Sikulifuta Azimio la Arusha - Mwinyi

Sikulifuta Azimio la Arusha - Mwinyi

- Wa-Tanzania tujifunze kulilia utawala unaoheshimu sheria, sio kuheshimu maadili ya anything else, isipokuwa sheria tu ya jamhuri, ama sivyo tutaendelea kubabaishana mpaka mwisho wa dunia. ooh ni Mwinyi, oooh sio blah! blah! Nchi zote zilizoendelea sasa hivi kuna one principle behind nayo ni heshima kwa utawala wa sheria!

Respect.


FMEs!

Mazee,

The spirit of the law is just as important as the letter of the law. You cannot legislate everything, hata ukiwa na some sort of a "Hitch Hiker's Guide to The Galaxy" ya legislation but you can use an ethical compass to guide your legislation and enact new laws.

Sheria inatoka kwenye maadili, hivyo kama huheshimu maadili unaweka msingi wa kutoheshimu sheria.Ndiyo maana Caesar alisema mke wake hatakiwi hata kushukiwa kwamba ana maadili mabaya, hii haikuwa sheria, ni maadili tu.
 
Mwanakijiji

Nimeanza kumsikia Waberoya akiimba "Nasadiki"...nakuchanganya na ile creed ya Nicea!

Waberoya.. karibu sana. NI kweli kuwa AD inahitaji mabadiliko ya hapa na pale. Kuna mambo ambayo mimi na Rev. tumekuwa tukizungumza ambayo yanaweza kubadilishwa na kuwa updated without losing the principles of AD. Unajua watu wengi wakisikia AD wanafikiria "nationalization, ujamaa villages n.k" lakini Azimio ni zaidi ya hayo.

So.. we'll get to that point ya nini furekebishe in the near future.

It is always good to see people stand in what they believe
It is good always to see people bearing and resolving critics in a positive way
It is always good to have a believer of certain beliefs, believing with open mind, who are ready to say , yes here we made mistake, but here we go again!

Leo wakiamka watu , mbali na serikali wakawa believer na watendaji wa AD, na kutumia resources kuwashawishi watu , then I will join them

Elimu hii, ni pamoja na wale wanaoamini bila kupeleleza na kujua; na kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu-AD is good but we need to sit down againa and say where we were wrong and where we shoul go on!, things are not easy at all, na hakuna jibu moja kwa matatizo ya maisha yetu. Huwa halalamikiwi mtu mmoja kwenye failure ya taifa. JKN, AHM, BWM, walishapita tunaishi leo.

wale waumini wa azimio amkeni sasa! dont pass blame to Mwinyi, kesho kuna wengine watatulaumu , 'je na nyie mlifanya nini'!
 
It is always good to see people stand in what they believe
It is good always to see people bearing and resolving critics in a positive way
It is always good to have a believer of certain beliefs, believing with open mind, who are ready to say , yes here we made mistake, but here we go again!

Leo wakiamka watu , mbali na serikali wakawa believer na watendaji wa AD, na kutumia resources kuwashawishi watu , then I will join them

Elimu hii, ni pamoja na wale wanaoamini bila kupeleleza na kujua; na kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu-AD is good but we need to sit down againa and say where we were wrong and where we shoul go on!, things are not easy at all, na hakuna jibu moja kwa matatizo ya maisha yetu. Huwa halalamikiwi mtu mmoja kwenye failure ya taifa. JKN, AHM, BWM, walishapita tunaishi leo.

wale waumini wa azimio amkeni sasa! dont pass blame to Mwinyi, kesho kuna wengine watatulaumu , 'je na nyie mlifanya nini'!
Tatizo lipo kwa Alhaji, kwa sababu yeye alijua ni kichuguu, lakini kwa makusudi mazima akasikiliza ushauri wa tipper za mchanga wa tani saba akaacha kuchukua ushauri toka mlima kilimanjaro, akifikiri au alidanganywa kwa kufanya hivyo atakuwa ameuza uraisi wake.

Mwl alivyo ka pembeni alikwisha yaelewa matatizo yake, na yaki mfumo, alikuwa na nafasi zuri ya kushauri.

Haya basi tusimlaumu Alhaji kwa yale yaliotokea, lakini madhali kama waliopita wanajua makosa yao, kama huyu mwingine (Mkapa) anaye tushauri tusisaini EPA, basi kesho kama kweli wanaipenda Tanzania waombe appointment au wamfuate JK wa sasa na kumpa Dira au kumshauri Raisi vitu vya kufanya ili turudi kwenye mstari na nchi iwe na dira, tunatoka wapi na tunakwenda wapi, lakini kama watu wengine walivyo sema kusema bila matendo hakusaidi. Yeye na Mkapa bado wana nafasi yao kiserikali/kichama na kama raia wengine wa nchi let them play their part now, sio wameisha jichotea halafu wanakaa pemeni wakimchekaa Muungwana kwa Pembeni.

Wanawaona vijana (serikali ) ya Muungwana wakigombana wenyewe badala ya kuwekeza fikra na nguvu zao katika kuiongoza Tanzania.
 
Halafu kwa nini watu wengine wanaongea kana kwamba wao ndio wawakilishi wa Watanzania wote, kana kwamba wao ndio wanajua sisi wananchi tunataka nini? Hii mijadala ya Azimio ni ishara kuwa kuna Watanzania wengi tu tunataka lirejee. Ndio maana hawa kina Sumaye na Mwinyi wanaanza kulizungumzia pia - wamesoma ishara za nyakati. Na wananchi tumelichapisha na kulisoma upya ili tujue siri ya mwelekeo wa nchi hii. Huu ni mwamko wa aina yake. Watu tumegundua tumepotea njia. Sasa tumeamua kuyarejea mapito ya kale, tuangalie wapi tumeanguka, tunyanyuke, tujifute mavumbi na kuifuata njia iliyo sahihi na tuwe na mwelekeo thabiti wa kuelekea Egalite. Hivi wengine hamjalichoka tu Azimio la MKUKUTA?


