Kaka point uliyoitoa ni kubwa na muhimu sana, ila ina matatizo mengi sana
Umsema ni declaration of certain prinples, just declaration? nothing else?
Azimio la Arusha ni azimio la shabaha tu, basi. Azimio hilo linatamka lengo la TANU kuwaongoza watu wa Tanzania, na linaweka shabaha ya zamendeleo. Tanzania haikuwa nchi ya Ujamaa ghafla siku ile ile ya tarehe tano Februari, au siku yoyote tokea hapo; wala kwa sababu hiyo tu Tanzania haijawa nchi yenye kujitegemea , au nchi iliyoendelea. Azimio la Arusha lisingeweza kufanya mambo hayo siku hiyo hiyo; wala isingewezekana, hata kama watu wangekuwa na ari, au nguvu kiasi gani, kutimiza shabaha hizo katika miezi michache hii tangu Azimio lipitishwe na TANU.
Azimio ndio mwanzo, siyo mwisho, wa safari ndefu sana ambayo bila ya shaka itakuwa na matatizo mengi. Ni muhimu kwetu kufahamu waziwazi mambo hayo, la sivyo tutashindwa kulifikia lengo lililotamkwa, na tunaweza kulitia Taifa letu hasara kubwa. Lazima tuelewe barabara Azimio la Arusha ni kitu gani, linasema nini, na maana yake nini, kwa sasa hivi na kwa siku zijazo.
Delaration za kutufanya waislamu na wakristo tunazisema kila siku na hatuzifuati! naweza nika declare kuwa mtanzania hili hali si mtanzania
Huwei kusem Chenge, Karamagi, RA, EL, na mafisadi wengine wengi ni watanzania wameisaliti nchi hii, na wengi watatokea , siamini kabisa kuwabana mafisadi tunaanza na declaration.
MKJJ najua unajua kuan watu leo hii wanatamani wangezaliwa ulaya, kuna watu wanatamani wassitwe watanzania , infact ndani ya Tz kuna watu hawajioni kama watanzania, declaration of these princples ni nzuri tena sana, ila,kama hakuna system ya kuwabana watu waishi sawa na walivyo declare ndiyo failure yenyewe!
Tutabaki Watanzania
Kwanza, Azimio la Arusha ni kukubali kwamba sisi ni Watanzania, na tunapenda kupata mendeleo kama Watanzania. Bila ya shaka tutapenda kubadili mambo yetu mengi katika nchi yetu. Lakini tumetamka kwamba mabadiliko hayo yatatokea jinsi tunavyokua kuelekea lengo fulani. Kukua huku lazima kutokane na mizizi yetu wenyewe, siyo kwa kujipachika katika shina na mizizi ya vitu vilivyo vigeni kwetu. Jambo hili ni muhimu sana, na maana yek ni kwamba hatuwezi kuchuku tu "msahafu' wa siasa za nchi nyingine, na kutimiza unavyosema pengine na mabadiliko kidogo, au pengine bila mabadiliko. Ndiyo kusema kwamba mabadiliko ya mambo yetu yatategemea haja zetu, kama tunavyoziona sisi, na yale yataelekea upande ambao sisi wenyewe tunaona unafaa kwa wakati huo. Tutapata nguvu kutoka katika maarifa ya binadamu wkwa jumla, na kutoka katika ujuzi wa watu wengine lakini mwanzo tunaanza na kuukubali kabisa Uafrika wetu, na imani kwamba kuna mambo yetu mengi ya zamani yatakayotufaa katika siku za mbele.
tuikosee na kulifanya AD lazima likubalike na wote, kuna watu ni madudu ni msonster hayana hata chembe ya huruma! hawa watu sheria tu ndiozo za kuwabana sio kwa declaration!
Kibaya zaidi hatutegemei wasio watanzania watusemee hizi declaration, CCM is failure waliyoyafanya nchii hii they dont qualify to be called Tanzanian! hivyo basi kila anayetaka AD we should find the other way not through CCM!!
Kuwa na uzalendo inatokea automatic, to love the land where I was born, siyo swala la kushawishiwa na mtu, kuwa nipende wazazi wangu waliponizaa, ni nitunze sehemu watakayoishi wajukuu zangu! nilinde mali asili ya vizazi vijavyo haihitaji AD!!
if we are not able to live with these common senses mpaka AD liseme then bado hajuaanza kuishi basi, Kutochagua kiongozi mzuri ni ishara ya utokuwa wazalendo na hii ni watanzania asilimia 98% hatuko serious kuchagua viongozi! tuna matatizo jamani!
When in the Course of human events it becomes necessary for one people to dissolve the political bands which have connected them with another and to assume among the powers of the earth, the separate and equal station to which the Laws of Nature and of Nature's God entitle them, a decent respect to the opinions of mankind requires that they should declare the causes which impel them to the separation.
ndiyo maana nasema tuna matatizo mengi basi ya kuyatatua kabla ya kuingia kwenye Azimio! it seems AD was supposed to be declared when all Tanzanian are equal in their senses!
Hivi Chenge si alikuwepo kipindi cha hayo azimio, ina maana Mwinyi alikuwa na uwezo wa kuwavua mpaka utanzania!!!!
That is exactly what I'm saying! Azimio la Arusha lilikuwa ni "Azimio" haikuwa Katiba au Sheria. Nyerere anaeleza hili katika Hotuba yake ya August 5, 1997 pale Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam (msisitizo wangu):
Kwa hiyo ndugu yangu AR ni kauli za shabaha, kauli za malengo.. ni sawa sawa na "roadmap" au "blueprint" ya jengo tunalotaka kujenga. Halikuwa jengo lenyewe na tulipoliandika hatukuwa na vifaa vyote vya kujenga jengo hilo! Hii ndio maana ya kuelewa "barabara".
Kutangaza na kuazimia ni vitu viwili tofauti. Mtu anaweza kutangaza kuwa "mimi ni Muislamu" lakini isimaanishe lolote na mwingine akasema "ameazimia kuwa muislamu" na tukamuona akianza kuswali, kuishika dini n.k Azimio la Arusha siyo Tangazo lisilo na maana; lilikuwa ni Azimio la kile tunachokitaka kama taifa na ni kutoka hapo ndipo tulianza kufuata kile tulichokiita "kujenga taifa" kwa misingi ya AR.
Hili ndilo Kosa.. na ninaamini hata hawa wanaotaka AR sasa hivi hawalijui. AR haina lengo la kuwabana kina Chenge na mafisadi no sir! AR ni ramani ya nyumba tunayotaka kuijenga, siyo silaha tupu ya kupigana na mafisadi. Tutakapoanza kurudi na kujenga Taifa kwa misingi ya AR utaona kuwa kumbe nyumbe yenyewe inawatosha watu wa namna gani, na miti gani itatakiwa kuondolewa na vigingi gani kufukuliwa ili tuijenge nyumba yetu. Sasa kama hilo itakuwa ni pamoja na kuwatia pingu kina Mkapa, na kumtimua madarakani JK na kundi lake au kuwabariki wote hao basi ni sehemu tu ya kujenga hiyo nyumba yetu.
Wapo wengi, nakutana nao kila siku, watu wanaonishangaa kwa mfano why I care so much abt Tanzania badala ya kuenjoy maisha ya Kimarekani.. wapo wanaoshangaa ninavyozungumza Kiswahilli utadhani nimetoka Tanga jana na wanakwazika ninapozungumza sentensi nyingi bila kuchangana na Kiingereza. Wanaona "naendekeza Bongo sana". Sasa ni watu walio duni wenye fikra hizo, watu ambao kwa mzungu ni kama Mungu wao wa aina fulani.
Sasa, AR tunapoliangaliia leo hii tuna bahati ya muda, usomi zaidi na kuelewa zaidi mambo ya kufanya vizuri kuliko wazee wetu in 1967. Kama vile Wamarekani wanavyoelewa zaidi katiba yao na Azimio lao la Uhuru leo hii kuliko in 1776. Hivyo, badala ya kulikana na kujaribu kulitupilia mbali kwa sababu ati wazee walishindwa ni jukuu letu kizazi chetu kukumbatia nyaraka hii muhimu kwa historia yetu na kuanza kutengeneza miundombinu yake ambayo italifanya lijikite na kuwa kweli kati yetu. Yawezekana kwa sehemu fulani halikufanikiwa sana kwa sababu kama tunavyoona leo hii uelewa wa watu wetu bado haujazama kulisoma na kulielewa. Na kitu kingine ni kuwa huwezi kulisoma AR peke yake ukaelewa kwa kina kwa mfano bila kusoma hotuba ya Nyerere niliyonukuu hapo juu miezi michache ikielezea AR ni nini hasa na lina lengo gani.
