Simulizi: Wanawake ni wauaji

Simulizi: Wanawake ni wauaji

Ahsante kipenzi kwa kuniita, nilishaisoma sehemu hii, nadhani nimeimaliza last wiki tu, ni story nzuri yenye mafunzo, wanawake kweli ni wauaji ila sio wote
Anhaa haamna neno, usijal
 
  • Thanks
Reactions: ram
EPS 02
========

“Karibu baba.” Sauti ya mama mkwe mtarajiwa ilinikarimu nilipomkuta akiwa nje amekaa kwenye kolido ya nyumba yao akiwa anasukwa na mwanaye mwengine wa kike.
“Asante mama shikamoo”
“Marahaba baba za huko”
“Safi tu mama sijui ninyi”
“Sisi kama unavyotuona baba tunamshukuru Mungu. Enhee mbona hivyo baba kwema!”
“ehe!hee..! Kwema tu mama.” Nilijibalaguza kwa kujichekesha baada ya kuhisi huenda mama Mamu kashastukia mchezo ila ananitega. Lakini kabla sijakaa sawa nilishangazwa na swali ambalo nilijikuta nashindwa kulielewa na kuuliza tena.
“Unasemaje mama!!?”
“Nimekuuliza mwenzio yuko wapi? maana alituaga anakuja huko kwako muda mlefu tu aliondoka hapa sasa umenishangaza nawewe umekuja muda huu ukiwa peke yako! ndio maana nimekuuliza awali kwema?”
Nilijikuta nashusha pumzi kwanza mara baada ya kusikia na kubaini kuwa Mamu hajafika kwao tangia muda ule alipoondoka kwangu.
“Vipi baba mbona huongei..! unatutisha wenzako” Sauti ya mshangao ya mama mkwe ilinitoa kwenye dimbwi la mawazo ya ghafla nilipokuwa nafikiria alipoenda Mamu muda wote ule hajafika kwao.
Niliogopa kimtindo ila nilificha machoni. Niliwaza kama kitampata kitu kibaya huko basi namimi nitahusika kwa kiasi kikubwa pia nilivyoelewa kuwa Mamu atakuwa kachanganyikiwa sana na anaweza kujifanyia hata kitu kibaya mwenyewe kutokana na kujua kiasi gani ananipenda na mara nyingi hakutaka nimuudhi kabisa.
“Hah, ni hivi mama kweli Mamu alikuja lakini hakukaa sana akadai kuwa kuna vitu amesahau na alinambia nimsubiri sasa nimekaa na nilipoona anachelewa sana ndipo nikaamua kuja huku kwa lengo la kumfata yeye. Ndio maana ulivyoniuliza yuko wapi nimeshangaa ina maana hujamuona huku kurudi?”
“Hee!! We babaa eeh ina maana awe karudi halafu mi nikudanganye! Mwanangu si mzururaji hebu usitufiche baba nambie umemuacha wapi mwenzio au nini kimetokea huko kwenu..?” Uso wa mama mkwe ulinawiri mseto wa mashaka na hasira hata kumsimamisha mwanae aache kumsuka.
“Hakuna chochote mama, usiwe na wasiwasi.” nilijaribu kumtuliza.
“sasa mbona hueleweki eleweki simu unayo kwanini hukumpigia kujua alipo hadi unakuja kumuulizia?”
“Okeeey, samahani mama nimekumbuka alinambia kabla ya kuja huku kuna sehemu kwa shogaake angepitia kule mwenge. Tena ngoja nimfate huko kabisa nahisi hajatoka”
Ilinibidi kudanganya na kuongea maneno ya matumaini hasa mara baada ya kumuona yule mama akizidi kubadilika.
Kiukweli nilitambua kitambo kuwa Mariam anapendwa sana na mamaye na ukizingatia yule mama alikuwa na watoto wawili tu. Wote wa kike, babayao alishafariki muda mlefu sana hivyo hata jinsi alivyowalea wanae kwa taabu na maadili walikuwa si watu wa kutokatoka ovyo wala kuzurura. Na ndio sababu kitendo cha kusikia mwanae hayupo kwangu kilianza kumchanganya kidogo nami nikatumia akili ya ziada kumtuliza na kumkwepa kwa kujidai naenda Mwenge kwa huyo shoga yake Mamu.
“Baba naomba utavyorejea uje na mwanangu tafadhali, kwanza kisheria na kidini bado hujakabidhiwa. Asilale huko! oohooo”
Aliongea yule mama kipindi nikiondoka kuelekea kituo cha daladala nikiwa na mawazo mara mbili na niliyokuja nayo.

