Sikuwa mjinga, niliamini niko sahihi, leo Ndugai amejibu


Details za mkataba ziwekwe hadharani ili tuuchambue kwa kina. Jiwe akiwa Mbunge na Waziri wa Ujenzi halikutia neno bungeni kuhusu mkataba huo.
Huo mradi wa Bagamoyo as long as yupo Mchina, sisi wabongo tunapaswa kuutazama mkataba kwa upya neno nadi neno...wale wapumbavu macho madogo wana hila kuliko mwanadamu yoyote juu ya uso wa nchi...
 
Ulinikera tu pale ulipotuaminisha kuwa ni Jasusi na una Maisha mazuri ( huna njaa kama Sisi ) na una Network Kubwa ila ukakosa Tsh 5,000,000/ za Faini pale Mahakamani Kisutu hadi Bakuli lilipopitishwa ndiyo ikapatikana na ukasalimika kwenda kuyaanza Maisha yako mapya Segerea.

Katika Uzi wako huu nimegundua mengi hasa juu yako na kwa Serikali na nchi yetu kwa Ujumla. Nianze kwa Kukupongeza kwa Uwasilishaji wako mzuri na makini hapa.

Unaonekana una Thinking Capacity kubwa mno na Laiti Wapuuzi fulani fulani wangechukua muda Kusoma yale uliyokuwa ukiwaandikia huko nyuma huenda leo Tanzania tungefaidika na mengi ya Kimaendeleo kupitia hizi Critical Analysis zako Ndugu.

Hiki ulichokiandika hapa kama kingekuwa ni Majibu ya Swali la Mtihani kuhusu Changamoto za Kiutawala na Uchumi kwa nchi ya Tanzania ningekupa Alama 85% ambayo Kitaaluma ni A ya Ufaulu wa juu kabisa.

Japo kuna maeneo mengine uliyogusia yanahitaji Mjadala zaidi kwa Maslahi mapana na Ustawi na Usalama wetu kama Watanzania na Taifa letu kwa Ujumla ila Bandiko lako hili ( Uzi wako huu ) una Faida nyingi kuliko Hasara kama Wahusika wakiusoma na Kuujadili Kiumakini na haraka sana Kurekebisha na Kufanyia Kazi mapungufu yetu kama nchi nikiamini kuwa hata kama tumetanguliwa ila bado hatujachelewa na tusikate tamaa kwani Tanzania ya Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan ( ya sasa ) ni makini na sikivu pia tofauti na iliyokuwepo iliyojaa Uwongo, Majungu, Ubishi, Kiburi, Dharau na iliyobobea katika Ufisadi uliovunja rekodi katika Historia ya Tanzania.

Umeandika Kimtizamo nimependa sana. Na pia kupitia huu Uzi wako kuna sehemu fulani hivi umenifungua Macho Kifikra zaidi kwamba huenda haya Machafuko ya Waasi yaliyoko sasa nchini Msumbiji yanachochewa kwa Siri na Mataifa Jirani ( hasa ya SADC ) kwa Kuhofia endapo hiyo Bandari Kubwa inayojengwa huko itaitajirisha mno Msumbiji, Uchumi wake Kukua kwa haraka, Bandari za Mataifa mengine kukosa Soko hivyo wameungana Kimkakati Kuimaliza Msumbiji ili lengo lake hili lisifanikiwe kwa Kuiogopa.
Njama kuu zinatokea South Africa kwani Bandari ya Darban ndiyo Bandari kuu kwa upande huu na ndiyo tegemezi kwa zimbabwe Botswana Zambia na hata msumbiji yenyewe hivyo uwepo wa Bandari kubwa mpya ni pigo kwa Bandari za Angora, Tanzania, kenya congo Brazzaville nk
 
Mnajikuta mnaujua mkataba kuliko Mzalendo namba moja, JPM. Wote mnaoshabikia kuliuza taifa letu pendwa hakika laana hii itakuwa juu yenu na vizazi vyenu.
Marehemu alitikisa kiberiti avute mpunga tokea kwa Wachina lakini kwa kuwa ile kampuni ni ya Serikali wakagoma kwa kudai kuwa tayari walitumia pesa nyingi kulipa wakazi wa Bagamoyo fidia na kufanya upembuzi yakinifu kwa gharama kubwa ndipo marehemu akaamua kuwasingizia kuwa watakusanya mapato wenyewe pasipo gawio na mengineyo kwa lengo la kuwakomoa, Cha muhimu ni Mkataba kuanikwa wazi hata kwenye mitandao au hata magazeti ili watanzania wote wauchambue vizuri wapate kubaini mapungufu yote kisha waje na jawabu sahihi la kufanikisha ujenzi wa Bandari pasipo Athari kwa pande zote mbili
 