Angalia Nyerere anavyoelezea AR kwenye kifungu kinachoendelea hicho hapo juu:
tuendelee na hoja zako:
Bado hujaelewa, AR ni azimio la njia mpango, sheria na taratibu zilitakiwa zitokane na hilo. Azimio la Uhuru la Marekani haikuwa Sheria iliyowapa watu wote uhuru, lakini kutoka hapo Katiba ya Marekani ndiyo ikachota misingi ya fikra hizo. As a matter of fact, AR ingetakiwa iwe kabisa sehemu ya Katiba yetu na isomeke pamoja na Katiba yetu kwani huwezi kuielewa Katiba ya Marekani vizuri bila kuelewa AU la Marekani! The two go the proverbial "hand in hand". AR siyo Sheria lakini ilitakiwa kuwa ni msingi wa Sheria zetu ili ziweze kuendana nalo.
Oh no sir! AR siyo mali ya CCM! CCM hawana haki hata kidogo ya kujaribu kumonopolize. AR ni mali ya Watanzania wote. Ni Azimio letu sisi. Ni ukweli wa kihistoria kuwa lilipitishwa na kikao cha TANU lakini what other alternative was there!? KUngekuwa na vyama vingi halafu TANU peke yake ikapitisha basi tungesema ni la kwao lakini wakati ule TANU ndiyo ilikuwa jumuiya ya Watanzania wote. AR na nyaraka mbalimbali zilizotolewa wakati wa TANU peke yake na wakati wa Chama kimoja ni haki na mali za Watanzania wote! Ndio maana binafsi siwezi kuona aibu au kuomba kibali kumtumia Nyerere au AR kwani siyo mali ya wana CCM na nitamwona mpuuzi mwana CCM ambaye atasimama na kutuambia AR ni mali ya TANU na CCM!!
Of course not; lakini watu kutaka kujua wapi unasimamia haigombi kutangaza msimamo wako. Natumia mfano wa Azimio la Uhuru la Marekani kuelezea hili tena. Mfalme George VIII hakuhitaji kusoma Azimio la Marekani kujua kuwa koloni lake linataka kuasi; lakini kwa Wamarekani ilikuwa muhimu (na wameandika hivyo kwenye AU wao) kumjulisha mfalme kwanini wamneamua kujitangaza kuwa huru. AR kwa upande wake ilikuwa ni kauli ya pamoja ya nini Watanzania tunataka na tunataka kukipata vipi badala ya kuacha watu wakisie. Ndiyo maana AR lilitangulia hatua mbalimbali zilizofuata baadaye.
Hivyo, AR halimfanyi mtu kuwa mzalendo au kumpa mtu mapenzi bali linampa nafasi ya kuelezea kwa pamoja msingi wa uzalendo wake huo na mapenzi yake hayo. AR ni msimamo wa pamoja kama ilivyokuwa kwa Azimio la Wamarekani. Kwa pamoja tumechukua msimamo huo.
Unachokosea hapa ni kutokukubali kuwa kuna wakati watu lazima wachukue msimamo na kuelezea kwanini wamechukua msimamo huo. Hii haiondoi ukweli wa kile ambacho kila mmoja mmoja ameshakikubali. Wamarekani walisema hivi mwanzoni kabisa katika azimio lao la Uhuru:
Azimio la Arusha linafuata mtindo huo huo; linaelezea msimamo wetu kwa pamoja na linatangaza yale tunayoyataka kuyafanya kwa misingi ya "decent respect to the opinions of mankind".
In this case, I'll leave sarcasm at bay.
You are still missing the full understanding of What AR is..
