FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 2,232
- 4,388
- Thread starter
- #421
STORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
********************
SEHEMU YA TISINI NA TATU
SONGA NAYO................
Zilipita dakika tano tangu tukio lile liweze kutokea ndipo Othman alikuwa anafika eneo la tukio akiwa kwenye mwendo wa kasi isivyokuwa kawaida. Alikuwa ana wasiwasi kubwa mno kwenye moyo wake kwani hakutamani jambo ambalo alikuwa analiwaza liweze kutokea. Alishuka kwenye gari ikiwa hata haijasimama vizuri huku akiwa anaita kwa sauti na kukimbia kwa sababu alikuwa anajua mahali ambapo walikuwepo lakini alikuwa amechelewa.
Aina ya mauaji ambayo aliyakuta lile eneo yalimsikitisha, alikagua kila gari hakuona mtu yeyote yule. Aliwagusa watu wale na kugundua kwamba miili yao ilikuwa ya moto bado kwa maana hiyo ni kwamba walikuwa wameuawa muda mchache tu uliokuwa umepita. Alikimbilia kila eneo la karibu na sehemu hiyo akiwa anaita kwa nguvu lakini hakuna kitu alifanikiwa kukipata. Alirudi kwenye eneo lile akaanza kuwakusanya wenzake ili awapakize kwenye gari na kwenda kuwazika kwa heshima, aliamini kwamba hawakustahili kufa vifo vya kikatili namna hiyo. Othman Chunga alipiga magoti kisha akapiga kelele kwa sauti kubwa sana kiasi kwamba kama kulikuwa na mtu wa karibu ndani ya lile eneo basi alimsikia vizuri kabisa bila tatizo.
*********
Usiku ulikuwa unazidi kuwa mzito, ilikuwa ni siku kwa ajili ya msiba wa mke wa raisi lakini mkuu wa majeshi alishiriki msiba huo kama vile alilazimishwa, hakuonekana kuwa mtu ambaye alikuwa anavutiwa nao sana jambo ambalo lilimshtua hata raisi mwenyewe, hakuwa akimwelewa vizuri mtu huyo, alihisi kulikuwa na jambo ambalo lilikuwa nyuma ya pazia na watu wengi hawakuwa wakilijua.
Alimpigia mtu huyo simu lakini simu yake ilikuwa inatumika, alichukizwa mno na jambo hilo, raisi mwenyewe hakuwa sawa kabisa tangu mchana wa siku hiyo aweze kumuona kiongozi wao hilo eneo, hakuona kama mambo yalikuwa sawa hivyo alihitaji kumdodosa mkuu wa majeshi ili kuona kama alikuwa na taarifa za kutosha aweze kumpatia kile ambacho kilikuwa kinaendelea. Alisonya na kumpotezea lakini wakati huo simu inaita mkuu wa majeshi alikuwa anaelekea nyumbani kwake, hakuwa kinyonge kiongozi huyo bali alikuwa akilindwa na makomando tisa kila anako tembea kwa sababu aliambiwa kwamba hakuwa salama.
Akiwa barabarani anatoka kwenye mizunguko yake alimpigia simu kijana wake kutaka kujua kama alikuwa wapi wakati huo na ndiyo wakati ambao raisi alikuwa anapiga simu hiyo hivyo ikamkutia akiwa anaendelea kuongea.
“Bashir uko wapi kwa sasa?”
“Nipo karibu na nyumbani kwako bosi, nimekuja kukusikiliza nafikiri ndani ya dakika kumi nitakuwa nimefika hapo”
“Safi, nina kazi ambayo nahitaji nikupatie mimi nafika ndani ya dakika kama ishiri zijazo kwahiyo unisubiri nje nafika mara moja”
“Sawa bosi”
Alimaliza kutoa maagizo kwa kijana wake mtiifu kisha akaikata simu hiyo na kuingia kuangalia simu zilizo ingia kipindi anaongea na simu hiyo. Alikutana na simu ya raisi, alisonya huku akiwa anaipiga. Mheshimiwa aliipokea huku akiwa na jazba kali, wote hao walijijua kwamba walikuwa ni vibaraka tu ni basi mmoja alikuwa na nafasi kubwa kumzidi mwenzake ila mwenye nafasi ndogo alitaka kuanza kujitengenezea ufalme wake bila mwenzake kujua wala kushtuka.
“Hello mheshimiwa” aliongea baada ya kupiga huku akiwa na sauti ambayo ilikuwa ya kujiamini kweli kweli.
“Naona siku hizi umekuwa na dharau kiasi kwamba unanisubirisha mimi kwenye simu?”
“Samahani kiongozi yalikuwa ni mambo yangu binafsi ila nadhani nimekupigia ili tuweze kuongea”
“Hivi unanionaje labda Medrick?”
“Sijakuelewa mheshimiwa”
“Namaanisha unanichukulia mimi kama nani kwako labda?”
“Wewe ni raisi wa taifa zima na ni bosi wangu pia kwahiyo nakuchukulia kwa uzito kama huo”
“Wote tunajua sio kweli, hakuna kitu unaheshimu kuhusu mimi”
“Hayo umesema wewe mheshimiwa”
“Whaaaaaat?”
“Unajua huwa unanidharau sana ila nimekuvumilia kipindi chote hiki hivyo kwa sasa sitakubali hizo dharau zako ziendelee kuwepo kwangu”
“Unajua unaongea na nani?”
“Naongea na Mr George, raisi wa Tanzania” raisi ni kama hakuwa anaamini kama alikuwa anaongea na mtu ambaye ni yeye aliyekuwa amemuweka kwenye hiyo nafasi”
“Kwahiyo umeamua kuionyesha rangi yako halisi kwangu sio?”
“Kama umesema hivyo ni sawa”
“Sitakusamehe katika hili Savato, nitakufanyia jambo baya ambalo hujawahi kufikiria kukutana nalo kwenye maisha yako yote”
“Una uhakika na jambo hilo George?” kwa mara ya kwanza bwana huyo alimuita raisi kwa jina lake bila kumpa hata ile heshima ya uheshimiwa, jambo hilo hata raisi mwenyewe lilimshtua kwa sababu mtu huyo alikuwa anaongea kwa dharau sana, haikuwa bure lazima kulikuwa na kitu kinampa hiyo jeuri.
“Kuna jambo ambalo unalijua na mimi silijui?”
“Sina uhakika, una ishu ya mhimu ya kuniambia George?”
“Ni kitu gani kinakupatia jeuri hiyo?”
“Hahahah hahaha kwamba unanitisha utanitoa kwenye hii nafasi? Huwezi kufanya hivyo bila kuwauliza wakubwa kwanza hivyo wewe mwenyewe ni kibaraka tu ambaye huwa unapenda kujificha kwenye mabawa ya hilo jumba jeupe ila huna lolote la maana ambalo unaweza kufanya kwa akili yako hivyo usije rudia kunitisha tena namna hiyo kwa sababu naweza nikafanya leo leo ukaondoka kwenye hiyo nafasi yako”
“Are you stupid?”
“Nisikilize George wewe ni miongoni mwa watu wapuuzi tu kuwahi kutokea hapa duniani, wewe ni mtu mjinga kwa sababu ulishindwa kujiongeza kabisa na kupiga hesabu zako vyema. Mimi nimekuelekeza alipo mlinzi wako na wewe umekurupuka kwenda kule bila kuumiza kichwa ukafanya ule ushenzi wako. Umefanya mwanamke amebakwa mbele ya mume wake kisha ukamuua mumewe tena ukitishia mpaka maisha ya watoto wake, unajua upuuzi wako uko wapi?
Kushindwa kujua kwamba lile eneo lilikuwa na kamera kila kona hivyo kila ulilo lifanya mle ndani mimi ninalo kwa video. Hivyo naweza kuamua kuisambaza video hiyo nina imani hautamaliza hata nusu saa hapo Ikulu kwa sababu hata mimi mwenyewe kama mkuu wa majeshi nitalazimika kutumia nguvu kukutoa. Hilo nimezungumzia kwenye uvunjifu wa katiba ya nchi, sasa umepiga mahesabu itakuwaje kama hii video ikifika kwa wakubwa? Kaulimbiu ya mhimu ni kwamba hautakiwi kuua watu wako, wewe umemuua mlinzi wako tena kwa kumdhalilisha, unahisi watakuacha? Jibu baki nalo mwenyewe.
Upumbavu wako mwenyewe ni kwamba nilikuingiza mkenge nawe ukaingia kwenye suala la kumuua mkurugenzi wa shirika la kijasusi la taifa na mpaka sasa wananchi hata hawajui, unajua hizi habari zikisambaa utakuwa kwenye hali gani wewe? Haya yote nayaongea kwa sababu nina ushahidi wake hivyo angalia kauli ambazo unaniambia mimi, nimeishika hatima nzima ya maisha yako hivyo kwa sasa utafanya kile ambacho nakitaka mimi na hii itabaki kuwa siri ya watu wawili baina yangu mimi na wewe na kama ukienda kinyume basi nitaachia ushahidi wote halafu nione utaishia wapi na hizo harakati zako za kipuuzi”
Raisi alitulia, raisi alinywea, angeongea nini tena mbele ya mtu huyo? Angefanya nini raisi wa Tanzania? Alibanwa kila kona, mwanaume huyo alimtafutia sanduku kwa akili ya muda mrefu naye akajiingiza humo. Mpaka wakati huo alikuwa chini ya mikono ya mkuu wa majeshi. Alichoka mheshimiwa.
93 inafika mwisho.
FEBIANI BABUYA.