Simulizi ya kweli kuhusu Gamboshi

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
16,524
2,000
Kabla ya simulizi-Maana ya maneno yaliyotumika kwenye simulizi
- GAMBOSHI ni makazi au eneo linalotumika kuhifadhia misukule.
- MSUKULE ni mtu aliyechukuliwa kwa njia ya kishirikina (kichawi) akiwa mzima (hai), lakini kwa upeo wa kawaida ni dhahiri kuwa amekufa.
Simulizi Inaanzia hapa
Nikuwa darasa la sita pamoja na rafiki yangu John, John alikuwa amenizidi kidogo kiumri. Siku moja tulikuwa tunatoka ktk uwanja wa mpira tulikutana na msichana mrembo ambaye ana kila sifa ya kuitwa mrembo, kwa kweli nilishindwa kujizuia nilijikuta mwili wote unasisimuka. Sikuficha hisia zangu nilimwambia rafiki yangu John, John akasema usijali utampata. Kweli John aliongeza hatua za kumfuata mrembo ikiwa na mimi nafuatia kwa nyuma mdogomdogo.
John: dada habari yako?
Mrembo: salama habari yako?
John: salama,Kwa jina naitwa John, sijui mwenzangu unaitwa nan?
Mrembo: naitwa Sheila.
John: Jina zuir sana. Samahani dada kuna mdogo wangu anaitwa Timoth, kusema ukweli amekupenda sana.
Mrembo: Yupo wapi?
John: Nyuma yetu.
Mrembo: Ohooo!! Timoth!
John: Umemjuaje?
Mrembo: Timoth anakaa jiraniyetu, mwambie kesho saa kumi jion nitamkuta kwao.
......****.....
Kesho yake nikiwa nimejiandaa vya kutosha ghafla mlango ukagongwa ,Duuh! moyo ukaniruka!
Mwanaume nikajikaza kwenda kuufungua mlango, nilipoufungua nikakutana na sura ya mrembo Sheila huku akiwa ananukia marashi kama ya pemba.
Akaingia ndani na mlango akaufunga na kuketi kitandani na kuanza kuvua nguo moja baada ya nyingine(kusema ukweli nilikuwa sijawahi kufanya mapenzi tangia nizaliwe nilijihis mkojo unanitoka).
Baadae akanifuata na kunikumbatia tukaendelea na mambo yetu yaleee
*****
Kusema ukweli hakuna siku niliyoweza kufurahia kama siku hiyo, maana ilikuwa siku yangu ya kwanza kufanya mapenzi. Nilijiona mwili wangu mwepesi sana pia nilitamani niwe na Sheila kila wakati.
Mapenzi yetu yaliendelea na kuwa motomoto kila mtu alitamani awe kama sisi.
Baada ya miezi miwili mapenzi yetu yaliyumba sana, baada ya bibi yake na Sheila ambaye alikuwa kama mlezi wake tangu enzi za utoto wake na alipinga sana mapenzi yetu yasiendelee.
Lakini kwa vile mimi na Sheila tulipendana hatukuona sababu ya kuachana.
Ilikuwa jioni mishale ya moja usiku,tukiwa tunatoka dukani na kipenzi changu kununua mafuta ya taa , mara mbele yetu ikatokea gari ambayo sikuweza hata kubaini imetokea wapi?
Nilijikuta nipo katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga nikiwa napumlia mashine huku mwili wangu umefungwa na bandeji.
Baadaye sikuweza tena kujua kilichoendelea baada ya kuchomwa sindano ya ganzi.
Baada ya siku tatu ufahamu ukanirejea lakini mwili mzima ulikuwa umebandikwa bandeji, nilifungua mdomo kwa shida na kumuuliza nesi "Sheila yupo wapi?" nesi akaniangalia huku machozi yanamlengalenga na kujikaza kisha kuniambia
SHEILA ALIFARIKI PAPO HAPO KWA AJALI YA GARI!
Baada ya kuniambia hayo maneno nilizimia na sikujielewa tena.
Baada ya wiki tatu nilipona na nikaendelea kwenda shule lakini mawazo juu ya mpenzi wangu Sheila yalinifanya nikonde.
Siku moja nikiwa darasani nimekaa peke yangu najisomea mara nikasikia sauti kama ya bibi yake na Sheila ,nikageuka nyuma nikamkuta amesimama kwenye kona ya darasa huku akiwa ameshika mkia wa ng'ombe na mkono wa kushoto ameshika kibuyu.
Niliogopa sana nilitamani kukimbia lakini nilishindwa.
Mara nikasikia sauti...
"SIKILIZA KIJANA NAJUA ULIMPENDA SANA MJUKUU WANGU LAKINI AMEENDA KUNISAIDIA KAZI ZA SHAMBANI, SASA BASI, NINAKUKANYA UTOE FIKRA ZA KUMKUMBUKA SHEILA WALA KUMUOTA, UKIENDELEA PIA NA WEWE UTAMFUATA UKASAIDIZANE NAYE SHUGHULI ZA SHAMBANI. NA KAMA UKIMWAMBIA MTU YEYOTE MANENO HAYA UTAHATARISHA MAISHA YOKO" .
Wakati naendelea kutafakari maneno hayo, mara mlango ukagongwa na kuangalia mlangoni na kukuta ni mlinzi anataka kufunga mlango, kugeuka nyuma bibi sikumuona tena.
Niliogopa sana lakini wazo la Sheila halikuweza kutoka kichwani mwangu.
Siku moja nikiwa natoka shambani nikiwa nimechoka pamoja na njaa nikapita sehemu nikachimba Nsibu(viazi) nikaviweka mfukoni huku begani nikiwa nimebeba jembe.
Wakati naendelea na safari yangu ghafla mbele yangu alinitokea fisi akiwa ameachama na meno yake kama shoka, mdomoni anatoa udenda akanirukia.
Aliponirukia nilianguka mpaka chini ,kabla hajafanya chochote nilimkamata kwenye shingo ipasavyo mpaka nikamuona anaanza kulegea.
Baada ya kuona sina msaada wowote niliamua kumuachia, liwe na liwalo maana nguvu niliishiwa, nilijaribu kulegeza mikono yangu ghafla nikamuona anajichomoa kwa nguvu na kukimbia kusikojulikana.
Niliinuka taratibu huku nikiwa nimechoka ,nguo yangu imechanika kwa kuburuzwa na makucha ya fisi, nikajipangusa na kuelekea nyumbani.
******
Siku moja nikiwa kwenye mgahawa nikijaribu kupunguza mawazo kwa kutumia kinywaji cha kilevi, ghafla nikasikia sauti ya Sheila nikageuka na kumwona kipenzi changu Sheila akiwa na kijana wameshikana mabega na kuegemeana
Sheila akaniambia.....
"TIMOTH NAJUA UNANIPENDA SANA LAKINI KUMBUKA KUWA MIMI NIPO DUNIA NYINGINE ISITOSHE NINA MPENZI MWINGINE. SASA BASI, NAKUOMBA USIWE UNANIWAZA NA KUNIFIKIRIA MAANA UNANIPA WAKATI MGUMU SANA KWA VIONGOZI WANGU"
Baada ya kumaliza kuzungumza Sheila aligeuka na kuondoka na kijana aliyekuja naye.
Nikabaki nashangaa kilichotekea na kuanza kufikiria jinsi ajali ilivyoweza kutokea nikiwa na mpenzi wangu sheila na kuweza kupoteza maisha baada muda mfupi, lakini leo hii namwona na Sheila akiwa mzima hana hata kovu moja.
Sikuwa na hamu ya kuendelea kukaa kwenye mgahawa niliinuka na kuelekea nyumbani nikiwa nimetawaliwa na mawazo.
Nilifika moja kwa moja nyumbani na kulala usingizi mzito.
Nikaanza kumkumbuka sheila na kuanza nikikumbuka mazuri aliyokuwa akinifanyia , nilishangaa sana baada ya kumuona bibi yake na Sheila akija kwa kasi sehemu tuliyokaa na Sheila.
Nilizinduka kutoka usingizini na kujikuta nikitokwa na jasho mwili mzima, kufumbua macho yangu sikuamini nilichokiona mbele yangu, alikuwa ni Sheila sikujua amepitia wapi wakati mlango umefungwa?.
Aliniamurisha na kunisonta kwa kidole na kusema "TIMOTH KAMA UNANIPENDA NIFUATE" niliinuka taratibu na kumfuata Sheila huku nikiongozwa na kidole chake.
Tulitembea umbali kama mita 100 kutoka nyumbani na kufikia kwenye mbuyu mkubwa.
Nilishangaa kuwakuta watu mbali mbali akiwemo bibi yake Sheila, kilichonishangaza sana ni kuona watu kutoka kijijini kwetu wengi wao ni wachawi akiwemo na shangazi yangu.
Bibi yake Sheila alisema " NILIKUONYA KUWA ACHANA NA SHEILA HUKUNISIKIA SASA UTAKUWA NA SHEILA SIKU ZOTE HUKU KUZIMU".
Kusema ukweli nilishangaa sana kuwaona watu mbalimbali kutoka kijijini kwetu kuwa ni wachawi mpaka wanaume!!!?, kilichonishangaza zaidi kuona mkubwa wa wachawi ni diwani wa kata yetu.
Shangazi ambaye pia naye ni mchawi alisema kabla sijaenda kujumuika na misukule wenzangu inanibidi nirudi nyumban kwetu nikashuhudie jinsi mazishi yangu yanavyofanyika.
Bibi yake Sheila alinichukua na kunipaka dawa mwili mzima tukaondoka kurudi nyumbani haikuwa mbali sana.
Baada ya dakika 2 tukafika nyumbani ,nilishangaa sana kukuta watu wamejaa nyumbani huku vilio vimetanda ikiwa sehemu nyingine wanachimba shimo.
Nikaingia moja kwa moja mpaka chumbani kwangu na kukuta gogo likiwa kitandani kwangu likiwa limefunikwa shuka.
Nilipoangalia pembeni yangu nilimuona mama yangu akiwa analia mpaka nilimuonea huruma, nilimfuata na kumuita lakini hakuweza kunisikia, nilijaribu kumgusa lakini hakuweza kuhisi chochote.
Niliondoka na kutoka nje na kuona watu wakizidi kulia, kilichonishangaza zaidi ni kuwaona wachawi walioniteka pia na wao wamejumuika na wanatoa kilio cha nguvu.
Baada ya kaburi kumalizwa kuchimbwa nilishuhudia wazee wa kijiji akiwemo diwani wa kata wakiingia kwenda kuchukua mwili wa marehemu.
Mwili wa marehemu ulifika sehemu husika tayari kwa kuagwa, vilio vilitanda sana nilishuhudia mama analia mpaka akapoteza fahamu.
Mzee mmoja alitangulia shimoni kwa ajili ya kuupokea mwili wa marehemu na kuupumzisha shimoni.
Vijana walichukua makoleo na kuanza kufukia shimo kwa fujo huku wakipokezana, nilishikwa na huzuni sana kuona wakizika gogo wakati mimi ni mzima, niliamua kujitumbukiza kwenye kaburi lakini nilishangaa sana kuona kila mchanga ulivyozidi kujaa shimoni na mimi ndiyo nilizidi kupandisha juu mpaka nikawa nje juu ya kaburi.
Baadaye bibi yake na Sheila alinifuata na kunishika mkono nikashtukia tayari nipo kambi ya wachawi na kupelekwa kujiunga na misukule wengine.
Maisha ya gamboshi nikayaanza, Sheila ndiye alikuwa mwenyeji wangu alijaribu kunielewesha mambo mengi sana.
Aliniambia kazi ya misukule ipo ya aina mbili kuna misukule kwa ajili ya nyama na misukule kwa ajili ya kulima mashamba ya viongozi wa wachawi.
Ukiwa mzembe wa kulima unaliwa nyama, ila mara nyingi wanaoliwa ni misukule kutoka mjini maana wazembe wa kulima.
Tukiwa tunazungumza na Sheila, kijana mmoja alikuja na kuniambia ninaitwa, nilienda kumkuta mkuu wa wachawi ameshikilia kisu kikali na kuniamrisha niachame mdomo ili aweze kukata ulimi wangu.
Sikuwa na kipingamizi nilinyanyua mdomo na kuomba sala ya mwisho, kabla sijaachama mkuu wa wachawi aliitwa akaondoka na kuniacha nikiwa nimesimama.
Baada ya muda mchawi mmoja alikuja na kuniambia niondoke, nilienda moja kwa moja mpaka kwa Sheila, kilichonishangaza nilimkuta Sheila akilia.
Aliinuka na kunikumbatia na kuniuliza vipi hawajakudhuru?, nilimjibu hawaja nidhuru.
Sheila alinipa njia nyingi za kujikinga ili wasinidhuru, alichonisisitiza zaidi nisiwe mwepesi wa kukubali haraka kitu wanachoniambia.
Kengere iligongwa na wote tulijumuika na kuamrishwa kuchukua majembe kwa ajili ya kulima, tulikusanyika wote kwa pamoja na kuamrishwa kufumba macho, na baada ya muda mfupi tukafumbua tukiwa kwenye shamba husika kwa ajili ya kulima.
Baadaye tuliamrishwa kuanza kulima, nililima kwa juhudi sana ili nisiweze kuchaguliwa kwa ajili ya kuliwa nyama maana mzembe analiwa nyama.
Baada ya muda kidogo kiongozi alikuja na kuteua vijana watano nikiwemo mimi na Sheila na wengine watatu ila wenzetu walikuwa tayari wamekatwa ulimi hawakuweza kuongea tena.
Alituamuru tufumbe macho,tukafanya kama tulivyoamriwa, ghafla tukafumbua tukiwa mbele ya mama moja mchawi akaanza kutueleza alichokuwa anataka kutoka kwetu.
"Samahani vijana wangu leo nataka tufuate nguvu kazi nyingine, nataka niwaongezee mume wangu maana naona siku hizi ameanza kuleta kiburi kwa sababu ya mali zake, mume wangu ni dereva wa magari, kinachotakiwa ni kumuangusha mfano wa ajali",alisema mchawi huyo.
Sikuwa na swali la kuuliza nikabaki nashangaa, kweli leo hii mimi nimekuwa msukule wa kusababisha kifo!!!!!????? Nilijiuliza kimoyo moyo, baada ya muda mfupi mama alituamuru tufumbe macho.
Tuliweza kufumbua macho yetu, sehemu tulipokuwa sikuweza kuitambua hata kidogo, tuliweza kufikia kando kando ya barabara, alituamrisha tumfuate, tulipofika katikati ya barabara alituamru tusimame na tupange msitari mmoja.
Alituonya tusitoke kwenye mstari hata kugeuka, ghafla nilishuhudia gari moja iliyokuwa inakuja mbele yetu aina ya scania.
Scania ilipokaribia ,mwenzetu mmoja aliogopa sana na kuruka nje ya barabara kulingana na kasi ya gari iliyokuwa imetulenga kutugonga, lakini upande wangu nilifumba macho na kumshikilia Sheila ,maana yeye sio mara yake ya kwanza kuangusha magari kwa mtindo huo.
Mama alikuja na kutushukuru pia kutuwekea dawa machoni, na kutuambia mwangalieni mpumbavu mwenzenu ,upumbavu alioufanya.
Kweli niliweza kushuhudia magari mawili aina ya Scania na katapila ambayo ilikuwa ikifanya marekebisho ya barabara, kwa jinsi nilivyoweza kushuhudia kwa macho yangu niliona kama Scania imepotea njia na kujigonga kwenye katapila.
Scania iliharibika sana maana ilijikunja kiasI kwamba dereva alibanwa na kuweza kufumuka tumbo, sehemu zote zilizokuwa karibu na eneo la tukio zilitapakaa damu maana utumbo wote ulifumuka.
Wanakijiji walijaa sana kwenye eneo la tukio kuna wengine waliweza kumsogelea msukule aliyejirusha na kujaribu kumhoji kwa nini yupo hapo, lakini kwa vile msukule alikatwa ulimi hakuweza kuzungumza chochote, nilishudia wananchi wenye hasira kali waliamuru auawe maana yaweza kuwa ndiye msababishi wa ajali.
Kweli kuna wengine waliweza kufuata mafuta ya taa na kuumwagia mwili mzima na kuwasha moto, kweli aliteketea mwili mzima na kuchimbwa shimo fupi na kufukiwa.
Mama alituambia siku na sisi tumefanya upumbavu kama alioufanya mwenzetu pia tutasurubiwa kama tulivyomshuhudia mwenzetu, niliogopa sana.
........*******........
Kulingana na jinsi alivyoweza kubanwa na vyuma mbalimbali vilivyokuwemo ndani ya gari haikuwa rahisi kwa wanakijiji kuweza kuutoa mwili wa dereva huyo ndani ya gari.
Kilichofanyika ni kutoa kiungo kimoja baada ya kingine na kukiweka kwenye mfuko, sehemu yote ilitapakaa damu na watu wenye roho za huzuni hawakuweza kushuhudia tikio zima waliondoka.
Baada ya tukio zima kulishuhudia, mama alikuja na kutupaka dawa machoni na kututambulisha kuwa tuliyekuwa tunamfuata ni huyu hapa, alikuwa mbaba wa makamo kama miaka 40-45.
Pia alituamuru tufumbe macho, baada ya muda akatuambia tufumbue macho.
Nilishangaa sana kwani sehemu tuliyofikia sikuweza kuitambua hata kidogo baada ya kama dakika 3 kupita nilishuhudia fisi mkubwa wa mabaka mabaka akija kwa kasi ya ajabu sehemu tulipo huku akiwa ameachama akitoa muungurumo pamoja na udenda mdomoni.
Alikuja mpaka sehemu tuliyosimama akapiga breki kwa kasi mpaka vumbi ikatokea, fisi aliposimama aligeuka na mama tuliyekuwa naye akapanda na kugeuka kwa nyuma huku akishikiria mkia wa fisi na kuondoka sehemu tulipokuwa kwa kasi ya ajabu.
Tukiwa tumebaki watatu ghafla ulikuja upepo kwa kasi na kuanza kutupeleka kusikojulikana, pia uliweza kututenganisha na wenzangu, nilienda kujigonga kwenye mti na kuzimia.
.........*****......
Nilikuja kuzinduka nikiwa sina jeraha hata kidogo, nikiwa nimekaa na wenzangu(misukule) tukiwa makundi mawili mbele kuna viongozi wa wachawi wakionesha nyuso za tabasamu kila mmoja.
Niligeuka pembeni yangu na kumuona Sheila akiwa amekaa kwa huzuni, nikamuuliza hapa tunafanya nini? Sheila alinijibu hapa ndipo sehemu ambayo watu hupikwa na kuliwa.
Nikiwa bado nashangaa nikanyanyua macho yangu kwa juu na kushuhudia moto mkubwa ukiwa unawaka na watu nikiwaona wanahangaika wakijaribu kujiokoa lakini walishindwa, wakiinuka wanaanguka na kubaki wakigaragara.
Nikamtazama Sheila ambaye alikuwa mwenyeji wangu, nikamuuliza juu kuna nini? Sheila alinijibu hawa wote wachawi wakifa huenda huko na kuteketezwa kwa moto.
NIiliendelea kumuuliza kwa hiyo huko ni kuzimu? Sheila hakunijibu alibaki akiniangalia na kuninyoshea kidole kuwa nisiendelee kumuuliza maswali kwani mkuu alikuwa anakuja.
Mkuu ambaye alikuwa diwanI kutoka kata yetu akasimama huku akionekana akiwa na tabasamu.
Niliweza kumshuhudia akinyosha kidole chake cha mkono wa kulia nikiwa nashangaa kipi anachofanya, nilishuhudia vumbi kwa wingi likijaa sehemu tuliyokaa, ghafla vumbi likatoweka na kushuhudia miamba 3 ya mawe ikishuka kutoka juu kwa kasi na kutua chini huku juu yake kulikuwa na masufuria yakiwa yamejaa maji.
Mkuu alinyosha tena kidole chake kama awali, miamba yote ilipasuka na moto mkali ulitokea na baada dakika 5 maji yaliyokuwa kwenye masufuria yalichemka asilimia 100%.
Mkuu alinyosha mkono wake na panga kali likatua mkononi mwake, aliweza kumfuata msukule mmoja ambaye tulimfuata kwenye ajali iliyotokea barabarani siku za nyuma.
Aliweza kumshika mkono na kuuvuta na kuunyanyua mkono wake ulioshikilia panga kali na kuukata mkono na kuutupia kwenye sufuria lenye maji yaliyochemka.
Alipomaliza kuukata mkono wa kushoto alimalizia na mkono wa kulia kisha akafyeka kichwa chake na kukidumbukiza kwenye sufuria tofauti, alimalizia kwa kukatakata miguu na kiwiliwili na kukidumbukiza vyote kwa pamoja kwenye maji yaliyochemka.
Watu 6 waliweza kupikwa siku hiyo, baada ya dakika 10 nyama zilikuwa tayari zimeiva na kisha kuipuliwa.
Tuliamrishwa kukaa makundi ya watu wanne wanne kama kawaida yetu mimi na Sheila tulikuwa pamoja baada ya muda kidogo nilishuhudia wali ukitua katikati yetu sikujua umepikwa saa ngapi?.
Sufuria la nyama za binadamu lilikuja huku likiletwa na bibi mmoja na kutuamrisha kila mmoja wetu ale nyama ya binadamu.
Nilijiuliza maswali mengi sana lakini sikupata majibu, bora waniue kuliko kula nyama ya binadamu.
Baada ya muda Sheila alifuatwa, na kubaki watu watatu kwenye kundi letu ,wenzangu waliendelea kula lakini mimi nilibaki nashangaa jinsi wanavyokula nyama ya binadamu bila hata aibu.
Nikiwa nimekaa, bibi mmoja alikuja na kuniuliza kwa nini hauli?, niliendelea kumwangalia bila kumjibu chochote.
Bibi aliondoka,lakini baada ya dakika 3 wachawi watatu walikuja, akiwemo na bibi wa awali na wanaume wawili, mwanaume mmoja aliniuliza, kwanini hutaki kula?, sikumjibu nilibaki namkodolea macho.
Waliniamrisha nisimame na kuwafuata sehemu wanayokwenda, walinipeleka mpaka kwa mkuu wa wachawi, nilifika nikasimama mbele yake alinitazama kwa jicho kali sana.
Kisha akaagiza bakuli lililojaa nyama na kuniamrisha nile, sikuweza kufanya alivyotaka nilibaki namtumbulia macho kama mjusi kabanwa mlango.
Kama alivyonifundisha Sheila kwamba nikiwa na kiburi hawawezi kunidhuru pia nisiwajibu chochote, mkuu aliamuru nipelekwe shambani kulima siku nzima peke yangu kama adhabu.
Sikuwa na kipingamizi niliweza kulima siku nzima ilipofika jioni walinifuata na kunirudisha kambini kujumuika na misukule wenzangu.
Asubuhi kama kawaida tuliamka na kupangiwa kila mtu sehemu ya kwenda mfano kulima, kusababisha ajal barabarani na wengine kubaki kambini.
Ilipofika zamu yangu nilipangiwa kufuata mtoto mchanga hospitalini nikiongozwa na mama mmoja wa makamo.
Sikuwa na kipingamizi maana ilikuwa kama mojawapo ya adhabu yangu niliyopewa na mkuu.
Tukiwa tunajiandaa kuondoka nilimuona Sheila akiwa peke yake ,nilimfuata, kabla sijazungumza kitu chochote aliniuliza umepangiwa wapi leo?
Nilimjibu kwenda hospitali kuchukua mtoto mchanga.
Sheila aliniangalia kisha machozi yakaanza kumtoka,nikamuuliza Sheila vip?, Sheila aliniangalia kisha akajifuta machozi na kuniambia wengi wanaokwenda hospitali huwa hawarudi wakiwa hai.
"Hospitali zilizo nyingi zimeimarika kwa kutumia jina la mungu, pia na wewe na hofia kama utarudi salama?",alisema Sheila
Nilijiuliza maswali mengi sana juu ya maneno aliyoniambia Sheila, lakini nitafanyaje wakati nipo chini ya wakuu?
Cha msingi kilichobaki ni kumuomba mungu yasije yakanitokea kama yanavyowatokea wenzangu.
Muda wa kuondoka kuelekea hospitai ulifika, mama yule yule tuliyeangusha naye gari aliniita na kuniambia nifumbe macho, na endapo nitafumbua macho katikati ya safari ndiyo utakuwa mwisho wa maisha yangu.
Baada ya kama dakika 1 na sekunde 45 mama aliniamuru nifumbue macho, nilipofumbua ,kusema ukweli sikuweza kutambua hospitali tuliyofikia ni hospitali gan?, maana ilikuwa ngeni upande wangu.
Mama alinipa dawa nyingine za kuweza kupaka katika sehemu zangu za mwili ikiwemo miguuni kwenye nyayo, baada ya hapo akanipa nyingine ya kunawa mikononi baadaye akaniambia nifuate nyuma yake, huku akinipa sharti la kutokugeuka nyuma.
Tuliweza kutembea mpaka wodi ya watoto wachanga huku mama akiniongoza, tulipofika tulikuta wanawake pamoja na manesi, ndani ya wodi kulikuwa na vitanda 4 ,vitanda 3 vilikuwa na watoto wachanga waliotoka kuzaliwa muda si mrefu.
Mama aliniambia tutoke nje tena, sikujua nje tunaenda kufanya nini tena?
Nilijiuliza moyoni, tulipotoka nje mama alinishika bega langu la kulia na kusema.....
"Mwanangu kati ya mitihani uliopewa huu ni mgumu kuliko mitihani ya mwanzo, sasa basi utaenda wodi tuliyotoka ukachukue kichanga kimoja, kabla hujakichukua ukiona mkono wako unapigwa shoti pindi unamchukua mtoto usiendelee badilisha kitanda".
Kweli nilifanya kama nilivyoelekezwa na mama, nilipoingia wodini nilikuta akina mama watano akiwemo na nesi mmoja.
Nikapiga hatua mpaka kwenye kitanda cha mtoto, nilipofika nikanyanyua mkono, kabla sijamfikia mtoto,nilihisi kama nimeingiza mkono kwenye mkaa wa moto.
Nilishindwa kujizuia nilipiga kelele kama mtoto mdogo na kuruka nikajibamiza kwenye ukuta wa wodi hiyo.
Watu wote waliokuwemo ndani ya wodi walisikia kelele, cha kushangaza mtu aliyepiga kelele hawamuona.
Bila kupoteza muda nesi alichukua bibilia na kuanza maombi.
Wakati anafanya maombi ,alipotaja jina la yesu mwili wangu wote ulitetemeka na kasi ya maumivu iliongezeka mwilini n akujiona kama nimo ndani ya jiko la mkaa wa moto.
Nikashuhudia kasi za maombi ndani ya wodi ikiongezea pia na mimi fahamu ilizidi kunitoka mwilini, ghafla niliona mwanga mkali ukinimulika nikajikaza kuutazama.
Niliona kama mkono wa mtu upo nje ya chumba nilijitahidi kuushika mkono mpaka nikafanikiwa kuushika na ulinivuta kwa kasi, nikatoka nje na maumivu ya mwili yaliongezeka zaidi ya mwanzo.
Nilifumba macho kwa maumivu niliyokuwa nayapata mwilini na fahamu zikanitoka sikuweza kujua tena kilichoendelea.
Baadaye nilikuja kuzinduka nikiwa nina makovu mwili mzima, nikatazama pembeni yangu nikaliona joka kubwa likiwa na vichwa vinne na kila kichwa kina mapembe mawili.....
SIMULIZI ITAENDELEA....
 

jumanne12

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
281
250
Da mtu wangu umenitahidi sana kuonyesha hisia zako lakini wewe unaishi maeneo gani? 1 maganzo 2 bairadi utemini kolandoto 3masagala 4songwa au unaishi gamboshi maana tangia nizaliwe sinapata mtu wa aina yako kumbe hata mchana kuna giza wadanganye hao vipofu wenzio mi nooooooo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom