Nilikuwapo ndugu yangu, ni siku ambayo ni vigumu kuisahau kama ulikuwapo lakini rahisi kuikebehi kama ulikuwa hujazaliwa. Hamasa, mwamko na mtumaini ya Watanzania na hasa vijana wakati huo yaliweza kuutikisa ulimwengu. Nakumbuka heshima aliyopewa Mtanzania nje ya mipaka yetu kwa aliyebahatika kusafiri wakati huo, ni kubwa. Hofu ilitanda si kwa majirani tu bali hata kwa mashirika ya kitaifa - kote walijiuliza itakuwaje hii kitu ikifaulu. Hapana, hali hii isiruhusiwe katu na vibaraka wakapatikana humu humu nchini na wakatumiwa ipasavyo kuihujumu.
Kama kuna watu wananipa kichefu chefu, ni huyu Mwinyi. Angekuwa mtu makini siku alipoombwa kugombea Uraisi angeweza kabisa akasema, thanks but no thanks, hivi viatu siviwezi - siwezi kuvuka huu mto kwani sijui kuogelea. Lakini Mwinyi being what he is, akatumbukia majini akiikokota nchi ya heshima - matokeo yake sasa tunayaona na kuyashuhudia. Okay, kabla yake tuliitwa masikini, sawa tulikubali na kukataa kuburuzwa, naam si masikini jeuri ? Na sasa tuko wapi ? Wezi wa kutupwa na tunamwibia nani ? Sisi, watoto wetu na wajukuu zetu. Mwinyi akae kimya, period.
Mzee Mag3, naomba unisaidie hasa sisi tulikokuwa hatupo kipindi hicho; maswali yangu siyaamini sana
1. Mlikuwa wavivu na hamkujua kufanya kazi mpaka mlipoambiwa muache uvivu ndiyo mfanye kazi?
2. AD lilikuwa na nguvu gani kisheria?
3. Je ipi bora kuweka systems zitakazowafanya watu wafanye kazi, au kuongea kuwa watu wafanye kazi?
4. Je ukiwa kaka kijana wa wakati huo na umeona hali ya sasa unasemaje? je watu hawajitegemei siku hizi kwa sababu hawana azimio?
5. Unaweza kurodhoseha mafanikio ya Nyerere mpaka Mwinyi anachukua nchi? na unaweza kusupport kuwa
hili tatizo ambalo halikuwepo kipindi cha Nyerere na
hili limetokea baada ya Mwinyi?
6. Azimio la Arusha lilikuwa ni siasa ya mlioamua wote au Nyerere tu na wengine 'mkasema zidumu fikra' zako? na kama ni moto uliokuwa kwa wote iweje Azimio lilikufa suddenly baada JKN kutoka madarakani? je si alama ya kuwa halikupokelewa na wengi? ni kama mtu anahubiri kanisani watu waache dhambi na akitoka hapo ni jukumu la kila mmoja kuamini au kukataa!
Mzee Mag3, kinachoendela hapa si kuwa watu hawajasoma azimio la arusha, wala kumtetea mwinyi, Ni kweli hakuna kingozi aliyeweza kuvaa viatu vya Nyerere, lakini kwa mantiki ipi?
1. Kupiga kura ya ndiyo na hapana?
2. Kusema zidumu fikra zako?
3. Kuwa non approachable?
4. Kutokuwa na demokrasia
5. Kupinga watu fulani wanaoleta mawazo ya maendeleo, typical example akiwa Mtei?
Au unasema kuvaa viatu vya Nyerere kama
1. Kupenda watu
2. Kupenda taifa lake
3. Kujitoa?
Yupi ambaye unafikiri angeweza kuvivaa viatu vya mwalimu?
Mimi naona sio kutokuvaa au kuvaa naona results ya mfumo wa kijamaa ambayo haukufanya watu wawe free kuwaza, kusema , kukosoa n.k ni athari mpaka leo hii
Ninaposema hayo msikosee na kusema namdharau MWALIMU hapana-he is a person who inspired me to think like him! but I amnnot to forcing people to agree with me! ni katika uwazi huu tutajua alikosea wapi na sisi tufanye nini!
Mag3 leo unaishi, unafanya kazi na watoto wako wanafanya kazi. ulishawahi kutangaza azimio la nyumbani kuwa kila mtu sasa afanye kazi??
AD was meant for UNITY, kuamsha ARI, kuleta UMOJA, kufanya mapinduzi ya KUJITEGEMEA kama taifa; lakini
1. Haukuwa msahafu!
2. Ilikuwa ni Imani ambayo mtu ana hiyari kupokea au kukataa!
3. Haikuwa system itakayomlazimisha kila mtu kuifuata!
Ili binadamu wanyoke na ku-obey Na wote kuwekana sawa lazima
1. weka/fuata katiba
2. weka/fuata sheria
3. weka system zitakazowalazimisha watu wazifuate !
Failure ya leo siyo kwa sababu ya AD, ni matatizo yetu makubwa sana; nimesema kama leo hii wakatokea watu na kusema AD is the only way, then inabidi tuwe na azimio lingine kabla ya Arusha! AZIMIO LA WATU BADILIKA NA KUFUATA SHERIA NA KATIBA
sijasema content za AZIMIO na hasa ujamaa wenyewe, uliotudumaza mpake leo hii!
Kaja Mkapa, Kaja Kikwete, matatizo mnataka mumtupie Mwinyi, then kuna wengine watamtupia Nyerere!
Lowassa, RA, Karamagi,Chenge, Balali, ... wote hawa wanasubiri azimio litangazwe ndio tuwapeleke jela!
Au mimi niliyezaliwa baada ya azimio nikiingia serikalini niibe, mkinikamata nijitetee kuwa Azimio halipo, it is not documented anywere that I should not steal!
wakubwa mtusaidie otherwise maswali haya hayakwepeki hata siku moja!
Yaani kwa watanzania ili viongozi wao waache wizi tangaza azimio la arusha au kigoma! au wapeleke Ngurdoto kwenye semina ya uongozi!!
We have problems, tatizo si kuwa au kutokuwa na azimio la arusha, tusipopata kiini cha tatizo letu then tutablame kila mtu dunia hii, we are living today, JKN alishapita na mchango wake tumeuona tunampa marks were he did right na mkasi where he didi wrong, si alikuwa binadamu?
Tusichanganye imani/beliefs na mambo ya kitaifa!
By the way, waafrika wote na matatizo yao walikuwa hawana maazimio!