Simulizi: Wanawake ni wauaji

EPS 22
========

"Mh! mkuu hapaaaa daah!! okeeee.. auuu au alimaanisha kwenye picha?!!"
"Swadakta Kimaro, alichokuwa ananielekeza marehemu Mnyungunyungu nimepata siri ya maana ya hayo maneno kuwa mr.X aliwahi kupiga nae picha na dalili kuu ya kumtambua mr.X ana kovu usoni mwake kwa hiyo itatubidi tuibe siku mapema wiki hii twende mkuyuni tuombe picha zote alizowahi kupiga mzee Mnyungunyungu miaka ya nyuma."
"sawa mkuu sasa tutajuaje jina halisi la mr.X kama tutamgundua kwenye picha kwa ushahidi wa hilo kovu? kumbuka atakuwa kabadilika mno kwa sasa ila jina ndio la msingi zaidi, sasa tutajuaje hapo...?"
"Naam, swali lako ni zuri lakini usiwe na wasi kwani kabla hajafa mzee Mnyungunyungu aliwahi mwambia yule mwanae mganga kuwa mr.X anamfahamu vizuri tu. kwa hiyo tutapoiona picha ya mtu mwenye kovu ktk ulbamu ya mnyungunyungu ndipo tutapomuuliza mwanae yule atutajie majina ya mtu huyo, na alikuwa nani enzi hizo na hapo itaanza kazi moja tu ya kumtafuta."
"hapo mkuu sina swali kabisa, naona mipango imekaa vizuri sana Mr.X lazima afichuke safari hii."
Aliunga mkono st;sajent Kimaro mara baada ya kusikia mazungumzo ya Kamishna wake bwana Shaaban Mwinchande.

* * * * * *

Siku ya siku ilifika ambapo kwa mara nyengine alioneka Kamishna Shaaban na St;sajent Kimaro wakiwa moto chini ndani ya Land cruzer New Model ya kijivu wakipangusa (wakiyapita) magari na kukanyaga barabara ipasavyo kuelekea kijiji cha Mkuyuni mkoa wa Morogoro.
Muda mwingi kila mmoja alikuwa bussy na yake kichwani huku wakipeana story za hapa na pale na walipoianza barabara ya vumbi iliyokuwa inaelekea morogoro vijijini ndipo st;sajent Kimaro alivunja ukimya uliotawala muda mwingi na kuyapamba mazungumzo wakati huo akiendeesha gari.
"Sasa mkuu endapo tukishindwa kuiona hiyo picha ya mtu mwenye kovu usoni unafikiria nini cha kufanya ambacho kitatusaidia zaidi"
"Mh! sidhaani kwa haraka harakaaaa... lakini we umefikiriaje kwani"
"ahkah! mi nakusikiliza wewe bosi wangu niko tayari kutii mipango yako na kufata vile usemavyo."
"Sikia Kimaro, mapigo ya moyo wangu yanadunda kwa furaha furani ambayo naiona dhahili ni ishara ya ushindi na akili zangu zinaniaminisha kabisa kwamba safari hii tutamjua Mr.X tu."
"sawa mkuu lakini inabidi twende tukiwa na mbinu mbadala pia."
"Hebu nishauli mbinu mbadala uliyonayo."
"sawa mkuu, mi nadhani itatubidi tutumie mbinu za kijeshi zaidi kum bana yule mganga mtoto wa mzee Mnyungunyungu"
"Mbinu za kijeshi? kivipi Kimaro."
Aliuliza kamishna Shebby kwa mshangao kidogo huku akimtazama st;sajent Kimaro kwanini amefikiria hilo ilhali walishapanga awali kwamba ktk mission ile hawatatakiwa kujionesha ama kugundulika wao ni kina nani hasa.
"Mkuu kuna kitu nilikifikiria sana toka uliponipa habari ya maneno uliyoyaunganisha aliyotamka marehemu Mnyungunyungu na kunijengea wazo ambalo nahisi kabisa lipo jirani na ukweli ama ndio ukweli wenyewe."
"Wazo lipi hilo tena!! hebu nambie."
"wazo kuwa ni nani anaweza kuwa mr.X"
"Mh! Kimaro acha utani hebu nifafanulie unahisi nini?"
"Akili zangu zinanambia kuwa huenda yule mganga aliyetupokea akawa ndie mr.X mwenyewe"
"Mh! unamaanisha mtoto wa mzee Mnyungunyungu?"
"Haswaa ndie huyo."
"Kivipi sasa hadi umehisi hivyo?"
"kutokana na maneno uliyoyaunganisha aliyosema mzee Mnyungunyungu na ukijumlisha hadithi ya Hussein ukigawanya tukio la barua, namba ya simu hadi kushambuliwa kule kibamba miaka hiyo.. Pia umli wake vile nilivyomuona bado akili yangu inasema kuwa mzunguko woooote uko palepale yule mganga ndie mr.X"
"Daaah! Kimaro leo kweli umeamua kuchemsha kupe walio kwenye ndonga (kichwa) langu, Mh!! lete prove ya kile usemacho."
"Sawa mkuu ninazo sababu, Kwanza kumbuka mara ya kwanza mke wa Hussein ambae ni Zai alipoonwa na baba mkubwa wa Hussein ambae ndie mzee Mnyungunyungu alionesha hali ya mshangao sana hadi kupelekea kumpa maneno ya mafumbo Hussein juu ya yule mwanamke. Hii inanijengea picha kuwa mzee Mnyungunyungu alimtambua Zai mapema kabla ya pale, inawezekana mtoto wake ambae ndie yule mganga nae walishakuwa na mahusiano... kuthibitisha hili rejea kauli za Zai kuwa hajawahi kumkatalia mwanaume aliyemtongoza ila wote akawapa mitihani ktk kumtafuta aliyempenda kweli na walishindwa wote kasoro Hussein aliweza na kumpata Zai so mmoja wa washindwaji anaweza kuwa mtoto wa Mnyungunyungu.
Pili, barua ya Hussein huenda alipewa na yuleyule mganga kwenye daladala na kwa kuwa alizijua dawa nyingi kuna uwezekano barua ile ilibeba nguvu za giza ndani yake na pindi iliposomwa na mke wa Hussein ilianza kumlevya taratibu na kujikuta anaanza kufanya mawasiliano ya siri na yule mganga pasi na kujitambua na hata siku walipokuwa wanaenda kwa ba mkubwa inawezekana waliwasiliana tena kwa msg na yeye ndie aliyemny'ang'anya mtoto Hussein na kumshambulia akishilikiana na wenzake aliowajua yeye vilevile hata Mzee Mnyungunyungu alitoa ushahidi ule kwa kumkingia mwanae kifua na kuificha ile siri na ndio sababu ya kuhama kwao ili kupoteza kabisa habari zile zisije kuzuka tetesi pale kijijini.
Tatu, Kipindi unamuuliza swali marehemu Mnyungunyungu juu ya mr.X kuna uwezekano mlaika mtoa roho alikuwa mbele yake na akashindwa kusema uongo hivyo alitaka kumfichua mwanae na ndio maana ya maneno ANA KOVU USONI.
Na hii ni dhahili kama siku ile hujamuangalia vizuri yule mganga mimi nilimuona vizuri zaidi kuwa ana kovu kubwa tu usoni.
Kwa sababu hizi kuu tatu nina mashaka ya kuthubutu kusema kuwa mtoto wa Mzee Mnyungunyungu ndie Mr.X.."

