TANZIA Silvio Berlusconi afariki dunia, aliongoza Serikali tatu za Italia na kumiliki timu ya AC Milan

Victoire

JF-Expert Member
Jul 4, 2008
24,143
56,606
Silvio aliwahi kumiliki team ya AC Milan. Kwa kipindi chake AC Milan ilikuwa ya moto.

======

Aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Italia, Silvio Berlusconi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86. Nguli huyo kwenye tasnia ya habari ameongoza Serikali tatu za Italia kutoka mwaka 1994 mpaka 2011 ambapo chama chake cha Forza kipo kwenye muungano unaoongoza nchi kwa sasa.

Berlusconi aliweza kurejesha jina lake kwenye siasa pamoja na kukumbwa na kashfa za ngono, rushwa pamoja na ukwepaji kodi.

Silvio amefariki katika hospitali ya Raffaele mjini Milan ambapo amekaa wiki sita akitibiwa maambukizi kwenye mapafu ambapo kabla hajapokelewa alikuwa pia na ugonjwa wa kansa ya damu.

Amezaliwa jijini Milan mwaka 1936 kwenye familia ya kipato cha kati na alijikita kwenye uwekezaji wa majengo wakati akianza biashara kabla ya kwenda kuanzisha kampuni ya Mediaset, chombo binafsi kikubwa zaidi cha habari nchini Italia, pia akamiliki timu ya AC Milan kuanzia mwaka 1986 mpaka 2017.

Chama cha Forza Italia kilianzishwa mwaka 1993 na mwaka mmoja baadae Berlusconi akawa waziri mkuu wa kwanza kupitia chama hicho bila kuwa na rekodi yoyote ya kuendesha ofisi ya Serikali. Silvio alilazimika kujiuzulu mwaka 2011 kutokana na mgogoro wa madeni

20230612_105830.jpg
 
R.I.P Berlusconi..
Alikuwa anapenda sana under 18
Ila jamaa alipenda sana mabinti.Sema pamoja na scandal za rushwa na ufisadi ,jamaa alirudi tena kwenye siasa 2017,na mwaka jana chama chake kilipata wabunge na yeye kushinda usenetor. Huku chama chake kikiongeza nguvu kwa mlengo wa kulia .Katika kushirikiana na chama cha waziri mkuu aliyepo sasa madame Giorgia Melon.
 
Kila wiki alikuwa anafanyiwa plastic/ cosmetic surgery. Alikuwa anapigwa botox na fillers za kutosha. Halafu lilikuwa pedophile na baguzi lilokubuhu. Alijitamva hawez tembea na madem weus.

Akwende zake huko.
Kafa sababu alikuwa na Leukemia. Kafa akiwa na miaka 86.Ni mingi sana.Jamaa aliienjoy maisha bwana.Kwani ukiwa hauna hela utafanya plastic surgery ?Alikuwa anapenda mademu wazuri.Kila mtu na taste yake.Ila alipenda mademu waarabu mabinti under 18 wa Morocco
 
Dah! Mwamba ameondoka huku akiwa hamfai chichote kile Muumba wake. Hadi raha.

Hii dunia ukiwa huna hela, kila usiku utajikuta ni mtu wa kulalamika, kutukana hovyo, kulaumu na pia kukata tamaa. Ila kwa jamaa money was not a problem at all.

Aisee tunatakiwa tupambane ili na sisi tufaidi mema yote ya hapa duniani.
Bongo pagumu sana kutoka siyo rahis kihivyo, hata ukitoa kafara unaishia kukamata million 50 tu madaf halafu mashart kibao, kutatuliwa rinda na sangoma, kunya njia panda kila siku, kulala chooni (choo cha shimo)
 
Kafa sababu alikuwa na Leukemia. Kafa akiwa na miaka 86.Ni mingi sana.Jamaa aliienjoy maisha bwana.Kwani ukiwa hauna hela utafanya plastic surgery ?Alikuwa anapenda mademu wazuri.Kila mtu na taste yake.Ila alipenda mademu waarabu mabinti under 18 wa Morocco
Huyu namfananisha na Amatus Liyumba. Every eligible P bongo jamaa alimega. Lakini ngwegwe mkono wa nyani ukamuondoa.

King Kong III

Silvio aliwahi kumiliki team ya AC Milan. Kwa kipindi chake AC Milan ilikuwa ya moto.

======

Aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Italia, Silvio Berlusconi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86. Nguli huyo kwenye tasnia ya habari ameongoza Serikali tatu za Italia kutoka mwaka 1994 mpaka 2011 ambapo chama chake cha Forza kipo kwenye muungano unaoongoza nchi kwa sasa.

Berlusconi aliweza kurejesha jina lake kwenye siasa pamoja na kukumbwa na kashfa za ngono, rushwa pamoja na ukwepaji kodi.

Silvio amefariki katika hospitali ya Raffaele mjini Milan ambapo amekaa wiki sita akitibiwa maambukizi kwenye mapafu ambapo kabla hajapokelewa alikuwa pia na ugonjwa wa kansa ya damu.

View attachment 2654860
R.I.P the Don, Jamaa alikua na hulka mithili ya Donald Trump. Mwenyezi Mungu amweke anapostahili Amen.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom