Simba Sc, Lawama hazitawasaidia, Mamilioni ya fedha anazotoa Azam kila mwezi kwa kila timu zimefanya ligi iwe na ushindani kuliko miaka iliyopita

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Kila timu inapokea si chini ya Milioni 40 kila mwezi kwajili ya kujiendesha, Hivi kwa akili ya kawaida tu unategemea ubora wa hizi timu uwe vilevile kama miaka ya nyuma??

🚨 Simba SC lawama haziwasaidii, wekezeni uwanjani zaidi kuliko nje ya uwanja !!

- Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Simba sc msimu huu wamewekeza zaidi katika LAWAMA bila kuzingatia uhalisia.

📌 Uhalisia uliopo msimu huu unawekwa vivuli na ku-deal na mambo ya nje ya uwanja.... Guys,, sio ndoto, wake up ! ilitegemewa lazima msimu huu utakuwa mgumu hasa kwa kuzingatia mambo yafuatayo ;

✅ Uwekezaji kwenye ligi ; Timu nyingi zimeimarika kutokana na pesa za wadhamini, Wachezaji wa timu nyingi wana concentrate na soka zaidi kwenye field na sio kuwaza watakula nini.

✅ Usafiri umeboreshwa, timu zinasafiri kwa wakati, hakuna timu inakwama kwa sababu ya nauli. Hili la kupunguza timu pia limesababisha kubaki na cream ya timu zenye ushindani.

✅ Timu zimepata pesa za kufanya usajili, sio ajabu tena kuona timu kama Geita gold inasajili Mchezaji wa ligi kuu kutoka Congo.

📌 Hizo ni baadhi ya sababu zinazofanya mechi ziwe ngumu na wala sio (TFF) wala (GSM) kama baadhi ya mashabiki wengi na viongozi wa Simba wanavyoaminishwa.

📌 Ubora wa Simba sc haujashuka sana umepungua kidogo hasa kwa washambuliaji, Isipokuwa wapinzani wao Yanga SC ubora wao umeongezeka.... Na hili utaliona kwenye namba.

- Msimu uliopita muda kama huu Simba sc walikuwa wameshafunga magoli zaidi ya (24+) lakini sasa hivi wana magoli (14) tu.

- Vice versa is true,, Yanga wao walikuwa wamefunga magoli (14) tu lakini msimu huu mpaka sasa wanamagoli (23).... Hapo (GSM) unamlaumu kwa lipi ?

- Msimu uliopita muda kama huu Yanga walikuwa wameshapoteza Points (15) lakini sasa hivi wamepoteza Points (4) tu.

Young Africans msimu huu
✅ 11 🤝 02 ❎ 00 = Walizopoteza (4)

Young Africans msimu uliopita
✅ 06 🤝 06 ❎ 01= Walizopoteza (15)

- Haikuwahi kutokea katika misimu (4) iliyopita, katika michezo (12) ligi kuu Simba sc wawe na michezo (5) ambayo hawakufunga goli lolote,, Lakini msimu huu imetokea, hapo utailaumu (TFF) ?

❎ Simba sc 0 - 0 Coastal union.
❎ Biashara Utd 0 - 0 Simba sc.
❎ Mbeya city 1 - 0 Simba sc.
❎ Mtibwasugar 0 - 0 Simba sc
❎ Simba sc 0 - 0 Yanga sc.

- Wakati huo wenzao Yanga katika michezo (13) wakiwa hawajafunga goli kwenye mchezo mmoja pekee v Simba sc !!!

- Kitu kibaya zaidi wanaSimba hawataki kukubali UKWELI, wanaishi kwa historia na hiki kitu ndicho kinaweza kuwachelewesha na kukumbuka shuka kukiwa kumekucha.

- Msimu huu ni tofauti, hapa niwasifu viongozi wa (TFF) na bodi ya ligi kwa kuweza kupanga ratiba vizuri....

- Misimu iliyopita mpaka sasa kungekuwa na viporo zaidi ya (4) lakini mpaka sasa timu (14) zimecheza michezo (13) isipokuwa Simba sc na Kagera sugar ambao wamecheza michezo (12) na wote tunajua nini kilitokea.

SOLUTION
---------------------------
- Kwa sasa Simba wanapaswa ku deal na tatizo na sio kutafuta mchawi,, Ukiniambia viwanja ni vibovu sitakuafiki.... Viwanja hivi ndivyo vilivyotumika katika misimu (4) ambayo Simba sc walikuwa mabingwa.

- Simba sc 0 - 0 Coastal ; Kwa Mkapa pia ni pabovu ? .... Muda bado upo, mbio za ubingwa bado mbichi wekezeni katika kuwanoa washambuliaji na sio KULAUMU.

- Simba SC wamepata penati (7) msimu huu mpaka sasa,, katika penati hizo wamekosa penati (5),, Hapo utamlaumu (GSM) ?! Hebu tuweni serious kidogo.

🔍 Tom cruz.
 
Ngoja waje Team Babra toka mahabusu waje wakutukane maana hawataki kuambiwa ukweli
 
Kwani mambo ya soka na polisi wapi na wapi? Kwani ile faini ilikuwa ya nn?
We mbumbumbu kumbe ni mtupu kabisa kichwani, jinai haiangalii we ni mchezaji au kiongozi wa mpira, muulize mwenyekiti wenu Evance Aveva nini kilimkuta, Ulizia utaambiwa Jamal Malinzi ni nani nae yuko wapi, hivi unajua kina Michael platin na Seif Blater ni kina nani na nini kiliwakuta?
 
Kwani mambo ya soka na polisi wapi na wapi? Kwani ile faini ilikuwa ya nn?
Wacha nikueleweshe ndugu, mfano tuko Taifa Kama washabiki ukanipiga adharani, tff watachukua hatua kukufungia kwa mujibu wa kanuni, pia jamhuri itakushikilia kwa jinai uliotenda au Mimi nitakushitaki km jamhuri haitakuchukulia hatua. Nadhani umeelewa.
 
Back
Top Bottom