* * * * *

Safari yangu ilinipeleka mpaka pande za fukwe za coco na lengo halikuwa kuogelea wala kufanya mazoezi bali ni kupunguza angalau robo ya mawazo yaliyoandamana kichwani. Niliichukia siku ile kwa kulaumu ni heri tusingekutana tu na Mamu kwani mipango yote ya kufurahi pamoja wikiendi iliyeyuka ghafla kama machozi ya samaki kwenye maji. Niliwazia nitamwambia nini yule mama endapo Mariam asingeonekana siku hiyo kabisa. Niliwaza pia ina maana Mamu anaweza akajifanyia tukio hata la kunywa sumu kwa kajiugomvi kale tuu! Na kama akifanya hivyo nini kitanikuta baadae..! si ndio itakuwa basi tena! Niliwaza mambo mengi sana na kuchukua tena simu kupiga namba ya Mamu lakini bado jibu likawa lilelile ndipo nilipogundua sasa Mamu atakuwa kani-'reject'.
Nilijisonya na kumtumia ujumbe nikimsihi na kumuomba popote alipo basi arudi nyumbani haraka wanamtafuta. Japo nilituma zaidi ya meseji tano lakini hakuna hata moja iliyojibiwa. Nikiwa bado nimekaa juu ya jiwe moja nimening’iniza miguu huku nikiirusharusha na kuangalia watu mbalimbali wakifurahia maisha ufukweni, ndipo nilipoangaza macho huku na kule moyo wangu ulilipuka ghafla nilipomuona binti mmoja akiwa kavaa kipensi chepesi kifupi kilichom-bana barabara huku akiacha sehemu kubwa za mwili wake nje ambapo kifuani alijisitiri na kisidilia kidogo cha kamba.
Macho hayakuamini nikionacho huku mapigo ya moyo yakiongeza mwendo wa msukumo wa damu. Kilichonistua zaidi si uzuri wake wala umbo lake ama mavazi, la hasha! bali nilipouona uso wake ambao niliujua vizuri mno. Nilishindwa stahimili kumtazama binti akiwa kashikwa kiuno na baunsa mmoja ambae kushoto kwake alishika pira kubwa la kuogelea. Hakuwa mwengine yule binti bali kipenzi changu Mariam akiwa na yule njemba wakielekea majini huku wakionesha nyuso za furaha.
Nilijikuta mwili ukinitetema kwa hasira na midomo kunichezacheza huku macho yakiwa hayaamini kile kilichokuwa kinaonekana.
"!!Shiit!!!...?!" Nilihamaki na kuruka pale juu ya jiwe na kukanyaga maji licha ya kuwa nilivaa viatu simpo na suruali ya jeans lakini sikujali wala kufikiria hilo zaidi nilitembea haraka kama mwanajeshi macho yamenitoka nikielekea kule alipokuwa kipenzi changu Mamu na yule baunsa kabla hawajafika kwenye kina cha kuogelea.
“Mamu hapa unafanya nini na huyu boya ni nani yako?” Nililianzisha punde nilipofika kwa kuwaputisha mikono waliyoshikana.
“Boya? Hii we kaka vipi.. Eti baby unamjua huyu!!?” Alijibu kwa taharuki Mariam huku akinishangaa na kujisogeza jirani zaidi kwa yule njemba aliyekuwa ananitazama kwa hasira. Moyo ulinichoma na kujikuta naongea huku midomo ikinicheza cheza kwa kutoamini kama yule ndie Mamu ninayemjua mimi au kivuli chake.
“Mamu !!? hivi umepatwa na nini lakini..!”
“Hivi baby unamuelewa huyu..” Aliongea Mamu kumuuliza yule baunsa kwa kauli iliyonichoma zaidi ya msumali wa moto uliopigiliwa katikati ya kidonda na kubaki natazamana na yule mwamba aliyevimbiana kishari. Alikuwa mtu wa miraba minne aliyestahili kuitwa jitu. Umbo lake komavu lililovimbiana misuli lilitosha kumuogopesha mpenda amani yeyote kama mimi. Jitu jeusi kipara lenye sura iliyobeba alama zote za uvunjifu amani lilinikazia macho na kunikoromea.
“Oyaa wee bwege, usitupotezee muda katika starehe zetu hebu jikatae haraka kabla sijakufanya kitu mbaya sasa hivi, tena usinihamshie wazimu oooohoooo POTEA!” Lilifoka lile baunsa na kunisukumia majini. Haa! nami sikukubali japo sikuwa baunsa wala kuwahi kucheza mchezo wa ngumi, nilijikaza kiume na kumsukuma pia huku nikirusha maneno ya ndaro.
“Oyaa usinitishe wewe hizo nyama tu hata kwenye sambusa zipo. Sikuogopi wala nini! kwan......”
Nilipayuka nikisahau kuwa mdomo huponza kichwa. Ndipo hamadi! Kabla sijamaliza kauli nilistukia napigwa ngumi kali ya meno iliyonipeleka moja kwa moja chini na niliponyanyuka ili nikabiliane naye alinibamiza na lile pira usoni hadi nikaona cheche za moto mbele yangu na nafsi yangu kutamani watu waje kutugombezea haraka kabla uhai haujaniponyoka. Lakini ubaya wa watu wa jiji la Dar ndio kwanza walikusanyika na kuzunguka eneo lile wakitufanya sinema pasipo kuniokoa. Hata kipenzi changu Mamu hakujali wala kusema chochote.
’PWAATCHAAA’
Maji yalichapachika zaidi ingawa yalikuwa ya ugoko lakini kwa nilivyodondoshwa mara ya tatu ilitosha kulowana mwili mzima huku mengine yakiniingia puani na mdomoni kana kwamba nilitupwa kwenye kina kilefu. Kilichonisikitisha zaidi ulinzi eneo la fukwe naweza kusema kama haukuwepo kabisa kwa raia zaidi askari wachache walikuwepo eneo la nyuma za fukwe wakilinda magari yaliyoegeshwa. Nilipiga hesabu za haraka na kuona kama nitazembea zaidi naweza kukata moto mikononi mwa njemba yule aliyenichachamalia kuutafuta ujiko mbele ya Mamu na umati ule.
Nilinyanyuka kwa mbwembwe huku nikijifanya nami namtafuta nimpachike zangu ndipo 'paaap' kwa kwa kasi ya kope niliinama sambamba na kutoa ukelele wa hatari na kumrushia maji sambamba na michanga usoni yule baunsa na alipozubaa tu sekunde zilezile nilipenya kwenye ukuta wa watu na kukimbia eneo lile kwa kasi ya mshale nikiwaacha wakizomea na wengine wakivunjika mbavu kwa vicheko.
Daaah!! katika siku nilizowahi kujisikia vibaya na kupatwa aibu kubwa ambayo sitoweza kusahau na hii pia ni mojawapo. Niliumia sana hususani pale nilipoisikia sauti ya Mamu ikiambaa juu ya sauti zile zilizokuwa zikinizomea pale ufukweni. Sikumbuki kwa kasi niliyotoka nayo kama lile jitu lilinifukuzia ama laa, lakini ninachokumbuka vizuri ni pale nikiwa ndani ya daladala mara baada ya kustuliwa na sauti ya dada mmoja.
“Wee kaka vipi! Simama vizuri unaniloweshaa…!!” Sauti hii ilinifanya nijibane zaidi mlangoni aliposimama konda huku abiria wengi wakinishangaa kwa mwonekano wangu. Nilikuwa zaidi ya kituko nilivyolowa chapachapa mchana ule wa jua kali. Ilinibidi nishuke tu kituo cha mbele kwa aibu. Taratibu mguu mosi mguu pili, nilihesabu hatua macho chini kama mwali wa kimakonde huku njia nzima kila niliyepishana nae akinishangaa si mkubwa wala mtoto.
Kwa mwendo wa sawajiko nilifika 'getto' na kuchojoa zile nguo za masahibu na kuvaa taulo. Ndipo niliduwaa zaidi nilipojitazama kwenye kioo cha 'dressing table' na kubaini kuwa nilikuwa na uvimbe kwenye paji la uso, jicho moja lilivilia damu pia mdomo wangu wa chini ulipasuka na kulikuwa na damu zimegandia sehemu ya kidevu. Nilisonya na kumlaani Mariam kwa uchungu mara machozi yalibisha hodi usoni mwangu na kilio kuniponyoka. Maumivu yaliyokufa ganzi awali sasa yalifufuka upya mwilini mwangu. Nilijikaza na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniokoa kwenye mikono ya jitu lile lililokosa huruma. Nilijikagua vizuri kinywa kilichosheheni uzito wa maumivu na kubaini kumbe hata jino moja la mbele liling'oka na fizi kuvimbiana. Nilidata zaidi kwa uchungu punde taswira iliporudisha tukio lile machoni mwangu na muda uleule niliamuaa kuifuta kabisa namba ya Mamu kwa amri ya nafsi yangu iliyotibuka na kutotamani kuonana nae tena..! Niliiendea ile suruali niliyoivua muda mfupi pale chini lakini nilipotazama mifukoni kutafuta simu nayo sikuiona hata pochi yangu ya fedha pia haikuwepo.
"Dooh! nimepoteza kila kitu shaabash!" Nilisema mwenyewe nilipobaini kuwa lazima nilividondosha kwenye hekaheka ile hasa nilipokumbuka kuwa hata kwenye daladala nauli sikulipa wala konda hakunidai punde niliposhuka kule njiani. Nilishusha pumzi na kumshukuru tena Mungu na kuwazia hata nitaponunua simu sitokuja kuirejesha namba yangu wala sitomtafuta tena Mariamu kivyovyote. Niliwasha jiko la mchina na kuchemsha maji kisha nilielekea moja kwa moja bafuni kwa zoezi la kujikanda na kujisafisha kabla ya kwenda famasi kununua dawa za kutuliza maumivu.

_________________
ITAENDELEA,,,,

Hahahaha...

Jamaa katia sana huruma, imesikitisha sana...

Ila Mariam kaniudhi sana... kisirani chote kile alichomletea jamaa yake ni ilikua gia tu, apate upenyo wa kwenda beach na huyo jamaa mwingine baunsa... alafu anamkana kabisa jamaa yake mbele ya baunsa, kupelekea jamaa kupewa kichapo...


Cc: mahondaw
 
pale mtu unapotamani kusoma hadithi na muda hautoshi...,
mara moja moja nitafuatilia kimya kimya
 
