Nimekukosea nini mheshimiwa mbona umeniandama sana?Mbaya zaidi ukaimalizia kwa habari mzee hasheem eti aende pangani.
Hapa umechemka sana
Umetisha sana mkuu, asante kwa kazi nzuri 🙏🏾STORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
********************
SUMMARY...............
**************
THE ODYSSEY OF GAVIN LucA
IDAIWE MAITI YANGU
Ilikutwa note book ndogo ambayo ilikuwa na maelezo mafupi ya safari ya maisha ya Gavin Luca. Kwenye hiyo Note book ndogo ambayo ilikutwa kulikuwa na maelezo mafupi yakiwa yanaeleza maana ya hiyo sentensi ambayo aliwahi kuwaachia ujumbe huo ndani ya msitu wa MAU huko Kenya.
Maana halisi ya maneno hayo matatu, alikuwa anawapa taarifa watu wake ambao alikuwa anawatafuta, kwa sababu walikuwa wanajua kwamba alishakufa, yale mauaji yote ya kikatili ambayo aliyafanya yeye, mambo yote ya kutisha ambayo aliyasababisha kwa kutumia mikono yake, alihitaji idaiwe maiti yake. Kwanini?
Kwa sababu ulimwengu uliwahi kujua kwamba amekufa muda mrefu maana yake yale yote ambayo yalikuwa yanatokea yeye hakuwa akihusika kabisa bali maiti yake ndiyo ambayo ilitakiwa kujibu. Maiti yake ndiyo ambayo ilitakiwa kudaiwa kwa matatizo ambayo yalitokea ndani ya taifa la Tanzania.
Safari ya maisha yake bwana huyu ilitoa funzo kubwa kwa kizazi hiki na miongoni mwa watanzania kwamba maisha ni mafupi muda mwingine kwa sababu ni wanadamu wanaamua kuyafupisha. Lakini kuna muda maisha yanakuwa marefu kama mtu akiishi kwa kufuata protocal (itifaki) huku akiwakumbusha watu kwamba “LIFE IS A GAME JUST OBSERVE THE RULES”
Safari ya maisha yake iliukumbusha ulimwengu kwamba malipo ya ubaya yanalipwa hapa hapa duniani na mara nyingi yanakuwa na matokeo mabaya. Gavin alitoa somo lingine la kutowapatia nafasi mbili wanadamu ambao hawastahili kupewa hizo nafasi kwa sababu kuendelea kuwalea kunazalisha matokeo mabaya kwenye maisha ya mwanadamu. Jishindie mechi zako mapema ili kupunguza majuto baadae.
Licha ya hayo mambo yote kutokea, Gavin Luca kwenye lile tukio ambalo lilitokea Kigamboni hata baada ya eneo lile kufukuliwa haukukutwa mwili wake. Mara ya mwisho alikuwa amejikita na kisu kwenye tumbo lake huku hali yake ikiwa mbaya isivyokuwa kawaida, sasa mwili wake ulienda wapi? Mimi na wewe hatujui.
Kwamba aliishi tena? Kama ni ndiyo, kwa sababu zipi wakati aliahidi kuyaondoa maisha yake?
Kama alikufa, mwili wake ulienda wapi? Ni kitendawili kingine ambacho kwa leo muda wangu unanitupa mkono kuweza kukitegua huenda tutakutana wakati mwingine tena kukipatia jawabu.
Yuko wapi babu yake mzee Hassan?
Ni nani ambaye alidaiwa kwamba alikuwa anazunguka naye kwenye ulimwengu wakati anatengenezwa kuwa kiumbe cha ajabu?
Mzee Hasheem alikuwa nani kwenye maisha ya Gavin kiasi kwamba akawa anaijua historia nzima ya familia hiyo? Na ni nguvu zipi ambazo mzee huyo alidaiwa kuwa nazo na wenzake kiasi kwamba wakaenda kufungwa ndani ya gereza la siri huko Tanga? Na kwanini afe kirahisi tu?
Vipi kuhusu familia ya Gavin Luca? Muda wote walikuwa wakiishi wapi! Hatima yao ilikuwa ni ipi baadae baada ya mambo yale yote kutokea?
Kuna uwalakini kwamba Othman alipotea na Sarah wakaenda kutengeneza familia bora mno, kama hilo lilitokea, ni nani alibaki kuilinda familia ya Gavin Luca?
Odhiambo Wambui, unalikumbuka hili jina si ndiyo? Huyu alikuwa ni mkurugenzi wa shirika la kijasusi la Kenya, alidai kwamba kuna wakati wake utakuja atahitaji Tanzania ilipie kwa sababu ya kuleta machafuko ndani ya taifa lake. Harakati zake ziliishia wapi? Kwamba alipotezea? Hapana sio kirahisi hivyo bwana! Huenda kuna lake jambo alikuwa nalo ila kwa bahati mbaya muda sio rafiki kabisa kwangu.
Usisahau kwamba mama yake mlezi na Gavin alidai kwamba kuna wakati mwanae nguvu ziliwahi kumshinda akaua jumla ya watu mia tatu na hamsini kiasi kwamba akaondoka naye na kwenda kumficha kwenye moja ya mapango porini. Kipi kilitokea huko mpaka wakaja kurudi tena? Ni jambo gani alilifanya kiasi cha kumrudisha mwanae kwenye hali ya kawaida mpaka akarudi mtaani tena? Kuna mengi huenda yalifanyika huko ila bado muda wangu unanigomea kabisa kutia wino kwenye hili.
Yakumbuke maneno ya Sarah vizuri, Sarah wakati anapewa historia ya maisha ya Gavin Luca na Othman Chunga, alipewa maelezo juu ya nguvu za ajabu za Gavin kwenye mwili wake. Mwanamke huyo alimuuliza Othman kama ana uhakika kwamba nguvu hizo zingeishia hapo tu? Kwa sababu kwa uelewa wake alikuwa anajua kwamba nguvu kama hizo za asili huwa zina tabia ya kuhama kutoka kizazi kimoja kwenda kingine.
Na Gavin alikuwa ana mtoto ambaye alimpata akiwa tayari na nguvu hizo kwenye mwili wake, je ni kwamba mwanae wa pekee LIONELA alikuwa amerithi hizo nguvu kutoka kwa baba yake? Au ni kwamba hizo nguvu zilipotea tu kirahisi namna hiyo kiasi kwamba hazitakuja kuwepo kwa mtu mwingine tena? Sina uhakika na hilo ila nakumbuka Sarah alisisitiza kwamba nguvu hizo kila zinapohama huwa zinakuwa ni hatari mno kwa sababu zinakuwa zinazidi zaidi kuliko hata kwa ambaye alikuwa nazo mwanzo.
Sasa swali la kujiuliza mimi na wewe ni kwamba Gavin Luca ambaye hata mwili wake haukupatikana, alikufa/kupotea nazo au ni kweli mwanae LIONELA alirithi hizo nguvu? Kama mwanae alirithi na ilidaiwa kwamba atakaye kuja kuzirithi atakuwa na nguvu za kutisha zaidi ni jambo gani linakwenda kuukumba ulimwengu?
Unaamini Gavin Luca alikufa au bado yupo hai?
Unaamini Lionela alirithi zile nguvu au hakuna namna nguvu hizo zingeweza kuhama?
Sina jambo la kuweza kukuahidi kwa sasa, MUNGU na wakati utaamua kama kutakuwa na majibu ya maswali haya. Kama tukikubaliana nayo kwamba kila kitu kiliishia pale pale basi hakutakuwa na haja ya kuweza kuyajibu maswali haya lakini kama wote hatutakubaliana kwamba kila kitu kiliishia pale basi nitakuja kujitokeza wakati mwingine kuweza kukujibu maswali haya.
Kama nilivyosema kwamba sitaki kuahidi ila majibu yako ndiyo yataamua kama nirudi tena hapa kukujibu au nisirudi. Kwa maana hiyo kuna uwezekano tukawa na SEHEMU YA PILI/ SEASON 2 ya andiko hili japo hili litategemea na majibu yako wewe juu ya hayo maswali hapo juu.
Unaweza kunijibu kwa njia zifuatazo.
SIMU: 0621567672 (WhatsApp)
0745982347 (Kawaida)
Email: thomasibabuya@gmail.om
Instagram: iamfebiani
Naam, ulikuwa nami tangu mwanzo kabisa wa andiko hili mpaka leo nakusanya nyaraka zangu na kutokomea kusiko julikana baada ya kujifungia ndani kwa muda kuweza kukuandalia chakula bora cha ubongo.
Nisema asante kwa kunivumilia muda wote mpaka sasa umekuwa nami, wewe ni mtu mhimu sana kwenye kazi yangu na maandishi yangu. Uwepo wako ndio ambao unamfanya FEBIANI BABUYA (Mimi) aendelee kuandika na kukusogezea haya maandishi hivyo ninatoa shukrani za dhati kabisa kwako.
Nina mengi ya kuzungumza nawe mtu wangu wa nguvu lakini muda sio rafiki ila ni matumaini yangu kwamba umeburudika kwa kila nukta ambayo umeigusa ndani ya simulizi hii.
Kwa kusema hayo, niseme tu nakutakia wakati ulio mwema kwako, kwa marafiki zako, ndugu zako, jamaa zako, familia yako bila kusahau nakutakia afya iliyo njema kabisa ili uweze kupambana na changamoto za kila siku za ulimwengu.
Nilikuwa hapa, nipo hapa na nitaendelea kuwepo hapa kwa ajili yako, namba yangu unayo hivyo unaweza ukanitafuta kwa muda wowote ambao unanihitaji, nipo kwa ajili yako kwa masaa ishirini na manne ya wiki.
Ni mimi mwandishi wako, FEBIANI BABUYA.
Tchao
MWISHO.
Respect 🤝Umetisha sana mkuu, asante kwa kazi nzuri 🙏🏾
Shukrani mkuu na poleKwa wadau wangu wote naombeni mnisamehe sana kwa sababu nilipata dharura ndo kwanza namaliza kuoga saivi.
Nimerudi nusu saa iliyopita.
Nawawekea muda huu hivyo kwa ambao mpo macho mtaipitia na wale ambao mmelala mtaamka nayo.
Mnisamehe sana na niwatakieni usiku mwema...
Tutaongea vizuri kesho.
Daaaah you deserve to be best author [emoji1363][emoji1363] nice workMmedamkaje wajukuu wa Nyerere!?
Kwanza nitoe shukrani zangu za dhati kwa kuwa nami pamoja kwenye andiko hili tangu naanza mpaka nalimaliza hapa hapa Jf.
Shukrani zangu ni kwa wale wote ambao walinunua, walio comment, waliolike, waliopita bila kusema chochote, walio kosoa, walio tukana.... Wote mmefanya kazi imezidi kwenda vizuri.
Niwaambie tu kwamba simulizi ya IDAIWE MAITI YANGU haijaishia hapa Bali huu ni mwanzo kabisa wa SIMULIZI hii.
