Simiyu: Kaya 70 zakutwa hazina vyoo, baadhi wanaweka vinyesi kwenye mfuko na kutupa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda amesema kuwa katika opereisheni aliyoiendesha kwa wiki moja kukagua suala la usafi kwa wananchi wa mkoa huo, zaidi ya kaya 70 kati ya 400 zilizokaguliwa zilikutwa hazina na vyoo kabisa.

Amesema kuwa kaya zote ambazo zilikutwa hazina vyoo, zilipigwa faini na kutakiwa kujenga vyoo haraka, ambapo amewataka wananchi wa mkoa huo kujenga tabia ya kuwa na choo bora na kukitumia.

Dkt. Nawanda amesema hayo leo, wakati wa maazimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Zanziba’r ambapo Mkoa wa Simiyu umeazimisha kwa kufanya usafi katika Mji wa Bariadi.

Amesema kuwa bado kuna changamoto kubwa ya kaya nyingi ndani ya mkoa kutokuwa na vyoo, ambao ameeleza hali hiyo imekuwa chanzo cha uwepo wa mlipuko wa magonjwa ya kuhara na kutapika.

“ Nimeshangaa leo wakati tunafanya usafi, tumekutana na mifuko ikiwa na vinyesi, hii inashiria watu bado hawazingatii usafi hata kidogo, lazima hatua kali zichukuliwe, tunalalamika kupata haya magonjwa lakini chanzo ni sisi,” amesema Dkt. Nawanda.

Mkuu wa kitengo cha usafi na udhibiti taka Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Pitter Subadi, amesema kuwa watu wote wasiopenda kufanya usafi hawatafumbiwa macho na badala yake watachukuliwa hatua kali za kisheria.
 
Tunatita vichakani. Kutita vichakani ndio mpañgo mzima
 
Sio huko Simiyu tu hata hapa Dar es salaam kwa Chalamila hali ni hiyo hiyo!
Nenda kule Mbezi beach sehemu inaitwa Rungwe kwa Nyerere na Mbuyuni uone watu walivyolundikana kwa maelfu lakini hawana sehemu ya kujisaidia, unafikiri wanajisaidia wapi ? Wanaojisaidia kwenye mifuko na kuitupa barabarani hivyo kuwa kero kwa wananchi wanaishi sehemu hizo. Pia ni hatari kwa kueneza kipindu pindu wakati wa mvua!
 
Back
Top Bottom