- Wa-Tanzania tujifunze kulilia utawala unaoheshimu sheria, sio kuheshimu maadili ya anything else, isipokuwa sheria tu ya jamhuri, ama sivyo tutaendelea kubabaishana mpaka mwisho wa dunia. ooh ni Mwinyi, oooh sio blah! blah! Nchi zote zilizoendelea sasa hivi kuna one principle behind nayo ni heshima kwa utawala wa sheria!
Respect.
FMEs!
Asante kwa shule kaka, je tutawezaje kumfanya kila mtanzania alitekeleze hilo azimio?
- Wa-Tanzania tujifunze kulilia utawala unaoheshimu sheria, sio kuheshimu maadili ya anything else, isipokuwa sheria tu ya jamhuri, ama sivyo tutaendelea kubabaishana mpaka mwisho wa dunia. ooh ni Mwinyi, oooh sio blah! blah! Nchi zote zilizoendelea sasa hivi kuna one principle behind nayo ni heshima kwa utawala wa sheria!
Respect.
FMEs!
- Wa-Tanzania tujifunze kulilia utawala unaoheshimu sheria, sio kuheshimu maadili ya anything else, isipokuwa sheria tu ya jamhuri, ama sivyo tutaendelea kubabaishana mpaka mwisho wa dunia. ooh ni Mwinyi, oooh sio blah! blah! Nchi zote zilizoendelea sasa hivi kuna one principle behind nayo ni heshima kwa utawala wa sheria!
Respect.
FMEs!
sidhani kama suala ni "kumfanya"..Mtanzania kutekeleza; ni sawasawa na huwezi kumfanya kila Mmarekani kutekeleza Azimio la Uhuru wao. La maana ni kushawishi watu wapate uelewa sahihi wa Azimio na kutoka hapo wao wenyewe watambua ni jinsi gani watafanya kile ambacho AR linasema. Na kwa jamii kiujumla kufikiria ni njia gani zitumike kulifanya Azimio liende na wakati wa sasa kama vile AU la Marekani linavyokuwa adapted katika siku za miaka ya leo.
Hatari ninayoiona ni kuwa watu wanataka tuikane historia yetu kana kwamba were curved from nothing na kuwa Taifa letu liliundwa pasipo kanuni au principles fulani. Tanzania haiwi Tanzania kwa sababu tunasema ni nchi ya Tanzania; Tanzania ni Tanzania kwa sababu iliundwa kutokana na misingi fulani. Tunapoikana misingi hiyo tunaukana Utanzania wenyewe. Ndio maana mtu akiwambiwa ni "unamerican" ni kitu kibaya sana si kwamba anaambiwa si Mmarekani, bali ameacha principles zinazomfanya Mmarakeni kuwa Mmarekani na uraia peke yake siyo principle hiyo. Ni kanuni enshrined in the Declaration of Independence and duly promulgated in the Constitution.
Mzee unalolisema ni zuri kweli lakini ni sheria hazitoki hewani tu; sheria hivi hivi haziundwi bila ya msingi. Mtu anaweza kuja na sheria yake na akasema tuifuate, tutafanya makosa kufuata sheria ambayo haina msingi.
Wazo huzaa Fikra
Fikra huzaa Sera
Sera huzaa Sheria
Sheria hutengeneza mfumo!
Azimio la Arusha ni Wazo!
Mzee unalolisema ni zuri kweli lakini ni sheria hazitoki hewani tu; sheria hivi hivi haziundwi bila ya msingi. Mtu anaweza kuja na sheria yake na akasema tuifuate, tutafanya makosa kufuata sheria ambayo haina msingi.
Wazo huzaa Fikra
Fikra huzaa Sera
Sera huzaa Sheria
Sheria hutengeneza mfumo!
Azimio la Arusha ni Wazo!
Utawala wa sheria utaheshimiweje wakati sheria zenyewe zimewekwa kwa maslahi fulani,most of them ziko very biased.
You are very right: nani anatengeneza sheria na katiba? si ni sisi wenyewe kupitia wawakilishi wetu? at least laws na katiba tuna sema ni watanzania wote wamehusika kujiwekea sheria zitakazowaongoza. Kama leo hii sheria na katiba zina mapungufu, basi ndiyo pa kuanzia kuzirekebisha. sio kuwaza AD wakati ni wazo, hata kama leo kila mtanzania akalikubali, still wako watakaofanya makosa na hatutawafanya lolote lile kwa hizo sheria.
