Nzi Chuma
JF-Expert Member
- Jun 21, 2015
- 472
- 1,142
STORY: MPAKA KIELEWEKE
MTUNZI: NIRA SAIRE
SEHEMU YA KWANZA
Nilikuwa nimeongozana na mke wangu tukitokea dukani eneo lile la ugenini nikiwa busy kwenye simu yangu huku nikiongea na mke wangu ambaye alikuwa nyuma yangu akinisemesha hili na lile. Mara nikagundua hali isiyo ya kawaida, mke wangu alikuwa kimya ghafla.. nikageuka haraka kutaka kujua nini kilimfanya awe kimya namna ile lakini cha ajabu sikumuona mke wangu. "khaaa, kabaki wapi huyu mwanamke?" nilijikuta nikiuliza kwa sauti ilhali nilijua fika kuwa nilikuwa peke yangu eneo lile lenye kiza cha kutosha. Uamuzi nilioufikia haraka ni kuamua kurudi nyuma kujaribu kumtafuta huku nikimpigia simu kwa maana nakumbuka alitoka nyumbani na simu yake. kitu cha ajabu simu yake iliita nyuma yangu baada ya kuwa nimetembea hatua chache tu, niligeuka nikaufuata muito ule wa simu ambao nilikuwa nikiujua kuwa ni wa simu ya mke wangu... kweli ilikuwa simu ya mke wangu ikiwa pale chini ikiendelea kuita, nilishikwa na bumbuwazi kwa sekunde chache nisijue hata cha kufanya kisha nikaiokota ile simu na kuanza upya safari ya kurudi eneo lile la madukani kujaribu kuona kama naweza kumuona mke wangu.
Nilitembea huku nikiangaza huku na huko nikiamini pengine ningemuona mke wangu lakini mpaka nafika eneo lile la maduka sikuwa nimemuona.
Nikajaribu kuvuka eneo lile na kuangalia maeneo ya mbele zaidi ila sikumuona.
Akili ikaniambia labda atakuwa amekwenda nyumbani, nikakimbia mpaka nyumbani ila mlango ulikuwa umefungwa kama ambavyo tuliuacha, mke wangu hakuwepo na funguo alikuwan azo yeye. Sikuwa na sehemu nyingine ya kumuangalia kwa maana tulikuwa hata hatujazoeana na majirani.
Moja kwa moja nikaenda mpaka duka lile ambalo tulikuwa tumenunua bidhaa dakika chache zilizopita kwani ndilo duka pekee ambalo tulikuwa tukinunua kwa muda wote wa siku tatu tangu tuhamie mji ule. Hata muuzaji wa duka lile tulikuwa tumeanza kuzoeana hivyo sikuwa na mtu mwingine wa kumfuata wakati ule zaidi yake.
“samahani Mangi” nilianza kumsemesha mara baada ya mteja aliyekuwa akamuhudumia kuondoka... “aisee mke wangu hajafiaka hapa?” niliuliza nikilingojea jibu kwa hamu huku nikitamani awe na chochote cha kusema ambacho kingesaidia kumpata mke wangu kwa maana hofu kubwa ilikuwa imeniingia tayari.. Mangi alionekana kunishangaa kidogo kisha akauliza..
“wewe si umeondoka hapa na mke wako hata dakika kumi hazijaisha?” kufika hapo nikachoka kabisa na kujikuta nikikaa kwenye benchi ambalo lilikuwa nnje pale dukani. Mwili wangu ulikuwa ukitetemeka kiasi ambacho kilimshangaza Mangi ambaye wakati huo alikuwa akijaribu kunisemesha lakini hata sikumbuki alikuwa anaongea nini kwa maana akili yangu hata haikuwa pale na wala sijui ilikuwa wapi.
Kugutuka nilimuona Mangi akiwa amesimama mbele yangu pamoja na watu wengine ambao walionekena kuwa wenyeji wa eneo lile wakitaka kujua nini kilikuwa kimetokea.
“Kijana hebu tueleze hali ambayo imetokea pengine tunaweza kusaidiana mawazo na jambo likawa jepesi” aliongea mzee mmoja wa makamo ambaye sikumfahamu ila moja kwa moja nikajua Mangi alimuita ili kuja kusaidia baada ya kuniona katika hali ile isiyoeleweka.
Nilijikaza nikawasimulia mkasa uliotokea, wakati naendelea kuongea watu walikuwa wanazidi kuongezeka.. mpaka namaliza kuongea kulikuwa na kundi kubwa sana, wake kwa waume.