"Uuuuuuppphhhhhh!!!!"
Alishusha pumzi kwa nguvu Kamishna Shebby huku akimtazama mara mbili mbili stafsajent Kimaro pasi na kumwambia chochote na ukimya ulifuata tena baina yao kipindi Shebby alipotulia na kuanza kuyachekecha maneno na prove alizotoa Kimaro sambamba na hadithi ya Hussein.
Kiupande furani yalimuingia yale maneno na kuzishawishi akili zake kuwa akubaliane na Kimaro lakini bado upande wa pili moyo wake Ulimkatalia kabisa kuwa yule mganga mtoto wa Mzee Mnyungunyungu kuwa ndie Mr.X

** ** ** **

Ilitimu majira ya saa saba mchana ambapo waliwasili kijiji cha Mkuyuni na kupaki gari yao eneo lile lile walipopaki pindi walipokuja awali na pembeni yake kulionekana imepaki difenda ya polisi na gari ya wagonjwa, na baada ya kushuka walivuka barabara na kuelekea moja kwa moja ile njia ya bondeni ambayo walipitishwa siku ile na yule kijana aliyeitwa Chibu.

Lakini cha ajabu siku hiyo hakukuonekana watu wengi eneo lile la stendi huku frem nyingi pia zilifungwa japo ilikuwa mchana na wakati wakishusha kile kibarabara waliwaona watu kwa mbali wengi wengi mbele yao huku wengine wakija nyuma yao na kuwapita wakionesha walikuwa na haraka ya kuwahi kule walipokuwa wanaelekea wenzao.
Hali hii iliwafanya hata wao kuzidisha mwendo ili wawakaribie wale watu wajue kulikoni.
"Wakuu .. wakuu wakuuuu salamualeikuuu waheshimiwaa.."
Ilisikika sauti kutokea nyuma yao ndipo walipogeuka kumuona aliyekuwa anawasalimia ndipo Kamishna Shebby na Kimaro walipotabasam baada ya kugundua alikuwa ni yule mpiga debe wa stend Chibu.
"aaah Chibu. waleikumsalaam vipi kwema."
"Aaah!! ndo hivyo bwana bado tunahema tuko pamoja na nilipowaona mnapita pale chini nikaona si mbaya niikatae tenda ya leo nikajumuike nanyi ndugu zangu ktk harakati za kwenda kumpumzisha mwenzetu."
"Harakati za kumpumzisha mwenzetu? mbona hatukuelewi Chibu?"
Aliuliza St;sajent Kimaro huku Kamishna Shebby akiwa nae kataharuki akijiuliza au ina maana mzee Mnyungunyungu hakuzikwa toka kipindi kile? wakati ilishapita wiki naa.
"Aaaah!! wakubwaa nyie si mmekuja tena kwenye huu msiba au hamuelekei kwa Mnyungunyungu?"
"Tunaelekea huko huko Chibu, sasa huo msiba wa nani tena?"
"Daah!! Mnanishangaza sasa, mi nimejua taarifa ya tukio lililotokea juzi ndio limewaleta huku kumbe sio..?"
"He!! unatuchanganya sasa Chibu kwani kumetokea tukio gani tena.!!?"
"Mnyungunyungu mtoto (jr) mzee wa nyanga na tunguli kakata kamba, yaani amekufa."
"Amekufa? mtoto yupi kwani"
"Mtoto wa Mnyungunyungu wakubwa aliyeachiwa mikoba."
"HAA!! Unamaanisha yule MGANGA?!!"
walistuka kwa pamoja baada ya Chibu kutikisa kichwa kukubaliana na swali waliloliuliza juu ya huyo aliyefariki.
ITAENDELEA..
 
EPS 23
========

"Ndio hivyo wakubwa hivi unavyoona shazi yote ipo huko baada ya mwili kurudishwa ukisindikizwa na diffenda ya polisi au hamkuiona hapo juu stendi! Noma sana wakuu mzee hakuchukua hata mwezi toka kavuta mdingi ake nae kaamua kujichinjilia mbali, ajabu sana."
"Ina maana alijiua?!!"
"Eeeeh, Alijikata koromeo wakuu, afadhali tushafika mtapata full data."
Aliongea Chibu kauli iliyowastua zaidi na kuwashangaza wakati huo tayari waliingia maeneo yale ambapo waliona watu wengi sana eneo lote la kijiji kile kuzunguka nyumba ya marehemu Mnyungunyungu sambamba na polisi wachache huku kila mtu akiwa mwenye huzuni na kutoamani kutokana na habari juu ya kifo cha mganga mrithi mtoto wa mzee Mnyungunyungu ikisemekana amejichinja koromeo mwenyewe na kujiua akiwa ndani ya Kibanda chake cha Uganga.

Hali ilitisha na kuwastaajabisha mno kina Shebby mara walipofika na kusogea pale msibani upande wa mbele kulipokuwa na turubai kubwa huku wakionekana watu wengi na ndipo walipoamua kuwasogelea wazee furani waliokuwa wamesimama wakijadili jambo na afsa mmoja wa polisi na ndipo walipowasalimia na hata wale wazee hawakupata tabu sana kuwatambua hususani Shebby.
"Karibuni sana wajukuu zangu karibuni."
"Ahsante Mzee, poleni sana."
Baada ya hapo walienda kukaa pale chini kwenye turubai kulipotandikwa mikeka mingi huku vichwani wote wawili wakitafakari habari zile kuhusu kifo cha yule mganga Mnyungunyungu mtoto ambae ndie pia walitegemea kuipata hiyo njia nyengine kuhusu Mr.X
Wakiwa wamekaa pale muda mfupi jeneza lililokuwa na mwili wa yule mganga lilitolewa na kuekwa sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya sala ya mwisho na kumswalia marehemu na baada ya hapo safari ya kuelekea makaburini ilianza huku nyuma kukisikika vilio mfurulizo vya kina mama.
Waliongoza pamoja kwenye msafara ule mpaka makaburini na alizikwa pembeni na alipozikwa mzee Mnyungunyungu mwenyewe aliyezikwa siku chache zilizopita.
Akiwa kasimama jirani kabisa na makaburi yale kipindi mwili wa yule mganga ukiingizwa kaburini Kamishna Shebby alitoa miwani yake mikubwa meusi iliyokuwa kwenye mfuko wa shati aliyovaa na kuitinga usoni kuficha macho yake yaliyoanza kubadilika rangi kwa uchungu aliokuwa nao wa kukosa uhakika ama kutomtambua mr.X huku akiwa bado haamini hisia alizoambiwa na st;sajent Kimaro pindi walipokuwa njiani kuwa yule ambae sasa wanamzika pale kuwa ndie Mr.X lakini pia swali jipya lililozidi kumchanganya ni kwanini amejiua?
Akiwa anatazama mazishi huku anatafakari ndipo uso wa Kamishna Shebby ulipotazamana na uso wa yule kijana aliyewapokea siku ile ya kwanza kule kibandani na kuwakaribisha ambapo babaake ambae ndie walikuwa wanamzika alikuwa ndani ya kile kibanda kama mganga mkuu wa pale baada ya hali ya mganga mwenyewe mzee Mnyungunyungu kuwa mbaya muda mrefu.

Uso wa yule kijana ambae alikuwa kashikwa mkono na mzee mmoja ulionesha huzuni sana kwani muda wote ulikuwa unatililikwa machozi tu kipindi babaake alipokuwa anazikwa.
Baada ya shughuli ya mazishi kukamilika watu walianza kutawanyika mazialani na kwa upande wa Kamishna Shebby na st;sajent Kimaro wao walikuwa ni miongoni mwa watu wa mwisho mwisho kabisa kutoka kule mazialani huku wakitembea taratibu pia wakizungumza kwa sauti za chini chini.
"Kazi ukizidisha kazi unapata Kazi juu ya Kazi. daah.."
"Yaani we acha Mkuu mi mwenyewe hapa akili yote imepigwa short kwa kutoamini hiki nikionacho."
"Hivi Kimaro unahisi kwanini amejiua? maana mi hainiingii akilini kuwa kifo cha babaake ndio kimpagawishe akili hadi kufikia hatua ya kujichinja mwenyewe!!"
"Mkuu nakubaliana na wewe kuwa kifo cha babaake hakikumchanganya akili ila pia nakubaliana na mawazo yangu kuwa yule ndie mr.X kwani nahisi kwa namna furani ujio wetu wa awali ulimuumiza hasa babaake alipotaja alama aliyokuwa nayo na huenda kajiua kwa kuficha aibu baada ya kuhisi sasa siri itajulikana kama yeye ndie aliyemchomekea kesi ndugu yake kwa sababu ya mwanamke."
"Mh!! sasa kama ndio hivyo huyo mwanamke yuko wapi?"
"Hapo hata mimi sijui labda tuchunguze majina ya wake zake labda mmoja anaweza kuwa ndie si nasikia nae alikuwa na wake watatu?"
"Mh!! ok ila kwanza Kimaro tusikurupukie huko mi navyoona sasa twende tukatoe pole zetu kwa wafiwa na tutafute mbinu gani tutaweza kuitumia ili tupate picha za Mnyungunyungu tuhakikishe kama tutamuona huyo mtu mwenye kovu au lah! ndipo tuanze kuchunguza historia na nyendo za marehemu tuone kama zinamach na mr.X"
Walikubaliana na kufika msibani kama kawaida ambapo safari hii watu walipungua sana huku wengi waliobaki walikuwa ni ndugu na majirani na baada ya kuwapa pole na kutoa mchango wao Kamishna Shebby alimvutia pembeni mzee mmoja yule anayependa kuvaa baraghashia na kuanza kuongea nae mawili matatu halkadhalika st;sajent Kimaro nae alikaa pembeni na bwana mmoja ndugu wa marehemu na kuongea nae mawili matatu na hii yote ilikuwa moja ya mipango yao kutafuta ukweli wa kifo cha yule mganga.
"..Ndio mzee wangu kwa hiyo unasema mlisikia kelele baada ya kijana wake marehemu kuingia kibandani asubuhi na kumkuta babaake akiwa amelala kwenye dimbwi la damu ameshika kisu huku koromelo likiwa nje, kwani si walikuwa wawili pale kibandani? inakuwaje hadi anajikata yule kijana asisikie pale nje."
yalikuwa ni maswali aliyokuwa anahoji Kamishna Shebby kwa yule mzee ambae nae hakuchoka kufunguka na kujibu.
"Mh! mwanangu ukweli wahenga walisema usilolijua ni usiku wa giza, kwani siku hiyo ilikuwa kawaida na siku nyengine ambapo mganga ndie anaechelewaga kufika na yule msaidizi wake ambae mwanae huwa ndie anawahi kufika, sasa ajabu siku hiyo Mganga aliamka mapema sana saa kumi na mbili kasoro akidai anataka awahi kijiweni kufanya maandilizi kuna mgeni wake muhimu angekuja siku hiyo na mishale ya saa mbili mwanae alipoenda kibandani ndipo alimkuta akiwa tayari keshakufa. Daah!! yaani ilionesha dhahili alipanga kujiua nahisi kifo cha babaake kilimchanganya sana nae kamfata alipo aaah!! mjukuu wangu hili pigo kubwa sana hapa kijijini."
Aliongea yule Babu na baada ya hapo shebby alimtuliza kwa kumpa maneno matamu ya pole kisha alimuangalia Kimaro kule alipokuwa na yule bwana mwengine na ndipo walipoaga na kuahidi wangerudi kumalizia misiba ile ambayo hitima zake zilipangiwa siku moja.

Wakiwa wameshajiandaa kwa nia ya kuondoka Kamishna Shebby ghafra machale yalimcheza baada ya kupata mbinu iliyomjia palepale na kumuomba faragha mtoto wa marehemu yule mganga na kusogea nae pembeni kidogo.
"Pole sana kaka kwa kumpoteza baba katika nyakati kama hizi nakusihi uwe na moyo wa kiume na uvumilivu wa kutosha katika kipindi kigumu kama hiki."
Aliongea kwa upole Kamishna Shebby.
"Asante kaka yote nimemuachia mungu"
Sawa ila naomba utusaidie kitu kimoja tafadhali japo najua kwasasa bado hujakaa sawa lakini naomba unisaidie kwani nitamfurahisha sana babaangu aliyenifanya nifike huku."
"Kitu gani kaka, usijali nambie tu."
"Ni hivi babaangu nae ni mzee sana lakini alikuwa ni rafiki mkubwa wa Mnyungunyungu enzi hizo na walipoteana pindi tulipohamia Nairobi kipindi hiko nilikuwa mdogo sana sasa miaka ya karibuni tumerudi nchini na baba alihitaji sana kuonana na rafiki yake mpaka akafikia kunipa data zote wapi alipo nami nikaanza kumtafuta lakini kwa bahati mbaya nimeambulia kushuhudia tu kifo chake, sasa nitawezaje kumliwaza babaangu walau kidogo niporudi tena zaidi ya kumpatia walau picha ya rafikiake kipenzi ili ibaki kuwa kumbukumbu yake pia..!! Kwa hiyo kaka nakuomba sana jitahidi uje na picha za Mnyungunyungu niangalie ipi itafaa niondoke nayo.."
Maneno ya Kamishna Shebby yalikuwa na uongo asilimia themanini ndani yake lakini yalimuingia vizuri yule kijana wala hakuhisi hata kidogo kama alikuwa anadanganywa.
ITAENDELEA...
 
EPS 24
========

"sawa ndugu yangu usijali ngoja niingie ndani nikuletee bahasha nzima uchague mwenyewe maana leo tu kuna ndugu walikuwa wanazitazama sebuleni na kuzitenganisha kwa kutunza zaidi kumbukumbu."
Aliongea yule kijana na kumuomba waingie ndani na kamishna Shebby huku wakimuacha St;sajent Kimaro nje akisubiri.
Na baada ya Shebby kuingia ndani na yule kijana ndipo alipotolewa mfuko wa bahasha ya kaki ambao ulijaa picha mbalimbali za mzee Mnyungunyungu toka enzi za ujana wake.
Moyoni Shebby alifurahi na kujiandalia umakini machoni na akilini mwake mara alipoanza kutazama picha moja moja akiitafuta picha ya mtu mwenye kovu usoni.
Lakini ajabu alitazama na kurudia karibu picha zote bila kumuona mtu tofauti mwenye kovu usoni zaidi ya yule mtoto wa mzee Mnyungunyungu aliyefariki kwa kujiua.
Alijikuta anapiga ana anado asijue picha ya kuchukua huku kichwani akijilazimisha kuamini kuwa huenda yule ndie alikuwa mr.X.
"Chukua hii kaka waliopiga babu baba na rafiki yao huyu ambae simjui lakini ni nzuri tu tena kipindi hiko baba bado kijana na hata babu hakuwa mzee sana"
Aliongea yule kijana na kumkabidhi picha moja baada ya kuona mgeni wake anachagua chagua tu picha asijue ya kuchukua.
Na baada ya Kamishna shebby kupokea ile picha alijifanya kufurahi japo akili yake ilishavurugika baada ya kuikosa hiyo picha yenye mtu mwenye kovu usoni kisha akatoka na kujumuika na st;sajent Kimaro na kuondoka.

** ** **
"Haiwezekani Mkuu, mi nilikwambia yule ndie mr.x tu. Umeamini sasa!!"
Aliongea Kimaro huku akipiga piga usukani wakati walipokuwa njiani kilomita chache toka watoke Mkuyuni.
"Mh!! kwa kweli Kimaro najilazimisha sana kukubali lakini bado upande wa pili moyo wangu unanipinga."
"Kwanini sasa Mkuu wakati vielelezo vyote umeviona? Yaani prove niliyokupa imeenda vilevile sasa wewe una prove ipi ambayo inakuaminisha kuwa yule sio mr.X?"
"Unataka nikupe prove..!?"
"Ndio Mkuu lakini samahani si kwa amri yangu ni kwa matakwa yako mwenyewe Mkuu"
"Sawa. Geuza gari haraka turudi twende kituo kikuu cha polisi Mkuyuni."
"HE!! kivipi sasa Mkuu"
"tofauti ya prove zako na zangu ni hivi.. wewe Kimaro una prove za maneno sana kwa kuunganisha matukio katika hali ya kufikirika ila mimi nina prove za vitendo sana katika kuunganisha matukio kwa vitendo halisi. Sasa GEUZA GARI MARA MOJA."
Aliongea Kamishna Shebby safari hii akiwa serious kupita kawaida hadi sauti yake ilibadilika mno na maneno yake ya mwisho aliongea kwa ukali kidogo na kwa sauti ya juu hadi Kimaro alishangaa na kuogopa kidogo baada ya kuona best ake mkuu wake akimuwekea uso wa mbuzi na kutumia wazfa wake ambao mara nyingi alikuwa hamuoneshi.
"SIMAMISHA GARI KIMARO."
Sauti hii ya juu kutoka kwa Shebby ilimfanya Kimaro kufunga breki za ghafra na kumshangaa inakuwaje Kamishna anachanganyikiwa na kubadilika ghafra kiasi kile.
"Shuka."
"Eeh!!"
"Shuka Kimaro Nipe funguo"
"Lakini mkuu sijakaidi agizo lako nilikuwa natafuta sehemu nzuri ya kugeuza."
"Tusibishane Shuka."
Aliongea kwa msisitizo Shebby huku akiwa amefungua mlango wa upande wake na kushuka na kuzunguka upande wa pili na kumfanya Kimaro nae ashuke huku akiwa na taharuki kubwa kwani hakuwahi kumuona Kamishna wake akiwa serious kiasi kile toka afahamiane nae.
"Zunguka kaa upande niliokaa"
"sawa mkuu"
Alitii haraka haraka Kimaro na kumuachia funguo Kamishna Shebby nae kukaa upande wa abilia kisha ndipo Shebby alipoitoa gari kwa kasi kwenye barabara ile ya vumbi ambayo haikuwa ikitumika sana na magari mara kwa mara na baada ya gari kuchanganya huku Kimaro akiwa kajifunga mkanda akimuangalia mkuu wake aliyekuwa bussy na usukani na ndipo ghafra gari ikiwa mwendo kasi Kamishna Shebby alivuta hand break na kupelekea gari kuzunguka kama zile za mashindano na kugeukia ilipotoka na bila kuremba Shebby alishusha hand break haraka na kuchochea mafuta kama ileile ambapo sasa walikuwa wanarudi Mkuyuni huku eneo zima la barabara kukiwa kumetimka vumbi kubwa sana.

Sio siri mwendo kasi aliokuwa anatembeza Shebby hata Kimaro mwenyewe ulimtisha kwani ilifikia Kipindi hata kokoto na mashimo yaliyokuwepo barabarani hayakusikika kabisa na kwenye miinuko na matuta gari ilipaa hadi watu waliokuwa maeneo ya pembeni ya ile barabara walibaki wameshika vichwa.
Hadi wakati huo st;Sajent Kimaro hakujua prove gani aliyokuwa nayo Kamishna wake na kwa jinsi alivyom badilikia alishindwa kabisa kumuuliza na kubaki akisali kimoyomoyo wafike salama kwani aliona dhahiri shahili mwendo ule haukuwa na usalama hata kidogo.

Kwa speed ya dakika tisa tu badala ya Arobaini kwa mwendo uliotumika toka pale alipogeuza gari Shebby na Kituo kikuu cha polisi Mkuyuni ambapo hadi polisi waliokuwa Kaunta waliacha shughuli zote na kuhamaki huku wengine wakiandaa bunduki zao wakihisi huenda wamevamiwa kwa jinsi gari ile ya kina Shebby ilivyoingia na Kupaki mbele ya Kituo.

"Twenzetu.."
aliongea Shebby baada ya gari kusimama na kushuka sambamba na Kimaro kuelekea mule ndani ya kituo kwa mwendo wa kikamanda.
"Haroo, mbona hamji kistaarabu kina nani nyinyi."
aliuliza askali mmoja aliyekuwa na cheo cha Coplo pindi alipotaka kuwazuia mlangoni kina Shebby kabla hawajasogea kaunta lakini punde shebby alipotoa na kuwaonesha kitambulisho chake tu askali wote waliokuwa maeneo yale walikakamaa na kumpa heshima stahiki kisha walimkaribisha na moja kwa moja walipelekwa kwa mkuu wa kituo kama jinsi alivyotaka Kamishna Shebby mwenyewe.

Kwa bahati nzuri pindi mkuu wa kituo kile alipoonana na Shebby tu walijikuta wote wakishangaana na kutoamini macho yao baada ya yule mkuu wa kituo kumpigia saloot Shebby pindi alipotoa kitambulisho.
"Shebby!!!?"
"John!!"
"Aaagh! kweli milima haikutani kumbe upo huku?"
walipeana mikono Kamishna Shebby na yule mkuu wa Kituo ambae ilionesha dhahili walifahamiana vizuri tu.
"Enhee, vipi familia tayari?"
aliuliza Shebby huku akisogeza kiti na kukaa wakati huo wote Kimario alikuwa kakaa pembeni akitazama mazungumzo ya wakubwa zake licha ya kuwa wote umli wao uliendana endana.

ITAENDELEA.........
 
EPS 25
========
"aaah! wea acha tu habari za wanawake ndio sitaki kabisa kuzisikia"
alijibu yule mkuu wa kituo huku akionesha yuko serious na kile anachozungumza na kumshangaza Shebby ambae alihoji.
"Kivipi tena John.?"
"Ndugu yangu yaliyonitokea ndio sitamani kabisa kutafuta familia kwa sasa wee acha tu, nahisi nina mikosi sana kwa wanawake"
"Duh! John.. kwani nini kilikupata mshkaji baada ya kuachana kipindi kile kozi ilipoisha wakati ulinambia ulitaraji kufunga ndoa siku si nyingi?"
"Ndugu yangu Shebby ni story ndefu sana ila nitakuhadithia kwa ufupi ilivyokuwa"
Aliongea John ambae alikuwa na wadhifa wa OCS kituo cha mkuyuni akiwa na cheo cha Inspecta na kuanza kukumbuka ilivyokuwa toka mara ya mwisho walipoachana na Shebby walipokuwa kwenye kozi maalum ya uongozi na usimamizi ndani ya idala ya ulinzi wa ndani miaka minne iliyopita ambapo John alianza kusimulia ilivyokuwa hadi kupelekea awe na msimamo wa kutohitaji kuwa na mwanamke kwa kipindi kile.

