JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,462
Zuio hilo limewekwa jana na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Yahya Nawanda, ambapo ameeleza kuwa mpaka sasa wagonjwa waliobanika kupatwa na magonjwa hayo wamefika 60 hadi 100.
Kutokana na hali hiyo na ili kuweza kudhibiti ongezeko la wagonjwa, Dkt. Nawanda ameeleza kuwa wameamua kupiga marufuku uuzaji wa vyakula katika magulio, minada mkoa mzima, pamoja na ulaji wa vyakula kwenye misiba.
“ Kuanzia sasa hakuna kupika chakula kwenye minada, magulio, lakini pia ulaji wa chakula kwenye misiba nayo kuanzia sasa tunazuia, tukimaliza kuzika kila mmoja atawanyike, hakuna kula,” amesema Dkt. Nawanda.
Amesema kuwa magonjwa hayo yamebainika kusababishwa na watu kutokuwa na vyoo bora, lakini pia utumiaji wa maji yasiyokuwa safi na salama, ambapo amebainisha wameanzisha oparesheni ya kuwakamata watu wote wasiyokuwa na vyoo.
Pia soma:
- Madai ya Mlipuko wa Kipindupindu Simiyu, RC asema ‘Ni Ugonjwa wa Matumbo, tumewapiga faini Wananchi wasio na vyoo’
- Bariadi yakumbwa na mlipuko wa kipindupindu