Namsimulia Rafiki yangu wa Kijani

Namsimulia Rafiki yangu wa Kijani

Mwafrika mmoja

Senior Member
Joined
Mar 15, 2019
Posts
104
Reaction score
234
Stori yangu inaanzia mbali, mwaka 2020 wakati ambao COVID-19 ilishika kasi, watu wanapunguzwa makazini, wengine wanapewa likizo bila malipo na wengine wanaendelea na kazi lakini mishahara inasua sua.

Maisha yangu yalikaba sana, nilikuwa nategemewa na pesa ninayopata haitoshi "NINATOKAJE?" ndiyo swali nililokuwa najiuliza.

Ukafika mwaka 2021, hakuna kilichobadilika kwangu.

Mwaka 2022 nikasema nisipokaza nitakufa njaa ilihali nje naonekana nina amani na furaha.

Nikaanza kutafuta fursa nje ya box, kwakuwa mimi kazi yangu ilikuwa ni ya kushinda mtandaoni sana, nikasema kwanini nisijaribu kutumia hii internet kuingiza kipato, kwasababu nilikuwa naona watu wengine wanavyotumia mtandao kupata pesa.

Nikaanza kujifunza skills mbalimbali na njia ambazo watu wanatumia kupata pesa mtandaoni, ndipo nikakutana na RAFIKI WA KIJANI.

Rafiki wa Kijani nilimfahamu kupitia YouTube pamoja na Freelancers mbalimbali walivyokuwa wakimuelezea nikavutiwa. Nikamsoma nikamuelewa na ndani ya mwaka huo wa 2022 nikafungua akaunti ya kwanza kwa rafiki yangu huyu wa Kijani.

Kiukweli mambo hayakwenda kama nilivyotarajia na kupewa imani na walimu mbalimbali juu ya namna ninavyoweza kuvuna pesa kupitia rafiki huyu.

Ndani ya mwaka huo wa kwanza niliyofungua akaunti, sikupata hata dola senti moja licha ya kupoteza muda wangu na akili.... NILIUMIA SANA.

Bado nilijipa moyo huenda bado sijamfahamu vizuri rafiki yangu huyu wa Kijani, katika kuongeza ujuzi na maarifa nikakutana na mentor mmoja kutoka Kenya ambaye nilimpata kupitia mtandao akanishawishi kuwa atanifundisha kila kitu na ndani ya miezi mmoja nitaanza kuingiza $100 hivyo anataka nimpe Tsh 250,000 ili nipate madini hayo, nikapambana nikamtumia pesa cha ajabu akani'block' kabla hata ya kunipa ujuzi wowote. NILIUMIA SANA kwa mara ya pili. Lakini siri hiyo nikabaki nayo mwenyewe sikuwahi kumwambia yoyote kwasababu nilijua ningechekwa.

Basi mambo yangu yalizidi kuwa mabaya 2023, uwezo wangu wa kazi ukawa mdogo sana, nilikuwa na stress muda wote.

Katikati ya mwaka 2023 nikapata pigo lingine kubwa zaidi, pigo ambalo liliniondolea hata kile kiasi kidogo nilichokuwa nategemea kupata kuendesha maisha yangu 💔💔.

PART TWO INAFUATA ........
 
Naona kabisa mwisho wa siku utafanikiwa kutoboa, na utawashawishi raia hapa kwamba mtu akitaka atoboe kama wewe akufate pm umpe madini. Hapo ndio waja watakapokuelewa vzr huko pm. Uongo?
 
Naona kabisa mwisho wa siku utafanikiwa kutoboa, na utawashawishi raia hapa kwamba mtu akitaka atoboe kama wewe akufate pm umpe madini. Hapo ndio waja watakapokuelewa vzr huko pm. Uongo?
Ni haki yako kuwaza .... haukatazwi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom