Simulizi: Mchawi

Simulizi: Mchawi

Hii hadithi kiboko mambo ya Uganga haya mwisho na wewe unakuwa mchawi kabisa
 
Shunie mm nakusubiri et uendelee na kisa chetu pendwa
At leat leo iweke at vipande 4 hv siyo mbaya kuna wadau wapo tayari kukuchangia vocha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sehemu ya 45

“Jana mkeo alirudi,”
“Eeh!” nilishtuka kusikia vile.
“Basi juzi jioni alikuja mkeo na mwanao na kukusubiri mpaka usiku bila kutokea, ilipofika usiku ilibidi alale kwenye korido asubuhi ya jana ndiyo kaondoka. Jana tena alikuja hapa bila mtoto alikaa mpaka saa tatu usiku akaamua kuondoka.”


SASA ENDELEA..



“Atakuwa amekwenda wapi?”
“Mmh! Kwa kweli sijui ila ameondoka na kuniomba mizigo yake niiweke vizuri na kusema atarudi kesho. Nia yake kuingia ndani amesema anaweza kuja na fundi ili amfungulie mlango. Kwa nini hukuacha funguo?”
“Safari ilikuwa ya ghafla sana.”
“Basi kwangu kuna mizigo ya mkeo,”
“Sawa,” nilichukua mizigo ya mke wangu na kuiingiza ndani.

Baada ya kuweka vitu vya mke wangu vizuri nilikaa kwenye kochi nikiwaza na kuwazua kauli ya mganga na niliyoyasikia muda mfupi kuhusu mke wangu kurudi nyumbani. Nilijiuliza kama mke wangu karudi ni kweli yule mwanaume amekufa kwa ajali kama alivyonieleza.

Nikiwa katikati ya mawazo Simon alibisha hodi, nilimkaribisha apite ndani kwa vile mlango ulikuwa wazi. Simon aliingia akionesha kuna kitu anataka kusema, baada ya kuketi alisema:
“Pole na safari.”
“Asante.”
“Mmh! Mzee unatisha.”
“Kivipi?”
“Jamaa tumemzika jana.”

“Jamaa gani?”
“Si mgoni wako.”
“Muongo!”
“Kweli tumemzika jana, kwa kweli mimi na wote tuliosikia sababu ya kifo chake tulijua ni kifo cha kawaida lakini aliyonieleza Shedu nimeshtuka sana.”
“Unashtuka nini wakati hata mgoni wa Shedu naye alilamba udongo.”

“Ni kweli alilamba udongo, kifo chake wengi walijua kilitokana na kumchukua mke wa mtu hata kufa kwake vilevile kulikuwa kama miujiza fulani. Lakini kifo cha mbaya wako kilikuwa cha ajali, gari lake liligongana uso kwa uso na gari la mafuta. Waliofika kwenye tukio wanasema wala hakuomba maji alifia palepale.”
“He! Kumbe kweli?” nilijikuta nikishtuka baada ya kusikia vile.

“Unashangaa nini?”
“Unajua aliyosema yule mzee mimi nilijua ametupa moyo baada ya kuonekana kazi imemshinda.”
“Kaniambia yote Shedu yaliyotokea huko, lakini ukweli unabaki palepale yule mzee ni tishio hasa kwenye kazi za visasi.”
“Lakini naamini adhabu aliyopewa ni kubwa sana.”

“Si ndiyo uliyochangua?” Simon aliniuliza amenikazia macho.
“Adhabu hii sikuichagua bali walinichagulia ili kumkomesha jamaa.”
“Basi tena ni kujipanga upya, shemeji amerudi?”
“Nasikia amerudi juzi jioni na kulala hapa, asubuhi inaonekana labda ameenda kwao.”

“Sasa ndo mkeo atulie kama umemuua huyo, akiendelea na tabia yake utaua wangapi?” Simon aliniuliza swali.
“Kwanza Simon hebu ondoa neno hilo la kusema nimeua, kazi yote kafanya mganga,” nilijitetea.

“Kwa sababu ya nani?”
“Yangu, lakini kwa uamuzi wa wengine mi nilitaka mke wangu tu.”
“Basi ndiyo hivyo mkeo atarudi jipange kuhakikisha kosa la awali halirudiwi.”
Tukiwa katika ya mazungumzo mlango uligongwa hodi, ilikuwa sauti ya mke wangu. Nilitamani ninyanyuke nikampokee lakini niliona aibu mbele ya Simon.

Nilimkaribisha kwa sauti aingie ndani.
Mke wangu aliingia na kuja moja kwa moja nilipokuwa nimekaa na kuja kupiga magoti kuomba msamaha.
“Samahani mume wangu najua nimekukosea kwa yote niliyokutendea, nimeamini yote ni matawi shina ni wewe. Najua nimekuumiza mume wangu kiasi cha kukufanya uchanganyike.

Yote ni kiburi cha nazi kushindana na jiwe, leo hii nimegeuka bundi kila kona nafukuzwa familia ya nilipokwenda hawataki hata kunisikia mama naye hataki kuniona nitakuwa mgeni wa nani,
“Mume wangu kazala nakuomba nipo chini ya kiguuu yako wewe ndiye kimbilio langu la mwisho nawe ukinifuikuzwa sina pa kwenda. Kazala mume wangu naomba unipokee tumlee mtoto wetu Zawadi.

Najuta kukukimbia mume wangu nimeamini si wajinga waliosema usiache m,bachao kwa msala upitao...Shemeji Simon nsakuomba niombee msamaha kwa mume wa ngu kazala ambaye nilimkosea kwa kuondoka bila kuaga zilikuwa ni hasira lakini leo hii zimekuwa hasara kwangu.

“Kazala bado nakuhitaji katika maisha yangu, rudisha moyo wako nipokee tena nakuahidi kuwa mke mwema katika maisha yangu yote yaliyobaki chini ya jua, nakupoenda kazala nakupenda baba Zawadi nipo chini ya miguu yako akinifukuza na wewe nitakuwa mgeni wa nani,” Mke wangu alilia kilio cha machungu kuonesha kweli ameumizwa na yaliyotokea.

Yote yaliyotokea kwangu hayakuwa tatizo kwangu zaidi ya mke wangi kurudi tena mikononi mwangu. Nilimnyanyua na kumkumbatia na kumweleza nimemsamehe. Nilimkumbatia mwanangu ambaye alikuwa kwenye afya nzuri na mke wangu.

Pamoja na kuumizwa roho na kifo cha mgoni wangu, lakini nilipata faraja ya ajabu mke wangu kurudi mikononi mwangu. Kwa mara ya kwanza niliamini uchawi upo na unafanya kazi.
Maisha yalianza upya huku mke wangu kila kukicha akijutia alichokifanya, nami nilimweleza yote aliyofanya nimemsamehe toka moyoni mwangu.

Hali ya utulivu ilirudi ndani bila mtu kunitilia wasiwasi juu ya kifo cha mgoni wangu kuwa nimekisababisha mimi, wengi waliamini ile ilikuwa amri ya Mungu.
Maisha nayo yaliendelea huku nikirudi katika hali yangu za zamani kutokana na mapenzi mazito niliyopewa na mke wangu. Haikuchukua muda toka arudi kubeba ujauzito mwingine ambao huu hakuwa na matatizo nao hakuuzungumzia kuutoa zaidi ya kuulea kwa ajili ya kusubiri siku ya kujifungua .

Hali ile ilinifanya niamini mke wangu kweli tukio lililotokea limempa fundisho. Muda ulipofika alijifungua mtoto mwingine wa kike ambaye nilimwita Happy kutokana na kuraha ya kurudi kwa utulivu ndani ya nyumba yetu. Watoto wetu Zawadi na Happy walikua vizuri huku mama yao akionesha kuwapenda na kuwajali tofauti na Zawadi alipokuwa mdogo alivyo bemendwa na mama yake.

Siku zilizidi kwenda nami nikizidi kuyafurahia maisha, mke wangu alichukua miaka mitatu na nusu toka arudi kuanza mambo yake. Nakumbuka aliniomba sana tutafute msichana wa kazi kwa ajili ya kumsaidia kazi za nyumbani. Kwa vile sikutaka kubishana na mke wangu nilikubaliana naye na kumpa ruksa ya kutafuta mfanyakazi.

Haikuchukua hata siku tatu msichana wa kazi alipatikana kuonesha alimuandaa hata kabla ya kunieleza. Kwa vile sababu zake zilikuwa na uzito nilimkubalia kumleta na kuanza kazi. Tuliendelea na maisha huku familia yetu ikiwa imeongezeka mtu mwingine.

Waswahili wanasema kaniki hata ukiifua na mito na bahari zote dunia na sabuni zote hata siku moja haiwi nyeupe. Pia hawakukosea kusema la kuvunda halina ubani. Toka aliporudi alikuwa na tabia ya kunywa pombe kitu ambacho mwanzo nilikikemea lakini alinibembeleza kwani alikuwa ameizoeshwa na alipokwenda.
Kwa vile nilikuwa nampenda nilimkubalia awe anakunywa siku mojamoja.

Sehemu tuliyokuwa tukiishi kulikuwa na Glosary karibu. Mara nyingi alimtuma msichana wa kazi na kumletea ndani na kunywa. Siku nyingine niliporudi sikumkuta ndani msichana wa kazi alinieleza kama nitarudi kabla hajarudi akamwite.
Nilimtuma akamwite japo muda ule alitakiwa kuwa nyumbani, alimfuata na baada ya muda alirudi akiwa amechangamka kidogo.

“Vipi mume wangu umerudi zamani?”
“Kama dakika tano, vipi umeanza lini kwenda baa kunywa?”
“Samahani mume wangu, leo jirani yetu God alinipa ofa hapo nje kwenye Glosary.”
“Hakuna tatizo ila usiiendekeze sana pombe.”
“Mume wangu si leo tu, tena nimepewa ofa na jirani.”

“Hakuna tatizo ila usiendekeze sana, kunywa siku mojamoja siyo mbaya.”
Kumbe ukaribu na jirani yangu ulikuwa na maana pana zaidi ya ujirani, mke wangu alianzisha uhusiano na jirani yangu ambaye nikiwa kazini alimgeuza mke wake. Nakumbuka siku moja usiku nilishtuka kitandani na kujikuta nipo peke yangu. Sikuwa na wasiwasi kwa kuamini huenda amekwenda msalani.

Kwa vile choo na bafu vilikuwa nje nilijua amekwenda kujisaidia tu, nilijilaza sikuchelewa nilipitiwa na usingizi. Niliposhtuka mke wangu alikuwa pembeni yangu katikati ya usingizi.

Siku ile kabla ya kulala nilipomgusa mke wangu aliniomba radhi kuwa tumbo limemshtuka ghafla. Kwa vile ile haikuwahi kumtokea nilimwacha na kuendelea kulala.

Siku ya pili tena nilipomgusa alinieleza bado tumbo linamuuma:
“Mke wangu umetumia dawa gani?”
“Si..sijatumia dawa yoyote mume wangu.”

“Mke wangu sasa utailea hali hii mpaka lini, kumbuka mumeo hamu zangu lazima nilizimalizie kwako.”
“Najua mume wangu, samahani kwa hilo mume wangu kesho nitakwenda hospitali.”
“Mmh! Sawa.”
“Nisamehe mume wangu,” mke wangu alisema huku akinibusu na kunifanya mwanaume nilegee.

Tulilala kama kawaida yetu kwa kukumbatiana kupeana joto la usingizi mpaka kila mmoja alipolala tuliachiana na kupeana migongo. Kama kawaida nilishtuka tena katikati ya usingizi na kujikuta tena peke yangu kitandani. Pia sikuwa na wasi nilijilaza kitandani lakini usingizi ulichelewa kunichukua nilitulia kitandani nikiwa nimetulizana macho nikiangalia dalini.

Muda ulikatika bila mke wangu kurejea kitu kile kilinitia wasiwasi na kuona labda yupo msalani tumbo limemzidia. Nilinyanyuka kitandani na kutoka nje kwenda kumuangalia mke wangu. Nilikwenda hadi msalani na kumwita kama yupo akijisaidia.

Hakukuwa na jibu lolote, niliingia msalani hapakuwa na mtu nilitoka nje na kujiuliza mke wangu atakuwa amekwenda wapi. Nilizunguka nyumba vilevile sikumuona niliamua kurudi ndani nikiwa na mawazo kibao kukosekana kwa mke wangu usiku mkubwa kama ule.

