Simulizi: Wanawake ni wauaji

Simulizi: Wanawake ni wauaji

EPS 25
========
"aaah! wea acha tu habari za wanawake ndio sitaki kabisa kuzisikia"
alijibu yule mkuu wa kituo huku akionesha yuko serious na kile anachozungumza na kumshangaza Shebby ambae alihoji.
"Kivipi tena John.?"
"Ndugu yangu yaliyonitokea ndio sitamani kabisa kutafuta familia kwa sasa wee acha tu, nahisi nina mikosi sana kwa wanawake"
"Duh! John.. kwani nini kilikupata mshkaji baada ya kuachana kipindi kile kozi ilipoisha wakati ulinambia ulitaraji kufunga ndoa siku si nyingi?"
"Ndugu yangu Shebby ni story ndefu sana ila nitakuhadithia kwa ufupi ilivyokuwa"
Aliongea John ambae alikuwa na wadhifa wa OCS kituo cha mkuyuni akiwa na cheo cha Inspecta na kuanza kukumbuka ilivyokuwa toka mara ya mwisho walipoachana na Shebby walipokuwa kwenye kozi maalum ya uongozi na usimamizi ndani ya idala ya ulinzi wa ndani miaka minne iliyopita ambapo John alianza kusimulia ilivyokuwa hadi kupelekea awe na msimamo wa kutohitaji kuwa na mwanamke kwa kipindi kile.

'''''
"Ndugu yangu, mkuu wangu kiukweli kama ulikuwa hujui leo nitakwambia ujue wazi ukae ukijua kuwa wanawake ni watu wa ajabu sana inatakiwa uwe na akili nyingi sana jinsi ya kuishi nao.
Kumbuka siku ile ya mwisho tulipokuwa tunaagana kwenye ile tafrija baada ya kozi kuisha nilikuonesha kwenye simu yangu picha ya mwanamke nilietaraji kumuoa baada ya kumaliza kozi na kupandishwa cheo kwani nilijua sasa maisha nitakuwa nishayaeka kwenye mstari tena kwa kuwa na mwanamke mzuri kama Tedy aaaah, nilijiona bonge la mjanja.
Sikia sasa ishu ilivyokuwa baada ya kuachana na kupoteana kipindi tulipomaliza kozi na kupewa likizo ya mwezi mmoja sikuamini nilichokikuta mtaani Dah!!..... Kumbe yule demu Tedy si alikuwa ananiigizia bwana, muda wote naeka nae malengo hata nikawa najinyima na kumtumia pesa tulipokuwa Kozini ili afungue mtaji wa saloon kama alivyonambia kumbe nae alikuwa anatumbua maisha na mpuuzi mmoja mchafumchafu mtoto wa mtaani pale na kunigeuza mimi chuma ulete.
Sio siri niliporudi almanusura niue mtu kwa hasira mara baada ya kupata data zote na nilipokuwa namuulizia kuhusu hiyo saloon alinizungusha zungusha kunipeleka hadi waliponasa kwenye mtego niliowatega ambapo kwa macho yangu niliwafuma wakiingia Guest moja huko Keko na nilipompigia Tedy kumuuliza alipo alivyonambia ndio nilizidi kuchoka daah! Eti 'ooh, nimeenda kwa bibi vikindu anaumwa sana nitakupigia baadae'...... Nilichomjibu nikamwambia kuwa hiyo guest haiitwi vikindu inaitwa Mumbu na hapo nilikata simu na kufata ushauli wa mzee wangu tuliekuwa wote kwenye gari ambae alinisihi mno nisipaniki wala kumchukia mwanaume aliyelala na mchumbaangu kwani mwenye makosa hasa ni mchumbaangu nami nikakubaliana na mzee nikaachana na Tedy toka siku hiyo nikampiga stop tusijuane tena.
sasa hiyo tisa kumi ni Angelina au malaika ndivyo nilivyopenda kumwita mtoto kutoka Arusha aliyekuja kufanya kazi za ndani nyumbani kwetu kipindi hiko kabla sijahamishiwa hapa Mkuyuni na kuwa ocs.
Angelina alikuwa mzuri, mwenye adabu na heshima, kila mtu nyumbani alimpenda kuanzia mzee mama na dada na hata tukashawishika tufanye mipango ili nimuoe na awe mmoja wa familia yetu.
Sasaa sijui nisemeee ujingaaaaa auu utahiiraa yani nashindwa kuelewa hawa wanawake vichwa vyao vilivyo kwani kipindi chote tunafanya mipango na kuzungumza na mamaake huko kijijini walionesha hali ya kukubali kumbe bwana yule mtoto Angelina alikuwa tayari mke wa mtu muda mrefu na alikuja Dar kufanya kazi za ndani kwa lengo la kumsubiri mumewe aliyekuwa migodini huko ataporudi nae arudi waendelee na maisha.
Sio siri hii iliniuma mno nilipokuja gundua na kushindwa kumuoa mwanamke ambae tayari moyo wangu ulishaelekea kwake na kuniangusha baada ya kusikia mumewe amerudi na mambo yamemuendea vizuri baada ya mgodi kutema na karudisha mapenzi kama kawaida.
Hapo nilipagawa sana na ndipo babaangu mzee Cyprian aliponihadithia kisa kimoja enzi zake kilichotaka kufanana na changu tena kutoka huko huko Arusha alimuona bint akiwa na askali mwenzake walipokuwa kikazi na kufanya utafiti na kueka nae mipango.
Lakini kwa kuwa mzee kipindi hiko tayari alikuwa na cheo kikubwa swala la ufatiliaji zaidi na habari alizituma kupitia kijana wake wa kazi ambae walikuwa marafiki kama mimi na wewe kufikisha salamu zake kwa familia ya yule binti na zawadi mbalimbali.
Kumbe bwana rafiki ake nae si alikuwa anampenda yule bint..!! na alipokuwa anaenda kule anajiwakilisha yeye ndie mtakaji na mzee wangu alipokuja kugundua ilikuwa tayari too late.
Lakini binti mwenyewe alimjua mzee wangu ila alikubali kumsariti na rafiki yake sijui kwanini yaani wanawake usiwaamini hata kidogo.
Ila kwa dua za mzee na jinsi alivyosononeka kumkosa yule binti ndipo ikatokea safari iliyomfanya nae rafikiake amkose yule bint na kuchukuliwa na jamaa gani sijui ambae mwishoe nasikia kumbe yule bwana alikuwa na tamaa ya utajiri si akamuua kinyama yeye yule binti sambamba na mtoto aliyezaa nae na hapo ikawa si Mzee wangu wala yule rafiki ake aliyeweza kuishi na yule binti lakini yoooote yalisababishwa na binti mwenyewe laiti angekuwa na msimamo awali wa kumkataa yule rafikiake mzee aliyeanza kumchombweza na kumpondea mzee pengine haya yale yote yasingetokea hadi kuangukia mikononi mwa huyo bwana aliyekuja kumuua.
Daaaah! basi bwana ndio hivyo mzee hamasa zake nilizielewa na baada ya hapo kila mwanamke ninaemuona mbele yangu kuna muda namuona kama kinyago vile kwa jinsi walivyonipotezea malengo na pesa bila faida yoyote. Saivi ishu yangu nikijisikia navuta cheche tu la bar basi tunamalizana kila mtu kimpango wake hahahahahaaaa.."
'''''''

Alimalizia kwa kucheka ocs John na kumuacha kamishna Shebby katika taharuki kubwa hata Kimaro nae alikaa vizuri pindi alipokuwa anaisikiliza story ya ocs John.

