Simulizi: Mchawi

Simulizi: Mchawi

SEHEMU YA 42

“Kwa nini tuandikie mate na wino upo? We twende halafu uniulize swali hilo baada ya kutoka kwa babu.”
Tulikubaliana kesho nikaombe ruhusa kazini ili twende Mkoa wa Tanga kwa mtaalam.
***

Siku ya pili nilikwenda kazini kuomba ruhusa. Bosi alinikubalia bila kuniuliza swali lolote. Kwa muda mfupi nilikuwa nimekonda kwa mawazo, usiombe kumpenda mtu asiyejua thamani ya upendo wako kwake. Sikutaka kuomba mkopo kwa vile zilikuwa tarehe za mshahara, wafanyakazi wengi mifuko ilikuwa imenona.

Kwa vile muda ulikuwa bado, baada ya ruhusa tuliondoka siku ileile saa tano na kufika Chalinze saa kumi na mbili jioni. Mwenyeji wangu alinieleza itatubidi tulale pale ili tuondoke siku ya pili kutokana na umbali wa kufika Lushoto. Tulilala Chalinze na kusubiri mpaka siku ya pili tupande basi linalotoka Dar es salaam kwenda Lishoto.

Siku ya pili tulipanda basi lililotoka Dar na kufika Lushoto kwenye Kijiji cha Mlalo saa kumi jioni. Hatukukaa, tulichukua usafiri mwingine wa baiskeli kuingia vijiji vya ndani zaidi mpaka katika Kijiji cha Tewe kilichokuwa kinasifika kwa kuwa na waganga wenye uwezo wa juu.

Tulifika Tewe majira ya saa kumi na moja jioni na kwenda kwa mtaalamu mzee Kidereko. Tulifika katika nyumba moja kubwa kiasi ya matofali na bati iliyokuwa imezungukwa na uzio wa miti ya minyaa.

Ndani kulikuwa na nyumba nyingine ndogo nne za miti na udongo na juu zilikuwa zimeezekwa kwa makuti ya mnazi. Tulikaribishwa na wenyeji wetu ambao walimfahamu sana Shedu na kuonesha mwenzangu ni mwenyeji sana pale.

“Jamani Shedu karibu,” dada mmoja aliyekuwa amejifunga kitenge kilichopauka alimchangamkia Shedu na kuonesha jinsi gani Shedu alivyokuwa mwenyeji pale kijijini.

“Asante Mwana, za hapa?”
“Nzuri ka Shedu, karibu mgeni,” nilikaribishwa na mimi huku nikipokewa mzigo wangu.

“Asante.”
Tulipelekwa hadi chini ya mti wa mwembe kulikokuwa na jamvi lililokuwa limechoka na pembeni yake kulikuwa na vigoda.
“Jamani karibuni.”
“Asante, za hapa?” Shedu aliuliza.
“Mmh! Kama unavyoziona, maisha magumu.”

“Mwana magumu wakati unatakata?”
“Inatubidi tuyazoee maisha ya huku kwa lazima, kwa vile hatuna jinsi nina imani nimekuona kidogo nitacheka.”

“Ondoa hofu, mzee yupo wapi?”
Amekwenda porini kuna kazi ya mtu amekwenda kumfanyia, nina imani muda wowote atarejea.”

“Ameondoka saa ngapi?”
“Toka saa tisa usiku.”
“Mmh! Inaonekana ni nzito.”
“Na kweli, kuna mtu alilazwa chini na wabaya wake akaletwa hajitambui na kutibiwa na mzee baada ya kupona aliruhusiwa.

Miezi minne baadaye alipigwa kombora lingine lililomkata kauli mpaka watu wakajua amekufa. Taarifa zilipomfikia mzee alikwenda mjini na kumnyanyua kisha alimweleza aje huku amtengeneze vizuri.

Alifika jana jioni kama ninyi na kulala hapa usiku ndipo walipoamka na kuelekea porini ambako atamfanyia kinga ambayo itamlinda mtu atakayemgusa ataondoka yeye.”

Nilijikuta nikivutwa na mazungumzo ya Shedu na yule msichana anayeitwa Mwana.
“Namuamini mzee, lazima mtu alale chini.”
“Tena amekasirika sana kitendo cha kupimwa nguvu na mtu.”
“Kidereko tena.”

“Mmh, na ninyi?”
“Ndugu yangu ana shida ndogo.”
“Shedu, shida ndogo ndiyo mpande basi kuja huku, si nasikia mjini kuna wataalam ambao hawana uwezo mkubwa, wakishindwa ndipo mnakuja huku?”
“Mwana kazi zangu zote huzifanya mzee Kidereko kwa hiyo hata rafiki yangu alipopatwa na tatizo sikutaka asumbuke wa waganga uchwara nikaona nimlete kwa mzee.”

“Mmh! Sawa, tena huyo anaingia.”
Kauli ya yule msichana ilifanya wote tugeuke kuangalia kwenye mlango wa uzio na kumuona mzee mmoja aliyekuwa akitembea kwa kujivuta na mkongojo mkononi akiwa na vijana wawili waliokuwa wamebeba kapu na majani mabichi mkononi.

Shedu alinyanyuka na kwenda kumpokea mzee Kidereko.
“Babuuu.”
“Babuuuu.”
Walikumbatiana na kuja nilipokuwa nimekaa, nami nilinyanyuka kumpokea mzee Kidereko.

“Shikamoo babu.”
“Marhahaba karibu.”
“Asante babu.”

Walipokelewa kikapu na majani waliyotoka nayo porini na kupumzika kwenye mkeka. Wote walipumzika kwa kujilaza kuonesha wamechoka sana. Kutokana na kuchoka sana vijana wale baada ya kujilaza usingizi mzito uliwachukua na kuanza kukoroma.

Lakini mzee Kidereko alinyanyuka na kuelekea ndani kwake na kutuacha tukiwa tumekaa kwenye vigoda. Muda nao ulikuwa unazidi kuyoyoma, kigiza kilianza kuimeza nuru ya mchana.
“Mzee huyu kiboko,” Shedu alinieleza kwa sauti ya chini.
“Kweli anatisha kwa maelezo mafupi inaonesha anaijua sana fani ya ‘mizizioloji’.”

Saa moja kasoro kililetwa chakula, wali na bata ambacho tulikuwa wote, baada ya chakula ndipo mzee Kidereko alipotuita pembeni kwa mazungumzo.

“Jamani karibuni, sikuweza kuzungumza na ninyi nilipofika tulikuwa hoi sana kama mlivyowaona wenzenu.”

“Ni kweli babu,” Shedu alijibu.
“Mmh! Shedu za siku?”
“Nzuri babu.”
“Mambo yako yanakwendaje?”
“Yanakwenda vizuri.”