Mkapa kufanya biashara ikulu, si tatizo la AD, tuna weakness katika mifumo na sheria zetu, swala la kuwa rais apunguziwe madaraka halihitaji AD linahitaji kukaa chini.
Vitu vingi kwenye AD ni very common sense na ari ambayo we can move on without AD, na still tukawa binadamu na watanzania. sheria na katiba ndio tuvililie sasa!
Nakubaliana na wewe kwa kiwango kikubwa tu...Tatizo langu tunaambiwa tuheshimu sheria bila kufundishwa umuhimu wa kuwa na tabia njema,tunaambiwa tuitii katiba wakati hata hatujiu umuhimu wake wa kuiheshimu...Ni bora tukafundishwa au tukalelewa kuwa na maadili mema kuliko kuzingatia masheria ambayo mengi yao kama nilivyosema awali hayana lolote..Manners are of more importance than laws..To me maadili ni bora kuliko masheria yenu..Eti tunaweka sheria za kudihbiti rushwa wakati wa uchaguzi wakati watanzania walio wengi wanalia njaa kali,Ni wao wenyewe (wapiga kura)wanaotaka haya..Asiye na pesa ni ngumu kupita..watanzania wengi hatuna maadili kabisa ikizingatiwa kuwa hata viongozi wetu wenyewe hopeless kabisa..Rais kufanya biashara Ikulu....and so on.
Wabz,
MMJ kanisaidi akukujibu nami nitaongeza yafuatayo.
Mara nyingine, wazo na imani inapoanza kukolea, wale ambao si waumini au wasioamini hufikia mahali wakalazimishwa kuamini. Natumia mfano huu kwa kutumia dini zetu mbili kuu za ukristo na uislamu na hata mfumo wa Ukomunisti na Ubepari.
Aliyepinga Ubepari alinyanyaswa, alityengwa na alilazimnishwa kuwa Bepari au alionekana ni adui (Hoover na McCarthy)! Kule Urusi na China walioukataa Ukomunisti walipelekwa Gukags.
Kwenye Ukristo na uislamu kulikuwa na Crudase na watu walichinjwa na kupoteza maisha kama si kutawanywa.
HIyo ni kukuonyesha kuwa kamwe hapawezi kuwa na uwiano au uhiari wa Wazo au Imani kukubalika kwa wingi mmoja wa Asilimia 100.
Ndivyo basi hata kwa Azimio la Arusha itabidi ushawishi ufanyike kwa namna hiyo. Lakini si lazima tutoe damu mtu, bali ni kwa kufanya matendo ya uchapakazi na mfano ambayo yataigwa na kusisimua na kuleta ushawishi kwa kin aTomaso.
Lakini hatutakosa kina Yuda, wasaliti....hao kina Chenge, Rostam, Lowassa na wengine wao ndio Mayuda wetu. Wanarubunika kwa tamaa binafsi na kusahau kuwa wote tunanafasi sawa na kinachotakikana ni kutengeneza mazingira mazuri.
Naomba niongelee hii dhana ya kusema Azimio lilileta vijiji vya Ujamaa, hakuna sehemu hata moja katika Azimio iliyosema kutakuwepo na vijiji vya ujamaa. Vijiji vya Ujamaa vilikuwa ni Sera ya Serikali, ilikuwa ni tamko la Serikali na si Azimio la Arusha. Sawa na kutaifisha, Azimio lilisema Wananchi wamiliki njia kuu za Uchumi, Serikali ikaunda sheria na kufuta umiliki binafsi.
Hivyo kwa mkao mwingine, Azimio ambalo lilitokana na wazo, njozi, dhana na dhamira, lilianza kutekelezwakama Sheria kwa maamuzi yaliyofanywa na Serikali. Je ni kwa nini h=basi Serikali hiyohiyo haikuendelza utekelezaji sahihi au kwa kutumia mbinu bora na sahihi kwa kwenda hatua kwa hatua kuhakikisha tunajisahisha?
