SIMULIZI: Nilipanga Nyumba Moja na Majini

SIMULIZI: Nilipanga Nyumba Moja na Majini

Hapa ni Mungu alimsaidia mpaka kufika kuyafukuza hayo majini, tena alivumilia because Mungu alitaka kudhihirisha uwepo wake. Katika Jina ya Yesu Kristu hakuna linaloshindikana.
 
Hapa ni Mungu alimsaidia mpaka kufika kuyafukuza hayo majini, tena alivumilia because Mungu alitaka kudhihirisha uwepo wake. Katika Jina ya Yesu Kristu hakuna linaloshindikana.

Yap,katika jina la Yesu,hakuna linaloshindikana!
 

“Kama kuna watu hawayajui haya nitakayoyaongea basi nawataka kuanzia sasa wajue kwamba, hapa Dar kuna mambo makubwa sana ambayo ukisimuliwa unaweza kusema si ya kweli, lakini wale wanaoyapata hayo mambo wanajua na wewe usiombe yakukute hata siku moja,” ndivyo alivyoanza kusimulia Bw. Humuli Samaki (43), mkazi wa Buguruni (kwa sasa) ambaye alipata mkasa mzito akidai alipanga nyumba moja na majini Magomeni, Dar es Salaam.

SASA ENDELEA MWENYEWE… “Si zamani sana mkasa huu uliponitokea, ilikuwa
mwaka 2009 tu, kwa hiyo naweza kusema ni
juzijuzi tu. Kwa sasa naishi hapa Buguruni, baada
ya kuhama kutoka Magomeni ambako nilipata
mkasa mzito na wa kuogopesha. Nilipanga

nyumba moja na majini.” Mwaka huo (2009), awali nilikuwa nikiishi
Mwanyamala Mwinjuma, jirani kabisa na Makao
Makuu ya Bendi ya TOT, hata Kapteni John Komba
nilizoeana naye kwa kuonanaonana naye pale

CCM-Mwinjuma, ingawa jina langu najua hakuwa
akilifahamu. Ile nyumba niliyokuwa nikiishi pale
Mwananyamala iliingia kwenye mgogoro wa

kifamilia na kufikishana mahakamani kwa ajili ya
kugawana mirathi. Hukumu ilipotoka ikaamriwa

iuzwe kisha ndugu wagawane fedha. Kwa maana hiyo, mimi na wapangaji wenzangu
watano, tulipewa notisi ya kuhama baada ya
mteja kupatikana. Huyu mteja anaitwa Masawe
anafanya kazi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

lakini sijui ofisi za wapi. Ilibidi mimi niangalie mwelekeo mwingine,
niliamua nibadili upepo, nikaishi Magomeni. Kwa
wakati huo nilikuwa sina familia. Sina mke wala
mtoto hata wa kusingiziwa, kwa hiyo nilikuwa
naishi peke yangu. Ni mwaka jana ndiyo nimeoa

mke wangu huyu, anaitwa Hadija Mashada. Rafiki yangu mmoja anayeitwa Mohamed Kombe
alinipa namba ya dalali kwani yeye anaishi
Magomeni hata sasa. Nilimpigia simu dalali wake,
anayeitwa Yusuf Mwamba, akaniita Magomeni
pale kwenye nyumba wanayosema aliwahi kuishi

Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere. Nilikwenda mpaka pale, nilimkuta amesimama nje
ya nyumba hiyo, tukasalimiana, akaniuliza nataka

nyumba yenye sifa gani, nikamweleza. Niliwajibu mimi mwenyewe sijui, lakini sikumaindi
sana. Akaja mama mmoja aliyesema anaishi
nyumba ya pili, akasalimia na kuniuliza maswali.

“Hamjambo wanangu?”
Tuliitikia wote, akauliza nani anahamia pale kati
ya sisi wote, tulikuwa watano mbali na dereva. “Ni mimi.”
“Ooo, mzima baba?”
“Mimi mzima mama.”
“Unaitwa nani?”
“Humuli Samaki.”

“Unahamia peke yako au uko na mke na watoto?”
“Peke yangu mama.”
“Humuli Samaki ni mwenyeji wa wapi?”
“Usukumani.”
“Haya, naamini uliaga wakati unaondoka
nyumbani.” “Hilo lilikuwa la kwanza mama.”

“Haya, kila la kheri.” Tuliendelea na kazi ya kuingiza vyombo ndani
hadi tukamaliza. Wale wenye gari wakaondoka,
nikabaki mimi peke yangu.

Nilijiwekea malengo kwamba, nihakikishe
naweka sawa kila kitu ili kesho yake nisiwe na

kazi hiyo zaidi ya kwenda kazini. Niliifanya kazi kwa muda wa saa tatu, mpaka kwenye saa saba
na nusu usiku nikamaliza. Nilibadili nguo, nikavaa taulo na kwenda kuoga.
Nilikuta bafu limetoka kutumika kama dakika
kumi nyuma, sikushangaa kwani si kuna
wapangaji wengine ambao tulitakuwa tunatumia

bafu moja. Usiku kabla ya kuzima taa, nilizima taa, nikapanda
kitandani. Kabla sijapata usingizi, niliwasikia
wenzangu wakicheka sana na kuongea huku
wameweka muziki. Lakini ule muziki haukuwa

wa kiarabu, kizungu wala kiswahili. Hata maongezo yao, mimi nilisikia sauti tu lakini
kusema walikuwa wanatumia lugha gani si rahisi.
Kuna wakati kama walikuwa wakiongea kihindi,
pia niliwasikia kama wanaongea kiarabu, nikajua

ni watu wa namna hiyo. Lakini sikulala mpaka nikampigia simu dalali
kumuuliza kama wale wapangaji wenzangu ni
weupe au waswahili kama mimi, akasema hata
yeye hajui kwani hakuwahi kuwaona hata siku

moja. Basi, nililala. Asubuhi niliamka nikiwa nimechoka
sana. Wakati nakwenda bafuni kuoga niligundua
ni mimi peke yangu ndiye niliyekuwa
nimetangulia kuamka, kwani bafuni hakukuwa

na maji yaliyomwagika kwa muda huo. Baada ya kuoga nilirudi chumbani kwangu
kujiandaa kwenda kazini. Wakati najiandaa,
nilisikia mlango ukifunguliwa, nikajua ni

wenzangu wanakwenda kuoga au chooni kama
ilivyo kawaida kwa wanadamu wakiamka
asubuhi. Niliamua kutumia nafasi hiyo kuwatambua.
Nilivizia pale niliposikia mlio wa maji bafuni na

mimi nikatoka kwenda kupiga mswaki kwa mara
ya pili. Sehemu niliyosimama, mtu akitoka bafuni
kwenda ndani ilikuwa lazima nimuone kwani

ilikuwa kiasi cha kugeuka tu. Lakini cha kushangaza, nilikuwa sisikii maji
kumwagika, nikageuka na kuona mlango wa
bafuni upo wazi. Mbali na mlango kuwa wazi, pia
chini nikaona alama za kandambili nne zikiwa
zimekanyaga, nikajua wametoka.

“Lakini wamepitaje hapa?” nilijiuliza. Nilirudi ndani, mlangoni kwao nilikuta kandambili
pea mbili zikiwa bado na majimaji kwa mbali,
jambo hili lilinifanya nijiulize sana.
Nilijipa ujasiri na kuamua kuchungulia ndani ya
chumba hicho kwa kutumia nafasi ya katikati ya

mlango ambapo niliweza kuona hadi kitanda lakini sikumwona mtu mwingine. Niliingia kwangu, nikaweka mswaki, nikavaa
vizuri na kuondoka zangu. Nilitegemea
wenzangu nimewaacha ndani, kwani nilipofika
mlangoni nilikuta umefunguliwa na upo wazi.
Nilirudi ndani hadi kwenye mlango wao.

“Wa ndugu,” niliita kwa sauti. “Jamani wa ndugu.” Ukimya ndiyo ulinifanya nibaini walishaondoka.
Kwani kulikuwa kimya sana na kandambili

zilikuwa pembeni ya mlango si pale pa kwanza. Nilifunga mlango mkubwa nikaondoka, mbele
nilimwona yule mama aliyekuja usiku kuniuliza
maswali. Alikuwa amesimama nje ya nyumba
yake, aliponiona akashutuka na kuita majina
mawili ya watu. Wakatoka watoto wake wawili, ni

mabinti wenye miaka kama kumi na nane na ishirini na mbili hivi.

“Hujambo kijana?” yule mama alinisalimia kwa
furaha.
“Sijambo mama, shikamoo.”
“Marhaba.” Kisha akawaambia kitu wale watoto
wake nao wakanikazia macho. “Mama umewaona majirani zangu hapa?”
“Majirani zako akina nani?”
“Wapangaji wenzangu.”

“Kijana, kua uyaone ya dunia. We si umeshakua,
utayaona ya dunia.”
Kauli hiyo iliniogopesha sana, nikashtuka na kumuuliza mama.
“Mama una maana gani?”
“Sisi hatutaki umbeya kijana.”
“We si umeambiwa utayaona kwa hiyo subiri tu,”

alidakia binti yake mkubwa. Miguu ilitetemeka, mwili uliisha nguvu, nikajikuta
nataka kukaa, lakini sikuweza. Nilichoamua ni
kuondoka huku nampigia simu yule dalali.

“Vipi hujambo bwana?”
“Mimi sijambo.”
“Za makazi mapya.” “Si nzuri bwana.”
“Kwa nini tena?”
“Sielewielewi.”
“Kivipi?”
“Kuna mambo kama si ya kawaida.”
“Yapi hayo?”
 
ILIPOISHIA :Nilichukua kama saa moja kutoka kazini hadi kufika nyumbani. Nje nilikuta mfuko wa rambo mweusi, ndani yake ulionekana kuwa na kitu kwani ulikuwa umetuna sana. Niliinama kuipekenyua ili nijue ndani kulikuwa na nini, nilishangaa kuona ni vipande vya nyama za kuchoma tena vilikuwa na moto.


"Kha! Atakuwa nani ameweka?" nilijiuliza mwenyewe, nikauacha palepale, mimi nikapanda ngazi za kuingia ndani. Mlango ulikuwa wazi hali iliyoashiria kwamba, wenzangu walisharudi. Nilisukuma mlango, nikaingia. Nilikutana na harufu ya pafyumu, nikahisi walikuwa wakijiandaa kutoka. "Jamani za leo?" nilisalimia kwa sauti ya juu licha ya kwamba, mlango wao ulikuwa umefungwa, hakuna aliyeniitikia, hilo sikulijali sana kwani niliamini kwa kuwa walikuwa ndani, isingekuwa rahisi wasikie salamu yangu.



Niliingia sebuleni kwangu, kisha nikaenda chumbani, kuna kitu kilinishangaza, nikasimama kwa mshtuko. Nilikuta sehemu nilipoweka kiberiti asubuhi siyo, nilikiacha juu ya meza, nikakikuta juu ya kitanda. Niliacha kioo na kitana juu ya kitanda, lakini nikavikuta kwenye stuli, niliguna!

Nilikishika kioo cha kukiangalia kwa umakini kama kina mabadiliko yoyote, lakini sikuona, nikashika kitana. Nilipokigaua sana pia sikuona kitu cha tofauti, nikaamua kuchania, nikahisi kuguswa na kitu kama nywele ndefu kama za mtu aliyefuga. Nilikiweka kitana juu usawa wa dirishani, nikaona nywelenywele nene, nyeusi, mwili wote ukasisimka.


Ninavyojua mimi, mwanamke mwenye nywele nyingi akichania kitana, ndiyo huacha nywele, sasa mimi nilikuwa na nywele fupi sana zisingeweza kuacha nywele ndefu kwenye kitana.


"Mh! Hapa kuna kinachoendelea," nilisema moyoni huku nikikaa. Nilishtuka zaidi kuona soksi zikiwa kwenye msumari nyuma ya mlango wakati niliacha chini.


"Huyu ni nani?" niliuliza kwa sauti ya ukali.
Ghafla nikasikia kicheko kutoka chumbani kwa wale wenzangu.
Nilikaa kwenye kochi, nikaanza kuangalia sehemu mbalimbali za mle ndani ambazo niliamini naweza kuona mabadiliko mengine mbali na yale ambayo nilishayaona, lakini sikubahatika.


Nilitoka, nikaenda sebuleni ambako nako nilianza kuangalia kila kona ya sebule. Nilishangaa kuona glasi ya maji ya kunywa ambayo niliitumia asubuhi kisha nikaacha maji yamejaa, ikiwa haina hata tone la maji mbaya zaidi, iliwekwa juu ya kabati ambapo mimi niliiweka kwenye meza ya katikati ya sebule.


"Mh! Hii kali sasa," nilijikuta nikisema kwa sauti, mara nikasikia kicheko tena kutokea upande wa pili kule kwa wenzangu. Sasa nikaanza kama kuhisi kitu kuhusu watu hao. Ni kwanini kila nilipoongea kwa sauti ndipo na wao waliangua kicheko?
Niliamua kujaribu tena, nikasema kwa sauti:


"Nitakuja kuua mtu, kweli tena." Nikasikia kicheko tena, safari hii kilidumu kwa muda.
Moyoni nikasema naanza kufanyia kazi uhusiano wa maneno yangu na vicheko vya wale majirani. Nilitoka kurudi chumbani, wakati napita kwenye korido, nilisimama jirani na mlango wao. Walikuwa wakiongea, lakini niliposimama mimi, kukawa kimya ghafla kama hakuna watu.


Nilipozama chumbani, nyuma wakaanza kuongea tena. Sikufunga mlango ili niweze kusikia wanachokiongea, lakini jamani kwa kusema ule ukweli wa Mungu, sikujua walikuwa wakitumia lugha gani katika kuwasiliana hata pale nilipojitahidi kutega masikio kwa umakini wa hali ya juu sana.


Kuna wakati utadhani wanatumia sana neno dotikom, lakini ukisema usikilize zaidi unasikia wakisema sana kotoko au kiburate, wakati mwingine sauti ya kike ilisema kaunto, ya kiume ikarudia hivyohivyo, kaunto.


Nia yangu kubwa ilikuwa kuwaona kwa sura na kufahamu kama ni ngozi nyeusi au nyeupe. Hilo peke yake lingenipa mwanga ni watu wa aina gani naishi nao pale ndani ya nyumba.
Nilisikia mlango wa chumbani kwao ukifunguliwa na mimi nikatoka haraka sana, cha ajabu sikuona mtu akitoka lakini mlangoni kulikuwa na kandambili pea moja tu wakati zilikuwa pea mbili.


Hilo lilimaanisha kwamba, mmoja wao alitoka kwenda chooni, nilichofanya ni kuamua kusimama katikati ya mlango wangu ili huyo aliyekwenda chooni akirudi nimuone. Ni kweli mmoja wao alikwenda chooni kwani nilisikia mlio wa maji.


Nilijiahidi kusimama mlangoni kwangu kumsubiria. Kwa ramani ya nyumba ile ilivyo, asingeweza kutoka chooni bila mimi kumwona hata kama angekuwa anataka kutoka kwenda nje au uani.


Mlio wa maji ulikosa kusikika, nikawa natumbulia macho kule huku moyoni nikisema:
"Leo ndiyo leo, asemaye kesho mwongo, hata afanyaje, hawezi kunichenga hapa hata kidogo," nilisema moyoni, ingawa wakati huo mapigo ya moyo yalikuwa yakinienda kwa kasi.


Nilipoanza kuhisi muda unakwenda na hakuna mtu aliyetoka, nikampa dakika tatu kwamba lazima atakuwa anavaa ndiyo maana anachelewa:


"Labda alikuwa anajisaidia haja kubwa, maana wengine huwa wanavua nguo zote, lakini mimi nipo, siendi kokote," nilisema moyoni nikiwa bado nimesimama mlangoni kwangu.
Baaad ya muda, nikasikia watu wakiongea chumbani kwao, nikashtuka, nilijikuta nikisema:
"Haa!"


Haraka sana nilitupa macho mlangoni kuangalia kandambili, nikazikuta pea mbili, nikashangaa:


"Ina maana amenipita hapahapa au? Haiwezekani, asingeweza kunipita hata kama ingekuwaje?" niliwaza. Nilitoka kuelekea chooni, nikakuta mlango uko wazi, nikachungulia ndani, hakukuwa na mtu, nikanyoosha mikoni, nikarudi ndani.
Nilifikia kwenye kochi sebuleni, nikahema kwa nguvu kwani niliamini nimo ndani ya miujiza mikubwa ya ndani ya nyumba ile.


"Hivi ni kwanini dalali alinidanganya hivi?" nilijiuliza mwenyewe nikiamini kwamba, dalali aliyenipangisha nyumba ile alijua mchezo mzima ila alitaka kupata fedha tu ndiyo maana alinipangisha bila kunipa tahadhari.


Nilitoka sebuleni, nikaenda chumbani, kitandani nikakuta ‘toilet paper' ikiwa imekatwa sehemu. Mimi niliicha pembeni ya dirisha, lakini ikaonesha kuna mtu aliichukua na kunyofoa kidogo kisha badala ya kuirudishia palepale, yeye aliiacha kitandani.


Mbali na ‘toilet paper' pia kuna kikopo chenye vijiti vyenye pamba za masikio kilikuwa kwenye stuli jirani na kitanda, lakini kwa muda huo kilikuwa kimeanguka chini halafu vijiti vimebaki kama vitatu tu kwa maana kwamba, aliyeingia kuchukua ‘toilet paper' ndiyo huyohuyo aliyechota vijiti vya pamba.

Nilianza kuhisi kuwa sikuwa kwenye nyumba salama, lakini kwa uthibitisho upi?


Usikose sehemu ya 03 leo jioni................
 
Back
Top Bottom