"Enhee, Mkuu wangu safari hii wapi sasa na wewe uko wapi"
aliuliza John
"Daah, nilikuja kwenye msiba huu uliotokea sehemu yako juu ya mganga wa kienyeji aliyekutwa amejichinja kibandani mwake sasa nilitaka kujua tafiti zenu mlipofikia na awali sikuwaza hata chembe kama ningekutana na mtu tunaefahamiana kama wewe"
"Oooh! ni kweli bwana Dah! uchunguzi wetu bado unaendelea taratibu ila tuliruhusu mazishi yaendelee baada ya ripoti ya daktari kuthibitisha kuwa hakukuwa na kiashilio chochote kuwa marehemu alishambuliwa zaidi ilionekana ni msongo wa mawazo ulichachamaa ghafra na kupelekea kujichinja.
Ila tukiwa kama polisi bado uchunguzi wetu hatujaufunga rasmi."
"Sawa vizuri John"
aliongea Kamishna Shebby huku mawazo yake yakiipitia story aliyosimuliwa muda mfupi na ocs John hasa kwenye kipengele alichonukuu story iliyomuhusu babaake kidogo ilimtia shaka Shebby na kuhisi kuna vitu vinaingiliana na story ile ya Hussein kuhusu mkewe Zai.
Alitamani kumuuliza zaidi lakini alitafakari njia ipi ya kumuingiza tena kwenye ile mada hadi afunguke zaidi kuhusu story ya babaake.?
Na ndipo hatimae Shebby aliliacha lile na kurudi kwenye azma yake juu ya prove aliyotaka kumuonesha Kiamro kuwa yule aliekufa si Mr.X japo alikuwa na kovu usoni.

"Sasa John hebu achana na ripoti ya daktari nihadithie kuhusu nyinyi mlivyopata taarifa ya kifo kile na mazingira mliyokuta hivi ni kweli yaliwapa picha kuwa yule mtu alijiua?"
aliuliza Shebby sasa akiwa serious kama alivyokuja na kumfanya hata ocs John kukaa makini kwa utulivu mara baada ya kuulizwa lile swali na kama kawaida yake Shebby aliingiza mkono kwenye mfuko wa suruali kulipokuwa na simu yake special aliyoitumia kwaajili ya kunasa sauti kwani ilikuwa na uwezo mkubwa sana wa kurekodi pindi ocs John alipoanza kuzungumza.
ITAENDELEA.....
25

Sent using Jamii Forums mobile app
 
EPS 26
========

"Ni hivi mkuu, tulipokea simu iliyoleta hiyo taarifa majira ya saa tatu asubuhi na vijana walipofika walichukua picha na kuhoji maswali mawili matatu ya msingi na katika maelezo waliyotupa raia hususani mtu wa kwanza kumuona marehemu ambae alikuwa mwanae waliosaidiana kazi alisema kuwa babaake siku hiyo aliwahi mapema kwa nia ya kuandaa mazingira kuwa kuna mgeni wake mteja wa siku nyingi toka enzi za babaake angekuja lakini asubuhi ileile yule kijana alipofika na kuingia mule kibandani ndipo aliposhangaa kukuta babaake akiwa chini damu zimetapakaa huku mkononi akiwa na kisu."
"Sasa we kama ocs baada ya vijana wako kuleta taarifa hii ulichukua hatua gani zaidi"
"Kwanza mkuu niliwaamuru wapeleke mwili moja kwa moja hospitali kwa vipimo zaidi kama huenda alivamiwa na watu na kumchinja kisha kumshikisha tu kisu."
"wazo zuri sasa baada ya majibu kutoka kuonesha kuwa hakushambuliwa ndio mkaungana moja kwa moja na ripoti ya daktari mkimaanisha hakuna tena upelelezi wowote si ndio?"
"Mmmh, hapana mkuu, kama nilivyosema awali bado tunafanya upelelezi wa chini kwa chini."
"Upelelezi gani John hivi ulifika hata eneo la tukio.?"
"mh, hapana."
"Umeona sasa, unakikaribisha kitambi rafikiangu usipende uheshimiwa wewe ni damu changa kama mimi bwana inabidi vitu vyengine tujieke mstari wa mbele wenyewe tusipende kutuma tuma tu"
aliongea kwa msisitizo Shebby na kuongezea kauli zilizowashangaza hadi polisi waliokuwa ofisi ya jirani na ocs waliotega masikio ya umbea na kuzungumza chinichini kujua alichokuwa anazungumza Kamishna na ocs wao.
Kauli hiyo ya Shebby haikumshangaza tu ocs bali hadii St;sajent Kimalo mwenyewe na kushangaa kamishna wake ana provement zipi hadi imefikia kusema kwa kujiamini kiasi kile.
"Yaani, ndio hivyo ocs John nakuhakikishia kuwa yule mganga HAJAJIUA bali AMEUAWA."
aliekea msisitizo kabisa maneno yake Shebby na kuwafanya rafiki zake ocs John na st;sajent Kimaro kuachama midomo wasijue wamjibu nini kwa kuogopa kuwa huenda wakaeleweka vibaya mbele ya mkuu wao.
"Najua vichwa vyenu vinatamani kuniuliza nina uhakika upi hadi nasema hivi lakini haya majibu yangu kwenu yatakuja kwa mtindo wa maswali na mtashindwa kuyajibu na kwasababu hiyo sitowapa mimi majibu ila kuna mtu mmefanya kosa sana kumuacha huru, nahitaji aletwe hapa mara moja na nitamuhoji mimi mwenyewe na kila mtu hapa atapata picha kwanini nasema yule mganga hakujiua wala hakutingwa na mawazo bali ameuawa na aliyesababisha kifo chake ni mr.X"
"MR.X..!!?"
alishangaa sana ocs John mara baada ya kamishna Shebby kupitiliza maneno na kujikuta anaropoka jina la mr.X ambalo kwa upande wa ocs John lilikuwa geni kabisa.
"Usijali John, ni hadithi ndefu sana ila nitakuhadithia japo si leo kwanza nataka utume vijana wako akakamatwe huyu mtu mara moja."
"sawa Mkuu, nani mtu mwenyewe vijana wakaifanye hiyo kazi sasa hivi aletwe hapa."
"Nahitaji akakamatwe mtoto wa marehemu aliyekuwa msaidizi wake, huyo wa mwanzo kabisa kumuona marehemu."
"sawa Mkuu."
Baada ya hapo ocs alimuita sub inspekta wake akusanye vijana saba haraka wachukue difenda kwenda kumkamata mtoto wa marehemu yule aliyejichinja ambae pia ni mjukuu wa marehemu Mnyungunyungu aliyetarajiwa kuwa mganga atayefatia na mara tu vijana walipopewa agizo lile walioonesha ushupavu wa hali ya juu hasa walipogundua kuwa aliyetoa amri ile alikuwa ni Kamishna na walionesha utiifu na ushupavu mbele yake ili wasionekane wachovu na ndipo gari ilipochomoka kwa speed kali kuwahi Mkuyuni stend ili waelekee kule msibani kutimiza amri waliyopewa.

Lakini ajabu toka waondoke wale vijana wa polisi walichelewa sana kurudi na kwa haraka zao zilizochangiwa na woga mbele ya Kamishna walijikuta wanaacha hadi radio call zao hali iliyomtia hasira Kamishna Shebby na kuwaamuru kimaro na ocs watoke pamoja nae waelekee huko walikoenda vijana wao.
Hali ile na amri za Shebby ziliwafanya polisi wote kuwa kimya na kuwa makini sana katika kazi zao muda ule wakimuhofia sana na kumtafsiri kuwa yule kamishna ni mkali mno na mkorofi bila kujua kumbe Shebby alikuwa mtu peace sana ila tu kichwa chake kilivurugwa hasa baada ya kujiingiza kwenye ishu ya kutaka kumjua Mr. X.

Walipofika nje huku escot ya difenda nyengine ikiwa tayari ishabeba vijana wakingoja amri ndipo waliishuhudia difenda waliyoituma ikirudi na kuwasili kituoni na vijana kushuka haraka haraka na macho ya Shebby yalishangaa kutomuona mtu waliyemuagiza zaidi ya wamama wawili.
Akiwa kakunja uso na kutaharuki Shebby alimwita sub inspector aliyeongoza ile mission muda ule kutaka aletewe ripoti yeye mwenyewe moja kwa moja bila kupitia kwa ocs kwanza kwa kuona kama anachelewa na ndipo wote watatu walitaharuki kusikia ripoti iliyorudi.
"Mkuu tumefanya kila jitihada za kufanikisha kuja na mtuhumiwa lakini hatukufanikiwa kumpata baada ya kutoweka masaa machache kabla hatujafika."
"AMETOWEKA!!!?"

