Muuza Kangala
JF-Expert Member
- Jul 21, 2021
- 1,126
- 4,169
Chifu Mangosuthu Buthelezi, Muanzilishi na kiongozi wa muda mrefu wa chama cha Inkatha Freedom Party(IFP) amefariki dunia Jumamosi ya leo, Septemba 09, 2023.
Buthelezi alianzisha IFP na baadae kuwa mpinzani mkuu wa chama cha ANC eneo la Kwazulu-Natal na Gauteng. IFP ilishiriki uchaguzi wa kwanza kidemokrasia nchini Afrika Kusini na kuwa sehemu ya Serikali ya kwanza ya kidemokrasia nchini humo.
Historia ya Buthelezi imejaa mkanganyiko baadhi wakimtaja kama mtu aliyesaidia kuiunganisha Afrika ya Kusini huku wengine wakimuona na mikono iliyojaa damu ya maelfu ya waafrika kusini waliouawa mwishoni mwa miaka ya 80 na mwanzo mwa 90.
Buthelezi amekaa kwenye siasa za Afrika kusini kwa miongo mitano akiiona nchi hiyo ikitoka kwenye ubaguzi wa rangi kuelekea nchi ya kidemokrasia.
Buthelezi anasemwa alimiani katika njia za amani ili kupambana na ubaguzi wa rangi kitu ambacho kilimpa majina mengi ikiwemo mpinga mapinduzi na msaliti.