EPS 16
========
* * * * * *

Saa tisa alasiri maeneo ya Kibamba kijiji cha Hakipo ambacho sasa kilikuwa si kijiji tena kutokana na jiji kupanuka na hata barabara ya pale njia panda ilikuwa ya lami pia hakukuwa na pori lolote kama ilivyokuwa zaidi ya miaka 25 iliyopitakwa mujibu wa hadithi ya Hussein.
Ilionekana gari moja ya kisasa aina ya Vorgie ikisimama mkabala na maeneo ya stend na walishuka vijana wawili watanashati wakiwa wamevaa suti nadhifu.
Mmoja wa wale vijana hakuwa mwengine bali ni Kamishna Shebby sambamba na dereva wake ambae pia alikuwa mlinzi wake wa karibu kunapotokea dharula yoyote.
waliingia kwenye duka moja lililokuwa jilani na kununua sigara ndipo Kamishna Shebby ambae ilikuwa ngumu mno kumtambua kama ni askali tena mwenye cheo kikubwa kutokana na alivyojieka, alimuuliza kitu yule mama aliekuwa anawahudumia pale dukani.
" Samahani mama, hivi ushawahi kumsikia mzee mmoja alikuwa mganga maarufu sana maeneo haya zamani aliitwa Mnyungunya?."
" Mnyungunyaaa.. Mnyungunyaaa mh!! hilo jina silikumbuki vizuri lakini nahisi kama niliwahi kulisikia ila nendeni palee kwenye kile kibanda cha kahawa kwa wale wazee wanaocheza bao ndio wenyeji wa mji huu haswaa nadhani watawasaidia"
Alijibu yule mama huku akinyoosha kidole kuwaelekeza kina Shebby na hapo ndipo walipomshukuru na kuvuka barabara mpaka pale kwenye kibanda cha kahawa na kuwasalimu wazee waliokuwepo pale.
" Karibuni sana kina baba"
walikaribishwa na mzee mmoja aliyeonekana kuwa mcheshi sana na ni mtaalam sana wa kucheza bao.
"Ahsanteni sana wazee wangu, samahani mzee naomba tuzungumze kidogo "
Aliongea Kamishna Shebby na kusogea pembeni kidogo na yule mzee mcheshi.
" Enhee baba nakusikiliza ipi shida yako."
Aliuliza yule mzee huku akimuangali kwa umakini Kamishna Shebby.
" Mzee nadhani utakuwa unafahamu kuhusu habari za aliekuwa mganga maarufu sana miaka ya nyuma katika kijiji hiki aliyeitwa Mnyungunya."
"Mnyungunya?.."
"Ndio mzee wangu"
"Mnyungunya babaa huyo simfahamu ila mganga wa zamani maarufu hapa kwetu aliitwa Mnyungunyungu."
Alijibu yule mzee ndipo kwa akili ya haraka Shebby alibaini kuwa huenda jina lilikosewa kidogo mtandaoni au yeye ndie alikopi vibaya.
"Eeeh, samahani mzee wangu ndie huyo huyo Mnyungunyungu"
"Enhee sasa baba shida yako wewe nini hasa "
"Shida yangu kubwa mzee ningependa kufahamu kama yu hai nielekezwe anapoishi nikaonane nae mwenyewe "
"Na kama alishafariki je? sema mwanangu kama una tatizo la kiufundi asilia nikupeleke kwa mafundi wengine manguli wa hapahapa"
"Hapana babu sina tatizo ila hata kama iwe amefariki ningependa kuonana hata na familia yake pia."
"kwani kijana wewe ni nani yake "
aliuliza tena swali yule mzee akionesha kuwa na wasiwasi na Kamishna Shebby.
Na kutokana na uwezo wa kuisoma akili ya mtu kiharaka kamishna Shebby alichomoa noti tatu za elfu kumi kumi na kumkabidhi kinyemela yule mzee pasi na mtu yeyote kuona.
"Mzee wangu mimi ni mtoto wa rafiki mkubwa wa mzee huyo na nina habari muhimu sana juu yake au familia yake."
"sawa mjukuu wangu sasaaa ngoja nikudokeze kitu hebu sogea kwa huku najua sitokosa walau hela ya kahawa hehehehe.."
Aliongea yule mzee kwa sauti ya chini huku akichekacheka na kumvutia tena pembeni Kamishna Shebby.
"Bwana huyo Mganga kweli alikuwepo hapa kijijini lakini alitoweka zaidi ya miaka 25 au 27 iliyopita kama sikosei na habari zake tunazijua watu wachache sana juu ya kutoweka kwake kwa sababu binafsi za kiusalama yeye na familia yake..
Ukweli ni kwamba Mnyungunyungu hapa alihama kimya kimya baada ya kesi ya mwanae mtoto wa mdogoake huku kukiwa na tetesi kuwa kuna matatizo yaliwakuta na familia yake japo hakuwahi kumwambia mtu ukweli na mimi ndie nilikuwa rafiki yake mkubwa enzi hizo japo kidogo alinizidi umli lakini inasemekana kuna watu walikuwa wanamuinda ndipo alipohama kinyemela na kukimbilia Morogoro kijiji cha mkuyuni kuendelea na maisha yake huko.
Kwa hiyo nisikufiche mjukuu wangu hapa huwezi kupata ukweli wowote zaidi juu ya taarifa za Mnyungunyungu labda uende huko Mkuyuni ambako aliendelea pia na shughuli zake za uganga."
.. Baada ya kupata taarifa zile Kamishna Shebby alimshukuru sana yule mzee na kumuongezea noti nyengine mbili za elfu kumi kumi na kumpa ishara dereva wake ya kuondoka baada ya kuwaaga wazee wengine pale kibandani
Akili yake ilimsukuma moja kwa moja kuwa sasa hana budi kuanza safari ya huko Morogoro jioni ile ile ikiwezekana asubuhi na mapema kesho yake wawe hapo Mkuyuni ili apate ukweli kuhusu huyo Mganga Mnyungunyungu juu ya kilichotokea zaidi ya miaka 25 nyuma.

* * * * * *

Hali ya hewa ilikuwa ya ukungu mwingi sana majira yale ya asubuhi siku hiyo huku kiubaridi kikipuliza na kuleta hali ya unyunyu wa majimaji sehemu zote za kijiji cha mkuyuni mkoa wa Morogoro ambapo ilionekana gari ile ya Kamishna Shaaban ikiwasili eneo lile la stendi ya mabasi yaendayo mjini na kuegesha sehemu moja kulipokuwa na nyumba ya wageni (guest) karibu kabisa na stendi.
Walishuka kwenye gari huku kichwani mwa Kamishna Shebby akiwa na hamu kubwa na shauku ya kujua habari zaidi kuhusu huyo mganga Mnyungunyungu.

" Samahani mkuu, hivi kwanini unaonekana kuguswa sana na yule Babu bubu hadi kufika huku kote?"
Aliuliza dereva wake ambae pia alikuwa na cheo cha Staff Sajent pindi walipokuwa wanavuka barabara kuelekea sehemu kulipokuwa na frem nyingi ambazo zilikuwa hazijafunguliwa bado huku kwa nje kulionekana vijana mbalimbali na wapiga debe.
" hahahahaaa Unataka kujua kwanini?"
Aliuliza Kamishna Shebby.
" Ndio bosi wangu "
" Kwasababu wanaake ni wauaji hahhaahaa "
" ha ha ha haaa "
Walicheka kwa pamoja wakati huo tayari walikuwa pale walipo wale vijana.
Kamishna Shebby na St,Sajent Kimaro mbali ya kuwa mtu na mkuu wake lakini pia walikuwa marafiki wakubwa na utani wa hapa na pale, hii yote ilichochewa na umli wao kuendana sana.

" Mambo vipi kaka."
Alimsalimu jamaa mmoja Shebby.
" Poa mkuu karibuni."
"oke, naomba tukuulize kitu, eti we ni mwenyeji hapa mkuyuni?"
"Yaah mkuu sana sana tuu mimi ndio Chibu mjukuu wa Mdede aliyekuwa chifu wa mwisho wa Mkuyuni hii.. hapa jisikieni kama mko kastama kea (customer care) vileee laivu (live) bila chengaaa.. waleee wa morogorooooo Mtoto mori ya kwanza mmeiwahii.. enhee. sema mkuu nawasikiliza "
aliongea kijana yule kwa mbwembwe hali iliyowafanya hadi kina shebby watazamane na kucheka pindi walipokuwa wanamsikiliza na kumuangalia anavyounganisha maneno yule kijana aliyejitambulisha kwa jina la Chibu wakati pia akiendelea kuitia wateja waliohitaji huduma ya usafiri alfajiri ile
ITAENDELEA...
 
EPS 17
========

"sawa bwana Chibu basi kwa kuwa hali ya hewa haijatulia kidogo hapa nje hebu tuingie mule mara moja tuzungumze.."
"Aaah, braza nangoja posho yangu kwanza hawa wajomba wanaweza kutimka afu nikakosa kifungua kinywa."
Alitilia mgomo kidogo Chibu baada ya kina Shebby kumuomba waingie kwenye mgahawa mmoja uliokuwa eneo lile ambao ulishafunguliwa na hapo ndipo Kamishna Shebby kwa utaalam wake alitumia akili ya ziada na kumuulizia kiasi cha posho yake ya upiga debe kwa gari ile na ndipo Chibu alipodanganya kwa kutaja kiasi cha juu kidogo na Kamishna shebby aligundua kama anadanganya lakini ilibidi ampe tu kwani alichohitaji yeye ni kitu kimoja tu kujua habari za ba mkubwa wa Hussein huyo Mnyungunyungu ili aweze pata majibu aliyoyakosa hata Hussein mwenyewe.
Na baada ya kumpatia kile kiasi cha pesa yule kijana ndipo walipoongozana hadi mule mgahawani.

Wahenga walisema ukitaka kumroga mwenye njaa akwambie akijuacho basi mkarimu kwa vyakula vizuri.
Na ndivyo alivyofanya Shebby baada ya kumuagizia Chibu supu kubwa ya samaki kwa chapati za mayai taratibu waliagiza na wao na kuanza kunywa huku wakipiga story.
"Ee bwana Chibu hivi unamfahamu mzee mmoja wa muda mrefu tu alikuwa hapa mkuyuni anaitwa Mnyungunyungu.."
"Mnyungunyunguuuuu okeee!! si yule mzee wa miti shamba babu wa tunguli au..!!"
"Haswaa.. ndie huyo hivi bado yupo?"
"Mh!! yule Yule mzee kwa kweli nina muda mrefu sana sijamuona anga hizi karibu miaka miwili sasa ila kuna kipindi nilisikia tetesi yuko hoi sana si unajua eji (age) nayo imepogoma sana "
"Sasaaa duh! utatusaidiaje Chibu."
"Msajili wakubwa mpo na Chibu hakitoharibika kitu. ngoja nimdadavue kwanza huyu makfish harafu nitawapeleka kule bondeni kwenye kijiwe chake pale ndo mtapata fulu nyuzi (full news)"
Aliongea Chibu huku akinyofoa mnofu mkubwa wa samaki na kuufinyanga sambamba na kipande cha chapati.

* * * * * *

Nusu saa baadae walikuwa washamaliza kupata kifungua kinywa na walionekana wakitelemka kilima kimoja na kuelekea kulipokuwa hiyo ofisi ya mganga Mnyungunyungu huku Chibu akiwa ndie kiongozi wa msafara.
Njia ilikuwa mbaya umbali wa mwendo wa zaidi ya nusu saa kufika huko kwenye hiyo ofisi huku njiani wakipita vilima vitatu vya panda shuka panda shuka lakini haikuwachosha kina Shebby kutokana na adhma yao ya kutaka kujua yaliyokuwa nyuma ya pazia miaka hiyo 27 iliyopita.
Hatimae walifika kwenye kibanda kimoja kilichozungushiwa vitambaa vyekundu na vyeusi ambapo nje kulioneka mabenchi ya kukalia na kulikuwa na kijana mmoja wa makamo ya kina Shebby akiwa ameketi pale na baada ya kuwaona wageni wale alisimama na kuwakaribisha kwa heshima.

"Sasa wakubwa hapa ndio penyewe na huyu kijana ni mjukuu wa mzee Mnyungunyungu na babaake pia yupo hapa nadhani watawatatulia matatizo yenu mi ngoja niwaache niwahi sokoni kule mida ya kupakia ndizi hii wasije kuniovateki (overtake) kwenye saiti (site) yangu buree. kwaherini wakubwa mtanikuta kule stend mtapotokaaa"
Aliaga chibu huku akiondoka na kama kawaida Shebby alimtazama na kutabasam kisha akamgeukia tena yule kijana
"Asante sana ndugu yangu enhee tumemkuta babu Mnyungunyungu?"
"Babu anaumwa muda mrefu tu ila hapa yupo baba ndie anayehudumia na kutibu watu. karibuni vueni viatu piteni ndani mkaonane nae.."
Alishusha pumzi kamishna Shebby kwa kushukuru pia kufika sehemu aliyoikusudia na baada ya kuambiwa habari ile ya ugonjwa wa Mnyungunyungu aliingia ndani huku mwenzake St,sajent Kimaro akibaki nje na yule kijana.

Aliingia na kumkuta bwana aliyekuwa amevaa upande wa shuka nyeusi (lubega) huku kiunoni amejifunga mkwiji mwekundu na kitambaa cheupe kichwani.
Na alipoingia tu alikaribishwa kwenye jamvi na kuanza maongezi.
" karibu sanaa.. karibu sanaaa sema shida yako kijanaa"
Alianza kuongea yule bwana mganga mtu mzima ambae kiumli wa muonekano aliendana na Hussein bubu.
"Bwana Mtaalam mimi sikuja kwa tatizo la kutibiwa ila nimekuja nina shida kubwa pengine kuliko matibabu na shida yangu ni kuonana na Mzee Mnyungunyungu"
"ooooh!! sawa kijana. mzee mnyungunyungu ni babaangu mzazi na kwa hivi sasa hapaswi kuonana na mgeni yeyote kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo kiafya si mtu wa kuongeleshwa wala kusumbuliwa..... Ni zaidi ya mwaka sasa toka aanze kuugua kwahiyo naomba kama kuna lolote linalomuhusu basi nitaarifiwe mimi kwa kuwa ndie mrithi wake wa kila kitu hapa na mambo yote nayaendeesha mimi."
aliongea yule bwana maneno ambayo yalimchoma Kamishna Shebby kwani shauku yake ni kuonana na huyo huyo ba mkubwa wa Hussein, tena amepata bahati bado yuko hai lakini yu mgonjwa.
Je, safari yake yote iishie pale na kurudi pasi na kumuona? moyo haukumpa kabisa kumaliza kila kitu na yule bwana mtoto wa mzee Mnyungunyungu na alitamani aende walau kumtazama tu hata kama hatozungumza chochote.

"sawa baba nimekuelewa vizuri lakini nakuomba sana tena sana nikamuone tu nafsi yangu ipate kuridhika kwa kuwa nimetoka mbali sana hadi kufikia hapa na nilihitaji kusikia habari ndogo sana kutoka kwake lakini nahisi bahati yangu inaelekea kuzama."
"habari gani hiyo tena ambayo unaona mimi nitashindwa kukusaidia?"
"Habari yenyewe mzee wangu si ya uganga ni habari ya miaka mingi kidogo nahisi yeye pekee ndie anaijua vizuri."
"Sasa mbona hunambii habari gani?? Hiyo miaka mingi mimi na wewe nani mkubwa? isitoshe yule ni babaangu najua kila kitu kuhusu yeye we nambie ni habari gani kwanza."
Aliongea yule bwana safari hii kwa sauti ya juu kidogo iliyomkasirisha kidogo Kamishna Shebby moyoni japo alificha hisia zake machoni na kuamua kumwambia kifupi habari aliyotaka kuisikia toka kwa mzee Mnyungunyungu.

"Sawa baba, unataka kujua habari gani niliyotaka kuisikia toka kwake?"
"Ndio nambie habari gani hiyo.!!"
"Habari kuhusu Mr. X.."
"..HEE!!..MR. X..!!!???."
Alistuka sana yule bwana hadi akaanguka pale juu ya kigoda alichokalia mara baada ya kulisikia jina la Mr. X.

Hali ile ilimstua pia Kamishna Shaaban na kushangaa mno kwa jinsi yule bwana alivyostuka hadi kupelekea kuanguka na kukaa tena haraka haraka huku akionekana wazi mapigo yake ya moyo kubadilika ghafra.
Kutokana na uzoefu na utaalam aliokuwa nao shebby juu ya kusoma saikology ya viumbe alielewa wazi kuwa yule bwana kuna vitu pia anavijua kuhusu huyo Mr.X na inaonekana amejijengea hofu ya miaka mingi moyoni mwake ambayo alishaanza kuisahau juu ya huyo Mr. X .

"Sikia kijana pokea kwanza hiki kibuyu na uongee ukweli wa nia uliyokuja nayo hapa na kama sio njema nakusihi uondoke sasa hivi kabla hayajakupata matatizo makubwa sanaaa AAgggmmbblblblblll"
Aliongea yule bwana huku akimpa Shebby kibuyu kimoja kikubwa kilichozungushiwa shanga nyingi juu yake na kutikisa kichwa kama mtu anaepandisha majini.
"Agh!! lakini mi sijaja kwa nia mbaya mzee!"
"Sawaaaa.. usiongee na mimi sasa ongea na mizimu kwanza ndio tuendeleee hahahaaa"
Ndipo Kamishna Shebby alipoamua kutii kwa kupokea kile kibuyu na kusema nia na sababu iliyomleta pale kisha kumkabidhi tena yule bwana aliyekuwa anayumbisha yumbisha kichwa mithili ya mwali anayenema huku safari hii kile kitambaa kilichokuwa kichwani alikishusha kabisa na kufunika uso wake.
ITAENDELEA.....
 
