Mbobo
JF-Expert Member
- Jan 13, 2017
- 1,395
- 1,822
Mkuu Jack Daniel ukipata free time endelea kutubariki na sehemu za kutosha tulioko safarini angalau tuburudike na simulizi hii mujarabu.
beb moneytalk upite hapa leo sijakuona kabisaSEHEMU YA SITINI NA NNE
Hebu kwanza futa machozi hayo ina ukilia ndiyo ndiyo inasaidia nini wewe ni mtoto wa kiume bwana, acha habari zako! aliongea Mzee Mgaya huku akimsogelea Samson taratibu.
Njoo baba yangu njoo ndani, eeh eti baba kuna nini kimetokea, kwasababu si kawaida yako kuja ukilia hivyo mwanangu eeh Kuna Nini? Halafu baba Jose na wewe usimkaripie mtoto wakati hujui kapatwa na nini siyo vizuri lakini ni vyema ukauliza upate jibu kwanza. aliweka kituo mama Kulwa huku wakiketi Kila mmoja akiwa na shauku ya kutaka kujua nini kinaendelea.
Mwalimu kanifukuza shule, kasema taratibu za uhamisho hazikukamilika.
aliongea Samson huku akifutwa machozi na mama Kulwa.
Mzee Mgaya na mkewe waliangaliana kitambo kidogo, huku kukiwa hakuna aliyemuongelesha mwenzake,
Mzee Mgaya aliinuka na kwenda chumbani ambapo alikaa kama dakika tano na kurudi sebuleni akiwa na begi fulani na kuchukua karatasi kama nne akampa mkewe azisome. hakuna aliyeongea chochote.
Hatimaye mama Kulwa akavunja ukimya,
Mmmmh, hii sasa balaa nadhani mwalimu ana mambo yake kwasababu mbona kama hizi karatasi zimetimia Kila kitu, halafu sidhani kama angepokelewa,kama taarifa zisingetimia, halafu mbona mambo yanazuka Sasa hivi, mambo yana miaka miwili yote?
Mama Kulwa alimwambia mumewe huku akimwangalia usoni.
Hapa mke wangu hatuna namna tena,tunatakiwa tuwe wapole na tuongee na mwalimu mkuu, kinyume na hapo huyu atachelewa zaidi na masomo yake na kujikuta anapitwa na vitu vingi. Kesho nitaenda shuleni kwao nitaongea naye mwalimu. aliongea Mzee Mgaya kwa upole sana huku taarifa ile ikionesha imemnyong'onyesha.
Eti baba Jose, kuna kitu kama kinanijia hivi,isijekuwa lile tatizo la yule mwalimu ndiyo anaamua kulipa kisasi eeh? aliuliza mama Kulwa
Mke wangu hujauliza swali bali unauliza majibu, hakuna kingine ni hayo tu. alikatisha Mzee Mgaya.
Aaaaah hapana kama ni hivyo huyu twende kwa maafisa wake tu, tutaanzia ngazi ya wilaya hadi Mkoa mtoto wetu atasoma tu, Wala hapaswi kumbembelezwa, asituletee ujinga wake, halafu nilikuwa namheshimu sana yule mwalimu mkuu, sikutegemea kabisa yeye kutetea mtu mjinga na mbakaji, badala yake nilifikiri angechukua hatua kwa mwalimu wake ili iwe fundisho kwa wengine.
Kumbe ni (akitoa tusi)
tatizo mnamdekeza Mimi ndiyo maana nilikwambia masuala haya ya Rahma sisi tukashitaki tu, wewe ukawa na pingamizi, Sasa hata haya tunaweza kwenda hata wizarani, Nini shida haiwezekani? mbona tunaweza kufichua maovu mengi tu, unadhani ni watu wangapi wanakosa haki zao kwasababu ya kukandamizwa na watu wenye roho mbaya kama hizi.
Hapana, Mimi sitakubali na nitasimama na huyu mtoto.
aliongea mama Kulwa kwa kujiamini.
(Huku akicheka kicheko fulani cha kivivu)
Mke wangu, wakati mwingine lazima ujue kuwa hapa Duniani hakuna haki Bali Kuna sheria nayo inatakiwa ifuatwe, vyombo husika vitaitafsiri sheria, na baadaye atakayekutwa na hatia hatua stahiki zitadili naye.
Lakini pia hata kama sheria iko upande wako na unajiona mwenye haki, lazima ujue kuwa hapa Duniani hatuwezi kuwa sawa kila mmoja, tabia zetu, maumbile yetu,haiba zetu na vitu vingi tumetofautiana.
Lingine mke wangu usipende kukaza sana kwenye Kila kitu, wape ushindi watu hata kama unaona hawastahili , kwakuwa hakuna madhara kwako au hakuna ulichopungukiwa, hii ndiyo Dunia, umesahau tulikuwa na kuku wetu watatu humu ndani tulipewa zawadi na watu wenye roho nzuri lakini wakaibiwa ndani ya siku tatu tu,mke wangu ulihamaki na ukawa unamhisi mwizi wetu na hata majirani walidai walimuona lakini nilikuzuia.
Kwanini? niliona ni vyema ukaachana na mambo mengi, tuna vitu vingi vinalala nje, Kuna magari Kuna vitu vingi vya thamani, lakini mwizi aliona Bora aibe kuku.
Mke wangu suala la Rahma kwakuwa hakubakwa, na yupo salama, tunatakiwa tuongeze ulinzi dhidi yake. Kama tulivyoongeza kozi kadhaa kwenye fence yetu ili kupambana na vibaka.
Tukirudi kwenye suala la Samson, ni dogo sana, yule mwalimu Mimi nitaongea naye, lazima niwe mpole hakuna jinsi,lazima nitaonana naye
alifafanua mzee Mgaya.
Halafu na wewe Samson unaona haya yote, Mimi wanangu wote nimesomesha na wanapambana na maisha yao, wamebaki wale mapacha ambao nao hawanisumbui kwakuwa sikai nao, Sasa basi jitahidi kuwa na nidhamu humu ndani. Siyo Mimi nahangaika halafu unanikatisha tamaa , sitapenda. aliweka kituo mzee Mgaya.
Sasa mke wangu kama nilivyokwambia, nimepata nafasi ya uvunaji wa miti ya furniture huko Ikwiriri njia ya kusini maana nilituma maombi na nimekubaliwa, hivyo naondoka Leo hivyo tafadhali naomba unipe gari lako maana njia ni mbaya Sasa kwa kutumia usafiri wa umma nitachelewa mambo yangu. aliongea kwa kubembeleza Mzee Mgaya.
Sawa ila tafadhali hilo gari baba, siyo Land cruiser hiyo najua mwendo wako, Mimi hiyo inanisaidia kwa mizunguko yangu hapa mjini, lakini si gari la maana la kwenda nalo huko wapi.mama Kulwa hakuacha masimango .
Gari ni gari tu mke wangu tena niendako hakufiki hata kilomita mia mbili nadhani masaa mawili na nusu nitakuwa nimefika na naondoka Leo Leo. aliaga Mzee Mgaya.
Sasa baba masuala yangu yatakuwaje? aliuliza kwa hofu Samson maana aliona ni makubwa halafu Mzee Mgaya anarahisisha na Kuna muda ni kama hajali hivi , akawa na hofu kubwa na alikosa raha.
Mimi narudi kesho jioni, maana leo naenda kulala shamba, kesho nakamilisha mambo yangu kule na kesho hiyo hiyo nageuka na jumatano asubuhi wewe jiandae unaenda shule kama kawaida. mzee Mgaya aliongea huku akitaka afunguliwe geti ili aondoke.
************************************
Kesho yake ambapo ilikuwa ni siku ya jumanne Samson, aliamka na kuendelea na kazi za pale nyumbani lakini Kila muda moyo ulimuuma akiona huenda akaacha shule kabisa akajikuta anakosa Raha hata kula ilikuwa kama anajilazimisha tu.
Mwanangu Samson baba yako atarudi leo na Namuamini Mzee Mgaya ataweka mambo sawa na utaendelea na masomo, Wala usijali wewe niamini Mimi na kesho wewe unaenda shule baba yako si alisema?
Kuwa na amani mwanangu. aliongea mama Kulwa akiwa anamliwaza Samson asiumie sana.
Geti liligongwa kwa nguvu huku Samson akienda kufungua kwa unyonge sana, macho yakagongana na Cathy, huku Sam akiwa na wasiwasi kidogo kwani juzi tu alimfanyia Cathy vitendo si vya kiungwana. Cathy alienda moja kwa moja hadi kibarazani alipokaa mama Kulwa wakasalimiana.
Mama nimekuja kukuomba msamaha, naomba nisiongee mengi sana, ila wewe nisamehe tu mwanao. aliongea Cathy huku akitoa tabasamu.
Mimi Sina neno ila niliwaza mwanangu kapatwa na nini, au nimemkosea jambo?lakini nashukuru kama hamna tatizo. aliweka kituo Mama Kulwa.
Mama gari lako liko wapi tena,
Maana umegeuza Taxi gari halikai nyumbani. alitania Cathy.
Baba yako Mzee Mgaya kalichukua, Tena tangu Jana na alisema anarudi leo.
Mamaa bwana kweli mapenzi ya watu usiyaingilie, nakumbuka kipindi kile unasema Mzee Mgaya hataendesha hata siku moja gari lako, nikakuambia usimalize maneno mama yangu. Cathy alizidi kumchokoza mama Kulwa maana alikuwa muongeaji sana.
Mwanangu ndoa ni kama gereza wakati nwingine, na gerezani mtu unaishia kwa amri Sasa Kuna vitu nashindwa kujipangia, hivyo unaacha mambo yapite ,
Tumezaa watoto, tunazeeka pamoja hivyo Kuna vitu vingine hupaswi kukaa misuli kushindana navyo. alifafanua mama Kulwa.
Dah ndiyo maana nakukubali mama yangu Kila nikija huwa naondoka na jipya, MUNGU akubariki, lakini mama mbona Leo hii ni jumanne halafuu hajaenda shule vipi? aliuliza Cathy.
Huyo anajisikia vibaya nadhani anaumwaumwa ,naona ataenda kesho alijibu kifupi mama Kulwa.
Basi namuomba akanisaidie kazi fulani pale home, eti Sam kwani unajisikia vibaya sana, aliuliza Cathy huku akimwangalia Sam usoni.
Samson nenda na dada yako ukamsaidie kazi anayosema kwanza nenda ukapajue kabisa, maana siku utatumwa kwake halafu usumbuke. masikini mama Kulwa, hakujua chochote kinachoendelea kwa wawili wale.
Samson alifurahi sana huku akisahau baadhi ya shida zake kwa muda.
Itaendelea.....................................
Hiii iachwe tuUtoe iyo avatar mkuu Mana mnanitisha
Yaani hata mm nmeshangaa aisee, sijui kwann watu Wana makasirikio hv khaaaa😡
Umenisikitisha sana Mkuu, jaziba za nini? Jitahidi kuitafuta amani ya moyo na maisha yako utayafurahia
Pole SANAAA Mkuu ndio binadam walivyo, anajijali zaidi yy pasipo kuangalia upande wa piliNdugu wapenzi na wafuatiliaji wa simulizi hii, napenda kuwakumbusha kuwa Mimi ni mpenzi wa simulizi nyingi sana humu jamvini,huku Kulwa langu pendwa zaidi ikiwa ni kule Jamii intelligence
Kwa maana hiyo nikawiwa kuandika na Mimi simulizi zangu ili tuburudike pamoja.wakati mwingine hizi simulizi hata usiposoma Wala kufuatilia hazikuongezei chochote wala hazikupunguzii chochote.
Mimi siuzi vitabu wala sifanyi biashara hizo Bali ni kwaajili ya burudani hivyo naomba tuheshimiane Wala Haina sababu ya kutukana au kumtolea mtu lugha chafu.
Tuheshimiane wananzengo.
Loading....................inaendelea
ndo napita sasa hivi babe
Mama Kulwa sometimes mtu sometimes anakuwa kalishwa pilipili kuchaaSEHEMU YA SITINI NA NNE

Binadamu hatujakamilika Mkuu utusamehe tu tunapo kukosea.Ndugu wapenzi na wafuatiliaji wa simulizi hii, napenda kuwakumbusha kuwa Mimi ni mpenzi wa simulizi nyingi sana humu jamvini,huku Kulwa langu pendwa zaidi ikiwa ni kule Jamii intelligence
Kwa maana hiyo nikawiwa kuandika na Mimi simulizi zangu ili tuburudike pamoja.wakati mwingine hizi simulizi hata usiposoma Wala kufuatilia hazikuongezei chochote wala hazikupunguzii chochote.
Mimi siuzi vitabu wala sifanyi biashara hizo Bali ni kwaajili ya burudani hivyo naomba tuheshimiane Wala Haina sababu ya kutukana au kumtolea mtu lugha chafu.
Tuheshimiane wananzengo.
Loading....................inaendelea
Cathy anaenda tena kupigwa mpini na dogo Sam. Daaah imeishia patamu sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
apa nasubiri kwa usongo naona kama Jack Daniel anachelewesha hiviCathy anamuomba Samson akafanye kazi ili ambandue.SEHEMU YA SITINI NA TANO
Samson aliingia kwenye gari la Cathy akiwa na amani fulani , akiwa kasahau kwa muda matatizo yake.Walienda kimyakimya huku wakiwa hawaongeleshani , huku Samson akimtupia jicho Mara mojamoja Cathy ambaye alikuwa bize na usukani wa gari.
Huyu naye vipi na Lori lake, huku anatafuta nini, anataka kutuchelewesha tu huyu. alilaumu Cathy baada ya Lori lililokuwa linageuza kutumia muda mwingi sana, akapenyapenya pembeni na kufanikisha kutoka huku likimtoka tusi zito sana Cathy. Yaani hawa ni wajinga sana Sasa huku barabara zilivyobana anageukaje pale, lengo ule mkontena aangushe kwenye nyumba ya watu tu. loooooh alionesha kukasirika sana Cathy.
Hatimaye walifika huku Cathy akifungua geti ambalo alibana na funguo kabisa,
Ikabidi Samson aulize,.
Kwani yule dada yuko wapi? Naona ulifunga kabisa.
Yule kasafiri kidogo kaenda kwao, siyo mbali ni hapahapa mjini na nitamfuata na gari baadaye. alijibu Cathy, akiwa anamkaribisha ndani Samson, karibu mwaya Sasa naomba tusaidiane tuset hili kabati jipya, likae vizuri maana kila nikijaribu siwezi.
Lilikuwa kabati fulani la nguo zuri na la kisasa, huku likiwa na urembo fulani kama dhahabu haswa zile komeo zake.
Dah hongera sana Mimi ile juzi nilishangaa unalitoa kabati zuri kabisa nikashangaa sana mbona kitu kinadai kabisa hiki. alisema Samson
Ni kweli kabati mbona bado liko vizuri lile, sema kwangu naona limepitwa na wakati, hivyo nimeamua kubadilisha.
Sasa hapa ndani limefikaje, maana kama mtu kalitoa dukani, kafikisha hapa ndani imeshindikana vipi kuliset likae mahala pake. aliuliza Samson.
Watu utawaweza ndugu yangu, nimetoka nao mjini , nikikodi gari lao Hadi hapo nje ya geti, wakadai wamefika, ikabidi niwaambie kuwa Sasa litaingiaje? wakadai niwaongeze hela, sikuwa na namna nikakubali wameingiza ndani huku wakilalamika oh hii kazi imeongezeka, Mara pesa ndogo yaani fujo tu, kufika hapa eti mtu kafika chumbani, nawaambia Sasa mbane hapo ukutani maana halijafika bado, wanataka hela tena eti,
Yaani mtu ukimpa kijikazi hapa mjini anataka shida zake zote atatulie hapohapo, nikawaambia acheni nikawalipa hela yao wakaondoka. aliweka kituo Cathy.
Sasa Mimi unanilipa shilingi ngapi, alitania Samson.
Kuhusu wewe utapewa hela yako wala usijali na pia si unanidai hela ya juzi wewe. aliongea Cathy huku akitabasamu kimahaba.
Eh nakudai, alijibu Samson huku akitazama chini hakutaka kukutanisha macho na Cathy.
Hata mimi pia nakudai ujue, tunadaiana mwenzangu, alisema Cathy na kumfanya Samson ainue kichwa kwa mshangao.
Cathy akaangalia pembeni kwa aibu.
Mwanamke ni mwanamke tu, kwenye hisia za lile tendo lazima uoneshe au na uwe chini kwa mwanaume hata kama una cheo cha aina gani.
Cathy aliinuka na kwenda kufunga mlango wake mkubwa na kurudi ndani, akawa kasimama mlangoni kana kwamba yeye ndiye mgeni, huku akionesha kama Kuna kitu anatafuta alizugazuga pale huku kimya kikiwa kingi hakuna aliyemuongelesha mwenzie. na Samson naye umeme wake wa chini ulikuwa kwenye high voltage kiasi cha kutaka kuunguza vitu, ila bado hakuna aliyemuanza mwenzie maana Samson bado alikuwa na uoga kwa kitendo alichofanya siku ile, aliona kama alimkosea sana Cathy. Masikini Samson utoto ulimsumbua alishindwa kujiongeza haraka.
Cathy alitoka tena nje ya chumba kile akimwacha Samson kakaa tu kitandani anasubiri aambiwe avae jezi husika wakati ni striker tegemeo hajui bila yeye hakuna litakalofanyika.
Masikini hofu ya kubaka ilimrudisha nyuma Samson
Cathy alirudi mle chumbani akiwa bize Mara afunue hapa Mara afanyaje,
Alionesha akitafuta kitu huku akiwa anasonyasonya Mara kadhaa, pengine aliona Samson ni Mzembe kwanini anashindwa kujiongeza.
Lakini baadae shetani alichukua nafasi kubwa, Sam akajiuliza kama nilichofanya siku ile angekuwa alikasirika , angeniita tena na leo?
Swali lile moja lilitoa majibu yote kwa Samson, ikabidi aanze kuvua Shati lake na kulitupia pembeni, akamshika Cathy kwa nguvu, na kumvutia kitandani,
Samuuuuh ushaanza fujo zako kama siku ile , mi sitaki bwana hebu niache , kwani lazima unifanye kila ukija, aliongea Cathy kwa sauti ya chini ya kulegea na kuzidiwa, Samson alishangaa mtu ambaye hataki, akiwa anaingiza mkono kwenye suruali yake, huku akiwa kafumba macho, lakini pia sura yake haikuonesha kama mtu asiyetaka. Samson akazidisha ufundi alimgeuza Cathy na kumlaza chali huku akimvua nguo zake , huku akishangaa mzigo wa shanga ambazo juzi hakuziona, kufumba na kufumbua walijikuta taabani huku Cathy akitweta akiwa anavuta kanga yake kwa aibu huku akimuinua Samson wakaingia bafuni kuoga. Baadaye walikuwa wakiagana huku Cathy akilazimisha amsindikize na gari lakini Samson alikataa huku sababu akizijua yeye.
Cathy alionesha kuchoka huku akimsifiasifia Samson ambapo alikuwa akijiongelesha mwenyewe,
Dah kweli usiidharau njiti Moja ya kiberiti kwani inaweza washa moto na kuunguza mji mzima yaani Samson mtu akikuangalia hawezi amini kabisa.
Cathy aliinuka na kuvuta droo ya kitanda na kutoa hela nyingi sana ikiwa ni malipo ya kazi zote ya jumapili na ya siku hiyo Samson aliweka pesa mfukoni na kuaga huku akijiona kidume sana maana Cathy huwa anajiona special sana labda kwakuwa hela haikuwa tatizo kwake.
Samson alifika pale home na kumkuta Rahma nje huku akiwa kama hayuko sawa, hakutaka kuhangaika naye kwani hakumuhusu lakini ile Samson anaingia ndani akashikwa mkono na Rahma.
Wewe Samson mbona umechelewa sana vipi, aliuliza Rahma kwa ukali.
Heee wewe vipi, hebu niachie asiniulize mama unaniuliza wewe kama nani hebu niache Rahma nitakupiga ujue. alitishia Samson.
Sawa haina shida Mimi sipaswi kukuliza siyo, halafu kule kwa Cathy ulienda kufanya nini kwanini usingekataa, Mimi sipendi uwe unaendaenda huko bwana. aliongea Rahma kwa sauti yenye mkwaruzo akionesha kukerwa sana.
Samson aliishia kushangaa huku akijiuliza huyu ama ni mchawi Sasa mbona Kila anachogomba kina ukweli, suala ni kwamba, kajuaje? Samson hakupata majibu ya haraka.
Vipi mama yuko wapi.
aliuliza Samson.
Yupo, katoka na baba Sasaivi, alijibu Rahma.
Kwani baba karudi.
aliuliza Samson kwa shauku maana ndiye mtu wa kwenda kumtetea shuleni kesho, hivyo kuambiwa karudi alifurahi sana.
Honi ya gari ilisikika huku Samson akikimbilia kwenda kufungua, gari likaingia huku wakishuka watu watatu Mzee Mgaya, mkewe pamoja na mke wa mwalimu mkuu, mmiliki wa baa kubwa pale mtaani kwao.
Karibu sana ndugu yetu, huyu ndiye yule kijana niliyekwambia , na wewe Samson hebu salimia watu, alaaaah.
Mzee Mgaya aliongea huku akimchimba mkwara Samson baada ya kumuona anajisahau.
Kwanza nawashukuru nyote kwa kudumisha uhusiano wetu wa siku nyingi nadhani ubize wangu kwenye ile biashara ndiyo unanifanya niwe mbali na nyinyi lakini na wewe shoga yangu umenisusa hauji kabisa pale kwangu, sijui umeokoka, maana Mara ya mwisho kuja nadhani miezi Saba iliyopita. aliongea mke wa mwalimu mkuu kwa utani.
Mwenzangu ubize tu, tangu niifungue ile biashara niliyokuambia basi situlii kabisa dada yangu. Hata hivyo usijali nitakutembelea tu.aliweka kituo mama Kulwa.
Mzee Mgaya alikuwa akiwasikiliza wanawake wale huku akijichekesha kwani yule mwanamke alikuwa msaada kwao wakati ule, akavunja ukimya.
Sasa shemeji tunaomba hayo yaishe na ongea naye jamaa yangu bwana Mimi nakuaminia shemeji.
aliongea kwa kujipendekeza Mzee Mgaya.
Kama nilivyokwambia shemeji kuwa yule mwalimu Sadick ni mwanangu ni mtoto wa kaka yangu kabisa, kaka yangu alimpata kipindi hicho akiwa kijana hivyo akawa Hana uwezo wa kumlea licha ya kususiwa, Mimi ndiye niliyemlea yule na kumsomesha kipindi hicho tuko mkoani morogoro, hivyo baada ya sisi kuhamia huku yeye tulimuacha kwa baba yake, kwani baba yake alikuwa ana msimamo tayari.
Baadaye tulisikia anajiunga na makundi ya uimbaji wa muziki ilihali yeye kasoma mpaka chuo cha ualimu nikasema mtoto wangu niliyemlea mwenyewe hawezi kupotea, ndiyo tukamfanyia mpango wa ajira huku, Alifafanua yule mke wa mwalimu mkuu.
Mzee Mgaya na mkewe waliangaliana Kisha wakaendelea kumsikiliza,
Hivyo nawaombeni basi legezeni masharti basi, maisha ni hayahaya, kwanza hatuna uhakika kama alitenda kosa Hilo Mimi Sadick namjua ana wanawake wengi sana kiasi Cha sisi kumuonya kuwa ajiheshimu hasa kwa wadhifa alionao Sasa kuja kusikia alitaka kubaka, hii Mimi sikuiamini ongeeni na Binti yenu vizuri. aliweka kituo yule mgeni
Basi shemeji hayo yameisha, fanya Kila uwezalo mshawishi Mr. Maana kijana atachelewa masomo. aliomba Mzee Mgaya.
Shemeji usijali hayo yameisha mbona wewe kesho mpeleke shule huyu kijana wetu.
Je, Samson atapokelewa kirahisi?
Vipi Rahma kwa Nini anamchukia Cathy kwanini amuombe Samson akamsaidie kazi.
Sehemu ijayo ina majibu.
Next episode is loading............................