Kwani Simba SC walikuwa wanacheza dhidi ya Pacome?

mwehu ndama

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
543
1,837
Kuna siku niliwahi kuwaita Simba SC club na mashabiki wake kwa pamoja na wachambuzi wao wa bahasha kama kituko cha taifa. Na hili limejidhihirisha jana, katika hali ya kushangaza baada ya Mbumbumbu FC kuifunga timu goigoi ya Jwaneng Galaxy iliyojaa wachezaji viwete, nilitegemea wangejikita katika kuzungumzia uzuri na mapangufu ya timu yao huku wakifurahia ushindi wao kwa kuupongeza uongozi wao na benchi la ufundi.

Cha ajabu makundi yote ya Mbumbumbu FC yaliibuka na kuanza kusema chama ni zaidi ya Pacome, mara hakuna mchezaji wa Yanga SC anaweza kuingia kikosi cha Simba SC mara Pacome anamengi ya kujifunza toka kwa mlevi wa ndola.

Hivyo tuhitimishe kwamba tumekubalian Simba SC Club kwa sasa mpinzani wao ni Pacome na sio Yanga SC wala timu zingine zinazoshiriki ligi kuu. Chama alitikanwa na mashabiki wao wenyewe nakusema; "Awaachie timu yao, leo hii haohao wanaibuka na kuanza kusema" tuliwaambia nyie yanga huyu chama ni moto kuliko Huyo pacome wenu," hili linafikirisha sana.

Pacome anatimiza wajibu wake kama mchezaji wa Yanga sc na wala haitaji sifa zozote, yuko pale kufurahia kipaji chake, na uzuri wa Yanga SC haina mchezaji tegemezi, Yanga SC ni jeshi.
 
Back
Top Bottom