“Kazini?”
”Panakwenda vizuri yale mambo yalienda kama ulivyoniahidi.”

“Kwa hiyo asante yangu umeniletea?”
“Ndiyo, tena nimeshukuru jamaa yangu kukubali kuja huku nilete na asante yako.”

“Na mkeo katulia?”
“Kila mtu anashangaa, hata ndugu walioanza kuiandama ndoa yangu wametulia.”

Kauli ile ilinishtua na kujiuliza ndoa ya Shedu ilikuwa na tatizo gani lililopata msaada wa babu? Lakini nilitulia kimya na kupanga kumuuliza tukiwa wawili japo nilianza kuhisi huenda kilichompata ndicho kilichonifikisha pale.

“Mmhu, mwenzio ana tatizo gani?” mzee Kidereko aliuliza.
“Kama langu, lakini la kwake limezidi, mkewe kamkimbia kabisa na inasemekana ameolewa kabisa na mtu aliyemchukua.”

“Mmh! Mjini mbona tabia za kuchukuliana wanawake zimeshamiri, wanadamu bwana! Wanawake wapo wengi lakini wanapenda wake za watu. Tatizo si kubwa kama mngekuja mapema mngeweza kugeuza leo hii.

Nitaifanya sasa hivi ili kesho alfajiri muwahi kurudi kwenu.”
“Nitashukuru mzee wangu, kweli mke wangu atarudi?” Nilijikuta nikiuliza.
“Hiyo kazi niachie mimi maadamu umeileta kwangu.”

“Nitashukuru mzee wangu.”
“Unataka aliyemchukua mkeo tumfanyeje?”
“Vyoyote ukakavyoona mzee wangu.”
“Tumuue?”

“Hapana.”
”Tumtie uchizi?”
“Mmh! Hakuna adhabu nyingine?”
“Zipo nyingi utakayotaka mwenyewe.”
“Yeyote ya kawaida la muhimu nimpate mke wangu.”

“Kazala lazima tumtie adabu, mzee mfanyie kama yangu.”
Nilishtuka na kujiuliza kama yake ipo vipi? Ilibidi niulize.

“Ulimpa adhabu gani?”
“Nilimpoteza kwenye sura ya dunia,” Shedu alijibu kwa kujiamini.

“Ha! Unamaanisha ulimuua?”
“Ndiyo! Kanitesa sana yule mshenzi kasababisha mwanangu wa kwanza afe baada ya mke wangu kumuacha na kwenda kwa huyo mwanaume na kusababisha mwanangu afe kwenye beseni la maji.”

“Mungu wangu!” nilishtuka na kushika mdomo.
“Kibaya mtu yule hakuishia hapo, alimchanganya mke wangu kiasi cha kudai talaka.

Nilimfuata na kumueleza aachane na mke wangu majibu aliyonijibu yalikuwa ya udhalilishaji. Eti aliniambia kama namuona mke wangu anafaidi kuwa naye na mimi niwe mpenzi wake.”
“Uwe mpenzi wake alimaanisha nini?”
“Eti niwe mkewe.”
“Mungu wangu!” kauli ile ilinishtua sana.

“Kazala wee acha tu, mtu akiwa na fedha ana dharau ndiyo maana jambo lako nililichukua kama langu. Kazala nimeteseka mpaka nilipoletwa huku kwa mzee Kidereko.”

“Ina maana ulikuwa humjui tokea awali?”
“Matatizo ndiyo yaliyonifanya nifike huku, we si unajua kabila langu?”
“Nilishangaa pale uliponileta huku na kabila lako, nikajua baba ndiye Mnyamwezi na mama mtu wa Tanga.”
“Walaa.”
“Yalikuwa mateso ya muda gani?”
“Miezi nane lakini kwangu ilikuwa miaka mia nane.”

“Pole sana, mhu ikawaje?” nilijikuta nikiwa na shauku baada ya kuona matukio yetu yanafanana sana.

“Baada ya kuletwa huku sikutaka adhabu kali, lakini babu aliniambia mtu huyo nikimchelewesha ataniwahi mimi.”
“Kutokana na mateso niliyoyapata na uchungu wa kifo cha mwanangu nilikubali.”

“mmh! Ikawaje?”
“Basi mzee akatengeneza mambo, sikuwepo ila waliokuwepo na kutoa ushuhuda walisema baada ya kwenda nyumba ya wageni na mke wangu ambaye yeye alijimilikisha na kuwa mkewe. Kutokana na maneno aliyoyasema mke wangu, aliyekuwepo kwenye tukio wakiwa faragha.

“Baada ya kumaliza mchezo wao uume haukupoa, uliendelea kusimama kama chuma na kumsababishia maumivu makali sana.

Alipopiga kelele za maumivu ilibidi achukuliwe na kupelekwa hospitali, huko alipigwa sindano za ganzi ili uume upoe lakini wapi, kila dakika maumivu yalikuwa makali, alilia mpaka sauti ikakauka.

Nasikia alinitaja mimi ili niende akaniombe msamaha.
“Nguvu zilimwisha mateso yale yaliendelea kwa saa nane, jioni uume ulinywea na yeye kufariki dunia.”

“Mmh! Aliteseka sana.”
“Yeye kwa saa nane mimi miezi minane, kuchanganyikiwa kubaya nakumbuka kuna kipindi nilikuwa natembea nikizungumza peke yangu. Kingine hali yangu ya kimaisha ilikuwa mbaya hapo ndipo nilipozidi kuumia.”

“Baada ya hapo nini kiliendelea?” nilijikuta nikivutwa na simulizi ya Shedu.
“Mke wangu alirudi huku mtaani kila mmoja akiniheshimu mpaka leo hakuna mtu wa kumgusa mke wangu. Hata akija mgeni lazima atapewa taarifa za yule jamaa aliyejitia kidume na kulamba udongo. Basi akipata taarifa ile humkalia mbali mke wangu.”

“Lakini mbona kama adhabu ni kubwa sana.”
“Kazala acha huruma, wanadamu si wa kuwachekea ona anavyoteseka kwa haki yako.”

“Sawa lakini kuua!” bado niliona adhabu ya kuua ni kubwa.
“Kijana acha ujinga, siku zote akuanzae mmalize,” mzee Kidereko alisema.
“Sawa mzee wangu, mi shida yangu kumrudisha mke wangu tu si kuua.”
“Sawa, ila lolote litakalotokea usirudi hapa.”

“Kwa nini babu?”
“Inaonekana hujihurumii, kwa hiyo naomba ukiondoka hapa usirudi labda uje na lingine. Mimi hupenda kufanya kazi mara moja ili usirudi hapa kwa kazi hiyohiyo. Kwa akili ya mkeo hata kama atarudi bado ataendelea kukusumbua. Nakueleza utarudi hapa nguo zipo kichwani.”

“Kwa nini unasema hivyo?”
“We si mtoto mdogo mambo mangapi kakufanyia mkeo nusra ujiue, kweli uongo?”

“Kweli.”
“Sasa kwa nini mtu aliyetaka kukusababishia ujiue unamuonea huruma? Nataka kukueleza huruma ikizidi hugeuka uchawi wa kukuzuru mwenyewe hasa kwa adui yako.”

Nilitulia kwa muda nikiwaza na kuwazua juu ya adhabu wanayotaka kuifanya kwa mwanaume aliyemchukua mke wangu. Kauli za kurudi nguo nimeweka kichwani zilinitisha sana na kujua kurudi pale nitakuwa mwendawazimu.

Niliwa nimezama kwenye dimbwi la mawazo mzee Kidereko alinishtua:
“Sasa amua tufanye kazi kamili au nusu?”
 
SEHEMU YA 43

Nilitulia kwa muda nikiwaza na kuwazua juu ya adhabu wanayotaka kuifanya kwa mwanaume aliyemchukua mke wangu. Kauli za kurudi nguo nimeweka kichwani zilinitisha sana na kujua kurudi pale nitakuwa mwendawazimu.

Niliwa nimezama kwenye dimbwi la mawazo mzee Kidereko alinishtua:
Sasa amua tufanye kazi kamili au nusu?
Mzee Kidereko fanya kazi kamili, Shedu alisema.

Shedu usimsemee mwenzako mwache aseme mwenyewe.
Mzee Kidereko usimsikilize huyu jamaa, sisi ndiyo tunajua anavyoteseka, tena kurudi na nguo kichwani umemhurumia atabakia jina. Juzi tu amechungulia kaburi.

Hata kama yote hayo yamemtokea bado ana hiyari ya kuepukana na tatizo hilo au kuendelea kuteseka.

Mzee tumetoka mbali shida yetu ni kulimaliza tatizo hilo hasa tukizingatia sasa hivi kaolewa kabisa, Shedu alizidi kushadadia.
Bado mwenye uamuzi wa mwisho ni yeye mwenyewe.

Ubishani ule ulinifanya nikumbuke mateso mazito aliyonipa mke wangu na dharau ya yule mwanaume, kwanza kumfanya mwanangu achelewe kutembea, pili kulala na mke wangu katika chumba na kitanda changu.

Ile ilikuwa ni dharau kubwa sana na mbaya zaidi kumchukua jumla na kumuoa, japo sikuwa na uhakika nalo lakini ile ilikuwa kauli ya mke wangu kwenye barua yake aliyoniandikia siku alipoamua kuondoka.
Moyo uliniuma mpaka machozi yalinitoka na mishipa ya kichwa kusimama.

Nilinyanyua sura kuwaangalia wote waliokuwa kimya wakisubiri jibu langu. Moyoni sauti iliingia ikiniambia mtu yule hastahili huruma hata kidogo.
Babu maliza kazi, nilijikuta nikitamka kwa sauti.

Kwa moyo wako au kwa kulazimishwa?
Kwa moyo wangu.
Kweli?
Kweli kabisa.
Kazala huo ndiyo uanaume, Shedu aliuunga mkono uamuzi wangu.
Basi ngoja tuifanye hii kazi ile kesho muwahi kuondoka.

Sawa.
Tulikwenda kwenye kibanda kimoja ambacho ndicho alikuwa akifanyia kazi zake. Kilikuwa na vitendea kazi vyake, baada ya kukaa kwenye mkeka aliagiza beseni dogo la maji, baada ya muda lililetwa. Baada ya kuletewa aliweka maji na kuniuliza:

Huyo bwana unamjua jina?
Simjui.
Nipe jina la mkeo.
Anaitwa Suzana.
Jina la mama yake?
Maria.

Baada ya kumpa majina yale alichukua dawa ya unga huku akilitaja jina la mke wangu kwa sauti ya chini, aliunyunyizia ule unga kwenye maji yale. Baada ya muda aliniita na kuniuliza:

Huyu si mkeo?
Ha! Ndiye, nilishtuka kumuona mke wangu ndani ya beseni lile ikiwa kama natazama video.
Ni kweli ni yeye? mganga aliniuliza tena.
Ndiyo mzee wangu.
“Na huyo aliyekaa pembeni yake unamjua?

Nilituliza macho yangu kumuangalia yule mwanaume aliyekuwa amekaa na mke wangu, akiwa kifua wazi na kugundua ndiyo yule mwanaume niliyemuona kitandani na mke wangu.
Huyu ndiye aliyemchukua mke wangu, nilisema kwa sauti, macho yakiwa yamenitoka pima.

Kweli ni yeye? aliniuliza tena mzee Kidereko.
Ndiye.
Sasa tunamtoa mkeo na kumbakisha mwenyewe kisha nitakuelekeza kitu cha kufanya.

Hakuna tatizo.
Baada ya kusema vile alichukua dawa ya unga na kunyunyizia kwenye maji huku akizungumza kwa sauti ya chini sana ambayo sikusikia anazungumza nini huku nikiangalia kwa macho yangu.

Mara nilimuona mke wangu akinyanyuka na kuondoka, akabakia yule mwanaume peke yake kwenye kochi.
Sasa nuiza kifo chochote unachotaka kimpate.

Cha ajali.
Nuiza.
Mganga alinipa unga ule niuweke kwenye maji kwa kuunyunyizia, nilifanya vile huku nikinuiza kutaka yule mwanaume afe kifo cha ajali kwa kuamini kifo kile hakiwezi kuwafanya watu waniwazie vibaya. Baada ya kunuiza kimoyomoyo, nilimwambia nimemaliza.

Baada ya kusema vile alichukua kisu kikubwa cha kuchinjia mbuzi na kukiweka kwenye yale maji na kusema:

Majibu ya kazi yetu tutaangalia asubuhi wakati mnaondoka kama haikukubali itabidi mbaki tufanye tena upya.

Lakini kazi zangu ninazowahi kufanya katika mia basi mbili tu ziligoma lakini niliporudia zilikubali.
Baada ya zoezi lile mganga alichukua beseni la maji na kutoka nalo nje, baada ya muda alituita nje kumfuata.

Tulipotoka katika kilinge cha mganga, tulikwenda kwenye sehemu tuliyopangiwa kulala ili asubuhi tuondoke kurudi Dar. Tulilala kwenye mkeka, tukiwa tumejilaza nilimuuliza Shedu.
Shedu kazi iliyofanyika hiyohiyo tu au kuna nyingine?

Kwa nini?
Naona tumefanya ya kumuua yule jamaa, vipi kuhusu mke wangu kurudi?
Jamaa akifa tu, mkeo anarudi nyumbani.
Itawezekana kweli?
Kama ingekuwa haiwezekani angekwambia, yule mzee amekwishaona kila kitu.

Mmh! Sawa.
Usiwe na wasi tukirudi utakubali na wewe mwenyewe utamletea huyu mzee zawadi.
Haya.

Tulilala mpaka alfajiri tulipoamshwa na mzee Kidereko, tulipoamka alitueleza kuwa ngoma imekuwa nzito.

Vijana ngoma imebuma.
Kivipi?
Muziki mnene, alisema huku akituonesha beseni lililokuwa na maji na kisu, lilikuwa kama jana lilivyowekwa.

Mbona hatuelewi?
Jamaa kajitengeneza sana.
Umejuaje?
Kama ingekubali tungekuta maji haya yamegeuka na kuwa damu.

Unafikiri ni kwa nini?
Jamaa anaonekana yupo sawa.
Kwa hiyo?
Kuna kazi ya ziada inatakiwa kufanyika, tuliyofanya ilikuwa ya kawaida sana.

Sasa itakuwaje?
Safari imekufa, tutarudia tena leo jioni.
Kauli ile ilinitisha na kuiona kama vita yangu na mwanaume aliyemchukua mke wangu ni kubwa sana tofauti na matumaini niliyopewa.

Hatukuwa na jinsi, tulikubali kushinda pale kijijini mpaka jioni tulipongia kwenye kazi nyingine. Safari ile alichemsha maji kwenye chungu, yalipokuwa yakichemka aliweka dawa na kunieleza nishike kisu na kukiingiza ndani ya yale maji yaliyokuwa yakichemka.

Japo ndani ya chungu hakukuwa na kitu kingine lakini kila nilipoingiza kisu kiligoma.

Vipi mbona huingizi kisu? mzee Kidereko aliniuliza.
Kimegoma, inaonesha kuna kitu ndani ya chungu, nilimweleza mganga baada ya kisu kugoma kuingia.

Hebu toa kisu, aliniamuru kukitoa kisu.
Nilitoa kisu, mganga alichukua dawa ya unga na kuiweka kwenye yale maji yaliyokuwa yakichemka kisha aliweka maji yaliyokuwa kwenye chupa ndogo na kunieleza nikiingize tena kisu.

Kisu kiliingia kama kinaingia sehemu iliyokuwa ngumu, ghafla maji kwenye chungu yalibadilika na kuwa damu.

Endelea kukiingiza kisu kwa nguvu, mganga alinieleza nitumie nguvu.
Kila nilivyojitahidi kukiingiza ilifika sehemu kikagoma kabisa kwenda mbele wala kutoka nje.
Chomoa kwanza.
Nilipochomoa kiligoma kutoka.

Kimegoma.
Hebu, ilibidi akitoe mwenyewe ndani ya maji ambayo yalikwishaanza kutoa harufu ya damu mbichi. Baada ya kukitoa kisu maji yalirudi katika hali ya kawaida. Hali ile ilimshtua mganga na kumsikia akishusha pumzi nzito na kusema:

Mmh! Hapa kazi ipo.
Nilimuona akikuna kichwa na kukitazama chungu ambacho ghafla kiliacha kuchemka japo moto ulikuwa bado unawaka. Nilijikuta nikichanganyikiwa, hata Shedu naye alionekana kushtushwa na tukio lile ambalo bado sikuelewa tatizo lipo wapi.

Nilisikia mganga akisema: Hapa lazima turoge kazi hii ifanyike saa nane za usiku, hatuna jinsi! Mtu tunayepambana naye si mtu mdogo, kajidhatiti ndiyo maana ameamua kufanya aliyotaka. Lakini muda si mrefu atanijua mimi ni nani, sijawahi kushindwa na kitu japokuwa hili ni tukio langu kubwa kunisumbua lakini lazima nitamaliza kazi.

“Kazi hii sasa hivi ninatakiwa kuifanya mwenyewe kwa vile wewe ni mwepesi, nitaondoka mwenyewe usiku nikirudi kila kitu kitakuwa kama kilivyopangwa.

Kwa jinsi hali ilivyokuwa, nilijua na siku inayofuata tutalala palepale na kuanza kuingiwa na wasiwasi kama ile kazi imemshinda. Pia nilikuwa na hofu ya kuchelewa hata kazini, lakini sikuwa na jinsi, siku ile tulilala palepale mpaka siku ya pili
 
BINAFSI NIKO TAYARI KUCHANGIA CHOCHOTE MAANA STORI ZAKO KWANGU NI MUDA WA KUPUMZISHA AKILI
SEHEMU YA 41

Siku ya Jumamosi ilipofika, nilikodi pikipiki kwa ajili ya kuzunguka makanisa yote ya mjini. Kanisa kubwa lilikuwa katikati ya mji pia madogo yalikuwa pembeni kidogo na mji hayakupungua manne.

Niliamini hata kama ningezunguka kutwa nzima nitaweza kufika toka kanisa moja kwenda lingine kwa wakati bila kuchelewa.

Dereva wa pikipiki aliniuliza swali baada ya kuzunguka zaidi ya mara mbili makanisa yote ambayo hayakuonesha dalili zozote za kufungwa ndoa.

“Sikiliza ndugu yangu, tutamaliza mafuta bure, kwa nini tusiende kwenye ofisi za kanisa ili tujue kuna ndoa au hakuna na kama ipo itafungwa saa ngapi? Hiyo itatusaidia kuja kwa wakati kuliko kuzunguka na kukufanya upoteze fedha nyingi.”

Wazo lile nilikubaliana nalo na kuamua kwenda kwenye ofisi za kanisa kuulizia kama kuna ndoa ilikuwa ikifungwa siku ile. Makanisa yote manne yalinieleza kuwa siku ile hakukuwa na ndoa yoyote ila Jumapili kulikuwa na ndoa nne ambazo zote zingefungwa kwenye kanisa kuu tu.
Niliamini katika ndoa zile nne lazima moja itakuwa ya mke wangu kipenzi Suzana, mama Zawadi.

Nilimshukuru dereva wa pikipiki ambaye kwa sasa angeitwa bodaboda. Nilikubaliana naye kunifuata nyumbani siku inayofuata na kunipeleka kanisani ili nikaweke pingamizi ndoa ya mke wangu.

Baada ya kurudi nyumbani nilikuwa na mawazo mengi kuhusiana na hiyo kesho na kujiuliza nitakapotoa pingamizi litakubaliwa au ndiyo nitaabika hasa kutokana na ndoa yetu kufungiwa Bomani.

Upande mwingine niliamini nitakuwa na nguvu ya kuvunja ndoa ya mke wangu kwa vile ilikuwa ikitambuilika kiserikali na vyeti nilikuwa navyo.
Nilipanga kesho nikienda kuweka pingamizi niende na vyeti vya ndoa ili kutia uzito pale mke wangu atakaponikana.