"Ametoweka toweka vipi! wakati nilimuacha mimi mwenyewe pale misibani na hayakupita hata masaa sita?!"
alihoji kwa mshangao Kamishna Shebby.
"Ndio hivyo mkuu na tumerudi baada ya kuona muda unaenda pia tulisahau mawailiano na tuko tayari kwa amri mtayotupa ila tumewaleta hawa wake wa marehemu wanaweza kutwambia wapi alipo mtoto wao."
"Huo ni upumbavu. sikutaka aletwe mjane yeyote hapa. Chukueni vitu vyenu kusanya vijana wako msako uanze mara moja hadi apatikane huyo kijana."
Alitoa amri Kamishna Shebby na kumuamuru Kimaro aendeeshe gari yao ambapo safari hii walipanda wanne sambamba na Mkuu wa upelelezi na jumla ya gari tatu zilitoka kituoni kuelekea Mkuyuni stendi huku jumla ya vijana wenye bunduki zaidi ya kumi na tano wakiwa kwenye difenda mbili katikati kukiwa na gari iliyowabeba kina Shebby na kituo kilibaki na askali wachache sana wakiongozwa na mama mmoja aliyekuwa nae na cheo cha sub inspecta.

Wahuni na watu wote Mkuyuni walipigwa na bumbuwazi mara baada ya kuona msafara wa polisi ukisimama kwa fujo zote maeneo ya stendi.
"Oya wana Kimenuka anga hizi tujikataeni.."
aliongea teja mmoja aliyekuwa anacheza kamali na wenzake pale stend mara baada ya kuona difenda zile za polisi.
Kilichoendelea pale askali walitawanyika na msako mkubwa ukaanza huku wahuni wengine wakikimbia ovyo kwa kuhofia huenda walikuja kukamatwa wao.
Kamishna Shebby pamoja na wenzake ocs John, st;sajent Kimaro na yule mkuu wa upelelezi wao waliongoza moja kwa moja mpaka pale msibani sambamba na askali watatu wenye bunduki.
Wakati huo Shebby nae alikuwa kashachukua pisto yake ndogo anayoiachaga kwenye dashibodi ya gari huku kimaro nae hivyo hivyo alichukua yake na kuichokea nyuma ya mkanda wa suruali na watu wote pale msibani walizidi kustaajabu kwani muda si mrefu uliopita walikamatwa wake wa marehemu na kuzua sintofahamu kwa kila mtu aliyekuwa pale msibani.
"Babu, naomba usiwe na wasi wasi tutajie wapi alipoenda yule mtoto wa huyu marehemu."
ilikuwa ni sauti ya Kamishna Shebby mara baada ya kumfata yule babu aliyekuwa amevaa kibaraghashia alipokuwa anaongea huku amezungukwa na watu waliokuwa wanaulizia kilichotokea muda mfupi kabla hawajaja kina Shebby.

ITAENDELEA.....
26

Sent using Jamii Forums mobile app
 
EPS 29
========

* * * * * *

Vijana walikuwa tayari na muda ule ule wakaanza kumkamata mzee mmoja mmoja waliyekuwa wakioneshwa na kamihna Shebby na Kimaro.
Watu wengi walishangaa tukio lililokuwa linaendelea kufanywa na wale askali licha ya kuwa walikuwa kwenye huzuni na msiba mzito na kitendo kile kilichoanza cha kamatakamata kilizidisha kilio kwa familia nyengine hususan watoto na wake wa wale wazee waliokuwa wanakamatwa.
"Halooo babu yule mwenzako mwenye baraghashia yuko wapi?"
aliuliza Kimaro pindi alipomfata mzee ambae tayari alishadhibitiwa na vijana wa polisi mara walipooneshwa.
"Haa! jamani mjukuu wangu kwani tumekosea nini mbona mwatuumiza kiasi hiki?"
alihoji yule mzee.
"babu jibu swali usiulize swali nisije kukuzimisha sasa hivi unavyotuona sisi ndo tushapagawa kuliko mtu yeyote hapa."
aliongea kiukali Kimaro na mara dakika zile zile Kamishna Shebby akiwa na askali mwengine walifika pale.
"vipi Kimaro inaonekana bado mzee mmoja."
"Kweli mkuu na ndio nilikuwa namuuliza huyu alipo mwenzake kabla vijana hawajaondoka nae"
alijibu Kimaro lakini dakika zile zile walisikia ukelele furani kutokea upande wa kaskazini kulipokuwa na nyasi nyingi na miti mikubwa michache na kabla hawajajua wafanyeje mara alikuja mtoto mmoja raia wa pale kijijini ambae ilisemekana ni mjukuu wa yule mzee waliekuwa wanamuulizia huku akiwa anahema sana kichwa chote kimetapakaa majani.
"vipi dogo?"
aliuliza haraka Kamishna Shebby huku akitoa pisto yake pale kiuononi.
"Babuu.. babuu yupo kuleee tulikuwa tunakimbia na jitu moja halina usoo aaaah! linataka kumuua babuu..."
aliongea kwa shida kutokana na hofu iliyojengeka kwenye kifua chake na kabla hajamalizia Kamishna Shebby alipiga risasi moja juu na kuwaamuru wenzake haraka wawahi eneo iliposikika ile sauti.

Walikata mapori haraka haraka huku wakiruka visiki na Kamishna Shebby aljikuta anakuwa na mbio kuliko wenzake na kuwahi ile sehemu ambapo alimkuta yule mzee akiwa amelala chini akiwa katapakaa damu pia akitokwa damu mdomoni na puani na kifuani mwake kulionekana ameshikilia mpini wa kisu kilichozama chote eneo la kifua upande ule wa moyo.
"Jasho lilikuwa linamvuja na kutaharuki shebby pamoja na wenzake waliofika muda ule huku wengine wakikagua maeneo ya jirani kuona kama kuna mtu mwengine.
"Nambie babu.. nambie tafadhali najua unajua nitajie nani Mr. X nitajie mzee wangu jitahidi nitajie hata cheo alichokuwa nachoooo.."
aliongea huku machozi yanamtoka shebby mara baada ya kupiga magoti na kumpakatia yule mzee aliyekuwa bado hajafa ila yupo katika hali mbaya na kweli alianza kujilazimisha kuongea kwa shida huku mdomo wake ukirusha mafunda ya damu yaliyokuwa yanamrukia usoni pia shebby.
"Huu.. missss..ta.X ni... nii..aaaghhhrrr...niii....."
Lakini akiwa anahangaika kusema kabla hajamalizia ni nani huyo mr.X mara kichwa cha yule mzee kilifumuliwa ghafra na ubongo kutawanyika sambamba na damu kutokana na risasi iliyotua bila kutoa mlio wowote mbele ya macho ya Kamishna Shebby OCS na st;sajent Kimaro.

