Madai ya Amrouche kuhusu Morocco ni siasa ya ukocha. Imenikumbusha fainali ya ASFC Lake Tanganyika Kigoma Yanga na Simba 2021

Mbochong'a

JF-Expert Member
May 2, 2011
761
1,294
Wakuu kwema? Heri ya mwaka mpya. Hope mko poa na mapambano yanaendelea. Mungu ni mwema.

Moja kwa moja kwenye mada. Hivi karibuni nilisoma taarifa mitandaoni inayosema kocha wa Taifa Stars Adel Amrouche amelalamika kuwa Morocco imekuwa ikiingilia maamuzi ya CAF na yenyewe kujipangia marefa wanaowataka wao.

Haya malalamiko ukiyachambua kwa pande zaidi ya moja utapata tafsiri nyingi sana. Lakini kwa mimi binafsi naona hapa ni kama amecheza na siasa ya maneno kwenye mpira. Hii ni nzuri kwa sababu kama hiyo tabia ipo basi kwa sasa itakuwa imeshagundulika na watahakikisha haitatokea.

Hii imenikumbusha mwaka 2021 kabla ya mechi ya fainali kati ya Yanga na Simba kwenye michuano ya kombe la Shirikisho la Azam msimu wa 2020/2021. Siku chache kabla ya mechi, baadhi ya wanachama na mashabiki wa Yanga walilalamika kuhusu mwamuzi aliyepangwa kuchezesha mechi hiyo ambaye ni Ahmed Arajiga. Walilalamika kuwa huwa anachezesha sana mechi za Simba na anawapendelea kutokana na kupata matokeo ya papatu papatu kwa kupendelewa na refa huyo.

Kilichotokea siku ya jumapili ya tarehe 25 mwezi julai pale Lake Tanganyika Kigoma kwa Arajiga ilikuwa ni amazing! Alichezesha mechi kwa umakini wa hali ya juu sana. Hakumpendelea Simba wala Yanga. Mechi iliisha vizuri sana kimaamuzi na Simba alipata ushindi wa goli moja kwa bila lililofungwa na Thadeo Lwanga akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona. Kwa hiyo hapo Arajiga alihakikisha hafanyi makosa na kupelekea maneno yaliyosemwa kuonekana ni ya kweli.

Ninachotaka kusema ni kwamba malalamiko ya Adel Amrouche yana faida sana. Hata mwamuzi wa leo atakuwa makini sana ili kusiwe na hisia hasi za kimaamuzi. Siasa ipo hata kwenye mpira. Kila la heri Tanzania.
 
Back
Top Bottom