Mwishoni kabisa kuna maswali hapo mengi tu kuhusu hatima ya GAVIN LUCA kama alikufa au alibaki hai, kama alikufa kilitokea nini na kama yupo hai nini kitatokea na aliwezaje kupona kwenye eneo kama lile? Kumbuka hakukuwa na ushahidi wowote wa kupatikana kwa mwili wake.
Pia kuhusu hatima ya zile nguvu zao na familia yao kwa ujumla.... Sasa hapo ndipo tunaipata sehemu ya pili ya simulizi hii ambayo inaenda kukupatia majibu kamili.
SEHEMU ya pili inaitwa THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA - LIONELA kwa kiswahili ikiwa na maana ya SAFARI YA GAVIN LUCA.
Habari njema kabisa ni kwamba simulizi hizi zipo tatu ambazo zote zinayazungumzia maisha ya familia ya GAVIN LUCA na hatima yao ambazo ni;
1. IDAIWE MAITI YANGU
2. SAFARI YA GAVIN LUCA
3. SIKU ZA MWISHO- GIZA LA MALAIKA au waweza Kuiita THE DARKNESS OF AN ANGEL
Ukifanikiwa kuzisoma zote tatu ndipo utakuwa umefanikiwa kuimaliza hii collection nzima.
Habari njema ni kwamba collection nzima ipo tayari yaani nilisha maliza kuiandika hivyo ni kazi yako tu kuisoma. SAFARI YA GAVIN LUCA tutaanza kuisoma taratibu na kama mods watakubali kubadili title basi nitaendelea nayo kwenye huu uzi ila wakizingua basi ninafungua Uzi mwingine.
Simulizi zote tatu zipo zimekamilika, kwa wale wa kununua unaweza kununua kuanzia muda huu na kwa wale wa mdogo mdogo kusoma hapa free tutaenda slowly but surely.....
Hivyo nakukaribisha kuja kuniunga mkono kwenye Moja kati ya collection bora sana kuwahi kuandikwa hapa Tanzania.....
Sijawasahau wadau wangu wa Fasihinet kule tayari nimeweka simulizi zote tatu hivyo unaweza kuzisoma kwa coin muda wowote kuanzia saivi..... Link [emoji116]
FasihiNet - Kiswahili Simulizi & Riwaya 📚
Explore captivating simulizi, hadithi, and riwaya in Kiswahili on FasihiNet.www.fasihinet.com
Tutaendelea kujuzana mengine ila kwa sasa niwatakieni wakati mwema.
Much respect to you FEBIANI BABUYA hakika umejua kutuburudisha Sana. Kazi yako ni njema mnoSTORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
********************
SUMMARY...............
**************
THE ODYSSEY OF GAVIN LucA
IDAIWE MAITI YANGU
Ilikutwa note book ndogo ambayo ilikuwa na maelezo mafupi ya safari ya maisha ya Gavin Luca. Kwenye hiyo Note book ndogo ambayo ilikutwa kulikuwa na maelezo mafupi yakiwa yanaeleza maana ya hiyo sentensi ambayo aliwahi kuwaachia ujumbe huo ndani ya msitu wa MAU huko Kenya.
Maana halisi ya maneno hayo matatu, alikuwa anawapa taarifa watu wake ambao alikuwa anawatafuta, kwa sababu walikuwa wanajua kwamba alishakufa, yale mauaji yote ya kikatili ambayo aliyafanya yeye, mambo yote ya kutisha ambayo aliyasababisha kwa kutumia mikono yake, alihitaji idaiwe maiti yake. Kwanini?
Kwa sababu ulimwengu uliwahi kujua kwamba amekufa muda mrefu maana yake yale yote ambayo yalikuwa yanatokea yeye hakuwa akihusika kabisa bali maiti yake ndiyo ambayo ilitakiwa kujibu. Maiti yake ndiyo ambayo ilitakiwa kudaiwa kwa matatizo ambayo yalitokea ndani ya taifa la Tanzania.
Safari ya maisha yake bwana huyu ilitoa funzo kubwa kwa kizazi hiki na miongoni mwa watanzania kwamba maisha ni mafupi muda mwingine kwa sababu ni wanadamu wanaamua kuyafupisha. Lakini kuna muda maisha yanakuwa marefu kama mtu akiishi kwa kufuata protocal (itifaki) huku akiwakumbusha watu kwamba “LIFE IS A GAME JUST OBSERVE THE RULES”
Safari ya maisha yake iliukumbusha ulimwengu kwamba malipo ya ubaya yanalipwa hapa hapa duniani na mara nyingi yanakuwa na matokeo mabaya. Gavin alitoa somo lingine la kutowapatia nafasi mbili wanadamu ambao hawastahili kupewa hizo nafasi kwa sababu kuendelea kuwalea kunazalisha matokeo mabaya kwenye maisha ya mwanadamu. Jishindie mechi zako mapema ili kupunguza majuto baadae.
Licha ya hayo mambo yote kutokea, Gavin Luca kwenye lile tukio ambalo lilitokea Kigamboni hata baada ya eneo lile kufukuliwa haukukutwa mwili wake. Mara ya mwisho alikuwa amejikita na kisu kwenye tumbo lake huku hali yake ikiwa mbaya isivyokuwa kawaida, sasa mwili wake ulienda wapi? Mimi na wewe hatujui.
Kwamba aliishi tena? Kama ni ndiyo, kwa sababu zipi wakati aliahidi kuyaondoa maisha yake?