Nimebaini kuwa kukata tamaa kwa wengi ambao hawaelewi wapi tumetoka ndio kunaletea mtizamo wa watu kama wewe. Kila mtu ana uhuru wa kuamini na kutowa mawazo yake lakini suwala la mmoja kusema kuwa anawasemea wengine halina nafasi hapa. Tunachokijadili ni mustakabali wa Taifa letu na kila mmoja ana haki ya kushiriki lakini tunapojadili jambo basi tuwe na hoja.

Sawa tunalipamba Azimio la Arusha lakini hilo azimio lilitufikisha pahala pabaya na wala hapakuwa na wakati wowore lilipotowa nuru kwa Watanzania. Azimio hilo ni zao la uongozi wetu wa sasa hivi kwani hata waziri au mbunge kijana wa sasa hivi wote ni zao la Azimio la Arusha. Kina kingunge na Malecela na wengineo walikuwa viongozi wakati huo na kina Nchimbi na mohammedi seif, Lowasa, Kikwete na wengine walikuwa viongozi wa umoja wa Vijana. Kwa mwenye akili akishaona hilo atafahamu kuwa Nyerere alihusika na kuliuwa Azimio la arusha kwani si alikuwa Rais wa Serikali na mwenyekiti wa CCM vyombo vilivyotutia katika umasikini na kutuumbia hawa viongozi wanaotuongoza sasa hivi? Ni jambo la kuchekesha kuona mtu kama Sumaye kulizuingumzia Azimio la Arusha akiwa sasa ni miongoni mwa walionufaika na kutofuatwa hilo Azimio. TUSIDANGANYANE AZIMIO LILIKUWA HALITEKE;EZEKI NA NI DHANA YA KUJIJENGA KISIASA NA HALINA NAFASI TENA KUREJEA KWANI WATANZANIA SASA HAWADANGANYIKI.
 
Sawa tunalipamba Azimio la Arusha lakini hilo azimio lilitufikisha pahala pabaya na wala hapakuwa na wakati wowore lilipotowa nuru kwa Watanzania. Azimio hilo ni zao la uongozi wetu wa sasa hivi kwani hata waziri au mbunge kijana wa sasa hivi wote ni zao la Azimio la Arusha. Kina kingunge na Malecela na wengineo walikuwa viongozi wakati huo na kina Nchimbi na mohammedi seif, Lowasa, Kikwete na wengine walikuwa viongozi wa umoja wa Vijana. Kwa mwenye akili akishaona hilo atafahamu kuwa Nyerere alihusika na kuliuwa Azimio la arusha kwani si alikuwa Rais wa Serikali na mwenyekiti wa CCM vyombo vilivyotutia katika umasikini na kutuumbia hawa viongozi wanaotuongoza sasa hivi? Ni jambo la kuchekesha kuona mtu kama Sumaye kulizuingumzia Azimio la Arusha akiwa sasa ni miongoni mwa walionufaika na kutofuatwa hilo Azimio. TUSIDANGANYANE AZIMIO LILIKUWA HALITEKE;EZEKI NA NI DHANA YA KUJIJENGA KISIASA NA HALINA NAFASI TENA KUREJEA KWANI WATANZANIA SASA HAWADANGANYIKI.
Ajabu tena washabiki wa hii a prone to fail system wanavyojaribu kuiremba na majina ya ajabu when it failed completely.

Sio kwetu tu nchi zote duniani zilizo jaribu namna ya maisha yale yalizidi kuongeza umaskini kwa watu wake, system ambayo ai encourage innovation, sytem ambayo doesnt encourage rapid development.

Hila sisi sijui tuna matatizo gani tena tunapigia debe a system of failure, kwa mbwembwe na hili fail understrong leadership.
 
TUSIDANGANYANE AZIMIO LILIKUWA HALITEKE;EZEKI NA NI DHANA YA KUJIJENGA KISIASA NA HALINA NAFASI TENA KUREJEA KWANI WATANZANIA SASA HAWADANGANYIKI.

sawa.. tuoneshe vipengele vya Azimio la Arusha ambavyo hukubaliani navyo na ambavyo vimesababisha umaskini kwa Watanzania.
 
Waberoya,

Ukisoma maelezo hayo juu, hasa yenye bold, naanza kuelewa kuwa unafahamu nini sisi wengine tunalilia. Ila kwa makusudi kabisa, unatafuta makosa ya AD na kuyatumia kuonyesha kuwa AD ni balaa ya Tanzania.

Hakuna anayesema THIS WAS ONLY. Narudia kusema, unafahamu nini sisi tunataka kusema ila unaPINDISHA kwa makusudi kabisa maelezo yetu ili tu kuonyesha kuwa tunafanya makosa makubwa kabisa.

Labda niandike kwa ufupi. Kuanzishwa kwa AD kulikuwa kumejaa makosa au nisema kulisaidia kwa wakati ule ila kabla JKN hajaondoka na hasa akifahamu kuwa tunaelekea kwenye vyama vingi (hili alisaidia lianzishwe Tanzania) kuna baadhi ya mambo ya AD alitakiwa kuyaingiza kwenye katiba ya nchi na yasiyofaa basi ayaaondolee mbali na yeye mwenyewe ALIUWE rasmi Azimio la Arusha. Nasema hivyo kwa sababu AD ilikuwa chini ya chama na nchi ilikuwa ni ya chama kimoja.

