Simulizi ya kweli: Mpaka kieleweke

Simulizi ya kweli: Mpaka kieleweke

STORY: MPAKA KIELEWEKE
MTUNZI: NIRA SAIRE

SEHEMU YA KWANZA

Nilikuwa nimeongozana na mke wangu tukitokea dukani eneo lile la ugenini nikiwa busy kwenye simu yangu huku nikiongea na mke wangu ambaye alikuwa nyuma yangu akinisemesha hili na lile. Mara nikagundua hali isiyo ya kawaida, mke wangu alikuwa kimya ghafla.. nikageuka haraka kutaka kujua nini kilimfanya awe kimya namna ile lakini cha ajabu sikumuona mke wangu. "khaaa, kabaki wapi huyu mwanamke?" nilijikuta nikiuliza kwa sauti ilhali nilijua fika kuwa nilikuwa peke yangu eneo lile lenye kiza cha kutosha. Uamuzi nilioufikia haraka ni kuamua kurudi nyuma kujaribu kumtafuta huku nikimpigia simu kwa maana nakumbuka alitoka nyumbani na simu yake. kitu cha ajabu simu yake iliita nyuma yangu baada ya kuwa nimetembea hatua chache tu, niligeuka nikaufuata muito ule wa simu ambao nilikuwa nikiujua kuwa ni wa simu ya mke wangu... kweli ilikuwa simu ya mke wangu ikiwa pale chini ikiendelea kuita, nilishikwa na bumbuwazi kwa sekunde chache nisijue hata cha kufanya kisha nikaiokota ile simu na kuanza upya safari ya kurudi eneo lile la madukani kujaribu kuona kama naweza kumuona mke wangu.

Nilitembea huku nikiangaza huku na huko nikiamini pengine ningemuona mke wangu lakini mpaka nafika eneo lile la maduka sikuwa nimemuona.
Nikajaribu kuvuka eneo lile na kuangalia maeneo ya mbele zaidi ila sikumuona.
Akili ikaniambia labda atakuwa amekwenda nyumbani, nikakimbia mpaka nyumbani ila mlango ulikuwa umefungwa kama ambavyo tuliuacha, mke wangu hakuwepo na funguo alikuwan azo yeye. Sikuwa na sehemu nyingine ya kumuangalia kwa maana tulikuwa hata hatujazoeana na majirani.
Moja kwa moja nikaenda mpaka duka lile ambalo tulikuwa tumenunua bidhaa dakika chache zilizopita kwani ndilo duka pekee ambalo tulikuwa tukinunua kwa muda wote wa siku tatu tangu tuhamie mji ule. Hata muuzaji wa duka lile tulikuwa tumeanza kuzoeana hivyo sikuwa na mtu mwingine wa kumfuata wakati ule zaidi yake.
“samahani Mangi” nilianza kumsemesha mara baada ya mteja aliyekuwa akamuhudumia kuondoka... “aisee mke wangu hajafiaka hapa?” niliuliza nikilingojea jibu kwa hamu huku nikitamani awe na chochote cha kusema ambacho kingesaidia kumpata mke wangu kwa maana hofu kubwa ilikuwa imeniingia tayari.. Mangi alionekana kunishangaa kidogo kisha akauliza..
“wewe si umeondoka hapa na mke wako hata dakika kumi hazijaisha?” kufika hapo nikachoka kabisa na kujikuta nikikaa kwenye benchi ambalo lilikuwa nnje pale dukani. Mwili wangu ulikuwa ukitetemeka kiasi ambacho kilimshangaza Mangi ambaye wakati huo alikuwa akijaribu kunisemesha lakini hata sikumbuki alikuwa anaongea nini kwa maana akili yangu hata haikuwa pale na wala sijui ilikuwa wapi.
Kugutuka nilimuona Mangi akiwa amesimama mbele yangu pamoja na watu wengine ambao walionekena kuwa wenyeji wa eneo lile wakitaka kujua nini kilikuwa kimetokea.
“Kijana hebu tueleze hali ambayo imetokea pengine tunaweza kusaidiana mawazo na jambo likawa jepesi” aliongea mzee mmoja wa makamo ambaye sikumfahamu ila moja kwa moja nikajua Mangi alimuita ili kuja kusaidia baada ya kuniona katika hali ile isiyoeleweka.
Nilijikaza nikawasimulia mkasa uliotokea, wakati naendelea kuongea watu walikuwa wanazidi kuongezeka.. mpaka namaliza kuongea kulikuwa na kundi kubwa sana, wake kwa waume.
“Jamaniiiii hali hii mpaka lini?” ilikuwa sauti ya mama mmoja mtu mzima ambaye alikuwepo akisikiliza maelezo yangu, kauli ile iliniacha njia panda.. inamaana matukio ya namna hii ni ya kawaida kutokea eneo lile? Nilikuwa nikijiuliza. Watu
ambao walikuwepo pale pia hawakuonekana kujiuliza ni wapi alipotelea mke wangu badala yake walionekana kunionea huruma.
Pemebeni nilimuona mzee yule ambaye alinitaka kuwaelezea ambacho kilinisibu akishauriana na wanaume wengine watatu kisha wakaja pale nilipo..
“Tumpelekeni kwa mzee Miale” aliongea yule mzee, wakanisaidia kunyanyuka na safari ya kuelekea kwa mzee Miale ambaye sikujua ni nani wala tunaenda kufanya nini kwake ikaanza.
Kwakweli nilikuwa nimechanganyikiwa nikajikuta nafuata kila ambacho naambiwa bila hata kuhoji.
Tulifika kwa mzee Miale tukabisha hodi na kupokelewa na mama mtu mzima kidogo.
“Karibuni jamani, kwema?” alitukaribisha mama yule akiwa na mshtuko nadhani ilitokana na wingi wa watu ambao tulikuwa tumeongozana nao.
“Sio kwema sana shemeji, huyu bwana tumemkuta?” aliongea mzee mmoja kwa niaba ya kundi lile.
“Hapana, huyu bwana ameenda kwenye
shughuli zake huko Michese ila atarudi asubuhi” alijibu yule mama ambaye nilikuwa nimegundua kuwa alikuwa mke wa mzee Miale. Yule mzee ambaye tulikuja naye akamchukua yule mama wakakaa kando kidogo na kuongea, nadhani alikuwa akimuhadithia kilichonikuta. Baada ya muda mfupi wakasogea ambapo tulikuwa tumesimama na yule mama akaongea..
“Pole kwa yaliyokukuta mwanagu, jikaze ndio ukubwa huo” akanitazama, nikaitikia kisha akaendelea..
“Sasa wewe nenda kapumzike kesho mida ya
saa mbili uje mzee atakuwepo” aliongea yule mama nami nikaitikia.

Tukaondoka njiani tukigawanyika kila mmoja akishika njia ya kuelekea kwake mpaka nikabaki na vijana wawili ambao tuliendelea kuongozana..
“Pole sana kaka, mimi ni jirani yako bwana, nakaa ile nyumba yenye rangi ya kijani kulia mwa pale kwako” aliongea mmoja wa wale vijana wenzangu huku mwingine akituaga na kufuata njia ambayo ilimuhusu.
“Asante aisee” nilimjibu tukaendelea na safari huku nikijaribu kudodosa juu ya ambacho anadhani kitakuwa kimempata mke wangu.
“Mimi ni mbumbumbu juu ya hili kama ulivyo wewe, ukifika kwa yule mzee kesho nadhani unaweza kupata majibu mazuri” alinijibu wakati huu tukiwa tumefika kwangu tukaachana.
Nilitembea hatua chache kuelekea ulipo mlango wa kuingilia nikakumbuka kuwa mlango ulikuwa umefungwa na funguo alikuwa nazo mke wangu, nikafikiri kwa muda na kisha kuamua kuwa kama simu iliachwa pale basi pengine na funguo ipo maeneo yale ila sikuiona kwakuwa kulikuwa na giza, hivyo nikaamua kurudi eneo lile nikaitafute kwa kutumia tochi ya simu ya mke wangu ambayo ilikuwa na mwanga mzuri tu.
Saa kwenye simu ilikuwa inaonesha kuwa ni majira ya saa sita kasorobo usiku, nikatembea polepole kuelekea eneo ambalo alipotelea mke wangu, nikafika na kuwasha tochi ya simu kisha nikaanza kuangaza kuitafuta funguo ya mlango wa nyumbni kwangu lakini nilishtushwa sana na ambacho nilikiona kama hatua tatu mbele ya ambapo nilikuwa nimesimama, zilikuwa ni nguo za mke wangu......
★★★★★★★★★★★
USIKOSE SEHEMU YA PILI
Kwa maoni au ushauri unaweza kunipata kupitia:
+255653686008
nirasaire@gmail.com
Pamoja sana mkuu
 
Story : Mpaka kieleweke
Mtunzi: Nira Saire
SEHEMU YA NANE

ilipoishia...
nikijitahidi kulazimisha mwendo wa paka yule, lakini kwa mbele nilimuona mnya yule mwingine ambaye alipitiliza aliwa anakuja kwa kasi upande ule ambao mimi nilikuwa nikitokea! Nilijaribu kuangalia huku na huko lakini sikumuona Mnaro, wasiwasi ukatanda moyoni mwangu.......

Endelea...

Nilijikaza nikaamua kuwa nitafanya lolote kukabiliana na wanyama wale, niliamini haukuwa wakati wangu wa kufa kwa maana niliishajiapiza kuwa sitokufa kabla ya kumrudisha mke wangu kipenzi katika maisha ambayo ameyazoea.
Muda huu nilikuwa nimewekwa kati, wanyama wawili wakiwa nyuma yangu na mmoja akiwa mbele yangu, wote wakiniijia kwa kasi huku nami nikikazana kuelekea mbele kama sikuwa nikimuona mnyama yule wa mbele yangu.
Nikajikuta nikitazamana usokwa uso na mnyama yule tukiwa tumeelekeana kama ambao tunataka kugongana, na unaelekea nia ya mnyama yule ilikuwa ni kugongana maana alizidi kuongeza mwendo akiwa ameikaza mno sura yake ya kutisha kama ambaye amedhamiria ubaya. Nami nikajifanya kama sina akili kama yeye na ninakusudia kugongana lakini nilipomfikia nikakwepa haraka akapitiliza kwa kasi kubwa huku mimi nikiyumba vibaya juu ya paka niliyekuwa nimempanda, nusura nianguke ila nikajikaza na kuendelea huku nikizibana mbavu za paka yule kwa miguu yangu ili nisianguke lakini nikajikuta nikiwa nimegundua kitu, kwa kumbana paka yule kwenye mbavu alikuwa akiongeza kasi kiasi ambacho sikutegemea.
Nikaendelea kubana mbavu z a paka yule ambaye akakazana mpaka kuwa wapoteza kabisa wanyama wale kwenye upeo wa macho yangu! Nikaenda nikipunguza kasi na hatimaye nikasimama na kujaribu kufikiri nawezaje kumpata Mnaro lakini sikupata jibu, wakati huo pia sikujua ilikuwa saa ngapi. Hofu ikaanza kunipanda nikijiuliza nitafanyaje kama kutakucha na watu wakanikuta katika mazingira yale nikiendesha nyau!
Nikaamua kurudi nyumbani kupitia njia ambayo ilinileta pale huku nikiwa najiuliza kipi kitanipata iwapo nitakutana na wanyama wale ambao walinikimbiza muda mfupi uliopita, lakini nilikwenda mpaka nikawa napaona nyumbani bila kukutana na wanyama wale, Mnaro pia sikuwa nimemuona na sasa nikawa najiuliza itakuwaje kuhusu mnyama yule kama mimi nitaenda nyumbani, je nitamuweka wapi. Nilikosa majibu na bado nilikuwa nina wasiwasi wa asubuhi kufika na kunikuta katika hali ile, hivyo nikaamua kumuacha mnyama yule achague pa kwenda nami niingie ndani. Nikaenda mojakwa moja mpaka kwenye ukuta ambapo tulipita wakati wa kutoka nichukua kijiti kile alichonipa Mnaro, nikakibana kwenye kidole cha mwisho kama ambavyo alinielekeza na kukwenda kujaribu kupenya kwenye ukuta lakini cha ajabu nilishindwa, nikajaribu tena na tena lakini ukuta ulikuwa imara. Nikajiuliza nakosea wapi lakini bado nilijijibu kuwa niko sahihi, nikajaribu tena ila kwa mara nyingine nikakwama. Nikiwa naendelea kuwaza hili na lile nikasikia sauti ya baba akikohoa sebuleni, hapo nikajua atakuwa ameamka na kufungua wa chumbachumbauchanguuachkuuacha wazio haitowwzekana tena ktenaimi kuingikuingiaikupitiamlangoni, hivyo nikaenda kugonga mlango mkubwa ambapo baba alinifungulia nikaingia na kumkuta akiwa na maswali mengi sana ikanibidi kumuhadithia safari nitokayo kuanzia mwanzo hadi mwisho, baada ya kisikia maelezo yangu baba alionekana kuhofia sana juu yapaka yule.
