R-K-O
JF-Expert Member
- Jun 27, 2023
- 482
- 2,138
Walengwa hasa ni wale wanaopata pesa za ghafla (zawadi, kuhongwa, betting, michezo, kuotea, boom la chuoni, n.k) na wale wanaojidunduliza.
kununua simu ni hatua ya kwanza tu, bado kuna mambo yanafuata. ni sawa na gari inabidi ununue kwa kuzingatia ulaji wa mafuta, bei za spare, gharama za mafundi, n.k. ukiparamia na huna pesa ya uhakika utaumia
Hizi simu za kisasa kwa wenzetu huko zinakotengenezwa, mambo ya internet hayanaga kikomo waweza kutumia hata gb 20 kwa siku, ni wewe tu, Kimbembe kipo huku sasa, mpaka leo ni mwendo wa kupimiwa GB,
Yani ukitaka kuiga matumizi ya simu kama huko majuu inabidi uwe na bando lisilo na mawazo ndio utapata raha hata ya teknolojia mpya zilizomo, Vinginevyo utakuwa umevamia mtumbwi wa vibwengo,
Sasa unakuta mtu ananunua simu ya bei kali sana mfano milioni 1 wengine hadi 2
Kwenye matumizi sasa anachofanya ni heri angebaki na simu ya laki 1 hadi 2 maana hata bando tu ni la mawazo.
Kwa usahauri wangu kama unataka ku enjoy hizi simu na uchumi wako si wa kipedeshee, angalia gharama ya simu + bando viwieane.
mfano kama una bajeti ya milioni na unajua kabisa bando linaweza kukupiga chenga, nunua simu ya laki 4 unaweza kupata google pixel nzuri kabisa halafu hio laki 6 wekeza kwenye bando, nenda hata tigo wakupe huduma ya postpaid gb 60 kila mwezi kwa elf 50.
Kama una bajeti ya milioni 2, nunua simu hata ya laki 8 hivi, nenda vodacom wakupe internet isio na kikomo laki 1 kila mwezi, utaenjoy zaidi kuliko kuwa na simu ya milioni 2 alafu bando hata la elf 2 kwa siku linakupiga chenga.