TANZIA Silvio Berluscon Waziri Mkuu wa zamani wa Italia afariki Dunia

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,744
218,335
Taarifa kutoka kwenye vyombo vya Habari vya kimataifa zinaeleza kwamba Waziri Mkuu wa Zamani wa Italia na Mmiliki wa Timu ya soka ya AC MILAN Silvio Berluscon amefariki Dunia Jijini Milan

Chanzo cha kifo chake kimetajwa kuwa ni Ugonjwa wa kansa ya damu uliomsumbua kwa muda mrefu .

Apumzike kwa Amani
---

1686588695945.png

Waziri mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86. Kifo cha Berlusconi kimetangazwa na msemaji wake hii leo.

Kiongozi huyo tajiri na maarufu alilazwa katika hospitali ya Milan siku ya Ijumaa ili kufanyiwa vipimo zaidi kuhusiana na ugonjwa uliyokuwa ukimsumbua wa saratani ya damu.

Berlusconi alikabiliwa na matatizo ya afya kwa miaka kadhaa
Berlusconi aliyekuwa na ushawishi mkubwa, alikabiliwa na matatizo ya kiafya kwa miaka kadhaa, huku akifanyiwa upasuaji wa moyo mnamo mwaka 2016 na kulazwa hospitalini mwaka 2020 baada ya kupata maambukizi ya UVIKO19. Licha ya kuchaguliwa tena kuwa Seneta mwaka jana, alionekana kwa nadra hadharani.

Berlusconi aliiongoza Italia kwa miaka tisa
Berlusconi aliyesalia kuwa kiongozi wa chama chake cha mrengo wa kulia cha Forza Italia, aliongoza nchi hiyo mara tatu na kwa jumla ya miaka tisa kati ya mwaka 1994 na 2011. Aliwashawishi wapiga kura kwa ahadi ya mafanikio ya kiuchumi kabla ya kufurushwa wakati mzozo wa madeni uliikumba nchi yake.
 
Taarifa kutoka kwenye vyombo vya Habari vya kimataifa zinaeleza kwamba Waziri Mkuu wa Zamani wa Italia na Mmiliki wa Timu ya soka ya AC MILAN Silvio Berluscon amefariki Dunia Jijini Milan

Chanzo cha kifo chake kimetajwa kuwa ni Ugonjwa wa kansa ya damu uliomsumbua kwa muda mrefu .

Apumzike kwa Amani
Gwiji wa burudani na siasa za Italy, apumzike kwa amani..
 
Taarifa kutoka kwenye vyombo vya Habari vya kimataifa zinaeleza kwamba Waziri Mkuu wa Zamani wa Italia na Mmiliki wa Timu ya soka ya AC MILAN Silvio Berluscon amefariki Dunia Jijini Milan

Chanzo cha kifo chake kimetajwa kuwa ni Ugonjwa wa kansa ya damu uliomsumbua kwa muda mrefu .

Apumzike kwa Amani
INNALLILAH WAINALLILAH Rajiuun.
Nazani huyu ni kati ya wamiliki wa kwanza kabisa kuwasikia wakimiliki timu
 
Taarifa kutoka kwenye vyombo vya Habari vya kimataifa zinaeleza kwamba Waziri Mkuu wa Zamani wa Italia na Mmiliki wa Timu ya soka ya AC MILAN Silvio Berluscon amefariki Dunia Jijini Milan

Chanzo cha kifo chake kimetajwa kuwa ni Ugonjwa wa kansa ya damu uliomsumbua kwa muda mrefu .

Apumzike kwa Amani
The Mafia himself
 
Huyu baba alimpiga mululu polisi alipokuwa akimfungulia mlango ili aingie kwenye gari
 
Cancer inamaliza sana watu tofauti na ilivyokuwa zamani, kuna mahali tunakosea.

Mwezi uliopita nimezika Shangazi yangu kwa ugonjwa wa cancer ya matiti.
 
Back
Top Bottom