'''''
"Ndugu yangu, mkuu wangu kiukweli kama ulikuwa hujui leo nitakwambia ujue wazi ukae ukijua kuwa wanawake ni watu wa ajabu sana inatakiwa uwe na akili nyingi sana jinsi ya kuishi nao.
Kumbuka siku ile ya mwisho tulipokuwa tunaagana kwenye ile tafrija baada ya kozi kuisha nilikuonesha kwenye simu yangu picha ya mwanamke nilietaraji kumuoa baada ya kumaliza kozi na kupandishwa cheo kwani nilijua sasa maisha nitakuwa nishayaeka kwenye mstari tena kwa kuwa na mwanamke mzuri kama Tedy aaaah, nilijiona bonge la mjanja.
Sikia sasa ishu ilivyokuwa baada ya kuachana na kupoteana kipindi tulipomaliza kozi na kupewa likizo ya mwezi mmoja sikuamini nilichokikuta mtaani Dah!!..... Kumbe yule demu Tedy si alikuwa ananiigizia bwana, muda wote naeka nae malengo hata nikawa najinyima na kumtumia pesa tulipokuwa Kozini ili afungue mtaji wa saloon kama alivyonambia kumbe nae alikuwa anatumbua maisha na mpuuzi mmoja mchafumchafu mtoto wa mtaani pale na kunigeuza mimi chuma ulete.
Sio siri niliporudi almanusura niue mtu kwa hasira mara baada ya kupata data zote na nilipokuwa namuulizia kuhusu hiyo saloon alinizungusha zungusha kunipeleka hadi waliponasa kwenye mtego niliowatega ambapo kwa macho yangu niliwafuma wakiingia Guest moja huko Keko na nilipompigia Tedy kumuuliza alipo alivyonambia ndio nilizidi kuchoka daah! Eti 'ooh, nimeenda kwa bibi vikindu anaumwa sana nitakupigia baadae'...... Nilichomjibu nikamwambia kuwa hiyo guest haiitwi vikindu inaitwa Mumbu na hapo nilikata simu na kufata ushauli wa mzee wangu tuliekuwa wote kwenye gari ambae alinisihi mno nisipaniki wala kumchukia mwanaume aliyelala na mchumbaangu kwani mwenye makosa hasa ni mchumbaangu nami nikakubaliana na mzee nikaachana na Tedy toka siku hiyo nikampiga stop tusijuane tena.
sasa hiyo tisa kumi ni Angelina au malaika ndivyo nilivyopenda kumwita mtoto kutoka Arusha aliyekuja kufanya kazi za ndani nyumbani kwetu kipindi hiko kabla sijahamishiwa hapa Mkuyuni na kuwa ocs.
Angelina alikuwa mzuri, mwenye adabu na heshima, kila mtu nyumbani alimpenda kuanzia mzee mama na dada na hata tukashawishika tufanye mipango ili nimuoe na awe mmoja wa familia yetu.
Sasaa sijui nisemeee ujingaaaaa auu utahiiraa yani nashindwa kuelewa hawa wanawake vichwa vyao vilivyo kwani kipindi chote tunafanya mipango na kuzungumza na mamaake huko kijijini walionesha hali ya kukubali kumbe bwana yule mtoto Angelina alikuwa tayari mke wa mtu muda mrefu na alikuja Dar kufanya kazi za ndani kwa lengo la kumsubiri mumewe aliyekuwa migodini huko ataporudi nae arudi waendelee na maisha.
Sio siri hii iliniuma mno nilipokuja gundua na kushindwa kumuoa mwanamke ambae tayari moyo wangu ulishaelekea kwake na kuniangusha baada ya kusikia mumewe amerudi na mambo yamemuendea vizuri baada ya mgodi kutema na karudisha mapenzi kama kawaida.
Hapo nilipagawa sana na ndipo babaangu mzee Cyprian aliponihadithia kisa kimoja enzi zake kilichotaka kufanana na changu tena kutoka huko huko Arusha alimuona bint akiwa na askali mwenzake walipokuwa kikazi na kufanya utafiti na kueka nae mipango.
Lakini kwa kuwa mzee kipindi hiko tayari alikuwa na cheo kikubwa swala la ufatiliaji zaidi na habari alizituma kupitia kijana wake wa kazi ambae walikuwa marafiki kama mimi na wewe kufikisha salamu zake kwa familia ya yule binti na zawadi mbalimbali.
Kumbe bwana rafiki ake nae si alikuwa anampenda yule bint..!! na alipokuwa anaenda kule anajiwakilisha yeye ndie mtakaji na mzee wangu alipokuja kugundua ilikuwa tayari too late.
Lakini binti mwenyewe alimjua mzee wangu ila alikubali kumsariti na rafiki yake sijui kwanini yaani wanawake usiwaamini hata kidogo.
Ila kwa dua za mzee na jinsi alivyosononeka kumkosa yule binti ndipo ikatokea safari iliyomfanya nae rafikiake amkose yule bint na kuchukuliwa na jamaa gani sijui ambae mwishoe nasikia kumbe yule bwana alikuwa na tamaa ya utajiri si akamuua kinyama yeye yule binti sambamba na mtoto aliyezaa nae na hapo ikawa si Mzee wangu wala yule rafiki ake aliyeweza kuishi na yule binti lakini yoooote yalisababishwa na binti mwenyewe laiti angekuwa na msimamo awali wa kumkataa yule rafikiake mzee aliyeanza kumchombweza na kumpondea mzee pengine haya yale yote yasingetokea hadi kuangukia mikononi mwa huyo bwana aliyekuja kumuua.
Daaaah! basi bwana ndio hivyo mzee hamasa zake nilizielewa na baada ya hapo kila mwanamke ninaemuona mbele yangu kuna muda namuona kama kinyago vile kwa jinsi walivyonipotezea malengo na pesa bila faida yoyote. Saivi ishu yangu nikijisikia navuta cheche tu la bar basi tunamalizana kila mtu kimpango wake hahahahahaaaa.."
'''''''

Alimalizia kwa kucheka ocs John na kumuacha kamishna Shebby katika taharuki kubwa hata Kimaro nae alikaa vizuri pindi alipokuwa anaisikiliza story ya ocs John.

"Enhee, Mkuu wangu safari hii wapi sasa na wewe uko wapi"
aliuliza John
"Daah, nilikuja kwenye msiba huu uliotokea sehemu yako juu ya mganga wa kienyeji aliyekutwa amejichinja kibandani mwake sasa nilitaka kujua tafiti zenu mlipofikia na awali sikuwaza hata chembe kama ningekutana na mtu tunaefahamiana kama wewe"
"Oooh! ni kweli bwana Dah! uchunguzi wetu bado unaendelea taratibu ila tuliruhusu mazishi yaendelee baada ya ripoti ya daktari kuthibitisha kuwa hakukuwa na kiashilio chochote kuwa marehemu alishambuliwa zaidi ilionekana ni msongo wa mawazo ulichachamaa ghafra na kupelekea kujichinja.
Ila tukiwa kama polisi bado uchunguzi wetu hatujaufunga rasmi."
"Sawa vizuri John"
aliongea Kamishna Shebby huku mawazo yake yakiipitia story aliyosimuliwa muda mfupi na ocs John hasa kwenye kipengele alichonukuu story iliyomuhusu babaake kidogo ilimtia shaka Shebby na kuhisi kuna vitu vinaingiliana na story ile ya Hussein kuhusu mkewe Zai.
Alitamani kumuuliza zaidi lakini alitafakari njia ipi ya kumuingiza tena kwenye ile mada hadi afunguke zaidi kuhusu story ya babaake.?
Na ndipo hatimae Shebby aliliacha lile na kurudi kwenye azma yake juu ya prove aliyotaka kumuonesha Kiamro kuwa yule aliekufa si Mr.X japo alikuwa na kovu usoni.