* * * * * *

Wakati huo upande wa pili makao makuu ya gereza mzee Mwinchande alighadhibika na kumpigia mwanae lakini simu safari hii haikupatikana kabisa.
"Kijana hebu naomba nisaidie aitwe huyo mfungwa mwenyewe nimuone anambie nini alichomuhadaa mwanangu hadi afikie huko kote."
aliongea mzee Mwinchande ndipo yule mkuu msaidizi alipoamua kumpigia simu ya mkononi coplo aliyesimamia jera za v.i.p na kumpa maelekezo na baada ya dakika kumi na tano aliletwa mzee Hussein eneo ndani ya ofisi ile kuu.
"Huyu hapa mkuu."
aliongea yule coplo aliyemleta huku akiwa ameongozana na askali wengine wawili waliomshika Hussein kipindi wanamkokota kwenda nae mahala pale.
"oke sawa, mnaweza kusubiri nje."
alitoa amri mkuu msaidizi na hatimae ndani wakabaki watatu yaani mkuu msaidizi, mzee Mwinchande na Hussein babu Bubu.
"Mtu mwenyewe ndio huyu?"
aliuliza mzee Mwinchande licha ya kuwa tayari alishaelekezwa kuwa ataletwa mfungwa mwenyewe aliyesumbua kichwa cha Kamishna Shebby na ndie yule aliyeletwa muda ule.
"ndio huyo mzee."
"sawa unaitwa nani bwana"
aliuliza mzee mwinchande huku akimuagalia kwa dhalau Hussein
"We bwanaaee si nakuuliza mie?"
aliuliza tena mzee Mwinchande baada ya Hussein kubaki kimya akiwatazama tu huku moyoni mwake akiwa kaghadhibika baada ya kuoneshwa dhalau.
"mzee wangu huyu muda mwengine anakuwaga sanamu hivyo hivyo sasa ngoja tum boost. coplo Yonaaa.."
alidakia mkuu msaidizi na kumwita coplo ambae alimuelekeza amboost Hussein aweze kusema na kweli coplo Yona alichomoa mkanda na kuanza kumtandika Hussein hadi mzee Mwinchande mwenyewe akazuia mara baada ya kuona tayari Hussein alipasuka hadi kwenye mdomo.
"Haya mzee mwenzangu mi nakwambia kwa ustaarabu lakini wewe unataka uambiwe kama ulivyozoeshwa. sasa narudia kabla sijaendelea wewe unaitwa nani?"
Alirudia kweli kauli yake mzee Mwinchande lakini Hussein alikuwa kiburi sana hasa anapogundua mtu anayeongea nae anamletea dhalau.
Vitasa viliendelea bila Hussein kujibu chochote hadi mzee Mwinchnde alianza kufoka.
"Yaani mwanangu anajitolea kusaidia mabubu yasiyo na fadhila wala mawazo kama hili??? Duuh! sasa Shebby kasema sema nae vipi mbona sielewiii hapa."
Kipindi alipokuwa analalama mzee Mwinchande na kumtaaja Shebby ndipo hapo ubongo wa Hussein ulivubuka kwa kujua kumbe yule mzee ni baba wa kamishna yule aliyejitolea kumsaidia.
"Kumbe wee ndie baba wa Kamishna Shebby."
aliongea kwa sauti yenye mikwaruzo Hussein mara baada ya kusikia kumbe yule mzee ni baba wa mkuu wa gereza Kamishna Shebby.
"Jamani msinipige kama huyu bwana ni baba wa Kamishna Shebby tafadhali niacheni niongee nae."
alisisitiza Hussein na hapo ndipo vijana wa coplo walipomuacha kumtandika mikanda na kumsimamisha aongee.
"Enhee! sema umemuhadaa na hadithi gani mwanangu mpaka haeleweki mambo yake."
"Lakini hapo sielewi kaka kwanini unasema nimemuhadaa."
"oke, utaelewa tu."
aliongea mzee Mwinchande huku akisukuma kiti chake na kukaa vizuri.
"Sikia bwana bubu, kwanza samahani kwa kukufokea mzee mwenzangu ila unajua mtoto anauma sana. sasa mi nilitaka kujua ni hadithi gani inayokuhusu uliyomsimulia mwanangu hadi kupelekea kuwa bussy kiasi hiki.? Naomba unijibu kweli na unihadithie walau kiufupi kwasababu mimi ni baba mzazi wa Shaaban pia ni Kamishna mkuu msaidizi mstaafu wa jeshi la polisi nchini kwa hiyo usiwe na hofu wala uoga wa kunihadithie ukweli ulichomwambia mwanangu tujue nini cha kufanya maana mpaka sasa nahisi mwanangu kajibebesha mzigo asioujua wapi pa kuutulia."
aliongea mzee Mwinchande na ndipo hapo Hussein alipofikiria na kukata shauri kuamua kuzungumza ukweli kile ambacho alikizungumza kwa Kamishna Shebby na hasa akikazia kuwa wanawake ni wauaji kwani aliamini huyo mtu aliyeitwa mr.X alijuana vizuri na mkewe lakini mkewe alimficha so ubaya wote kaufuga mkewe na pia mission aliyokuwa anaifanya Shebby ni kutafuta ukweli kuwa huyo mr. X alikuwa nani?

"Uuuuuppphhhhh!!!!! ... yaani hadithi yako imenishangaza sana na kuniumiza pia pole sana bwana."
alihema mzee Mwinchande na kumpa pole bwana Hussein bubu baada ya kuguswa na kisa chake.

ITAENDELEA...
29

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WANAWAKE NI WAUAJI..!?
EPS 42
========
BY - MTOTO WA BECKER (The Special Thinker)
______________________
______________

"Pole sana mzee wangu kwa kumpoteza shujaa akiwa bado na umli mdogo vile"
alivunja ukimya Cj4 mara tu walipoanza kukaribia mkoa wa Pwani na kuzifufua hasira za maumivu zilizokuwa kifuani mwa Kamanda mkuu wa Jeshi la polisi mstaafu mzee Cyplia.
"Aaagh! yaani mwanangu unavyosema hivyo unazidi kunitonesha kidonda cha mwanangu John! aaagh! mungu ampumzishe kwa amani."
"Daah! binafsi mzee wangu nimeamua kujikita katika upelelezi wa kujua kilichotokea kwani inasemekana chanzo kabisa ni mfungwa aliyekuwa gereza alilosimamia Kamishna wetu yule mtoto wa kamanda wako msaidizi enzi zenu "
"Aaagh! ndio mtoto wa Mwinchande!"
"eeh, sasa kumbe alikuwa katika mpango wa kumsaidia yule mfungwa baada ya kujua story yake na ukweli halisi wa kesi ulikuwa kule morogoro lakini alipoenda kufanya tafiti na kusaidiana na askali wa kule ndo yakatokea ya kutokea"
"Mh! sasaa kidooogo naanza kupata mwangaza"
aliongea mzee Cyplian na kumfanya Cj4 azidi kutuliza umakini kwani tayari moyoni mwake alishaanza kumuhisi huenda yule mzee akawa ndie Mr X lakini aliamua kuongea vile ili kumpoteza na kujifanya hajamstukia kitu ili iwe rahisi kumteka kimazungumzo
"Mwangaza gani tena mzee wangu"
"Kwa yaliyotokea ila naamini hadithi ya huyo mfungwa ndio funguo ya kumjua muhusika aliyewafanyia unyama wanangu.,,,,"
kauli ya mzee Cyplian ilibeep ubongo wa Cj4 wakati huo tayari walikuwa wanaingia Chalinze lakini mara ghafra kabla mzee Cyplian hajaendelea wala Cj4 hajauliza chochote ghafra walishangaa kuona basi lililokuwa linatokea njia ya Tanga likipitiliza na kuingia mkuku mkuku barabara kuu huku likiwa limewasha taa na kupiga honi mfurulizo kuashilia kuwa aidha dereva limemshinda au limekata breki na kutokana na speed aliyokuwa anakuja nayo Cj4 alijikuta anashindwa kusimama na kuhamia barabara ya pili ili apate kulikwepa lakini bahati haikuwa yake baada ya kukutana na kiuno cha tela la roli lililofunga breki za ghafra kwa kuogopa kulivaa basi lililokosa muelekeo na kusababisha tela kugeuka kuelekea usawa wa gari la kina Cj4 huku kikisikika kishindo kikubwa sambamba na milio ya breki iliyosababisha cheche kuwaka barabarani na kelele za hofu toka kwa wafanya biashara na watu mbalimbali zilizosikika Chalinze nzima.

Hakuna aliyeelewa jinsi gani ile gari ndogo Landcruiser nyeupe iliyokuwa inaendeeshwa na Cj4 ilivyofika fika kule kwenye tawa za umeme tena ikiwa imechakazwa mno sehemu za mbele, na baada ya watu kukimbilia hususani wale wahuni na vibaka mpaka pale ilipokwamia ile gari walimshuhudia mzee mmoja kwa ndani akiwa kabanwa ipasavyo kwenye kiti na bashboard huku ule upande wa dereva kukiwa patupu na ndipo vijana wale wa kihuni walipong'ang'a kuuchomoa mlango mmoja uliojikunja ili wapate kuingia na kuitoa blufkes waliyoiona kwa ndani wakiamini lazima kutakuwa na hela tu.
Lakini kabla hawajafanya hivyo walistushwa na sauti ya mtu akiwaamuru waondoke haraka ikitokea nyuma yao na walipogeuka kutazama walimshuhudia askali mmoja ambae mavazi yake ya juu yalichafuka kwa damu iliyokuwa inaendelea kuvuja kutokea kichwani na ndipo wale wahuni wote walipotimua mbio.
Hakuwa mwengine bali ni Cj4 dereva wa ile gari nyeupe iliyokwamia pale kwenye matawa ya umeme akiwa na jeraha lililokuwa linavujisha damu nyingi huku ikiwa haieleweki alitokajetokaje kutokana na kubondeka vibaya hasa ule upande aliokaa yeye.
Alimuangalia mzee Cyplian na moyo kumuuma zaidi mara baada ya kugundua kuwa alishafariki pale eneo la tukio na hapo hapo kwa speed bila kujali damu zilizokuwa zinamvuja Cj4 alianza kukimbia kuelekea barabara kuu ambapo jumla ya magari sita yalipata ajali iliyosababishwa na lile basi lililopoteza muelekeo ambalo lilianguka na kuseleleka upande wa pili hadi kwenye vibanda vya mama lishe na kusababisha maafa makubwa mara baada ya derva kulazimisha kukata kona licha ya mwendo kasi lililokuwa nao.
Kitu cha kwanza kufanya Cj4 akiwa kama mtu aliyechanganyikiwa alisimama na kulitazama eneo lile la ajali na kuanza kupiga hesabu alizozijua yeye wakati huo maaskali ndio walikuwa wanawasili eneo lile licha ya kwamba kituo hakikuwa mbali na mahala palipotokea ajali.
(''Hii ni ajali ya Kutengeneza kabisaaa,'')
aliwaza Cj4 na kukimbilia kwenye ile basi na kuvunja kioo cha mbele kwa kupiga teke kali na alibahatika kumchomoa dereva ambae licha ya kwamba hali yake ilikuwa sio nzuri lakini alijitahidi kuzungumza
"Jitahidi kuongea mimi ni askali nimekushika, nambie mara ya mwisho mlisimama wapi kwa ufasaha kabisa"
alionga Cj4 kumuuliza yule dereva ambae alitoa maelekezo kwa shida huku akimwambia kuwa gari iliferi breki baada ya kuhisi waya maalum uliopita kwenye propela ulioshikilia vipira vilivoenda kukamata ringi za taili za mbele kuwa ulikatika ghafra na hakujua chanzo.
maneno yale ya yule dereva yalizidi kumuaminisha Cj4 kuwa ile ajali ilitengenezwa tu sio bure lakini kama imetengenezwa wamefanyafanya vipi hao watu? hapo akakosa jibu ndipo alipotaka kumuuliza tena yule dereva mara askali wengine walifika eneo lile na kuanza kuwatoa majeruhi wa kwenye basi wakishilikiana na wananchi huku naye Cj4 akipigiwa saloot na askali aliowapita cheo na wakimsihi wampeleke nae akatibiwe kwani alikuwa kaumia sana kichwani licha ya kuwa yeye mwenye alijiona yuko sawa.
Na wakati akiwa kasimama akiangalia pilika pilika zilizokuwa zinaendelea za uokozi na wapiga picha eneo lile mara macho yake yaligongana mara mbili na macho ya binti mmoja aliyevalia kiislamu usoni mwake akifichwa na nikabu nyeusi akiyaacha macho tu huku akitembea kwa madaha bila wasi kuelekea sehemu aliyopaki gari yake ndogo lakini kila alivyokuwa anapita alipogeuka macho aliyaelekezea kule kwa Cj4 na kwa ile Landcruide iliyobondeka kwenye Tawa za umeme na hapo hapo aret ya hatari iligonga kichwani na Cj4 na kuhisi yule mwanamke ndie aliyesababisha ile ajali na kuanza kupata ufumbuzi basi huenda mzee Cyplian hakuwa mr.X kama alivyomuhisi awali ila alitia shaka kuwa huenda mzee Cyplian kuna vitu alivijua kuhusu mr X na ndio maana mr X amewatuma vijana wake kufanya ujanja wowote ili mradi wahakikishe mzee Cyplian hatoboi ukweli wala siri yoyote kuhusu mrX.
Lakini akiwa na maswali lukuki Cj4 kila alipomtazama yule bint moyo ulimtuma amzuie tu kwani macho ya yule binti yalionesha wazi kuna kitu anataka ahakikishe kule ilipodondokea ile gari na ndipo alipowaponyoka polisi wenzake na kukimbilia upande wa pili ilipokuwa ile gari ya yule bint ambayo ndio ilikuwa inaondoka taratibu eneo lile lakini kwa bahati mbaya zaidi Cj4 alianza kujisikia kizunguzungu kabla hajafika na kujikuta anadondoka katikati ya barabara ambayo ilikuwa inazungushiwa utepe wa kuzuia magari yasipite upande ule na macho yake yaliishia kuitazama kwa mbali ile gari pindi alipokuwa anadondoka na kupoteza fahamu.

* * * * * *

Akiwa amekaa huku mawazo na hasira juu ya yaliyopita hususani mr X na vifo vya rafiki zake huku akiwazia kukutana na Hussein bubu, ndipo Shebby alistushwa na sauti ya babaake pindi alipokuwa anaongea kwa njia ya simu kwa mshtuko mkubwa na kumfanya atoke na kukimbilia sebuleni aliposimama mzee Mwinchande akiendelea kuongea na simu.
"Vipi baba nini kimetokea?"
aliuliza kwa taharuki Shebby baada ya kuuona uso wa babaake ukionesha kushangazwa na kustushwa na alichokuwa anakisikia
"ajali mwanangu"
"Ajali? nani tena!"
"Mkuu mstaafu wa jeshi la polisi Kamanda Cyplian anasadikika amepata ajali mbaya wakati akiwa njiani kuja Dar"
"Kha!! ilikuwaje sasa, si yule babaake marehemu ocs wa Mkuyuni?"
"haswaaa, yaani aaagh! namkumbuka vizuri alikuwa mkubwa wangu na mtu wa karibu kipindi hiko daah!"
"Daah! shit, amepona?"
"Bado hatujapata hakika"
Baada ya Shebby kuzipata habari zile muda ule ule alichukua simu yake na kumpigia kamanda wa mawasiliano ya idala ya dharula na alipouliza walithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na tayari kuna timu ya vijana ilikuwa njiani kuelekea huko.

Aliingia ndani Shebby na kujiandaa kwa kuvaa gwanda zake hali iliyowashangaza wazazi wake na kumuuliza kulikoni lakini alichojibu kiliwashangaza wote.
"Baba najua ni ajali tu imetokea lakini kuonana na mzee Cyplian ni jambo la muhimu sana kwangu ktk njia za kumjua mr X"
alijibu Shebby na kutoka mkuku na kuchukua gari aina ya Jeep na moja kwa moja aliondoka kwa speed maeneo ya kwao mara baada ya mlinzi kufungua geti huku akiwa hataki kusikia chochote toka kwa babaake ala mamaake.

