Utitiri wa vibanda imani kuifanya Serikali kubadili Sheria ya Jumuiya kwa taasisi za dini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema serikali itaangalia namna ya kubadilisha Sheria ya Jumuiya ili kuwe na utaratibu wa utoaji wa huduma za kiroho, hasa kutokana na kuwapo kwa utitiri wa vibanda imani.

Simbachawene aliyabainisha hayo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu ajali iliyotokea Moshi, ambako watu 20 wamepoteza maisha na wengine 16 kujeruhiwa. Kati ya hao watoto ni wanne na 16 ni watu wazima.

Alisema pamoja na kongamano hilo kuwa na kibali cha siku tatu, kuanzia Januari 30 hadi Februari Mosi mwaka huu, kilichoombwa na Mchungaji wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Elia Mwambapa, lakini wanaonesha walikiuka masharti ya kibali ambacho ni kongamano kuendelea baada ya saa 12 jioni.

Simbachawene ambaye alitoa pole kutokana na tukio hilo, alisema ili kuepukana na madhara makubwa zaidi siku zijazo, wizara yake itaangalia namna ya kuifanyika marekebisho ya Sheria ya Jumuiya ambayo ndiyo inayotumika kusajili taasisi za dini.

“Serikali inaheshimu haki ya kuabudu na ni haki ya kikatiba, lakini lazima tuangalie pengine hata sheria na kanuni zetu haziko sawa sawa, kwa sababu wengine wanakuja na sabuni ukiogea matatizo yameisha na utakuwa na tajiri.

Mwingine atakuja na maji, mafuta au maziwa, na wakati mwingine ukisikiliza mahubiri unaweza kujiuliza kuna Mungu kweli hapa,” alisema Simbachawene aliyeshika wadhifa huo hivi karibuni.

Aliongeza, “tunaona ni vizuri watu tukaweka utaratibu wa utoaji wa huduma za kiroho, vibanda imani vimekuwa vingi lazima kuweka utaratibu.

Mfano Rwanda ukitaka kuanzisha huduma lazima uwe na shahada ya kwanza ya Theolojia, sisi hajutaweka hilo sharti, ila tutaanza kufikiria huko.”
 
Maisha yamezifi kuwa magumu serikali iliangalie hili
Watu kinachowasumbua ni njaa inayozidi kuitafuna jamii,biashara,kilimo vyote vimedorora wakati kodi zimekua kubwa....shida wa tz hatupendagi kuongea ukweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa vibanda imani maana yake nini kiserikali?na yule wa kule kilimanjaro nae kasema makanisa makubwa laiti wengetimiza wajibu wao haya yasingetokea, sasa ni yepi hayo? IMANI IMANI jamani!!!
 
Msibadili sheria kwa sababu ya tukio...bali kwa sababu kuna haja ya kufanya hivyo.
Ushauri: usitunge sheria ukiwa na hasira au furaha...subiri busara itawale ndiyo utunge sheria.
 
Kwa mtazamo wangu nadhani huyu waziri anakosea sana kusema VIBANDA IMANI...to me thats an insult,kiheshima zinaitwa nyumba za ibada,au nyumba za imani,aliongea poa sana ila pumba aliyoisema ni hiyo VIBANDA IMANI.

kuhusu watu waliokufa pale lile ni kosa la kibinadamu la mwamposa kukosa kuweka utaratibu mzuri,hilo halihusiani na imani,hata serikali kuna wakati inashindwa kuweka utaratibu mzuri na watu wanakufa.

Point to note lililotokea ni janga ila wanasiasa wasianze kutaka kupata umaarufu kupitia hili.
 
ANKO JEI,
Nafikiri serikali haiwezi kukwepa lawama. Wanahitajika kutoa ruhusa baada ya kuombwa kufanyika mkutano wowote kwa sababu wanapaswa kuweka ulinzi na mazingira ya usalama. Je, kwa nini hawakufanya hivyo.

Tumeshuhudia mara kadhaa mikutano ya kisiasa ikizuiwa kwa sababu ya kutokuwa na 'uwezo wa kuhakikisha usalama'. Kwa kutoa ruhusa waliwahakikishia waombaji na waudhuliaji uwezo huo. Tutashangaa kama wahusika wataachwa na kuwaandama hao manabii na mitume.
 
Binafsi kw alichokua anaongea mkuu wa kilimanjaro pale sio sawa ata kidogo ajatumia hekima wala busara na yeye alikurupuka tu kufata mkumbo kwa yale watu walikua wanasema
 
mi napata kujiuliza askari police walikuwa wap mpaka mtu akazidisha muda na wao wapo pia wao walikosea kazi yao
 
Back
Top Bottom