"Sasa John hebu achana na ripoti ya daktari nihadithie kuhusu nyinyi mlivyopata taarifa ya kifo kile na mazingira mliyokuta hivi ni kweli yaliwapa picha kuwa yule mtu alijiua?"
aliuliza Shebby sasa akiwa serious kama alivyokuja na kumfanya hata ocs John kukaa makini kwa utulivu mara baada ya kuulizwa lile swali na kama kawaida yake Shebby aliingiza mkono kwenye mfuko wa suruali kulipokuwa na simu yake special aliyoitumia kwaajili ya kunasa sauti kwani ilikuwa na uwezo mkubwa sana wa kurekodi pindi ocs John alipoanza kuzungumza.
ITAENDELEA.....
 

Hussein alitaka kumtoa Zai bikra kwa kidole cha kati...

hehehehe...


Cc: mahondaw
 
kwa hiyo na huyu uliyemtagi naye ni mmoja wao
 
Mbona kimya story haiendelei jamanii nataka kumjua Mr.X na mwisho wa bwana Hussein kula lupango
 

Daah!
Inasikitisha sana... bado sijapata picha kwa nini Zai mke wa Hussein aamue kumaliza mume wake...


Cc: mahondaw
 

Then nani atakua kafanya hayo mauji?

Kule walipokua wanaelekea ni kwa mjomba wake, na ndiyo matatizo yalipowakuta, yeye kudhulika na kusemekana familia yake kuawa... na pia kakutwa na kiganja cha binadamu kilichovingirishwa hirizi ndani ya mfuko wake... Na hapo hapo Hussein alishasemaga mjomba wake yupo vizuri kwenye mambo ya ulozi pia...

Lakini kabla ya hapo mjomba alishamuonyaga kuhusu Zai... huyo Mr.X inawezekana akawa ni mjomba wake? Lakini mbona sauti iliyokua ikisema muacheni sijawaambia mumue ni ya Zai mke Hussein?


Cc: mahondaw
 

Du!!

Unataka kusema mwanamke wa Hussein wa kwanza (Mariam) ndiyo karatibu haya mauaji akishirikiana na Baba Mkubwa wa Hussien...

Haki tena inachanganya? Je na sauti ya mke wa Hussein (Zai), imekuaje imesikika clear kwamba ni yeye?


Cc: mahondaw
 

Mpaka hapa bado inaonekana muuaji siyo Mariam... bingwa wa blow job anaeenda kufa kwa cancer ya koo...


Cc: mahondaw
 
Endelea basi Madame S weekend yangu hii tangia niamke niko apa na pale kwenye bandika bandua zako, ndo nimeishia hapa sasa usipoendelee sijui kingine gan nifanye hii siku iishe so please endeleza Madam
 
Endelea basi Madame S weekend yangu hii tangia niamke niko apa na pale kwenye bandika bandua zako, ndo nimeishia hapa sasa usipoendelee sijui kingine gan nifanye hii siku iishe so please endeleza Madam
Ngoja nimalize kufturu ntaweka usijali
 
EPS 26
========

"Ni hivi mkuu, tulipokea simu iliyoleta hiyo taarifa majira ya saa tatu asubuhi na vijana walipofika walichukua picha na kuhoji maswali mawili matatu ya msingi na katika maelezo waliyotupa raia hususani mtu wa kwanza kumuona marehemu ambae alikuwa mwanae waliosaidiana kazi alisema kuwa babaake siku hiyo aliwahi mapema kwa nia ya kuandaa mazingira kuwa kuna mgeni wake mteja wa siku nyingi toka enzi za babaake angekuja lakini asubuhi ileile yule kijana alipofika na kuingia mule kibandani ndipo aliposhangaa kukuta babaake akiwa chini damu zimetapakaa huku mkononi akiwa na kisu."
"Sasa we kama ocs baada ya vijana wako kuleta taarifa hii ulichukua hatua gani zaidi"
"Kwanza mkuu niliwaamuru wapeleke mwili moja kwa moja hospitali kwa vipimo zaidi kama huenda alivamiwa na watu na kumchinja kisha kumshikisha tu kisu."
"wazo zuri sasa baada ya majibu kutoka kuonesha kuwa hakushambuliwa ndio mkaungana moja kwa moja na ripoti ya daktari mkimaanisha hakuna tena upelelezi wowote si ndio?"
"Mmmh, hapana mkuu, kama nilivyosema awali bado tunafanya upelelezi wa chini kwa chini."
"Upelelezi gani John hivi ulifika hata eneo la tukio.?"
"mh, hapana."
"Umeona sasa, unakikaribisha kitambi rafikiangu usipende uheshimiwa wewe ni damu changa kama mimi bwana inabidi vitu vyengine tujieke mstari wa mbele wenyewe tusipende kutuma tuma tu"
aliongea kwa msisitizo Shebby na kuongezea kauli zilizowashangaza hadi polisi waliokuwa ofisi ya jirani na ocs waliotega masikio ya umbea na kuzungumza chinichini kujua alichokuwa anazungumza Kamishna na ocs wao.
Kauli hiyo ya Shebby haikumshangaza tu ocs bali hadii St;sajent Kimalo mwenyewe na kushangaa kamishna wake ana provement zipi hadi imefikia kusema kwa kujiamini kiasi kile.
"Yaani, ndio hivyo ocs John nakuhakikishia kuwa yule mganga HAJAJIUA bali AMEUAWA."
aliekea msisitizo kabisa maneno yake Shebby na kuwafanya rafiki zake ocs John na st;sajent Kimaro kuachama midomo wasijue wamjibu nini kwa kuogopa kuwa huenda wakaeleweka vibaya mbele ya mkuu wao.
"Najua vichwa vyenu vinatamani kuniuliza nina uhakika upi hadi nasema hivi lakini haya majibu yangu kwenu yatakuja kwa mtindo wa maswali na mtashindwa kuyajibu na kwasababu hiyo sitowapa mimi majibu ila kuna mtu mmefanya kosa sana kumuacha huru, nahitaji aletwe hapa mara moja na nitamuhoji mimi mwenyewe na kila mtu hapa atapata picha kwanini nasema yule mganga hakujiua wala hakutingwa na mawazo bali ameuawa na aliyesababisha kifo chake ni mr.X"
"MR.X..!!?"
alishangaa sana ocs John mara baada ya kamishna Shebby kupitiliza maneno na kujikuta anaropoka jina la mr.X ambalo kwa upande wa ocs John lilikuwa geni kabisa.
"Usijali John, ni hadithi ndefu sana ila nitakuhadithia japo si leo kwanza nataka utume vijana wako akakamatwe huyu mtu mara moja."
"sawa Mkuu, nani mtu mwenyewe vijana wakaifanye hiyo kazi sasa hivi aletwe hapa."
"Nahitaji akakamatwe mtoto wa marehemu aliyekuwa msaidizi wake, huyo wa mwanzo kabisa kumuona marehemu."
"sawa Mkuu."
Baada ya hapo ocs alimuita sub inspekta wake akusanye vijana saba haraka wachukue difenda kwenda kumkamata mtoto wa marehemu yule aliyejichinja ambae pia ni mjukuu wa marehemu Mnyungunyungu aliyetarajiwa kuwa mganga atayefatia na mara tu vijana walipopewa agizo lile walioonesha ushupavu wa hali ya juu hasa walipogundua kuwa aliyetoa amri ile alikuwa ni Kamishna na walionesha utiifu na ushupavu mbele yake ili wasionekane wachovu na ndipo gari ilipochomoka kwa speed kali kuwahi Mkuyuni stend ili waelekee kule msibani kutimiza amri waliyopewa.

Lakini ajabu toka waondoke wale vijana wa polisi walichelewa sana kurudi na kwa haraka zao zilizochangiwa na woga mbele ya Kamishna walijikuta wanaacha hadi radio call zao hali iliyomtia hasira Kamishna Shebby na kuwaamuru kimaro na ocs watoke pamoja nae waelekee huko walikoenda vijana wao.
Hali ile na amri za Shebby ziliwafanya polisi wote kuwa kimya na kuwa makini sana katika kazi zao muda ule wakimuhofia sana na kumtafsiri kuwa yule kamishna ni mkali mno na mkorofi bila kujua kumbe Shebby alikuwa mtu peace sana ila tu kichwa chake kilivurugwa hasa baada ya kujiingiza kwenye ishu ya kutaka kumjua Mr. X.

Walipofika nje huku escot ya difenda nyengine ikiwa tayari ishabeba vijana wakingoja amri ndipo waliishuhudia difenda waliyoituma ikirudi na kuwasili kituoni na vijana kushuka haraka haraka na macho ya Shebby yalishangaa kutomuona mtu waliyemuagiza zaidi ya wamama wawili.
Akiwa kakunja uso na kutaharuki Shebby alimwita sub inspector aliyeongoza ile mission muda ule kutaka aletewe ripoti yeye mwenyewe moja kwa moja bila kupitia kwa ocs kwanza kwa kuona kama anachelewa na ndipo wote watatu walitaharuki kusikia ripoti iliyorudi.
"Mkuu tumefanya kila jitihada za kufanikisha kuja na mtuhumiwa lakini hatukufanikiwa kumpata baada ya kutoweka masaa machache kabla hatujafika."
"AMETOWEKA!!!?"

"Ametoweka toweka vipi! wakati nilimuacha mimi mwenyewe pale misibani na hayakupita hata masaa sita?!"
alihoji kwa mshangao Kamishna Shebby.
"Ndio hivyo mkuu na tumerudi baada ya kuona muda unaenda pia tulisahau mawailiano na tuko tayari kwa amri mtayotupa ila tumewaleta hawa wake wa marehemu wanaweza kutwambia wapi alipo mtoto wao."
"Huo ni upumbavu. sikutaka aletwe mjane yeyote hapa. Chukueni vitu vyenu kusanya vijana wako msako uanze mara moja hadi apatikane huyo kijana."
Alitoa amri Kamishna Shebby na kumuamuru Kimaro aendeeshe gari yao ambapo safari hii walipanda wanne sambamba na Mkuu wa upelelezi na jumla ya gari tatu zilitoka kituoni kuelekea Mkuyuni stendi huku jumla ya vijana wenye bunduki zaidi ya kumi na tano wakiwa kwenye difenda mbili katikati kukiwa na gari iliyowabeba kina Shebby na kituo kilibaki na askali wachache sana wakiongozwa na mama mmoja aliyekuwa nae na cheo cha sub inspecta.

Wahuni na watu wote Mkuyuni walipigwa na bumbuwazi mara baada ya kuona msafara wa polisi ukisimama kwa fujo zote maeneo ya stendi.
"Oya wana Kimenuka anga hizi tujikataeni.."
aliongea teja mmoja aliyekuwa anacheza kamali na wenzake pale stend mara baada ya kuona difenda zile za polisi.
Kilichoendelea pale askali walitawanyika na msako mkubwa ukaanza huku wahuni wengine wakikimbia ovyo kwa kuhofia huenda walikuja kukamatwa wao.
Kamishna Shebby pamoja na wenzake ocs John, st;sajent Kimaro na yule mkuu wa upelelezi wao waliongoza moja kwa moja mpaka pale msibani sambamba na askali watatu wenye bunduki.
Wakati huo Shebby nae alikuwa kashachukua pisto yake ndogo anayoiachaga kwenye dashibodi ya gari huku kimaro nae hivyo hivyo alichukua yake na kuichokea nyuma ya mkanda wa suruali na watu wote pale msibani walizidi kustaajabu kwani muda si mrefu uliopita walikamatwa wake wa marehemu na kuzua sintofahamu kwa kila mtu aliyekuwa pale msibani.
"Babu, naomba usiwe na wasi wasi tutajie wapi alipoenda yule mtoto wa huyu marehemu."
ilikuwa ni sauti ya Kamishna Shebby mara baada ya kumfata yule babu aliyekuwa amevaa kibaraghashia alipokuwa anaongea huku amezungukwa na watu waliokuwa wanaulizia kilichotokea muda mfupi kabla hawajaja kina Shebby.

ITAENDELEA.....
 
EPS 28
========

Alijikuta anakata simu aliyokuwa anazungumza na babaake na kuwaita wenzake haraka waje washuhudie kile alichokuwa anashuhudia na wote walipofika na kutazama kule juu walistaajabu sana baada ya kuona mwili wa yule kijana ukining'inia kwenye moja ya tawi lililojificha la ule mti huku shingoni mwake kupitia juu ya kichwa kukionekana kamba iliyofungwa kwenye lile tawi.

"Haa!! Ina maana nae kaamua kujinyonga!!?"
alitahayuri Ocs mara baada ya kuushuhudia mwili wa yule kijana ukining'inia pale juu.
Hali ile ilimtisha kila mtu na kuwachanganya vichwa askali wote wasijue kwanini yanatokea yale katika ile familia hususani kwa upande wa Kamishna Shebby alibaki na bumbuwazi na kuzidi kuamini kuwa hawa watu hawajiui bali yupo muuaji tena hayupo mbali kabisa na wao na huyo anayewaua atakuwa kwenye mtandao wa mr.X tu si vinginevyo kwani aliamini kulopoka kwake siku ya kwanza pale chumbani alipokuwa anaugua mzee Mnyungunyungu huwenda ikawa ndio chanzo cha matatizo kwenye hii familia na kupelekea vifo vya wote waliokuwa na walau tetesi juu ya mr.X
((('hivi huyu Mr. X ni mtu wa aina gani mwenye mbinu kiasi hiki na kugundua mitego yetu yote na kutuwahi kabla hatujafanikisha walau kupata njia ya kuanzia. Daah!! siku ya kumgundua huyu mtu sitothubutu kumfikisha kwenye sheria ya nchi, nitamuhukumu mwenyewe haiwezekani ghaa!!')))
Alijisemea mwenyewe Kamishna ndani ya moyo wake kipindi nae akichukua picha kupitia simu yake eneo lote la tukio.

Alimuamuru ocs na kufanywa mawasiliano ya haraka kustopisha zoezi lililokuwa linaendelea kule kwa vijana wao na kuwataarifu waje eneo la tukio.
Baada ya vijana wote kufika pale huku umati mkubwa wa watu ukijazana maeneo yale na kila mtu kutoamini kile akisikicho ama akionacho eneo lile.
Baada ya vijana wa jeshi la polisi kufanya jitihada na kufanikisha kuushusha ule mwili amri ilitoka na kuubeba mpaka zilikopaki difenda na kuupeleka hospital kwaajili ya uchunguzi zaidi huku kina shebby na askali wachache wakibaki bado eneo la tukio kwa uchunguzi zaidi.
Katika tafiti na maswali yalikuwa kichwani mwake kamishna Shebby bado alihisi lazima kati ya wale wazee mmoja wapo akawa kwenye mtandao wa mr.X na ndie aliyevujisha siri za yeye kutaka kumjua mr.X na ndio sababu za vifo vya wale watu ambao aliamini wangmsaidia kwa namna moja kuijua njia ya kumjua mr.X.

Ndipo hapo Kamishna Shebby alipowaita pembeni kina Kimaro na kujadili nao.
"Eti mmepata picha gani kuhusu haya matukio hususani hili la sasa ni kweli yule mtu amejinyonga mwenyewe au nini kimefanyika?"
"Daah! kiukweli mkuu hii inachanganya sana, nikisema hajajinyonga mwenyewe sasa nani kampandisha kule juu!! dah! kama nae kajinyonga ni kwasababu zipi! yaani bado mimi sijapata picha"
aliongea ocs huku akiwa katika hali ya sintofahamu.
"Vipi Kimaro unasemaje?"
aliuliza tena Shebby
"Mh! mkuu mimi bado natafakari sijapata jibu lolote kwakweli"
alijibu kimaro huku akitazama kwenye ule mti na ndipo akabaki yule mkuu wa upelelezi ambae alikuwa hajaongea kitu.
"Mkuu, mi naona kama huyu mtu hajajinyonga kwa ridhaa yake na nimeanza kutia shaka huenda hata babaake nae hakujichinja kwa ridhaa yake na vifo vyao wote vimesababishwa na mtu mmoja ambae nahisi atakuwa na mbinu kubwa sana za kijeshi na yupo karibu mno na hii familia."
Aliongea yule mkuu wa upelelezi ambae maneno yake yaliungwa mkono moja kwa moja na Kamishna Shebby.
"sawa kabisa, sasa hapa kuna mchezo wa akili nyingi sana unaoendelea na usikute muuaji anatuangalia tunavyopagawa na pengine tuko jirani nae muda mwingi baada ya tukio.
Sikia Kimaro nina mashaka na wale wazee watano huenda mmoja wapo akawa ni mtu wa karibu na mr.X na ndie aliyevujisha habari kwa mr.X kwamba kuna watu wanamfatilia kutaka kumjua sasa mr.X ameamua kuwaua wote walio na fununu walau kidogo kuhusu yeye na hii inanihakikishia kuwa MR.X yuko hai."
"Duh! mkuu sasa hapa tufanyeje."
"Inabidi sasa hivi ocs tuongozane na vijana tuwakamate wazee hawa wote twende nao tukawabane tuweze kumjua anayevujisha siri kwa mr.X kabla hatujachelewa kwani kwenye hii familia watu pekee waliokuwa na siri za mr.X wote washakufa na aliyebaki ndio kichaa hana kumbukumbu zozote hawezi kusaidia kitu naamini sasa hata huyo mzee anaweza kutoroka na muuaji aliyetumwa na mr. X na habari zake kubaki kizani milele."
Baada ya Kamishna Shebby kuongea yale wote walikubaliana na kumuunga mkono kisha ocs alichukua radio call na kuongea na sub inspector wake kumpa maelekezo kamili.

* * * * * *

Baada ya mwanae kukata simu na kubaki na taharuki asijue kulikoni mzee Mwinchande alimuangalia yule mkuu wa gereza msaidizi kwa mshangao hali iliyomfanya mkuu saidizi nae ashangae na kumuuliza.
"Vipi baba kulikoni? anasemaje mkuu."
"Kijana kumbe kuna mission za kijeshi zinaendelea huko tena mbali nawe unajifanya hujui?"
aliuliza kwa mshangao mzee Mwinchande na kujikuta anafichua kile alichozungumza na mwanae ambae alimuomba asimwambie mtu zaidi atakuja kumuelezea mwenyewe.
"Mission zinaendelea? mbona sifahamu mzee wangu kuhusu hiko usemacho?"
"Ufahamu vipi na uko ofisi moja na mwanangu tofauti vyumba tu? ina maana hujui kama Kamishna wako yupo morogoro muda huu kwenye kazi maalum tena inaonekana nyeti sana kwa jinsi alivyokuwa anaongea hadi akanikatia simu!!"
aliongezea mzee mwinchande na kumfanya yule mkuu msaidizi abaki ameduwaa mithili ya mtu aliyebaini kitu furani na kutokana na mzee Mwinchande kuwa na uzoefu wa miaka mingi wa kiaskali aligundua baada ya kuutazama uso wa yule msaidizi wa Shebby na kum bana maswali pale pale.
"Hivi kuna mabadiliko gani alikuwa nayo Kamishna yako hivi karibuni au mna tatizo gani baina yenu hadi aanze kuondoka pasi na kukuaga mtu wa jilani kama wewe?"
"Mh! kiukweli mzee wangu hatuna tatizo lolote mimi na mkuu wangu ilaaa..."
aliongea na kusita kidogo baada ya kuhisi si vyema kuongea habari za mkuu wake na kuijadili tabia yake pasi na lidhaa ya mkuu wake mwenyewe.
"sasa mwanangu unataka kunificha habari za mwanangu mwenyewe?"
"hapana mzee"
"Basi kama sivyo unasita nini. Hebu niambie ukweli umeona mabadiliko gani kuhusu mwanangu siku za karibuni hadi aondoke na kuwa na mission pasi na kukutaarifu mission gani."
alikazia mzee Mwinchande na kumfanya yule msaidizi kueleza kila kitu alichokuwa anakijua na kuhisi ndicho kilichom badilisha Kamishna wake mpaka kuwa na mission za siri.
"Kiukweli mzee wangu huenda hili ninalohisi ndio ama sio sina uhakika ila tokea mkuu alipoanza kuwa karibu na mfungwa mmoja humu gerezani alikuwa na mambo ya ajabu ajabu ya kuandika kwenye kuta ovyo ovyo kuwa wanawake ni wauaji mara kwenye miti anachunachuna na kuandika hayo maneno halikadhalika na tabia yake ya kuropoka kwa sauti kubwa muda mwengine hayo hayo maneno na gerza zima lilimtambua yule bwana nusu chizi lakini ajabu mkuu akafanya jitihada anazozijua yeye hadi akafanikisha kuzungumza nae na inaonekana hadithi ya huyo bwana ilimgusa sana mkuu na hapo ndipo akaanza kuwa bussy sana na kutoka nje ya gereza mara kwa mara so, nahisi huenda kuna upelelezi amaeamua kuufanya binafisi juu ya kesi ya yule bwana ambayo ilisemekana ameonewa kwa mujibu wake mwenyewe."
"Oooohoooo! Duh! sasa mwananguuu ina maana anataka kumsaidia huyo mtu."
"Nahisi mzee, lakini sijui kilichomshawishi maana kesi yenyewe ni ya zaidi ya miaka ishirini na saba."
"Hee!! hivi Shebby mwanangu akili zake zimeingiwa nini hadi ashawishike kufanya upelelezi wa kesi ya miaka kibao namna hiyo? hee!!"
Alitahayuri na kukunja uso mzee Mwinchande kisha akatoa tena simu yake na kuanza kubinya binya namba.

ITAENDELEA...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…