EPS 18
========
"Hiki hapa tayari baba"
"sawa sawaaa.. kieke hapo chini.. mmmmmnnnbbllllllllll.."
Alijitingisha yule bwana kwa kutetemeka kwa nguvu na kutulia kama dakika tano ndipo akajifunua uso huku safari hii alionekana presha yake kupungua sana na kuwa kawaida kidogo.
"Enhee kijana umesema unataka kujua habari kuhusu Mr.X!!"
"Ndio mzee wangu"
"Sawa na je umelitoa wapi hilo jina la huyo mtu hadi ukataka kujua habari zake na kipi kilichokusukuma uje hapa."
"Mzee wangu mimi niliwahi kuwa mfungwa ktk gereza la KINDU lililopo Kimbiji lile la watu wenye makosa mazito na huko nilipata rafiki mtu mzima tu kama wewe anaitwa Hussein na katika kuzoeana na kuhadithiana vitu ndipo aliponambia kisa chake mpaka akfungwa kwa na vitisho alivyovipata juu ya huyo Mr.X lakini alihisi huyu Mzee Mnyungunyungu kuna vitu alivielewa mapema kuhusu huyo mr.X lakini kwa bahati mbaya hakuwahi kumwambia hadi alipohukumiwa huko jera.
sasa mimi nimepata bahati ya kutoka mapema baada ya rufaa yangu kushinda sasa ndo moyo wangu umenisukuma kumtafuta mzee Mnyungunyungu ili anidokeze akijuacho ambacho hakuwahi kumwambia mwanae kuhusu huyo Mr.X alikuwa nani.."
Aliongea kwa kutia uongo ndani yake ili asiweze gundulika kama yeye ni askali kamishana Shebby wakati huo wote yule bwana alitulia akimuangali na kumsikiliza kwa umakini kabisa.
"Ooooh!! kweli mungu mkubwa. kumbe ndugu yangu Hussein bado mzima? mi nilishasahau kabisa nilijua alihukumiwa kunyongwaa daah.. masikini"
Alisikitika sana yule bwana na kumuangalia usoni kamishna Shebby na kumwambia.
"Pole sana kijana na wewe kwa yaliyokupata sasa kabla sijaendelea ningependa kujua iwapo ukishajua kuhusu huyo Mr.X utachukua hatua gani?"
"Mh!! mzee wangu nafikiria kuifufua upya hii kesi ili ujulikane ukweli ikiwezekana rafiki yangu aachiwe huru.."
"hahahahahahaaaa kijana hebu usifanye nichekee miee hahaha aachiwe huru?!! ufufue kesi!!? aaah.. huo utani sasa."
"Kweli mzee wangu naomba unihadithie unachokijua juu ya huyo Mr.X"
"Sawa mwanangu nitakwambia japo najua hutokuja kufanikiwa chochote na kama Mr.X yuko hai akisikia tu kuna kijana anataka kuichafua historia yake basi nina hakika atakupoteza kabisa kijana utasahaulika kwani huyo mtu uliyemtaja laiti ungemtaja miaka zaidi ya ishirini iliyopita naimani nishakutia panga la kichwa muda mrefu tuu"
"Kivipi baba, kwani alikuwaje huyo mr.X na aliwafanyia nini?"
Aliuliza kamishna shebby huku akibonyeza kimtindo kitufe cha kurekodi kwenye simu yake pasi na yule bwana kujua wakati akijiandaa kumpa habari juu ya kile akijuacho kuhusu Mr.X...
alijieka sawa yule bwana mganga mtoto wa mzee Mnyungunyungu na alianza kumsimulia hadithi yote aijuayo kuhusu Mr.X.......

*<>* <*> *<>*
................................
* * *

' ' ' ' 'Nakumbuka toka kipindi nakua hadi nafikia umli wa ujana niliishi na baba nikiwa ni mtoto wake wa tatu na wa mwisho kati ya wanaume na watano katika uzawa wetu ambao jumla tulikuwa kumi na sita.
Mara nyingi mimi ndie nilikuwa jirani na baba pengine kuliko wanae wote waliotangulia na baba alipenda sana kuwa jirani nami hasa mara baada ya mamaangu kufariki nikiwa mdogo sana.
baba alioa wake zaidi ya watano na kazi yake kubwa ilikuwa ni kutibu watu matatizo yao kwa njia hii ya asili na alijijengea umaarufu mkubwa sana kutokana na kuwafanikishia mambo yao watu wengi pindi walipokuja kwake.
Hii ilimfanya kutembelewa na wageni mara kwa mara kutoka sehemu tofauti tofauti na kufika nyumbani kipindi hiko tunaishi Kibamba ndanindani katika kijiji kilichoitwa Hakipo.
Katika ujana wangu baba alinifanya kuwa msaidizi wake katika kukaribisha wageni mara baada ya kuferi kimaajabu kidato cha sita nae akanisihi niachane na shule kwani mizimu ilinichagua kati ya wanae kuwa mimi ndie nitaefaa kurithi huu mkoba hivyo nilipaswa kufundishwa mapema mila na taratibu zake.
Awali nilichukia sana na sikuwahi kuota kuja fanya kazi hii lakini baba alianza kunijenga taratibu kwa kunieka katika kitengo cha kupokea wageni na kuwakaribisha pindi wanapokuja kukutana nae.

Siku zilikatika huku nikiwa nishaizoea ile kazi ya kukaribisha wageni na kwenda kuchimba dawa porini alizokuwa ananifundisha mzee wangu na nikaanza kuzoeleka na baadhi ya wateja wakubwa wa baba.
Katika makuzi yangu sikuwahi kuwa na mazoea makubwa na Hussein japo tulijuana kama ndugu na hata ilipofika siku tunapata habari ya kesi yake kila mtu alisikitika huku wengi tukimlaani kutokana na kitendo alichoifanyia familia yake lakini mara zote baba alitusema sana na kutupasha kuwa Hussein hakutenda hayo makosa ila kuna mtu amemuingiza katika huo mtego kwa ajili ya mwanamke ambae alikuwa mke wa Hussein.
Tulipomuhoji vizuri na kumuuliza baba juu ya taarifa zile alizotwambia kama ana uhakika nazo alisema haswaa ana uhakika nazo kwani aliligundua tatizo toka siku ya kwanza alipotambulishwa mke wa Hussein na alijaribu kumnusuru mwanae katika matatizo ambayo alihisi lazima yatatokea huko mbele lakini jitihada zake zilishindikana kutokana na Hussein kuonesha hali ya kumpenda sana mkewe na kutopenda kuzungumzia mahusiano yao japo baba alijitahidi kumuonesha ishara za kumfanya awe makini na mkewe lakini Hussein alionesha kudhalau na kumuamini mno mkewe na hilo kwa mujibu wa baba ndio lililokuja kumponza Hussein.

Habari hizi hata sasa zilituchanganya sana na kutomuelewa vizuri baba asemacho juu ya ukweli alioujua na mara nyingi baba tangu Hussein akamatwe alijieka bussy mno na kesi ile hata ofisi yake ilikuwa nadra sana kufunguliwa na tulipojaribu kumuuliza atufafanulie zaidi kivipi adai Hussein kaponzwa na mkewe wakati nae kauawa kinyama alichotujibu ni kimoja tu tena kwa kifupi sana kwamba 'tuamini kwanza Hussein hana hatia' kisha baadae tutajua siri zote.
Maneno haya yalifanya tupunguze kumghasi baba juu ya kutaka kuelewa kuhusu ya siri aliyoibaini na siku zilienda hatimae ulifika mwaka Hussein hajahukumiwa.

Lakini sitosahau wiki moja kabla ya kesi iliyomuhukumu rasmi Hussein kwa yaliyotukuta na hiyo ndio ilikuwa siku yangu ya kwanza kulijua na kulisikia hilo jina la Mr.X..
aaaagh!! omba usikie tuu bwana mdogo huyo Mr.X hakuwa mtu mzuri hata chembe na atapokuhitaji uingie kwenye anga zake vigumu sana kumkwepa alikuwa na mbinu nyingi mnooo.
Imepita miaka mingi sasa lakini ukinitajia hilo jina Mr.X moyo wangu hulipuka sana na naikumbuka hii wiki kama vile ilikuwa wiki iliyoisha ya mwezi huu tuliopo.
Mambo yenyewe yalikuwa hivi..................

ITAENDELEA......
 
EPS 19
========

Siku moja majira ya saa tano usiku tulipokuwa tumelala huku kijiji chote kikiwa kimya kabisa kutokana na umeme kutokuwepo kipindi hiko kulikuwa na giza totoro.
Siku hiyo usingizi wangu ulikuwa wa mang'amung'amu sana na nilitoka nje mara kwa mara kujisaidia hususan haja ndogo.
Kumbe wakati nilipofungua mlango wa nje na kuelekea chooni kuna watu walibanisha pembeni na kuingia ndani pasi na mimi kujua chochote na kutahamaki niliporudi ile nafunga mlango nilipigwa na kitu kizito maeneo ya kisogoni na kupelekea kuanguka chini na nilipojaribu kuinuka nilihisi kizunguzungu na kuanguka tena ndipo sikukumbuka chochote kilichoendelea baada ya kupoteza fahamu.

Niliporejewa na fahamu nilijikuta sehemu ambayo sikuitambua ni wapi zaidi ilikuwa ndani eneo kama la gofu la jengo lililoacha kutumika miaka mingi huku nikiwa sambamba na familia yangu yaani mke na mwanangu aliyekuwa na umli wa miaka mitatu tu kipindi hiko pamoja na wadogo zangu wakike wawili mama mlezi aliekuwa mke wa baba pamoja na baba mwenyewe.
Kwa ujumla tulikuwa kama sita tukiwa tumefungwa kila mmoja kwenye nguzo kubwa ya chuma tena tukiwa kama tulivyozaliwa.
Aaagh!! Mr.X mtu m baya sana hafai hata kusimuliwa kwani unyama tuliofanyiwa na vijana wake ulikuwa wa kutisha sana Usiosimulika huku tukiwa hatujui sababu kubwa ya kututeka na kutufanyia ukatili na unyama kiasi kile.

