SIMULIZI: Nilipanga Nyumba Moja na Majini

SIMULIZI: Nilipanga Nyumba Moja na Majini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
"Kama kuna watu hawayajui haya nitakayoyaongea basi nawataka kuanzia sasa wajue kwamba, hapa Dar kuna mambo makubwa sana ambayo ukisimuliwa unaweza kusema si ya kweli, lakini wale wanaoyapata hayo mambo wanajua na wewe usiombe yakukute hata siku moja," ndivyo alivyoanza kusimulia Bw. Humuli Samaki (43), mkazi wa Buguruni (kwa sasa) ambaye alipata mkasa mzito akidai alipanga nyumba moja na majini Magomeni, Dar es Salaam.

SASA ENDELEA MWENYEWE


"Si zamani sana mkasa huu uliponitokea, ilikuwa mwaka 2009 tu, kwa hiyo naweza kusema ni juzijuzi tu. Kwa sasa naishi hapa Buguruni, baada ya kuhama kutoka Magomeni ambako nilipata mkasa mzito na wa kuogopesha. Nilipanga nyumba moja na majini."

Mwaka huo (2009), awali nilikuwa nikiishi Mwanyamala Mwinjuma, jirani kabisa na Makao Makuu ya Bendi ya TOT, hata Kapteni John Komba nilizoeana naye kwa kuonanaonana naye pale CCM-Mwinjuma, ingawa jina langu najua hakuwa akilifahamu.

Ile nyumba niliyokuwa nikiishi pale Mwananyamala iliingia kwenye mgogoro wa kifamilia na kufikishana mahakamani kwa ajili ya kugawana mirathi. Hukumu ilipotoka ikaamriwa iuzwe kisha ndugu wagawane fedha.

Kwa maana hiyo, mimi na wapangaji wenzangu watano, tulipewa notisi ya kuhama baada ya mteja kupatikana. Huyu mteja anaitwa Masawe anafanya kazi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) lakini sijui ofisi za wapi.

Ilibidi mimi niangalie mwelekeo mwingine, niliamua nibadili upepo, nikaishi Magomeni. Kwa wakati huo nilikuwa sina familia. Sina mke wala mtoto hata wa kusingiziwa, kwa hiyo nilikuwa naishi peke yangu. Ni mwaka jana ndiyo nimeoa mke wangu huyu, anaitwa Hadija Mashada.

Rafiki yangu mmoja anayeitwa Mohamed Kombe alinipa namba ya dalali kwani yeye anaishi Magomeni hata sasa. Nilimpigia simu dalali wake, anayeitwa Yusuf Mwamba, akaniita Magomeni pale kwenye nyumba wanayosema aliwahi kuishi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Nilikwenda mpaka pale, nilimkuta amesimama nje ya nyumba hiyo, tukasalimiana, akaniuliza nataka nyumba yenye sifa gani, nikamweleza.

Niliwajibu mimi mwenyewe sijui, lakini sikumaindi sana. Akaja mama mmoja aliyesema anaishi nyumba ya pili, akasalimia na kuniuliza maswali.
"Hamjambo wanangu?"
Tuliitikia wote, akauliza nani anahamia pale kati ya sisi wote, tulikuwa watano mbali na dereva.
"Ni mimi."
"Ooo, mzima baba?"
"Mimi mzima mama."
"Unaitwa nani?"
"Humuli Samaki."
"Unahamia peke yako au uko na mke na watoto?"
"Peke yangu mama."
"Humuli Samaki ni mwenyeji wa wapi?"

"Usukumani."
"Haya, naamini uliaga wakati unaondoka nyumbani."
"Hilo lilikuwa la kwanza mama."
"Haya, kila la kheri."

Tuliendelea na kazi ya kuingiza vyombo ndani hadi tukamaliza. Wale wenye gari wakaondoka, nikabaki mimi peke yangu.
Nilijiwekea malengo kwamba, nihakikishe naweka sawa kila kitu ili kesho yake nisiwe na kazi hiyo zaidi ya kwenda kazini. Niliifanya kazi kwa muda wa saa tatu, mpaka kwenye saa saba na nusu usiku nikamaliza.

Nilibadili nguo, nikavaa taulo na kwenda kuoga. Nilikuta bafu limetoka kutumika kama dakika kumi nyuma, sikushangaa kwani si kuna wapangaji wengine ambao tulitakuwa tunatumia bafu moja.

Usiku kabla ya kuzima taa, nilizima taa, nikapanda kitandani. Kabla sijapata usingizi, niliwasikia wenzangu wakicheka sana na kuongea huku wameweka muziki. Lakini ule muziki haukuwa wa kiarabu, kizungu wala kiswahili.

Hata maongezo yao, mimi nilisikia sauti tu lakini kusema walikuwa wanatumia lugha gani si rahisi. Kuna wakati kama walikuwa wakiongea kihindi, pia niliwasikia kama wanaongea kiarabu, nikajua ni watu wa namna hiyo.

Lakini sikulala mpaka nikampigia simu dalali kumuuliza kama wale wapangaji wenzangu ni weupe au waswahili kama mimi, akasema hata yeye hajui kwani hakuwahi kuwaona hata siku moja.

Basi, nililala. Asubuhi niliamka nikiwa nimechoka sana. Wakati nakwenda bafuni kuoga niligundua ni mimi peke yangu ndiye niliyekuwa nimetangulia kuamka, kwani bafuni hakukuwa na maji yaliyomwagika kwa muda huo.

Baada ya kuoga nilirudi chumbani kwangu kujiandaa kwenda kazini. Wakati najiandaa, nilisikia mlango ukifunguliwa, nikajua ni wenzangu wanakwenda kuoga au chooni kama ilivyo kawaida kwa wanadamu wakiamka asubuhi.

Niliamua kutumia nafasi hiyo kuwatambua. Nilivizia pale niliposikia mlio wa maji bafuni na mimi nikatoka kwenda kupiga mswaki kwa mara ya pili. Sehemu niliyosimama, mtu akitoka bafuni kwenda ndani ilikuwa lazima nimuone kwani ilikuwa kiasi cha kugeuka tu.

Lakini cha kushangaza, nilikuwa sisikii maji kumwagika, nikageuka na kuona mlango wa bafuni upo wazi. Mbali na mlango kuwa wazi, pia chini nikaona alama za kandambili nne zikiwa zimekanyaga, nikajua wametoka.
"Lakini wamepitaje hapa?" nilijiuliza.

Nilirudi ndani, mlangoni kwao nilikuta kandambili pea mbili zikiwa bado na majimaji kwa mbali, jambo hili lilinifanya nijiulize sana.
Nilijipa ujasiri na kuamua kuchungulia ndani ya chumba hicho kwa kutumia nafasi ya katikati ya mlango ambapo niliweza kuona hadi kitanda lakini sikumwona mtu mwingine.

Niliingia kwangu, nikaweka mswaki, nikavaa vizuri na kuondoka zangu. Nilitegemea wenzangu nimewaacha ndani, kwani nilipofika mlangoni nilikuta umefunguliwa na upo wazi. Nilirudi ndani hadi kwenye mlango wao.
"Wa ndugu," niliita kwa sauti.
"Jamani wa ndugu."

Ukimya ndiyo ulinifanya nibaini walishaondoka. Kwani kulikuwa kimya sana na kandambili zilikuwa pembeni ya mlango si pale pa kwanza.

Nilifunga mlango mkubwa nikaondoka, mbele nilimwona yule mama aliyekuja usiku kuniuliza maswali. Alikuwa amesimama nje ya nyumba yake, aliponiona akashutuka na kuita majina mawili ya watu. Wakatoka watoto wake wawili, ni mabinti wenye miaka kama kumi na nane na ishirini na mbili hivi.
"Hujambo kijana?" yule mama alinisalimia kwa furaha.
"Sijambo mama, shikamoo."
"Marhaba." Kisha akawaambia kitu wale watoto wake nao wakanikazia macho.
"Mama umewaona majirani zangu hapa?"
"Majirani zako akina nani?"
"Wapangaji wenzangu."
"Kijana, kua uyaone ya dunia. We si umeshakua, utayaona ya dunia."
Kauli hiyo iliniogopesha sana, nikashtuka na kumuuliza mama.
"Mama una maana gani?"
"Sisi hatutaki umbeya kijana."
"We si umeambiwa utayaona kwa hiyo subiri tu," alidakia binti yake mkubwa.

Miguu ilitetemeka, mwili uliisha nguvu, nikajikuta nataka kukaa, lakini sikuweza. Nilichoamua ni kuondoka huku nampigia simu yule dalali.
"Vipi hujambo bwana?"
"Mimi sijambo."
"Za makazi mapya."
"Si nzuri bwana."
"Kwa nini tena?"
"Sielewielewi."
"Kivipi?"
"Kuna mambo kama si ya kawaida."
"Yapi hayo?"


Itaendelea chini; hapa - SEHEMU YA TATU
 
Haijachanganya hapa, bado nasubiri mambo kama ya balkisi na suzana niyaone hapa! BADILI TABIA, Paloma msikae mbali atii!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

waka huu mbona tutakoma, ntakesha hapa..... Kuke kwengine kwa chai chungu sitaki hata kusogea nishaona nutakuwa addicted loh
 
Last edited by a moderator:
2013, bado tunaogopa majini badala ya umaskini?

Yako wapi?
Mbona mie sijawahi yaona?

Mie hg wangu kidogo ashambuliwe ni 'mwanga' kisa ana vifurushi visivyoeleweka mara maganda ya karanga mara nini.
Nikasema tu, mwacheni aamini aaminiyo, sie haitudhuru.
 
2013, bado tunaogopa majini badala ya umaskini?

Yako wapi?
Mbona mie sijawahi yaona?

Mie hg wangu kidogo ashambuliwe ni 'mwanga' kisa ana vifurushi visivyoeleweka mara maganda ya karanga mara nini.
Nikasema tu, mwacheni aamini aaminiyo, sie haitudhuru.

LOL! Wazungu sasa hivi wanahangaika kujua kama kuna uwezekano wa watu kuishi kwenye sayari nyingine sisi huku waTanzania tunahangaika kufikiria ni namna gani ya kupambana na majini na chuma ulete. Mweeeh! Africa (Dark continent) ni raha sana.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Tunasubiria mkuu lakini chonde chonde usitufanye tukeshe kama CHAI TAMU Ooooh!! sorry, CHAI CHUNGU
 
Kongosho huamini MAJINI mpaka uyaone mkuu???? kwani MUNGU umewahi kumuona kaka???? mbona unaamini kwamba Yupo!!
 
Nilipanga Nyumba Moja na Majini -3

"Wale wapangaji wenzangu siwaelewi kabisa."
"Kivipi?"
"Ah! Watu gani mimi mgeni nimehamia washindwe kutoka kunisalimia ili angalau tufahamiane?"

Dalali alicheka sana kisha akasema:

"Wale ndivyo walivyo bwana, si unajua tena malezi, mwingine kalelewa vile, mwingine hivi. Ila ulichokisema ni kweli, haiwezekani nyumba mnayoishi mpate mgeni halafu msitambuane, sasa mkikutana njiani je?"

"Si ndiyo hapo sasa," nilisema nikijifanya lawama zangu ni kwa ajili ya hilo tu, lakini kumbe nilikuwa na zaidi ya hapo.

Kazini siku hiyo nilishinda sina amani, sina raha, mwili ulikuwa kama umetoka kufanya kazi nzito ambayo sijawahi kuifanya kwa siku nyingi, wenyeji wa Pwani wanaita mavune.

Kwa upande mwingine nilitamani sana jioni ifike ili nikaone siku hiyo kitatokea kitu gani kipya kwenye nyumba ile. Jioni ilifika, nikaondoka kazini, sikutaka kupitia popote, dukuduku langu lilikuwa kwenda nyumbani tu.

Nilichukua kama saa moja kutoka kazini hadi kufika nyumbani. Nje nilikuta mfuko wa rambo mweusi, ndani yake ulionekana kuwa na kitu kwani ulikuwa umetuna sana. Niliinama kuipekenyua ili nijue ndani kulikuwa na nini, nilishangaa kuona ni vipande vya nyama za kuchoma tena vilikuwa vya moto.

"Kha! Atakuwa nani ameweka?" nilijiuliza mwenyewe, nikauacha palepale, mimi nikapanda ngazi za kuingia ndani. Mlango ulikuwa wazi hali iliyoashiria kwamba, wenzangu walisharudi. Nilisukuma mlango, nikaingia. Nilikutana na harufu ya pafyumu, nikahisi walikuwa wakijiandaa kutoka.

"Jamani za leo?" nilisalimia kwa sauti ya juu licha ya kwamba, mlango wao ulikuwa umefungwa, hakuna aliyeniitikia, hilo sikulijali sana kwani niliamini kwa kuwa walikuwa ndani, isingekuwa rahisi wasikie salamu yangu.

Niliingia sebuleni kwangu, kisha nikaenda chumbani, kuna kitu kilinishangaza, nikasimama kwa mshtuko. Nilikuta sehemu nilipoweka kiberiti asubuhi siyo, nilikiacha juu ya meza, nikakikuta juu ya kitanda. Niliacha kioo na kitana juu ya kitanda, lakini nikavikuta kwenye stuli, niliguna!

Nilikishika kioo na kukiangalia kwa umakini kama kina mabadiliko yoyote, lakini sikuona, nikashika kitana. Nilipokigaua sana pia sikuona kitu cha tofauti, nikaamua kuchania, nikahisi kuguswa na kitu kama nywele ndefu kama za mtu aliyefuga. Nilikiweka kitana juu usawa wa dirishani, nikaona nywelenywele nene, nyeusi, mwili wote ukasisimka.

Ninavyojua mimi, mwanamke mwenye nywele nyingi akichania kitana, ndiyo huacha nywele, sasa mimi nilikuwa na nywele fupi sana zisingeweza kuacha nywele ndefu kwenye kitana.

"Mh! Hapa kuna kinachoendelea," nilisema moyoni huku nikikaa. Nilishtuka zaidi kuona soksi zikiwa kwenye msumari nyuma ya mlango wakati niliacha chini.

"Huyu ni nani?" niliuliza kwa sauti ya ukali.

Ghafla nikasikia kicheko kutoka chumbani kwa wale wenzangu. Nilikaa kwenye kochi, nikaanza kuangalia sehemu mbalimbali za mle ndani ambazo niliamini naweza kuona mabadiliko mengine mbali na yale ambayo nilishayaona, lakini sikubahatika.

Nilitoka, nikaenda sebuleni ambako nako nilianza kuangalia kila kona ya sebule. Nilishangaa kuona glasi ya maji ya kunywa ambayo niliitumia asubuhi kisha nikaacha maji yamejaa, ikiwa haina hata tone la maji mbaya zaidi, iliwekwa juu ya kabati ambapo mimi niliiweka kwenye meza ya katikati ya sebule.

"Mh! Hii kali sasa," nilijikuta nikisema kwa sauti, mara nikasikia kicheko tena kutokea upande wa pili kule kwa wenzangu. Sasa nikaanza kama kuhisi kitu kuhusu watu hao. Ni kwa nini kila nilipoongea kwa sauti ndipo na wao waliangua kicheko?

Niliamua kujaribu tena, nikasema kwa sauti:

"Nitakuja kuua mtu, kweli tena." Nikasikia kicheko tena, safari hii kilidumu kwa muda.
Moyoni nikasema naanza kufanyia kazi uhusiano wa maneno yangu na vicheko vya wale majirani. Nilitoka kurudi chumbani, wakati napita kwenye korido, nilisimama jirani na mlango wao. Walikuwa wakiongea, lakini niliposimama mimi, kukawa kimya ghafla kama hakuna watu.

Nilipozama chumbani, nyuma wakaanza kuongea tena. Sikufunga mlango ili niweze kusikia wanachokiongea, lakini jamani kwa kusema ule ukweli wa Mungu, sikujua walikuwa wakitumia lugha gani katika kuwasiliana hata pale nilipojitahidi kutega masikio kwa umakini wa hali ya juu sana.

Kuna wakati utadhani wanatumia sana neno dotikom, lakini ukisema usikilize zaidi unasikia wakisema sana kotoko au kiburate, wakati mwingine sauti ya kike ilisema kaunto, ya kiume ikarudia hivyohivyo, kaunto.
Nia yangu kubwa ilikuwa kuwaona kwa sura na kufahamu kama ni ngozi nyeusi au nyeupe. Hilo peke yake lingenipa mwanga ni watu wa aina gani naishi nao pale ndani ya nyumba.

Nilisikia mlango wa chumbani kwao ukifunguliwa na mimi nikatoka haraka sana, cha ajabu sikuona mtu akitoka lakini mlangoni kulikuwa na kandambili pea moja tu wakati zilikuwa pea mbili.

Hilo lilimaanisha kwamba, mmoja wao alitoka kwenda chooni, nilichofanya ni kuamua kusimama katikati ya mlango wangu ili huyo aliyekwenda chooni akirudi nimuone. Ni kweli mmoja wao alikwenda chooni kwani nilisikia mlio wa maji.

NilijiTahidi kusimama mlangoni kwangu kumsubiria. Kwa ramani ya nyumba ile ilivyo, asingeweza kutoka chooni bila mimi kumwona hata kama angekuwa anataka kutoka kwenda nje au uani.

Mlio wa maji ulikosa kusikika, nikawa natumbulia macho kule huku moyoni nikisema: "Leo ndiyo leo, asemaye kesho mwongo, hata afanyaje, hawezi kunichenga hapa hata kidogo," nilisema moyoni, ingawa wakati huo mapigo ya moyo yalikuwa yakinienda kwa kasi.
Nilipoanza kuhisi muda unakwenda na hakuna mtu aliyetoka, nikampa dakika tatu kwamba lazima atakuwa anavaa ndiyo maana anachelewa: "Labda alikuwa anajisaidia haja kubwa, maana wengine huwa wanavua nguo zote, lakini mimi nipo, siendi kokote," nilisema moyoni nikiwa bado nimesimama mlangoni kwangu.

Baada ya muda, nikasikia watu wakiongea chumbani kwao, nikashtuka, nilijikuta nikisema: "Haa!"

Haraka sana nilitupa macho mlangoni kuangalia kandambili, nikazikuta pea mbili, nikashangaa: "Ina maana amenipita hapahapa au? Haiwezekani, asingeweza kunipita hata kama ingekuwaje?" niliwaza. Nilitoka kuelekea chooni, nikakuta mlango uko wazi, nikachungulia ndani, hakukuwa na mtu, nikanyoosha mikoni, nikarudi ndani.

Nilifikia kwenye kochi sebuleni, nikahema kwa nguvu kwani niliamini nimo ndani ya miujiza mikubwa ya ndani ya nyumba ile.

"Hivi ni kwa nini dalali alinidanganya hivi?" nilijiuliza mwenyewe nikiamini kwamba, dalali aliyenipangisha nyumba ile alijua mchezo mzima ila alitaka kupata fedha tu ndiyo maana alinipangisha bila kunipa tahadhari.

Nilitoka sebuleni, nikaenda chumbani, kitandani nikakuta 'toilet paper' ikiwa imekatwa sehemu. Mimi niliicha pembeni ya dirisha, lakini ikaonesha kuna mtu aliichukua na kunyofoa kidogo kisha badala ya kuirudishia palepale, yeye aliiacha kitandani.

Mbali na 'toilet paper' pia kuna kikopo chenye vijiti vyenye pamba za masikio kilikuwa kwenye stuli jirani na kitanda, lakini kwa muda huo kilikuwa kimeanguka chini halafu vijiti vimebaki kama vitatu tu kwa maana kwamba, aliyeingia kuchukua 'toilet paper' ndiye huyohuyo aliyechota vijiti vya pamba.

Nilianza kuhisi kuwa sikuwa kwenye nyumba salama, lakini kwa uthibitisho upi? Moyoni nikasema nitajua tu, mimi ndiyo mimi.

Nilikaa ndani kwangu hadi usiku ulipoingia, nikasema nibadili nguo kwa kuvaa bukta na singilendi halafu nitoke kwenda kula gengeni kwani siku hiyo sikuwa najisikia kupika chochote. Ni mara nyingi nilipenda kula gengeni.

Nilitoka, nikasimama mlangoni ili nifunge mlango wa chumbani, nilipoangalia chini, upande wa wenzangu nilikuta nje ya mlango wao pana vijiti vya pamba za masikioni vikiwa vimetumika, nikiwa katika mshango, mbele nikaona tishu ikiwa imefutiwa majimaji yenye rangi nyekundu kama damu.

Nilitembea kwa wasiwasi, nikatoka nje, sikufunga mlango kwa funguo, lakini niliubamiza tu, funguo nilikuwa nazo, nikaenda gengeni kula.

Pale kwenye genge ambapo si mbali sana na nyumbani, alikuja yule mama aliyeniuliza mimi ni mtu wa wapi, nilimsalimia, lakini kabla hajaitikia alishtuka kuniona.
"Upo kijana wangu?"
"Nipo mama, nimetoka kazini nimekuja kupata kidogo."
"Pole sana, uoe sasa."
"Huo ndiyo mpango wangu mama."
"Ee, uoe halafu mimi nitakupa vyumba viwili pale kwangu, nakuahidi."
"Nashukuru sana mama. Naanza kujipanga."
"Sawa, vipi wenzako lakini?"
Nilisita kumjibu, nikabaki namwangalia tu, naye alibaini kwamba nimepata mshtuko na swali lake.
"Vipi wapangaji wenzako, naamini utakuwa hujaonana nao?"
"Ni kweli mama, tena hebu nakuomba kidogo," nilisema nikienda pembeni kidogo ili na yeye anifuate tukaongee.
"Niambie," alianza kusema.
Nilimuuliza kama kuna anachokijua chochote kile kuhusu wale wapangaji wenzangu. Alianza kwa kusema:
"Kusema ule ukweli sina kwa undani, ila napenda kukwambia kwamba, unaishi na watu ambao unahitajika moyo wa ziada ili uweze kuendelea kuishi nao.
"Pale mbali na wewe, pameshakaa wapangaji wengine saba, tena wote kama wewe, hawajaoa. Lakini kinachoshangaza ni kwamba, wanaondoka baada ya wiki mbili, mmoja aliondoka baada ya siku tatu tu."
"Kwa hiyo hakuna hata mmoja aliyewahi kukwambia ameona nini kule ndani?"
"Hakuna."
"Lo! Mimi mama mambo ninayoyaona yanatisha."
"Kama mambo yapi, nisimulie kidogo."
Nilipotaka kuanza kumsimulia huyu mwanamke, ghafla alitokea msichana mmoja, mweupe, mrefu kiasi, amejazia sehemu mbalimbali za mwili, akaguna na kusema:
"Kaka Humuli mambo vipi, za siku?"
Nilipata kigugumizi kikubwa kumjibu mambo poa kwani sikumjua na sikuwa nakumbuka chochote kuhusu yeye, sura yake ilikataa kichwani mwangu.
"Wewe ni nani kwani?" nilimuuliza.
Akaachia tabasamu kwa mbali, uzuri wake ukaongezeka.
"Ha! Humuli, hunikumbuki mimi, kweli?"
"Sikukumbuki hata kidogo."
"Sasa we binti, kama wewe ndiyo unamkumbuka si umkumbushe mlionana wapi?" yule mwanamke alisema kwa sauti ya mshangao.

Lakini yule msichana mrembo alimwangalia yule mwanamke kwa macho yaliyojaa hasira&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];
"Mama uhusiki."
"Najua, lakini unapoteza muda kwa kuzungushazungusha wakati kumbe wewe unamkumbuka, yeye umeshajua hakukumbuki na amekwambia tayari."
Nilishangaa kumwona yule msichana akibetua kichwa kama aliyekuwa akiweka vizuri nywele zake, ghafla yule mwanamke niliyekuwa naye akajishika kichwa na kulalamika kinamuuma sana.
"Jamani kichwa! Kichwa jamani, daa!"
"Vipi mama, imekuwaje kwani?" nilimuuliza.
"Kichwa Humuli, kinavuta ghafla! Uwiii."
Nilianza kuogopa, nilihisi naangukiwa na msala maana akifa pale na watu waliona nikienda naye pembeni si nitahojiwa mimi?
"Kwani mama una kawaida ya kuumwa kichwa?" nilimuuliza nikimsogelea ambapo yeye sasa alikuwa ameinama.
"Sina, ndiyo nashangaa hapa."

Niliona hakuna dawa nyingine zaidi ya kumpeleka kwake ili nikaungane na familia yake kumpeleka hospitali. Lakini kabla ya kufanya hivyo niliinua macho ili nimwambie yule dada anisaidie na kama anataka kunikumbusha, hayo yangefanyika baadaye.

Ile naanaza kusema anti huku nikiwa nimeinua macho, nilishangaa kutomwona yule msichana pale.
"Khaa!" nilijikuta nikisema hivyo.
"Mama twende nyumbani ili tukupeleke hospitali na watoto wako."
"Ha! Mbona kimeachia," alisema akionekana kushangaa na kuniangalia, alikuwa amepanua kinywa.
"Kweli?"
"Eee, niko mzima kabisa."
"Au?" nilitaka kusema neno lakini zikulimaliza, nikahisi ulimi unakuwa mzito si kwa kushikwa bali kwa matakwa yangu.
"Humuli."
"Naam."
"Ni kweli yule binti humjui?"
"Simjui mama."
"Kuna mawili hapo, humjui au humkumbuki."
"Vyote mama, simkumbuki na pia simjui."
"Lakini wewe si alikutaja kwa jina?"
"Mwenyewe nilishangaa sana."

"Basi Humuli nimeshaelewa, kwaheri, nimeelawa ni kwa nini nimeugua kichwa na yule ni nani, pole sana wewe kijana," alisema yule mwanamke huku akiondoka zake kuelekea kwake.
Nilimtazama, lakini baadaye nilirudi kwenye kibanda cha chipsi.
"Mzee nakuona na miss jini," muuza chipsi mmoja alisema.
"Yupi, yule mwanamke?"
"Hapana, yule msichana."
"Mi simjui, kwani anaishi wapi? Maana kasema ananijua, ameniita na jina."
"Khaa! Kumbe wewe kama sisi. Huyu dada anaishi mitaa hiihii, lakini hakuna hata mmoja anayejua nyumba anayoishi!

"Kuna jamaa mmoja anaitwa Maleke, Maleke aliwahi kumfuatilia kwa nyuma lakini alishindwa kujua aliingia nyumba gani!"
"Mh! Au jini?" niliuliza kwa mshtuko mkubwa.
"Ndivyo watu wanavyosema, sasa alipokuja kusimama na wewe, tukawa tunabishana, wengine wanasema ni miss jini, wengine siye, lakini alipokuwa anaondoka tukagundua ni miss jini."

Basi, tuliishia hapo, nikachukua chipsi zangu na kwenda nazo nyumbani, niliamua kwenda kulia kule.

Nilifika, nikasukuma mlango mkubwa nikazama ndani kwangu. Lakini wakati napita kwenye usawa wa chumba cha wale wenzangu nikasikia vicheko, tena vicheko kwelikweli.

Sikuwajali, nikaingia sebuleni kwangu, nikafunga mlango kwa ndani, nikaweka chipsi juu ya meza, nikaenda pembeni ya chumba ambako kuna ndoo ya maji ili nichote ya kunawa. Wakati naanza kula nilihisi na kugundua kitu. Niligundua mabakimabaki ya chipsi na kuku juu ya meza yangu wakati ukweli ni kwamba, tangu nimehamia pale sikuwahi kula chipsi wala kuku.

"Humu ndani kuna mtu anaingia kufanya mambo yake, lini mimi nimekula chipsi na kuku humu ndani?" nilijiuliza, nikasikia kicheko kutoka kwa wenzangu.

"Haa! Haaa! Ha! Haaaaaaaa."

Niliinua macho kuangalia juu kwenye 'silingbodi' kama vile niliyekuwa nimeona kitu, akili yangu ikawaza kitu cha dakika chache nyuma, nacho ni hiki:

"Humuli."
"Naam."
"Ni kweli yule binti humjui?"
"Simjui mama."
"Kuna mawili hapo, humjui au humkumbuki."
"Vyote mama, simkumbuki na pia simjui."
"Lakini wewe si alikutaja kwa jina?"
"Mwenyewe nilishangaa sana."
"Basi Humuli nimeshaelewa, kwaheri, nimeelawa ni kwa nini nimeugua kichwa na yule ni nani, pole sana wewe kijana."
Je, ni kwanini Humuli aliyarejea mazungumzo yake na yule mwanamke aliyeumwa kichwa ghafla?

Fuatilia baadae, HAPA - SEHEMU YA SITA
 
Back
Top Bottom