Ndipo Uanadamu unapochukua sura na ndipo ambako sasas tunalilia Azimio tukiamini eti Azimio litaletaSheria au Miiko. hiyo ni dhana potofu. Azimio linachofanya ni kutupa ramani ya kujitambua kuwa kama tunataka kujenga nyumba yetu iliyo imara, basi tunahitaji Watu, ardhi siaisa safi na uongozi bora. Azimio linasema ili nyumba ijengeke, tunahitaji juhudi na maarifa na uzao wa sisi kukamilisha ujenzi wa nyumba hii ni kujihakikishia Usalama wetu na Uhuru wetu na zaidi ni kujikinga na unyonge ambao unaweza kutuletea Ujinga, Umasikini na maradhi.
Ni uchaguzi wetu na ndio ni hiari kama tunataka kujenga hii nyumba na kufuata kanuni tulizoziandika ili uimara wake upatikanne. Kama Mzee Mag3 alivyosema, pale Mnazi Mmoja sikju ile mwakak 1967 alivyoshuhudia na Jasusiakiwa jirani, ni wengi walishawishika na kuikubali hamasa na azma ya kujijengea nyumba mpya bila kutegemea kujengewa na mtu mwingine. Lakini katika mkusanyiko huo, kulikuwa na waliokuwa na mawazo yao tofauti na kutokana na udogo wao wa kitarakimu, wakaamua kutumia mbinu zingine kujijenga na kutangaza vita.
Mwaka 1992 pale Zanzibar, kundi hili lililokuwa dhaifu ki-kauli siku ile pale Mnazi Mmoja, kundi hili likajipatia dhamana na mamlaka ya kuwa na sauti ya juu na ya mwisho na wao wakamuru kuvunjwa kwa ujenzi wa nyumba ambayo walishaanza kuihujumu tangu tulipokuwa tukiijenga. Ndio mchwa ambao Mzee mwinyi anawasema huku akijisahau kuwa yeye ndiye aliyekuwa Mfalme wa Mchwa!
Asanre tena, umezungumzia dhana ya ushawishi ambayo ndiyo tuliyoisema tangu hapo awali. Ninaamini kama watu wangelipokea azimio kwa moyo wote na kuwaingia damuni, basi tawala zilizofuata siyo tu zingeonyesha viongozi wenye kufuata AD bali hata wananchi pia. Naona watu wengi kutolifuata kwa vitendo, ila kufanya assumptions za kuwa ni waumini wa AD.
Katika ushawishi huu ndugu yangu MKJJ bado utakutana na watu wasiotaka ngonjera, watu walio greedy , wasiojali kuwa kuwa na ''title ya utanzania au mtanzania ni amana au heshima kwao'' hao wapo na wataendelea kuwepo! and they dont care, tena wako ukisema wewe sio mtanzania ndiyo umewapa sifa!!
Mwisho, je kuna kura, kikao, au namna yoyote iliyoonyesha azimio lilikubaliwa na watu wengi hata kama si wote?
kuna watu walihamishwa kwa nguvu kuanzisha vijiji vya ujamaa , are they still proud kujiita watanzania?
they were happy inspite tha fact kuna watu walikufa?
Hivi mimi nikiwa mtanzania leo hii baada ya kushawishiwa na AD, na nikazijua value zangu za kitanzania, na kuringia utanzania wangu, je wakija watu wengine wanawaweza kunipoka kirahisi utanzania wangu?
mbona leo hii hatuoni watanzania wanaoliabudu au kulitekeleza AD kwa vitendo?
na hasa nyie mliokuwepo kipindi hicho, are they not Tanzanian anymore? au uasili wao wa-kitanzania kwa mujibu wa AD unaondoka saa ile unapolikana Azimio?
!au ili uwe mtanzania unayefuata AD lazima viongozi wawaongoze? na kwa maana nyingine viongozi wa Tanzania wana uwezo wa kuuondoa utanzania wa mtu , kama hawatekelezi AD au wana uwezo kutunza utanzania wa watu kama wanafuata AD
Ni nani mtanzania leo hii anayesema anatekeleza kwa vitendo AD japo hata kama viongozi mnasema wameliua? kama haiwekani kutekeleza AD bila serikali in place then it was failed!