“Jamaniiiii hali hii mpaka lini?” ilikuwa sauti ya mama mmoja mtu mzima ambaye alikuwepo akisikiliza maelezo yangu, kauli ile iliniacha njia panda.. inamaana matukio ya namna hii ni ya kawaida kutokea eneo lile? Nilikuwa nikijiuliza. Watu
ambao walikuwepo pale pia hawakuonekana kujiuliza ni wapi alipotelea mke wangu badala yake walionekana kunionea huruma.
Pemebeni nilimuona mzee yule ambaye alinitaka kuwaelezea ambacho kilinisibu akishauriana na wanaume wengine watatu kisha wakaja pale nilipo..
“Tumpelekeni kwa mzee Miale” aliongea yule mzee, wakanisaidia kunyanyuka na safari ya kuelekea kwa mzee Miale ambaye sikujua ni nani wala tunaenda kufanya nini kwake ikaanza.
Kwakweli nilikuwa nimechanganyikiwa nikajikuta nafuata kila ambacho naambiwa bila hata kuhoji.
Tulifika kwa mzee Miale tukabisha hodi na kupokelewa na mama mtu mzima kidogo.
“Karibuni jamani, kwema?” alitukaribisha mama yule akiwa na mshtuko nadhani ilitokana na wingi wa watu ambao tulikuwa tumeongozana nao.
“Sio kwema sana shemeji, huyu bwana tumemkuta?” aliongea mzee mmoja kwa niaba ya kundi lile.
“Hapana, huyu bwana ameenda kwenye
shughuli zake huko Michese ila atarudi asubuhi” alijibu yule mama ambaye nilikuwa nimegundua kuwa alikuwa mke wa mzee Miale. Yule mzee ambaye tulikuja naye akamchukua yule mama wakakaa kando kidogo na kuongea, nadhani alikuwa akimuhadithia kilichonikuta. Baada ya muda mfupi wakasogea ambapo tulikuwa tumesimama na yule mama akaongea..
“Pole kwa yaliyokukuta mwanagu, jikaze ndio ukubwa huo” akanitazama, nikaitikia kisha akaendelea..
“Sasa wewe nenda kapumzike kesho mida ya
saa mbili uje mzee atakuwepo” aliongea yule mama nami nikaitikia.
Tukaondoka njiani tukigawanyika kila mmoja akishika njia ya kuelekea kwake mpaka nikabaki na vijana wawili ambao tuliendelea kuongozana..
“Pole sana kaka, mimi ni jirani yako bwana, nakaa ile nyumba yenye rangi ya kijani kulia mwa pale kwako” aliongea mmoja wa wale vijana wenzangu huku mwingine akituaga na kufuata njia ambayo ilimuhusu.
“Asante aisee” nilimjibu tukaendelea na safari huku nikijaribu kudodosa juu ya ambacho anadhani kitakuwa kimempata mke wangu.
“Mimi ni mbumbumbu juu ya hili kama ulivyo wewe, ukifika kwa yule mzee kesho nadhani unaweza kupata majibu mazuri” alinijibu wakati huu tukiwa tumefika kwangu tukaachana.
Nilitembea hatua chache kuelekea ulipo mlango wa kuingilia nikakumbuka kuwa mlango ulikuwa umefungwa na funguo alikuwa nazo mke wangu, nikafikiri kwa muda na kisha kuamua kuwa kama simu iliachwa pale basi pengine na funguo ipo maeneo yale ila sikuiona kwakuwa kulikuwa na giza, hivyo nikaamua kurudi eneo lile nikaitafute kwa kutumia tochi ya simu ya mke wangu ambayo ilikuwa na mwanga mzuri tu.
Saa kwenye simu ilikuwa inaonesha kuwa ni majira ya saa sita kasorobo usiku, nikatembea polepole kuelekea eneo ambalo alipotelea mke wangu, nikafika na kuwasha tochi ya simu kisha nikaanza kuangaza kuitafuta funguo ya mlango wa nyumbni kwangu lakini nilishtushwa sana na ambacho nilikiona kama hatua tatu mbele ya ambapo nilikuwa nimesimama, zilikuwa ni nguo za mke wangu......
★★★★★★★★★★★
USIKOSE SEHEMU YA PILI
Kwa maoni au ushauri unaweza kunipata kupitia:
+255653686008
nirasaire@gmail.com