Sikuwa mjinga, niliamini niko sahihi, leo Ndugai amejibu

Hayati JPM alikuwa sahihi kwa sababu aliusoma mkataba na kufanya maamuzi. Ndugai anadai alikuwa misled, yeye akiwa Kama mkuu wa chombo kinachoisimamia serikali alifanya nini. Mbona anasema Sasa wakati JPM kendazake? Unafiki tu.
 
Huu mradi uwekwe wazi sio kwamba Hayati alikuwa mbaya completely hapana kuna vitu visipowekwa wazi vitaleta UTATA huko mbeleni.

Hatukatai maendeleo lakini yaje yale tutakayokubaliana nayo na kwasasa ni vyema Mh. Rais akurudisha vichwa ndani ya bunge kutoka upinzani ili vikapeane changamoto na wasomi wetu wa CCM ndani ya bunge tusonge mbele.
Kumbuka marehemu wenu hakuwa wazi pia,
Amlichukua mikopo akasema tunaanzisha miradi kwa pesa za ndani
 
Yericko Nyerere haya mambo ya kuambiwa unahitaji mda kuyatafakali.

Machina ni mfanya Biasahara kama wafanya biashara wengine. Kama mambavyo Barick wamekuwa wakitupiga kwentye Madini kwa sasabu tu tunasubiri gawio huku wao wakitangaza hasara ndio hivyohivyo Bagamoyo inaenda kuwa.

Pili. Unajifunza nini kuhusu Sirilanka? Wachina si wamejenga pale bandari?

Afu ukisema Bandari ya DAR ni ya mizigo ya ndani nakushangaa? . Uwepo wa bandali ya Bagamoyo ni kuua ya Dar hili halina ubishi. Na inaenda kuwa gofu.
 
Kwani wananchi huwa hawatoi maoni kamati za bunge zikiwa zina review miswada? Issue hapa ni mkataba kuwa wazi kwa wananchi and since hauwezi tu kutolewa mtandaoni hakuna namna zaidi ya walau kufika bungeni ili tujue content na fall back position zetu
HIZO POSITION ZENU MLIZOKULA HELA ZA WACHINA NDIO ZINAWASUKUMA KUSEMA KUWA MWENDAZAKE ALISHAURIWA VIBAYA !! MNGEKUWA NA UBAVU KWANINI HAMKUPIGA KELELE WAKATI MWENYEWE YUKO HAI? MNA MAANA ALIKUWA HANA AKILI YA KUJUA KUWA ANASHAURIWA VIBAYA!
 
Kwanini tusiboreshe bandari ya Tanga, dar na Mtwara,

Kwanini tujenge mpya kwa mapesa yote hayo.

Tutumie the same amount kuboresha zilizopo.
 
Kama izo hoja tatu ni za kwel basi rais alifanya vizur sana kuukataa huo mkataba
 
tuweni makini na wachina wanatesa sanaa nchi za afrika na soon waafrika tutaanza kuongea kichina maana lengo lao kuu ni kuwa na pendera yao ya Africa State Of China.
 
HIZO POSITION ZENU MLIZOKULA HELA ZA WACHINA NDIO ZINAWASUKUMA KUSEMA KUWA MWENDAZAKE ALISHAURIWA VIBAYA !! MNGEKUWA NA UBAVU KWANINI HAMKUPIGA KELELE WAKATI MWENYEWE YUKO HAI? MNA MAANA ALIKUWA HANA AKILI YA KUJUA KUWA ANASHAURIWA VIBAYA!
Tafuta michango yangu humu kuhusu mradi wa Bagamoyo...... Niliandika humu kuhusu multiplier effect ya mradi kwamba ina outscore hasara za mradi.

Shida watu waliangalia kodi tu na kupanua Bandari zingine ila hawaangalii ukubwa wa mradi kwamba una faida lukuki za long term. Mfano kwa ukwasi mabenki yetu, Ajira (Indirect), Enterprise growth, spillover ya teknolojia, suppliers, feeding SGR, ATCL etc, aaah name it

Hayo ndio ya kufocus sio kelele za miaka 99 sijui nchi kuuzwa kana kwamba negotiatiors wetu hawana
 
Kwanini tusiboreshe bandari ya Tanga, dar na Mtwara,

Kwanini tujenge mpya kwa mapesa yote hayo.

Tutumie the same amount kuboresha zilizopo.
Wapi wamesema hiyo hela tunayo

Hapo ni uwekezaji wa PPP kama tu uchimbaji madini ambapo serikali ni wana hisa ingawa hawajaweka hela yoyote kwenye operating cost but wana hisa 16%.