Mwendo aliokuwa anatembea Shebby nimeshindwa hata kuuelezea mara baada ya kupita maeneo ya Kibaha na kutembea upande ambao ulikuwa haumruhusu lakini alifosi hivyohivyo huku akipiga honi mfurulizo lakini ghfra alipokuwa anapandisha kilima cha kuingia Mlandizi almanusura nae apate ajali baada ya kukosana na gari ndogo aina ya toyota creaster uso kwa uso na kusababisha wote wayumbe na yule dereva mweney wa toyota bado kidogo atumbukie mtaroni lakini nae alikuwa mtaalam sana na alifanikiwa kuidhibiti gari na kutulia tena barabarani na kuangalia nyuma kwa kutumia site mirror ambapo aliishuhudia ile Jeep nayo ikiendelea kuambaambaa pembeni ya barabara na kukaa sawa huku speed ikiwa pale pale.
Chaajabu alitabasamu yule dereva badala ya kuchukia na kuendelea kupiga gea na hakuwa mwengine bali ni yule yule binti aliyejiziba uso kwa nikabu ambae Cj4 alimtilia shaka kule Chalinze.
42

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WANAWAKE NI WAUAJI..!?
EPS 47
========
BY - MTOTO WA BECKER (The Special Thinker)
______________________

"Asha, hapana mwananguuuu.... Usiongeeee kwa sauti hiyooooo... aaaaaaah Najua itakuwa ngumu kuelewa harakaharakaaa mamaaa .. ila huyo mzee unayemuona mbele yakooo ndiee....ndieeeee.... ndie babaako Mzaziiiiii....hiiiii"
aliongea kwa kujikaza kisabuni yule mama mbali ya kuwa alikuwa na uchungu mzito moyoni mara baada ya kujitonesha kidonda cha kumkumbuka marehemu dadaake.
"Whaat!! Mamaaa!!?.."
alitaharuki Asha na kugeuka kumtazama Hussein kwa mshangao wa hali ya juu na kumtazama tena mamaake ambae sasa nae alikaa kitako na kuanza kujifuta machozi kwa kanga huku akimuangalia mwanae Asha ambae alikuwa bado kataharuki.
"Asha mwanangu, huyo ni babaako.. Huyo ndie Hussein babaako ambae tulikuficha ukweli miaka yote ila leo nitahadithia kila kitu na yoote ambayo huenda hata Shemeji Hussein hukuyajua... naomba Asha unisikilize kwa umakini sana mwangu."
aliongea kwa uchungu Zena huku akijifuta tena machozi ambayo yalikuwa hayakomi kumtoka na kumfanya Asha aungane nao na kukaa kabisa pale chini huku upande wake wa kushoto alionekana Hussein na kulia kwake alionekana mamaake ambae ni Zena.
"Asha... Asha kwanza naomba utambue mimi si mamaako mzazi, nimeumia sana leo na naikumbuka sana barua ya dada aliyoniachia sambamba na maneno yake ambayo yote yalisafiri na maji mara baada ya mafuriko siku chache baada ya kifo chake kabla hawajaja wale wafadhili kukuchukua kwa msaada ulipokuwa darasa la nne baada ya kupita miaka sita ya maisha magumu na maajabu yako shuleni.
Mwanangu japo ilionekana sahihi kukuacha uende kulelewa na watu wengine tena ukiwa na umli wa miaka kumi tu na japo faida yake nimeiona na naiona mapaka sasa unanilea lakini ukweli nimeenda kinyume kabisa na maagizo aliyoniachia dadaa ambae ni mamaako. aaagh! Hussein unisamehe sikuwahi kumleta Asha wala kumwambia ukweli ambao dada alinisisitiza pindi atapokua nimwambie...
Eee Mungu nisamehe lakini sidhani kama nimechelewa, naahidi sasa nitawaambia ukweli wote nilioujua kuhusu Asha Dada na Hussein."
sauti ya mkwaluzo iliyoonesha dhahili imebeba maumivu mazito kutoka moyoni ilisikika ikitoka midomoni mwa Zena na kumfanya hata Dk Asha aanze kulengwa na machozi huku Hussein bubu yeye ndio kabisa alibaki kaganda kama sanamu akili na masikio yote aliyaelekeza kwa Zena japo macho muda wote yaliganda kwa Asha.
Alimeza funda la mate Zena huku akirekebsha sauti yake kwa kukohoa kidogo kwa kujikaza kiume na kuanza kusimulia kisa chote kilichokuwa nyuma ya pazia juu ya maisha ya Mariam na Asha.

* * * * *
(MIAKA 23 ILIYOPITA)
>>>
..................Simulizi Ya Zena....................
^^^
Sintoisahau ile siku dada aliponipigia simu akiwa anaongea kwa shida sana akinisihi niende haraka kwake kwa sauti ambayo ilinitisha na kunipa wasiwasi hali iliyonipelekea niache shughuli zote nilizokuwa nafanya nyumbani na kukimbilia kituo cha daladala pasi na kumuaga yeyote wala kumsubiri mama ambae alikuwa ameenda kwenye shughuli ya harusi ya mtoto wa rafikiake mwananyamala,
nilisimama kituoni na muda mfupi ilitokea daladala iliyokuwa inaelekea kule nilipokuwa naenda ambako ndipo alipopanga dada Mariamu na mara baada ya daladala ile kusimama kituoni nilipanda na baada ya mwendo wa dakika kadhaa gari ilifika kwenye kituo nilichokuwa nashuka na kushuka huku nikitembea mwendo wa haraka haraka kumuwahi dada ambae nilikuwa najua kuwa anaumwa lakini sikuwahi kuwaza kama ugonjwa aliokuwa anatuambia ungeweza kumzidia na kumfikisha katika hali mbaya kiasi kile kama nilivyotafsiri kupitia sauti yake niliyoisikia simuni muda mfupi.

Sikuamini pindi nilipoingia ndani moja kwa moja na kumkuta mtoto wa dada ambae ni Asha kipindi hiko akiwa na miaka minne tu akiwa analia pale chini huku akimtingisha mamaake aliekuwa amelala huku nzi wengi wakiwa wamemjalia sehemu ya koo na mdomo ameuacha wazi ulimi kiwa umemtoka mithili ya mtu aliyekuwa amebanwa na kitu shingoni.
'Daaadaa!!....daadaaaa..!' Niliita kwa uchungu na kumsogelea pale chini huku machozi yakinitoka nikiwa sielewi nini kimempata dadaangu kufikia katika hali ile ya kushindwa hata kuitika na kubaki akinitazama tu huku macho yake yakitokwa machozi mfululizo na kunijengea imani ni kiasi gani alikuwa anapata maumivu makubwa sana ya ugonjwa ambao hadi dakika huo nilikuwa sijaujua hadi pale nilipojitutumua kumuinua kwa lengo la kumrudisha kitandani kabla sijafanya taratibu za kuita gari ya kumuwahisha hospitali na hapo ndipo niliposhangaa kuona uchafu uliokuwa unatoka chini kidogo ya shingo ya dada karibu na eneo la bega tena ajabu ulikuwa unatokota kadri alivyokuwa anataka kujaribu kusema kitu ama kumeza mate na kunifanya nitaharuki na kugundua sababu za nzi wengi kumzonga dada Mariamu.
'Aaaaaaaah..daadaangu nini tena kimekupata?!!'
Nilijikuta najisemea mwenyewe huku machozi yakinitoka kila nilipokuwa namuangalia na Asha alivyokuwa analia tena huku akiwa kashika bakuli ya plastiki mkononi akitingisha miguu ya mamaake bila kujali uwepo wangu.
"maamaaa tata ujiiii... mama ujiiiii.."
Sauti na maneno ya Asha yalizidi kuniliza na kubaini kuwa zaidi kilichokuwa kinamliza Asha ni njaa na ilionesha wazi hakukupikwa chochote siku hiyo toka asubuhi na masikini ya Mungu mtoto mdogo kama Asha ambae bado akili yake ilikuwa haijakomaa, hakuwa anajua nini kimempata mamaake hadi wamekaa na njaa muda wote na hakuwa na chochote cha kufanya kwa umli wake zaidi ya kumtingisha kwa kumuamsha mamaake apike basi huo uji ambao niligundua ndio kilikuwa chakula kikubwa alichokizoea yule mtoto.
Sikuwa na cha kufanya zaidi ya kutoka kuomba msaada kwa majirani mara baada ya milango mengine miwili ya ile nyumba iliyokuwa na vyumba vitatu tu alipopanga dada kuonekana makufuri yakining'inia na kuashiria wahusika hawakuwepo na kwa bahati mbaya hata wale majirani niliowafata ambao asilimia kubwa niliwakuta wanawake baada ya waume zao kuwa kwenye mishughuliko hawakuweza kabisa kunipa msaada.
Hali hii ilinishangaza mno kwanini wale majirani wamekuwa na roho mbaya kiasi kile kwani kila niliyemfata kumuomba tena huku nikiwa nalia kama mtoto alionesha kunihurumia na nia ya kunisaidia lakini nilipomuelekeza nyumba yenyewe basi hubadilika na kuzuka sababu nyengine tofauti huku wengine wakidiriki kunicheka kabisa na kunitajia kiasi kikubwa cha pesa kama nitakuwa nataka msaada wao.
Nilihumia na sikujua sababu za msingi kwanini waltu wa pale walimchukia sana dadaangu na kushindwa kunisaidia walau kumbeba kumfikisha barabarani stendi ya Taxi kwani kiukweli eneo lile alipokuwa anaishi dada hakukuwa na njia ya kuruhusu gari lolote kufika hata bajaji.
Sikuwa na jinsi nilijikaza tena kiume na kupiga moyo konde nilikimbia kama mwizi ama kichaa moja kwa moja hadi pale stendi na kuwaita vijana wawili ambao nilipatana nao kiasi furani cha pesa na kukubaliana nami kwenda kum beba huyo mgonjwa kumleta kwenye Taxi ambayo nayo niliongea na dereva wake aliekubali kutusubiri.

Nilitangulia ndani na kumfunika dada vizuri hususani sehemu za juu kuuficha uchafu uliokuwa unavuja na kutoa harufu kali kwa kitenge changu ambacho nilijifunga kiunoni na kujikuta nabaki na skin tight ndefu ambayo awali nilikuwa siwezi kutembea mtaani nikiwa nimevaa yenyewe tu pasi na kujifunga walau kanga ama kitenge lakini siku hiyo nilijikuta najisahau kabisa kwa kuchanganyikiwa na laiti kama nisingekuwa na walau hiyo skin tight basi hata uchi kabisa ningetembea pasi na kujijua wala kujihisi.
Lakini kila nilipokuwa namuangalia dada alinionesha machoni kuwa kuna jambo anataka kunambia lakini anashindwa na nilipomtazama kwa makini alinipa ishara kwa kuangalia kwenye dressing table yake na kuniangalia mimi, alifanya vile kama mara tatu ndipo nilipoenda kuangalia hapo kwenye dressing table kuna nini na nilipekuwa kuangalia ndipo nilipoiona bahasha kubwa ya barua ikiwa imeandikwa jina langu kwa nje na ndipo nilipomuangalia dada ambae aliniashilia kwa macho kuwa ndio hiko kitu alichomaanisha lakini kwangu sikuona umuhimu wa kukaa chini kuanza kusoma barua wakati dadaangu amelala anateswa na maumivu makali..!!
Nilichofanya niliitumbukiza kwenye handbag yangu ile barua na
kuwaruhusu wale vijana waingie ambapo walipoingia niligundua mshtuko wao na adha ya harufu ya ajabu waliyokutana nayo mule ndani ambayo mimi sikuihisi nilipoingia hadi pale nilipojionea kidonda cha dada kilichokuwa kinavuja uchafu na hata hivyo sikukerwa hata chembe kwa ile harufu zaidi ya kuniongezea simanzi
47

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika "WANAWAKE NI WAUAJI".

Binafsi nimejifunza mengi sana hapa.....vilevile nimependa, jinsi mtunzi alivyoyasuka matukio yake, kiukweli amejitaidi sana. Hongera zake....

Napenda kusema asante sana Madame S, kwa kushare nasi hii kitu....Ubarikiwe madam.

WANAWAKE NI WAUAJI..!? (74)
BY - MTOTO WA BECKER (The Special Thinker)
_________________________
____________________

^^^^^^^^^^^^^^
* * * * *
>>>
^^^^^^^^^^^^
* * *
^^

Ni katika makaburi ya Makanya Dar es Salaam wanaonekana watu wawili wakiwa wote wamevaa nguo nyeusi mmoja akiwa ni mtu mzima na mwengine mtoto wa miaka isiyozidi 14 wakiwa wamepiga magoti mbele ya makaburi yaliyojengewa kwa mtindo wa kufanana baada ya kuyasafishia na walionekana walifika pale kwa muda mrefu sana na kulikuwa na hadithi ndefu aliyokuwa anaisimulia yule Mkubwa kwa yule mtoto huku akimuonesha onesha makaburi yale.

"Hadithi hii imeniuma sana baba Cj4 aaah!! Mungu wasamehe ndugu zangu wote, kwa hiyo nini kilitokea sasa baada ya baba kujua kumbe mama alikuwa Ninja mara aliporudiwa fahamu?"
aliuliza yule mtoto.
"Baada ya babaako Kamishna Shebby kuzinduka ilikuwa tayari kashachelewa mara baada ya bibi ako kuzidiwa ghafra kwa presha iliyomshuka pindi alipogundua kumbe mumewe babu yako Mr X alikuwa amemtumia mamaako zaidi ya alivyojua yeye, kwani bibiako alijua kama mumewe anamtumia Asha lakini si kwa mauaji bali ni kumueka tu karibu ili amfiche kama yeye ni mtu m baya dhidi ya babaake ambae ndie babu yako mzazi Hussein.
Ilibidi sasa mamaako amuwahi kakaake ambae pia ni babaako pale chini pindi alipozinduka lakini nae alichelewa hata mimi pia nilichelewa kumuwahi kutokana na kumuweka chini babu yako Hussein aliyekuwa kashakufa na kumuwahi bibi yako Zai kwa kumpa msaada bila kujua nyuma yangu Shebby amezinduka na kwa kuchanganyikiwa kwa kile akionacho alishindwa kujizuia na kuiokota tena bastora yake na hapo nilisikia tu mlio wa risasi sambamba na kelele za mamaako Asha na nilipogeuka hakuwa Asha aliyepigwa risasi bali ni Shebby mwenyewe alijipasua kichwa na kusambaratika ubongo palepale.."
alipofika hapa kidogo alisita na kwa mara ya kwanza Cj4 chozi lilimdondoka hadhalani toka afuzu mafunzo ya Ukomando Cuba zaidi ya miaka 20 iliyopita.
"Mwanangu Hussein, sikumbuki lini ilikuwa mara ya mwisho kutoa chozi kwani hata kipindi yale yote yanatokea sikudondosha chozi. Zaidi nilisimama kiume kukabiliana nayo kwani ilibidi nimuache bibiako Zainab niliyeona wazi kuwa yupo katika hatua za kumalizikia baada ya presha kushuka sana na kushuhudia mwanae akijimaliza na hapo ilibidi niluke kishujaa kumuwahi mamaako Asha ambae nae alikuwa anataka ajimalize kwa bastora ile ile aliyojimalizia babaako.
Jinsi nilivyoruka sikuwahi kufundishwa wala kudhani kama nina uwezo wa kuluka vile, lakini ndivyo ilivyokuwa niliweza kumuwahi mamaako na kumuokoa mbele ya kifo alichokuwa anajitengenezea mwenyewe na nilichokifanya niliubetua mshipa wake mdogo wa fahamu uliokuwa nyuma ya sikio na kumzimisha.
Hapo ndipo nilipoweza kuwasiliana na mkuu wangu wa majeshi na kumpa taarifa zote kabla sijaondoka eneo lile huku nikiwa nimem beba mamaako ambae sikujua kumbe tayari tumboni ulikuwapo wewe."
Story ya Cj4 ilimuuma sana yule mtoto lakini alionesha alikuwa jasiri sana na mwenye moyo wa uvumilivu kwani alikuwa anatokwa machozi lakini aliweza kusikiliza kwa umakini na kuuliza maswali muhimu.
"Kwa hiyo baba Cj ilikuwaje sasa ulipoondoka na mama hasa pale fahamu zilipomrudia?"
"Mwanangu Hussein, mamaako kwanza alichelewa sana kupata fahamu hadi nilianza kuhofu lakini alipopata fahamu nilikuwa nae kwenye kambi maalum ya kijeshi ambapo ndipo nilipoelekea mara baada ya kutoka pale kwenye ile nyumba.
Niliongea nae na kumpanga kwa maneno ya kishujaa na mbinu maalum ambazo utakutana nazo pindi utapokuwa kama mimi hapo baadae, nikikutazama naona wazi utakuwa zaidi ya mimi.
Basi mamaako japo ilikuwa ngumu kuelewa lakini tuliweza kumdhibiti ndani ya kambi ile iliyokuwa haijulikani kabisa na watu wengi hadi kwa wanajeshi wengi wenye vyeo vya chini.
Japo alikuwa ni wa kuzimia mara kwa mara lakini hatimae aliweza kutulia taratibu kadri siku zilivyozidi kwenda hadi tulipomgundua kuwa alikuwa na mima baada ya kumfanyia vipimo vya utrasound pindi tulipoona tumbo linazidi kuwa kubwa na kugundua uwepo wako.
Sikuweza kuhudhulia mazishi ya babaako, bibiako, babu ako na babu ako mlezi wa babaako Mr X ambao wote walizikwa kwa pamoja hapa kama unavyoona makaburi yao yalivyofatana kwa sababu ya kuwa karibu na mamaako na kumliwaza japo niliweza kuyashuhudia baadae kupitia rekodi kamili ya ule mkanda tulioutazama tena sote jana usiku.
Serikali ndio waliolizima suala lile baada ya taarifa za ripoti yangu kamili kufika kwa muheshiwa Rais."
"sawa baba, sasa mama nae alikufa kufa vipi?"
"Mamaako kilichomuua ni sumu iliyokuwa mwilini mwake iliyokuwa ikimtafuna muda mrefu.
Sumu hiyo ilitokana na kile kisu cha kininja alichochomwa na Tyga siku ile usiku... Kwa hiyo siku aliyokuwa anajifungua ndio siku aliyofariki pindi alipokuwa anakupush kwa nguvu kumbe alikuwa anajimalizia baada ya sumu kushambulia sana maeneo ya uti wa mgongo na mbavu.
Mamaako alikufa kishujaa kwa kuwa aliweza kuvumilia hadi akafanikisha kumzaa Shujaa mpya ambae ni wewe mwanangu Hussein niliyeamua kukupa jina hili la babu yako ambae pia alikufa mikononi mwangu lakini kupitia wewe nikaona kama amezaliwa tena mikononi mwangu.
Na hivyo ndivyo ilivyokuwa Hussein wewe ulikuwa chini ya usimamizi wangu wala hukuwa na ndugu yeyote zaidi yangu.... Simama sasa nataka nikuulize nami maswali yangu."
aliongea Cj4 na kusimama sambamba na mtoto Hussein ambae ndie alikuwa mtoto halali wa Marehemu Dokta Asha au Lady Ninja na Marehemu Kamishna Shebby.

"Ulivyoelewa historia yako asili yake na matatizo yote chanzo ni nini?"
"MWANAMKE"
alijibu Hussein bila hata kusita.
"Vizuri na je, ulivyosoma historia ya ushujaa wa Samson dhidi ya Wafiristi hadi siri zake zikabainika na kukamatwa kupata mateso makali hadi alipoomba nguvu kumrudia na kufa pamoja na mamia ya watu je nae kilichomponza hasa chanzo ni nini?"
"MWANAMKE"
alijibu tena Hussein.
"Vizuri sana, na vipi kuhusu asili ya dhambi ya baba etu Adam kusariti ahadi aliyopewa na mungu na kushawishika kula lile tunda, kihistoria ulivyosoma shetani alimtumia nani kumshawishi kiurahisi Adam."
"MWANAMKE"
"Ni kweli mwanangu Hussein na hivi unajua kwanini Wanawake ni wengi kuliko Wanaume?"
"hapana baba Cj4, sijui."
"Basi ni kwasababu mtu wa kwanza kufa alikuwa ni mwanaume na alikuwa mtoto wa Adam aliyepigana na ndugu yake sababu ikiwa ni mwanamke. na hapo ndipo uwiano wa namba ulipozidi.
Kwa hiyo kwa uelewa wa kawaida kabisa umeona kumbe hata mtu wa kwanza kufa chanzo ilikuwa nini?"
"MWANAMKE baba Mh!!"
"Huo ndio ukweli ambao alikuwa anamaanisha babu yako wala si uchizi.. hivi unajua chanzo cha mimi kukuhadithia hadithi ya maisha ya asili ulipotokea chanzo ni nini?"
"Ndio baba chanzo ni Halima mtoto wa baba Kanali Suma mara baada ya kusababisha nimepigana na kumuumiza Amos mtoto wa Luten Frenk."
alijibu kwa upole Hussein.
"sawa kwa hiyo Halima ni nani?"
"ni mwanamke baba"
"kwa hiyo chanzo cha kukuhadithia ukweli huu na kukuonesha video ya mazishi mpaka sasa tupo hapa chanzo ni.....?"
"MWANAMKE"
"Ndio, sasa umejifunza nini hapa."
"Naapa baba Cj4 mbele za Mungu, mbele ya makabuli haya ya ndugu zangu kuwa nitakuwa makini makini sana na Wanawake kamwe sintokuwa mzembe wa kuwaaamini kwa asilimia zote kwa kuwa Wanamke wana ulemavu wa upeo na udhaifu wa asili."
aliapa kwa nguvu na sauti ya kumaanisha Hussein.
"sawa unadhani kwanini umeapa hivyo? hivi kiapo chako uko sahihi kweli?"
"Naamini baba Cj4 nipo sahihi, na ili nikuaminishe nipo sahihi kusema kuwa 'wanawake wana ulemavu wa upeo na udhaifu wa asili' nataka nikuulize swali."
"Uliza tu mwanangu."
"Je ni dini gani kati ya ukristo na uislam pamoja na matawi yake inasema Mungu alituma manabii na mitume wanawake kwaajili ya kuwaogoza na kuwaokoa watu?"
"Mh!! HAKUNA mwanangu wala sijawahi kusikia."
"unadhani Mungu ana upendeleo kwa wanaume?"
"Hapana, ila ninachojua Mungu alimuumba mwanamke kwa sababu ya kumtuliza na kumliwaza mwanaume."
"kwa hiyo hapo baba ndipo kwenye 'ulemavu na dhaifu wa asili ya mwanamke' japo wenyewe hawataki na naamini mwanamke asiyekubali kuwa dhaifu mbele ya mwanaume naamini ni muuaji na mwanamke asiyekubali kuwa ana ulemavu wa upeo basi atajiamulia vitu kama bibi Zai na faida yake ataiona mwishoni na atakuwa muuaji tu."
aliongea kwa uchungu Hussein na Cj4 alishangaa kuona maneno ya Hussein mtoto yanashabiana na nukuu za marehemu Hussein mkubwa na kuamua amkumbatie kwa nguvu pindi alipoona anazidi kuongea huku akilia na kumsihi sasa inatosha waondoke.
"Basi mwanangu basi mwanangu tuondoke sasa ila zingatia haya na ufanye utafiti na uwaokoe wanaume wengi wasiojua hili pamoja na kuwaelimisha wanawake wakubali udhaifu wao ili matatizo zaidi yasiendelee kutokea na kabla hujaongea nao wala kuwasimulia waulize kwanza je, WANAWAKE NI WAUAJI..!? sikiliza na uhesabu majibu yao kisha uwasimulie story hii na ikiwezekana uiandike kabisa na uitolee Kitabu ili wengi wakipate na mara utapomaliza kuwasimulia/kuandika waulize tena kwa mshangao swali lilelile la mwanzo kuwa WANAWAKE NI WAUAJI..!? uone tena majibu yao."

_________________________
____________
* MWISHO *
___________
__________________________

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom