mahakama ya kazi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2013
- 1,520
- 245
Acha kuendekeza njaa wewe tumia akili yako vizuri, nakupa mfano mdogo tu hapo chini:
Wadanganyika bana! lini tutajikomboa? yaani unashabikia wizi wa mchana kweupe jua kali kabisa.
Ndugu yangu nakupa mfano rahisi tu ambao Azam Media watawanyonya watanzania na vilabu husika.
Kitu kikubwa ambacho Azam Media wanataka kufanya ni kuuza king'amuzi kupitia hiyo channel ya mpira.
kwa hesabu ya haraka tu ni kuwa:
1. Kama watauza ving'amuzi 400,000 na kuweza kupata TZS 10,000 kila kimoja kama faida.
2. Watapata jumla ya TZS. 4,000,000,000.
3. Azam wanatoa TZS. 100,000,000 kwa kila Timu ambazo ziko 14 kwenye Ligi.
4. Jumla ya TZS. 1,400,000,000 Zitatumika kwenye Timu.
5. Ina maana Azam Media watapata Faida ya TZS. 2,600,000,000.
Sasa wewe Mdanganyika angalia hapo tu kwenye King'amuzi tu pekee yake jinsi tutakavyopigwa mashabiki wa soka.
Na hapo bado Monthly fee ya King'amuzi.
Nionavyo mimi Yanga madai yao ni ya Msingi na Azam wa lengo zuri lakini linatakiwa liwe wazi, mambo ya kutoa hela kijumla jumla yalishapitwa na wakati, Azam media na Timu zote zikae chini waweke makubaliano ya % kwenye mapato ya Urushaji wa mechi hizo badala ya kuja na Sh. 100,000,000 eti unawalingishia timu masikini kuwa ni hela kubwa.
Naipongeza Yanga kwa kulijua hilo, hayo ndo mawazo yangu. Amkeni tumeenda shule za nini?
hiyo faida imepatikana?