Asante kama lilikuwa wazo, nufurahi kwa wewe mwanafunzi wa Nyerere kusema hili. However, wazo linaweza kukataliwa au sio? why is it kuwa kuna watu wanalazimisha hili wazo liwe mfumo? wakati halijapita kwenye ngazi ya sera na sheria? na tufanyeje lifikie hizo ngazi tatu kabla ya kuwa mfumo.
AD was there, it is an history kuna watu wanafanya makosa kusema turudi huko,
Hili unalolisema ni kweli. Leo hii nikiangalia naweza kusema kuwa ukiondoa Mwalimu mwenyewe sijaona bado mtetezi wa kweli wa Azimio la Arusha. Azimio la Arusha linahitaji intellectual preparation ya kulielewa. Huwezi kuelewa AR bila ya kuelewa falsafa iliyosababisha uwepo wa Azimio hilo.
Matokeo yake ni kuwa wale waliokuwa wameitwa kulitekeleza walilijongelea kana kwamba ni sheria! Mara zote nataka uliangalie AR kama AU la Marekani. Vyote viwili pekee vinabakia kuwa ni Ideal.. ni mpaka pale unapoviangalia kwa mwanga wa rational thought na kuapproach them with certain moral focus hutaweza kulisimamia. Ndio maana Nyerere alipoliangalia AR miaka mingi baadaye hakuona makosa (ukiondoa ya lugha mbalimbali); ni sawasawa kabisa na Mmarekani akiangalia Azimio la Uhuru miaka karibu 300 na zaidi baadaye anauona ukweli wake!
Sasa, nitakuwa si mkweli kama nitajenga hoja kuwa katika ushawishi utaweza kuwashawishi watu wote. Katika mapambano na kushawishi watu huitaji kushawishi wengi; unahitaji kushawishi wachache ambao wanaamini kile unachosimamia na wako tayarri kukitetea. Ukiangalia sana, Nyerere alifanikiwa labda kuwashawishi si zaidi ya watu 10 katika uongozi wa juu wa taifa lake juu ya AR mmojawapo ni Mzee Kawawa na uongozi wa awali wa JWTZ na JKT. Hawa walikuwa tayari kulitekeleza AR kwa vitendo.
Lakini hata leo hii tunaona ilivyoshida kwa kiongozi anayekubalika kuweza kushawishi watu wake na hasa viongozi wenzake. Tunaona jinsi Barack anavyohangaika na suala moja tu la Sheria mpya ya Afya ya Marekani. Pamoja na ujiko wake wote na mbiu ya "Change" si rahisi kuwaingiza wote kwenye meli hiyo. Imembidi hata afunge safari kwenda kwani kina Kucinic kuwashawishi na kupata kura zao.
kuna kura iliyoonesha Azimio la Uhuru la Marekani lilipigiwa kura na kukubaliwa na watu wengi? Ukweli na uzuri wa hoja za azimio haitegemei wingi wa kura. Lakini, kama kukubaliwa lilikubaliwa, inabidi urudi 1967 uone jinsi Watanzania kwa maelefu yao walivyoandamana nchi nzima kuliunga mkono Azimio! Kama ni kura ilipigwa ya ndiyo!! Ukitaka kuuliza waulize kina Seith Benjamin ambao leo hii wanabakia kama mfano wa vijana waliokuwa tayari kutoa maisha yao kusimamia. Wale walikuwa ni mashahidi wa mwanzo wa Azimio, leo hii tumeanza kuinuka mashahidi wa mwisho wa Azimio!
Azimio was more than kuhamisha vijijini kwa nguvu. Sijui kama unajua historia of "how the west was conquered" hapa Marekani. Jinsi gani sehemu kama California na kwingine zilivyoingizwa katika himaya ya Marekani. Unafikiri watu wa huko wako proud kuwa Wamarekani? i bet you they are! Lakini wakane historia yao? absolutely not!
Kufa ni sehemu ya mabadiliko na maendeleo. HIvi unajua daraja la San Fransisco lilivyojengwa ni watu wangapi walikufa? Leo hii nilishatoa changamoto hapa mtu aniambie ni watu wangapi walikufa wakati wa operesheni ya vijiji vya ujamaa na watu hao familia zao ni zipi na makaburi yao yako wapi!? Kwa muda mrefu propaganda ya uongo imekuwa ikienezwa kuwa "maelfu" ya watu walikufa na hakuna mtu hata mmoja mwenye ushahidi wa kisayansi wa hao "maelfu" waliokufa ambao wasingekufa katika mazingira waliyokuwepo.
Yaani, kwa mfano watu kule Tunduru walisogezwa kuwa karibu karibu, wakati huo huo wengine wakafa kwa kuliwa na simba, lakini je katika miji yao waliyokuwa wamekaa peke yao tuna uhakika gani kanma hao Simba wasingewatafuna bado?
Hakuna ushahidi wowote wa maelefu ya watu kufa kwa sababu ya villagelization.. kama upo uwekeni wazi! Kama kuna watu walikufa walikuwa kama sehemu ya gharama ya mabadiliko. Thats how the world has been made. Kuanzia Marekani, Japani, na Uchina watu wamekufa kwa bahati mbaya kutokana na utekelezaji wa sera mbalimbali.
Utanzania hauwezo kuporwa na mtu mwingine. Lakini Mtanzania (raia) anaweza kuwa na sera ambazo ni kinyuma na Tanzania kama vile wapo raia wa Marekani ambao wanasimama kinyume na taifa lao na hata kujaribu kulitakia mabaya.
Hujasikia tunalalamika na maziko ya AR; bahati mbaya hawakulifukia vizuri!
Utanzania siyo Uraia tu, ni pamoja na kanuni za msingi zinazomfanya Mtanzania kuwa Mtanzania. Mmarekani ni Mmarekani kwa Uraia lakini Umarekani ni falsafa inayotokana na maisha yanayojenga Umarekani. Umarekani ni pamoja kukumbatia misingi iiliyounda taifa la Marekani. Tanzania vivyo hivyo, huwezi kuwa na Utanzania (sizungumzii uraia) bila kukumbatia misingi ya Utanzania huo. Mtanzania anaweza asiwe na Utanzania (faslafa ya maisha) japo ana uraia wa Tanzania!
!
Kama viongozi hawasimamii misingi iliyoliunda Taifa letu wanapoteza Utanzania wao (siyo uraia). Utanzania ni pamoja kushikilia imani zile za Azimiio la Arusha na pamoja na mambo mengine kadhaa.
Si ndio maana tunataka kulifufua? Idea haifi! Believe me.. you can not kill an idea.. thats why leo hii tunazungumzia AR wakati in the middle 90s na hata mwanzoni mwa 2000s tulikuwa na aibu. Leo hii watu wanalisoma AR na kuanza kuona how far we have drifted from our founding principles as a nation!
Wazo linaweza kukataliwa hata kupingwa; lakini ili likataliwe ni lazima likataliwe na wazo bora zaidi na lenye ukweli zaidi. Kukataa wazo kwa sababu hulipendi hakufanyi wazo hilo kuwa baya. Leo hii kipo kizazi ambacho kinataka kupush kule.. we are trying to create a new synthesis of AD.. a synthesis which is based on intellectual argument, rational reasoning and a need to accept truth as it stares at us waiting for our assent.
Ukijenga nyumba na kila ukijaribu kuweka dirisha na mlango unaona havikai sawasawa utakuwa hamnazo kama utaenda kwa waganga kutafuta au utalazimisha "liwalo na liwe". Utakuwa mwenye hekima kama utaamua kuangalia ramani ya mchoro wa nyumba kuona kama vipimo na vinginevyo unavyofanya vinakubaliana nalo.
AR ni road map ambayo leo hiit unataka tuiangalie; it is one of the founding documents of our nations. We have to proudly go back and have a second look and ask ourselves where we went wrong. As a matter of fact we know where and when we went wrong!!!
Waberoya... umelisoma Azimio lote la Arusha?
Received, supported and ready for action see my previous post and comment accordingly.Though my stands is, we need to modify some issues, and we need few people as you have pointed out and from there we need to spread the good news, we should never wait for Kkiwete, we all need to take this as our burden,!