WANAWAKE NI WAUAJI..!?
EPS 46
========
BY - MTOTO WA BECKER (The Special Thinker)
______________________
______________
Na kweli majira ya saa nne asubuhi Shebby aliwasili pale hotelini na kukutana na Hussein bubu.
"Karibu baba karibu sana"
alikaribisha Hussein akiwa mwenye furaha pindi alipofungua mlango na kumkuta aliyemgongea kuwa ni Kamishna Shebby
"Ahsante sana baba"
alijibu Shebby na kuingia ndani.
"sasa baba ilikuwa nije kesho lakini nimekuja leo kwa sababu frani zitazofanya nikuongezee muda wa kuendelea kuwepo hapa lakini nilikuwa naomba unisaidie jambo moja"
"Usijali baba, usijali kabisa nakusikiliza na kabla hujasema naamini niko tayari kama litakuwa ndani ya uwezo wangu"
alijibu na kukaa vizuri Hussein huku akimuangalia na kumsikiliza Kamishna Shebby kwa umakini mkubwa.
"Sawa mzee wangu, ni hivi... Kipindi nilipokuwa nauguza jeraha la mguu nilitokea kupendana na binti ambae ndie alikuwa daktari wangu alienisaidia kwa kiasi kikubwa sana hadi nikafikia hatua hii ya kuwa kama awali..."
"Ndio baba endelea"
"Sasaa, nilimuahidi kuwa nitafanya mpango wa kujitambulisha kwao ili tufanye taratibu za kufunga ndoa na kuwa mke na mume.... sasa Shida yangu baba nakuomba wewe uwe mshenga wangu unisaidie kuandika barua ya posa nikupeleke hadi nyumbani kwao na wewe ndie utayeingia na kunitambulisha sambamba na barua."
"Mh! mwanangu lakini mbali na kukutibu tu umechunguza tabia yake kiumakini?"
"Kwa hilo baba sina shaka"
"Haya mwanangu mimi kwako sina pingamizi kwa hilo, fanya tuiandike hiyo barua na hata leo hii ukitaka unipeleke niko tayari kwa hilo kwa moyo mmoja ila nasaha zangu kwako ziko palepale usiwaamini wanawake wala usiwachukie kumbuka kuwa Wanawake ni Wauaji"
aliongea Hussein na kumfanya Shebby atabasamu na ndipo alipotoka na kurejea tena akiwa na bahasha sambamba na karatasi na kwa msaada wa Hussein wakaanza kuiandika barua.
* * * * * *
"Mamaaa, mamaa, mama kaa tayari tayari leo usitoke kwenda popote"
"Kivipi Asha mwanangu mbona ratiba zako sizielewi!"
"mama bwana, ni hivi... yule mchumba niliekwambia barua yake inakuja leo"
"Hee, ni wewe kweliii Asha au mwengineee"
"Ni mimi mama mbona huamini!?"
"Mh! unajua toka uliponambia siku ile nilichukulia mzaha kwa itikadi zako za kutojichanganya na watu, sasa sijui imekuwaje kuwaje hadi ulikubali kuacha shughuli zako na kumtibu mgonjwa yule tena ukidiliki kukaa kwao kwa zaidi ya miezi miwili na kama haitoshi unarudi na kuniambia ndio mchumbaako? au mlikuwa mnafahamiana muda mrefuu!!!"
"hahaha hapana mama ni mapenzi tu, basi si unajua wewe ndie mama na wewe ndie baba. Ikija barua ijibu malizana nao bhaasi ahhaha"
"Hahahaaa haayaa mwanangu nimekuelewa"
Yalikuwa ni mazungumzo ya dk Asha akiwa na mamaake ndani ya nyumba moja ya kifahari ambayo walikuwa wanaishi wao wawili tu yaani mama na mwana.
Haikujulikana kama yule mama alikuwa na watoto wengine ama laah, lakini mara nyingi pale alikuwa anaishi na Asha ambae yeye alikuwa mtu wa kutoka mno na alihakikisha mamaake anakuwa ni mwenye furaha siku zote.
Baada ya masaa matano kupita yule mama akiwa amekaa sebuleni mara alarm ya mlango iligongwa na alipoinuka kufungua alikutana na mlinzi wao wa getini akiwa kasimama mlangoni.
"Samahani mama, kuna mzee furani anahitaji kuonana na nyinyi vipi nimruhusu apite?"
"Mruhusu tu"
"Sawa Asante mama"
alijibu mlinzi na kukimbilia tena getini na kumruhusu kuingia ndani ya jengo huyo mzee aliyemzungumzia ambae alikuwa ni Hussein bubu mara baada ya kuoneshwa nyumba husika na Shebby ambae alikuwa kasimamisha gari mita hamsini na eneo lilipokuwa geti la kuingilia kwa kina Asha.
"Habari mama"
"Salama karibu"
alijibu yule mama ambae alikuwa na mwili wa wastani mara baada ya kusalimiwa na Hussein na kumruhusu akae.
Hussein hakuchelewa kujielezea kilichomleta pale na yule mama hakuonesha kupinga wala kuwa na maswali mengi zaidi ya kukubali na kuipokea ile barua
"Ahsante sana mama kwa ukarimu wako, vipi lakini mzee bado hajarudi kazini.?"
"haha Hapana usijali mzee kwa bahati mbaya hatunae siku nyingi"
"Oooh pole sana mama"
alijibu Hussein na kunyanyuka akijiandaa kuaga mara baada ya kupewa tarehe ya kuja kuchukua barua ya majibu lakini kabla hajaaga alikumbuka kitu frani
"samahani mama hivi unaitwa nani.?"
"Ahaa mi naitwa Zena Hamisi Kidongo"
alijibu huku akiwa katabasamu yule mama lakini ikawa tofauti kidogo kwa Hussein mara baada ya kulisikia lile jina.
"ZENA HAMIS KIDONGO!!?"
"Eeeh kwani vipi baba mbona umeonesha kulishangaa kidogo jina langu baya sana nini?"
"Hapana mama, hilo jina sio geni sana labda nikuulize unamfahamu Mariam Hamis Kidongo"
"MARIAM? Haah!! huyo ni Marehemu dadaangu kabisa we umemjuaje na alifariki miaka mingi sasa"
alistaajabu yule mama na kumuangalia kwa makini Hussein ambae alijikuta anakaa chini kabisa akiwa kapigwa na bumbuwazi zito usoni mwake na machozi kuanza kumtoka akiikumbuka barua ya mariam iliyomuelekeza kuhusu ugonjwa wake na habari juu ya mtoto wake wa kike ambae alikuwa anaitwa Asha na kuanza kuamini kuwa huyu aliyekuja kumchumbia huenda akawa ni mwanae kabisa kwani hata jina alilotajiwa na Shebby pindi walipokuwa wanaandika barua ni Asha Hussein
"Zenaa.. Oooh! Mi naitwa Hussein.. aaagh ndioooo Hussein Bakari... Hussein yule wa dadaako Mariam"
aliongea huku machozi yakimtoka Hussein kama mtoto
"Haa! Ina maana wewe ni Shemeji Hussein tuliyesikia umefungwa maisha sijui Kunyongwaa aaagh Ashaaaaaaaa ni mtoto wako aliekuachia dada!!aaaaaaaa Munguuuuu"
alistaajabu yule mama na kuangusha kilio kilichomstua Asha mara baada ya kusikia anaitwa na kuanza kushuka haraka juu alipokuwa na kufika sebureni ambapo hakuamini alichokuwa anakiona na hakujua kisa na mkasa mpaka mamaake na yule mzee ambae alijua ni mshenga kugalagala chini wote wakiwa wanalia kwa uchungu mithili ya familia moja iliyopokea taarifa ya kifo cha ghafra kwa mtu waliyempenda na kumtegemea.
"Mamaa .. maaamaa!!! Vipi nini kimetokea tena?"
alifika haraka pale sebureni Asha huku akiuliza kwa mshangao na kumuinua mamaake ambae hakuwahi kumuona akiwa analia kwa uchungu kiasi kile tangia apate fahamu zake mara baada ya kurudi kutoka India alipokuwa amepelekwa akiwa bado mdogo na wafadhili walioishi nae kwa zaidi ya miaka kumi kabla ya kufariki kwao nae na alipofuzu masomo yake ya udaktari hakutaka kuendelea kubaki nje zaidi ya kurejea nyumbani Tanzania ambapo alipokelewa na mamaake yule ambae alimuonesha mapenzi kama mtoto wake wa kumzaa mbali na ukweli kuwa mamaake mzazi hakuwa yeye.
"Mamaa mamaaa hebu nyamazeni basi mnambie nini kimetokea! Eti we mzee umeleta habari gani tena iliyomkosesha furaha mamaangu?"
aliuliza kwa hasira Asha na kumuangalia Hussein bubu ambae yeye aliacha kulia kwa sauti na kukaa kitako akimtazama Asha akiwa haamini kama hii leo anakutana na mwanae ambae hakuwahi hata kum beba akiwa mtu mzima tena mrembo na asilimia kubwa alifanana na mamaake ambae alikuwa mwanamke wa kwanza kumpenda kwa dhati Hussein mbali ya kuwa alikuja kumtenda vibaya