SIMULIZI: Nilipanga Nyumba Moja na Majini

SIMULIZI: Nilipanga Nyumba Moja na Majini

Duu hapo ndo hatari mkuu sasa huyo dada si ni jini ndugu .....jamaa ana guts mi nisinge rudi kwenye hiyo nyumba na asubuhi faster nasepa kutafuta nyumba nyingine

Teh teh teh teh!.sasa ukifanya hivyo si sinema utakuwa umeisha imaliza?
Sisi wengine bado tunataka uhondo!
Leta vitu MziziMkavu!
 
Last edited by a moderator:
[h=1]Kısa cha kusısımuwa-5-[/h]
ILIPOISHIA :
Nilipata kigugumizi kikubwa kumjibu mambo poa kwani sikumjua na sikuwa nakumbuka chochote kuhusu yeye, sura yake ilikataa kichwani mwangu.
"Wewe ni nani kwani?" nilimuuliza.
Akaachia tabasamu kwa mbali, uzuri wake ukaongezeka.
"Ha! Humuli, hunikumbuki mimi, kweli?"
"Sikukumbuki hata kidogo."
"Sasa we binti, kama wewe ndiyo unamkumbuka si umkumbushe mlionana wapi?" yule mwanamke alisema kwa sauti ya mshangao.
ENDELEA SASA…


Lakini yule msichana mrembo alimwangalia yule mwanamke kwa macho yaliyojaa hasira…

"Mama uhusiki."
"Najua, lakini unapoteza muda kwa kuzungushazungusha wakati kumbe wewe unamkumbuka, yeye umeshajua hakukumbuki na amekwambia tayari."
Nilishangaa kumwona yule msichana akibetua kichwa kama aliyekuwa akiweka vizuri nywele zake, ghafla yule mwanamke niliyekuwa naye akajishika kichwa na kulalamika kinamuuma sana.
"Jamani kichwa! Kichwa jamani, daa!"
"Vipi mama, imekuwaje kwani?" nilimuuliza.
"Kichwa Humuli, kinavuta ghafla! Uwiii."
Nilianza kuogopa, nilihisi naangukiwa na msala maana akifa pale na watu waliona nikienda naye pembeni si nitahojiwa mimi?
"Kwani mama una kawaida ya kuumwa kichwa?" nilimuuliza nikimsogelea ambapo yeye sasa alikuwa ameinama.
"Sina, ndiyo nashangaa hapa."
Niliona hakuna dawa nyingine zaidi ya kumpeleka kwake ili nikaungane na familia yake kumpeleka hospitali. Lakini kabla ya kufanya hivyo niliinua macho ili nimwambie yule dada anisaidie na kama anataka kunikumbusha, hayo yangefanyika baadaye.
Ile naanaza kusema anti huku nikiwa nimeinua macho, nilishangaa kutomwona yule msichana pale.
"Khaa!" nilijikuta nikisema hivyo.
"Mama twende nyumbani ili tukupeleke hospitali na watoto wako."
"Ha! Mbona kimeachia," alisema akionekana kushangaa na kuniangalia, alikuwa amepanua kinywa.
"Kweli?"
"Eee, niko mzima kabisa."
"Au?" nilitaka kusema neno lakini zikulimaliza, nikahisi ulimi unakuwa mzito si kwa kushikwa bali kwa matakwa yangu.
"Humuli."
"Naam."
"Ni kweli yule binti humjui?"
"Simjui mama."
"Kuna mawili hapo, humjui au humkumbuki."
"Vyote mama, simkumbuki na pia simjui."
"Lakini wewe si alikutaja kwa jina?"
"Mwenyewe nilishangaa sana."
"Basi Humuli nimeshaelewa, kwaheri, nimeelawa ni kwa nini nimeugua kichwa na yule ni nani, pole sana wewe kijana," alisema yule mwanamke huku akiondoka zake kuelekea kwake.
Nilimtazama, lakini baadaye nilirudi kwenye kibanda cha chipsi.
"Mzee nakuona na miss jini," muuza chipsi mmoja alisema.
"Yupi, yule mwanamke?"
"Hapana, yule msichana."
"Mi simjui, kwani anaishi wapi? Maana kasema ananijua, ameniita na jina."
"Khaa! Kumbe wewe kama sisi. Huyu dada anaishi mitaa hiihii, lakini hakuna hata mmoja anayejua nyumba anayoishi!
"Kuna jamaa mmoja anaitwa Maleke, Maleke aliwahi kumfuatilia kwa nyuma lakini alishindwa kujua aliingia nyumba gani!"
"Mh! Au jini?" niliuliza kwa mshtuko mkubwa.
"Ndivyo watu wanavyosema, sasa alipokuja kusimama na wewe, tukawa tunabishana, wengine wanasema ni miss jini, wengine siye, lakini alipokuwa anaondoka tukagundua ni miss jini."
Basi, tuliishia hapo, nikachukua chipsi zangu na kwenda nazo nyumbani, niliamua kwenda kulia kule.
Nilifika, nikasukuma mlango mkubwa nikazama ndani kwangu. Lakini wakati napita kwenye usawa wa chumba cha wale wenzangu nikasikia vicheko, tena vicheko kwelikweli.
Sikuwajali, nikaingia sebuleni kwangu, nikafunga mlango kwa ndani, nikaweka chipsi juu ya meza, nikaenda pembeni ya chumba ambako kuna ndoo ya maji ili nichote ya kunawa.
Wakati naanza kula nilihisi na kugundua kitu. Niligundua mabakimabaki ya chipsi na kuku juu ya meza yangu wakati ukweli ni kwamba, tangu nimehamia pale sikuwahi kula chipsi wala kuku.
"Humu ndani kuna mtu anaingia kufanya mambo yake, lini mimi nimekula chipsi na kuku humu ndani?" nilijiuliza, nikasikia kicheko kutoka kwa wenzangu.
"Haa! Haaa! Ha! Haaaa…aaaa."
Niliinua macho kuangalia juu kwenye ‘silingbodi' kama vile niliyekuwa nimeona kitu, akili yangu ikawaza kitu cha dakika chache nyuma, nacho ni hiki:
"Humuli."
"Naam."
"Ni kweli yule binti humjui?"
"Simjui mama."
"Kuna mawili hapo, humjui au humkumbuki."
"Vyote mama, simkumbuki na pia simjui."
"Lakini wewe si alikutaja kwa jina?"
"Mwenyewe nilishangaa sana."
"Basi Humuli nimeshaelewa, kwaheri, nimeelawa ni kwa nini nimeugua kichwa na yule ni nani, pole sana wewe kijana."


Je, ni kwa vnini Humuli aliyarejea mazungumzo yake na yule mwanamke aliyeumwa kichwa ghafla? Fuatilia
baadae...
 
KISA CHA KUSISIMUWA-6

ILIPOISHIA -:
Niliinua macho kuangalia juu kwenye ‘silingbodi' kama vile niliyekuwa nimeona kitu, akili yangu ikawaza kitu cha dakika chache nyuma, nacho ni hiki:
"Humuli."
"Naam."
"Ni kweli yule binti humjui?"
"Simjui mama."
"Kuna mawili hapo, humjui au humkumbuki."
"Vyote mama, simkumbuki na pia simjui."
"Lakini wewe si alikutaja kwa jina?"
"Mwenyewe nilishangaa sana."
"Basi Humuli nimeshaelewa, kwaheri, nimeelewa ni kwa nini nimeugua kichwa na yule ni nani, pole sana wewe kijana."
SASA ENDELEA…

Nilianza kuamini kwamba, kuna uhusiano mkubwa kati ya yule msichana na wale wapangaji wa pale ndani nilipo, inawezekana alinijua jina kwa sababu naishi nao na wana uwezo wa kujua jina la mtu kulingana na mazingira yao.
Pia niliwaza kwamba, kuna uwezekano mkubwa yule msichana alitokea baada ya maono yao kuniona mimi na yule mama wa jirani tukitaka kuwazungumzia wao kama wapangaji wenye maajabu hivyo hawakupenda iwe hivyo ndiyo maana msichana akaibuka na kusababisha mvurugano.
"Itakuwa kweli, ndiyo maana yule mama naye alisema ameshajua ni kwa nini aliugua kichwa ghafla, alijua yule msichana ni nani na kwa nini yeye kasikia maumivu ya ghafla vile."
"Lakini pia kuna wale wauza chipsi, nao niliwakumbuka hasa yule mmoja aliyesema yule msichana wanamjua, anaishi mtaani, lakini hawajawahi kubaini anaishi nyumba gani na kwa mzee nani wala anajishughulisha na nini," hayo yote niliyawaza mimi.
Nilisimama, nikachukua sabuni ya kuogea ambayo haijafunguliwa, nikaipiga chini kwenye kapeti kwa hasira huku nikisonya, nikasema kwa sauti ya chini:
"Humu ndani naishi na majini."
Kule chumbani nikasikia wakicheka.
"Si unaona, nimesema mimi, lazima naishi nao humu ndani, da! Najuta sana," nilisema. Kicheko kikasikika tena, safari hii kilikuwa cha juu zaidi kuliko kile cha awali.
Moyo ulijaa mawazo, akili ilihisi uchungu wa maisha, niliwaza fedha nilizozilipa kwa ajili ya kupanga mle ndani, nikamkumbuka dalili, niligundua alichofanya ni kunitapeli na hakuna lingine wala hakuwa msaada kwangu.
"Mimi ni mwanaume, kama niliweza kupata fedha za kupanga hapa, sishindwi kupata nyingine za kupanga sehemu nyingine tena mbali na hapa," nilisema kwa moyoni.
***
Usiku nikiwa nimelala, nilichelewa sana kupata usingizi, ghafla nikaona taswira za watu ukutani, wawili tena wakiwa wamesimama, ni mwanamke na mwanaume. Niliogopa sana, nikainua kichwa polepole kuwaangalia kwa umakini, japo kulikuwa na giza, lakini niliweza kuona vizuri lakini si kwa uwazi mkubwa kama ambavyo taa ingekuwa inawaka.
Ni kweli walikuwa watu wawili kama nilivyoona, tena weupe nikimaanisha si watu weusi. Walikuwa wakionesha vitendo vya kucheka huku wakijinyonganyonga.
Kuna wakati walitembea mpaka jirani na kitanda changu kisha wakageuza na kurudi pale ukutani. Nilipeleka mkono hadi kwenye swichi ya kitanda (bed switch), nikawasha, cha ajabu sikumwona mtu wala dalili pale ukutani.
Niliamka nikiwa nahema kwa kasi mpaka nikajishika kifuani, nikafungua mlango na kutoka nje ili nijifanye nakwenda chooni lengo langu lilikuwa kupata picha kwa wenzangu kukoje maana niliwashuku wao na wale walioonekana chumbani kwangu.
Kwa wenzangu niliwasikia wakikoroma kwa zamu. Nikajiuliza ina maana si wao waliokuja chumbani kwangu? Niliona ni utani wa hali ya juu.
Niliamua kurudi chumbani na kukatisha safari ya kwenda chooni, nikafunga mlango wangu kwa funguo na kupanda kitandani, nilizima taa ili nione kama yale mauzauza yatatokea tena.
Ukimya ulitawala kwa muda bila kujitokeza chochote, nikaanza kupitiwa na usingizi kwa kusinziasinzia, ghafla ukutani nikawaona tena wale watu wawili.
Safari hii walikuja hadi kitandani, wakakaa, wakasimama, wakaenda kwenye kabati, wakafungua, wakatoa mashuka na kujifunika, wakayarudisha, wakaenda nyuma ya mlango, wakatungua mashati yangu mawili, wakagawana na kuyavaa kisha wakayavua, mmoja mwanaume akaenda sehemu yenye redio, akapeleka mkono, nikajua anataka kuiwasha, lakini hakufanya hivyo.
Nilichoamua kukifanya akilini ni kuwasha taa kwa ghafla na kuwavamia na nilipanga kumvamia mwanamke nikiamini ndiye aliyekuja kule kwenye chipsi. Polepole nilipeleka mkono hadi kwenye swichi, nikawasha taa kwa ghafla huku macho yangu yakiwa kwao, lakini sikumwona hata mmoja! Kwangu haikuwa mapambano bali nilichukulia kama changamoto za maisha.
***
Asubuhi, niliamka nikiwa nimechoka sana, lakini kabla sijatoka kitandani nilisikia nje ya mlango kukiwa na hali ya watu kutembeatembea tena kwa kasi, niliinua shingo ili nione kama nitasikia zaidi, lakini kukawa kimya.
Niliamka, nikatoka, nilikwenda sebuleni kwanza kuangalia kama kuko salama.
Nilishangaa kukuta mezani kuna mfuko wa rambo uliojaa chipsi kuku kama nilivyonunua mimi, lakini zangu nilikula, sasa zile sikujua zilitoka wapi.
Niliubeba ule mfuko nikatoka nao, nilifungua mlango mkubwa wa nje nikautupia pembeni kidogo, niliporudi, nikaenda chooni, mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani kwani hata niliposhika kitasa na kukivuta kilikuwa kigumu.
Hii iliashiria kwamba kuna mtu, kwa hiyo moyoni nilisema nisimame palepale nje ya mlango hadi atoke. Nilisimama eneo ambalo akitoka tu, uso kwa uso na mimi.
"Tuone leo, wao si wajanja, leo nimemnasa mmoja wao," nilisema moyoni.


Je, nini kiliendelea? Fuatilia Leo jioni..Usikonde tu.
 
SASA JIACHIE

Ushuzi ulisikika bayana kutoka humo chooni. Matundu ya pua yangu yalipigwa busu na harufu kali ya ule ushuzi. "Hatoki mtu hapa" nilinong'ona huku mkono wa kulia umeziba matundu ya pua yangu. Nilisikia mlio wa maji mithili ya mtu anayejitawadha. Kuwa kimya! Nilivuta pumzi kwa shauku ya kumwona huyo mmoja wao. Nikasubiri!

Mara nikasikia majirani zangu wakicheka. Nilipoangalia mlangoni kwa majirani nikaona malapa pea mbili lakini moja bado ina majimaji. Nikaamua kwenda kuujaribu mlango wa chooni ili kuona kama bado umefungwa kwa ndani. Sikuamini macho yangu. Mlango ulikuwa wazi na nilipochungulia ndani sikumwona mtu yeyote, isipokuwa majimaji na vipovu vya sabuni. "Mbona sikusikia mlango ukifunguliwa? Mbona sikumwona akipita hapa? Mbona...." nilijiuliza maswali mfululizo moyoni yasiyo na majibu, macho nimeyakodolea humo chooni......



Najaribu kupunguza taharuki wakuu, mwingine aendeleze. tupokezane hadi jion. Mambo ya Mzizimkavu hayo.....
 
KISA CHA KUSISIMUWA-7

ILIPOISHIA JANA USIKU:

Niliamka, nikatoka, nilikwenda sebuleni kwanza kuangalia kama kuko salama. Nilishangaa kukuta mezani kulikuwa na mfuko wa rambo uliojaa chipsi kuku kama nilivyonunua, lakini zangu nilikula, sasa zile sikujua zilitoka wapi.
Niliubeba ule mfuko nikatoka nao, nilifungua mlango mkubwa wa nje nikautupia pembeni kidogo, niliporudi, nikaenda chooni, mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani kwani hata nilipokishika kitasa na kukivuta kilikuwa kigumu.
Hii iliashiria kwamba kulikuwa na mtu, kwa hiyo moyoni nilisema nisimame palepale nje ya mlango hadi atakapotoka. Nilisimama eneo ambalo akitoka tu, atakutana nami uso kwa uso.
"Tuone leo, wao si wajanja, leo nimemnasa mmoja wao," nilisema moyoni.
ENDELEA SASA…


Dalili zote zilionesha kwamba mle chooni mlikuwa na mtu kwani niliweza kusikia hata kuhema kwake, mara mlio wa maji, mara alikohoa, tena kwenye kukohoa nikabaini mtu mwenyewe alikuwa ni mwanamke ndiye aliyekuwa mle.

"We kohoa mpaka utapike, lakini mimi nipo hapa mpaka utoke," nilisema moyoni.
Nilikaa sana, ikafika mahali nikachoka, lakini moyoni nikasema siondoki hata iweje, lakini nilishtuka kitu, niligundua muda mrefu sijazisikia zile dalili kama maji au kuhema, nikafunguka akili.
"Mh! Siyo kwamba ametoka?"
Ile namalizia kusema ‘ametoka?' nikasikia kicheko kutoka kwenye chumba chao. Vicheko vikubwa sana cha kike na kiume.
Nilirudi chumbani mwili ukinisisimka, hapo ndipo niliamini mia kwa mia kwamba, nilikuwa nadili na watu wasiokuwa wa kawaida.
Niliingia chumbani, nikampigia simu dalali.
"Haloo," niliita.
"Haloo. Halooo," nilirudia lakini sikupokelewa.
Nikiwa nimeachana na simu, mara iliita yenyewe, alikuwa ni dalali nikapokea.
"Haloo," niliita.
"Haloo," niliitikiwa lakini sauti haikuwa ya dalali.
"Mzima bwana?" nilisalimia.
"Tuone leo, wao si wajanja, leo nimemnasa mmoja wao."
Ha! Nilishtuka sana, nilisikia sauti yangu mwenyewe ikisema hivyo. Ikaendelea.
"We kohoa mpaka utapike, lakini mimi nipo hapa mpaka utoke."
Nilikata simu, nilikuwa nahema sana, mapigo ya moyo yalikuwa yakienda kwa kasi ya ajabu huku nikishindwa kuona sawasawa.
"Hii ni hatari sasa," nilisema.
***
Usiku wa siku hiyo sikulala kusema kweli kwani kila nilipofikiria maisha yale sikuona sababu ya kuendelea kuishi pale. Moyoni nilisema kwamba, ni afadhali ningeishi na watu ambao ni majambazi kuliko hawa, nafuu ningepanga nyumba moja na makahaba kuliko kupanga nyumba moja na majini.
Nilichoamua, asubuhi nikifika kibaruani tu niombe ruksa kisha nianze kumsaka yule dalali na pia nitafute dalali mwingine ambaye atanitafutia vyumba kwingine na si maeneo yale tena kwani niliyaona yana nuksi.
***
Asubuhi kulikucha salama kabisa, tena usiku wa siku hiyo sikuona mauzauza wala dalili zake. Nilikwenda kuoga bila kukagua mazingira, moyoni nilisema liwalo na liwe kwa maana kwamba, wawepo wasiwepo sawa tu.
Bafuni niligundua wameshaoga kwani kulikuwa na majimaji ya muda mfupi uliopita. Nilipomaliza kuoga, nilijiandaa na kutoka. Nje nilikutana na mtu ana mkokoteni, akanisalimia.
"Za asubuhi bwana mkubwa?"
"Salama, karibu sana."
"Asante, kuna watu fulani wanaishi humu nina shida nao."
Aliposema hivyo nilishtuka sana, niliamini yeye ni mmoja wa wale ila amejigeuza kwa kujifanya ana shughuli za mkokoteni.
"Unawajua kwa sura?" nilimuuliza huku nikiwa na wasiwasi maana alinikazia macho.
"Siwajui."
"Sasa una shida nao kivipi watu usiowajua kwa sura?"
Ni kwamba, kuna binti mmoja huwa wanamtuma niwaletee maji, nikifika hapa huyo binti anabeba madumu kupeleka ndani, sasa jana nilikutana na huyo binti nikamuuliza kuhusu malipo yangu ya mwezi sasa, akasema nije nifuatilie mwenyewe."
Nilishangaa sana kusikia hivyo. Nijuavyo mimi mle ndani mna watu wawili, mwanamke na mwanaume, sasa kama kuna binti hilo lilikuwa jipya kwangu, labda lakini.
"Huyo binti naye anaishi humu au?" nilimuuliza.
"Sidhani, inaonekana kama huwa wanamtuma tu."
"Kwa nini huamini kama anaishi humuhumu ndani? Hafanani na wao wenyewe?" hili swali niliuliza likiwa na mtego mkubwa sana, nilitaka nijue uhalisia wake.
"Siwezi kusema hafanani wakati wao siwajui kwa sura."
Hapo ndipo nilipopataka, nilidhani atasema hafanani nao, ningejua ni walewale.
"Oke, nadhani wameondoka kwenda kazini."
"Ah! Sasa mimi fedha zangu nitazipataje jamani?"
"Subiri wakirudi jioni."
"Wewe utakuwepo?"
Nililishangaa swali hilo, hakuwa akinidai mimi lakini anataka niwepo?
"Unataka niwepo?"
"Ee."
"Kwa nini?"
"Naamini utanisaidia kuzipata fedha zangu."
"Uliwahi kuja wakagoma kukupa?"
"Siyo hivyo, ila kila nikija, nikigonga mlango huwa hawafungui."
"Basi nitakuwepo."
"Asante kaka. Nije saa ngapi?"
"Saa moja nitakuwa nimerudi."
Aligeuza mkokoteni na kuondoka zake huku akisema:
"Muda huo nitakuwa nimefika kaka."
Niliondoka kwenda kazini kuomba ruksa. Lakini wakati naondoka, mfanyakazi mwenzangu mmoja aliniuliza nakwenda wapi, nikaamua kumsimulia kwa ufupi kisa changu.



Je, nini kiliendelea? Fuatilia usiku wa leo
 
KISA CHA KUSISIMUWA PART 8

ILIPOISHIA:

"Uliwahi kuja wakagoma kukupa?"
"Siyo hivyo, ila kila nikija, nikigonga mlango huwa hawafungui."
"Basi nitakuwepo."
"Asante kaka. Nije saa ngapi?"
"Saa moja nitakuwa nimerudi."
Aligeuza mkokoteni na kuondoka zake huku akisema:
"Muda huo nitakuwa nimefika kaka."
Niliondoka kwenda kazini kuomba ruksa. Lakini wakati naondoka, mfanyakazi mwenzangu mmoja aliniuliza nakwenda wapi, nikaamua kumsimulia kwa ufupi kisa changu.
ENDELEA MWENYEWE…


"Kha! Sasa hapo tatizo liko wapi, mbona dawa ipo rahisi sana."

"Rahisi! Ni ipi hiyo?"
"Sikia, twende pembeni nikakusimulie," aliniambia yule mfanyakazi mwenzangu huku akiangalia kulia na kushoto kama mabosi watatokea.
Tulikwenda kusimama pembeni, akaanza kuniambia:
"Sikiliza, kama unaishi nyumba ya namna hiyo, unachotakiwa kufanya, kila siku asubuhi na jioni au usiku unapuliza bangi ndani ya nyumba, kama ni majini, mapepo sijui nini, utaona mambo poa kabisa."
Sikuamini maneno hayo, nikamuuliza mara mbilimbili kama ni kweli.
"Khaa! Nina mjomba'ngu aliwahi kuishi kwenye nyumba ya hivyo, akaenda sehemu akaelekezwa dawa ni hiyo, akaitumia, mpaka sasa anaishi kwa raha hakuna cha majini wala mapepo," alisema.
Nilimsikiliza nikianza kuamini kwa mbali, lakini nilifika mahali nikamuuliza hiyo bangi mimi nitavuta au nitaiwasha ili itoe moshi yenyewe?
"Ukishaiwasha, utaiweka mezani au popote ndani kwako, lakini angalia isizimike ili moshi wake usambae chumba kizima au sebule nzima."
"Hilo linawezekana," nilimwambia nikimtumbulia macho.
Kwa sababu nilikuwa nimeshaaga, ilibidi niondoke tu na kurudi baadaye. Nilikwenda mtaani, nilitafuta bangi nikapata maeneo ya Kariakoo, nikaitia mfukoni.
Nilizurura sana siku hiyo, saa tisa kamili nilikuwa njiani narudi kazini. Nilipiga hesabu za kufika kazini na kuondoka, maana muda wa kazi ni saa tisa na nusu.
Wakati napita pale Kituo cha Polisi Msimbazi, fujo zikazuka, kuna machinga wawili walikuwa wanapigana kwa sababu ya kugombea sehemu ya kufanyia biashara, katika ugomvi huo mimi nilibaini mmoja wao ndiyo mwenye kosa.
Nikampa laivu kuwa yeye ndiye mwenye tatizo, alikuja juu, akachukua boksi lenye viatu na kunirushia, likanipata kwenye bega la kulia, sikukubali, nikaokota jiwe na kumrushia, likampata mkononi.
Polisi walifika haraka sana, wakanikamata mimi, yeye na yule machinga niliyeona anaonewa, tukapelekwa Msimbazi polisi.
Tulipofika pale, afande aliyetukamata alituamuru kuvua viatu, mikanda, simu kuweka pembeni. Halafu mmoja alianza kutusachi mifukoni. Wakati tendo hilo linaanza kwa wenzangu, ndipo nikakumbuka mimi mfukoni nina vipisi viwili vya bangi.
Nilitaka kutoka mbio kituoni hapo, lakini sehemu tuliyokaa, ningesema nitoke, nisingefika nje au hata kama ningefika ningekamatwa au kupigwa risasi kama mhalifu, nilitetemeka, mwili uliisha nguvu.
Ilipofika zamu yangu kusachiwa, askari mwenyewe alishangaa kuniona nachezesha miguu kama niliyebanwa na haja ndogo, akaniuliza:
"We vipi, unaumwa?"
Nikamjibu naumwa afande.
"Unaumwa nini?"
"Sijui, nadhani homa."
Hakunijibu, alianza kwa kutumbukiza mkono kwenye mfuko usiokuwa na kitu, akahamia wa nyuma ambao una waleti, akapeleka wa kulia kwangu ambao ndiyo wenye bangi, aliposhika, akakunja sura, alipotoa akashtuka sana na kusema:
"Haa! Hii bangi siyo?"
Sikumjibu kwani niliamini ameshaijua, wenzake waliokuwa kaunta wakaacha mambo yao na kunigeukia mimi, nao wakashangaa sana. Mmoja alikuwa amekaa juu ya stuli, akashuka huku akiniangalia kwa kunikazia macho.
"Unakuja kituo cha polisi na bangi, wewe unatutafuta nini sisi?" aliuliza yule aliyeshuka kwenye stuli.
Niliambiwa nafunguliwa kesi ya pili, ya kwanza kupigana na kujeruhi ya pili kukutwa na bangi!
Nilijitetea nikisema bangi ile si kwa ajili ya kuvuta bali nilikuwa nina shida nayo.
"Wewe usitufanye sisi watoto wadogo, tunawajua ninyi raia," alisema yule afande aliyenisachi.
Lakini afande mmoja wa kike ambaye muda wote alikuwa akiangalia tu, akawaambia wenzake:
"Lakini huyu kaka mbona hafanani na kuvuta bangi, muulizeni ana shida nayo gani?"
Wale wenzake wakanigeukia na kuniuliza:
"Haya, wewe mwananchi, raia kabisa, unaweza kuwa na shida gani na bangi mbali na kuvuta?"
Niliwasimulia kila kitu, tena nilifika mahali nikawaambia kama kuna asiyeamini, tuongozane hadi nyumbani, Magomeni akaone maajabu ambayo hayahitaji kuelekezwa sana ili kuamini kama yapo au la!
Palipita ukimya wa sekunde kadhaa, mmoja wao akaniuliza:
"Kama ni kweli au tufanye ni kweli, ni kwa nini umemuumiza huyu?"
Nilisema kilichotokea, yule chinga niliyemsaidia naye akanitetea kwa kusema hivyohivyo, lakini afande mmoja akasema nilijichukulia sheria mkononi ambapo ni kosa kisheria.
Niliomba sana wanisamehe kwa yote, nikasingizia kwamba ni kwa sababu kichwa changu hakipo sawa kwa kuishi nyumba moja na majini.
Namshukuru mmoja wao aliniambia niondoke lakini nihakikishe situmii bangi katika kujitibu kwani serikali haiamini kama bangi ni dawa.
Nilipotoka, nilikwenda kununua nyingine, lakini akili iliingia hisia kwamba, huenda yule dada wa ajabu mle ndani ndiye anayecheza michezo ili kunikwamisha kwenda na bangi ndani ya nyumba, nikasema moyoni ngoja ninunue hii nione kitakachotokea, nikanunua tena misokoto miwili.


Je, nini kiliendelea? Futatilia baadae.....
 
KISA CHA KUSISIMUWA PART 9-

ILIPOISHIA:
NAMSHUKURU mmoja wao aliniambia niondoke lakini nihakikishe situmii bangi katika kujitibu kwani serikali haiamini kama bangi ni dawa.
Nilipotoka, nilikwenda kuinunua nyingine, lakini akili iliingia hisia kwamba, huenda yule dada wa ajabu mle ndani ndiye anayecheza michezo ili kunikwamisha kwenda na bangi ndani ya nyumba, nikasema moyoni ngoja ninunue ili nione kitakachotokea, nikanunua tena misokoto miwili.
SASA ENDELEA…


Nilitembea kuelekea kituo cha daladala. Njiani nilimpigia simu yule mfanyakazi mwenzangu aliyenijulisha kuhusu dawa ya kutibu nyumba yenye majini, nikamwambia sitaweza kurudi kwani nilipata wakati mgumu kidogo njiani.

Alinielewa, akaniuliza kama nimepata, nikamjibu kila kitu kimekwenda sawa, lakini sikumwambia kuhusu timbwili lililojitokeza.
Nilipanda daladala nikashuka Magomeni, niliingia ATM kutoa fedha kidogo, kisha nikatoka. Wakati natafuta mwelekeo wa kwenda nyumbani, nilimkumbuka dalali, nikampigia simu.
"Halo."
"Halo habari za kazi bwana?"
"Nzuri, pole na kazi na wewe mwenzangu?"
"Nimepoa. Bwana vipi kuhusu nyumba?" nilimuuliza.
"Nyumba imefanyaje?"
"Si nilikusimulia matatizo yake, umesahau?"
"Kwani ulisema matatizo yake yakoje vile?"
Nilimwelezea kwa kirefu, nikafika mahali nikamwambia hadi nilivyompigia simu halafu ikapokelewa na sauti ya ajabuajabu, alicheka sana.
"Wewe bwana acha kunichekesha.
"Kwa nini unasema hivyo?"
"Yaani simu yangu mimi halafu apokee mtu mwenye sauti ya ajabuajabu, kwa nini sasa?"
"Mimi pia sijui."
"We ulikosea namba."
"Labda bwana mi siwezi kukazania sana," nilimjibu kwa kinyongo kwani namba yake niliisevu na ninapompigia huwa nasachi jina tu, sasa nilikosea kivipi?
"Enhe, unasemaje bwana?" aliniuliza.
"Nimeshakwambia bwana."
"Kwa hiyo unashauri nini?"
"Nataka pesa zangu nikapange kwingine."
"Da! Hilo halitawezekana kirahisi bwana, maana mpaka nimpate mpangaji mwingine atoe fedha ndipo nikulipe wewe na mpangaji atakayekuwa tayari kutoa fedha lazima akute nyumba tupu, sasa wewe utalikubali hilo?"
"Naweza kulikubali, ila tuandikishiane."
"Kwamba?"
"Kwamba unajikomiti nikiondoka, akiingia mpangaji mwingine tu unanilipa pesa zangu."
"Ngoja nitakupigia," alisema dalali na kukata simu.
Nilipokuwa nakaribia nyumbani, nikakutana na yule msukuma mkokoteni wa maji.
"Kaka za kazi?"
"Nzuri, vipi wewe?"
"Niko sawa, ndiyo unarudi?"
"Ndiyo."
"Najua jamaa hawajarudi, nitakuja muda uleule tuliopanga."
"Sawa, karibu sana."
"Asante sana."
Niliingiza funguo ili kufungua mlango, lakini nikagundua kwa ndani kulikuwa na funguo nyingine maana nilichungulia.
Nilipousukuma, ulifunguka. Hii ina maana wale watu wa ajabu walikuwa wamesharudi, wako ndani. Niliingia ndani, nikafungua mlango wa sebuleni, nikaingia humo.
Nilifikia kwenye kochi kubwa, nikajilaza. Sikuangalia kama kweli wenzangu walikuwa wamesharudi, ila nilisikia sauti ya muziki wa redio, nikajua wapo.
Mara nikasikia mlango wao mmoja ukifunguliwa, nikasikia mtu akitoka. Kwa mara ya kwanza nilisikia akisema:
"Kama utamkamata anavuta bangi apelekwe polisi, ndiyo dawa yao watu wa aina hii."
Nilishtuka, nikakaa. Nikawaza kama ninachosikia ni cha kweli au?
Huyo aliyekuwa akisema hayo ni mwanamke na ilionekana alitoka kuelekea uani. Nikatoka ghafla, nikaona kisigino cha mguu mmoja kikimalizia kuingia chooni.
Nilirudi chumbani huku najiuliza kama hawa watu walisema vile kwa sababu wamejua mimi nimenunua bangi au? Na ni kwa nini wazungumze Kiswahili kwa mara ya kwanza siku hiyo?
Baada ya dakika mbili, nilimsikia akirejea chumbani kwake huku akisema:
"Mimi mtu anayevuta bangi siku yoyote na mahali popote pale, nikimwona nampeleka polisi ajue mimi ni nani. Haiwezekani watu wawe wanavuta bangi hovyo tu.
Moyoni nikasema hata iweje, hii bangi leo lazima niichome humu ndani. Mkienda polisi msipoenda mtajua wenyewe.
"Mimi siwezi kuishi katika mazingira magumu namna hii wakati pesa ni yangu. Kwa nini ustaarabu usiwepo?" nilisema moyoni nikipeleka mkono mfukoni ili kutoa ile bangi niliyonunua mara ya pili.
Niliipata, nikaitoa. Niliiweka kwenye meza kisha nikaendelea kulala nikiusaka usingizi kwa nguvu zangu zote maana nilijisikia kuchoka sana. Hapo nilikuwa sijaenda chumbani kwangu.
Sikumbuki ni muda gani nilipitiwa na usingizi, ila nakumbuka wakati nalala ilikuwa saa kumi na moja. Nilipokuja kushtuka ilikuwa saa kumi na mbili na nusu. Ina maana nililala kwa saa moja na nusu.
Jicho langu moja kwa moja lilitua kwenye bangi pale mezani, sikuiona.


Je, nini kiliendelea? Fuatilia leo jioni usikonde.....
 
Sasa nyie wapambe mnaoburudika na hivi visa vya MziziMkavu MBONA HIZO "like" ZENU MNAZIONA MAALI SANA??

Yeye MziziMkavu ukisema chochote anakugongea "like" !!
Nyie mnaburudika BURE KUTOA Hivyo vi "like " vyenu MNAONA LABDA ATAONGEZEKA AFYA AU??

ACHENI HIZO! kama mimi ndio MziziMkavu naanzisha hadithi taamu kama hii. Halafu nikiona hamna "like " kwa wingi. Namuua steringi katikati ya story halafu najifanya UMEME UMEKATIKA!
NAWAACHA KWENYE VICHWA VYA HABARI TU!
Manake hamna maana!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom