Waberoya
Platinum Member
- Aug 3, 2008
- 15,169
- 10,785
Waberora,
Azimio la Arusha liliweka miiko. Ila kwa vipi lilikataza kuiba, hicho kitu hakipo duniani.
Hata leo Tanzania ukiuwa unaweza kunyongwa kikatiba, ila hiyo sheria haizuii watu kuuwa. Sasa unaponiuliza hilo, sijui uma maana gani. Isije kuwa yale ya kuuliza pua iko wapi wakati mdomo unauona.
Sasa hivi hiyo miiko tu haipo. Sasa hata Yona na Mramba kuwashitaki na kushinda ili jamaa waende jela hicho kitu hakipo. Walau zamani mtu anaweza kushtakiwa na akafungwa au kufukuzwa kazi. Lowassa pamoja na kuvunja miiko, bado WALIMUOMBA aangalie kipi cha maana akifanye. Yes, aangalie na si ashtakiwe na kufukuzwa kazi na mwisho kufungwa. Hii ndiyo hali mbaya ya vacuum iliyotokea baada ya kuvunjwa kwa AD.
Kukaa chini na kuangalia tabia zenu hilo ni kupoteza muda. tabia zetu pote duniani ziko sawa kabisa. Ila wenzetu wanafuatilia sana sheria. Kama JKN angelifahamu hili na kujenga kitu kama FBI, CIA na Sherrif/POLISI basi ninaimani leo hii watu kama Rostam Azzi, Lowassa na akina Mramba wangelikuwa wafanyakazi bora wa Tanzania huku wakiiletea Tanzania faida kubwa. Siwezi kushangaa kuwa hawa watu walikuwa na moyo sana ila wakakatizwa tamaa na wale wengine wa zamani. Kama Kikwete aliona wanavyoiba wengine, leo hii kawa juu unafikiri yeye ataacha? Ila kuna chombo chochote kinafanya ULINZI na USALAMA wa rasilimali zetu?
Haijalishi AD au katiba au chochote kile wewe utakaa na kusema tukifanye. Tanzania inabidi tuwe na chombo cha kuwalinda viongozi. Wabunge tumeshaona haliwezekani. Kama tukiwa na FBI yetu na hawa jamaa hawafanyi mchezo (kumfunga paka kengele) basi mchezo utakuwa umeisha. Miiko iwepo na chombo maalumu kisimamie. Huu ndiyo mzizi wa fitina.
Kama kuna kiongozi hafai, basi sidhani kama atakwenda juu. Leo hii tunasikia Mrema wa TANROAD kaajiliwa kwa mlango wa nyuma. Boss mpya wa NHC kaajiriwa kwa mlango wa nyuma. Pesa kibao zimetumia kumchagua CEO na watu wanakuja kuajiri kivyao na hakuna kitu kinatokea kwa hawa Mawaziri. Sasa unategemea huyu boss wa NHC atakuwa kweli makini? Kwanza ataambiwa achote pesa aipe CCM na hatapinga kwani wamemuajiri kwa kutumia penseli. Wanamtisha kuwa ukileta ya kuleta, form one utafutwa.
Asante Sikonge naona sasa umekuja mahali pazuri kabisa, Ikiwa leo hii sikonge tuitaitisha Azzimio la Arusha na kulipa nguvu ya kisheria badala ya maneno, nitakuwa wa kwanza kuandamana toka kwetu kijijini mpaka Arusha! Ikiwa leo hii tunasema vongozi hawana hofu ya woga kwani hakuna chombo cha kuwamonitor basi jibu lake ni kuwa hatuna dira, hatuna viongozi, hatuna taifa, AD can be in effective only kama litakuwa na nguvu za kisheria na watu mahususi wa kulitekeleza, offcourse TAKUKURU ingekuwa hivyo , lakini wote walewale,
Yes, lianzishwe na wananchi, liwe na nguvu ya wananchi, lwe na nguvu ya kisheria, liweze kuamua na kutekeleza wanayoyaona wao sawa , kama vile kukamata mafisadi n.k Japo tatizo kubwa tena itakuwa katiba , kuwa madaraka ya rais inabidi yapunguzwe.
Please lisiwe maneno wala kulazimishana, wala kuhubiriana kma dini vile! tukifanya hivyo tunakosea!
Mkuu Waberoya, I wish I had the time lakini hata hivyo nitatafuta muda nitoe majibu kwa kiasi ninachoweza. Bahati mbaya najaribu kufanya shughuli nyingi kwa wakati moja ingawa napitia humu kila nikipata muda mfupi.
Hata hivyo kabla sijaanza naomba tuelewane kitu kimoja. Kwanza, pamoja na kuwa kijana wakati huo, sikuwahi kujiunga na TANU hata siku moja wala sikuwahi kukipigia kura TANU (au CCM) hata siku moja. Sababu kubwa ni kuwa toka nikiwa shuleni sikuamini katika demokrasia ya chama kimoja na hata shuleni nilishiriki sana katika mijadalo kama ilivyoitwa "debate" wakati huo. Pili, sikuwahi kufanya kazi serikalini kama civil servant, kwani toka nimalize shule nilifanya kazi nje ya nchi kwenye makampuni mbalimbali - kazi nilizozitafuta mwenyewe.
Lakini pamoja na yote niliheshimu msimamo ulioonyeshwa na uongozi wa wakati huo. Nchi iliheshimika kwa kuwa na vision ya kitaifa na kuwa na kiongozi aliyekuwa tayari kuitetea kwa nguvu za hoja. Nilichoweza kugundua mapema kabisa ni kuwa ingawa wananchi wa kawaida wengi walimpa support, wako ambao mchana walihubiri maji lakini usiku walikunywa mvinyo. Mkuu Waberoya, nikipata nafasi tena nitapitia hoja zako moja baada ya nyingine kama ulivyozitoa ila tu naomba uelewe ni katika misingi niliyoyaelezea hapo juu.
Mzee Mag3 nimekuelewa asante kwa kuwa na misimamo, na kujitoa kunielimisha,
Caliber ya JKN ya kujitoa na kupenda watu that is the character that I will always adore him for, lakini madhaifu mengine tutayasema bila woga! na bila kuonyesha dharau , ni kujadili kwa sababu tuko huru na tuendako safari ni ndefu, naweza kuwa rais kesho ebo! nataka kujifunza na kukosoa.
Nimefurahi Mag kusema haukupenda chama kimoja, wengi wapenzi wa Nyerere ni washabiki na wapenzi! wana jukumu kubwa la kuwa wawazi!
Mtu mmoja alisema, nihubirie madhaifu yako, nihubirie wapi ulikwama na ukafanyaje kujikwamua, niambie wapi umeshindwa na unafikiri kwa nini ili na mimi niwe mwangalifu, niambie wapi niwe makini! Nyerere alikuwa mzuri yet alikuwa mwanadamu, kujua udhaifu wake ni mwanzo wa sisi kujifunza pa kukanyaga, kama na kama tu tutakuwa watu wa kufanya na sio kusema tunafuata AD ili hali vitendo haviko hivyo! AD ni dini kwangu mimi, ni hamasa kama vile jeshini nothing else
Kama utajibu jaribu pia kuweka faida za Ujamaa