Simpendi na sikumchagua Magufuli lakini naunga mkono 100% msimamo wake kuhusu Korona

Kukiri Corona ipo ndio njia ya kwanza kukabiliana nayo, siku zote huwezi pigana na adui usiemjua.

Rais lazima atoe kauli ili kila mmoja wetu ajue Corona ipo na achukue hatua za kujilinda kwa umakini.

Kauli ya Rais sio sawa na kauli yangu au yako, hiyo itachujuliwa kwa uzito unaostahili na wengi wataanza kuwa serious na huu ugonjwa.

Lakini Rais kuendelea kukaa kimya au kusema Tanzania hakuna Corona ndio kunapelekea watu kudharau kuchukua hatua za kujilinda.

Huko vijijini wengi hawana access ya internet kujua hali halisi tofauti na sisi tuliopo mijini, wao wakisikia Magifuli kasema hakuna Corona wanaamini hivyo, wanaendelea kuchapa kazi.

Hili halihusiani na lockdown au vyovyote, muhimu watu wajue Corona ipo seriously na wajilinde badala ya kuamini haipo wakati wengine wanaugua na hata kufa.
 
Waeleze watu ukweli ili kila mtu achukue tahadhari na sio kutangaza kuwa hakuna Corona.
Umekwisha ambiwa korona ipo na jihadhari, nawa mikono kwa maji yanayotiririka, sanitizer mikono mara kwa mara, keep distance, jifukishe NYUNGU SAANA.

Sasa akuite Chato akuambie ndio utaelewa. WAJINGA NDIO WALIWAO. Full bunch of Facebook personalities in JF.
 
Umekwisha ambiwa korona ipo na jihadhali, nawa mikono kwa maji yanayo tiririka, sanitizer mikono mara kwa mara, keep distance, jifukishe NYUNGU SAANA.

Sasa akuite Chato akuambie ndio utaelewa. WAJINGA NDIO WALIWAO. Full bunch of Facebook personalities in JF.
Jiulize hao wanaomua kuwaambia watu Corona ipo tena huku wakihatarisha maisha yao wangechagua kukaa kimya au kuunga mkono kauli za Magufuli, wangapi leo hii wangejua corona ipo?

Tumia akili kufikiri na si kutukuza watawala na matendo yao hata yale yasiyofaa.
 
Umekwisha ambiwa korona ipo na jihadhali, nawa mikono kwa maji yanayo tiririka, sanitizer mikono mara kwa mara, keep distance, jifukishe NYUNGU SAANA.

Sasa akuite Chato akuambie ndio utaelewa. WAJINGA NDIO WALIWAO. Full bunch of Facebook personalities in JF.
Mkuu kuna shw ya nandy na koffie vp utaenda?
Hivi karibuni pia kuna simba cup pia


Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Unaunga mkono kutokugunga biashara au kutokutoa maelekezo ya kunawa, kukaa mita moja na kuvaa barakoda. ? Kuna mengi sio swala mmoja ya Corona
Kwani aliyehamsisha kuchukua tahahari baada ya vyokufunguliwA ni nani?? Kama sio Rais?? Aliesema watu wavae barakoa hata za kushona ni nani? Kama sio JPM? Hivi huko ufipani mnawaza nini juu ya taifa letu??
 
Back
Top Bottom