Kama alikufa, mwili wake ulienda wapi? Ni kitendawili kingine ambacho kwa leo muda wangu unanitupa mkono kuweza kukitegua huenda tutakutana wakati mwingine tena kukipatia jawabu.
Yuko wapi babu yake mzee Hassan?
Ni nani ambaye alidaiwa kwamba alikuwa anazunguka naye kwenye ulimwengu wakati anatengenezwa kuwa kiumbe cha ajabu?
Mzee Hasheem alikuwa nani kwenye maisha ya Gavin kiasi kwamba akawa anaijua historia nzima ya familia hiyo? Na ni nguvu zipi ambazo mzee huyo alidaiwa kuwa nazo na wenzake kiasi kwamba wakaenda kufungwa ndani ya gereza la siri huko Tanga? Na kwanini afe kirahisi tu?
Vipi kuhusu familia ya Gavin Luca? Muda wote walikuwa wakiishi wapi! Hatima yao ilikuwa ni ipi baadae baada ya mambo yale yote kutokea?
Kuna uwalakini kwamba Othman alipotea na Sarah wakaenda kutengeneza familia bora mno, kama hilo lilitokea, ni nani alibaki kuilinda familia ya Gavin Luca?
Odhiambo Wambui, unalikumbuka hili jina si ndiyo? Huyu alikuwa ni mkurugenzi wa shirika la kijasusi la Kenya, alidai kwamba kuna wakati wake utakuja atahitaji Tanzania ilipie kwa sababu ya kuleta machafuko ndani ya taifa lake. Harakati zake ziliishia wapi? Kwamba alipotezea? Hapana sio kirahisi hivyo bwana! Huenda kuna lake jambo alikuwa nalo ila kwa bahati mbaya muda sio rafiki kabisa kwangu.
Usisahau kwamba mama yake mlezi na Gavin alidai kwamba kuna wakati mwanae nguvu ziliwahi kumshinda akaua jumla ya watu mia tatu na hamsini kiasi kwamba akaondoka naye na kwenda kumficha kwenye moja ya mapango porini. Kipi kilitokea huko mpaka wakaja kurudi tena? Ni jambo gani alilifanya kiasi cha kumrudisha mwanae kwenye hali ya kawaida mpaka akarudi mtaani tena? Kuna mengi huenda yalifanyika huko ila bado muda wangu unanigomea kabisa kutia wino kwenye hili.
Yakumbuke maneno ya Sarah vizuri, Sarah wakati anapewa historia ya maisha ya Gavin Luca na Othman Chunga, alipewa maelezo juu ya nguvu za ajabu za Gavin kwenye mwili wake. Mwanamke huyo alimuuliza Othman kama ana uhakika kwamba nguvu hizo zingeishia hapo tu? Kwa sababu kwa uelewa wake alikuwa anajua kwamba nguvu kama hizo za asili huwa zina tabia ya kuhama kutoka kizazi kimoja kwenda kingine.
Na Gavin alikuwa ana mtoto ambaye alimpata akiwa tayari na nguvu hizo kwenye mwili wake, je ni kwamba mwanae wa pekee LIONELA alikuwa amerithi hizo nguvu kutoka kwa baba yake? Au ni kwamba hizo nguvu zilipotea tu kirahisi namna hiyo kiasi kwamba hazitakuja kuwepo kwa mtu mwingine tena? Sina uhakika na hilo ila nakumbuka Sarah alisisitiza kwamba nguvu hizo kila zinapohama huwa zinakuwa ni hatari mno kwa sababu zinakuwa zinazidi zaidi kuliko hata kwa ambaye alikuwa nazo mwanzo.
Sasa swali la kujiuliza mimi na wewe ni kwamba Gavin Luca ambaye hata mwili wake haukupatikana, alikufa/kupotea nazo au ni kweli mwanae LIONELA alirithi hizo nguvu? Kama mwanae alirithi na ilidaiwa kwamba atakaye kuja kuzirithi atakuwa na nguvu za kutisha zaidi ni jambo gani linakwenda kuukumba ulimwengu?
Unaamini Gavin Luca alikufa au bado yupo hai?
Unaamini Lionela alirithi zile nguvu au hakuna namna nguvu hizo zingeweza kuhama?
Sina jambo la kuweza kukuahidi kwa sasa, MUNGU na wakati utaamua kama kutakuwa na majibu ya maswali haya. Kama tukikubaliana nayo kwamba kila kitu kiliishia pale pale basi hakutakuwa na haja ya kuweza kuyajibu maswali haya lakini kama wote hatutakubaliana kwamba kila kitu kiliishia pale basi nitakuja kujitokeza wakati mwingine kuweza kukujibu maswali haya.
Kama nilivyosema kwamba sitaki kuahidi ila majibu yako ndiyo yataamua kama nirudi tena hapa kukujibu au nisirudi. Kwa maana hiyo kuna uwezekano tukawa na SEHEMU YA PILI/ SEASON 2 ya andiko hili japo hili litategemea na majibu yako wewe juu ya hayo maswali hapo juu.
Unaweza kunijibu kwa njia zifuatazo.
SIMU: 0621567672 (WhatsApp)
0745982347 (Kawaida)
Email: thomasibabuya@gmail.om
Instagram: iamfebiani
Naam, ulikuwa nami tangu mwanzo kabisa wa andiko hili mpaka leo nakusanya nyaraka zangu na kutokomea kusiko julikana baada ya kujifungia ndani kwa muda kuweza kukuandalia chakula bora cha ubongo.
Nisema asante kwa kunivumilia muda wote mpaka sasa umekuwa nami, wewe ni mtu mhimu sana kwenye kazi yangu na maandishi yangu. Uwepo wako ndio ambao unamfanya FEBIANI BABUYA (Mimi) aendelee kuandika na kukusogezea haya maandishi hivyo ninatoa shukrani za dhati kabisa kwako.
Nina mengi ya kuzungumza nawe mtu wangu wa nguvu lakini muda sio rafiki ila ni matumaini yangu kwamba umeburudika kwa kila nukta ambayo umeigusa ndani ya simulizi hii.
Kwa kusema hayo, niseme tu nakutakia wakati ulio mwema kwako, kwa marafiki zako, ndugu zako, jamaa zako, familia yako bila kusahau nakutakia afya iliyo njema kabisa ili uweze kupambana na changamoto za kila siku za ulimwengu.
Nilikuwa hapa, nipo hapa na nitaendelea kuwepo hapa kwa ajili yako, namba yangu unayo hivyo unaweza ukanitafuta kwa muda wowote ambao unanihitaji, nipo kwa ajili yako kwa masaa ishirini na manne ya wiki.
Ni mimi mwandishi wako, FEBIANI BABUYA.
Tchao
MWISHO.
Febian Babuya.... Respect mkuuSTORY: IDAIWE MAITI YANGU
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
********************
FINAL................
Mpaka wakati huo alikuwa ameua walinzi wasio pungua arobaini, alisogea mbele alikutana na eneo kubwa ambalo lilionekana kuwa kama ukumbi lakini kwa pembeni yake kulikuwa na vinjia vidogo vidogo kukiwa na milango. Kuna mlango mmoja ambao ulinakshiwa kwa dhahabu ulikuwa unalindwa na wanaume wawili ambao walikuwa vifua wazi, alitakiwa kumalizana nao hao kwanza ndipo aweze kuingia ndani.
Hawakuwa na maswali ya kuanza kumuuliza, kuingia hilo eneo maana yake alikuwa ni adui kwao hivyo haikuwa na haja ya kuuliza maswali mengi. Mkono ulimkosa kwenye nguo yake mwanaume ambaye alikuwa ameshambulia mkono wake ulikuwa mwepesi yaani ulipunguzwa kwa huo upanga wake, wakati anahitaji kujiuguza alikutanishwa na ngumi ya kwenye moyo mpaka eneo hilo lilibonyea.
Alibaki amesimama hivyo hivyo roho ikiwa inaukimbia mwili wake, mwenzake alishangaa, kushangaa kwake akiwa kazini lilikuwa kosa kubwa analifanya, alisokomezewa upanga kwenye uume wake, aliinama kuhitaji kujutia kitendo hicho alikutana na mguu wa uso akiwa ameegamia mlango alikutana na viganja viwili ambavyo viliunganishwa kwa pamoja. Ile nguvu ambayo ilitumika ilipita na ule mlango wa mninga, mwamba huyo eneo la tumbo lilichanika baada ya kudakwa na nyama hizo kuvutwa kwa nguvu.
Mlango ulivunjika na yeye akiwa amekufa tayari, upanga ulidondokea ndani. Gavin alikuwa ndani ya sehemu ya bwana huyo lakini alikuwa ameingia sehemu ambayo huenda hakutegemea kuwepo, walisimama manjinja wanne mbele yake.
“Moja kati ya makosa makubwa ambayo niliyafanya ni kutojua kwamba uliwahi kuzaliwa na hata baada ya kulisikia jina lako niliamua kulipuuzia nikijua kuna mtu anatafuta jina tu kama walivyo vijana wengi wa kitanzania. Kama ningelijua hilo basi hili jambo lisingetufikisha usiku wa manane kama huu kuanza kusumbuana, nafikiri napaswa kutorudia kosa la namna hii wakati mwingine ujao, kosa ambalo almanusura liniingize kwenye hasara kubwa ambayo sikuwahi kuifikiria kabla” ni sauti ambayo ilikuwa inasikika kupitia ukutani, ilionekana kabisa kwamba eneo hilo lilikuwa na kamera na mtu ambaye alikuwa anaongea hivyo alikuwa anaona kila kitu kilichokuwa kinaendelea hapo.
“Kwenye ujana wangu niliitafuta sana nafasi Gavin, nilifanya kila namna ili niwe sehemu ambayo naweza kutambulika. Baada ya kuamua kujitoa sadaka mwenyewe nilifanikiwa kuingia Ikulu tena kwa maumivu makali mno halafu akatokea mtu mmoja mzaliwa wa kijijini kwenye maisha magumu akabeba kila kitu bila kujali nilikitoa wapi. Kama haitoshi akaamua kunidhalilisha mbele ya wananchi wangu mwenyewe kama mbwa, hakujali aibu ambayo ningeipata, hakujali juu ya mateso ambayo nilipitia wala hakujali mimi ningejisikiaje, alikuwa amejawa na ufahari na umaridadi ambao alikuwa anautafuta kwa nguvu zote. Huyo ni baba yako ambaye namzungumzia hapa ndiyo maana baada ya pale nilitumia kila kitu changu kuhakikisha nakuwa ndiye binadamu mwenye nguvu zaidi, niliwatengeneza watu wangu kila sehemu mpaka ndani ya biashara zake kwa sababu nilitaka kuuteketeza ufalme wake na miliki yake yote
Kwenye hilo nikiri nimefeli mpaka sasa kwa sababu wewe bado unaishi lakini hata pesa zake bado sijazipata ila ni kheri kwangu kwa sababu nilimuua. Unajua wahenga walisema kwamba “Simba mwenda pole ndiye mla nyama” niliamua kuuishi huo msemo kwa sababu una maana kubwa kwa mtu mwerevu ndiyo maana niliamua kuigiza kifo changu ili niweze kuikamilisha kazi yangu kwa amani bila kujulikana kama nipo hai maana yake bwana yule angejiachia na ndilo kosa ambalo alilifanya mpaka nikamuua. Leo kazi ni kwako Gavin kama ukifanikiwa kuwaua hao wanaume mbele yako basi utapata bahati ya kuonana na mimi ana kwa ana na kama una uwezo basi ulipe kisasi kwa ajili ya familia yako ambayo niliiua kwa mkono wangu mwenyewe”
Maneneo yalikuwa yanaeleweka mwanaume huyo akitamba huku haonekani. Zoezi lilikuwa kuwamaliza wale maninja ndipo apate bahati ya kukutana naye ili wamalizane wenyewe. Baada ya hilo kupita umeme ulizima ghafla na baada ya dakika mbili ulirudi tena, wakati unarudi Gavin alikuwa amepiga goti akiwa ameyafumba macho huku akiwa anatokwa na damu tumboni ambapo alikatwa, kwenye bega lake kulikuwa na kisu ambacho kilinasa hapo lakini na kwenye ubavu wake mmoja kulikuwa na kisu kidogo kiligotea hapo.