Wakaja wajanja wakanja wakaona hili ni tatizo kwao. Wakitumia njia mbalimbali na nina imani hata hao IMF na World Bank, wakaanza kulihujumu kidogokidogo kwa miaka mingi. Mwisho ikaoenekana kwa watu wengi (soma maelezo ya FMes hapo nyuma) kuwa AD inatajirisha watu wachache na kuwazuia wao. Ndipo wakamuweka sawa Mzee Mwinyi.
Mwinyi bila kufahamu/kwa kufahamu akauvaa mkenge na kwenda Zanzibar na kuliuwa kabisa AD.

Baada ya kuuwa AD rasmi, yale mabaya yote na mazuri ya AD yakawa yamekufa. Katika mazuri machache ya AD ilikuwa MIIKO YA VIONGOZI. AD ilikuwa na hili swala muhimu. Viongozi dunia nzima wana matatizo yaleyale ya kutaka kujitajirisha. Nchi za wenzetu huwa wanakwama kufanya hivyo kwa sababu ya miiko ya viongozi na kuwepo vyombo maalumu ambavyo vipo tayari kuwashughulikia mara wanapovunja hiyo miiko.

Kinachoendelea kwa sasa Tanzania ni vacuum ya MIIKO YA VIONGOZI. Kama Mwinyi angelivunja AD na kuichukua miiko ya viongozi na kuiingiza kwenye katiba ya Tanzania, naamini kuwa leo hii angelikuwa anaheshimika zaidi ya JKN. Baada ya miiko ya viongozi kuondolewa, leo hii viongozi wa Tanzania wanajifanyia chochote wanachokitaka bila ya kuogopa kuchukuliwa hatua yoyote.
Wizi wa EPA, Richmond, Deepgreen nk ni mifano michache ya viongozi kujisikia wako juu ya sheria. Kitendo cha waziri kwenda kuweka sahihi mikataba nje ya Tanzania na tena kwenye caffee inatia kinyaa.

Kikwete na ubovu wake, kama akirudisha miiko ya viongozi na kuweka chombo kinachojitegemea cha kulinda hiyo miiko, basi atakuwa ni shujaa wangu mkubwa. Ila hata miiko ikiwekwa na kuwepo chombo kama TAKURURU ambacho kinashughulikia vidagaa, basi ni kupoteza tu pesa.

Ndiyo maana wengine tunaamini kuwa kwa Tanzania inabidi aje kichaa ambaye risasi mbili tatu zitatembea kwa wale wote watakaokuwa wanataka kumpinga kwa vitendo. JKN hawakumpinga kwa maneno ila vitendo, wakammaliza na AD yake.


Narejea tena kuwa Nyerere alishiriki katika kuliondowa AD baada ya kuona kuwa alishindwa kulisimamia. Kwa wale wazee hebu tujaribu kukumbuka enzi zile ni nani alikuwa katika tabaka teule? Nani waliowakitanuwa mitaani? Kama kulikuwa na wafanyabiashara walikuwa wachache sana. Waliowakitanuwa ni viongozi wa Serikali na Chama (kulikuwa hakujulikani tofauti ya watu hawa). Hapo ndio najiuliza hilo la kubakisha miiko ya viongozi lingesaidia nini iwapo wao hawakuhitaji hisa kwani mashirika ya umma yalitosha kuwapa wanachotaka.
Halafu huyu Julius Nyerere tunaemjuwa aliwahi kukosa nguvu ya kupinga alichoona kuwa hakitaki? Tuone mfano wa Serikali ya Tanganyika aliizima single handed. Hili linanifanya niamini kuwa mwenyew alishabaini kuwa Sera yake ilifeli, kwani si utamaduni wa CCMkuwa Mwenyekiti Mstaafu anabaki katika Kamati Kuu? sasa angalia nguvu take halafu ujiulize kwanini hakupinga hili? Jawabu ni rahisi ! Akitafuta nani wa kubeba msalaba kama alivyofanya alipojitia kungatuka!
 
Received, supported and ready for action see my previous post and comment accordingly.Though my stands is, we need to modify some issues, and we need few people as you have pointed out and from there we need to spread the good news, we should never wait for Kkiwete, we all need to take this as our burden,!

Mkuu Waberoya, nimerudi kidogo na nimejaribu kupitia maoni mbalimbali ya wanajamvi na kwa kiasi yamenitia moyo sana. Mengi niliyotaka kusema yamesemwa na sidhani kama kuna haja tena ya kuyarudia - pongezi kwa wote mlioshiriki. Wazo au pendekezo huanza kwa mtu moja na ubaya au uzuri wake hupimwa kwa kuangalia nama hilo wazo lilivyopokelewa na jamii kwa ujumla wake. Siku ile nilibahatika kuwa katika viwanja vya Mnazi Moja na nlilshuhudia Azimio lilivyopokelewa na na wananchi kwa ujumla wao. Pamoja na kwamba sikuwa mwanachama wa TANU (nadhani nilkuwa rebel) sina shaka kwamba siku hiyo Tanzania ilisimama ihesabiwe nayo kama taifa lenye heshima na dira.

Kama kijana msomi (tukipata uhuru mwaka 1961 tayari nilikuwa secondari), nililisoma Azimio na nililielewa na kulikubali. Wazo hata likiwa zuri namna gani katu haliwezi likakubalika kwa jamii nzima kwa wakati moja - ndio ubinadamu huo. Lakini ukweli unabaki pale pale kuwa Azimio lilikubalika kwa Watanzania wengi akiwemo mimi kijana niliyeasi toka mwanzo kabisa mfumo wa utawala wa chama kimoja. Azimio halikuongelea mfumo wa vyama wala vijiji vya ujamaa bali lilitoa picha ya taifa ambalo tulitaka kulijenga. Swala kwamba kuna wachache walianguka na kukanyagwa njiani si la msingi kabisa kwani hakuna mapinduzi duniani yameweza kufanikiwa bila gharama yoyote.

Azimio la Arusha lilimtaka kila mwanachi kwanza kuutambua Utanzania wake, pili kuulinda Utanzania wake na tatu kuutetea Utanzania wake. Hakuna wakati tumewahi kujivunia Utanzania wetu kuliko miaka iliyofuatia baada ya kutangazwa kwa Azimio. Hakuna wakati tumewahi kuheshimika kama Watanzania kuliko mwishoni mwa mika ya 60 na mwanzoni mwa miaka ya 70. Tuliweza kutembea vifua mbele kwa sababu tulikuwa na kitu kinaitwa identity kilichotutofautisha na mataifa mengine ya Afrika. Azimio la Arusha lilipigwa vita vya ndani na nje kwa sababu tu ilituhakikisha usalama wa ardhi na rasilimali zetu na hivyo kulinda urithi wetu. Alichokuja kukifanya Mwinyi ni kuiweka nchi yetu rehani - no, we must get that country back !
 
Makoko wa Uk , kama upo kwa malikia basi utaona hoja za mwalimu zilivyo fanikiwa , mfano ukitaka kupeleka maji kwa watu na ukapunguza gharama si utawashauri wakae sehemu moja ili uweze kuwapatia hiyo bidhaa iwe shule hospitali, maduka, barabara nk na hapo ulipo utaona watu wana kaa kwenye estate, na kuwezesha kujenga miji kutokana na kuwepo kwa watu.

Enzi za UDA basi usafiri mpaka mid night kutegemeana na sehemu, na la asubuhi linaanza mapema. neighbour hood watch ndio sawa sawa na hizo nyumba kumi kumi na kutambuana nani anafanya nini, tatizo kikifanyika kwetu sisi waswahili, unalalamika fulani mnoko kweli.

Sera za Mwalimu ilikuwa ni kuwaondoa Wathungu na ....... ili maduka tushikilie thithi ngozi nyeusi bali ilikuwa ni gradual process ya sisi kujitambua kwamba tunaweza, tuimarishe elimu yetu hata ingefika wakati wa soko huria nk tungekuwa tunajua kutetea kilicho chetu, sio sasa hivi aliye kuibia akikuletea kapelo unamfrahia na kumuongezea nguvu akuibie zaidi.

Yaani Mwl alitekeleza sera za Idi Amini kwa kutumia technique.


Nini faida ya sera bila utekelezaji? AD lililetwa 1967 na mpaka anangatuka Mwalimu hakuna chochote ambacho kilitekelezwa na msimamizi Mkuu alikuwa mwenyew Nyerere.
Hivyo Watanzania watapata maji masafi ,elimu bora, afya njema kwa Sera bila utekelezwaji? Na iwapo anaetowa Sera anashindwa kuisimamia na kuitekeleza nini faida yake? Kama sera ni dhana basi tungeshaondowa umasikini kwa MKUKUTA, tungekwishapata maisha bora kwa MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA na sera nyingi nyengine.
Tunahitaji kuelezwa Azimio la Arusha liliwafanyia nini Watanzania hadi pale lilpovunjwa.
 
Nilikuwapo ndugu yangu, ni siku ambayo ni vigumu kuisahau kama ulikuwapo lakini rahisi kuikebehi kama ulikuwa hujazaliwa. Hamasa, mwamko na mtumaini ya Watanzania na hasa vijana wakati huo yaliweza kuutikisa ulimwengu. Nakumbuka heshima aliyopewa Mtanzania nje ya mipaka yetu kwa aliyebahatika kusafiri wakati huo, ni kubwa. Hofu ilitanda si kwa majirani tu bali hata kwa mashirika ya kitaifa - kote walijiuliza itakuwaje hii kitu ikifaulu. Hapana, hali hii isiruhusiwe katu na vibaraka wakapatikana humu humu nchini na wakatumiwa ipasavyo kuihujumu.

Kama kuna watu wananipa kichefu chefu, ni huyu Mwinyi. Angekuwa mtu makini siku alipoombwa kugombea Uraisi angeweza kabisa akasema, thanks but no thanks, hivi viatu siviwezi - siwezi kuvuka huu mto kwani sijui kuogelea. Lakini Mwinyi being what he is, akatumbukia majini akiikokota nchi ya heshima - matokeo yake sasa tunayaona na kuyashuhudia. Okay, kabla yake tuliitwa masikini, sawa tulikubali na kukataa kuburuzwa, naam si masikini jeuri ? Na sasa tuko wapi ? Wezi wa kutupwa na tunamwibia nani ? Sisi, watoto wetu na wajukuu zetu. Mwinyi akae kimya, period.
Wacha bwana! Maiti ana uchaguzi? Nafikiri Watanzania wengi hawkubali hili la kufa kwa jeuri na natowa changamoto kuwa wewe mwenyewe si mkweli kwa unayoyasema.

Watanzania gani hao waliotayari kufa kwa jeuri (proud) you are joking! Tunapokea kanga na kilo ya mchele kuwapa uongozi waliowateule leo unambie kuwa tuna jeuri ya kufa! Hali halisi inaonyesha kuwa walio wengi wanashukuru kwa aliyoyafanya Mwinyi kwani wao ndio waliokuwa wakifa na njaa baada ya kufilisika serikali.

Kwa bahati mbaya walio wengi tangu uhuru hadi leo hawajawahi kuwa na uchaguzi wa namna ya kuishi, wakati wa Nyerere walihamishwa kwenye vijiji visivyo na huduma na kuishia kufa njaa na sasa wanashuhudia viongozi wao wakifisadi na kujilimbikizia vipato angalau kwa wakati ule wa mwinyi aliwanusuru na njaa na kuwafundisha kuvaa vizuri japo mitumba, kuwaletea nafuu ya usafiri kwa chai harage na kuwapa uhuru wa kusema ambao sasa tunautumia kumkejeli.
 
Nini faida ya sera bila utekelezaji? AD lililetwa 1967 na mpaka anangatuka Mwalimu hakuna chochote ambacho kilitekelezwa na msimamizi Mkuu alikuwa mwenyew Nyerere.


Tunahitaji kuelezwa Azimio la Arusha liliwafanyia nini Watanzania hadi pale lilpovunjwa.

Sasa tayari umeshasema halijafanya kitu unaweza vipu kuuliza lilifanya nini? Ungekuwa na fikra huru ungeomba upatiwe elimu kabla ya kuamua kama Azimio lilifanikiwa kwa kiasi chochote au la.

Kama tayari unajua Azimio la Arusha halikufanya chochote basi hakuna maelezo yanayoweza kukutosheleza kukuambia nini ilifanya. Empty the bucket first in order to carry more water!
 
Sikonge,
Mkuu sina maana ya kutukana ila kuzungumzia Ukweli.. Wakati Mwinyi anaingia madarakani nina hakika tena sii kidogo kwamba naijuia Tanzania ile kuliko wewe!...Naijua kwa sababu nilikuwa katikati ya mgawanyiko wa pande zote za kisiasa nikiwa nimewahi kufanya kazi serikalini, mashirika na hata kuishi na kutembelea Ulaya nchio za kibepari kabla kabisa hatujauvaa Ubepari tukipigwa msasa wa Ujamaa. hivyo mimi niliufahamu Ubepari na Ujamaa kinyume nyume na yawezekana wewe ukikuwa bado ukisoma shule...

Na ninakuhakikisha kwamba mashirika yote ya Umma yalikuwepo na yakifanya kazi vizuri sana isipokuwa tatizo kubwa lilikuwa urasimu, wizi na ufisadi ulofanyika makusudi ktk kipindi cha kwanza cha mwinyi kuyaua hayo mashirika kama vile Mramba alivyoliua shirika la ATC makusudi.

Viongozi wote wa mashirika haya walitajirika kipindi cha Mwinyi kama tunnavyoona leo viongozi wa serikali na taasisi zake wakijitajirisha chini ya Utawala wa Kikwete. Sasa itaka[po fika mashirka hata binafsi kufa tutakuja sema Ubepari hauna faida?..hali tatizo sii uwekezaji chini ya mfumo wa Kibepari bali ni sisi WATU wenyewe..
Leo hii huwezi kupata huduma safi pasipo kutoa kitu, hakuna biashara ama kiwanda hata kimoja kisicho ibiwa.. wizi imekuwa part ya matumizi ktk mahesabu.

Hadi Mwinyi anaingia madarakani, hayo mashirika ya Umma yalikuwa hayazalishi kwa kiwango chake..hili lilikuwa tatizo la kiutendaji na sii la viwanda ama mashirika ni sawa na tatizo la Umeme leo hii wakati Mitambo yetu inauweza wa kuzalisha MW 3000 ila ni asilimia 15 tu ya umeme huo unazalishwa! tatizo la maji nalo ukiangalia linachangiwa na utekelezaji na sii kutokuwepo kwa maji ama mitambo..

Sasa itakuwa ujinga mkubwa ukinambia jibu sahihi hapa ni kuuza mitambo yote ya Umeme kwa sababu ni magofui hali sisi wenyewe ndio tumeshindwa kuikarabati na tatizo sii fedha wala uwezo wa wataalam wetu..
Kifupi, Tatizo la Umeme na maji nchini ni tatizo linalosababishwa na WATU kama vile ajari inaposomwa kwamba sababu imetokana na Human error!
na kikubwa hapa mkuu wangu hatubishani ili mradi bali kuitafakari hotuba ya Mwinyi na kuapata jibu..

Haya, ukimsoma Waberoya utashindwa hata kuelewa anacholenga kwani ni huyu huyu anayesema Azimio la Arusha halikuwa na maana lakini akiunga mkono maneno ya Mwinyi kwamba halijafa!..I mean anajipinga mwenyewe kwa kusifia kifo cha Azimio hilo wakati huo huo akikubaliana na Mwinyi kwamba Azimio la Arusha limeboreshwa..

Mkuu nisome vizuri maeklezo yangu yote yanazunguka ktk kupinga kauli ya Mwinyi.. Ubora ama Ubovu wa Azimio la Arusha haikuwa Issue kabisa ktk maelezo yangu lakini maadam unataka tuzungumzie mazuri ya Ujamaa naweza kabisa kutafuta muda tukadali ingawa swala hili tumekwisha lizungumzia sana huko nyuma..Kisha basi haiwezi kukusaidia chochote kwani maadam umeisha ondoka ktk Ukristu (Ujamaa) ukasilimu na kuwa Muislaam Bepari) itakuwa kazi kubwa kwangu ama Padre kukurudisha ktk Ukristu -Usishtuke, natoa ni mfano tu mkuu!


Sawa Mzee wangu kwa darasa lakini kwa vile umekubali mwenyewe kuwa ulikuwa zao la wateule wakati ule wa Azimio la Arusha nahisi kwanini unakuwa na msimamo ulionao. Ni msimamo wa kifalsafa na si wa hali halisi.

Katika darasa lako umeshindwa kuonyesha sababu zilizoletea kuondoshwa kwa AD. Iwapo hili azimio lilikuwa na faida kama unavyotaka niamini basi ungekuwa mbele kuniambia kuwa hakukuwa na ufisadi wala ubadhirifu wakati wa AD. Hili la ufisadi na kujilimbikizia mali ngilo linalotufanya tujadiliane sasa na iwapo yaliopo sasa ni yale yale yaliokuwepo wakati wa AD basi tuna maana gani ya kulirejesha?

Nilisema huko juu na sasa nasema tena! Si nyinyi mliokuwa wateule wakati wa AD ambao ndio mnaoendelea kututawalka na kuhodhi kipato? Naomba ukanushe hayo na urudi na kujiuliza iwapi conscious ya hao waliokuwa wakiamini AD. Kwa fikira zangu tatizo naona kuwa sasa wateule wameingiliwa kati na wafanyabiashara na hilo ndio linaloleta mgogoro kwani mwananchi wa kawaida wa Tanzania hajawahi kufaidi matunda ya Sera za wateule angalau kuamzia kipindi cha mwinyi wananchi walio wajanja wachache wameweza kuvuka daraja na kuwa miongoni mwa wateule kwa kuwa Mwinyi alifunguwa madirisha kama anavyosema mwenyewe.
 
sawa.. tuoneshe vipengele vya Azimio la Arusha ambavyo hukubaliani navyo na ambavyo vimesababisha umaskini kwa Watanzania.


Kipengele kikubwa unachokihitaji ni kuwa lliizuia jitihada ya mwananchi wa kawaida kujiendeleza na kumtaka abaki masikini kwa kumkataza mfanyakazi kujipatia kipato kwa uwezo wake. Hivyo hawa wanaofanyakazi baada saa za kuajiriwa wana kosa?
 
Sasa tayari umeshasema halijafanya kitu unaweza vipu kuuliza lilifanya nini? Ungekuwa na fikra huru ungeomba upatiwe elimu kabla ya kuamua kama Azimio lilifanikiwa kwa kiasi chochote au la.

Kama tayari unajua Azimio la Arusha halikufanya chochote basi hakuna maelezo yanayoweza kukutosheleza kukuambia nini ilifanya. Empty the bucket first in order to carry more water!


Naam niliposema halikufanya kitu nilisema kwa mtazamo wangu na nilipouliza niliuliza ili kuona na kueleweshwa kuwa pengine siko sahihi. Hili la fikira huru linanzia na kuwa na msimamo na jukumu la kuubadilisha msimamo au kuusapoti ni jukumu la wengine.
Hili la pili ni kuwa labda kuwe hakuna maelezo muafaka basi kweli porojo tu na hata iwe kitabu haiyoniridjisha. Nilipojiunga na Forum nilijuwa tangu mwanzo kuwa kutakuwa na tofauti ya mawanzo.
 
Unajua Mkandara unazungumzia theories wakati hali halisi inakusuta kwa hayo unayoyaeleza.au wakati anaingia mwinyi ulikuwa bado huujuwi dunia? Mashirika yalitowa ajira kwa watu jee wangelipwa nini wakati mashirika hayazalishi na wala serikali haina pesa za kuwagawia wafanyakazi kama ngawira?

Unapozungumzia kuondowa miiko ya uongozi unakusudia miiko hiyo ni ipi? Azimio la Arusha halikuwa na mipaka kati ya kiongozi na mwananchi wa kawaida kwani kwenye Azimio hilp unajua Kiongozi ni nani? Iwapo kila mfanyakazi anazuiliwa kupata kipato cha ziada nini maana yake? Wafanyakazi wafe njaa chini ya malipo dubi na yasiyokuwepo? Taifa la Watanzania hapo likisemwa kuwa la wafanyakazi na Wakulima sasa mihimili ya uchumi inaponyimwa mfanyakazi na mkulima yuko kijijini na Serikali haina Fedha za kuendesha biashara nchi itaenda vipi. Ndio maana Marmo amesema kuwa mambo mengi yanasababisha hali hii tunayojadiliana nayo.

Ngekewa tuko pamoja
Licha ya mashirika kuwa mengi na karibuni yote kundeshwa kwa kodi za wananchi na uchapishwaji wa noti mpya kila kukicha (refer Nyirabu-Nyerere relationship), serikali ilikuwa inafanya kazi ambayo haiihusu kabisa. Hebu angalia utitiri wa kazi au biashara ambazo serikali ilikuwa inahodhi:

Kampuni ya Kuku
Kampuni ya Maziwa
Kampuni ya Ng'ombe
Kampuni ya Usagishaji
Kampuni ya Usafirishaji ( UDA, KAMATA, KAU...RU, MA, etc.)
Kampuni ya Uvuvi
Kampumi ya Kilimo na Chakula
Kampuni ya Viatu
Kampuni ya Chai
Kampuni ya Chumvi
Kampuni ya Sukari (SUDECO)
Kampuni ya Magari
Na mengine mengi (orodha ni ndefu) ambayo serikali haikuwa na ulazima wa kuyaanzisha kuyahodhi huku yote yakiendeshwa kwa urasimu wa serikali. Watendaji wake wakuu wakilipwa mishahara na marupurupu yasiyolingana kamwe na uzalishaji wake. Namba ya ajira katika makampuni yote hayo haikujali uwezo halisi wa mahitaji ya biashara.

Tungeendelea kuchekesha na tusingekuwepo hapa tulipo kamamaamuzi sahihi ya kurekebisha uchumi yasingechukuliwa.

Azimio la Arusha halikuwa ni msahafu au biblia kana kwamba haliwezi kurekebishwa. Azimio la Arusha msingi wake pia uliegemea katika mawazo ya mtu mmoja au kikundi kidogo cha watu.

Azimio la Arusha ndiyo lililoweka misingi mibovu ya uchumi wa nchi yetu kwa kuwanyang'anya uwezo wa kufikiri watanzania wazawa katika kuchemsha bongo zao na kuibuka kuwa wafanyibiashara wakubwa, badala yake walitakiwa wafanye kazi zaidi kwenye serikali au mashirika yake kwa ajili ya kujenga uchumi wa nchi yetu changa na huku ikwaachia uwanja mpana usiokuwa na upinzani watanzania wenye asili ya kiasia wakitawala fursa ya kufanya biashara kwani wao Azimio la Ausha halikuwagusa kabisa. Walipewa haki zote za kufanya biashara bila ya kuulizwa kama wana maduka mawili au zaidi, biashara zaidi ya moja, nk.

Turudi nyuma katika ukweli, kipndi ambacho Mwiny yuko madarakani ilikuwa ni kipindi ambacho mabadiliko mengi na makubwa ya kiuchumi na kisiasa yalikuwa yana fanyika duniani. Kwa mfano, mabadiliko ya mfumo wa siasa ya vyama vingi, kuanguka kwa Soviet, urekebishaji wa uchumi kwa nchi masikini nk. Wote tunakumbuka jinsi IMF na WB walivyokuwa wanatuasa tubadilishe sera zetu ili kuvutia mabadiliko ya kiuchumi. Ili kuyakubali yote hayo kama kiongozi wa nchi kunahitaji ujasiri na busara tele la sivyo ukigoopa kugeuka jiwe basi itabidi ung'atuke tu.

Hata hivyo ni lazima tuangalie ni kwani nini tunakuwa na Kiongozi wa nchi anayechaguliwa na wananchi kila baada ya muda fulani na kumwekea ukomo?

Hii ni wazi kuwa tunahitaji mawazo mbadala ndiyo maana kwa kila nchi yenye busara imeweza kuona mbali na kuhakikisha kuwa kuna kuwa na uongozi mpya kabisa kila baada ya miaka fulani. Kwa mantiki hiyo basi ni vema kila kiongozi aingiaye madarakani afanye jambo ambalo litaweza kusahihisha ukomo wa kufikiri wa kiongozi aliyepita.

Kwa mfano kabla ya uongozi wa Mwinyi, kiongozi aliyekuwepo
aliamini kuwa wananchi kupiga mswaki wa mti na mkaa ilikuwa ni 'sawa tu', kuogea sabuni ya kufulia iliyo katika kiwango cha chini kabisa ni 'sawa tu', kupangia wananchi kiwango cha manunuzi ya bidhaa muhimu kwa wiki au mwezi kama vile sukari nusu kilo kwa mwezi mzima kwa familia ni 'sawa tu' kuogea sabuni ya Lux na kutumia Colgate ni kuhujumu uchumi.

Kutopatia nafasi watoto wanaomaliza darasa la saba nafasi ya kuendelea na elimu ni 'sawa tu'.

Sasa unapofikia mahali unapewa nchi ipo katika hali kama hiyo wewe kama kiongozi mpya wa nchi utaendelea kutumikia mawazo ya kiongozi aliyepita? ni wazi kuna limitations, ni vema kiongozi akaja na mikakati ya kubadilisha hali hiyo na hasa anapoona kuwa 'si sawa'.

Pamoja na mambo mengi, siasa zote za nchi yeyote zisifike mahali masuala muhimu ya ustawi wa wananchi yakataifishwa kwa kisingizio cha kulinda madili ya viongozi, ni vema wakati hao viongozi walipoweka namna ya kudhibitiana basi hayakupaswa kutuathiri sisi wananchi wa kawaida ambao si sehemu yao.

Ninadiriki kusema kuwa Azimio la Arusha ndiyo chanzo cha kuona wanazuoni wetu wazuri tu wanaacha kazi zao nzuri na kukimbilia siasa kwani tayari walishajengwa mawazoni mwao kuwa kwenye siasa ndiyo kila kitu. Kila mtu anafikiria ubunge na si kufanya biashara kwani kila mtendaji mkuu katika mashirika ya serikali alipewa nyumba bure, usafiri wa kumwaga yeye na mkewe na watoto na mjomba na shangazi. Hakukuwa na ufuatiliji wa mtendaji huyo, sana sana akiharibu basi atahamishwa kwenda kuharibu pengine
 
Ajabu tena washabiki wa hii a prone to fail system wanavyojaribu kuiremba na majina ya ajabu when it failed completely.

Sio kwetu tu nchi zote duniani zilizo jaribu namna ya maisha yale yalizidi kuongeza umaskini kwa watu wake, system ambayo ai encourage innovation, sytem ambayo doesnt encourage rapid development.

Hila sisi sijui tuna matatizo gani tena tunapigia debe a system of failure, kwa mbwembwe na hili fail understrong leadership.

Kwa hiyo sasa hivi baada ya kuachana na system ile kuna mafanikio? Itakuwa vizuri ukiyaweka mafanikio tuliyoyapata baada ya kuachana na ile system iliyo fail. Na pia utueleze ni rapid development ipi tuliyoipata tangu tuachane na system ile.
 


Ninadiriki kusema kuwa Azimio la Arusha ndiyo chanzo cha kuona wanazuoni wetu wazuri tu wanaacha kazi zao nzuri na kukimbilia siasa kwani tayari walishajengwa mawazoni mwao kuwa kwenye siasa ndiyo kila kitu. Kila mtu anafikiria ubunge na si kufanya biashara kwani kila mtendaji mkuu katika mashirika ya serikali alipewa nyumba bure, usafiri wa kumwaga yeye na mkewe na watoto na mjomba na shangazi. Hakukuwa na ufuatiliji wa mtendaji huyo, sana sana akiharibu basi atahamishwa kwenda kuharibu pengine


Chukua Azimio la Arusha na utuoneshe kutoka humo ndani ni mambo yapi ambayo a. Hukubaliani nayo na b. Ungeyarekebisha na kwa vipi.
 
Hali ya uchumi alipoingia Alhaj ilikuwa mbaya kweli, lakini unapotaka kufanya chochote kuna vitu vya msingi , na vingine ni vile vinavyo imarisha vitu vya msingi, na niliwahi kuongea na mtu moja ambaye ni swahiba/rafiki/ndugu wa alhaj ambaye ni mtu wa system mpaka leo, yeye alilalamika rukhsa ya mwinyi ambayo haikuwa na taratibu, yaani mambo yanajiendea holela holela.

Sasa nikirudi kwenye suala la uchumi wakati Alhaji anaingia ndio ulikuwa na mapungufu yake na hata mwalimu alisema yeye hakuwa malaika au hakukosea, sasa nini kilicho takiwa kufanywa na Alhaji, ni kujaribu kuondoa au kupunguza mapungu yalio tokea huko nyuma, nayo ni ya management za haya mashirika ambayo yalikula taji na mapungufu mengine. madhali yalionekana na mimi na wewe ni wazi na yeye na viongozi wake waliyaona. sasa ni ilitakiwa kifanyike, moja ilitakiwa kufanyika semina elekezi kwa viongozi wa hayo mashirika na makatibu wakuu na mawaziri kuwaelezea nini kinachotarajiwa toka kwao na faida ya kusimamia vizuri mashirika yalio chini ya wizara zao, kubadili mfumo wa uteuzi wa Bodi members, na kuachana na kuweka rafiki/shemeji nk wa kwenda kukuleta pororo.

Kupunguza mzigo wa kiuongozi kwa serikali/raisi angeongeza nguvu kwa bunge kuwa-grill viongozi wa haya mashirika kuhusu matokeo ya biashara zao, na pale walipo hiyaji kuuza iwe nyumba nk wange fanya tathimi ya njia bora ya kutekeleza hiyo sera. na kwa kuwa tulikuwa tunaelekea kwenye soko huria iwe soko la mitaji nk , basi wange ya tayarisha vizuri haya mashirika kufika huko na hata kutuwekea watanzania wote mazingira mazuri ya kununua hizo shares panapo majaliwa, iwe ni kiongozi au mtanzania wa kawaida.

Lakini kilicho fanyika kipindi cha mzee ruksa ni mipango ya siku hadi siku, badala ya kuwa na mikakati ya muda mrefu.

Na kwa kuwa wewe naelewa unajua Management basi ni vizuri sisi sote tukajikita katika ile pyramid ya Management na aina ya mikakati ya kila moja.

Top Management 5 to 10 to 20 years
Middle management 1 year to 5 years
Operational level ni daily.

Lakini kilicho fanyika na Top management Yetu ( Baraza la Mawaziri ) ni kufanya Operational level decision, kwamba unauza shirika bila kujua baada ya hapo nini kitatokea, yaani hawakufanya Socio-economic impact assesment na ku-control hizo after effects za matokeo ya maamuzi yao, in short waliangalia maslahi binafsi zaidi kuliko ya nchi.

Hivyo ndio kosa la Mzee ruksa lilipo na litaendelea kutula mpaka atakapo tokea Dikteta moja akarekebisha hali.

August,

Unaonesha wewe ni academician zaidi ya hali halisi.

Wakati Mwinyi anakabidhiwa nchi kulikuwa na mashirika ya umma nadhani kama sikosei karibia 400. (naweza kurekebishwa). na mengi ya mashirika hayo yalikuwa yanategemea ruzuku ya serikali au kuchotewa toka benki za serikali kwa ajili ya kujiendesha. Wakati huo huo serikali inahitaji fedha za kuendesha shughuli zake kwa maana ya kuwatumikia wananchi, ambapo sehemu ya pesa hizo tumekuwa tukipatiwa na wafadhili kabla hata ya Mwinyi kuingia madarakani. Je, unadhani kulikuwa na muda kuyafanya hayo unayoyasema wakati huohuo wale ambao wanakupa msaada wanakuelekeza kuacha kumwaga pesa kwenye mashirika ambayo hayana tija badala yake hizo pesa zichangie katika bajeti yako?

Kumbuka masharti ya IMF na WB yalilenga katika kuboresha uchumi na kuifanya serikali ijitoe katika uendeshaji biashara na kuwaachia watu binafsi ili wajitegemee na kuwa mhimili wa kujenga uchumi. Mawazo yako ni mazuri lakini wazo la serikali kuendelea kufanya biashara hilo ninalikataa kabisa. Ninaunga mkono urejeshwaji wa shughuli za biashara kutoka serikalini na kwenda kwa watu binafsi.
 
Chukua Azimio la Arusha na utuoneshe kutoka humo ndani ni mambo yapi ambayo a. Hukubaliani nayo na b. Ungeyarekebisha na kwa vipi.

". . . The Arusha Declaration and the actions relating to public ownership which we took last week were all concerned with ensuring that we can build Socialism in our country. The nationalization and the taking of a controlling interest in many firms were a necessary part of our determination to organize our society in such a way that our efforts benefit all our people and that there is no exploitation of one man by another.'

a) Sikubaliani na serikali kumiliki njia kuu za uchumi kwani zinamuacha mwananchi asiweze kutumia uwezo wake katika kuweza kuzimiliki njia hizo kuu za uchumi. Matokeo yake serikali ilianzisha National Poultry Co. Ltd na nyinginezo ili ifuge kuku na badala ya kuwaachia wananchi wafanye biashara hiyo kwa ushindani zaidi.

b) Ningehakikisha kuwa serikali inajitoa katika kufanya biashara moja kwa moja na kuwaacha shughuli hizo zifanywe na wananchi ili wao ndiyo wawe ni mhimili wa kweli wa uchumi wa nchi hii. Ninatambua kuwa kujituma kw mtu mmoja mmoja ndiyo ndiyo njia nzuri ya kuifanya jamii izalishe na kutumia resources zake kwa mgawanyo unaotokana juhudi za uzalishaji.

Ningehakikisha kuwa mashirika yote ambayo ni mzigo kwa walipa kodi na hayachangiii katikapato la taifa ninayauza mara moja. Na yale mashirika mengine ambayo yanajimudu basi ningehakikisha yanabinafsishwa na wananchi wenye kupenda wananunua hisa humo. Ningehakikisha yale mashirika ambayo ni nyeti kama Reli, Bandari, Posta, Ndege na mengine machache kama hayo yanabinafsishwa na serikali inabakiza hisa chache kwa ajili ya interest ya watanzania wote.
 
Back
Top Bottom