Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,175
- Thread starter
- #361
SEHEMU YA 105
Dickson na Nandy walikuwa wakirudi jijini Dar es Salaam wakitoka katika Visiwa vya Zanzibar ambapo walikwenda kwa ajili ya fungate yao.
Mioyoni walikuwa na furaha tele kwani baada ya kupitia vikwazo mbalimbali hatimaye wawili hao walikuwa wameoana na kuwa pamoja.
Ndani ya boti kila mtu alikuwa akiwaangalia, hawakuamini kama watu hao ndiyo walikuwa wameoana huku mwanaume waliyekuwa wakimwangalia, aliyekuwa na sura nzuri ndiye aliyeamua kumuoa mpenzi wake huyo huku akiwa amepooza.
Walionekana kuwa na furaha kupita kawaida, mule ndani walikuwa wakizungumza mambo mengi na watu wengine, hawakusita kuwaambia kuhusu muujiza wa Mungu ambao angeufanya baadaye katika mwili wa Nandy.
Kila mtu aliiona imani yao, hawakutaka kuwa na hofu na kitu chochote kile kwani kwa kila kilichokuwa kikiendelea waliamini kwamba ulikuwa ni mtihani tu ambao mwisho wa siku kulikuwa na matokeo yake.
Walipofika Dar es Salaam, wakapokelewa na ndugu, jamaa na marafiki na kuelekea nyumbani. Maisha kama wanandoa yakaanza, kila siku Dickson alikuwa akienda kazini alipokuwa akisimamia biashara nyingi za baba yake na kurudi jioni.
Mapenzi yalikuwa motomoto, kila alipokuwa akirudi nyumbani alikuwa na zawadi kwa ajili ya mke wake huyo ambaye mpaka katika kipindi hicho hakukuwa na maendeleo yoyote mwilini mwake zaidi ya kuwa vilevile kama alivyokuwa kipindi cha nyuma.
Baada ya kukaa kwa siku kadhaa ndipo Dickson akapigiwa simu kutoka katika Kituo Kikuu cha Polisi na kuambiwa kwamba kulikuwa na mzigo wake kutoka gerezani.
Hakujua ulikuwa ni mzigo wa nini, hakujua alipelekewa na mtu gani. Muda huo aliopigiwa simu alikuwa akirudi nyumbani kwake, akakatisha safari, akakata kona na kuelekea huko.
Njiani alikuwa na mawazo mengi, alichanganyikiwa, alijitahidi kukumbuka kama kulikuwa na mtu aliyekuwa akimfahamu huko mpaka kutumiwa mzigo wake lakini hakukumbuka kitu chochote kile.