Sikupi pesa ila nakupa mchongo, amua wewe

Sikupi pesa ila nakupa mchongo, amua wewe

Yaan uwongo uwongo tuu..
Hiyo fivver sijui mdudu gani an ukianza process zao ndo utajua ujui kuna sehemu unafika watahitaji taarifa zako za bank na hapo ndo utajua ujui unaanza kuambiwa mambo ya kulipia

Faken
Wapi wamekwambia mambo ya kulipia?. Njoo nikufungulie akaunti bure ili uwe shuhuda
 
Siku chache zilizopita niliwapa stori ya rafiki yangu wa kijani ambaye amenisaidia kuona upande mwingine wa dunia ya freelancing. Wengi mliuliza:

"Huyo rafiki ni nani?"

Leo nimeamua kumleta rasmi.

Jina lake ni FIVERR.

Usichanganyikiwe na kizungu, ngoja nikuelezee kwa lugha rahisi.

Fikiria una ujuzi wowote unaoweza kumsaidia mtu mwingine. Inaweza kuwa kuandika, kutengeneza logo, kuhariri video, kufundisha Kiswahili, kupanga safari za watalii, kupiga picha, kutengeneza content za mitandao ya kijamii au hata kurekodi sauti tu.

Tatizo huwa moja.

Unajuaje wateja wanaokuhitaji?

Hapo ndipo rafiki yangu wa kijani anapoingia.

FIVERR ni kama dalali wa mtandaoni, lakini tofauti na baadhi ya madalali tunaowafahamu, huyu hakimbii na pesa za watu. 😄

Yeye anakupa sehemu ya kutangaza ujuzi wako kwa dunia nzima.

Mteja akiona huduma yako na akaipenda, anakupa kazi.

Lakini kabla hujaanza kazi, mteja analipa kwanza pesa kwa Fiverr.

Fiverr ndiyo inashikilia pesa hizo kwa usalama.

Wewe unafanya kazi.

Mteja anathibitisha kuwa ameridhika.

Kisha Fiverr anakutumia pesa zako.

Rahisi hivyo.

Jambo ambalo watu wengi hawalijui ni kwamba hapa si lazima uwe na PhD, Masters wala Bachelor ndiyo upate kazi.

La hasha.

Kama una ujuzi ambao unaweza kumsaidia mtu kutatua tatizo, tayari una nafasi.

Unaweza kuwa:

✅ Mwongoza watalii

✅ Mwalimu wa Kiswahili kwa wageni

✅ Mpiga picha

✅ Content Creator

✅ Graphic Designer

✅ Video Editor

✅ Virtual Assistant

✅ Voice Over Artist

Kitu kingine kinachonivutia kuhusu Fiverr ni tofauti yake na platform nyingi za freelancing.

Kwenye platform nyingi, wewe ndiye unatakiwa kutafuta kazi.

Unaandika maombi.

Unaomba nafasi.

Unashindana na mamia ya watu.

Wakati mwingine unakosa kazi hata baada ya kutuma maombi mengi.

Lakini Fiverr mara nyingi mteja ndiye anayekutafuta.

Anaona profile yako.

Anaona kazi zako.

Anakutumia ujumbe moja kwa moja.

Mnakubaliana bei.

Analipa.

Unafanya kazi.

Unalipwa.

Ndiyo maana hata mtu aliyeanza leo anaweza kupata nafasi ya kupata oda yake ya kwanza ikiwa amejipanga vizuri.

Hatua za kufuata ni rahisi sana, kwanza unaingi kwenye platform kwa kusearch google, halafu unajiunga kwa kutumia email yako ya Gmail, halafu unajaza taarifa zako za profile ikiwemo ujuzi wako, uzoefu wako, potfolio na vyeti vyako kama unavyo (siyo lazima sana kwa kuanzia) halafu hatua inayofuata baada ya hapo ni kutengeneza GIG (tangazo la kuitangaza huduma unayotoa) kwa wateja. Ukishamaliza, kinachofuata wewe ni kusubiri upate message za wateja wanaohitaji uwafanyie kazi kisha wakulipe.

Pesa za kukupa sina, nashare haya ili nawe uweze kujitengenezea kipato mtandaoni.

Fursa mtandoni zipo

Watu wanalipwa kila siku

Swali ni:

Je, wewe uko tayari kujifunza na kujaribu?

KAZI NI KWAKO, ingia ujaribu ukikwama nipo kukusaidia!

CHAO 🟢
Shukrani sana bwana mdogo kwa somo hili zuri! Watu wengi hapa duniani huwa wanadhani lazima uwe na vyeti vikubwa kama chura kiziwi na PhD zake za mchongo kumbe unachohitaji ni ujuzi unaoweza kulipika tu. kwa uzoefu wangu Fiverr imesaidia vijana wengi sana duniani kujiajiri wakiwa vyumbani mwao. Barikiwa sana mdgo wetu kwa kushare madini haya bila malipo yoyote maana wengine huwa wanalipisha! 💎🇹🇿
 
Tatizo nahisi kama skilĺ hv maana nilchosomea ni ki za ki technician zaidi ...sijui kuhusu graphic design labda nijaribu hio ya kufundisha kiswahili ila sasa nayo si inatakiwa uwe mzuri kwenye lugha nyingine pia sasa kingereza chetu chenyewe cha kuunga unga
 
Fursa Fursana 😀

Taarifa za bank ili wajue pa kukuwekea pesa zako, usiopoge. Utajiri unahitaji risk 😂😂😂
Kuna pesa inabidi pia utoe wewe ...
Mambo ni mengi mi ni graphic designer nimefanya hiyo joining ya huo mtandao mpaka nikachoka as if unaomba mkopo loan board
 
Tatizo nahisi kama skilĺ hv maana nilchosomea ni ki za ki technician zaidi ...sijui kuhusu graphic design labda nijaribu hio ya kufundisha kiswahili ila sasa nayo si inatakiwa uwe mzuri kwenye lugha nyingine pia sasa kingereza chetu chenyewe cha kuunga unga
Hiyo ya technician ni ipi?, kama huna skill yoyote unaweza kuweka huduma ya kuwatumia watu wa nje kitu chochote halali wanachohitaji kutoka Tanzania, yaani unatafutia mfano unga wa mtama 😀 halafu unawatumia, baadaye ukipata skill nyingine unaongeza huduma
 
Yaan uwongo uwongo tuu..
Hiyo fivver sijui mdudu gani an ukianza process zao ndo utajua ujui kuna sehemu unafika watahitaji taarifa zako za bank na hapo ndo utajua ujui unaanza kuambiwa mambo ya kulipia

Faken
Zamani sana niliwai jiunga na hyo app..... Hakuna hayo mambo ya kulipia, labda iwe sasa hvi.

Kuna ndugu yngu alikuwa anaitumia sana kupata kazi ndogondogo miaka ya 2017

Alichosema mleta uzi kipo sahihi na si utapele.
 
Zamani sana niliwai jiunga na hyo app..... Hakuna hayo mambo ya kulipia, labda iwe sasa hvi.

Kuna ndugu yngu alikuwa anaitumia sana kupata kazi ndogondogo miaka ya 2017

Alichosema mleta uzi kipo sahihi na si utapele.
Sijasema utapeli ila nimezungumzia ishu moja muhimu mno, watu wanavyo rahisisha mambo humu as if wamefungua now hiko kitu.

Process ya kuwa verify huko kwa huo mtandao ni complex mkuu..
Kuna kipengere ukifika inabidi utoe taarifa zako za bank na hapo utahitaji kulipia..
 
Yaan uwongo uwongo tuu..
Hiyo fivver sijui mdudu gani an ukianza process zao ndo utajua ujui kuna sehemu unafika watahitaji taarifa zako za bank na hapo ndo utajua ujui unaanza kuambiwa mambo ya kulipia

Faken
Duuuh,hii mbona mpya
 
Back
Top Bottom