Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 260
- 998
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa wananchi wa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu kwa vifo vya watu wanne kufuatia ajali ya lori aina ya Scania iliyotokea katika Kijiji cha Mwamishari Juni 16 saa 3 usiku, akisema watu hao walikuwa kwenye usafiri wa kwenda kwenye mkutano wake.
Kabla ya kufika kwenye mkutano huo, Rais Samia ambaye yuko kwenye zaiara ya siku tano mkoani Simiyu, pia aliwatembelea majeruhi waliolazwa katika hospitali ya wilaya hiyo.
Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu leo Juni 17 imesema mbali na vifo hivyo, ajali hiyo imesababisha majeruhi 15, ambapo 13 kati yao ni wanaume.
"Ajali hiyo ilisababishwa na uzembe wa dereva kwa kushindwa kulimudu gari akiwa kwenye kona kali. Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu," imesema taarifa hiyo.
Pia soma ~ Watu wanne wapoteza maisha katika ajali, Polisi Wasema walikuwa wanatoka kwenye zoezi la chanjo ya mifugo na utambuzi