Sie tunatoa ardhi wao wanatoa pesa.... Serikali maybe inaweka guarantee tu ya mradi. Sio mkopo kwa serikali ya Tz!!

Na kama hoja tuendeleze iliyopo ina maana hta SGR ama Nyerere Dam tusijenge kwa sababu kuna reli tayari ma kuna Mtera tayari??

Kina cha bagamoyo kina uwezo wa kuingiza meli kubwa kuzidi hata Mombasa/Lamu docks.

Embu tuwe positive..... Kma kuna clause mbovu ziwe renegotiated sio kuutupa mbali mradi sababu investment yake tu itaingiza output kubwa kuliko hata bandari zilizopo.
 
Huu mkataba wa bandari ya Bagamoyo usipowekwa wazi kwa wananchi hakuna upande wa kuuamini. Kujadili hili jambo ni kulenga shabaha gizani tu.
Tundu Lissu, Lema na Chadema kwa ujumla mkitaka kuuwa legacy ya hayati rais Magufuli kwa watanzania itabidi ufanye yafuatayo.

Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?.

Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.

Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.

Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?

Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche ,Lema,Lisu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege

Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?

Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe ,itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?

Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?

Watakaposema lazima watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa
hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga,
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa?

Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni watanzania.

Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.

Muda utaongea .
 
Huu mkataba wa bandari ya Bagamoyo usipowekwa wazi kwa wananchi hakuna upande wa kuuamini. Kujadili hili jambo ni kulenga shabaha gizani tu.

Huu mradi ukianza CAG atakuja na kashfa kubwa kuliko zote zilizowahi kutokea.
Kuna shetani mkubwa ashamnyemelea Yuda Iskariote
 
Kwanza kutoka bagamoyo hadi bandari ya dar kuna umbali gani ? Mbona ni jirani sana hiyo mizigo ya mataifa kwanni wasishushie bandari ya dar
Mkataba huo magufuri aliuona ikulu na akausoma mwenyewe unaposema alishauliwa vibaya siwaelewi
Ansema mkataba nimeusoma ni hovyo sana hata chizi barabarani hawezi kuusaini mkataba wa kipumbavu sana
 
Huu mkataba wa bandari ya Bagamoyo usipowekwa wazi kwa wananchi hakuna upande wa kuuamini. Kujadili hili jambo ni kulenga shabaha gizani tu.
Umenena vyema Mkuu. Na bahati nzuri JPM ashaondoka na mtizamo wake. Hao waliobaki nao watekeleze yao.
 
Hii nchi inawapumbavu wengi kuliko wajinga.
Yaani leo hii Yeriko anataka tuamini kuwa huu mradi ni wa manufaa kwetu kuliko kwa Mchina na mu Oman?.
Ni kweli tumekuwa wapumbavu kiasi hiki?

Mtu anakuambia atagharamia kila kitu wewe toa ardhi tu na rasilimali nyingine...halafu kutakuwa na chombo cha kukusanya mapato na si TRA ila TRA watachukua gawio kutoka kwa chombo hicho! Kweli?

Miongoni mwa viongozi wa hovyo nchi hii kwasasa ni Ndugai.
Ni mnafiki.
Ni tapeli.
Yaani hajui watu wanaakili kuliko yeye.

Tuna watu wa hovyo sana nchi hii.
Yaani tunatakiwa kuaminishwa leo kuwa mchina ni mkombozi wetu.

Eti Tanzania ifanywe kitovu cha uchumi wa dunia. Dah. Yaani Yeriko umetudharau kiasi hicho?
Eti Dubai na Marekani sijui gani huko zigawane uchumi na Tanzania.

Eti mizigo yote Africa ipitie Bagamoyo!!
Eti leo Tanzania iwe na eneo linaloitwa Bagamoyo nchi zote Africa zije kuchukulia bidhaa zake hapo.

Ee Mungu tunusuru. Kama kuna mahali Mungu tumekukosea tusamehe tu jamani.

Yaani kuna kakikundi ka watu wanaamini wao ndo wanauwezo wa kufikiri kwaniaba ya Watanzania wote.

Tuacheni na vi miji vyetu na vibandari vyetu.

Narudia tena kusema....hii Username muimark.....kuna siku nitajitambulisha hadharani.
Ila wakati huo katika hali ambayo haitatarajiwa na wengi.

AMEN.
 
Hapa we umewakilisha maoni tu hujawekwa indicators za mkataba.

Kupitia maoni yako tu kuna mapungufu tayari, kama sheria zetu zinaruhusu uwekezaji wa 33yrs na 99yrs kwanini sisi tukasaini miaka 99 tukaacha miaka 33?
 
40 Reactions
Reply
Back
Top Bottom