Mtani naona tayari na wewe umeingia kwenye mtego wa Rage na washirika wake Azam......Rage akishaona hela tu anasahau kila kitu.....
Mkataba wa Bodi ya Ligi kuu na Azam Media unazua maswali mengi kuliko majibu, mkataba hauna uwazi na haueleweki,.....Mkataba huu ni ule muendelezo wa ubabe wa TFF dhidi ya vilabu vya mpira wa miguu vya Tanzania...
Kwa wanaoijua TFF hawatayashangaa madudu haya ya Bodi ya Ligi kuu ya Bara...Huu ni muendelezo wa ubabe wa TFF wa kuziburuza timu na kutoweka wazi mikataba/kutosjirikisha klabu katika mikataba...Mfano ni ule mkataba baina ya TFF na VodaCom kudhamini Ligi kuu ya Bara....
Pamoja na kwamba Azam Media wana malengo mazuri kwa soka la Tanzania bado kuna mambo yamejificha ambayo yanatia mashaka katika kataba huu ambao umesainiwa harakahara na Wallace Karia na wenzake.....Hakukuwa na uwazi katika kufikia makubaliano hayo....Binafsi ningeomba mkuu wangu
Masuke unisaidie katika haya:
Bodi ya Ligi Kuu inakaribia kumaliza muda wake na ni ya muda, Jeni ni nani amewapa akika Karia mamlaka ya kuingia mkataba wa miaka mitatu na Azam Media?....
Kuna zabuni ilitangazwa kabla ya Azam Media kupewa haki hiyo ya kurusha matangazo ya mechi za EPL?,Je zabuni hiyo ilitangazwa lini na kwenye chombo kipi na mchakato wa kumpata mshindi ulifanyika lini?
Timu zinazoshiriki Ligi Kuu zilihusishwa katika mchakato huu?...
Ukiacha suala la Dau kubwa, kigezo cha uzoefu na uwepo wa chombo kinachoitwa Azam Media vilizingatiwa?, maana ni ajabu na ni kitu cha kushangaza kuona Azam Media wanapewa kazi kubwa kama hiyo ilhali hawajawahi kurusha matangazo hata siku moja na hata ufanisi wao haujulikani......Ni ile hadithi ya kuuziwa mbuzi kwenye gunia?....
Kigezo kwamba hakuna TV nyingine inayoweza kutoa fedha nyingi zaidi ya Azam TV kingejulikana kupitia ushindani wa zabuni na si kwa kudhania kama walivyofanya Bodi ya Ligi kuu, Azam TV walitakiwa washindanishwe na TV nyingine ili mshindi apatikane na kwa kupitia ushindani wa Zabuni ndio ingejulikana kama hakuna TV nyingine inaweza kulipa fedha nyingi kama Azam ama la, lakini si kwa hii dhana ya kudhania......Hizi ni zama za uwazi na si zama za kuendeshana za enzi za FAT ya akina Ndolanga na Rage wake.....
Suala la Star TV kuwalipa Azam waoneshe mechi zao ni lingine....Halihusiani kabisa na hili la sasa.....
Mkataba wa Azam Media na Bodi ya Ligi kuu unaacha maswali mengi sana kuliko majibu na Bodi ya Ligi kuu na Azam Media wanajua fika kwamba timu ndogo/myingine ukiacha Simba, Yanga, Azam na nyingine zenye wadhamini hazitapinga mpango wa kupewa milioni 100 kwa mwaka (hata kama wananyonywa) kiwango ambacho hawakukitegemea kukipata katika maisha yao.....Cha msingi ni kuwepo na uwazi katika mkataba na taratibu za zabuni zifuatwe.....