Akaamua kutoka nnje ili kuangalia kama atamuona, ila akarudi akiwa na amani kabisa "nadhani litakuwa limeondoka, unadhani lingebaki hapa asubuhi tungewaeleza nini majirani kama wangeliona?.. alisema baba, maneno ambayo yalikuwa ni yakweli kabisa..
nami nikaridhika na kuamua kwenda kulala maana nilikuwa nimechoka sana.
Nikaingia chumbani kwangu na kujifungia kisha nikapanda kitandani kwaajili ya kulala lakini kabla hata usingizi haujanichukua
Nikasikia mtu akipiga makofi ya kupongeza, nilijishangaa kuona hata sikushituliwa na hali ile, nadhani nilikuwa nimeanza kuzoea maisha yale ya mauzauza..
"Umenifurahisha sana safari hii" ilisema sauti ile ambayo niliitambua moja kwa moja kuwa ni ya Mnaro, kisha ikaendelea "ukiendelea kuwa na ujasili kama ambao umeuonesha leo basi tutafanikiwa haraka kuliko ambavyo tulitegemea" maneno haya ya mwisho yakanisisimua na kuirudisha hali yangu ya uchangamfu kutoka kwenye uchovu na uvivu niliokuwanao pale kitandani, nikaamka na kuwasha taa, nikaweza kumuona Mnaro ambaye alikuwa kwenye pembe moja ya chumba kile kisha akaja moja kwa moja na kukaa na mimi pale kitandani.. "uliniacha katika wakati mgumu sana nilipokuwa sikuoni, nilikuwa na hofu sana iwapo watu wangenikuta katika mazingira yale ningefanyaje" nilifungulia maongezi kwa kumuelezea Mnaro juu ya wakati mgumu ambao nilibakinao baada ya kukosa muongozo.. "unadhani ni sisi pekeyetu tulikuwa tukifanya shughuli za kichawi huko nnje?" Aliuliza Mnaro lakini akaendelea kabla sijamjibu "kuna maelfu ya wachawi ambao walikuwepo huko mtaani lakini hakuna hata mmoja ambaye alikuwa akiogopa" kufika hapo nikagundua kuwa alikuwa anataka kuonesha ni namna gani mimi ni muoga.. "tatizo hata muda wenyewe sikuwa nikiujua nikahofia pengine panaweza kukucha nikiwa bado sijarudi" nilijaribu kujitetea.
"Wachawi hufanya shughuli zao hata mchana, kukucha kungekuzuia nini? Kuns mengi sana yanaendelea hata kwenye jamii ya hapa mtaani, ni macho yenu tu hayaoni" baada ya kusema hayo akatoa kachupa kutoka kwenye mkoba wake ule wa ngozi na kunikabidhi..
Nikajaribu kuitikisa kujua kulikuwa na nini ndani yake, nikagundua kulikuwa na kitu kama chumvi hivi..."iwapo utapaka dawa hiyo usoni, hamna ambacho hautokiona" alinieleze nami nikafungua na kujaribu kujioaka kidogo, kweli ilikuwa ni kama chumvi na haikuwa ikibaki usoni, baadala yake ilikiwa ikianguka chini wakati naipaka, naye akaniambia haina shida, lengo limetimia tayar. Nilivutiwa kuona haibaki usoni kwa maana kumbe ningeweza kuipaka na kutembea nayo kuelekea popote.

Mnaro hakuwa na jambo lingine la kuzungumza na mimi kwa usiku ule hivyo akaniaga na kuondoka nami usingizi ukanichukua.
Nilikuja kuamka asubuhi majira kama ya saa moja na robo na kuamua kuelekea bafuni kujiswafi kabla ya kuendelea na mipango mingine, lakini nilipofika bafuni nikagundua kuwa sabuni ilikuwa imeisha hivyo nikaamua kwenda dukani kwanza kununua sabuni, lakini nilipotoka nnje tu nikapatwa na mshangao kuona paka yule mkubwa ambaye nilikuwa nikimfanya usafiri usiku akiwa amesimama katikati ya uwanja wa nyumbani pale. Nikarudi ndani na kumuita baba na kumuelezea ambacho nilikiona pale nnje kwa maana yeye alinihakikishia usiku kuwa paka yule alikuwa aneondoka. Tukatoka nnje pamoja ilikumuona paka yule ila baba hakuwa akimuona. Nikagundua kuwa ni ile dawa ambayo nilijipaka usoni ndiyo inayonitofautisha uwezo wangu wa kuona na wababa hivyo nikajifanya kama ambaye nilijichanganya na kumruhusu baba arudi ndani, "acha mawazo mwangu, utachanganyikiwa. Matatizo ni sehemu ya maisha" alisema baba huku akirudi ndani nami nikafarijika kuwa hata watu wengine hawatoweza kumuona paka yule hivyo nikaendelea na safari ya dukani.

Nilipata sabuni kisha nikaanza safari ya kirudi nyimbani, njiani nilikitana na dada ambaye huwa anatembeza vitafunwa asubuhi kwenye majumba, hata kwangu huwa anapita na wakati mwingine huwa tunanunua, lakini kitu cha ajabu leo alikuwa uchi, uchi kabisa wa mnyama "habari za asubuhi kaka, vipi nikiletee vitumbua ?" Alinisalimia na kuuliza dada yule, nadhani hakijua kama niligundua kuwa alikuwa uchi. "Hapana, sitaki vitumbua vinavyouzwa uchi" nilimjibu kikorofi dada yule baada ya kumuona kuwa anajaribu kunifanya mjinga ikiwa ninaona kinachoendelea, nilijutia pia muda wote wa nyuma ambao nilinunua bidhaa zake. Dada yule alioneshwa kushtushwa na kauli yangu ila akajikaza na kujifanya kama hanielewi, "haya kama huhitaji, nitakuletea siku nyingine" alisema dada yule akijichejeshachekesha nami nikamjibu "usikanyage tena kwangu machawi mkubwa wee" kufikia hapo alionekana kukasirika waziwazi "kwani wewe sio mchawi? Usingekuwa mchawi usingejua kama mimi ni mchawi.. kwanza huna lolote nimeshawachezea mara ngapi pale kwako, kama unajiona umekua tutaonana usiku" alibwata dada yule huku akiendelea na safari yake kwa kasi, nami nikaendelea na safari yangu kuelekea nyumbani.

Nikiwa hatua chache kutoka nyumbani nikaona watu wengi sana wakiwa pale kwangu, nikashtuka na kukaza zaidi mwendo, nilipokaribia zaidi niliweza kumuona na yule paka mkubwa katikati ya wale watu..

Usikose sehemu ya tisa.

Kwa maoni au maswali, unaweza kunipata kupitia:
+255653686008
nirasaire@gmail.com
 
Back
Top Bottom