Upande wa wale ninja, mmoja likuwa ametenganishwa na kichwa chake lakini mwingine kichwa chake kilikuwa kimepasuka vibaya huku amekufa. Ni ninja wawili tu ambao walikuwa hai mpaka wakati huo huku mmoja wao akiwa amevunjwa mguu wake, hakuwa anaweza kusimama vizuri tena kwa wakati huo. Gavin akiwa amefumba macho alikumbuka namna tukio hilo lilivyofanyika, kukatika kwa umeme ilikuwa ni kumpotezea yeye uwezo wa kupambana kwa sababu hao ninja ndio ulikuwa muda wao mwafaka.
Yeye kwenye kiza alilazimika kutumia zaidi hisia kwa sababu hakuwa anaona, alihisi kuna ujio wa mtu pale alipokuwepo aliinama, alikutana na mguu ambao ulitua kwenye uso wake akapata maumivu makali lakini wakati huo huo alikuwa ameirusha ngumi yake ambayo ilikutana na mguu wa ninja mmoja na kusababisha mguu huo kuvunjika.
Alikosea mahesabu yake alijikuta akishambuliwa kwa visu kwenye mwili wake, aliuzungusha upanga wake ambao ulitua na kuitenganisha shingo ya ninja mmoja huku akiutumia mguu wake wa kushoto kujibinua na kutua kwenye kichwa cha ninja mmoja ambaye alijibamiza chini kichwa chake kikapasuka vibaya huku naye akipokea viganja vizito kwenye mabega yake pamoja na kisu kiasi kwamba alipiga magoti kwa maumivu makali ambayo alikuwa ameyapitia.
Kwenye mdomo wake alikuwa anavuja damu, akiwa bado ameyafumba macho yake alihisi ujio wa mtu, ninja mmoja alipotea eneo hilo, alikuwa ametuliza mlango wake wa sita wa fahamu kwa ustadi mkubwa kwa sababu alijua ni lazima mtu huyo alikuwa anamjia alipo. Aligundua kwamba mtu huyo alikuwa anatokea pembeni akiwa anakuja kwa kasi, Gavin alijivuta nyuma kama upepo kisha akauchia upanga wake kwa nguvu kubwa mpaka ukawa unatoa cheche kuelekea kwa yule ninja ambaye mguu wake ulikuwa mbovu.
Ninja yule naye alikuwa amerusha nyota mbili nzito ambazo zilikuwa zinazunguka, Gavin wakati amejivuta nyuma na kurusha upanga alikuwa ameikaza mikono yake na bila shaka ile nguvu haikuwa yake, alikuwa anaitumia ile nguvu ambayo ilikuwa ndani yake. Alifanikiwa kumdaka yule ninja ambaye alikuwa amepotea kwa maajabu kwenye mbavu, alizivunja mbavu za bwana huyo kwa nguvu lakini hata zile nyota ambazo zilirushwa na mwenzake zilimkuta ninja mwenzake kwa sababu alikuwa ametumika kama ngao wakati Gavin anazitenganisha mbavu zake.
Ninja huyo alifia akiwa kwenye mikono yake, alimshusha na kumtoa kitambaa usoni, alikuwa na asili ya China ninja yule. Wakati huo yule ambaye alikuwa amevunjwa mguu alibaki amesimama akiwa hata hatikisiki. Upanga ule ulipita kwenye moyo wake na kutokezea nyuma ukaenda kukita kwenye ukuta. Alikufa akiwa amesimama baada ya sekunde kama thelathini ndipo mwili wake ukashuka chini.
Ukuta ulifunguka, ndani yake alionekana mwanaume mtu mzimz haswa ambaye alikuwa kwenye kanzu, alisimama eneo ambalo ulikuwa ni kama ulingo, ni kweli alikuwa mwenyewe raisi wa zamani wa Tanzania kama ambavyo alikuwa ameambiwa Gavin. Alinyanyuka akiwa anavuja damu kwenye mwili wake na mdomoni, ndo kwanza vita ilikuwa inaanza, aliambiwa kuhusu uwezo wa mtu huyo ambaye kwa historia yake ni kwamba aliwahi kuzihitaji nguvu hizo ambazo Gavin alikuwa nazo lakini hakupewa kwa sababu hakuonekana kustahili akafanikiwa kuzipata nguvu zingine kwa namna ambayo aliijua mwenyewe hivyo hakuwa mnyonge na Gavin alikuwa amejeruhiwa tayari.
Gavin alinyanyuka kama mzimu, alidunda mara mbili na kwenda kutua juu ya kamba ya eneo ambalo liliandaliwa kama ulingo kisha akajigeuza akatua ndani kabisa ya ulingo akiwa anachomoa kisu kwenye bega lake na kukitupa chini.
“Ni wakati wa mimi na wewe kuzimaliza tofauti zenu Gavin Luca japo leo hautakuwa na huo uwezo wa kutoka hapa ukiwa hai” aliongea bwana huyo mkono wake ukiwa unabadilika na vinyweleo vikasimama. Mwili ulituna na kuufanya kuwa mgumu isivyokuwa kawaida, macho yake mboni zilibadilika na kuwa na rangi ya blue, naye hakuonekana kuwa wa kawaida.
Wanaume hao wawili waliupanga mkono kwa pamoja, Natron alijisogeza mithili ya mtu ambaye alikuwa anapelekewa mbele na rimoti, mwili wake ulikuwa umekomaa isivyokuwa kawaida. Ngumi kumi na tano alizirusha ndani ya sekunda tatu, ni tano ambazo ziliingia kwenye tumbo la Gavin tena kwenye jeraha, aliangukiwa kwenye kamba akadunda kamba hizo zikamrudisha tena dimbani.
Alipigwa mtama mkali na kupigwa na ngumi nzito ambayo ilimtaka kumtoa nje ya ulingo huo lakini aliidaka nguzo ambazo inatumika kuzungushia kamba akarukia ndani kwa mara nyingine. Alitembea kwa nguvu kumfuata Natron, mikono yake ikiwa imekunjuliwa, ilikuwa na maana ya kuanza kunyofoa nyama kwenye mwili wa Natron ambaye alilishtukia jambo hilo.
Alirudi nyuma hatua kadhaa akiwa anamkwepa mwanaume huyo, Gavin alishambulia kifuani wakati bwana huyo anazidi kukwepa kwa mehesabu, Gavin aligeuka kwa kasi na kuinamia kwa Natron upande wa nyuma ambapo alizamisha mkono wake tumboni, alitoka na bonge la nyama eneo hilo hali ambayo ilimfanya Natron kugusa kiasi lakini wakati huo hata yeye aliizamisha mikono yake kwenye mgongo wa Gavin kama sio kuukaza angeuvunja uti wa mgongo.
Walikuwa wanaangaliana kwa matamanio makubwa, kila mtu alikuwa na nguvu za ziada kwenye mwili wake hali ambayo ilikuwa inawafanya wawe sawa. Mikono yao ilikutana katikati kila mtu akarudi nyuma, sarakasi za Gavin hazikuwa zikihesabika, alishuka na mguu wake ambao ulidakwa alipigwa kwenye unyayo lakini wakati huo huo yeye mwenyewe aliachia kisigino cha mguu mwingine kikatua kwenye kidevu cha Natron kila mtu akadondokea upande wake kisha wakanyanyuka tena.
Wote walikuwa wanavuja damu, Natron alitembea kwa Zigzaga akiwa anauzunguka ulingo kwa nguvu na kasi kubwa, Gavin alikuwa anamsoma mwanaume huyo. Walikutana katikati ambapo Natron aliinama kwa kupiga goti wakati Gavin akipita juu na kumkosa bwana huyo, Gavin alisindikizwa na goti la kisogo ambapo mikono yake ilitua kwenye kamba mpaka kamba ikakatika kwa nguvu ambayo aliitumia kutua nayo.
Aligeuka lakini alichelewa kwa sababu alikutana na ngumi nyingi za uso ambazo zilimfanya asione vizuri, alipigwa kiganja shingoni mpaka kumeza mate ukawa mtihani, Natron alikuwa anashambulia kwa kasi mpaka pale ambapo Gavin aliunyoosha mkono wake na kulinyofoa sikio lake ndipo bwana huyo alirudi nyuma akiwa anaukunjua mguu wake akivua kanzu yake na kubaki na suruali tu. Mguu ulimkita Gavin kifuani akatoka nje kabisa ya ulingo na kutua karibu na pale ulipokuwepo upanga wake.
Aliuzungusha mkono wake ukatua kwenye ule upanga ambao aliushika kwa mkono wake kwa ustadi mkubwa huku akiwa anaunguruma kwa makelele. Akiwa ameushika upanga ule alipiga makelele mengi na kuuzamisha kwenye mbavu yake, jambo hilo lilimshangaza hata Natron mwenyewe kuona mtu ambaye alikuwa ameanza kumuelemea akijishambulia mwenyewe.
Kadri sekunde zilivyokuwa zinazidi kwenda ndivyo Gavin alivyokuwa anazidi kupiga makelele kiasi kwamba hata ule upanga kwenye mkono wake ulimponyoka kuelekea alipo Natron, alifanikiwa kuukwepa lakini ulimbaraza na kutua kwenye nguzo moja ambayo ilikatika upanga ulidondoka nayo. Bwana huyo aliukimbilia upanga huo ambao ilikuwa ndoto yake kuushika kwani aliamini kwamba ilikuwa haki yake tangu akiwa huko China.