Nilikaa kitandani nikijiuliza mke wangu usiku ule amekwenda wapi au amezidiwa na kuamua kwenda kwao. Lakini nilijua lazima angenijulisha kuliko kuondoka kimyakimya akijua mumewe nipo.
Nikiwa bado nimekaa kitandani niliuona mlango ukifunguliwa taratibu, alitulia kutaka kuona nani anayeingia vile kwa kunyata huenda ni mwizi.

Baada ya mlango kufunguliwa ulitangulia mguu kisha mwili. Kumbe alikuwa mke wangu katika vazi la kanga moja.
Aliponiona alishtuka mpaka kanga ilimdondoka na kubakia mtupu, hakuiokota alibaki amesimama kama mwanga aliyekamatwa akiwanga.

Nilimwangalia mke wangu na kushindwa kumuelewa kuwa katika hali ile ya kutahayali.
“Vipi mke wangu?” nilivunja ukimya baada ya kutazamana kwa muda.
“Sa.sa...” alishindwa kuzungumza.

“Unatoka wapi?”
“Msalani, tumbo lilinizidia nikachelewa kutoka.”
“Ulienda choo kipi?”
“Cha nje.”
“Kweli?”
“Ndiyo mume wangu.”
“Na sasa hivi ndiyo unatoka huko?”
“Ndiyo mume wangu,” alijibu vidole vikiwa mdomoni.

“Wakati mi naingia chooni wewe ulikuwa wapi?”
“Wee umekwenda chooni saa ngapi?”
“Hebu kwanza vaa nguo.”
Mke wangu aliinama na kuokota kanga na kujifunga kisha alirudi kusimama alipokuwa awali vidole akirudisha mdomoni kama namtomgoza.

“Mke wangu ulikuwa wapi?”
“Chooni mume wangu,” mke wangu aling’ang’ania jibu lake.
“Si kweli nimeshtuka usingizini na kukaa macho kwa muda mrefu nikawa na wasiwasi labda umezidiwa na tumbo. Nimekuja chooni sikukuona nimzunguka nyumba yote sikukuona sasa hicho choo gani ulichokwenda?”

nilimuuliza nikiwa nimesimama karibu yake huku nikiyaona mapigo ya moyo yakimwenda mbio.
Mke wangu alishindwa kunijibu kitu kilichozidi kunipandisha hasira na kuona kuna mchezo mchafu ninachezewa. Nilimuuliza mke wangu kwa hasira huku niivuta kanga aliyojifunga ambayo yote ilibakia mkononi kwangu na kumbakiza tena mtupu..

“Niambie ukweli ulikuwa wapi, kama utanidanganya nitakacho kufanyia hutasahau mpaka unaingia kaburini. Ni mwaka wa tatu na nusu toka moyo wangu upone majeraha. Hujaridhika unauchubua tena, niambie ulikuwa wapi?”
“Samahani mume wangu nilipokuwa narudi toka chooni nilipofika kwenye mlango wa God, aliniita kwake mara moja lakini sijafanya kitu chochote mume wangu.”

“Leo hukufanya kitu, siku zote ulizokuwa ukienda kwake mlifanya nini?” Majibu yake yalinipa nguvu ya kutengeneza uongo unaofanana na ukweli
Swali langu lilimpa wakati mgumu kujibu na kubakia kuuma meno, nami nilipata nafasi ya kuongeza maneno yangu ya uchungu.

“Mke wangu wewe ni kiumbe gani, umefanya nimechuma dhambi kwa ajili yako, tumetulia umeanza tena kibaya zaidi nyumba tunayoishi. Wewe ni kiumbe gani? Mke wangu umerogwa na nani mpaka kuwa katika hali hii?”

“Nisamehe mume wangu ni shetani tu nipo chini ya miguu yako sitarudia tena,” mke wangu alipiga magoti kama mwanga akiwa hana kitu mwilini.
“Haya nieleze ukweli umeisaliti ndoa yetu toka urudi mara ngapi?”

“Kwa haki ya Mungu mara nne.”
“Na wanaume wangapi?”
“Mmoja mume wangu ni God tu, ukweli wa Mungu toka nimkubali ni wiki ya pili. Nimejitahidi kumkatalia lakini amekuwa akinisumbua ikiwemo kunipa ofa na fedha na pombe. Siku zote shetani ana nguvu nimejikuta nikimkubalia na kukusaliti kwa mara nyingine mume wangu.

“ Najua jinsi gani ninavyokuumiza lakini nakuomba usiniache, pombe ndiyo sababu mume wangu nitaiacha. Siku aliyonipa ofa ya pombe ndiyo ukawa mwanzo wa kunisumbua kimapenzi, kwa kweli nilijitahidi sana lakini nilijikuta nimemkubalia bila kujua. Naomba mume wangu usiniache, mama aliisha niambia siku nikifanya ujinga kwako na wewe kunifukuza basi nitafute pa kwenda nisirudi kwake. Nakuahidi mume wangu sitafanya ujinga tena na pombe leo ndiyo mwanzo na mwisho.”

Japo kauli ya mke wangu haikuwa na nguvu ya kunishawishi kumsamehe hasa baada kujua ametoka kwa mwanaume baada ya kunikimbia kitandani na kwenda kufanya uchafu wake. Kikubwa kichoniuma kilikuwa jirani yangu kuonesha dharau kwa kutembea na mke wangu akijua ni mke wa mtu. Kilichoniuma zaidi kilikuwa kumshawishi kunitoroka kutandani na kuniacha peke yangu nimelala.

Roho iliniuma kufanywa bwege kiasi kikubwa, kwangu ilikuwa dharau kubwa sana ambayo iliuumiza sana moyo wangu kwa jinsi alivyonidhalilisha kumchukua mke wangu nikiwa nimelala naye kitandani ile ilikuwa dharau mbaya sana ambayo ilitakiwa kulipa kisasi cha historia.

Mke wangu niliamini hana kosa ila kuna watu walitaka kuniona mimi ni nani. Nilipanga mwisho wa wiki niende tena kwa babu kumtia adabu. Tena mtu huyo sikuwa na huruma naye hata kidogo niliapa kumbakisha jina. Nilimsamehe mke wangu na kumuomba abadilike la sivyo sitamuuliza kitu chochote tena na wala sitamfukuza.

Mke wangu alinihakikishia kutulia hata rudia tena kosa kama lile, siku ile niliiacha ipite lakini moyoni nilikuwa na maumivu na hasira kama nyoka aliyekanyagwa mkia. Nilijitahidi kuficha kilichonikuta kwa watu wote huku nikiomba mwisho wa wiki ufike upesi.
Siku zote mke wangu hakuacha kuniomba msamaha, nilimueleza nimemsamehe toka moyoni na si mdomoni. Jirani yangu baada ya kugundua nimegundua hila zake ya kumchukua mke wangu, akawa anatoka alfajiri na kurudi usiku tumelala. Moyoni nilijisemea wyeye arukeruke lakini siku zako ya kuishi duniani zilikuwa zinahesabika nikifika kwa mzee Kidereko lazima uulambe udongo.

Moyoni niliapa siri ile hataijua mtu yeyote, baada ya kumsamehe mke wangu nilijilazimisha kuishi maisha ya kuilazimisha furaha huku moyoni nikiwa na maumivu makali kutokana na tabia za watu kumgeuza mke wangu jamvi la wageni.

Kwa vile dawa yao niliijua sikutaka kubishana na mtu zaidi ya kupanga safari ya kwenda kwa Mzee Kidereko Tewe. Hakuna aliyegundua mabadiliko yangu kazini na nyumbani. Wengi walijua uhusiano na mke wangu ni mzuri pia tabia yake alikuwa ameilekebisha.

Hata safari yangu niliyoipanga mwisho wa wiki ilikuwa siri yangu sikumwambia hata mwenyeji wangu Shedu aliyenipeleka Tewe kwa mzee Kidereko. Moyo wangu ulikuwa umeingia woga kuiogopa aibu ya kuonekana bwege kama wamejua mke wangu karudia makosa yaleyale.

Siku ya ijumaa baada ya kazi niliianza safari yangu huku nikimuaga mke wangu kuwa nakwenda nyumbani kwa wazazi nimeitwa ghafla. Mke wangu alinitakia safari njema huku akinihakikishia kwa maneno mazito.

“Mume wangu najua huniamini tena moyoni mwako, lakini nakuahidi mbele ya muumba ambaye hakosekani kila sehemu, yeye ndiye shahidi yangu kwa haya nitakayo yasema mbele yako muda mfupi kabla hujaenda kuwaona wazazi. Ni kwamba nimekuwa kama kaniki isiyobadilika rangi hata ukifuliwa na kusuguliwa vipi.

“Lakini hili ninalo lisema mbele yako kama nitarudia tena kosa mume wangu basi Mungu anigeuze kiumbe chochote cha ajabu au kuyachukua maisha yangu,” mke wangu alisema kwa sauti ya uchungu.

Mke wangu alizungumza maneno mazito ambayo yalinitoa machozi na kuamini kile kiapo kilitoka moyoni mwake na kujutia alichokifanya. Pamoja na kutaka kumuamini bado nilimuona kama mjusi asiyeweza kugeuka kuwa nyoka hata ukimpaka unga.

Nilijua kile kilikuwa ni kilio cha majuto lakini mke wangu alikuwa na akili za mbuzi kujisahau baada ya tukio kutulia. Kwa upande mwingine kiapo cha mke wangu nilikiona kizito ambacho alijichagulia adhabu kama atarudia upumbavu wake.

Wazo la kubadili safari yangu lilikuja na kuona hakuna haja ya kwenda kwa mzee Kidereko nitulie tu na kufanya mambo mengine. Wazo lile nilitaka kulipa nafasi lakini aibu ya mtu kutembea na mke wangu ilikuwa kubwa kwangu, kwa kuamini kila nitakapokutana na mgoni wangu moyo wangu ungekosa amani. Baada ya kusimama kwa muda nikishauriana na moyo wangu nilishtuliwa na mke wangu aliyeonekana kunifuatilia kwa karibu.

“Mume wangu najua huniamini lakini namuomba Mungu tena na tena aniepushe na tabia hii ambao imekuwa chukizo kwako bado umenisamehe mume wangu japokuwa sijui unaniwazia adhabu gani kunipa. Lakini narudia tena kuapa mbele yako na muumba wangu kama nitarudia tena nitakuwa sifai kuishi Mungu ayachukue maisha yangu.”
“Mke wangu nimekusamehe toka moyoni mwangu wala sina nilichokipanga kukufanyia. Ila huyu mshenzi ataniona.”
“Mshenzi gani mume wangu?”

“God lazima awe mfano kwa mtu yeyote atakayekugusa nimechoka..nimechoka kila siku kuwa mimi tu,” nilisema kwa uchungu japokuwa sikupenda mke wangu aijue dhamira yangu.
“Mume wangu nimekuahidi haitatokea tena madhara yake nimeyaona, nikifanya tena heri Mungu anigeuze mnyama sifai kuwa mwanadamu.”

“Nimekuelewa mke wangu, wacha niwahi usafiri japo sina uhakika nitaondoka na gari gani muda umekwenda sana.”
“Nikutakie safari njema mume wangu, wasalimie baba na mama mashemeji na wifi zangu.”

“Salamu zimefika.”
Niliwaaga na wanangu kisha niliondoka na nguo chache za kubadili kwa siku moja mbili nitakazo kuwa huko na kuomba Mungu nilirudi jumapili usiku ili jumatatu niamkie kazini.

Niliondoka nyumbani saa kumi na moja jioni had sokoni na kununua vitu vya kumpelekea mzee Kidereko. Baada ya kununua mahitaji muhimu nilikwenda njia panda ambako nilibahatika kupata basi la kutoka Mwanza ambalo lilikuwa limechelewa kidogo.

Kutokana basi kuchelewa njiani baada ya kuharibika dereva aliendesha kwa mwendo wa kasi tuliingia Chalinze saa nne na nusu za usiku. Niliteremka na kwenda kutafuta nyumba ya wageni. Nililala mpaka asubuhi ya siku ya pili saa mbili asubuhi, nilipanda basi la Shambalai kutoka Dar kwenda Lishoto. Niwasiri Mlalo majira ya saa kumi na moja jioni.
Kwa vile niliisha kuwa mwenyeji nilikodi baiskeli mbili moja ilinibeba mimi na nyingine ilibeba bidhaa nilizonunua kwa matumizi ya kijijini ambazo alizipenda mzee Kidereko.

Nilipofika nilipokelewa kwa furaha na yule msichana aliyetupokea siku za nyuma. Litokana na muda mrefu kupita bila kufika kule kijijini, nilimkuta ana mtoto mdogo wa kama mwaka na nusu. Baada ya kupokelewa nilikaribishwa chini ya mti na kupewa mkeka nijipumzishe kwanza.

Mzee Kidereko sikumuona nilijiuliza atakuwa amekwenda kwenye kazi zake za porini au sehemu gani.
Baada ya muda nilimuuliza mtoto wa mzee Kidereko ambaye nilikuwa nikizungumza naye habari za safari.

“Vipi mzee yupo wapi?”
“Yupo ndani amelala siku hizi amekuwa mgonjwamgonjwa sababu ya uzee na kazi za mikiki. Kuna kazi moja ilikuwa nzito sana huwezi kuamini tulijua mzee amekufa. Kazimika kwa wiki nzima kitandani na alipopata ufahamu amekuwa mgonjwamgonjwa muda mwingi anapumzika na kazi nyingi za mzee anafanya kaka.”

Habari zile zilinishtua baada ya kusikia mganga anaumwa kufikia hatua ya kushindwa kuzifanya kazi zake na kumpa mtu mwingine. Niliamini uwezo wa mzee Kadereko ni karama toka kwa Mungu lakini mwanaye ni uganga wa kujifunza hauna nguvu sana. Nilihoji uwezo wa kaka yake kwa wateja waliokuja.
“Umesema kaka yako anashika mikoba ya baba yenu, kweli ana uwezo kama mzee?”

“Kwa kweli sijasikia malalamiko yoyote kutoka kwa wateja ila kazi ikiwa kubwa sana anaifanya mwenyewe.”
“Kwa hiyo kazi zingine anazifanya mwenyew?”
“Ndiyo, bado hajaiacha rasmi kwa vile bado anamkomaza kaka ila akikomaa kazi zote atazifanya yeye.”
“Nikitaka kazi yangu aifanye yeye itakuwaje?”

“Utakusikiliza kama itakuwa nyepesi ataifanya kaka, sema tu hujafanya naye kazi lakini kila kukicha amekuwa akiivaa sawasawa kofia ya baba.”
“Na mzee huamka saa ngapi?”
“Muda wake umekaribia.”
“Kwa hiyo mgeni akifika anaonana na kaka yako?”
“Hapana, mgeni yeyote aliyetoka mbali lazima aonane kwanza na mzee ili kumpa faraja ya safari yake ndefu ya kuja kijijini.”

“Mmh! Kama hivyo sawa.”
Tukiwa katika ya mazungumzo alitumwa mtu kuniita naitwa na mzee ndani. Nilinyanyuka hadi sebuleni kwake, aliponiona alinyanyuka kwenye kiti chake cha uvivu na kunikaribisha.

“Kazala karibu baba.”
“Asante baba, shikamoo.”
“Marahaba, karibu sana.”
“Asante, pole na matatizo.”
“Asante, lakini ndiyo maisha tuliyochagua hatuna budi kukubaliana nayo.”
“Vipi unaendeleaje?”
“Ndiyo nimeisha kuwa mgonjwa sina kingine zaidi ya kusubiri tu mauti unichukue.”
“Hapana baba, nina imani ukitumia dawa utakuwa sawa tu,” nilimpa moyo.

“Hapana, pigo nililokutana nalo ni Mungu tu, lakini namshukuru hata nikifa leo kuna mrithi nimemuacha japo si kwa kiwango changu lakini atawasaidieni sana. Ningekufa na kinyongo kama dhoruba lile lingeniua bila kuacha mrithi wangu. Lakini sasa hivi wala sina wasiwasi mauti yanichukue tu.”
“Baba maneno gani hayo ya kuchoma moyo,” maneno ya mzee Kidereko yalinitisha.

“Kukuchoma moyo kivipi Kazala? Wakati kila mwanadamu lazima atakufa hakuna atakaye ishi milele.”
“Ni kweli baba, lakini basi tupe maneno ya kutupa moyo si unajua tunakutegemea.”
“Kazala usiogope kufa kwa vile kifo kipo hata usipotaka kukisikia.”
“Kwani mzee wangu hiyo kazi ilikuwa nzito kuliko ya kwangu?” nilimuuliza.

“Hii mwanangu temea chini, unajua tunafamnya kazi na watu wengi wenye nyadhifa serikalini na watu wa kawaida. Kuna kigogo mmoja wa serikalini ambaye nilimsaidia kupata ubunge na kumweleza ipo siku atakuwa mtu mkubwa serikalini.
“Kwake aliona kama ndoto ya mchana basi baada ya kupata ubunge tu kwenye baraza la mawaziri na yeye akatajwa. Alikuja hapa akiwa haamini kilichomtokea kwa kweli alichanganyikiwa. Nilimwambia bado namtengenezea mazingira ya urais.

“Kwa kweli nyota yake ikawa inang’ara kila kukicha hata vyombo vya habari vikawa vikimtaja sana kama mrithi wa rais anayemaliza muda wake. Kumbe kuna watu wakawa wanamtafuta ili kumzima kama kibatari. Kuna siku aliingia ofisini asubuhi bila kujua kuna bomu limetegwa. Alipokaa kitini alikutana na bomu alikuwa afie palepale kwenye kiti.

“Lakini kinga niliyompa ndiyo iliyomsaidia. Kwa vile familia yake ilikuwa ikijua kila kitu wamchukua na kumleta huku mara moja akiwa nusu mfu. Baada ya kuletwa nilifanya kosa kubwa kwa kufanya kazi kimazoea bila kuangalia uzito wa tatizo lile.

“Nilijua tatizo lile si kubwa kutokana na nilivyomkinga kumbe watu walihangaika na kufuata uchawi mpaka Nigeria ili kummaliza baada ya waganga wa hapa kuchemsha. Baada ya kuletwa nilimhudumia bila kujikinga nilifanikiwa kulitegua bomu alilotupiwa. Wakati likitoka kikanipamia kwa vile sikuwa sawa lilinitishisha si kitoto.

“Kutokana na uzito wa kitu kile na mimi nilivyo kidharau nilikuwa nife lakini nami nilikuwa sawa ndipo liliponilaza wiki nzima nikiwa sijitambui nusu mfu.

Vijana wangu walishindwa ilibidi afuatwe mganga mwingine kuja kunizindua. Toka nilipozinduka hali yangu su nzuri mwili umekuwa mgonjwamgonjwa. Lakini mshukuru Mungu hali yangu inaendelea vizuri.”
“Una muda gani toka upatwe na matatizo haya?”
“Mwaka sasa.”
“Mbona muda mrefu huna mabadiliko yoyote?”

“Ninayo makubwa sana, ehe za siku?”
“Nzuri mzee wangu, za miaka na wewe?”
“Kama ulivyozikuta, ila nashukuru sana kwa kutukumbuka kila mara, vitu vyako unavyotutumia tunavipata kwa kweli umekuwa kijana wa ajabu kukufanyia kazi moja lakini umekuwa akitukumbuka tofauti na watu niliowawezesha kimaisha hawatukumbuki mpaka wawe na shida.”
“Kila mtu ana roho yake, wapo wasiojua kushukuru hata wakipewa.”
“Ni kweli mwanangu, haya leo kwetu una tatizo gani tena?”

“Kama la awali.”
“Mkeo katoka nje ya nyumba tena?” mzee Kidereko alishtuka.
“Ndiyo mzee wangu.”
“Kwa hiyo unatakaje?”
“Kwa vile yule jamaa kanifanyia dharau ya kutembea na mke wangu nataka afe kifo cha mateso na aibu.”

“Hakuna tatizo, japo kazi hii si kubwa lakini nitakufanyia mwenyewe.”
“Nitashukuru mzee wangu.”
“Unataka kifo cha aina gani?”
“Chochote ili wadoezi wa wake za watu wakome.”

“Kwa vile mkeo haaminiki nitakufundisha baadhi ya adhabu atakazowapa wagoni wako ili usisumbuke kuja huku kila mara. Nitakupa zawadi moja kubwa sana nina imani huenda utakaporudi usinikute.”
“Unataka kwenda wapi?”
“Na uzee huu ukiuondoa si kifo, nataka nikifa nikuachia zawadi ya kukusaidia katika maisha yako.”

“Zawadi gani?”
“Tego ya mtu anayetembea na mke wa mtu na vitu vingi nitakupatia ili uweze kujilinda hata kuwasaidia waliokuzunguka.”
 
Sehemu ya 46

Nataka nikifa nikuachia zawadi ya kukusaidia katika maisha yako.”
“Zawadi gani?”
“Tego ya mtu anayetembea na mke wa mtu na vitu vingi nitakupatia ili uweze kujilinda hata kuwasaidia waliokuzunguka.”

“Nitaweza kweli?” kazi ile niliona kama nzito.
“Utaweza tu wala si kazi ni vitu vyepesi kama utakuwa tayari.”
“Haya baba hakuna tatizo.”
Tulikubaliana siku ya pili anipeleke porini akanionesha baadhi ya dawa za kuwakomesha wadoezi wa wake za watu.

Siku ya pili alfajiri tuliondoka nyumbani na kuelekea porini, ajabu siku ile tulikuwa wawili tu mimi na mzee Kidereko ambaye pamoja na maradhi umri nao ulimtupa. Tulikwenda kwenda wa taratibu kwa mwendo wa saa nne bila kupumzika hadi kwenye pori kubwa ambalo lilikuwa na miti mingi.

Mzee alioninesha miti mingi na kazi yake kwa ajili ya kutibu maradhi pia alinionesha baadhi ya miti ukiitumia hugeuka kuwa uchawi wa kumzuru mtu. Nilijiuliza miti ile nitaijuaje kwa mara moja kwa vile sikuwa mganga wala mzoefu wa kazi ile.

Kwa upande wangu niliona kama vile mzee Kidereko alikuwa akipoteza muda wake kunionesha vitu ambavyo nilijua siwezi kuvikumbuka.
Alinitembea hadi kwenye mti mkubwa mfano wa mbuyu, tulipofika pale tulisimama na kunieleza niweke mkoba chini na kuniomba nivue shati, nilivua shati na kubakia na suruali kisha akinipa kaniki kujifunga kwa chini na kukiacha kifua wazi.

Alichukua maji yaliyokuwa kwenye chupa na kuyaweka mdomoni kisha aliyapiliza kuelekea kwenye ule mti mkubwa. Baada ya kumaliza zoezi lile alichukua unga wa dawa na kuurusha sehemu nne za dunia na kusema kwa sauti.

“Hodi mizimu.. hodi majini yote kianzia Kibwengo na majini yote..hodi tumekuja kutaka msaada wenu.. tunajua ninyi mna nguvu, mizimu yote na majini tupokeeni tufanye kazi yetu,” baada ya kusema maneno yale nilisikia kitu kama muungurumo ambao haukudumu muda mrefu ulinyamaza.

Baada ya hali ile kutulia nilimsikia mzee Kidereko akisema:
“Asante mkuu wa mti huu asante mizimu yote asante majini yote.”

Alipomaliza kusema vile alinieleza nikae chini kwenye mwinuko miguu nikiinyoosha kuuelekea ule mti mkubwa. Nilikaa chini na kuuelekea mti mkubwa kama nilivyoelekezwa na kutulia kusubiri maelekezo mengine.

Baada ya kukaa alivyonieleza alichukua shanga zilizokuwa zimetengenezwa kama mkufu na hirizi mbili ya rangi yekundu iliyokuwa kubwa na nyeusi ilikuwa na ukubwa saizi ya kati akanivisha shingoni na vitu vile kulalia kifuani.

Baada ya kuvisha vitu vile nilitulia kusubiri kinachoendelea, alitoa kibuyu kidogo chenye shanga shingoni kwenye mkoba na kukiwekea kwenye mikono yangu.

Kisha Mzee Kidereko alikichukua kile kibuyu kidogo na kukiweka kichwani kwangu kwangu kisha alianza kuzungumza kwa sauti kama anazungumza na mtu.
“Mizimu nimekuja na mgeni, huyu ni mtu muhimu sana kwangu, naomba mumpe nguvu za kuweza kujilinda hata kufanya mambo yake mwenyewe kwa msaada wenu. Nimemleta huku ili ili muwe naye karibu kwa vile maisha ya mwanadamu si ya kudumu.”

Baada ya kusema vile ulizuka upepo mkali ulinitisha, ulivuma kwa muda kidogo kitu kilichoongeza hofu moyoni mwangu kisha ulitulia na kurudi hali ya kawaida. Baada upepo kutulia mzee Kidereko alikitoa kibuyu kichwani na kunirudishia mkononi na kunieleza:

“Nuia mambo yako yote kwenye kibuyu hicho.”
“Ninuize nini?” niliuliza kwa vile nilikuwa sijui cha kunuiza.
“Chochote kuhusiana na maisha yako pia na kilichokuleta. Huku ndiyo kila kitu wote tunategemea huku mpaka kukuleta kwangu umekuwa mtu muhimu sana hata nikifa uwe na kinga ya mizimu na majini.”

Nilitulia na kunuiza kupata fedha ili maisha yangu yawe juu pia mtu yeyote atakaye mgusa mke wangu basi afe kifo cha aibu. Baada ya kunuiza nilimweleza mzee Kidereko nimemaliza. Alikichukua kile kibuyu na kukizungusha kichwani kwangu mara kadhaa huku akinuia maneno yake kwa sauti ya chini yenye kusikika lakini sikuelewa anazungumza nini.

Baada ya kuzungumza vile aliweka kibuyu chini na kunishika mikono yote na kuninyanyua chini. Baada ya kusimama upepo wa mwanzo ulivuma tena na kufanya baadhi ya vitu vilipeperuka kwa kasi ya upepo ilikuwa tofauti na mwanzo.

Baada ya muda upepo ulitulia alinieleza nizunguke ule mti mkubwa mara saba huku nikinuia tena. Nilifanya vile kwa kuuzunguka mara saba kisha nilirudi akipokuwa amesimama mzee Kidereko. Baada ya muda palitokea mtikisiko wa ajabu kama mti ule mkubwa unataka kung’oka. Niliingiliwa na hofu ya kuangukiwa na mti ule mkubwa na kuamini tusingeweza kupona kama ungetuangukia.

Ningekuwa peke yangu ningetoka mbio lakini mzee Kidereko alikuwa yupo katika hali ya kawaida wala uso wake haukuonesha wasiwasi wowote. Baada ya muda mtikisiko ule ulitulia. Mzee Kidereko alinipa kipande cha mti na hirizi ndogo nyekundu.

“Hivi vitu vitakusaidia katika mambo yako, hakikisha unakuwa na vitu hivi muda wote. Hivi ndivyo vitakuwa kinga yako popote kipande cha mti hiki kila ukitaka kufanya jambo lolote gumu tafuna kidogo na kunuiza kisha fanya ulichopanga kufanya kitakwenda kama ulivyopanga.

Baada ya kutoka pale tuliingia katikati ya pori ambalo lilikuwa linatisha sana, mzee Kidereko aliendelea kunielekeza baadhi ya miti ambayo ikichanganywa na mti mwingine ulikuwa unafanya kitu gani, kwa kweli ilikuwa yataka moyo kuyapokea yale, mengine yalitakiwa uwe na moyo cha chuma sababu yalikuwa yakitisha sana niliamini ule ndiyo uchawi niliowahi kusikia.

Tulipofika kwenye mti mmoja alinieleza mti huu ukiuchanganya na mafuta ya mnyama na maji ya maiti unamlaza mtu kitandani bila kuamka hata miaka kumi kama bado muda wake wa kufa haujafika. Mti mwingine nilielezwa ni kichanganya na kitu gani naweza kumaliza ukoo mzima kwa kutumia mkungu wa ndizi ambayo inatengenezwa na na dawa nyingine kila ndizi ikiiva mtu mmoja anaondoka ile ilikuwa ni dawa ya kisasi.

Miti na vitu vya kuchanganyia nilivyoelekezwa sitaweza kuviweka hadharani kwa kuhofia watu wenye roho mbaya wanaweza kuvifanyia kazi na kuwaumiza wenzao. Mzee Kidereko aliendelea kunifundisha vitu vingi vya kiganga na kichawi.

Siku zote mtu akitibu huwa mganga lakini akizuru au kuua huwa mchawi. Mzee Kidereko alinionesha mambo mengi sana. Alinifundisha kumtega mwanamke anayetoka nje ya ndoa.

Alinionesha tego la kung’ang’aniana, mwanaume kufariki baada ya kufika kileleni au kukojoa damu na usaha mpaka anakufa. Alinionesha tego nyingi sana ambazo utengenezaji wake haukuwa mgumu, baada ya kumaliza zoezi alilonipelekea porini ilikuwa yapata saa kumi na moja jioni.
Njiani wakati tunarudi nilimuuliza vitu nilivyoviona kule porini.

“Babu,” nilimwita
“Naam,” aliitikia huku akinitazama.
“Naweza kukuuliza baadhi ya vitu vilivyonitatiza?”
“Uliza chochote wala usihofu mwanangu,” mzee Kidereko alinitoa wasiwasi.
“Ule upepo ulikuwa ukiashiria nini?”

“Ile ni ishara kukubaliwa.”
“Na ule mtikisiko?”
“Ule ni kukaribishwa kwenye mizimu, huwezi kufanya kazi yako yoyote bila kukaribisha na wenyeji wa mti ule. Pale ndipo penye mizimu na majini yote ambayo yapo pale kwa ajili ya kutusaidia kutulinda na kutuelekeza dawa.”
“Ina maana kila ukiwa na tatizo lazima uje huku?”

“Hapana, ukiisha kuwa chini yao hukulinda muda wote.”
“Kwa hiyo na mimi nitakuwa chini yao?”
“Utapata ulinzi si mkubwa sana kwa vile kuna vitu unatakiwa kutoa pia kuwa tayari kuwa mganga.”
“Kama sitaki kuwa mganga?”
“Utapata ulinzi wa muda mfupi hasa katika vita yako inayoendelea.”

Safari ya kurudi nyumbani ilikuwa ndefu kuliko tulivyo kwenda, kwani upande wangu nilikuwa nimechoka sana. Tukiwa njiani akinionesha baadhi ya majani ya miti miwili nichume ambayo alinieleza nikichanganya na kitu kingine nikiwa nyumbani nitamfanya mbaya wangu ninavyotaka. Kwa vile nilikuwa sijiamini nilimweleza kazi ile alifanye yeye lakini mengine nitafanya mimi.

Tulifika nyumbani saa tatu na nusu usiku tukiwa hoi, kwa vile ilitakiwa niondoke kesho yake mzee Kidereko hakutaka kupumzika alializa mara moja kazi iliyonipeleka na kuniuliza mbaya wangu nataka afe kwa mtindo gani.
“Mzee wangu nataka kila mtu ajue mimi ndiye niliyefanya vile baada ya kutembea na mke wangu,” nilijibu bila hofu.

“Sawa basi kitakacho mtokea nina imani itakuwa fundisho na mfano kwa wote wenye tabia kama hizo.”
Kama kawaida alichukua beseni la maji, alinipa dawa ya unga na kuniambia ninyunyize ndani huku nikilitaja jina la mbaya wangu huku nikiendelea kunyunyizia ule unga kwenye beseni. Baada ya muda maji yaligeuka rangi na kuwa meusi.

“Basi,” mzee Kidereko alinieleza niache kunyunyizia dawa baada ya maji kugeuka rangi.
Alichukua dawa nyingine kwenye chupa na kuiweka kwenye beseni, baada ya muda maji yale yalikuwa meupe huku God, mbaya wangu akionekana amekaa kwenye kochi.
“Ndiye yeye?” mzee Kiredeko aliniuliza.

“Ndiyo.”
“Muangalie vizuri.”
“Ni yeye,” nilimuhakikishia mzee Kidereko.
Baada ya kumweleza aliniletea vitu viwili na kuniambia.
“Hapa kuna vitu viwili chagua kimoja, kisu kwa ajili ya kumuua ukiwa hukuhuku ukifika utamkuta mbaya wako amekufa. Hii chumba una uchawi wa kumuua taratibu katika mateso mazito.”

Nilichagua ya kifo cha taratibu cha mateso mazito. Baada ya kushika chupa yenye uchawi wa kuua taratibu, alichukua chupa nyingine na kutoa dawa ningine ya unga na kuiweka kwenye maji kisha alisema niiweke ile dawa kuhakikisha inampata mgoni wangu mwili mzima.

Nilifanya zoezi lile kwa umakini mkubwa baada ya kuhakikisha dawa imemfikia kila kona ya mwili, mzee Kidereko alitoa chupa ambayo ilionesha ina damu na kumimina kidogo kwenye maji na kuniambia nikiweke kile kisu ndani ya maji yale. Nilifanya kama alivyonielekeza kwa kukiweka kisu ndani ya maji bila vikwazo kama vya mwanzo kiliingia moja kwa moja.

Baada ya kumaliza zoezi lile alichukua lile beseni na kutokanalo nje baada ya muda alirudi na kunitaka nikapumzike kujiandaa na safari.
“Haya kijana wangu kazi imeenda vizuri mtu wako ni mwepesi hakutupa kazi yoyote, hivyo kalale kwa amani ili kesho uwahi kazini.”

Baada ya zoezi lile kukamilika niliagana na mzee Kidereko na kwenda zangu kulala nikiwa nimechoka sana kwa kazi na safari ya kutwa nzima. Siku ya pili kama nisingeamshwa niwahi usafiri lazima ningechelewa, pamoja na kuamshwa bado mwili ulikuwa mzito kutokana na mwili kuwa bado umechoka.

Niliamka na kujiandaa na safari, ajabu siku ile sikuonana na mzee Kidereko kutokana na kuwa amechoka sana ila nilipewa mzigo wa dawa na vitu tulivyochuma porini. Kabla ya kuondoka nilioneshwa kazi ya jana tuliyofanya na mzee Kidereko, mmh! Inatisha beseni lilikuwa na damu tupu maji yote yaligeuka damu kitu kilichofanya niulize hali ile ina maanisha nini.

“Ile ni kuonesha mambo yamekwenda vizuri asilimia mia moja.”
“Kwa hiyo jamaa haponi?”
“Yaani sasa hivi ni marehemu mtarajiwa.”

Baada ya maelezo yale vijana wa mzee Kidereko walinisindikiza mpaka kituo cha basi cha Mlalo ambako nilipanda basi la Shambalai. Kwa vile niliwahi nilipata siti nzuri sehemu ya mbele upande wa dirishani. Muda ulipofika Basi liliondoka Mlalo na kunifanya niwaze ya nyumbani mbaya wangu nini kitampata.

Kwa vile nilikuwa nimechoka sana baada ya gari kuondoka kituoni sikuchukua muda niliuchapa usingizi wa haja. Nilishtuliwa na abiria mwenzangu ambaye nilizungumza naye wakati nakaa kwenye siti yangu kuwa nateremkia Chalinze.

“Kaka..kaka,” aliniita.
“Naam,” nilifumbua macho kumsikiliza.
“Ulisema unashukika wapi?”
“Chalinze.”
“Tumefika watakupitiliza mpaka Dar.”
“Ooh! Asante,” nilishukuru huku nikiufuta uso wangu.

Niliamka na kuteremka kwenye gari macho yakiwa mekundu kutokana na kuuchapa usingizi kisawasawa. Nilipoulizia muda ule ni saa ngapi niliambiwa saa nane mchana kuonesha tumewahi kidogo. Kwa vile nilikuwa sijala nilikula chakula kabisa pale kabla ya kuunganisha usafiri. Baada ya kula sikutaka kupoteza muda nilipanda basi lililokuwa likipita muda ule.

Japokuwa halikuwa na siti nilipanda hivyohivyo , tulipofika mbele ya safari mtu mmoja aliteremkia njiani nami nilipata siti mpaka nyumbani. Saa kumi na mbili na nusu niliteremka kwenye basi na kuchukua usafiri mpaka nyumbani. Mke wangu aliponiona alifurahi sana, alinipokea kwa kunikimbilia na kunikumbatia kidogo aniangushe.
“Waawoo mume wangu karibu jamani.”

“Asante.”
“Za huku?”
“Nzuri.”
Alinipokea vitu nilivyonunua njiani na kuelekea wote ndani, tulipofika kwa vile nilikuwa nimechoka sana baada ya kuoga sikutaka kuzungumza nilipanda kitandani mpaka siku ya pili ya jumanne nilipoamka kujiandaa kwenda kazini.
“Mume wangu hujanijulisha hali ya wazazi nyumbani,” mke wangu aliniuliza wakati nikijiandaa kwenda kazini.

“Hawajambo wanakusalimia.”
“Sasa mbona hukuniambia mpaka nimekuuliza au bado una yaleyale hayajaisha?” mke wangu aliniuliza kwa sauti ya kilio.
“Hapana mke wangu, kwangu yaliisha baada ya kukusamehe huwa siweki kitu moyoni kwa muda mrefu,” nilimtoa hofu.
“Sasa kwa nini toka jana hujanipa habari za nyumbani au sitakiwi kuzijua?”

“Hapana mke wangu nisamehe sana, nilijua jana nilikueleza, kwa vile jana sikwenda kazini nilitaka niwahi.”
“Jamani mume wangu baada ya kusalimiana na kukuulizia habari za uko ukasema nzuri na kuniomba ulale kwa vile ulikuwa umechoka hata chakula cha usiku hukutaka, tumeongea saa ngapi?”
“Basi nisamehe lakini nilijua nikirudi kazini tungezungumza mengi.”

“Nimekusamehe mume wangu kwa vile nakupenda sana.”
“Nashukuru kwa kunisamehe wacha niwahi kazini.”
Niliagana na mke wangu kuelekea kazini huku nikirudia kauli ya mke wangu eti ananipenda sana. Nilicheka mwenyewe na kujiuliza kama kupendwa ndiko huko basi wasiopendwa wanateseka zaidi. Moyoni bado nilikuwa nawaza kifo cha aibu atakachokipata jirani yangu.

Nilipofika kazini ilikuwa ajabu hakuna aliyeniuliza jana nilikuwa wapi, kila mmoja nilizungumza naye kama siku iliyopita tulikuwa wote hata mtu wangu wa karibu Simon tulipokutana naye aliniuliza habari za nyumbani na si jana nilikuwa wapi.

Niliendelea na kazi mpaka jioni, niliporudi nyumbani kupumzika, nilipofika nyumbani nilipata taarifa za God kuhama nyumbani. Niliamini kufanya vile kulikuwa sawa na mfa maji asiyejua kuogelea lazima afe maji kwa vile maji hayana rafiki sawa na kifo.
*****
 
Sehemu ya 47

Niliendelea na kazi mpaka jioni, niliporudi nyumbani kupumzika, nilipofika nyumbani nilipata taarifa za God kuhama nyumbani. Niliamini kufanya vile kulikuwa sawa na mfa maji asiyejua kuogelea lazima afe maji kwa vile maji hayana rafiki sawa na kifo.
*****
Siku zilikatika huku nikimuona mbaya wangu akidunda kama kawaida bila kuonesha dalili zozote za mabadiliko. Kwa kweli kitu kile kiliniumiza sana na kuona kama niliyoelezwa na mzee Kidereko ni uongo hata mgoni wangu wa kwanza alikufa kwa amri ya Mungu si nguvu zake. Kama ingekuwa kweli basi ningesikia hata anakohoa.

Kwa kweli nilijikuta naingia kwenye mateso mapya ya kuumizwa kumuona mbaya wangu akiendelea kudunda. Sikukubali nilipanga safari ya kurudi tena kijijini kwa mzee Kidereko nikajue ukweli au na kwa yule amechemsha. Niliomba ruhusa kazini ya siku mbili na kufunga safari kwenda Tewe kwa mzee Kidereko ili tukaangalie tumekoea sehemu gani.

Kama kawaida nilifika kwa mzee Kidereko majira ya saa kumi na mbili jioni, hali ya pale ilinishtua kidogo ilionesha kupooza na kujiuliza kulikoni. Nilipokewa kama kawaida, kwa vile sikutaka kuwa kule kwa muda mrefu nilitaka kuoana na mzee Kidereko mara moja ili kesho yake alfajiri nirudi zangu nyumbani.

“Jamani vipi mbona kama hampo katika hali ya kawaida kuna usalama?”
“Mmh! Upo.” Alinijibu msichana aliyenipokea ambaye alikuwa tayari kanizoea.
“Kweli?”
“Kweli kwani vipi?”
“Ule uchangamfu niliouzoea umepotea.”

“Ni kweli.”
“Kuna nini?”
“Msiba.”
“Msiba! Wa nani?” nilishtuka.
“Mzee hatunaye.”
“Naniii? Hapana..hapana,” sikukubaliana na ile kauli.

“Kweli kabisa, swahibu yako hatuko naye.”
“Hapana ..hapana, naomba mniambie ukweli.”
“Kweli kabisa sasa inakimbilia wiki ya pili.”
“Jamani basi acheni utani naomba unieleze ukweli,” bado sikukubaliana na ile kauli.

“Najua huwezi kuamini, si wewe tu kila mteja wake aliyekuja hakuamini, lakini ukweli utabaki palepale mzee Kidereko amefariki dunia.”
“Mungu wangu, mbona naadhilika mimi Kazala,” nilijikatia tamaa.

Kwa kweli sikujielewa nilihisi nguvu zikiishia na kwenda chini bila kupenda kiza kinene na kuzungumzungu kilitanda mbele yangu kilichoendelea sikujua.
Niliposhtuka nilijiokuta nipo katikati ya kiza kinene, Nilipatwa na mshtuko na kujishangaa pale nilipokuwa ni wapi. Pamoja na kiza kizito kulikuwa kinya sana.

Nilitulia nikitafakari pale ni wapi, ghafla nilisakia sauti kama mtu akitembea mara niliona mwanga wa kibatari. Bado nilikuwa njia panda kujiuliza pale ni wapi na nimefikaje.
“Kaka... Kazala...kaka Kazala.” Iliniita sauti ya kike sikuitikia mara moja mpaka aliporudia zaidi ya mara nne ndipo nilipoitika.

“Naam.”
“Amka.”
Nilinyanyua nilipokuwa nimelala na kukaa kitako na kijishangaa kuhisi baridi nilipojishika niligundua nipo kifua wazi na mwili ulikuwa umegandiwa na majani.
“Amka,” yule mwanamke aliyenifuata alinipa mkono kuninyanyua.

Baada ya kunyanyuka tulitoka nje na kugundua kumbe nilikuwa nimelazwa chumbani. Nilipewa maji ya kuoga na kuvaa nguo zangu, baada ya kuoga nilikutana na mtoto wa mzee Kidereko ambaye aliandaliwa kwa ajili ya kurithi mikoba ya baba yake.

“Ndiyo ndugu, yangu pole sana,” alianza kwa kunipa pole.
“Asante, ni kweli?” nilimuuliza swali ambalo akilini mwangu lilikuwa vigumu kukubalika mara moja kuwa mzee Kidereko anaweza kufa haraka hivyo.

“Ukweli gani ndugu yangu?”
“Kuhusu kufa kwa mzee Kidereko.”
“Ni kweli, mzee amefariki wiki mbili zilizopita.”
“Mungu wangu nitakuwa mgeni wa nani?”
“Unataka kuniambia mke wako bado tu hajatulia?” Aliniuliza huku akinikazia macho.

“Hapana ila yule mtu bado anadunda tena kwenye afya njema, nilikuja kwa mzee kumuuliza tumekosea wapi?”
“Hebu nipe mkono,” aliniomba mkono wangu aliushika na kuutazama kwenye kiganja na kunieleza:
“Mbona sioni tatizo lolote?”
“Kwa upande wangu naweza kuwa sawa, kwa huyo mbaya wangu naona kama kuna tatizo.”

Aliagiza maji kwenye beseni kama alivyokuwa akifanya mzee Kidereko. Baada ya kuletewa aliingiza mkono na kuwa anatafuta kitu kisha alitoa mkono uliokuwa umetapakaa damu na kunifanya nishtuke kuiona hali ile.
“Mbona hakuna tatizo Kazala.”
“Na hiyo damu?”
“Ni uhai wa mbaya wako unapunguzwa kila kukicha.”

“Mwezi sasa mbona yupo hai wala haoneshi dalili za kuugua?”
“Kazala ulitaka mbaya wako afe kifo cha mateso sasa tatizo nini?”
“Mbona haoneshi dalili zozote za kuugua?”
“Kazala hujui tu lakini mbaya wako wiki sasa yupo katika mateso mazito, kama angejua ni wewe basi angekuja kukuomba msamaha.”

“Unanidanganya, mbona anatembea yupo sawa?”
“Wiki hii umemuona?”
“Sijamuona ila yupo anadunda.”
“Basi hali yake ni mbaya sana sasa hivi yupo kwenye mateso mazito sana.”
“Mmh! Sawa, lakini bado siamini,” bado sikuamini maneno ya mganga niliona ananipa moyo na kwa vile mzee Kidereko amekufa nilijua kila kitu kilikuwa kimekufa.

“Muulize mtu wa karibu yake atakupa jibu ambalo litakushangaza sana. Mzee angekuwepo angekushangaa sana.”
“Basi nimekuelewa, na nini hasa sababu ya kifo cha mzee?”

“Ni kifo kama vifo vingine, japo alikuwa na uwezo mkubwa katika karama aliyopewa, lakini alibakia kuwa kiumbe wa kawaida anayeweza kuumwa, kula, kulala na hata kufa kama viumbe wengine.”
“Lakini naona amekufa haraka sana?” bado sikuamini.

“Kwa akili za kibinaadamu tutaona amekufa haraka lakini mzee mwenyewe alijua yupo ukingoni katika maisha yake.”
“Na nini kilichomfanya ajue muda wake wa kuishi umeisha, naona ni wiki tatu toka ajitabirie kifo na kweli mauti yamempata!” nilishangazwa na kauli ya mzee Kidereko kujitabiria kifo.

“Ni kweli kifo chake alikiona na kuomba akifa tulie kama wanadamu wa kawaida ameondoka na si kukufuru, pia alisema kama kumlilia ni siku ya kufa tu lakini siku nyingine ni kumshukuru Mungu. Na kweli alipokufa tulilia siku moja baada ya hapo tulimshukuru Mungu.”
“Kwa hiyo mambo yangu mengine nani atanisaidia?”

“Kwako naimani hakuna kazi nzito, nakuahidi kukusaidia kwa muda wote usihofu niamini nitakufanyia kazi kwa uhakika.”
“Sawa nashukuru sana, ila nakupeni pole sana kwa kifo cha kipenzi chetu.”
“Nashukuru sana, ila kifo chake kitabakia palepale kwa kuamini kazi ya Mungu haina makosa.”

“Kwa mbaya wangu uniambiaje?”
“Kazi imefanyika subiri majibu, ungetaka tumkate mara moja kama kwa kwanza, sasa hivi tungekuwa tumemsahau.”
Kwa vile muda ulikuwa umekwenda kililetwa chakula tulikula pamoja kisha tuliendelea kuzungumzo hadi usiku sana nilikwenda kulala kuisubiri siku ya pili nilirudi nyumbani. Usiku ulikuwa mrefu kuwaza taarifa ya kifo cha mzee Kidereko.

Pamoja na kuwa kifo ni haki ya kila kiumbe kinachoishi, lakini kifo cha mzee Kudereko bado sikuamini pamoja na kunieleza nisiogope kifo lakini kwa karama zake sikuamini kufa kirahisi namna ile. Mwanaye pamoja na kunitoa hofu katika matatizo yangu bado sikumuamini kuzifanya kazi zangu.
Niliamini huenda safari ile iwe ya mwisho kurudi Tewe kwa kuona hakuna mwenye nguvu tena baada ya mbuyu kuanguka.

Lakini kwa upande mwingine nilijiona kama mtu niliyetaka kukosa shukrani kwani baadhi ya vitu nilioneshwa na mzee Kidereko kwa ajili ya kuvifanyia kazi nilitakiwa kuvifanyia majaribio.Kutokana na kauli ya mzee alinifundisha ili nisumbuke kwenda kwake kila mara kwa vile hakupenda kila jambo nikimbilie kwake labda liwe zito sana.

Siku ya pili nilirudi nyumbani na siri yangu moyoni huku nikitafuta taarifa za God zina ukweli gani kutokana na kauli za mtoto wa mzee Kidereko. Niliamini mzee Kidereko alijua nini kitafuata pia hakuamini uwezo wa mwanaye na kuamua kunifundisha siraha za maangamizi pindi nivamiwapo.

Taarifa zilizoletewa kuhusiana na mgoni wangu God, nilitakiwa niwe na moyo wa chuma kuzipokea. God alikuwa na siku nne toka apelekwe kwao kutokana na kutokwa damu zisizokata sehemu ya haja kubwa kama mwanamke aliye kwenye siku zote. Ugonjwa ambao haukuonekana katika vipimo vya hospitali ilibidi achukuliwe na ndugu zake wanaoishi Dar ili kumpeleka kwa mtaalam Bagamoyo.

Wiki moja toka niliporudi toka Tewe kwa marehemu mzee Kidereko nilipata taarifa zingine ambazo hazikinishtua sana japo zilikuwa zikisikitisha kuwa God alifariki wiki moja iliyopita akiwa njiani kupelekwa kwa mganga Bagamoyo.
Mi moyo kwatu baada ya kumtia adabu mbaya wangu na kuapa kila atakayemgusa mke wangu sitakuwa na simile naye. Adhabu yangu nilipanga kuwa kifo tena cha mateso


Utaendelea Leo jioni.
 
Sehemu ya 47

Niliendelea na kazi mpaka jioni, niliporudi nyumbani kupumzika, nilipofika nyumbani nilipata taarifa za God kuhama nyumbani. Niliamini kufanya vile kulikuwa sawa na mfa maji asiyejua kuogelea lazima afe maji kwa vile maji hayana rafiki sawa na kifo.
*****
Siku zilikatika huku nikimuona mbaya wangu akidunda kama kawaida bila kuonesha dalili zozote za mabadiliko. Kwa kweli kitu kile kiliniumiza sana na kuona kama niliyoelezwa na mzee Kidereko ni uongo hata mgoni wangu wa kwanza alikufa kwa amri ya Mungu si nguvu zake. Kama ingekuwa kweli basi ningesikia hata anakohoa.

Kwa kweli nilijikuta naingia kwenye mateso mapya ya kuumizwa kumuona mbaya wangu akiendelea kudunda. Sikukubali nilipanga safari ya kurudi tena kijijini kwa mzee Kidereko nikajue ukweli au na kwa yule amechemsha. Niliomba ruhusa kazini ya siku mbili na kufunga safari kwenda Tewe kwa mzee Kidereko ili tukaangalie tumekoea sehemu gani.

Kama kawaida nilifika kwa mzee Kidereko majira ya saa kumi na mbili jioni, hali ya pale ilinishtua kidogo ilionesha kupooza na kujiuliza kulikoni. Nilipokewa kama kawaida, kwa vile sikutaka kuwa kule kwa muda mrefu nilitaka kuoana na mzee Kidereko mara moja ili kesho yake alfajiri nirudi zangu nyumbani.

“Jamani vipi mbona kama hampo katika hali ya kawaida kuna usalama?”
“Mmh! Upo.” Alinijibu msichana aliyenipokea ambaye alikuwa tayari kanizoea.
“Kweli?”
“Kweli kwani vipi?”
“Ule uchangamfu niliouzoea umepotea.”

“Ni kweli.”
“Kuna nini?”
“Msiba.”
“Msiba! Wa nani?” nilishtuka.
“Mzee hatunaye.”
“Naniii? Hapana..hapana,” sikukubaliana na ile kauli.

“Kweli kabisa, swahibu yako hatuko naye.”
“Hapana ..hapana, naomba mniambie ukweli.”
“Kweli kabisa sasa inakimbilia wiki ya pili.”
“Jamani basi acheni utani naomba unieleze ukweli,” bado sikukubaliana na ile kauli.

“Najua huwezi kuamini, si wewe tu kila mteja wake aliyekuja hakuamini, lakini ukweli utabaki palepale mzee Kidereko amefariki dunia.”
“Mungu wangu, mbona naadhilika mimi Kazala,” nilijikatia tamaa.

Kwa kweli sikujielewa nilihisi nguvu zikiishia na kwenda chini bila kupenda kiza kinene na kuzungumzungu kilitanda mbele yangu kilichoendelea sikujua.
Niliposhtuka nilijiokuta nipo katikati ya kiza kinene, Nilipatwa na mshtuko na kujishangaa pale nilipokuwa ni wapi. Pamoja na kiza kizito kulikuwa kinya sana.

Nilitulia nikitafakari pale ni wapi, ghafla nilisakia sauti kama mtu akitembea mara niliona mwanga wa kibatari. Bado nilikuwa njia panda kujiuliza pale ni wapi na nimefikaje.
“Kaka... Kazala...kaka Kazala.” Iliniita sauti ya kike sikuitikia mara moja mpaka aliporudia zaidi ya mara nne ndipo nilipoitika.

“Naam.”
“Amka.”
Nilinyanyua nilipokuwa nimelala na kukaa kitako na kijishangaa kuhisi baridi nilipojishika niligundua nipo kifua wazi na mwili ulikuwa umegandiwa na majani.
“Amka,” yule mwanamke aliyenifuata alinipa mkono kuninyanyua.

Baada ya kunyanyuka tulitoka nje na kugundua kumbe nilikuwa nimelazwa chumbani. Nilipewa maji ya kuoga na kuvaa nguo zangu, baada ya kuoga nilikutana na mtoto wa mzee Kidereko ambaye aliandaliwa kwa ajili ya kurithi mikoba ya baba yake.

“Ndiyo ndugu, yangu pole sana,” alianza kwa kunipa pole.
“Asante, ni kweli?” nilimuuliza swali ambalo akilini mwangu lilikuwa vigumu kukubalika mara moja kuwa mzee Kidereko anaweza kufa haraka hivyo.

“Ukweli gani ndugu yangu?”
“Kuhusu kufa kwa mzee Kidereko.”
“Ni kweli, mzee amefariki wiki mbili zilizopita.”
“Mungu wangu nitakuwa mgeni wa nani?”
“Unataka kuniambia mke wako bado tu hajatulia?” Aliniuliza huku akinikazia macho.

“Hapana ila yule mtu bado anadunda tena kwenye afya njema, nilikuja kwa mzee kumuuliza tumekosea wapi?”
“Hebu nipe mkono,” aliniomba mkono wangu aliushika na kuutazama kwenye kiganja na kunieleza:
“Mbona sioni tatizo lolote?”
“Kwa upande wangu naweza kuwa sawa, kwa huyo mbaya wangu naona kama kuna tatizo.”

Aliagiza maji kwenye beseni kama alivyokuwa akifanya mzee Kidereko. Baada ya kuletewa aliingiza mkono na kuwa anatafuta kitu kisha alitoa mkono uliokuwa umetapakaa damu na kunifanya nishtuke kuiona hali ile.
“Mbona hakuna tatizo Kazala.”
“Na hiyo damu?”
“Ni uhai wa mbaya wako unapunguzwa kila kukicha.”

“Mwezi sasa mbona yupo hai wala haoneshi dalili za kuugua?”
“Kazala ulitaka mbaya wako afe kifo cha mateso sasa tatizo nini?”
“Mbona haoneshi dalili zozote za kuugua?”
“Kazala hujui tu lakini mbaya wako wiki sasa yupo katika mateso mazito, kama angejua ni wewe basi angekuja kukuomba msamaha.”

“Unanidanganya, mbona anatembea yupo sawa?”
“Wiki hii umemuona?”
“Sijamuona ila yupo anadunda.”
“Basi hali yake ni mbaya sana sasa hivi yupo kwenye mateso mazito sana.”
“Mmh! Sawa, lakini bado siamini,” bado sikuamini maneno ya mganga niliona ananipa moyo na kwa vile mzee Kidereko amekufa nilijua kila kitu kilikuwa kimekufa.

“Muulize mtu wa karibu yake atakupa jibu ambalo litakushangaza sana. Mzee angekuwepo angekushangaa sana.”
“Basi nimekuelewa, na nini hasa sababu ya kifo cha mzee?”

“Ni kifo kama vifo vingine, japo alikuwa na uwezo mkubwa katika karama aliyopewa, lakini alibakia kuwa kiumbe wa kawaida anayeweza kuumwa, kula, kulala na hata kufa kama viumbe wengine.”
“Lakini naona amekufa haraka sana?” bado sikuamini.

“Kwa akili za kibinaadamu tutaona amekufa haraka lakini mzee mwenyewe alijua yupo ukingoni katika maisha yake.”
“Na nini kilichomfanya ajue muda wake wa kuishi umeisha, naona ni wiki tatu toka ajitabirie kifo na kweli mauti yamempata!” nilishangazwa na kauli ya mzee Kidereko kujitabiria kifo.

“Ni kweli kifo chake alikiona na kuomba akifa tulie kama wanadamu wa kawaida ameondoka na si kukufuru, pia alisema kama kumlilia ni siku ya kufa tu lakini siku nyingine ni kumshukuru Mungu. Na kweli alipokufa tulilia siku moja baada ya hapo tulimshukuru Mungu.”
“Kwa hiyo mambo yangu mengine nani atanisaidia?”

“Kwako naimani hakuna kazi nzito, nakuahidi kukusaidia kwa muda wote usihofu niamini nitakufanyia kazi kwa uhakika.”
“Sawa nashukuru sana, ila nakupeni pole sana kwa kifo cha kipenzi chetu.”
“Nashukuru sana, ila kifo chake kitabakia palepale kwa kuamini kazi ya Mungu haina makosa.”

“Kwa mbaya wangu uniambiaje?”
“Kazi imefanyika subiri majibu, ungetaka tumkate mara moja kama kwa kwanza, sasa hivi tungekuwa tumemsahau.”
Kwa vile muda ulikuwa umekwenda kililetwa chakula tulikula pamoja kisha tuliendelea kuzungumzo hadi usiku sana nilikwenda kulala kuisubiri siku ya pili nilirudi nyumbani. Usiku ulikuwa mrefu kuwaza taarifa ya kifo cha mzee Kidereko.

Pamoja na kuwa kifo ni haki ya kila kiumbe kinachoishi, lakini kifo cha mzee Kudereko bado sikuamini pamoja na kunieleza nisiogope kifo lakini kwa karama zake sikuamini kufa kirahisi namna ile. Mwanaye pamoja na kunitoa hofu katika matatizo yangu bado sikumuamini kuzifanya kazi zangu.
Niliamini huenda safari ile iwe ya mwisho kurudi Tewe kwa kuona hakuna mwenye nguvu tena baada ya mbuyu kuanguka.

Lakini kwa upande mwingine nilijiona kama mtu niliyetaka kukosa shukrani kwani baadhi ya vitu nilioneshwa na mzee Kidereko kwa ajili ya kuvifanyia kazi nilitakiwa kuvifanyia majaribio.Kutokana na kauli ya mzee alinifundisha ili nisumbuke kwenda kwake kila mara kwa vile hakupenda kila jambo nikimbilie kwake labda liwe zito sana.

Siku ya pili nilirudi nyumbani na siri yangu moyoni huku nikitafuta taarifa za God zina ukweli gani kutokana na kauli za mtoto wa mzee Kidereko. Niliamini mzee Kidereko alijua nini kitafuata pia hakuamini uwezo wa mwanaye na kuamua kunifundisha siraha za maangamizi pindi nivamiwapo.

Taarifa zilizoletewa kuhusiana na mgoni wangu God, nilitakiwa niwe na moyo wa chuma kuzipokea. God alikuwa na siku nne toka apelekwe kwao kutokana na kutokwa damu zisizokata sehemu ya haja kubwa kama mwanamke aliye kwenye siku zote. Ugonjwa ambao haukuonekana katika vipimo vya hospitali ilibidi achukuliwe na ndugu zake wanaoishi Dar ili kumpeleka kwa mtaalam Bagamoyo.

Wiki moja toka niliporudi toka Tewe kwa marehemu mzee Kidereko nilipata taarifa zingine ambazo hazikinishtua sana japo zilikuwa zikisikitisha kuwa God alifariki wiki moja iliyopita akiwa njiani kupelekwa kwa mganga Bagamoyo.
Mi moyo kwatu baada ya kumtia adabu mbaya wangu na kuapa kila atakayemgusa mke wangu sitakuwa na simile naye. Adhabu yangu nilipanga kuwa kifo tena cha mateso


Utaendelea Leo jioni.
Nikiingia jf cha kwanza kuangalia post yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sehemu ya 48

Wiki moja toka niliporudi toka Tewe kwa marehemu mzee Kidereko nilipata taarifa zingine ambazo hazikinishtua sana japo zilikuwa zikisikitisha kuwa God alifariki wiki moja iliyopita akiwa njiani kupelekwa kwa mganga Bagamoyo.

Mi moyo kwatu baada ya kumtia adabu mbaya wangu na kuapa kila atakayemgusa mke wangu sitakuwa na simile naye. Adhabu yangu nilipanga kuwa kifo tena cha mateso.

Najua msomaji utashangaa kutoa hukumu kubwa kiasi kile, ni kweli lazima hukumu iwe kubwa kwa vile wanawake wasioolewa ni wengi kuliko walioolewa kwa nini mtu amfuate mke wa mtu? Kwa hilo mtanisamehe na wala sikuwa tayari kumweleza mke wangu kama bado anaendelea na tabia yake chafu aache japo aliniahidi hatarudia tena huku akibubujikwa na machozi ya uchungu.

Siku zote niliamini mwanamke huwa hana kosa kwa vile yeye hufuatwa na mtu anayemfuata anajua kabisa ni mke wangu kibaya mtu huyo anayenifahamu vizuri. Mtu anayekufahamu na kukuchulia mkeo mpaka kufanya vile amekudharau, basi mimi kazi yangu nilipanga moja kumlambisha udongo kila atakayetembea na mke wangu.

Mzee Kidereko alinikataza kutengeneza tego kwa mke wangu kwani alinieleza siyo zuri sana, lingeweza kumsumbua hata kumletea madhara anapofanya mapenzi na mtu kama nikiwa nimesafiri.

Kwa vile nilifundishwa vitu vingi na dawa zingine zilikuwa zinapatikana kwenye maduka ya dawa za asili ambazo ukizitengeneza kwa kuchanganya na baadhi ya vitu unatengeneza bomu la hatari.

Namshukuru Mungu baada ya kifo cha mgoni wangu hali ya utulivu ilirudi kwenye nyumba yangu huku mke wangu akijitadi kuonesha amebadilika kweli hata mavazi yake yalikuwa ya heshimu aliijali familia yake kuliko kitu chochote siku zote. Alijitahidi kunifanya niamini makosa aliyofanya yalimuumiza sana na kutokuwa tayari kuyarudia tena.

Kwa upande wangu sikuwa na tatizo lolote nilimuacha afanye lolote ila kazi kwa huyo atakayenichukulia mke wangu ndiye ambaye angezipata salamu zangu.
Siku zilikatika nikiwa na siri nzito moyoni ya mke wangu kutoka nje ya ndoa mara ya pili na kuchukua uamuzi wa kuyakatisha maisha ya mpangaji mwenzangu katika mateso mazito.

Mke wangu alijua nimemsamehe na ile kubakia siri yetu, kweli ilibakia siri yetu lakini adhabu niliyoitoa kwa ajili ya mtu aliyetembea naye ilikuwa kubwa sana ambayo niliingilia hukumu ya Mungu ambayo alitakiwa yeye kutoa uhai wa mtu na si mwanadamu kama mimi.

Nilimshukuru Mungu siri ile nzito ilibakia moyoni mwangu niliamini kama rafiki yangu Simon angesikia alichokifanya mke wangu cha kuomba msamaha huku akilia kwa uchungu tena mbele yake kuwa hata rudia tena na kusikia amerudia kosa lilelile la kutembea na mpangaji mwenzangu pia nami kwenda kwa mzee Kidereko na kumuua kwa mateso mazito mpangaji mwenzangu kwa kifo cha mateso mazito.

Taarifa zilisema God kabla ya kufa aliteseka siku tatu katika maumivu makali huku damu zikimtoka mpaka akawekewa kanga nzima kuzuia damu.

Nataka kukuambia uchawi upo jiepushe na vitu vya watu mateso yake makubwa hasa kutembea na mke au mume wa mtu. Kwangu mimi pamoja na kuyafanyiwa yote na marehemu mzee Kidereko huku nikipewa moyo kila nililotaka litatimia, mwanzo niliona ni uongo hata kifo cha mgoni wangu wa kwanza nilijua ni amri ya Mungu.

Lakini kifo cha mgoni wangu wa pili na yote niliyoelezwa yakatokea niliamini kweli uchawi upo unaua na unatesa katika mateso mazito.
Mwaka ulikatika toka kifo cha mgoni wangu huku ndoa yangu ikizidi kuimalika. Wakati huo mke wangu alikuwa ameshika ujauzito mwingine.

Wakati huo maisha nayo yalizi kuninyookea wakati huo nilikuwa nimepandishwa cheo baada ya dawa za mzee Kidereko na kuwa mtunza stoo ya vifaa vya ujenzi wa barabara. Mwili nao ulichukua nafasi yake na kitambi juu.
Yeyote aliyeniona wakati wa mateso ya ndoa yangu nilipobakia kichwa tu kama kiluilui cha chura asingeamini.

Nilipendeza kazi ilinikubali niliweza kutengeneza fedha kwa kuuza vifaa vya ujenzi kwa kuandika vifaa vingi ambavyo vichache vilifanya kazi na nilivyozidisha niliuza na kupata fedha ambayo iliniwezesha kununua kiwanja na kujenga nyumba huku nikipanga baada ya nyumba yangu kwisha basi niwachukue wazazi wangu ambao muda ule nami niliona muda muafaka kuwahudumia wazazi wangu ambao Mungu alinitunzia ili waje wale jasho la mtoto wao.

Siku zote Mungu akikuandikia ndiyo hakuna kipingamizi, kila mpango niliopanga uliniingizia fedha. Kama nilivyoelezwa na mzee Kidereko kwamba kila atakayenifanyia ubaya basi utamrudia mwenyewe.

Mafanikio yangu kazini baadhi ya watu yaliwaumiza.
Mfanyakazi mwenzangu mmoja alikwenda kwa bosi kunichongea kuwa naliibia kampuni. Taarifa ile ilifanya nisimamishwe kazi na uchunguzi ulianza mara moja, katika hesabu za vifaa stoo, ilionekana kila kitu kipo sawa na kufanya aliyekwenda kunichongea kufukuzwa kazi kwa kusa la udanganyifu.

Baada ya kukosa ushahidi nilirudishwa kazini.
Niliamini maisha nimeyapatia kwa kipindi kile, baada ya kukamilisha nyumba yangu nilitaka kwenda kufanyia surprise wazazi wangu ya kuwahamisha. Taarifa ya ujenzi wa nyumba niliwapa na kuniombea kwa Mungu isimame haraka.

Baada ya kumaliza nyumba yangu ningekwenda kuwachukua japo sikuwaeleza kuwachukua moja kwa moja hiyo nilitaka kuifanya baada ya kuwachukua.

Niliazima gari la kampuni Land Cruser, nililiendesha mwenyewe hadi nyumbani kwa kutumia saa tatu badala ya tano kwa mwendo wa kasi niliokuwa nikitembea nao.

Nilipoingia eneo la nyumbani nilikuwa na hamu ya kuonana na wazazi wangu. Kila nilipokuwa nikikaribia nyumbani furaha ilizidi mara dufu kuwaona wazazi wangu. Lazima niseme ukweli katika vitu nilivyokuwa nikivipenda chini ya jua, walikuwa wazazi wangu ambao kwangu waliyokuwa kila kitu.

Naamini upole na busara ya ndoa nilirithi kwa baba ambaye alinieleza udhaifu wa mwanamke ambao siku zote kuwa mwalimu wao ni mmoja, kwa hiyo tulitakiwa tuwavumilie sana na kunieleza mwanamke unatakiwa kumuacha baada ya ndani kukosekanaa suruhu pia kushindwa kwa wazazi wa pande mbili.

Kwangu mimi niliamini kumfumania mke ni taraka isiyo na shaka. Lakini mapenzi yangu kwa mke wangu yalikuwa makubwa sana kiasi cha kushindwa kutoa uamuzi mzito kama ule kwa kuamini mke wangu atajirekebisha.

Pamoja na dhambi niliyochuma ya kutoa roho ya viumbe wawili kwa ajili yake. Kwangu niliamini walistahili adhabu ile kutokana na wao kujua kabisa waliomshawishi ni mke wa mtu. Duniani wanawake walioolewa ni wachache kuliko wasio na wanaume mtu kumfuata mkeo ni uchokozi wa makusudi.

Mtu kuwaacha wanawake wote kumfuata mkeo, adhabu yoyote utakayompa ni saizi yake kabisa. Kwangu niliamini mke wangu hana kosa ila aliyemfuata na kumshawishi akijua ni mke wa mtu huyo ndiye niliyeamini ndiye mwenye makosa na alistahili adhabu,
Baba yangu alinieleza siku zote mwanamke moyo wake huwa mwepesi kushawishika kama mama yetu Hawa alivyoshawishiwa na kusababisha wanadamu tuishi katika shida vivyo hivyo kizazi chake nacho kitakuwa hivyo.

Kwa udhaifu wa wanawake nilikuwa tayari kumpigania mke wangu, baada ya kuwatia adabu ndoa yangu ilitulia na kujikuta nikiona matunda ya kumpigania mke wangu ambaye siku zote niliamini ni mwanamke bora kwangu.

Nilipokaribia nyumbani ambako nilikuwa nimeanzisha ujenzi mpya wa nyumba ambayo nilipanga kuipangisha yote na kuondoka na wazazi wangu kwenda kukaa nao karibu ili wale matunda ya mtoto wao. Siku zote mke wangu ndiye aliyekuwa akinishawishi niwalete wazazi wangu karibu.

Nilipofika nyumbani sikukuta mtu nje ila mlango ulikuwa wazi, pembeni kulikuwa na vyombo vilivyokuwa vikioshwa na kuachwa bila kumaliziwa, kuonesha wenyeji wangu hawako mbali. Niliita kwa sauti:
“Mamaaa..babaaa, nimefika mwanenu,” nilisema huku nikigonga mlango.
“Pita ndani baba,” sauti ya mama ilijibu toka ndani.

Niliingia hadi sebuleni ambako hapakuwa na mtu. Nilijiuliza kauli ya mama inatoka nje au ndani? Nilikiwa bado nimesimama sauti ya mama ilitoka chumbani kwao ikiniita.
“Kazala.”
“Naam mama, vipi unaumwa?”
“Hapana, ila baba yako ndiye simwelewi.”
“Kafanya nini tena baba?” nilishtuka.
“Ingia chumbani.”

Niliingia chumbani kwa wazazi wangu na kumkuta mama amemlaza baba mapajani kwake akionesha anaumwa sana.
“Mama! Kuna nini?” hali ile ilinitisha.
“Hii hali hata siielewi baba yako alikuwa mzima kabisa, muda mfupi uliopita tulikuwa nje wote tukizungumza mi’ naosha vyombo yeye akisoma gazeti.

Mara ghafla alisema kitu kimemchoma chini ya mbavu kama kichomi na kumfanya ainame kwa maumivu.
“Nilimsaidia kumuingiza ndani ili apumzike lakini muda unavyozidi kwenda joto la mwili liliongezeka na jasho jingi kumtoka. Nilichukua maji na kitambaa kumkanda mwili wote kidogo joto limepungua.

“Kabla sijatoka nje kaanza kulalamika kichwa kinamuuma kama kinataka kupasuka. Mpaka baba yako anatokwa machozi ujue kashikika kweli. Kichwa kilipoanza kumuuma alikuwa akilalamika, lakini kauli ilikata ghafla kila nikimwita hakufumbua mdogo waka kujigeuza alitulia tu kama unavyomuona,” mama alisema kwa huzuni.

“Mmh! Utakuwa ugonjwa gani unaobadilika kama kinyonga?”
“Ninavyo utazama si wa kawaida yaani kilichotokea ni muda mfupi, lakini mpaka sasa ukimuangalia baba yako kama kaugua wiki nzima.”

Niliiangali hali ya baba kwa kweli ilikuwa mbaya, sikuamini kauli ya mama eti baba kaumwa muda mfupi ndiyo kawa vile. Niliamini ananidanganya kwa vile nimetokea nyumbani ghafla bila taarifa.
“Mama si kweli, inaonekana baba kaumwa muda mrefu, kwa leo tu ndiyo awe hivi? Haiwezekanani ugonjwa wa muda mfupi awe hivi,” sikukubaliana na mama.

“Mwanangu nikudanganye ili iweje? Kawaulize hata majirani kuhusu hali ya baba yako. Wao nao hawajui kama yupo kwenye hali hii. Nina imani wakimwona hataamini. Mwanangu hiki ni kitu cha kunishangaza sana.”

“Sawa mama nimekuelewa, basi tumuwahishe baba hospitali.”
“Ngoja nikamwite rafiki yake baba Pasko akusaidie, mimi hata nguvu sina,” mama alionekana amechanganywa na ugonjwa wa baba.

“Basi mama wahi.”
Baada ya mama kutoka nje, nilimsogelea baba na kuushangaa uso wake ulikuwa umekonda na midomo kumkauka. Hali ile ilionesha baba hakuumwa muda mfupi kama mama alivyosema. Niliamini alikuwa akiumwa kawaida ila siku ile ndiyo alizidiwa sana. Nilimwita baba aliyekuwa amekata kauli kwa sauti ya chini.
“Baba..baba..amka, mimi Kazala mwanao nipo hapa,” lakini baba hakunyanyua mdomo wala kukapua macho.
 
Sehemu ya 49

Baba..baba..amka, mimi Kazala mwanao nipo hapa,” lakini baba hakunyanyua mdomo wala kukapua macho.
Nilijiuliza baba yangu anaumwa nini mpaka kuwa katika hali kama ile. Mama alirudi na mzee Samweli baba Pasko na kuingia ndani.

Mzee Samweli alipomuona alishtuka na kuhoji.
“Jamani mzee mwenzangu kapatwa na nini?”

“Kama nilivyokueleza,” mama alimjibu mzee Samweli, kwa vile mimi nilikuwa sijui chochote juu ya ugonjwa wa baba.
“Ha! Kazala umekuja saa ngapi baba?”
“Hata dakika tano sina nimefika na kukutana na hali hii, shikamoo baba.”
“Marahaba, Jamani si nimepita nimewaacha mnazungumza hapo nje?” Ilionesha mzee Samweli naye alishtuka sana kuiona hali ya baba ilivyokuwa.

“Kama nilivyokueleza,” mama alijibu akiwa amejikunyata kwa hofu ya ugonjwa wa baba.
“Mama, baba alikuwa akiumwa kabla ya leo?” nilijikuta nikimuuliza mama swali la awali ambalo jibu lake sikukubaliana nalo.
“Mwanangu muulize hata baba Pasko kama baba yako alikuwa akiumwa hata kidole.”

“Kazala baba yako alikuwa mzima wa afya njema, asubuhi tulikwenda wote kwenye kahawa na kurudi. Baada ya muda nilipita nikielekea ofisini kulikuwa na kikao cha kata, wakati wa kurudi nimewakuta mama na baba yako wapo nje mama yako akiosha vyombo na baba yako akisoma gazeti na kumuomba akimaliza kusoma aniazime.

Nashangaa kuelezwa anaumwa tena amekata kauli na kushangaa zaidi kuonekana kama ameumwa muda mrefu,” kauli ya mzee Samweli ilinishtua sana.
“Sasa hii itakuwa nini?” niliuliza baada ya kuchanganywa na taarifa ile.
“Tumwahishe kwanza hospitali tu,” mzee Samweli alitoa wazo.

Nilitoka kwenda kufungua gari kisha nilirudi ndani kusaidiana na mzee Samwel kumbeba baba kumpeleka nje kwenye gari. Baada ya kumweka vizuri kwa kumlaza kwenye miguu ya mama, nililiondoa gari kuelekea hospitali. Mzee Samweli alitusindikiza.

Sikutaka kwenda hospitali ya wilaya niliamua kwenda moja kwa moja hospitali ya taifa, ambako kulikuwa na rafiki yangu aliyekuwa mkoani na baadaye kuhamishiwa hospitali ya rufaa.
Tukiwa njiani alisikia baba akikoroma kwa muda kisha alivuta mkoromo mrefu na kutulia. Hali ile ilinishtua na kunifanya nimuulize mama.

“Mama vipi tena?”
“Hakuna tatizo, twende tu.”
Niliendesha gari kwa kasi, kidogo nipate ajali lakini nilimshukuru Mungu nilifika salama. Nilipofika tulichukua kitanda haraka na kuja kumchukua baba aliyekuwa amelegea sana.

Nilishtuka kumuona mama akizidi kutokwa na machozi. Nilijua ni kutokana na uchungu wa ugonjwa wa ghafla wa baba. Baada ya kufanikiwa kumlaza kwenye kitanda cha mataili, tulimuingiza moja kwa moja kwa daktari hata bila kukata cheti.

Daktari aliacha kazi zote na kumuhudumia baba ambaye ilionesha wazi yupo mahututi. Baada ya kumwagalia huku akimpima kwa kumminya baadhi ya sehemu ya mwili. Baada ya muda aliomba wote tutoke nje, wote tulitii amri na kutoka nje kumuacha daktari afanye kazi yake.

Kilichokuwa kikinishangaza machozi ya mama yaliyokuwa yakiendelea kububujika, pamoja nami kuwa na uchungu nilijikaza huku nikimuombea kwa Mungu.

“Mama usilie baba atapona tu,” nilimsogelea mama kumliwaza.
“Tumuombe Mungu lakini...” mama hakumalizia alinamisha kichwa chini na kuendelea kumwaga machozi na kunifanya nizidi kuwa katika wakati mgumu.
“Mama nini? Baba atapona tu.”
Baada ya muda daktari alitoka na kuuliza:

“Nani muhusika wa mgonjwa?”
“Wote, mimi mtoto na huyu ni mama yangu mke wa mgonjwa,” nilijibu mimi.
“Basi nakuomba wewe ndani mara moja.”
“Mimi,” niliuliza huku nikijishika kifuani.
“Ndiyo.”

Niliingia chumba cha daktari ambako baba alikuwa amelazwa kwenye kitanda kilichokuwa kimezungushwa pazia za kijani. Baada ya kuingia ofisini nilikaribishwa kwenye kiti na kutulia kwa muda huku daktari akiandika kwenye karatasi.

“Samahani ndugu yangu, mzee anaitwa nani?”
“Hasani Kazala.”
“Mzee ameumwa kwa muda gani?”
“Kwa maelezo ya mama, saa moja iliyopita alikuwa haumwi kitu chochote.”
“Wewe unakaa wapi?”

“Mkoani.”
“Umefika lini?”
“Kama robo saa iliyopita na kukuta hali ya baba imebadilika nusu saa iliyopita.”
“Una ndugu zako?”
“Nipo peke yangu kama roho kwa wazazi wangu.”

“Kwa vile wewe ndiye kichwa na mwanaume nataka kukueleza ukweli kuhusu hali ya baba yako,” daktari alinyamaza na kuvuta pumzi na kunifanya nimtazame usoni.
“Wewe mwanaume, baba yako amefariki.”

“Eti baba kafanya nini?” nilishtuka kidogo nianguke kwenye kiti.
“Jikaze ndugu yangu, wewe mtoto wa kiume kwani unatakiwa kumpoza mama ambaye anakutegemea.”
“Daktari kweli baba amekufa?” niliuliza kama sikumsikia mwanzo.

“Kitambo, mmemleta hapa akiwa tayari ameisha kata roho.”
“Nini kimemuua?” nilimuuliza huku nikijifuta jasho la mshtuko.
“Kwa kweli mpaka tumfanyie uchunguzi wa kitaalamu.”
“Mmh! Sawa.”
“Basi mweleze mama vizuri ili asipate mshtuko.”

“Sawa nimekuelewa, japokuwa najua ni kazi kumweleza bila kupata mshtuko.”
“Jitahidi wewe ndiye unayetegemewa kwa sasa baada ya baba yako,” maneno ya daktari yalinijaza nguvu.
Nilitoka hadi nje huku nikijikaza kiume ili kuhakikisha mama namweleza kwa utaratibu ili asipatwe na mshtuko.

Pamoja na kujikaza moyoni nilikuwa na uchungu wa kumpoteza baba yangu kipenzi. Nilikwenda kumweleza mama hali halisi iliyokuwa ndani.
Nilishangaa kumkuta mama ameinama kwenye kifua cha mzee Samweli kuonesha anabembelezwa.

“Mama..mama,” nilimwita huku nikijitahidi kuficha maumivu makali moyoni.
“Kazala mwanangu kuna mabadiliko?” mama aliniuliza huku akinitazama macho yake yalikuwa yamejaa machozi.

“Ya nini mama?”
“Ya hali ya baba yako.”
“Mama..ba.b..,”
“Kazala najua.. najua kila kitu najua mwanangu, nilichokiona najua ndicho ulichokutana nacho ndani, pole mwanangu,” kauli ya mama ilinishtua na kujiuliza anamaanisha nini.

“Kipi mama?”
“Hakuna chochote naijua hali ya baba yako ndiyo maana mwanangu unatokwa na machozi.”
“Ma..ma.m.ma,” kauli ya mama ilinifanya nishindwe kuzungumza na kuhisi maumivu upya.

Nilikumbatiana na mama kila mtu alitokwa na machozi tulilia kilio cha kimyakimya.
“Jamani najua tumeumia wote, lakini muda huu tunatakiwa tujue marehemu wetu tunamhifadhi vipi?” mzee Samweli alisema.

“Wanataka kumfanyia uchunguzi ili kujua kifo chake kimetokana na nini?” nilijibu huku nikiachiana na mama.
“Hapana mwanangu baba yako alikataa kumlaza mochwali au kufanyiwa uchunguzi wa kifo chake. Aliwahi kusema akifa azikwe tu, kwa vile kila mwanadamu kifo ni haki yake.”

“Mama ni ghafla sana, lazima tujue sababu ya kifo chake.”
“Ukijua ndiyo utamrudisha duniani?” mama aliniuliza swali akiwa amenikazia macho yaliyojaa machozi.
“Hapana mama, ila ni muhimu kujua.”
“Siwezi kwenda kinyume na agizo la baba yako, hata mimi mama yako nikifa nizikwe siku hiyohiyo sitaki kilazwa kwenye mafriji au kufanyiwa uchunguzi wa kifo changu.”

“Sasa tutafanyaje ukiwa amefariki muda huu? Hatuwezi kumzika leo, lazima tuwataarifu ndugu na jamaa, mazishi lazima yawe kesho.”
“Hilo halina tatizo.”
“Sasa mwili wa baba tutaufanya nini?”
“Tunatakiwa tuuchukue leo ukalale nyumbani ili uzikwe kesho.”

“Sawa mama,” nilikubaliana na mama.
Tuliingia chumba cha daktari ambako mwili wa baba ulikuwa umelazwa kwenye kitanda na kuzungushiwa pazia za kijani. Tulitaka kuutengeneza kabla ya kumchukua. Wote watatu tulisogea kwenye kitanda kilichokuwa na mwili wa baba.

Kitu kilicho tushangaza wote kilikuwa uso wa baba kuwa katika hali ya kawaida. Uso wake haukuwa na mkunjo wowote, haukuwa uso uliokonda alikuwa yuleyule baba yangu ninaye mtambua.
Hali ile ilitufanya tutazamane, mzee Samweli hakuvumilia alisema.

“Hapana hii mpya, sijawahi kuona mgonjwa akonde akifa anenepe.”
“Hata mimi nashangaa!” mama alisema.
“Hapa si bure, kuna sababu,” nilichangia.
“Wee! Koma, maneno gani hayo,” mama alinikomesha, siku zote hakuamini ushirikina aliuita mambo ya kishenzi.

“Mama hii si hali ya kuiacha ipite hivihivi, lazima kuna kitu baba kafanyiwa kama ameugua kwa muda mfupi na kukonda uso na kufa kisha kurudi kwenye hali ya kawaida, hata ukikataa kuna kitu.”
“Kazala achana na mawazo ya kijinga, baba yako amekufa tumzike na tumuombee kwa Mungu.”
“Sawa mama,” nilikuba kishingo upande.

Baada ya taratibu zote za kuustiri mwili wa baba na kuchukua kalatasi ya taarifa ya kifo. Tuliuchukua mwili wa baba kwa kukodi pick up. Mama na mzee Samweli walitangulia na mwili wa baba mimi niliondoka na gari nililokuja nalo.

Njiani roho iliniuma sana baba yangu kushindwa kuiona nyumba yangu, heri angeingia hata mara moja kwenye nyumba yangu, ambayo ndiyo niliiandaa kwa ajili ya kuwalea wazazi wangu.

Lakini nilichopanga kilienda tofauti, niliumia sana tena sana kumpoteza baba yangu aliyekuwa mtu muhimu sana kwenye maisha yangu. Ndiye aliyekuwa taa na dira yangu, siku zote alinipa nguvu sehemu niliyokata tamaa na kujiona ninacho hata kama sina.

Bado nilitakiwa kumshukuru Mungu kuniachia mama yangu ambaye niliamini ndiye nitaye ekeza nguvu zangu zote kwake baada ya kumpoteza baba kipenzi.
Kingine kilichonipa wakati mgumu wa taarifa ya ugonjwa wa baba wa kuugua ghafla kisha kukonda kama mtu aliyeugua kipindi kirefu na baada ya kufa, uso wake kurudi kwenye hali ya kawaida.

Kwangu mimi nilijua ule ni mchezo nimechezewa bila kujua nimechezewa na nani. Roho iliniuma sana kufariki kwa mzee Kidereko kwangu ningejua kila kitu. Moyoni mwangu sikumuafikiri mama kukubali kirahisi kiasi kile, ingekuwa mimi, mwili wa baba nisingeuzika haraka ungekaa hata mwaka mzima mochwali ili nipate uhakika wa kifo chake.

Niliamini kifo kile hakikuwa cha kawaida na pengine baba yangu hakufa aligeuzwa msukule.
Nilipanga baada msiba kwisha nisafiri kuchunguza kifo cha baba ambacho kwa upande wangu sikukubaliana nacho.
****
 
Back
Top Bottom