Siri ile sikutaka kumshirikisha Simon kwa kuhofia kunipa ushauri mbaya ambao ungeharibu mipango yangu yote. Ushauri wa Simon mwanzo niliuamini lakini baada ya ushauri wake kusababisha mke wangu kukimbia, sikumuamini tena na kuona ndiye chanzo cha matatizo yangu.

Siku ya pili, baada ya kufuatwa na dereva wa pikipiki niliwasili kanisani saa tatu asubuhi japokuwa ndoa ilikuwa ikifungwa saa saba mchana.

Nilikaa pale mpaka saa nne na nusu ndipo magari ya maharusi na ndugu na jamaa walipoanza kuingia. Muda mfupi kanisani pakawa na watu wengi na magari kutokana na harusi nne kufungwa, nilisubiri kwa hamu nimuone mke wangu akitaka kufunga ndoa na kuweka pingamizi.

Nami nilikuwa mmoja wa watu niliowahi ndani viti vya mbele kanisani kusubiri ibada ya ndoa. Kanisa lilijaa watu wengi sana pamoja na maharusi wote. Kwa vile mabibi harusi walikuwa wameziba nyuso zao, iliniwia vigumu kumtambua mke wangu ni nani kati ya wale wanne.

Baada ya taratibu zote kufanyika ndoa zilianza kufungwa moja moja huku nikisubiri kwa hamu kuiona sura ya mke wangu. Ajabu ndoa zote zilifungwa bila kuiona sura ya mke wangu. Nilijikuta napagawa na kujiuliza nilielezwa ndoa nne au tano?

Baada ya ndoa zote kufungwa bila kushuhudia sura ya mke wangu, watu wote walitoka kanisani na kubakia peke yangu. Nilijiuliza mke wangu atakuwa amekwenda kufunga ndoa wapi.

Nikiwa nado nimesimama kama sanamu nikiwa bado na matumaini huenda kuna ndoa nyingine ingekuja kufungwa, nilishtuliwa na mhudumu wa kanisa.
“Ndugu vipi mbona huondoki na wenzako?”

“Samahani kaka kuna ndoa nyingine zaidi ya hizi?”
“Hakuna, leo kulikuwa na ndoa nne tu hakuna zaidi ya hizi.”

“Mmh! Sijui watakuwa wamekwenda kufunga ndoa wapi?” nilijikuta nikizungumza peke yangu kwa sauti.
“Kina nani?” mhudumu wa kanisa aliniuliza.

“Ooh! Samahani,” nilijikuta nikijibu na kuondoka bila kuaga mpaka nje ya kanisa.

Nje ya kanisa watu walikuwa ndiyo wanamalizikia kuondoka, nilijikuta nimerudi nyumbani kwa miguu na kumsahau dereva wa pikipiki aliyenipeleka. Kwa kweli nilikuwa nimechanganyikiwa na kuamini kama maneno aliyonieleza mke wangu yana ukweli basi atakuwa amefunga ndoa siku ile.

Usiku ulikuwa mrefu kwangu, usingizi ulinikimbia kabisa. Mawazo yote yalikuwa kwa mke wangu na kuona kama kweli ameolewa basi atakuwa amenifanyia ukatili mkubwa sana. Siku ya pili ilikuwa Jumatatu, sikuweza kwenda kazini, nilikuwa kama mtu niliyefiwa, hata chakula kilinishinda.

Jioni Simon alikuja kunitazama na mmoja wa wafanyakazi wenzangu na kunikuta nimejilaza sebuleni mikono kichwani huku pembeni ya macho yangu yakiweka michirizi na kulowesha kwenye mito ya kochi. Simon alinishangaa sana na kuniuliza:

“Kazala una matatizo gani?”
“Simon wewe si wakuniuliza swali kama hilo, unajua vizuri matatizo yangu,” nilimjibu bila kumuangalia.
“Kazala umetoka nyumbani kufuata mapenzi au kazi?”

“Nimefuata kazi.”
“Unaacha kwenda kazini kwa ajili ya mwanamke, nilikueleza toka zamani kuwa huyu mwanamke si chaguo sahihi kwako, lakini ukaona labda nakuchokonoa majibu sasa umeyaona.”

“Simon usiseme hivyo wewe ndiyo sababu ya mke wangu kunikimbia.”
“Mimi?” Kauli yangu ilimshtua Simon.
“Ndiyo.”
“Mimi nimefanya nini?” alionesha kushangaa.

“Ushauri wako ndiyo sababu ya mke wangu kukimbia.”
“Kweli aliyekuroga amekufa, kitendo cha kumfumania mkeo ni mimi? Si ulitaka kufa kwa mawazo nimekusaidia bado huoni msaada wangu?”

“Msaada gani wakati mke wangu kanikimbia.”
“Mkeo yule sawa na kuku aliyelala nje, si kuku tena ni kwale.”
“Lakini umeona lawama zote zinatokana na ninyi watu wa pembeni kuingilia ndoa yangu.”

“Hao watu wa pembeni unaowalaumu ndiyo waliomponya mwanao aliyekuwa fundi majiko.”

“Pamoja na hayo, lakini ninyi ndiyo chanzo cha mke wangu kukimbia.”
“Kwani shemeji kaenda wapi?” Shedu, mfanyakazi mwenzangu aliyeongozana na Simon aliniuliza.

“Hata najua yule mwanamke kaamua kuniua ningali hai,” nilizungumza kwa sauti ya kukata tamaa.
“Kazala wanawake wamekwisha mpaka uchanganyikiwe kiasi hiki?” Shedu aliniuliza.

“Kwani huyo aliyemchukua mke wangu hakuona wanawake wengine mpaka kamchukua mke wangu? Kibaya zaidi jana kamuoa kabisa.”
“Utani huo! Atamuoaje mke wa mtu?” Shedu alishtuka.

“Mpaka kamtoa kwangu atashindwa vipi kumuoa kabisa?”
“Kwa hiyo Kazala bado unampenda mkeo?” Shedu aliniuliza akinikazia macho.
“Tena sana.”
“Na akirudi utakuwa tayari kumsamehe?”

“Ndiyo, najua si akili yake ni ushawishi wa watu wenye fedha wanaoona maskini kama sisi hatuna haki ya kuwa na wanawake wazuri.”

“Mtu mwenyewe unamjua?”
“Kwa sura namjua ila sijui anakaa wapi?”
“Upo tayari kumeza mfupa?”

“Una maana gani?”
“Najua huna uwezo wa kushindana na yule bwana kwa nguvu na fedha, lakini lipo kimbilio la wanyonge nakwambia mkeo atarudi mwenyewe.”
“Kimbilio la wanyonge! Kimbilio gani?” nilishtuka kusikia vile na kutaka kulijua hilo kimbilio la wanyonge.

“Kwa babu.”
“Kwa babu una maana gani?”
“Kwa mganga wa kienyeji.”
“Kweli ataweza?” nilimuuliza kutaka uhakika.

“Bwana wee tena hawa wanaopenda wake za watu kazi yake ndogo sana, nakwambia ndani ya siku mbili mkeo atarudi, ikivuka haifiki wiki.”

“Kweli?”
“Kweli kabisa, unajua taarifa zako nimezisikia toka kwa swahiba wangu hapa, roho iliniuma na kuona umefanyiwa ukatili, kibaya nasikia jamaa ana mke yaani asiridhike na mkewe aje amchukue wako? Tena nitakupeleka mguu kwa mguu hadi kwa mzee wangu, nakuapia mkeo atarudi,” Shedu alinihakikishia kunirejeshea furaha.

“Kama kamuoa?” niliuliza swali ambalo kwangu lilikuwa tata.
“Nimekueleza mkeo atarudi, si mkeo wa ndoa?”
“Ndiyo.”
“Basi atarudi huyo, tukifika kwa babu kazi imekwisha.”

“Gharama zake?”
“Si kubwa sana, utamudu tu.”
“Huyo babu yupo wapi?”
“Tanga katika Wilaya ya Lushoto Kijiji cha Mlalo kisha unaingia ndani zaidi kuna sehemu inaitwa Tewe, hapo temea mate chini kuna kufuru za ajabu, watu wanaweza hata kumfufua maiti akatembea.”

“Nauli yake si kubwa?”
“Ya kawaida utaimudu.”
“Mmh! Nipo tayari hata kesho.”
“Itabidi muombe ruhusa ya siku mbili ili mwende na kurudi,” Simon aliyekuwa kimya muda wote alichangia.
“Lakini Shedu usemacho ni kweli?” pamoja na Simon kuchangia bado sikumuamini Shedu.

“Kwa nini tuandikie mate na wino upo? We twende halafu uniulize swali hilo baada ya kutoka kwa babu.”
Tulikubaliana kesho nikaombe ruhusa kazini ili twende Mkoa wa Tanga kwa mtaalam.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SEHEMU YA 44

“Kazi hii sasa hivi ninatakiwa kuifanya mwenyewe kwa vile wewe ni mwepesi, nitaondoka mwenyewe usiku nikirudi kila kitu kitakuwa kama kilivyopangwa.
Kwa jinsi hali ilivyokuwa, nilijua na siku inayofuata tutalala palepale na kuanza kuingiwa na wasiwasi kama ile kazi imemshinda. Pia nilikuwa na hofu ya kuchelewa hata kazini, lakini sikuwa na jinsi, siku ile tulilala palepale mpaka siku ya pili.

Siku ya pili baada ya kufungua kinywa, nilipelekwa porini ambako nilichanjwa juu ya kichuguu kupewa kinga kwa ajili ya kupambana na adui yangu ambaye alionekana amejidhatiti katika nguvu za giza.

Nilipewa kinga ambayo nilielezwa hakuna mtu anayeweza kunigusa na hata mambo yangu yatakuwa na wepesi tofauti na mwanzo. Kutokana na kazi kuwa nzito nilitakiwa kununua mbuzi mwekundu. Nilifanya vile kwa kutoa fedha kisha aliwatuma watoto wake kwenda kumtafuta mbuzi huyo mwekundu asiye na baka lolote.

Watoto walirudi jioni wakiwa na mbuzi kwa ajili ya kafara yangu ya usiku ya kumkomesha mbaya wangu. Siku ile tuliendelea kusota kwa mganga mpaka majira ya saa mbili ndipo mbuzi yule alipovishwa sanda na kuchinjwa na damu yake kumiminiwa ndani ya shimo lililochimbwa kama kaburi.

Tulimzika ndani ya shimo lile akiwa ndani ya sanda na mganga akatuambia tukalale kwa ajili ya kujiandaa na safari ya siku ya pili alfajiri.
Vijana wangu kazi imekwenda vizuri, kesho safari ya kurudi mjini ipo kama kawaida.

Tutashukuru mzee wangu, nilishukuru kwa vile nilikuwa nimeshaanza kuchoka kijijini.
Kazi imekwenda vizuri inaoneka hata tiba niliyokupa asubuhi imekusaidia sana.
Kwa hiyo mzee kazi itakwenda kama ilivyopangwa? nilimuuliza.

Shaka ondoa, japo kazi ilikuwa ni kubwa bado usiku nitatoka peke yangu kwenda kumaliza kazi ndogo iliyobakia.
Je, ikienda kinyume? bado nilimdadisi mganga.

Haiwezi, nilichokifanya ni uchawi mkubwa sana. Mganga alinihakikishia.
Kauli ile ilinishtua na kujiuliza uchawi na uganga una tofauti gani, sikutaka kuuliza kitu lakini moyoni niliomba basi kafara yake ifanikiwe ili turudi mjini kwani maeneo yale yalikuwa yameanza kunikera. Tulilala mpaka siku ya pili ambapo tuliamshwa saa kumi na moja na nusu alfajiri, baridi ikiwa kali sana.

Nilidhani tungeambiwa tujiandae na safari lakini haikuwa hivyo, tulipewa taarifa iliyonivunja nguvu na kutamani kulia. Tulielezwa kuwa mzee Kidereko tangu aondoke jana usiku hajarudi hivyo tulitakiwa kuingia porini kumtafuta.
Kwangu yale yalikuwa mapya na kujiuliza tunakwenda kumtafuta sehemu gani porini.

hatukuwa na jinsi, tuliondoka zaidi ya watu sita wakiwemo watoto wawili wa kiume wa mganga na wasaidizi wake kuelekea porini huku msaidizi wake akitangulia mbele na usinga ili kutuelekeza mzee Kidereko yupo wapi.

Tulitembea porini kwa saa mbili bila kupumzika bila kujua mzee Kidereko yupo wapi. Lakini muda wote msaidizi wake aliyekuwa ametangulia mbele na usinga alitueleza kuwa muda sio mrefu tutamuona mzee Kidereko. Baada ya mwendo kidogo tulishtuka kuona matone ya damu.

Ningekuwa peke yangu ningetimua mbio au kubadili njia lakini mwenye usinga alielekea upande uleule. Tuliwafuata nyuma mimi na Shedu walipoelekea huku nikijiuliza zile damu ni za nini?

Tuliendelea kuzifuata zile damu ambazo ziliongezeka kila tuliposogea mbele huku ikionesha majani kuvurugwa kama kulikuwa na vita nzito.

Huyu hapa, sauti ya mtoto wa mzee Kidereko ilitushtua sote na kugeukia kwenye majani yaliyoonekana kulala kama kulikuwa na ugomvi wa tembo.

Tuliposogea nilishtuka kumuona mzee Kidereko amelala akiwa ameshikilia pembe nyeusi iliyokuwa imefungwa na kitambaa chekundu kwa chini na mwili wake hasa sehemu za kifuani na tumboni zikionesha damu iliyoanza kuganda.

Nilijua mzee Kidereko ngoma imemshinda na kusababisha mauti yake, baada ya kumuona wasaidizi wake walitueleza turudi nyuma. Walitoa unga mweupe na kuanza kuurusha eneo lote kisha walitoa maji kwenye chupa ndogo na kumwagia kichwani mzee Kidereko ambaye bado alikuwa ametulia kama tulivyomkuta.

Kazi ilikuwa nzito, alisema msaidizi wake aliyekuwa akifungua kichupa kidogo na kutoa dawa aliyoiweka kwenye pua ya mzee Kidereko. Baada ya sekunde chake alipiga chafya mfululizo na kuamka, alikaa kitako na kututazama wote kisha alimuuliza msaidizi wake.

Umekuja na utanduo?
Ndiyo
Nipe.
Alitoa pembe ndogo na kumkabidhi mzee Kidereko, aliichukua na kuifungua kwa chini kisha alitoa unga mweusi na kuuweka mkononi na kupuliza kidogo uliobakia aliutupia wote mdomoni na kunyanyuka. Tuliongozana naye kurudi nyumbani.

Tulipofika alikuwa amechoka sana baada ya kuoga na kula aliingia ndani mwake kulala. Tulibakia njia panda na Shedu bila kujua nini kinaendelea kwani tulikuwa tumemaliza siku ya nne, tofauti na ruhusa tuliyopewa kazini ya siku mbili. Nikiwa nimekaa na Shedu chini ya mti nilimuuliza rafiki yangu.

Shedu nini kinaendelea mbona sielewi?
Kazala hata mimi nimechanganyikiwa, hata sijui nini kinaendelea.
Shedu usipojua wewe mimi si ndiyo nazidi kuchanganyikiwa kabisa.
Kazala haijawahi kutokea toka nimfahamu mzee Kidereko.

Sasa hii ni nini?
Yaani sielewi, ni wazi aliyemchukua mkeo ni mtu aliyejidhatiti sana.
Kwa hiyo kazi imemshinda?
Mmh! Sijajua, hebu tusubiri aamke.
Kwa kweli nimeshakata tamaa.

Kazala huwezi kuamini, hata mimi nimechanganyikiwa, toka nimfahamu mzee Kidereko na sifa zake kwa kazi nzito alizowahi kufanya hii yako imekuwa ya kwanza kumtokea. Hajawahi kushindwa na kitu, hata wasaidizi wake nao wamechanganyikiwa.

Sasa huku tutakaa siku ngapi wakati tumezidisha siku moja zaidi ya muda tulioomba?
Tumsubiri aamke ili tujue nini kinaendelea, kama ameshindwa tujue moja.

Na akisema hajashindwa tutafanyaje kama hajawahi kushindwa hawezi kukubali kirahisi namna ile, lazima anaweza kutueleza tuongeze siku.
Tutamuomba tuondoke kuwahi kazini ili tupange siku nyingine turudi.
Siamini kama ataiweza tena kama ametaka kufa nina wasiwasi kama atalazimisha anaweza kufa bure.

Kweli nimeamini mwenye uwezo wa juu ni Mungu peke yake, nilivyomuamini mzee Kidereko amechemka kwa siku nne. Kweli hakuna marefu yasiyo na ncha.

Maneno ya Shedu yalinikatisha tamaa na kurudiwa na imani yangu ya awali kuwa hakuna uchawi bali kuna mazingaombwe. Nilijikuta nikianza kumuwaza upya mke wangu na kuamini hakukuwa na suluhu yoyote ya kumrudisha zaidi ya kuendelea kuteseka. Mpaka jioni inaingia mzee Kidereko alikuwa bado hajaamka.

Pale nyumbani palikuwa kimya kila mtu aliendelea na shughuli zake kama hakikutokea kitu chochote cha hatari.

Jioni ya siku ile tulizunguka kwenye baadhi ya vijiji, giza lilipoingia tulirudi nyumbani. Tulikuta mzee Kidereko bado hajaamka, kitu kilichotutia wasiwasi kwani alilala kuanzia asubuhi mpaka jioni. Nilijiuliza usingizi gani huo au ndiyo kapitiliza kabisa?

Hali ya utulivu uliokuwepo ilizidi kutupa wasiwasi na kujiuliza nini hatma ya yote. Majira ya saa tatu usiku tulifuatwa na yule binti aliyetupokea siku ya kwanza tuliyofika.

Mzee anawaita.
Mzee gani? nilijikuta nikiuliza.
Jamani kaka Kazala hapa nyumbani kuna wazee wangapi?
Mmoja.
Basi ndiye anayewaita.
Ameamka?
Ndiyo.

Saa ngapi?
Muda mrefu ameoga amekula na kupumzika.
Lakini hajambo?
Hajambo mbona hali ile ya kawaida tumeizoea kazi hii yataka moyo la sivyo utaiacha.

Tuliongozana na yule msichana hadi ndani ya nyumba ya mzee Kidereko, ilikuwa tofauti na siku zote ambazo huzungumzia nje, chini ya mwembe au kilingeni kwake. Alipotuona alitukaribisha.

Karibuni vijana wangu.
Asante mzee, shikamoo.
Marahaba karibu mketi.
Asante.
Tulikaa kwenye viti vya kukunja na kusubiri alichotuitia. Baada ya ukimya mfupi alizungumza.

Vijana wangu.
Naam mzee, tuliitikia kwa pamoja.
Kwanza poleni kwa kuwachelewesha tofauti na tulivyokubaliana na matarajio yenu.

Kawaida mzee, tukupe pole wewe kwa matatizo uliyokutana nayo, nilimpa pole kwa kuamini hata kama angekufa mimi ndiye ningekuwa chanzo.

Wala usihofu ile ni moja ya kazi zetu, kazi nyingine lazima ujitolee uhai ufe wewe au afe yeye.
Kwa hiyo kazi imekuwa nzito?
Ilikuwa si nzito sana japo kidogo iondoke na roho ya mtu.

Unamaanisha nini?
Baada ya kafara ya mbuzi mwekundu, kazi iliyokuwa imebakia ni kummaliza kabisa kumbe katika sehemu ya uhai wake kuna ulinzi mkubwa uliomzunguka yaani atakayegusa lazima aondoke.
Baada ya kuingia porini ili kumalizi kazi, kilikuja kitu cha ajabu ambacho nimepambana nacho mpaka alfajiri.

Ilikuwa vita nzito ambayo kwangu ilikuwa mara ya pili japo hii ilikuwa kubwa kidogo. Lakini mpaka naishiwa nguvu nilikuwa nimemaliza kazi, kama ningeishiwa nguvu sijamaliza ningekufa mimi.

Mungu wangu, nilishtuka.
Usishtuke ni jambo la kawaida kwetu waganga.
Kwa hiyo?
Kesho mnaweza kurudi kazi imeisha.
Kuhusu yule jamaa itakuwaje?
Kazi imeisha hivi mkirudi mtakuta msiba.
Msiba?

Ndiyo.
Wa nani?
Wa adui yako.
Kafa lini?
Alfajiri ya leo.
Mmh! Umejuaje?
Ndiyo kazi yangu, wewe umeleta si juu yako kujua kila kitu kinachofanyika zaidi ya kufanikisha kilichokuleta.

Nini kilichomuua?
Wewe ulitaka afe kwa nini?
Ajali.
Basi kafa kwa ajali leo alfajiri, asingekufa ningekufa mimi.

Mmh!
Basi nina imani kazi imekwisha japo ilikuwa nzito nashukuru imeisha salama. Japokuwa kuna wakati nilianza kuchanganyikiwa. Lakini niliamini nitamuweza tu asingeweza kushindana na mimi huku ndiko Tewe hakujawahi kushindwa kitu.

Basi tunashukuru, na mke wangu?”
Atarudi mwenyewe wala hakuna haja ya kutumia dawa kwa vile aliyekuwa akimzuzua ameshakufa.

Mmh! Mzee kweli atarudi?
Baada ya kifo kafukuzwa na ndugu wa huyo mwanaume na kumuona yeye ndiye nuksi.

Kwa hiyo?
Utamuona mwenyewe anarudi kuomba radhi, nina imani atatulia kwani kama ni adhabu atakuwa ameipata.

Tuliagana na mzee Kidereko nikiwa siamini na kuona kama vile mzee kazi imemshinda na kuamua kutuondoa kijanja. Tulikwenda kulala kujiandaa na safari ya kesho alfajiri kurudi tulipotoka ili tuwahi kazini japo tulikuwa tumepitisha siku mbili.

Tuliamshwa alfajiri ya siku ya pili kwa ajili ya safari, kwa vile kulikuwa na baridi kali hatukuweza kuoga, tulinawa uso tu.
Kazala mwanangu kazi yangu japo ilikuwa ngumu lakini nimeimaliza vizuri sana. Ningekuwa mtu mwepesi pale uliponikuta mngekuta mzoga wangu.

Ukisema mzoga una maana gani? nilimuuliza.
Mngekuta nimekufa.
Mmh! niliguna.

Kazi ilikuwa nzito tofauti na nilivyofikiria kumbe mtu yule naye amejidhatiti kwa miti shamba lakini Tewe ni kila kitu hatujawahi kushindwa na kitu.

Nashukuru mzee wangu, na kuhusu mke wangu?
Atarudi tu haitakiwi kutumia nguvu, mkewe anakupenda sana Kama nilivyokueleza jana alipokwenda kunawaka moto.

Asante mzee wangu nitashukuru sana.
Ila nakuomba kitu kimoja, ulilofanya huku libakie siri yako watu wao ndiyo watakaozungumza yao kuhusiana na kifo cha mgoni wako. Na kifo hiki ni vigumu mtu kujua kwa vile mazingira ya kifo chake hakuna mtu atakuwa na wasiwasi kwa kuamini ni amri ya Mungu.

Sawa mzee wangu, nitafanya hivyo.
Haya nawatakia kazi njema, mzee Kidereko alimpatia Shedu kifurushi kidogo na kumwambia:
Hii ni zawadi yako.
Asante, Shedu alipokea kile kifurushi nikijua ni cha dawa japo sikutaka kujua dawa ya nini.

Sikutaka kuhoji kapewa nini kwa vile ile ilikuwa hainihusu, baada kila kitu kwenda kama kilivyopangwa tulisindikizwa na vijana wa mzee Kidereko kwa baiskeli mpaka Mlalo ambako tulifika saa moja kamili asubuhi, kabla magari ya kuelekea Dar hayajaondoka. Tulibahatika kupata tiketi kwenye basi la Umba kwani basi la Shambalai lilikuwa limejaa. Tuliingia na kukaa kwenye siti ya watu wawili.

Saa mbili gari liliondoka Mlalo na kuelekea Dar es Salaam, Shedu alionesha alikuwa na usingizi kwani safari ilipoanza tu aliuchapa usingizi, mimi niliendelea kuuangalia Mji wa Mlalo. Akili yangu ilikuwa njia panda nisipate jibu kuhusu mwanaume aliyemchukua mke wangu kufariki dunia kwa ajali kama ni kweli.
Akili yangu haikuamini, nilijua yule mzee katutoa kisiasa ili tu tusiondoke tukiwa hatuna imani naye.

Sifa alizonipa Shedu na niliyoyakuta niliona kuna tofauti kubwa. Lakini sikutaka kuumiza kichwa, ukweli na uongo wa mganga nilijua ningeujua baada ya kufika mjini.
Kwa vile nami niliamka alfajiri pia usingizi wa sehemu usiyoizoea huwezi kulala vizuri, nami usingizi ulinipitia bila kujijua.

Nilishtuliwa usingizini na Shedu ambaye alionekana ameamka kipindi wakati mi bado ninachapa usingizi.
Kazala amka tupate chakula cha mchana.
Wapi hapa? niliuliza baada ya kuona tumefika kwenye kituo cha basi.
Korogwe.
Sasa ni saa ngapi naona jua kali?
Saa saba.

He! Kumbe nimelala sana! nilijishangaa kulala muda mrefu bila kuamka.
Tuliteremka Korogwe na kupata chakula cha mchana kisha tulirudi kwenye basi kuendelea na safari ya kurudi kwetu. Tulifika Chalinze saa tisa na nusu alasiri, kwa vile tulikuwa tukirudi nyumbani tulipanda basi linalotoka Dar saa kumi na nusu jioni. Tuliingia kwetu usiku wa saa nne.

Kwa vile muda ulikuwa bado Shedu alikwenda kwake na mimi nilirudi kwangu. Nilichoshukuru siku ya pili ilikuwa Jumamosi hakukuwa na kazi hivyo niliamini ningelala sana. Baada ya kula chakula nilichonunua nilioga na kulala kutokana na kuwa nimechoka sana.
Nilipopanda kitandani nilishtuka siku ya pili tena kwa kugongewa na jirani yangu. Nilifungua mlango na kutoka nje.

Vipi jirani za asubuhi, ulisafiri?
Nzuri, ndiyo.
Mbona hukuaga?
Ilikuwa haraka sana samahani kwa hilo.
Jana mkeo alirudi,
Eeh! nilishtuka kusikia vile
 
Back
Top Bottom