Wakati napata fahamu vizuri nilipojaribu kugeuza shingo huku na huko sikuamini macho yangu nilipowaona ndugu zangu tena wakiwa watupu kabisa kama walivyozaliwa.
Nilijikuta nafumba macho na kulaani kile kitendo kwa kupiga kelele na ndipo walipoingia watu watatu wenye bunduki wakiwa wamevaa kininja na kunifungua mimi pekee kisha kuunza kunitembeza mbele ya wenzangu sehemu ambayo nilikuwa nawaona kwa ukaribu kabisa na kuamua kufumba macho yangu lakini bado walitupiga na kutulazimisha tutazamane.
Sintosahau jinsi walivyokuwa wanamuhoji kila mmoja kwa kumlazimisha kutaja viuongo nyeti walivyomuonesha toka kwa mwengine, hawakujali huyu baba wala huyu dada au mama kiufupi walitudhalilisha mno.
Hakuna kati yetu aliyejua kipi kisa na mkasa hadi yanatukuta yale na tulidhalilishwa na kuteswa kwa siku mbili toka kwa wale watu ambao walitwambia kuwa tujisikie amani ndani ya ngome ya Mr. X.
Lakini hakukuwa na amani yoyote zaidi ya mateso na udhalilishwaji wa kinyama kwani sitosahau siku walipomlazimisha baba kwa mateso makali mpaka akubali kuingiliana na mama tena mbele ya macho yetu?
Daaah!! yalikuwa ni zaidi ya matusi na yote yalitekelezwa kwa amri iliyokuwa inatolewa na huyo Mr.X kwa njia ya sauti iliyukuwa inasikika mule tulipofungwa kupitia vispika ambavyo hatukuweza kuviona na pia nahisi kulitegwa kamera maalum kwani alikuwa anacheka mno kila kinachoendelea nahisi alikuwa anakiona.
Hali ilitisha sana nililia mno kuona unyama ule na siku hiyohiyo walinilazimisha na mimi kumuingilia mdogo wangu wa kike na ndio sababu ya kovu hili unaloliona usoni kilikuwa ni kisu kilichokuwa na moto ambacho alinibandika nacho shavuni mmoja wa wale watesaji wa Mr. X pindi ilipotoka amri kwa Mr.X na kwenda kinyume nilipoweka mgomo wa kumuingilia ndugu yangu tena mbele ya mke wangu , mwanangu na wazazi wangu!! lakini bado wakaona haitoshi ndipo Mr.X alipowaamuru wale watesaji wamuingilie kwa pamoja wenyewe mbele yetu na walipomaliza wale wawili akaja na yule watatu na alimuingilia tena kupitia njia iliyoharamishwa.
Aaaaaaaaaaagh!!!! iliniuma sana niliposikia kelele za maumivu toka kwa ndugu yangu lakini sikuweza kutoa msaada wowote zaidi ya kufumba macho na kulia kwa uchungu.
Hakuna kati yetu aliyeweza kuuangalia unyama ule wala aliyeweza kuzuia machozi kumtoka, mke wangu tu alizimia zaidi ya mara mbili mule kwenye mateso.
Ki ukweli ilituuma kupita maelezo na hatukumjua huyo Mr. X wala hatukujua kwanini aliamua kutuma vijana wake kututeka na kutudhalilisha kiasi kile.

Baada ya siku nyengine mbili kupita walikuja watu wengine nao wakiwa wamevaa kininja ila mmoja wao alikuwa mwanamke na nilimtambua kutokana na sauti pindi walipofika na kuongea na wale walinzi wengine kisha wakamchoma sindano ya shingo baba na baada ya muda mfupi alinong'onyea na kuanguka ndipo walipomfungua na kumbeba kisha kuondoka nae sehemu isiyojulikana na hatukumuona tena kurudishwa.
Tulilia sana na kutilia mgomo hata chakula walichokuwa wanatuletea kwa kuamini washamuua baba basi na sisi bora watuue tu lakini baada ya siku tatu walitubananisha kwa kutuchoma sindano zilizotufanya wote kupoteza fahamu na tulipokuja kustuka ajabu tulijikuta tupo nyumbani tukiwa tumelala huku pembeni yetu tulimuona baba akiwa amekaa akilia kwa uchungu.

Ilikuwa kama sinema kwa kweli wote tulijikuta tukilia kwa nguvu kama watu waliopata habari ya kifo cha ghafra kwa mtu waliyempenda na kumtegemea.
Kila mmoja alijiziba sehemu zake za siri kwa kukimbilia vyumbani kwa aibu hadi majirani walipokuja kutugongea kwani ilikuwa ni usiku mkubwa tu lakini baba alitoka na kuzungumza nao akidanganya kuwa tulifiwa na ndugu yetu huko Mbeya na aliporudi ndani alituita na kutusihi tunyamaze kisha akatwambia tusiwe na hofu tukalale ila kesho yake kila mmoja apange vitu vyake vizuri kwa kujiandaa na safari ambayo hatukujua ni ya wapi.
Na kweli tulijiandaa na usiku wa siku ya pili tulipomuuliza baba juu ya safari hiyo na kwanini tulitekwa na wale watu na huyo mr.X ni nani na yeye aliponyeka vipi mikononi mwao na kwa nini wametuacha.?
Chaajabu maswali yote yale baba alitujibu kwa ufupi sana na alikuwa mkali mno pindi alipoona mtu akimuhoji zaidi.
Alitwambia kuwa tulikuwa mateka wa Mr. X kwa sababu yake na alipochukuliwa siku ile alienda kukutana na huyo Mr. X na usalama wetu pia umepatikana kwa sababu yake.
Basi tufanye na tufuate vile alivyotuelekeza huku akituonya asije kuthubutu yeyote kati yetu kumwambia mtu juu ya kilichotukuta na hata kulitaja hilo jina Mr. X kama tutapenda kuendelea kuishi.

Basi baada ya hapo ndipo siku ya tatu lilikuja kundi la vijana waliokodiwa na baba kutusaidia kubeba mizigo na kupeleka eneo lilipoishia roli lililotusafirisha mpaka hapa Mkuyuni.
Sikujua baba amepataje pesa nyingi kwa haraka vile hadi kuweza kuhama na kununua nyumba muda mfupi hapa Mkuyuni lakini baada ya mwezi mmoja mama mlezi alifariki ghafra na moja ya sababu za kifo chake baada ya uchunguzi ni mawazo ya muda mrefu na hii ilitokana hasa na tukio lile la kutekwa na Mr.X ambalo lilibaki kuwa siri yetu na pia vitendo alivyofanyiwa kule tulipotekwa.
Kama hiyo haikutosha kumaanisha kiasi gani Mr. X ameharibu saikology za ndugu zangu ndipo baadae mdogoangu yule wa kike aliyebakwa na kuumizwa na wale vijana alianza kupata maradhi ya mara kwa mara ya kichwa na kupoteza fahamu ambapo miaka mitatu baadae alirukwa kabisa akili na kuchanganyikiwa.
Tatizo lake nalo halikutokana na kulogwa bali nina hakika ni vile vile vitendo alivyofanyiwa kwa Mr.X.
Moyo wangu unamchukia msana tena saaana Mr.X na naomba siku zote kama amekufa mungu amzidishie adhabu kali zaidi huko alipo.

Moyoni nilieka nia ya kulipiza kisasi na mara nyingi nilipenda kumpeleleza baba apate kunambia huyo Mr.X ni nani hasa baada ya siku moja kuhoji kuwa namfahamu vizuri kwani alikuwa ni moja ya wateja zake wa zamani lakini nilishindwa kujua ni nani kutokana na wingi wa wateja niliokuwa nawapokea pale kijiweni.
Lakini baba alikuwa mgumu na m bishi mno kumuanika mtu huyo aliyetudhalilisha na sikujua kwanini baba aliogopa kiasi kile hadi kutusema mno zaidi ya kutuonya na kutuhadharisha mara kwa mara kuwa tusahau habari za Mr. X kwasababu tutaponyanyua ulimi kuzitaja hadhalani basi tutakuwa tumejihatarishia maisha yetu kwani hata kupona kwetu awali ilikuwa ni bahati tu hivyo tusahau.
ITAENDELEA..
 
EPS 20
========
Basi mwanangu miaka ikasonga hadi hii leo maisha yanasonga kila mtu amesahau habari za huyo Mr.X na hadithi yake imebaki kuwa siri ya sisi watu wanne tulio hai japo kovu lake mioyoni mwetu bado lipo.
Pia ukweli ni kwamba hakuna aliyejua siri ya kuwa Mr.X ni nani zaidi ya baba mwenyewe mzee Mnyungunyungu na endapo akifariki ndio basi na ukweli unaoutafuta utakuwa umekufa rasmi. ' ' ' '

<*> <*> <*>
......................................

* * * * * *

Alimaliza kuhadithia juu ya alichokijua kuhusu Mr. X yule bwana na story hii ilimfanya kwa mara nyengine Kamishna Shebby kudondosha chozi hasa mara baada ya kujua unyama waliofanyiwa familia ya mzee Mnyungunyungu na kuelewa sababu za kuhama kwao hata akapata hisia na taswira ya picha kwa kuunganisha na story ya Hussein alibaini kichwani mwake kuwa ba Mkubwa hakumsariti kwa makusudi mwanae kutokana na ushahidi alioutoa pale mahakamani inawezekana alimkandamiza Hussein kwania ya kuikomboa familia yake iliyokuwa mikononi mwa Mr. X ambae ndie alikuwa adui wa Hussein babu bubu.
Lakini swali bado lilibaki pale pale kuwa huyo Mr. X alikuwa nani?

Jibu hili alijua aliamini ni mtu mmoja tu ndie analo ambae sasa ni mzee sana na yuko hoi taabani kwa ugonjwa wa muda mrefu na hakuitajika kusumbuliwa.
Sasa alijiuliza moyoni Kamishna Shebby je ina maana safari yake iishie pale na kurudi na majibu yale tu bila kujua siri walau jina halisi tu la huyo mr x na kazi aliyokuwa anafanya? atawezaje kuifufua kesi ya miaka mingi bila kuwa na maelezo ya ushahidi yakinifu utaoeleweka mbele ya mahakama? ataonekana ni Askali kiongozi mzembe kiasi gani kwa kuyaamini maneno ya mfungwa tena wa miaka mingi juu ya kesi iliyokaribia kumzidi hata umli bila kuwa na ushahidi wa kutosha na vielelezo muhimu?
Bado aliamini ni sehemu moja tu na ni mtu mmoja tu awezae kumpa mwanga kwenye njia ya kiza anayotaka kupita kwenda ulipo ukweli wenyewe kwani aliamini endapo atafanikiwa kumjua Mr.X na kumkuta angali yu hai basi yeye ndie atafumbua mafumbo yote tena kiurainiii kutokana na mbinu alizokuwa nazo Kamishna Shebby alizozijua mwenyewe.
Aliamini kuwa hakuna ujanja wowote pa kuupata huo mwangaza zaidi ya kuongea na Mzee Mnyungunyungu walau maneno machache tu hata na alikuwa tayari hata kwa kulazimisha endapo watajaribu kumzuia kuonana nae.
Lakini akiwa bado anatafakari Kamishna Shebby juu ya kutaka apelekwe kumuona mzee Mnyungu nyungu na kabla hajazungumza kitu mara aliingia yule kijana mjukukuu wa Mnyungunyungu aliyewapokea pale nje na kuita.
"Baba .. babaa.. kuna wazee wamekuja Unahitajika haraka nyumbani babu amezidiwa sana.."
Maneno haya yaliustua mno moyo wa Kamishna Shebby na kukurupuka sambamba na yule bwana pale chini kwa lengo la kuwahi huko alipo mgonjwa huku moyoni akisali na kuomba mzee Mnyungunyungu asifariki kabla hajamwambia Mr.X alikuwa nani.

Walitoka nje na kuwakuta wale wazee wakiwasubiri huku st;sajent Kimaro nae akiwa kasimama na alipomtazama Kamishna Shebby kwa kukutanisha nae macho alimuuliza kwa ishara za kiaskali kama amefanikiwa lakini Kamishna hakumjibu zaidi ya kumpa ishara waongozane na wale wazee haraka waelekee kule wanapoenda.

Baada ya mwendo mfupi walifika kwenye nyumba moja kubwa ambapo ilionekana wazi walioishi pale wote ni watu wa familia moja huku kila waliemuona pale nje akionesha uso wa huzuni kasoro mama mmoja wa makamo ambae alionekana akiwa anacheka cheka na kuchezea vitu ovyo.
Wenyeji waliingia ndani kwanza kuona hali ya mzee Mnyungunyungu ilivyo huku kina Shebby wakiachwa kwanza pale nje baada ya kukaribishwa na kina mama waliowakuta na kupewa vistuli.
Kichwani shebby alimtambua yule mama aliyeonekana wazi kurukwa na akili kuwa ndie yule mtoto wa mzee Mnyungunyungu aliyetendewa ukatili kipindi hiko na vijana wa Mr. X kwa mujibu wa hadithi ya bwana mganga mtoto wa Mnyungunyungu aliyekuwa nae kibandani muda mfupi uliopita.

* * *

"Vipi hao vijana ni wageni wako?"
Aliuliza kwa sauti ya chini mzee mmoja pindi alipokuwa ndani na yule bwana mganga wakiwa wamesimama wakimuangalia mzee Mnyungunyungu aliyekuwa anakoroma kiajabu huku wote wakijua sasa hakuna cha kumsaidia zaidi ya kungoja tu akate roho.
"Haa!! we acha tu kaka, hawa walikuwa ni wageni wa baba lakini ndio basi tena ashawakosa."
Aliongea kwa huzuni yule mganga na kusogea kitandani alipokuwa mzee Mnyungunyungu na kupiga magoti huku machozi yakim bubujika.
"Jikaze bwanaa vipi!!? usikufuru inapaswa tumuombee aondoke kwa amani akapumzikee"
Aliongea mzee mwengine aliyekuwa amepakata kichwa cha mzee Mnyungunyungu aliyelala pale kitandani pindi alipokuwa anahangaika na roho na kumzidisha machungu yule bwana badala ya kumtuliza kwani licha ya kwamba alijua babaake alikuwa mzee sana na kwa hali aliyokuwa nayo ndio basi tena hawezi kuamka lakini pia ilikuwa ngumu moyoni mwake kuukubali ukweli ule huku akifikiria juu ya siri nzito anayoondoka nayo babaake.
Siri ya kuwa nani alikuwa Mr.X.!?

"Aaaagh!! baabaaaangu siaminiii mimii kama ndio unaniacha katika kipindi kama hiki huku ukiondoka na siri iliyofichika miaka yoteeee aaah.."
Maneno yale yaliwashangaza wazee wote waliokuwemo mule ndani wasijue ni siri gani huku wengine wakimsihi anyamaze na aache kukufuru kwani Mzee Mnyungunyungu alikuwa bado hajafa japo hakuonesha matumaini ya kupona.
"Nyamaza bwanamkubwaa usikufuruu"
Aliongea mzee mwengine aliyevaa kibaraghashia.

* * * *

Baada ya uzalendo kumshinda pale nje huku akiwazia juu ya jitihada zake kuwa zinaelekea kuzama hasa baada ya kuhisi kuna mtu analia kwenye chumba walichoingia wenyeji wake, ndipo Kamishna Shebby aliamua kujitoma mule ndani kwa taharuki kubwa kuhakikisha kama kweli mzee Mnyungunyungu ndio basi kashafariki.

"Eee Mola baba.. mpe walau dakika moja tu anitajie jina halisi la Katili huyo Mr. X.."
alijikuta analopoka Kamishna Shebby baada ya kuingia ghafra na kuwastua watu huku macho yake yakiangukia pale alipopiga magoti yule mganga huku kitandani akionekana Mzee Mnyungunyungu akitapatapa.
"MR. X !!!!!!??"
Kila mtu alitahayuri na kujikuta wanalitaja kwa pamoja hilo jina Mr. X kwani hakuna kati ya wale wazee aliyewahi kulisikia hilo jina.
Lakini cha ajabu walipotahayuri na kulitaja kwa mshtuko mkubwa lile jina walishangaa kusikia Mzee Mnyungunyungu akikohoa kwa nguvu mfululizo na kupunguza kukoroma ndipo ajabu ya mungu alifumbua macho kisha kugeuza shingo taratibu na kumtazama Kamishna Shaaban pale aliposimama mlangoni.
Watu wote walibaki wametumbua macho hata yule mganga mtoto wa mzee Mnyungunyungu alistuka na kusogea pembeni kidogo huku akimuangalia babaake kwa mshangao mkubwa kwani haikuwahi kutokea wala kusikia kuwa mtu anayetapa tapa dakika za mwisho akikaribia kutokwa roho akakohoa na kufumbua macho tena.
"Allahu akbar.!!" (Mungu mkubwa)
Alitaharuki yule mzee mwenye baraghashia huku nae akisogea eneo lililokuwa jirani na mlango waliposogea na wale wengine wakihofia huenda mzee Mnyungunyungu alitaka kuondoka na mtu ama si hivyo basi ule ulioamka ni mzuka tu ila ye mwenyewe kashakufa.
"Yesu wangu!!"
Alisikika mzee mwengine wa kilokole ambae yeye alitoka nje moja kwa moja kwa hofu na kuwahi alipokuwa anaishi kwa lengo la kufata biblia.
Lakini katika hali ya utofauti na kushangaza kamishna Shebby ndio kwanza alisogea haraka pale kitandani huku akipiga magoti na kuanza kumuongelesha mzee Mnyungunyungu kama vile amechanganyikiwa.
"Tafadhali mzee nakuomba nitajie tu huyo mtuu.. Naomba usiondoke na hii siri, nimemuona Hussein jela amenambia kila kitu najua hukumuangamiza makusudi ila jitahidi unambie alikuwa nani huyo Mr.X.."
Aliongea Kamishna huku akiwa kaishika mikono ya mzee Mnyungunyungu.
 
EPS 21
========

Watu wote walikuwa wameganda bila kusema chochote utadhani wamepigwa upepo wenye ubaridi wa ubaridi ganzi.

Alipomtazama kwa makini usoni yule mzee Kamishna Shebby alibaini kuwa anataka kuongea kitu hivyo alimuinamishia sikio karibu yake na kumsikiliza kwa makini na kweli mzee Mnyungunyungu kwa tabu kubwa alianza kuongea.
"X ...kwe.. een..kwen..yeepichhhh..aa..aan..an,, Kooo..koovuu.uuusoo..soooni..iiih"
"Ndio babu kovu usoni ndio jina lake au!! jitahidi babu yangu nambie alifanya kazi gani nchini. jitahidi tafadhali mzee wangu.."
Wakati huo alipoanza kuongea kwa shida mzee Mnyungunyungu yule mwanae mganga alisogea tena na kutaka kumuondoa kamishna Shebby pale huku akimshika kifua na kumkumbatia kwa nguvu babaak akiwa haamini kama kweli amepata hata uwezo wa kuongea ghafra ile kwani hajawahi kutamka neno lolote zaidi ya miezi mitatu toka azidiwe hasa.
Lakini Kamishna aligoma na kumtoa yule mganga kwa kumuomba amuache asimtingishe vile apate kusma zaidi na kufichua ukweli juu ya Mr. X na alipokubali na kumlaza tena babaake ili aendelee kuongea ndipo mzee Mnyungunyungu alipoanza kujibinya kwa nguvu pindi alipotaka kuendelea na sauti kushindwa kutoka kabisa huku akiwa amachama mdomo na ndipo ghafra badala ya kusema ulisikika mkoromo mkubwa wa ajabu na hali ya mzee Mnyungunyungu kubadilika zaidi huku macho yakiwa yamemtoka kupita kifani..
"Aaaaaagh!! Babuuu Mnyungunyunguuuuu.."
Alipiga kelele na kuita Kamishna Shebby aliposhuhudia Mzee Mnyungunyungu akiutoa ulimi na macho na hatimae kubaki kimya.
Kwa hali ya kuchanganyikiwa Kamishna Shebby aliendelea kumtingisha kwa nguvu mzee Mnyungunyungu hadi wale wazee wakaja kumuondoa pale na kumtoa nje kwani sasa ilikuwa dhahili mzee Mnyungunyungu hakuwa hai.

Vilio vilisikika nje baada ya kila mtu kugundua kilichokuwa kinaendelea ndani hasa baada ya Kamishna Shebby kutoka na hata St,sajent Kimaro alishangaa mno kumuona bosi wake akitokwa machozi mbele za watu na kubaini kuwa mtu waliyemfata ambae ilisadikika yu mgonjwa atakuwa amefariki bila kuupata ukweli walioufata.
Na hivyo ndivyo ilivyokuwa, Mzee Mnyungunyungu hatimae aliaga kweli dunia na siri juu ya mr X ikibaki kifuani mwake na hakuna atayejua tena nani mr.X.

Aliegama kwenye ukuta mmoja wa nyumba ile kamishna Shebby akiwaza na kuwazua nini afanye ndipo baada ya dakika kadhaa alimwita dereva wake na kumvutia pembeni.
"Kazi ishakuwa ngumu zaidi sasa."
"kivipi mkuu"
"Usinite mkuu kwenye hii mission tafadhali utawastua watu kama wakitusikia"
Aliongea kwa sauti ya chini Kamishna Shebby na kuendelea.
"Hatuna muda wa kuendelea kupoteza hapa, mwite yule mganga chukua ripoti na docoment muhimu za mawasiliano then wape laki moja ya pole tuondoke."
"Sawa mku.. ee sawa mshkaji wangu"
Alizuga Kimaro mara baada ya kujisahau tena na kutaka kumwita mkuu kwa mara nyengine.
Baada ya Kimaro kufanya kama alivyoagizwa na Shebby alitoka yule kijana na kuwasindikiza mpaka stend kuu Mkuyuni na safari ya kurudi Dar ikaanza.

* * * * * *

Kama kawaida baada ya kurudi Gerezani majira ya usiku Hussein alichukuliwa na kwenda kukutana na Kamishna Shebby na kumpa habari zote kuhusu babaake mkubwa mpaka kifo choke na habari zile zilimsikitisha sana Hussein na kumuuma moyoni.
"Daaah ina maana kumbe baba Mkubwa hakufanya vile kwa ridhaa yake? aagh, sasa nani huyo mshenzi mr.X!!"
Aliuliza swali hili kwa hasira sana Hussein huku akimtazama Kamishna Shebby.
"Hilo ndio swali ambalo ni fumbo kubwa sana ambalo sijui tutalifumbuaje kwani jibu la uhakika nani alikuwa mr.X ndio kaondoka nalo marehemu Mnyungunyungu. Aaagh!! hata mimi nakanganyikiwa sana baba"
Aliongea kwa upole Shebby huku akichekecha kichwa.
"Basi mwanangu usijitie mawazo kwa kesi ambayo haina uhai tena kwani sasa sioni hata faida ya kumjua huyo mr.X wala usihangaike baba endelea na kazi nyengine tu, haya yetu yashapita tena."
Aliongea Hussein safari hii kwa unyonge sana.
Na baada ya kumaliza maongezi yale yaliyochukua zaidi ya nusu saa Hussein alirudishwa tena jela huku kwa upande wa kamishan Shebby akifikiria sana juu ya kushindwa kwake kuunasa ukweli muhimu sana uliofichwa miaka yote.

Aliamua kuwasha tena ile rekodi pindi alipokuwa anazungumza na yule mganga na alipokumbuka maneno machache ya mzee Mnyungunyungu alichukua note book na kuanza kuyaandika na kuyaunganisha kwa upeo wa hali ya juu na ndipo moyo wake ulimripuka mara baada ya kuvumbua kitu kwenye yale maneno machache ya mwisho ya mzee mnyungunyungu.
"Yees!! hapa kuna ukweli uliojificha kwenye haya maneno."
aliwaza moyoni Kamishna Shebby na kuyaunganisha tena vizuri yale maneno na kupata sentensi ya maneno sita sahihi aliyokuwa amezungumza mzee Mnyungunyungu yaliyomuelekeza kitu cha msingi sana juu ya mr.X na moyo wake haukuamini mara baada ya kuiona njia ambayo aliamini itakuwa ndio msaada wake wa mwisho kumjua huyo mr.X

Asubuhi yake alimwita rafiki ake ambae pia alikuwa dereva wake aliyejulikana kama st;sirjent Kimaro na kumwambia alichogundua kuhusu maneno yale ya mzee Mnyungunyungu.
"Hembu nione ulivyoyaunganisha."
Aliongea Kimaro na kuyasoma yale maneno ambayo kamishna Shebby aliyaunganisha kwa kuyapa namba.
1-mr X 2-kwenye 3-picha 4-ana 5-kovu 6-usoni.
"umegundua nini Kimaro"
"Hapa mkuu inaonesha marehemu alikuwa anakuelekeza jinsi alivyo mr.X kuwa ana alama ya kovu usoni mwake."
"sasa Kimaro ukisema Kovu tu haitoshi kwani wengi wana makovu usoni ila hebu pitia tena hayo maneno nataka unambie nitamjuaje mr.X!"
Aliuliza swali la mtego Kamishna Shaaban kuupima uwezo wa kufikiri aliokuwa nao st;sajent Kimaro ktk uvumbuzi kwani alimjua nae alikuwa si haba ktk kutafiti ni moja ya askali wacheche waliokuwa na vipaji pia za kazi ile ya upelelezi ndio maana alipenda sana Kamishna Shebby kutembea na St; sajent Kimaro.
ITAENDELEA....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom