Simulizi ya kweli kuhusu Gamboshi

SEHEMU YA 03

Ilipoishia..…..
Tukiwa kwenye mazungumzo na Sheila ,mama mmoja alikuja kunichukua na kwenda sehemu husika ya kupikia watoto, nilikuta moto mkali ukiwaka huku juu yake kuna sufuria lililo chemka mpaka linakuwa jekundu.
Mama huyo aliniletea kitoto kichanga kikiwa hai na kuniamuru nikitupie ndani ya sufuria harafu nianze kukaanga mpaka nihakikishe yamekuwa mafuta ndani ya sufuria.
Endelea..........
Nikiwa nafikiria na kuwaza jinsi ya kuanza kumchemsha mtoto ghafla niliiona pete yangu ya mkononi niliyopewa na babu ikicheza na kubadilika rangi mara kijani, bluu na mpaka ikawa rangi ya dhahabu wakati rangi yake ni nyeupe.
Kwa kweli nilishikwa na bumbuwazi kama chizi fulani.
Nikamtazama mtoto, sura ya huruma ilinijaa usoni na mwili mzima kupooza.
Mama aliyenikabidhi mtoto alikuja na kuanza kunifokea akisema muda wote huo ulikuwa hujaanza kuchemsha????????? Unasubiri nini??? Hicho kiburi chako kitakuisha tu, unajifanya unajua sana!!.
Alinitukana matusi mengi sana kiasi kwamba uvumilivu ulinishinda, sura ya hasira ilinijaa usoni.
Mama huyo nilimfuata na kumshushia kofi takatifu la usoni mpaka akaanza kuona mchelemchele machoni mwake na kupiga kelele za kilio kama mama mjamuzito mwenye uchungu.
Kitendo cha kumpiga huyo mama nadhani ndiyo ulikuwa mwanzo wa mateso maana adhabu niliyopewa ni zaidi ya kifo, maana nilitamani kufa lakini ilishindikana lakini mungu alikuwa upande wangu.
Mkuu wa wachawi alinifuata kwa hasira huku akihema kama mwanariadha amemaliza kukimbia mbio za marathoni, alinifuata sehemu niliyokuwa nimesimama na kunirushia ngumi ya kichwani.
Nikajisemea moyoni liwalo na liwe .
Mkuu wa wachawi nilimkwepa na ngumi yake kutua ukutani.
Alikasirika sana na kuweza kunyoosha mkono wake wa kushoto ghafla alianza kubadilika sura na kuwa joka la ajabu.
Niligeuka nyuma ili niweze kukimbia angalau niweze kujiokoa lakini nilishangaa kuona mlango uliokuwa wazi umejifunga na pia nilishindwa kukimbia kwani nilianguka papo hapo kama gunia lililojaa mchanga.
Sikuwa na nguvu za kukimbia, ghafla joka la ajabu lilianza kunifuata.
Kusema ukweli sikuwa na nguvu za kuinuka, nilikumbuka kuwa nina pete ambayo ilikuwa ikinisaidia kipindi cha nyuma lakini nilishanga kutokuiona tena pete hiyo niliyopewa na Babu ili iweze kunisaidia.
Joka lilikuwa likinisogelea kwa kunifuata kichwani na mpaka likanifikia likaanza kuninusa nusa.
Wakati linafanya hayo yote nilikuwa nimelowa mkojo na kinyesi kilikuwa kinanitoka mithili ya mbuzi anachinjwa kwa kuning'inizwa kwa kamba juu ya mti.
Joka lilisogea karibu yangu na kunitemea mate machoni mwangu.
Nililia kama mtoto mdogo maana maumivu niliyokuwa nayapata ni kama umeweka pilipili sehemu za siri.
Nilibebwa na kupelekwa kusikojulikana maana nilikuwa sioni, macho yangu yaliziba na kuwa kipofu.
Nilipelekwa sehemu ambayo nilihisi kama nimeingizwa kwenye handaki.
Nilipofikishwa hapo ghafla nilianza kuhisi joto na mwili mzima kuniwasha.
Mara nikaanza kusikia harufu ya damu ya binadamu na kusikika sauti ikisema omba sara ya mwisho.
Kabla sauti haijamalizika nilisikia kishindo kikitua mbele yangu, baada ya muda kidogo nilipokea kofi takatifu la usoni ambalo lilinipeleka mpaka chini ambapo niliweza kuangukia kwenye moto.
Itaendelea sehemu ya 4
 
SEHEMU YA 04

Ilipoishia...........................

Endelea....................
Baada ya kupokea kofi takatifu nilipoteza fahamu sikuweza tena kujitambua kutokana na maumivu ya moto niliyoyapata.
Nilikuja kuzinduka nipo chini ya mti nikiwa na Sheila akiwa ananihudumia huku mwili wangu ukiwa umepakwa dawa za majani mabichi yaliyopondwa hasa sehemu niliyoungua moto.
Nikiwa najisikia maumivu nilimtazama Sheila kwa huruma na kunyanyua mkono wangu wa kuume, naye Sheila aliupokea.
Nikamuuliza "Nimefikaje hapa? Na wewe umenionaje?"
Aliuchukua mkono wangu taratibu!!!!!! Huku machozi yakimtiririka na kisha alinisogelea na kunikumbatia huku akitabasamu na kusema...
"Timothy amini usiamini nimekuhudumia siku tano bila ya wewe kujitambua siamini leo umezinduka!!" .
Sheila alipomaliza kunieleza alinikumbatia tena kwa furaha, nikamuuliza hapa nimefikaje??
Sheila alinyamaza kwa muda kisha akasema
"Ni stori ndefu sana, siku moja nilikuwa nimekaa na misukule wenzangu babu mmoja alinitokea na kuniuliza Timothy unamfahamu???
Nikamjibu ndiyo namfahamu akaniambia leo ni siku ya pili amepoteza fahamu tena alienda kutupwa baada ya kugundulika kuwa alikuwa amekufa, nilishtuka na kumuuliza yupo wapi?????
Babu alinichukua na kunileta mpaka hapa ulipo na kuanza kukata kata majani na kuyaloweka mwenye maji na mengine nikakupaka mwilini mwako".
Wakati Sheila anaendelea kunisimulia ghafla nyoka mkubwa alikuja sehemu tulipokuwa tumekaa na Sheila.
Kadri nyoka huyo alivyokuwa anatusogelea Sheila naye alizidi kuondoka na kuniacha peke yangu maana mimi nilikuwa bado sijapata nguvu za kutosha.
Nyoka alipanua mdomo wake na kunitemea mate mwili mzima, nilipiga kelele kutokana na maumivu niliyokuwa nayapata, ghafla nilipata nguvu na kunyanyuka na kukimbia huku nikiendelea kupiga kelele.
Ghafla mbele yangu Babu alitokea na kuanza kunicheka, nilipogeuka nyuma nyoka sikumuona tena.
Babu nilimuuliza nyoka yupo wapi?
Babu akatabasamu na kusema ina mpaka sasa hujanizoea tu????.
Babu akasema sikia kijana mpaka kufikia hapo nimetumia nguvu zangu binafsi, kwanza macho yako nimeyatengeneza kwa kutoa upofu uliokuwa umepewa na kisha kumleta Sheila aje akuhudumie.
Babu nilimuuliza,mbona pete yangu siioni?
Babu akajibu pete niliichukua kwa sababu nilihofia mkuu wa wachawi angeichukua maana nguvu alizokuja nazo sio za kawaida.
Wakati naongea na Babu,Sheila alikuwa amesogea karibu yangu na yote aliyokuwa anayasema Babu aliyasikia.
Ghafla kilitokea kimbunga kilichoambatana na upepo mkali na vumbi, baada ya muda Babu alinishika mkono wa kushoto na kunivalisha pete.
Baada ya muda babu alipotea na kutoweka kimiujiza.
Dakika chache mkuu wa wachawi alitokea mbele yetu na kunyanyua mkono wake huku akitusonta kidole, tulijikuta tumefika kambini.
Kama kawaida tukajichanganya na misukule wenzetu na stories zikaanza kuchukua nafasi yake na masela (misukule) ambao ni wageni bado ndimi zao hazijakatwa.
Nilishangaa kumuona mkuu wa wachawi akija sehemu tuliyokuwa tumekaa na moja kwa moja mpaka sehemu nilipokuwa nimekaa akanishika mkono na kuondoka naye.
Tuliondoka na kuingia porini, mbali kidogo na kambi, tulifika sehemu kulikuwa na mti mdogo
tulisimama.
Mkuu alisema "kijana una nyota kali sana haijawahi kutokea kwa mtu nimemuua aje apone?!! Kama ulivyofanya wewe , sasa basi nitakachokuambia naomba ufanye".
Babu alinyoosha mkono wake na shoka kali likatua mkononi mwake na kuniamuru nichukue shoka.
Shoka nillilichukua nikalishikilia. Mkuu aliniambia nigeuke nyuma yangu na kuniamuru niukate mti ambao tulikuwa tumesimama nikamjibu kwa kujiamini HAKUNA TABU MKUU!!!!!!!!!!!!!!!!.
Mti niliusogelea na kujitemea mate mkononi na kuishika shoka kisawa sawa nikainyanyua kwa nguvu zangu zote na kuliachia kwenye mti.
Duh!! kabla shoka halijatua nilishaanga kuona sura ya mama wakati nilimuacha nyumbani.
Itaendelea sehemu ya 5
 
SEHEMU YA 05

| Powered by Malunde
Tangaza biashara yako hapa, kwa kubofya hapa
← Newer Post Older Post →
Home
Utamaduni Lake Zone_HII HAPA SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU "GAMBOSHI"
Kurasa za mwanzo na mwisho magazetini leo October 01 2014
Utamaduni Lake Zone_SIMULIZI YA KUTISHA KUHUSU "GAMBOSHI" LEO SEHEMU YA 3
ULIIONA SIMULIZI YA KUTISHA YA GAMBOSHI SEHEMU YA TATU? KAMA HAPANA,IKO HAPA
Utamaduni Lake Zone_ SEHEMU YA PILI-SIMULIZI YA KUTISHA KUHUSU "GAMBOSHI"
 Saturday, October 25, 2014
 utamaduni lake zone
Kama tulivyoawaahidi kuwaletea simulizi mbalimbali kuhusu kanda ya Ziwa Victoria,kupitia ukurasa/kipengele chetu kipya cha" UTAMADUNI LAKE ZONE" ,angalia juu kwenye blog,kila siku za Jumamosi ,leo Malunde1 blog inakuletea sehemu ya TANO ya simulizi ya kusisimua kuhusu Gamboshi
BONYEZA HAPA KUSOMA SIMULIZI YA "GAMBOSHI" SEHEMU YA 4,3,2 NA1
SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU GAMBOSHI SEHEMU YA5
Mtunzi; Timotheo Mathias
MAZINGIRA; Shinyanga vijijini.
Simu yake- 0765676242 (WhatsApp)
timotheomathias0@gmail.com
Maana ya maneno yaliyotumika kwenye simulizi
-GAMBOSHI ni makazi au eneo linalotumika kuhifadhia misukule.
- MSUKULE ni mtu aliyechukuliwa kwa njia ya kishirikina (kichawi) akiwa mzima (hai), lakini kwa upeo wa kawaida ni dhahiri kuwa amekufa
Ilipoishia...........................
Mkuu alisema "kijana una nyota kali sana haijawahi kutokea kwa mtu nimemuua aje apone?!! Kama ulivyofanya wewe , sasa basi nitakachokuambia naomba ufanye".
Babu alinyoosha mkono wake na shoka kali likatua mkononi mwake na kuniamuru nichukue shoka. Shoka nillilichukua nikalishikilia. Mkuu aliniambia nigeuke nyuma yangu na kuniamuru niukate mti ambao tulikuwa tumesimama nikamjibu kwa kujiamini HAKUNA TABU MKUU!!!!!!!!!!!!!!!!.
Mti niliusogelea na kujitemea mate mkononi na kuishika shoka kisawa sawa nikainyanyua kwa nguvu zangu zote na kuliachia kwenye mti.
Duh!! kabla shoka halijatua nilishaanga kuona sura ya mama wakati nilimuacha nyumbani.
Endelea...........................
Nilipoiona sura ya mama shoka niliizuia na kuiachia chini na kukaa chini ya mti huo.
Nikiwa nimekaa chini nilianza kuwaza kilichonitokea kwa muda huo mfupi, kwani nilikumbuka kuna siku ambayo msukule aliagizwa kukata mti na mti uligeuka kuwa mama yake lakini yeye aliukata kutokana na shinikizo la mkuu.
Baada ya siku moja msukule alipelekwa nyumbani ili kushuhudia mazishi ya mama yake na mimi nilikuwa mojawapo ya msukule tulioenda kushuhudia mazishi hayo.
Baada ya kufika tulikuta watu wakilia wengine wakiwa wamezimia baada ya marehemu kufa kwa kukatika tu, wakati jana yake alikuwa mzima.
Kwa upande wetu sisi haikuwa rahisi wao kutuona hata kutusikia maana tulikuwa tumepaka dawa machoni na mwili mzima.
Tulishuhudia mazishi yakifanyika huku wakiwa wanazika gogo na mwili wa marehemu kuuacha ndani ya nyumba ukiwa hai.
Walipomaliza kuzika Gogo,tuliingia ndani ya nyumba ili kumchukua mtu wetu, tulipoingia ndani bibi tuliyeenda naye alimuita marehemu jina lake na kuitika.
Baada ya hapo alichomoa fimbo yake aliyokuwa ameichomeka kiunoni na kumpigia mgongoni kisha kumshika mkono na kuanza kutoka naye nje.
Wakati tunatoka nje tukiwa na mtu wetu mama mmoja alituangalia sana mpaka tukahisi kama ametugundua na anatuona.
Kiongozi wetu ambaye ni bibi alisema huyu mbona anatuangalia sana? "Hebu ngoja tuhakikishe kama kweli anatuona".
Bibi alinyanyua mkono wake juu, ghafla mshale ulitua mkononi mwake na tukashuhudia fisi mkubwa wa madoa madoa meusi na meupe, mbele yetu kama kawaida yake mbele mrefu nyuma mfupi.
Fisi huyo alikuja kwa kasi ya ajabu hadi tulipokuwa tumesimama kisha akafunga breki huku akisindikizwa na vumbi la kutosha nyuma yake.
Bibi alipanda juu ya fisi na kushikilia vizuri mshale wake na kumwamru fisi aondoke kwa kasi huku fisi akimlenga yule mama tuliyehisi anatuona.
Baada ya yule mama tuliyehisi anatuona kuona fisi anakuja anaenda upande wake huku akilengwa ,alianza kupiga kelele huku akikimbia ovyo na kuwafanya watu waliokuwepo kwenye mazishi wakibaki midomo wazi wasijue kilichotokea huku wakimshangaa.
Bibi aliweza kumpata na kumrushia dawa iliyomfanya awe bubu na kushindwa kuwaelezea alichokiona.
Bibi alirudi na wote tuliweza kuondoka kuelekea kambi, lakini huyo mama tuliyemchukua msibani alikakaa siku tatu tu na siku ya nne alichinjwa na kuliwa nyama.
Kuna siku nikiwa nimekaa nimejiinamia nikiwaza yote yaliyotokea mkuu wa wachawi alinifuata na kunishika mkono na wote tukaanza kurudi kambini.
Tulipofika Sheila aliitwa na bibi mmoja pia na yeye aliitwa kwa mkuu, mkuu alimwambia bibi kuwa mwezi ujao ni sikukuu itakayofanyika nchini Nigeria, na huko zinahitajika nyama laini kama wanafunzi wa shule za msingi na baadhi ya walimu wao.
Nimekuchagulia vijana shupavu na imara utawatumia katika mashule huko vijijini kuleta wanafunzi.
Mkuu alipomaliza alitukabidhi mabegi yaliyosheheni pipi, biskuti na hela za sarafu, tayari kwa safari kwenda kuleta roho za watu kama tulivyoagizwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom