Simu yangu android juu kushoto alama hii inamaana gani

amarina

Senior Member
Joined
Jan 5, 2025
Posts
181
Reaction score
290
Naomba msaada wa kitaalam hii alama ya mshale kama diversion flan
1000048134.jpg

Inanitia wasiwasi
 
Kama wewe una mpenzi basi mpenzi wako anasikiliza calls zako.
 
Kucheki au kuhakikisa ni nani ambae izo calls zinaenda kwake:

Bonyeza *#21# kisha piga utapata nambaya huyo mtu anaesikiliza calls zako.

Menu nyingine izo:
*#62# (hapa kama aliset ukiwa hupatikani yeye ndio apatikane)
*#61# (hapa kama ww haupokei cm yy ndio apatikane)
*#67# (hapa kama cm busy yeye apatikane)
 
Hiyo alama ya mshale uliyoiona juu ya skrini ni alama ya Call Forwarding (Call Divert). Inamaanisha kuwa simu yako imewekwa kwenye hali ya kuhamisha simu zako kwenda namba nyingine au voicemail. Kwa mfano: ukipigiwa na line yako iko busy, imezima au huna network, simu zinaweza kuelekezwa moja kwa moja kwenda kwenye namba nyingine uliyochagua au voicemail.

Alama hii haionekani muda wote, hujitokeza tu pale ambapo forwarding imewashwa. Iwapo utaizima, alama hiyo hupotea moja kwa moja. Mara nyingi forwarding inaweza kuwashwa kwa makusudi na mtumiaji au wakati mwingine kwa makosa.

Jinsi ya kuiweka (ku-activate) Call Forwarding

Unaweza kuifanya kwa njia mbili:

(a) Kupitia USSD Codes
Forward simu zote (kila mtu akikupigia itaenda namba nyingine):
*21*NUMBER# kisha bonyeza Call
Mfano: *21*0712345678#

Forward simu ukiwa busy (unazungumza tayari na mtu mwingine):
*67*NUMBER#

Forward simu usipojibu:
*61*NUMBER#

Forward simu ikiwa unreachable (simu imezima/haina network):
*62*NUMBER#

(b) Kupitia Settings za simu

Fungua Phone/Dialer App

Nenda Settings > Call Settings > Call Forwarding

Chagua aina ya forwarding unayotaka (Always, Busy, No Answer, Unreachable)

Ingiza namba unayotaka simu zako ziende.

Jinsi ya kuitoa (ku-disable) Call Forwarding

Kama hutaki simu zako zi-forward tena:

##21# Inafuta forwarding ya simu zote.

##67# Inafuta forwarding ukiwa busy.

##61# Inafuta forwarding usipojibu.

##62# Inafuta forwarding ikiwa unreachable.

##002# Hii ndio code ya universal, inafuta forwarding zote kwa pamoja (busy, unanswered, unreachable na all calls).
 
Nikitaka simu za mtu zije kwangu nabonyeza ngapi mkuu
 
Back
Top Bottom