Simbachawene: Serikali kuangalia upya utaratibu wa kuanzisha Makanisa, Wachungaji watapaswa kuwa na Shahada ili kupunguza "Vibanda Imani"

UKO SAHIHI

Waziri haelewi anachoongea nafikiri alikuwa aongee opposite kuwa waumini wa dini ndio wawe na digrii za dini sio viongozi wa dini.Kwa sababu kama ni uelewa labda waumini ndio hawana

Sababu mtu kama mfano TB JOSHUA au Mzee mwasapile wa kikombe cha babu elimu hawana lakini maprofesa na ma doctor walienda kukinywa NA kWA TB JOSHUA NIGERIA HUFURIKA KIBAO.Imani ni kitu complicated

Yeye asisitize tu usalama maeneo ya ibada kuwa viongozi wa dini wahahakikishe kuna usalama kwenye maeneo yao ya ibada.Hayo mengine ya wanaabudu nini awaachie wenyewe kama watakanyaga mafuta au mavi ya kiongozi wa dini shauri yao
Daktari JPM, habari bila picha hainogi
tapatalk_1567993480702.jpg
 
Umeanza kukwama na wewe simba!
hiyo ni ajar ni kama ajar zingine,suala hili ni la watu wenyewe,,waelewe iman sahihi lakin na serikal ipunguze ukali wa maisha...nyie ajira mmezibana,watu wanakimbilia kwenye mafuta ndio kuna uwezekano pengine wa kupata ajira....
Acheni kuyumbisha dishi....khar ya maisha ni ngumu,moyo wa mwanadam nao umeumbwa na imani,hata jiwe unaweza amin..
 
Waziri wa mambo ya ndani Mh Simbachawene amesema kufuatia vifo vya watu 20 kwenye Huduma ya Mwamposya huko Moshi, serikali itaangalia upya utaratibu wa kusajili hizi Huduma.

Simbachawene amesema Wachungaji wanaoanzisha Huduma za kiimani watapaswa kuwa na shahada ili kupunguza " Vibanda Imani" vilivyozagaa kila kona.

Rwanda wamefanikiwa kudhibiti Vibanda Imani kwa kutumia utaratibu huu, amesisitiza Simbachawene.

Source Clouds tv!
[/QUOTE
Tena Shahada zitoke Seminary au Vyuo vya Theology vinabyojulikana. Sio Vyuo vinavyofundishwa na Nabii Tito na Mfalme Zumaridi.
 
Waziri wa mambo ya ndani Mh Simbachawene amesema kufuatia vifo vya watu 20 kwenye Huduma ya Mwamposya huko Moshi, serikali itaangalia upya utaratibu wa kusajili hizi Huduma.

Simbachawene amesema Wachungaji wanaoanzisha Huduma za kiimani watapaswa kuwa na shahada ili kupunguza " Vibanda Imani" vilivyozagaa kila kona.

Rwanda wamefanikiwa kudhibiti Vibanda Imani kwa kutumia utaratibu huu, amesisitiza Simbachawene.

Source Clouds tv!
kabisa naunga mkono hoja
 
Si kila kitu cha kuiga kutoka Rwanda , mmeiga utekaji inatosha mengine jiongezeni , wekeni tu utaratibu mzuri wa kudhibiti umati basi , Yesu Kristo alikuwa na digrii ngapi ?
 
Upumbavu wa hapa zitaibuka itikadi za kivyama khs suala hili.

CCM(watamuung mkono Simbachawene-sababu ni mwenzao) Vs CDM(Watapinga suala hilo sababu tu aliyeongea ni Simbachawene).

Ndio maisha ya kijinga tuliyojichagulia.

dodge
 
Naona hata waumini wawe na shahada pia maana sio kwa kuburuzwa huko

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Dini ni biashara inayolipa sana!

Ukitaka kumchota akili mnyama,mchote kwa kumpa chakula;ukitaka kumchota akili binadamu,mchote kiimani.

Imani sometimes huzaa ujinga, na ujinga kwenye imani huzaa upofu!

Hiyo habari ya kuwa na shahada wala haitasaidia.
nini kifanyike?
 
Tumechelewa Sana twaweza kwenda kukopi kwa wenzetu Rwanda itatusaidia Sana kuondokana na wafanyabiashara Hawa wasiolipa Kodi.

Lazima mtu awe na degree ya Theology Toka kwenye Chuo kikuu kinachotambulika na serikali. Awe pia amepitia School of Healing . Kama unapenda kazi ya mungu Basi uisomee na ugeuke kuwa passion na sio malinzi wa site Mara kaibuka kawa mtumishi sehemu Mara kakusanya watu kaanzisha kabisa Mara anapiga kelele mtaani watu hawalali Wala hawapumziki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama nchi itaendelea kuwa na kundi kubwa la Wajinga sidhani kama itasaidia sana.

Muhimu ni Serikali kuwa na miongozo yake kwa hawa 'Watumishi", haswa kwa wale wanaokusanya 'Mburula' wengi.

Serikali izuie baadhi ya mambo yasio na maana yoyote...kwani hata wanavyoibiwa/dhulumiwa ni sawa tu kwamba wamekaa pembeni kuwaacha Wananchi waibiwe, mbona Benki au taasisi zinazojishughulisha na mambo ya pesa serikali inaingialia kati?
 
We
UKO SAHIHI

Waziri haelewi anachoongea nafikiri alikuwa aongee opposite kuwa waumini wa dini ndio wawe na digrii za dini sio viongozi wa dini.Kwa sababu kama ni uelewa labda waumini ndio hawana

Sababu mtu kama mfano TB JOSHUA au Mzee mwasapile wa kikombe cha babu elimu hawana lakini maprofesa na ma doctor walienda kukinywa NA kWA TB JOSHUA NIGERIA HUFURIKA KIBAO.Imani ni kitu complicated

Yeye asisitize tu usalama maeneo ya ibada kuwa viongozi wa dini wahahakikishe kuna usalama kwenye maeneo yao ya ibada.Hayo mengine ya wanaabudu nini awaachie wenyewe kama watakanyaga mafuta au mavi ya kiongozi wa dini shauri yao

Well said, for some reason naona Waziri haja digest msimamo wa USA kuhusu Taifa letu linapo kuja suala wanalo dai wao kwamba ni ukihukwaji mkubwa wa haki za binadamu/raia Nchini.

Huu si wakati mzuri wa kuwapatia akina Pompeo na Trump kisingizio cha kuliwekea Taifa letu punitive sanction kwa kisingizio cha kudai eti tanakihuka haki za binadamu, tusipo kuwa makini tukaanza kuingilia imani za raia kwa kuwawekea vikwazo baadhi ya viongozi wa dini kwa visingizio vya shahada ya theolojia - suala hilo akina Pompeo na Trump watalipokea kwa mikono miwili na kuiwekea Tanzania vikwazo vya kiuchumi - tusichezee shilling kwenye tundu la choo, USA ikisha anza kukufatilia kwa karibu unapashwa kuwa makini sana na statements ambazo viongozi wetu wana zitoa kwenye vyombo vya habari.
 
Back
Top Bottom