Bandari za Dsm Tanga mtwara haziwezi kufa kwani ni mapito ya meli nyingi zikiwa njia kuelekea sehemu nyingi Duniani na pia zinaweza kutumika kama Bandari ya Capetown, Pot Elizabeth, East London za kule South Africa zinavyotumika kuleta bidhaa za ndani ya Nchi na pia kupokea meli za kitalii, Bandari ya Bagamoyo itakuwa Bandari ya kimataifa tu ili kuileta Tanzania iwe Dubai ya Africa kwani Reli na uwanja mwingine wa Ndege za mizigo vitajengwa Bagamoyo na kuipelekea Bagamoyo kuwa jiji kubwa Barani Africa, mikataba irejewe upya itengenezwe mikataba isiyo na shaka kwa watanzania
 
Details za mkataba ziwekwe hadharani ili tuuchambue kwa kina. Jiwe akiwa Mbunge na Waziri wa Ujenzi halikutia neno bungeni kuhusu mkataba huo.
Mikataba ya awali Magufuli alikubali pasipo kuweka pingamizi alipoingia ikulu akawageuka Wachina akijua wataleta mpunga mwingi kumbe Wachina nao wana hesabu zao zingine kwenda Nchi zingine ambazo hakuna magumashi kama Tanzania
 
Bandari za Dsm Tanga mtwara haziwezi kufa kwani ni mapito ya meli nyingi zikiwa njia kuelekea sehemu nyingi Duniani na pia zinaweza kutumika kama Bandari ya Capetown, Pot Elizabeth, East London za kule South Africa zinavyotumika kuleta bidhaa za ndani ya Nchi na pia kupokea meli za kitalii, Bandari ya Bagamoyo itakuwa Bandari ya kimataifa tu ili kuileta Tanzania iwe Dubai ya Africa kwani Reli na uwanja mwingine wa Ndege za mizigo vitajengwa Bagamoyo na kuipelekea Bagamoyo kuwa jiji kubwa Barani Africa, mikataba irejewe upya itengenezwe mikataba isiyo na shaka kwa watanzania
Yale yale tulipinga Chato sasa ni Bagamoyo. Haya ni mapambano ya wakubwa wawili. Samia asiingizwe kwenye vita hii should remain neutral na atekeleze miradi ya urithi. Ushauri.
 
Kauli hii ya Ndugai ni tosha kumuundia tume ya kumchunguza; kubadirika kwa msimamo wake kunatia shaka sio bure!!! Kama alivyosema mwendazake ule mradi wa bandari ya Bagamoyo ni wa KIJINGA; hakuna mtu mwenye akili timamu na mzalendo ambale angekubaliana na yale masharti!!! Pengine uwe mgogo kama Ndugai.
Huo mkataba umeuona? Ndugai anadai Rais alikua misled? Rais anadai mkataba ni mbaya.

Suluhu draft ya mkataba upelekwe bungeni kuliko mnachukua speculation tu za wanasiasa.

Yani hujauona hata ila umeanza kuukosoa?
 
Huo mkataba umeuona? Ndugai anadai Rais alikua misled? Rais anadai mkataba ni mbaya.

Suluhu draft ya mkataba upelekwe bungeni kuliko mnachukua speculation tu za wanasiasa.

Yani hujauona hata ila umeanza kuukosoa?
Rais alituambia kwanini mkataba haukuwa to our national interests; sababu alizozitoa ni genuine unless uwe umenunuliwa na wachina!!!

Ndugai hajasema kwanini anadhani Rais was misled [ maneno ambayo aliogopa kusema mwendazake alipo kuwa hai] kitu kinachoonesha jinsi alivyokuwa mnafiki!!
 
Rais alituambia kwanini mkataba haukuwa to our national interests; sababu alizozitoa ni genuine unless uwe umenunuliwa na wachina!!!

Ndugai hajasema kwanini anadhani Rais was misled [ maneno ambayo aliogopa kusema mwendazake alipo kuwa hai] kitu kinachoonesha jinsi alivyokuwa mnafiki!!
Kwanini unaamini Rais yupo sahihi na Ndugai ni muongo? Ilihali mkataba hujawahi kuuona?

Si JPM hyu hyu alidanganya kuwa ATCL inatoa gawio/Dividend kumbe hta hawaja break even wala kucover operating expenses toka 2016!!

Nadhani ingefaa tupige kelele mikataba iwe reviewed na kamati za bunge kuliko kurely kwenye maneno ya populists!!
 
