Simba yaizuia Yanga kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,193
8,009
Baada ya CAF kutoa maelekezo kuhusiana na mashindano ya Super Cup, uwanja wa Benjamin Mkapa umefungwa isipokuwa kwa mashindano ya kimataifa pekee.

Kwa hiyo mashindano mengine yoyote ikiwemo yale ya Ligi ya NBC yataendelea katika viwanja vingine, kwa hiyo Yanga na Simba watalazimika kutumia viwanja vingine kama vile Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya mashindano hayo.

Ikumbukwe ni Simba pekee kutoka Tanzania ndiye anategemewa kushiriki katika mashindano hayo ya Super Cup. Kwa tafsiri nyingine ni kuwa ushiriki wa Simba katika Super Cup umeharibu uenyeji wa Yanga katika mashindano ya ndani na hawana la kufanya masikini.
 
Kwaajili ya soko la ajira na kufungua milango zaidi, sio mbaya!

Sidhani kama Simba ataendelea kuwa huko peke yake kutoka TZ/EA. Na kwa jinsi wanavyosua sua, pengine watani wao wakaingia.

Lakini, kujiita klabu kongwe, kununua wachezaji kwa mamilioni ya fedha, kisha msingi wa mchezo wenyewe ukiwa ni kiwanja cha kuchezea na cha mazoezi hawana, hii si ni sawa na wanasiasa kuhesabu miaka ya uhuru kwa furaha huku mafanikio makubwa yakiwa ni KUKOPA tu?

Jangwani pale, kama si CCM, ingekuaje?
Kariakoo, si ni kwa nguvu za wafanyabiashara wa kiarabu pengine?

Kimsingi, Simba anatumia kilicho cha wadanganyika wote, Yanga nao zamu ikifika, wanatumia hapo hapo.
 
Simba bado hajaridhika na aibu anayoileta kwa nchi kwenye club bingwa bado anataka kuitangaza nchi vibaya kupitia super cup!
Simba sio kwamba inataka yenyewe, bali inatakiwa na CAF. Kuna watu walienda kujialika kwenye mkutano wa CAF kule Arusha kwenda kumuona Rais wa CAF, lakini amewapotezea. Ni suala la kitaalamu, sio lobbying
 
IMG_0909.jpg
 
Back
Top Bottom