha ya hali ya juu moyoni mwangu, nilitamani kumdandia mwanamke yule ambaye nilijua alikuwa Sauda wa Mnaro na kumkumbatia ila mazingira hayakuruhusu hivyo nikajikaza na kufanya kama hukukuwa na kitu ambacho kimetokea.
Baada ya kama dakika moja tu mkono ule wa kulia wa Sauda uliapata mtu akaushika nami nilipojaribu kumpa mtu mwingine mkono wangu wa kushoto nilishangaa akiupokea bila ubishi, nadhani ni kutokana na udhamini ule wa Sauda ambaye alionekana kumjua.
"Kuna mtu ambaye hajashikwa mkono?" Aliuliza bwana yule mbabe, lakini palikuwa kimya, kisha akaongea tena "bila shaka mtu huyo hajaja hapa lakini najua nyote mnajua kua lazima tutamkamata, uwezo wa Magugi sio wa kufananishwa na mtu yeyote..." kabla hajamaliza mzee yule ambaye alikuwa amekaa muda wote alisimama akaongea kwa hasira "hakuna wa kushindana na Magigi ikiwa nitaamua jambo.
Sasa nasema endeleeni na shughuli zenu lakini nawahakikishia mtu huyo nitamkamata kabla siku haijaisha, hakuna anayepajua Muifufu kuliko mimi kati ya watu wote walioko hai, familia yoyote ambayo itampokea mtu huyo nyumbani kwake basi hukumu ya mtu huyo itaihusu pia familia hiyo" alimaliza kuongea mzee yule na watu wakaanza kutawanyika kwa makundimakundi kila kundi likiwa na uelekeo wake, nikamuona pia Sauda akiondoka kufuata uelekeo ambao aliujua yeye hivyo nikaona utakuwa ujinga wa karne kama sitomfuata.
Nikaendelea kumfuata polepole Sauda ambaye alikuwa kwenye kundi la watu wengine wakiondoka eneo lile, tukaendelea kwenda mimi nikifuata polepole mpaka Sauda akawa ametengana na watu wale na kubaki pekeyake, akaendelea kwenda mpaka kwenye nyumba moja kuukuu akaingia humo, nami nikaendelea kumfuata nikiamini alitaka nimfuate kwa maana alikuwa akigeuka nyuma na kutizama kama namfuata kila baada ya hatua kadhaa.
Nikaingia ndani ya jumba lile ambamo tulikuta watu wengine wawili mmoja akiwa mwanamke mzee na mwingine alikuwa ni mwanaume wa makamo!.
Sauda akanitbulisha kwa watu wale ambao walionekana kujua kila kitu juu ya mpango wangu kisha akamtaka bwana yule kuandaa mpango mzuri "sasa Mkude nataka uhakikishe kuwa huyu bwana anafanikiwa kuingia nyumbani kwa Magugi kisha mambo mengine yatafuata" aliongea Sauda maneno ambayo yalinishtua sana, kuingia kwa Magugi tena? mtu ambaye ameapa kuwa atanipata kabla siku haijaisha, tena nijipeleke mpaka kwake? Niliwaza..
"Hakuna shida, ingawa ili kumuingiza kwa Magugi itagharimu maisha ya mtu asiye na hatia" aliongea bwana yule ambaye kwa harakaharaka alionekana mpole sana.
"Unazungumzia mtu mmoja? Jambo hili ni lazima litimie hata kwa kuua mamilioni ya watu" alijibu Sauda kwa maneno yale ambayo hayakufanana hata kidogo na muonekano wake..

Usikose sehemu ya 15

nirasaire@gmail.com
 
Nipo huko kwenye hilo group lakin nmejuta kujiunga..toka asubh kupo kimyaaaaa yaani wale watu wa ajabu ila nahisi nao watakuwa wenyeji wa maifufu
jaman unajiungaje ? mkuu niunge basi
 
kwann mkuu
Anataka kupiga ela juyo.
Sasa Huo sio ustaarabu wewe mwandishi. Sema hivo,
kwa anaetaka kuendelea kupata hii hadithi lipia kiasi kadhaa nakutumia yote WhatsApp kwa mawasiliano zaidi ni pm au linamba lako. Mbona u.ekuwa wa ajabu ghafla Kama Hapo qachawi wako wa kufikilika. Umekera sana.
Tabia za kimama hizo
 
Kuna sehemu nimeandika nauza??!! Nimesema unitafte upate mwendelezo mkuu
sasa kama huuzi unataka tukutafute ili iweje na kwa nn hautaposti tena mpaka tukufuate wasap
tunashukuru kwa stori yako ila umeboa tena sànaa kama ungesema tangia mwanzo kwamba u need money
 
Back
Top Bottom