SIMULIZI: Nilipanga Nyumba Moja na Majini

SIMULIZI: Nilipanga Nyumba Moja na Majini

"Kama kuna watu hawayajui haya nitakayoyaongea basi nawataka kuanzia sasa wajue kwamba, hapa Dar kuna mambo makubwa sana ambayo ukisimuliwa unaweza kusema si ya kweli, lakini wale wanaoyapata hayo mambo wanajua na wewe usiombe yakukute hata siku moja," ndivyo alivyoanza kusimulia Bw. Humuli Samaki (43), mkazi wa Buguruni (kwa sasa) ambaye alipata mkasa mzito akidai alipanga nyumba moja na majini Magomeni, Dar es Salaam.

SASA ENDELEA MWENYEWE


"Si zamani sana mkasa huu uliponitokea, ilikuwa mwaka 2009 tu, kwa hiyo naweza kusema ni juzijuzi tu. Kwa sasa naishi hapa Buguruni, baada ya kuhama kutoka Magomeni ambako nilipata mkasa mzito na wa kuogopesha. Nilipanga nyumba moja na majini."

Mwaka huo (2009), awali nilikuwa nikiishi Mwanyamala Mwinjuma, jirani kabisa na Makao Makuu ya Bendi ya TOT, hata Kapteni John Komba nilizoeana naye kwa kuonanaonana naye pale CCM-Mwinjuma, ingawa jina langu najua hakuwa akilifahamu.

Ile nyumba niliyokuwa nikiishi pale Mwananyamala iliingia kwenye mgogoro wa kifamilia na kufikishana mahakamani kwa ajili ya kugawana mirathi. Hukumu ilipotoka ikaamriwa iuzwe kisha ndugu wagawane fedha.

Kwa maana hiyo, mimi na wapangaji wenzangu watano, tulipewa notisi ya kuhama baada ya mteja kupatikana. Huyu mteja anaitwa Masawe anafanya kazi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) lakini sijui ofisi za wapi.

Ilibidi mimi niangalie mwelekeo mwingine, niliamua nibadili upepo, nikaishi Magomeni. Kwa wakati huo nilikuwa sina familia. Sina mke wala mtoto hata wa kusingiziwa, kwa hiyo nilikuwa naishi peke yangu. Ni mwaka jana ndiyo nimeoa mke wangu huyu, anaitwa Hadija Mashada.

Rafiki yangu mmoja anayeitwa Mohamed Kombe alinipa namba ya dalali kwani yeye anaishi Magomeni hata sasa. Nilimpigia simu dalali wake, anayeitwa Yusuf Mwamba, akaniita Magomeni pale kwenye nyumba wanayosema aliwahi kuishi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Nilikwenda mpaka pale, nilimkuta amesimama nje ya nyumba hiyo, tukasalimiana, akaniuliza nataka nyumba yenye sifa gani, nikamweleza.

Niliwajibu mimi mwenyewe sijui, lakini sikumaindi sana. Akaja mama mmoja aliyesema anaishi nyumba ya pili, akasalimia na kuniuliza maswali.
"Hamjambo wanangu?"
Tuliitikia wote, akauliza nani anahamia pale kati ya sisi wote, tulikuwa watano mbali na dereva.
"Ni mimi."
"Ooo, mzima baba?"
"Mimi mzima mama."
"Unaitwa nani?"
"Humuli Samaki."
"Unahamia peke yako au uko na mke na watoto?"
"Peke yangu mama."
"Humuli Samaki ni mwenyeji wa wapi?"

"Usukumani."
"Haya, naamini uliaga wakati unaondoka nyumbani."
"Hilo lilikuwa la kwanza mama."
"Haya, kila la kheri."

Tuliendelea na kazi ya kuingiza vyombo ndani hadi tukamaliza. Wale wenye gari wakaondoka, nikabaki mimi peke yangu.
Nilijiwekea malengo kwamba, nihakikishe naweka sawa kila kitu ili kesho yake nisiwe na kazi hiyo zaidi ya kwenda kazini. Niliifanya kazi kwa muda wa saa tatu, mpaka kwenye saa saba na nusu usiku nikamaliza.

Nilibadili nguo, nikavaa taulo na kwenda kuoga. Nilikuta bafu limetoka kutumika kama dakika kumi nyuma, sikushangaa kwani si kuna wapangaji wengine ambao tulitakuwa tunatumia bafu moja.

Usiku kabla ya kuzima taa, nilizima taa, nikapanda kitandani. Kabla sijapata usingizi, niliwasikia wenzangu wakicheka sana na kuongea huku wameweka muziki. Lakini ule muziki haukuwa wa kiarabu, kizungu wala kiswahili.

Hata maongezo yao, mimi nilisikia sauti tu lakini kusema walikuwa wanatumia lugha gani si rahisi. Kuna wakati kama walikuwa wakiongea kihindi, pia niliwasikia kama wanaongea kiarabu, nikajua ni watu wa namna hiyo.

Lakini sikulala mpaka nikampigia simu dalali kumuuliza kama wale wapangaji wenzangu ni weupe au waswahili kama mimi, akasema hata yeye hajui kwani hakuwahi kuwaona hata siku moja.

Basi, nililala. Asubuhi niliamka nikiwa nimechoka sana. Wakati nakwenda bafuni kuoga niligundua ni mimi peke yangu ndiye niliyekuwa nimetangulia kuamka, kwani bafuni hakukuwa na maji yaliyomwagika kwa muda huo.

Baada ya kuoga nilirudi chumbani kwangu kujiandaa kwenda kazini. Wakati najiandaa, nilisikia mlango ukifunguliwa, nikajua ni wenzangu wanakwenda kuoga au chooni kama ilivyo kawaida kwa wanadamu wakiamka asubuhi.

Niliamua kutumia nafasi hiyo kuwatambua. Nilivizia pale niliposikia mlio wa maji bafuni na mimi nikatoka kwenda kupiga mswaki kwa mara ya pili. Sehemu niliyosimama, mtu akitoka bafuni kwenda ndani ilikuwa lazima nimuone kwani ilikuwa kiasi cha kugeuka tu.

Lakini cha kushangaza, nilikuwa sisikii maji kumwagika, nikageuka na kuona mlango wa bafuni upo wazi. Mbali na mlango kuwa wazi, pia chini nikaona alama za kandambili nne zikiwa zimekanyaga, nikajua wametoka.
"Lakini wamepitaje hapa?" nilijiuliza.

Nilirudi ndani, mlangoni kwao nilikuta kandambili pea mbili zikiwa bado na majimaji kwa mbali, jambo hili lilinifanya nijiulize sana.
Nilijipa ujasiri na kuamua kuchungulia ndani ya chumba hicho kwa kutumia nafasi ya katikati ya mlango ambapo niliweza kuona hadi kitanda lakini sikumwona mtu mwingine.

Niliingia kwangu, nikaweka mswaki, nikavaa vizuri na kuondoka zangu. Nilitegemea wenzangu nimewaacha ndani, kwani nilipofika mlangoni nilikuta umefunguliwa na upo wazi. Nilirudi ndani hadi kwenye mlango wao.
"Wa ndugu," niliita kwa sauti.
"Jamani wa ndugu."

Ukimya ndiyo ulinifanya nibaini walishaondoka. Kwani kulikuwa kimya sana na kandambili zilikuwa pembeni ya mlango si pale pa kwanza.

Nilifunga mlango mkubwa nikaondoka, mbele nilimwona yule mama aliyekuja usiku kuniuliza maswali. Alikuwa amesimama nje ya nyumba yake, aliponiona akashutuka na kuita majina mawili ya watu. Wakatoka watoto wake wawili, ni mabinti wenye miaka kama kumi na nane na ishirini na mbili hivi.
"Hujambo kijana?" yule mama alinisalimia kwa furaha.
"Sijambo mama, shikamoo."
"Marhaba." Kisha akawaambia kitu wale watoto wake nao wakanikazia macho.
"Mama umewaona majirani zangu hapa?"
"Majirani zako akina nani?"
"Wapangaji wenzangu."
"Kijana, kua uyaone ya dunia. We si umeshakua, utayaona ya dunia."
Kauli hiyo iliniogopesha sana, nikashtuka na kumuuliza mama.
"Mama una maana gani?"
"Sisi hatutaki umbeya kijana."
"We si umeambiwa utayaona kwa hiyo subiri tu," alidakia binti yake mkubwa.

Miguu ilitetemeka, mwili uliisha nguvu, nikajikuta nataka kukaa, lakini sikuweza. Nilichoamua ni kuondoka huku nampigia simu yule dalali.
"Vipi hujambo bwana?"
"Mimi sijambo."
"Za makazi mapya."
"Si nzuri bwana."
"Kwa nini tena?"
"Sielewielewi."
"Kivipi?"
"Kuna mambo kama si ya kawaida."
"Yapi hayo?"


Itaendelea chini; hapa - SEHEMU YA TATU
Duh hiz story sio za kusoma usiku hiv
 
Nilipanga Nyumba Moja na Majini -MWISHO

"Lini umeniambia?"
"Wewe sijawahi kukupigia simu kukwambia? Tena ukasema kama vipi nihame lakini sitarudishiwa kodi ya nyumba na mimi nikakujibu niko tayari kwa hilo&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];"
"Sasa wewe ulikuwa ukiteswa kwa lipi, weka ushahidi hapa kwamba ulikuwa ukiteseka sana."
"Sina haja, mimi ndiyo najua."

Wakati tukijibizana hivyo, wale waombaji walikuja juu kwa kuomba. Walipaza sauti sana wakisema moto uteketeze kila hila na jambo lolote ambalo linakwenda kinyume na mimi ndani ya nyumba ile.

Ghafla, nilimwona yule dalali akianza kuyumba kama mlenvi, alikwenda kulia, kushoto, akasimama, akawa

kama ananijia mimi, nikamkwepa, akaenda kushoto na kuanguka puu!
Kwangu ilikuwa ni furaha kwani nilipata picha kwamba, yule dalali alikuwa anahusika moja kwa moja na matukio yote ya ajabu mle ndani. Niliwaita wale watu wanaofanya maombi na kuwataka washuhudie ambapo walipomwangalia dalali waliongeza mkazo wa maombi yao.

Mwisho, dalali aliamka akiwa kama hana ufahamu, alikalishwa chini na kuhojiwa ambapo alisema mambo ya ajabu sana. Alisema mwanaume aliyekuwa akiishi ndani ya vyumba vile ni yeye na mkewe, akasema mkewe ni jini kwa asilimia mia moja ila yeye si jini bali mkewe alimfanya awe na uwezo wa kutoonekana wala kujulikana na mtu.

Alipoulizwa kama alikuwa anapata faida yoyote kwa kitendo cha kugeuka kuwa jini alijibu hakuna ila alikuwa anasikia raha.

"Mfano, huyu bwana tangu ameishi humu hajawahi kutuona kwa macho lakini sisi tulikuwa tunamuona siku zote, tulikuwa tunaingia chumbani mwake na kumfanyia mambo yetu yeye hajui."
Jambo lingine ambalo lilinishangaza sana ni pale dalali huyo aliposema yeye alikuwa na uwezo wa kujua anachokusudia kukifanya mtu hata akiwa Dodoma na akakizuia mapema. Ila, anashindwa kujua endapo mtu huyo atakuwa anakusudia kufanya jambo kwa kuliwaza moyoni mwake bila kulisema kwa mtu.

Nilimuuliza mfano, akajibu mfano ni mimi na mfanyakazi mwenzangu tulipokuwa tumepanga kutumia bangi kuwaangamizi yeye na mkewe, walijua kwa sababu tulijadili kwa sauti ndiyo maana wao walijua. Akaongeza hata nilipoingia ndani na yule mzee aliyeshindwa akatimua, walijua tumepanga ndiyo maana wakawahi kwa kuchukua simu na kufanya mahoka mengine.

Yule mzee mkubwa wa wale waombaji akamuuliza: "Ina maana mkeo jini kwa sasa yuko wapi?"

Yule bwana akajibu atakuwa amerudi ujinini kwa sababu wakati wanaanza kuomba mkewe ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhisi anaungua moto na kuanza kulia kwa sauti mpaka ndugu zake wakajitokeza kumtwaa kwenda naye ujinini.

Yule mzee mkubwa wao akauliza swali jingine ambalo na mimi nilitaka kuuliza. Alimuuliza hivi: "Sasa watu wanasema majini wana uwezo mkubwa, wanaweza kupata fedha na mali yoyote ile, sasa kama wewe ulikuwa mume wa jini kweli ni kwa nini aliamua uwe dalali?"

Dalali akajibu: "Mimi sikuwa dalali, bali nilijifanya dalali ili nipate mtu wa kumpangisha ndani kwa sababu mimi na mke wangu tulipenda kuwachezea watu wanaoishi ndani.

"Mimi nina eneo Ilala la kuuza magari, pia nina duka kubwa sana Mnazi Mmoja, sina shida ya maisha wala ya fedha."

Kwa maneno yake hayo nilikubaliana na yeye kwani ni kweli hali yake haikuwa ya kuchoka. Hata siku ya kwanza nilipokutana naye nilishangaa dalali gani ana mwonekano wa kibosibosi ingawa hakuwa na gari. Hapo na mimi nikapata nguvu ya kumuuliza swali:

"Sasa bwana dalali wa bandia, uliwezaje kusababisha mimi nipate namba yako ya simu kwa rafiki yangu anaitwa Mohamed Kombe na akasema wewe ni dalali unaitwa Yusuf Mwamba?"
"Sikia bwana Humuli. Nimeshasema sisi tuna uwezo wa kujua kile kinachojadiliwa mahali na kukifanyia kazi.
Dalali anayeitwa Yusuf Mwamba yupo, huyo rafiki yako tulimchezesha ulimi wakati wa kutaja namba, akazitaja zangu badala ya za Yusuf."

Nilichoka kabisa, yule mzee mkuu akasema tumwingize ndani maana watu waliokuwa wakipita walianza kukodolea macho pale nje.

Kule ndani, dalali aliendelea kuzungumza mambo mengi sana lakini kuna wakati alijipinda na kujishika mgongo akidai anahisi maumivu makali ya moto. Alisema sehemu hiyo ipo kama kuna mtu amebandika jiko la mkaa.

"Mungu amekuponya sana labda kama hutajutia matendo yako ya nyuma," alisema yule mzee aliyenisaidia.
"Mimi sitaki tena, kwanza najuta kwa nini niligeuka adui na kufanya vile kwa watu wengine. Naomba mniombee sana kwa huyo Mungu wetu."

Yule mzee alimwelekeza kanisa lake ambalo halikuwa mbali na pale nyumbani, yule dalali akasema atakwenda kesho yake mapema.

Mimi pia nilialikwa, nikakubali kwenda kesho yake. Walipoondoka, nilibaki na dalali. Wasiwasi ulinishika lakini

nikawa nasikilizia. Kila baada ya dakika tano dalali aliingia chumbani kwangu na kuniomba nimsamehe kwa yote yaliyopita.

Usiku nililala usingizi mzuri hadi kunakucha kiasi kwamba sikuamini kama ni kweli ile nyumba ilikuwa vile. Kesho yake nilikwenda kazini, jioni nilikwenda kwenye lile kanisa ambapo nilimkuta dalali ameshafika.

Tulianza kuwa waumini wa kanisa hilo. Baada ya wiki mbili, dalali alimleta mke wake na mtoto mmoja ndani, kumbe alioa na familia yake ilikuwa Dodoma. Baada ya mwezi mmoja na mimi nilihamia Buguruni ambapo nilioa lakini bado nasali kulekule Magomeni na yule dalali.

Namshukuru sana Mungu kwa kunipigania. Ile mikono ilikuwa si salama bila neema ya Mungu. Nadhani shetani alipanga nife lakini ameshindwa katika jina la Mungu. Amina.

MWISHO.
Asante kwa somo zur
 
Mkuu acha ufala igiza Movie kama Annabelle
 
300068_529619623715243_975920888_n.jpg
 
Back
Top Bottom