Gavin hata hakuwa anauwazia upanga kwenye mikono ya Natron kwa sababu alitoka anakimbia akiwa anadunda kuja alipo bwana yule, alikuwa anakimbia kwa kasi ya mashine ambapo alikigusa kile kisu ambacho alikichomoa mwenyewe, alikigusa kwa mguu kikaruka mpaka juu akakidaka mkononi akiwa anamfuata Natron ambaye alikuwa ameushika ule upanga kwa nguvu akimsubiri mtu wake kwa hamu kubwa. Gavin hakuukwepa ule upanga ambao ulizama karibu na bega lake lakini naye alikizamisha kisu kwenye jicho la Natron ambaye alijivuta nyuma na kuutoa upanga kwenye mwili wa Gavin huku yeye naye kisu kikitolewa kwenye jicho ambalo alikuwa amelipoteza tayari.
Alikunja sura yake kwa maumivu Natron, Gavin licha ya kwamba alikuwa anamwaga damu hakujali, ilikuwa ndo namna pekee ya kumuua mtu huyo kwa sababu kukwepa kwepa ingewachukua muda mrefu kumaliza zoezi lao. Alikuwa anakuja kwa kujizungusha kwa spidi kubwa ambayo kwa mtu mwenye macho ya kawaida angeona maluwe luwe tu lakini Natron hakuwa wa kawaida.
Ule ujio wake akiwa na kile kisu kidogo mkononi ulimfanya kukutana na upanga ambao ulizama shingoni kwake lakini yeye mwenyewe alikizamisha kile kisu chote kwenye eneo la moyo la Natron na kukisindikiza na ngumi kali huku naye akisindikizwa kwe teke zito ambalo liliuzamisha upanga tumboni zaidi. Gavin Luca alipiga makelele akiwa anautoa huo upanga kiasi kwamba hiyo hali ilimshtua hata Natron mwenyewe ambaye wakati anajiuliza alimona mwanaume huyo anakuja kwake akiwa ana ule upanga, naye alihema na kuja kwa kasi ambapo walikutana katikati na kupishana kila mmoja akiwa ameangalia upande wake kama alivyokuwa anaenda kushambulia. Natron kifua kilikuwa kimechimbika vibaya mno baada ya kukutanishwa na upanga huo huku yeye akiwa na kisu kwenye mkono wake ni wazi kwamba kasi ya Gavin ilimzidi.
Jambo la kushangaza ni kwamba Gavin hakuonekana kama anapata maumivu licha ya kwamba alikuwa anamwaga damu nyingi. Natron alikituma kisu akiwa anakuja kwa kasi kubwa kumaliza kazi yake, Gavin alikiruhusu kile kisu kizame kwenye tumbo lake lakini yeye mwenyewe aliugeuza upanga wake na kuurusha kama ameususa, alijigeza wenyewe na kuligawanyisha paja la Natron akiwa amebakiza hatua kadhaa kumfikia Gavin.
Alikosa kabisa balansi na kuhitaji kumuangukia Gavin ambaye kadri muda ulivyokuwa unazidi kwenda mwili wake ulikuwa unajiongeza nguvu wenyewe, hakuwa anahisi jambo lolote lile na hiyo ndiyo ile hatari ambayo ilisemwa tangu mwanzo. Alimdaka Natron na kulishika jicho lake moja ambalo lilibakia akiwa analitoboa kwa vidole vyake mpaka akalinyofoa kabisa akalikanyaga na miguu yake.
“You killed them, you killed my twin brother. You deserve to die” alitamka akiwa anakidaka kifua cha Natron ambaye alikuwa anapiga makelele ya kuhitaji kuachiwa akiwa anamshambulia Gavin kwa ngumu mtu ambaye hakuonekana kuzijali ngumi hizo. Alikuwa anakigawanyisha kifua kwa mikono yake huku akionekana kabisa nguvu zake alianza kushindwa kuzimudu, zikawa zinamuendesha. Mwanaume alianza kukitawanya kifua vipande viwili, Natron alikuwa analia mithili ya mtoto mchanga aliyekuwa ametoka kuzaliwa wakati huo.
Kifua kilikuwa kinapasuliwa kwa lazima kwa kugawanyishwa na mikono kiasi kwamba vitu vya ndani vikawa vinaonekana. Gavin aliingiza mkono wake na kuuchomoa moyo wakati ambao Natron alikuwa amekata tamaa na kuamua kubonyeza kibatani kidogo kwenye suraali yake kiunoni akianza kulegea taratibu.
Gavin aliutupia moyo pembeni na kuzamisha mikono yake kwenye tumbo ambapo aliutoa utumbo nje huku akipiga makelele ambayo yalikuwa yanamuongezea maumivu ya mwili. Wakati huo eneo hilo lilianza kumeguka na majabali yakaanza kushuka, lilikuwa linaanza kujifunika taratibu ila hakujali. Aliupiga mwili huo ngumi nyingi mno mpaka ukabaki legelege kama chapati mpaka alipo hakikisha mtu wake amekufa tena kifo kibaya mno.
Gavin alipiga magoti akiwa anaunguruma na jasho jingi linamtoka, mwili wake ulikuwa unasisimka wakati wote, alikuwa anajisikia kuendelea kufanya jambo lile ambalo alitoka kulifanya. Aliuokota upanga wake na kujizamishia tumboni wakati huo ile sehemu ikawa inajifunika taratibu huku yeye akidondokea nje ya ulingo ule akiwa na upanga wake tumboni. Hatimaye eneo lile lilionekana kutitia kwa ndani na ule muungurumo wake ulisababisha tetemeko la ardhi mpaka kwa watu ambao walikuwa wanaishi umbali kadhaa kutoka eneo lile yalipokuwepo makazi ya THE IMMORTALS.
104 inafika mwisho.
FEBIANI BABUYA.