SIKUWA MJINGA, NILIAMINI NIKO SAHIHI, LEO NDUGAI AMEJIBU.

Na Yericko Nyerere

Job Ndugai mfuasi kindakindaki wa hayati John Magufuli aliyeapa kumuongeza muda wa kutawala Tanzania, ananirejesha nyuma miaka miwili iliyopita 22 December 2019 nilipoandika Makala nikipinga hotuba ya Rais Magufuli akikataa kuendelea na ujenzi wa Mradi ya Bandari ya Bagamoyo, nilipinga hoja alizozijenga Rais ili kuualalisha katazo lake juu ya mradi husika.

Nilieleza wazi kwamba, Kuna mambo katika nchi yanahitaji uchunguzi kubaini pengine kuna hujuma katika taifa, hii inatokana na michakato mingi muhimu ya kichumi na kijamii imekuwa ikiishia njiani na kuliacha taifa katika hasara kubwa. Hii ni hujuma inahitaji mwarobaini kulitibu.

Mifano ya michakato ambayo kwamiaka mingi imeikuwa ikiishia njiani ni kama vile sekta ya nishati ambapo uzalishaji wa umeme limekuwa jambo linalotumiwa kama mchakato wakuzuka na kufa kwa miaka mingi sana tangu mwaka 1994 ilipokuja kitu kinaitwa umeme wa dharula kuokoa taifa (IPTL), ikafata michakato mingi yenye kuumiza taifa na haikufanikiwa hadi tukafika kuchimba Gesi mtwara tukapoteza mabilioni, gesi hadi Kinyerezi, kufumba na kufumbua mradi umetelekezwa sasa tunaimba mradi wa Bonde la Rufiji. Twende tuendelee..

Serikali ya awamu ya nne ilianzisha mradi wa kimkakati kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara duniani, mradi huu ilikuwa ni kujenga bandari ya Bagamoyo kwa ubia kati ya China na Omani wenye thamani ya dola bilioni 10, Serikali ya Tanzania katika mradi huu ilikuwa haiweki pesa yoyote isipokuwa ardhi na raslimali zingine, huku Uchina na Omani wakiweka mtaji na utaalamu.

Kwamjibu wa mapendekezo ya mkataba wa awali wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingekusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na haki ya kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badala yake ingekusanya gawio toka kwa chombo cha wabia kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu.

Huu ni moja ya mradi ambo kimsingi ulikuwa umeitangazia dunia vita vya kiuchumi toka kwa washindani wetu ambao ni nchi jirani na zinazotuzunguka. Kwakuwa Afrika yote ingepokelea bidhaa zake toka ulimwenguni hadi Bagamoyo, sawa na ilivyo Dubai ambayo ndio mlango wa Afrika kupokelea bidhaa zake.

Afrika inaingiza bidhaa toka Uchina kwa 88.8% na kiwango cha 98% ya bidhaa hizo zinapita Dubai. Hivyo kujengwa kwa Bandari ya Bagamoyo kungefunga nyia ya Dubai na bidhaa zote za Afrika kutoka China kupita Bagamoyo. Hii inamaana kwamba uchumi wa Dubai na Marekani ambayo ndio mdau mkuu ungemegwa. Mradi huu ulikuwa ndio msingi halisi wa kuanzisha mradi wa reli ya kisasa ya SGR, bila Bandari itakayozalisha mizigo kwa wingi SGR itakuwa ni kwakubeba abiria tu badala ya mizigo.

Serikali ya awamu ya tano katika hali ya kustaajabisha imeutupilia mbali mradi huo kwakutoa sababu ambazo hazina nguvu na zingine za kushangaza sana, mimi naitafsiri kama ni hujuma kwa taifa, izingatiwe kuwa tayari taifa lilishaingia gharama kubwa kuanzia kwenye upembuzi yakinifu, na kusaini mikataba ya awali. Kitendo cha kusitisha katika hatua hii ni kulitia hasara taifa. Moja ya hoja zilizotolewa na rais kama sababu ni kwamba masharti ya wabia nikuwa TRA hairuhusiwi kukusanya mapato, hoja hii ya Rais alikuwa sahihi lakini bahati mbaya alishindwa kufafanua wazi sababu za TRA kutokuwa miusanya mapato ya ubia. Pengine hili Rais alidanganywa.

Pili rais alisema kuwa masharti ya wabia nikuwa Tanzania hairuhusiwi kuendeleza bandari zake zingine. Hoja hii nayo inautata mwingi sana, Bandari zingine zote ziko kwaajili ya ndani, na mradi huu ulikuwa kwa shughuli za kimataifa. Sasa hoja ya kuwa tusikarabati bandari zetu zilizopo ni hoja isiyo na mashiko, Hili inawezekana kabisa Rais hakuambiwa ukweli.

Hoja ya Tatu aliyoitumia Rais Magufuli kukataa mradi ule, ilikuwa kwamba, wabia wanataka wapewe umiliki wa ardhi kwa miaka 99. Hili si la mwekezaji bali la sheria zetu ambazo zinatoa uwekezaji katika ardhi kwa miaka 33 hadi 99. Sasa hoja hii haiwezi kuwa kwa wabia wawili tu kati ya watatu ikiwemo Tanzania yenyewe. Hili nalo kuna uwezekano watu waliamua kumpotosha rais wetu.

Chakusikitisha kwa nchi yangu, Katikati ya mvutano wetu na wabia hadi Rais Magufuli kusitisha mradi, Rais wa Msumbiji Philip Nyusi kwakutumia majasusi wake waliotanda kila pembe ya Afrika na kwingineko, amefanya mageuzi makubwa, amechukua wazo lilelile ambalo limekataliwa Dar es Salaam na wajuvi, amekwenda kulisimika katika Bandari ya Nacala kwakuingia ubia na Wachina kwa Dola bilioni 5 za Kimarekani, hii ni Bandari inayotarajiwa kuwa lango kuu la kiuchumi Afrika.

Wakati hili halijapoa, Mwaka 2017 tu juzi Tanzania tulipowazuia wazungu wasisafirishe madini ghafi na makinikia yao, tuliimba nyimbo kwamba Tanzania itajenga vinu vya kuchenjulia madini hapahapa, na nyimbo ziliimbwa kisiasa zikaitikiwa kishabiki kwa beti za kinafiki kwelikweli. Leo nyimbo haziimbwi, hakuna anayejua kama viwanda vimeshajengwa au laa na hakuna anayehoji hilo kwakuwa ukihojihoji tu basi ukinusurika sana utaenda mochwari au Ubelgiji, tulishazoe vimbunga kwamba vitavuma na kutulia.

Lakini huku sisi tukiwa tumebadili nyimbo sasa tunaimba nyimbo za Standard Gauge nk, Rwanda kwakutumia majasusi wao waliotanda kila pembe ya Dunia, imelichukua wazo lilelile la Tanzania imejenga vinu vya kuchenjulia madini na inatarajiwa kwamba hadi 2024 Rwanda iwe ndio nchi ya kwanza barani Afrika inayosafirisha madini kwa wingi nje ya Afrika. Kumbuka na elewa Rwanda sio mzalishaji wa Dhabu, Almasi wala chochote kiitwacho madini isipokuwa kwenye kilimo cha chai na kahawa huko. Hivyo anategemea viwanda vyake vipokee madini ghafi toka Tanzania, Kongo, Zambia akusanye kodi yake na kugonga muhuri wa madini unaotambulisha kuwa ni madini toka Rwanda nk. Sisi tumelala. Siasa inanguvu bana.

Kwa maoni yangu ninafiki kuna tatizo kubwa kwenye eneo la Ujasusi katika nchi yetu, hasa ujasusi wa Kiuchumi, na hili ndilo lilikuwa msingi wa mimi kuandika Kitabu changu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi. Michakato mingi ya kiuchumi katika nchi hii imekuwa haina mafaa ama inaliacha taifa katika makovu makubwa yasiyozibika. Hii inazaa uhalali wa kuhitaji mageuzi makubwa katika Idara ya Ujasusi nchini kuanzia kwenye ideology, sheria, misingi, kanuni, na mambo anuai ndani ya idara ya ujasusi nchini.

Ujasusi kwa nchi zilizoendelea kama China, Israel, Urusi na Marekani, unafanywa na watu ambao ni smart na wanajengwa kuwa smart ili kuweza kumudu ugumu wa kazi hiyo na kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa. Majasusi katika nchi hizo hawapewi kazi kwasababu ya ujomba ujomba na kujuana.
Ni kweli asilimia kubwa ya information's zenye thamani katika kazi ya ujasusi huwa zinaletwa na "human intelligence" badala ya magazeti, TV na source nyingine za habari.

Kwa maana hiyo basi ni lazima kuwe na watu competent ambao wana uwezo wa kukusanya habari za kijasusi ili tuweze kupata information's za maana na kujenga uwezo wa kuzifanyia kazi informations hizo. Imagine wakati ule wa vita baridi jinsi Directorate 16 ya KGB ilivyoweza kufanya kazi ya kununua sensitive navy information za USA na kuweza kutengeneza balance ya navy fleet bila USA kugundua kwa miaka 17 kupitia kwa Johny Walker junior!

Tanzania kwenye balozi zetu kuna majasusi. Lakini ni majasusi wa aina gani? Wale wa kujua kuongea kifaransa na kireno na lugha nyingine za mataifa ya nje bila upeo wowote wa Technologia? Kama kuna sehemu tunakosea basi ndio hapo. Majasusi wengi wa Tanzania au tunaoambiwa kuwa ni watu wa system wengi katika tafsiri ya kijasusi ni "informers". Ujasusu kama ujasusi hapa Tanzania ni kama hakuna. Usalama wa Taifa au TISS/UWT msingi wao uliounda chombo hiki ni "power defensive", yaani wajibu mkubwa unaelekezwa kwenye kumonitor mwelekeo wa kisiasa Tanzania hasa kuwadhibiti oppositions na elements zote za upinzani na assasinations za elements zozote zinazoonekana kuwa against na himaya ya CCM.

Idara ya Usalama wa Taifa hii tuliyonayo leo ilianzishwa na CCM 1997 kutoka katika muundo wa kijamaa wa chama kimoja, hii ni baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo bado unaiserve CCM kwanza kisha Taifa linatafsiriwa salama kupitia matokeo ya uimara wa ccm, kama yakifanyika mageuzi ya kimuundo, kisheria, kikanuni na kisera, uimara wa Taifa hautatafsiriwa kupitia uimara wa ccm madarakani, na mambo mengi tunayolalamikia sasa juu ya taifa hayatakuwepo tena. In simple words, taswira kubwa inayoonekana yauhakika ni kazi yao ya kulinda viongozi, kusafiri na viongozi na kuilinda CCM.

Nje ya mambo ya Ujasusi wa Kiuchumi ambao mimi ndio ninaoupigania siku zote uongoze nchi, Naweza kusema Tanzania tuko vizuri katika Ujasusi wa kidola kuliko nchi yoyote pengine Afrika nzima, Hili limefanya kuimeza idara na kuonekana siasa ambazo ndio zinabeba taswira kubwa ya ubora ama udhaifu wa ujasusi Tanzania, Eneo la Ujasusi wa Kidola Tanzania kuna vitengo vya wachapakazi hasa kiko jeshini.., kitengo cha ujasusi ambacho kilikuwa kiko free from politics party ni CMI (central military intelligence). Lakini bahati mbaya muundo na aina ya uongozi wa Magufuli ulikiingiza katika siasa pale kilipofanywa kuwa decision maker wa nchi, lakini upande wa foreign assets ndio wazuri sana wako bize kukusanya taarifa hatarishi dhidi ya nchi...

Kwa undani zaidi Soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.
View attachment 1747076
Kuhusu Bandari ya bagamoyo,haujadadavua vzr,kipengere Cha miaka 99,umekuwa shallow sana,
 
Huu mradi wa bagamoyo ujadiliwe kwa kina kabla ya kuamuliwa Cha kufanya, ndugai haaminiki.Kwa Nini asubiri mpaka jpm afe ndo aseme? Je hoja za Jpm zimejibiwa ipasavyo?
 

Attachments

  • 2736317-18d679f7a5f0d520b2b3467822105fdc.mp4
    5.5 MB
Mnajikuta mnaujua mkataba kuliko Mzalendo namba moja, JPM. Wote mnaoshabikia kuliuza taifa letu pendwa hakika laana hii itakuwa juu yenu na vizazi vyenu.
Ndugai kabadilika ghafla, sielewi Kuna nn.Tatizo kuu la viongozi wetu ni unafiki, yaani spika wa bunge anamuogopa rais kutoa ushauri kwa maslahi ya taifa?
 
Moja, Mkataba umeuona au unajitia jasusi lakiuchumi huku huna data!!
Pili, kuzuia madini lilikuwa jambo lisilofaa? Na je, unajua nini kinachelewesha ujenzi wa mitambo ya uchenjuaji?

Tatu,je unajua uharamia wa Rwanda kwenye madini ya Congo? Unadhani mitambo ya kuchenjua wanajenga wakitegemea madini ya tz?

Tusiwe wepesi kurukua hoja nyeti bila deep study! Utajiita jasusi kumbe nibange tuu zinakusumbua lkn huna welewa wa kutosha kwenye mada unazosimamia!
Jifunze kwanza kabla ya kufunza la utaponza wengine!!
 
SWALI KWA WASUKUMA:

UWANJA WA NDEGE CHATO ILIKUWA SAWA ILA BANDARI YA BAGAMOYO SIO SAWA?

MKATABA UWEKWE WAZI.
 
Back
Top Bottom