Sikulifuta Azimio la Arusha - Mwinyi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sikulifuta Azimio la Arusha - Mwinyi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Synthesizer, Mar 19, 2010.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, amesema Azimio la Arusha halijafutwa kama watu wengi wanavyodhani. Mwinyi alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa Benki ya Biashara ya Ukombozi, inayomilikiwa na Kanisa Katoliki.

  ***

  Ujumbe kwa Mwinyi:

  Ningependa kukumkumbusha Mheshimiwa Mwinyi kile alichosema Mwal. Nyerere baada ya Azimia la Zanzibar, kwamba "Wale wenye akili tukatambua Azimio la Arusha limeshafutwa".

  Basi Mheshimiwa Mwinyi, kumbuka unapotoa kauli sizizo na msingi kama hiyo hapo juu wapo watu na akili zao wanaokusikiliza, kama alivyosema Mwalimu Nyerere. Kama huna cha kuongea afadhali ukae kimya na kufurahia pension yako. Kuna mengi uliburuzwa kufanya na wenye pesa, ambayo ni bora kwetu tukayasahau na kuganga yaliyopo, kwa sababu kama kuna kiongozi aliyetengeneza msingi wa ufisadi Tanzania basi ni wewe Mwinyi.

  Uliharibu misingi ya Azimio la Arusha kufikia hatua watu kuona elimu haina maana tena, bali kuwa mfanya biashara fisadi na wa tenda hewa. Uliua heshima yote ya kuwa mfanyakazi wa serikali na mashirika yake na kufanya wafanyabisahara, hasa wahindi, waonekane watu bora sana nchini. Ukaua heshima ya Ikulu, ya ofisi za Wizara, ya mamlaka za vyombo vya serikali, ukakuza mamlaka na utu wa pesa, tofauti kabisa na misingi ya Azimio la Arusha.

  Ukatudanganyia "economy liberalization" wakati hasa policy yako ilikuwa "ufisadi liberalization".

  Leo hii unathubutu kusema hukuua Azimio la Arusha!!! Hiki ni kichefuchefu kibaya zaidi ya cha mimba changa.

  Mwinyi huna la kutuambia Watanzania, na tunakustahi sana, huenda usivyostahili.

  =====================
  KWA WASIOJUA, HII NDIYO HOTUBA YA MWINYI MWAKA 1991.

  MAAMUZI YA ZANZIBAR, 1991
  HOTUBA YA MWENYEKITI WA CCM, RAIS ALI HASSAN MWINYI WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAZEE WA CHAMA, VIONGOZI WA TAIFA, MASHIRIKA YA UMMA NA WATU BINAFSI JUU YA UFAFANUZI WA MAAMUZI YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA KATIKA KIKAO CHAKE CHA ZANZIBAR: DIAMOND JUBILEE DAR ES SALAAM, TAREHE 25/2/1991


  Ndugu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Mkoa wa Dar es Salaam,
  Ndugu Katibu Mkuu,
  Ndugu Mwenyekiti wa Wazee wa Dar es Salaam,
  Ndugu Viongozi wa Chama na Serikali na
  Ndugu zetu waalikwa,

  Kabla ya yote, labda niseme kwamba kwa kuwa tumo katika mwezi wa pili tokea kuanza kwa mwaka mpya, nami sijapata nafasi ya kukutana nanyi wazee, na vyema nitumie nafasi hii kwanza kukutakieni heri ya mwaka mpya, na baraka zote za mwaka 1991. (Makofi). Ninakuombeeni uzima, nguvu, baraka na mafanikio.

  Pili, tuna kawaida katika nchi yetu, kwamba kila linapotokea jambo muhimu katika Taifa, tunatafuta nafasi ya kukutana nanyi na kukuelezeni. Hivyo, leo napenda kuzungumza nanyi wazee wa dar es Salaam na, kupitia kwenu, iwe ninazungumza na Wazee wenzenu wa tanzania nzima. Kwa hiyo, hayo nitakayokuambieni nyinyi, ninawaambia pia Wazee wa Taifa letu wote kwa jumla.

  Hivi karibuni Halmashauri Kuu ya Taifa ilifanya kikao chake cha kawaida Zanzibar, ambacho kilijadili mambo mbalimbali. Kikao hicho kilimalizika kwa kutoa maamuzi maalum. Maamuzi hayo yana uzito mkubwa. Inaelekea baadhi yetu, pamoja na vyombo vyetu vya Habari, hatukuyaelewa vizuri maamuzi hayo. Kwanza, nataka nivivue na lawama Vyombo vyetu vya Habari. Maana hatukuwa nao huko. Kwa hivyo walitangaza vile walivyoelewa. Kwa sababu hiyo nimeona ni vyema kuzungumza nanyi ili kusahihisha matangazo ya vyombo vyetu. Nimeona ni vyema kutumia nafasi hii kutoa ufafanuzi.

  LAZIMA TWENDE NA WAKATI

  Inaelekea kuna hofu kwamba Azimio la Arusha linageuzwa. Kwa hiyo, tokea mwanzao, kabla ya kusema lolote, nataka tuelewane kwamba siasa yetu bado ni ile ile ya Ujamaa na Kujitegemea. (Makofi). Haikugeuka wala hatutazamii kuigeuza. Kwa hali yoyote sisi Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi hatutaigeuza Siasa hii. (Makofi) . Kule Zanzibar tulizungumza mambo mengi, miongoni mwao, ni kutoa tafsiri ya baadhi ya vipengele vya Azimio ili vifanane na wakati tulionao.

  Azimio la Arusha, kama tunavyojua, limetangazwa mwaka 1967. Hii leo tuko katika mwaka 1991. Imepita miaka mingi, zaidi ya 20 tokea kutangazwa kwa Azimio la Arusha. Na katika kipindi cha miaka 20 yametokea mabadiliko mengi duniani na pia katika hali ya maisha yetu. Hali yetu ya sasa, hasa ya kiuchumi, siyo ile ile ya mwaka 1967. Ndio maana mishahara ya wafanyakazi ingawa imeongezeka sana lakini bado haikidhi mahitaji yao - haiwatoshi hata wale wanaopokea mishahara mikubwa miongoni mwetu. Isitoshe, wakati wa Azimio idadi ya Watanzania ilikuwa ndogo. Sasa hivi idadi yetu imeongezeka zaidi ya mara mbili. Kwa sababu ya wingi wetu mahitaji yetu nayo yemeongezeka sana, wakati mapato yetu yamekuwa yakipungua wakati wote.

  Kwa hivyo ni dhahiri kwamba jamii ya Tanzania lazima itie maanani mabadiliko haya na ijiandae kwenda na wakati. Kama hatukwenda na wakati, kazi yetu itakuwa ni kufukuzia wakati - jambo ambalo hatulimudu.

  Tabia ya wakati ni kama ile ya bahari. Bahari inakupwa na kujaa mapaka ukiongoni mwa maji. Baadaye maji hukupwa polepole, mpaka kufika wakati ikawa maji yote yamekwishaondoka ufukoni. Samaki werevu huondoka nayo hayo maji, yaani yakijaa huja nayo, yakitoka kutoka nayo, vinginevyo hupwelewa. Samaki watakaozembea kufuta maji watajikuta wamechelewa wanatapatapa juu ya mchango wakati maji hayo hayapo. Hiyo ndiyo maana ya kupwelewa (Makofi).

  Hapa Afrika, kwa mfano, imeanzishwa mipango mbalimbali ya ushirikiano wa uchumi. Mipango hiyo ni pamoja na Ushirikiano wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADCC) na Eneo la Soko Nafuu (PTA). Afrika pia imeazimia kuunda Jumuiya ya Uchumi. Nchi zinazoendelea nazo zimedhamiria kuzidisha ushirikiano miongoni mwao. Nchi yetu lazima ifanye mabadiliko ili iweze kushiriki kwa ukamilifu katika shughuli zote hizo zinazosaidia maendeleo yetu.

  KILA ZAMA NA MWONGOZO WAKE

  Ndugu Wazee, Msahafu wa Waislam unasema ‘LIKULLI AJALIN KITABU" Mwingereza mmoja kaitafsiri aya hiyo hivi: ' TO EVERY AGE ITS BOOK" yaani "Kila zama ina Kitabu (Mwongo) chake". Na sisi Wana-CCM tunakubali kuwa "kila Zama zinahitaji kuwa na Mwongozo wake". Azimio la Arusha ni Mwongozo wetu wa msingi. Ni dira inayoongoza mwelekeo wa jamii yetu. Lakini tafsiri zake zinabidi zirekebishwe kila inapohitajika ili zisipitwe na wakati. Miongozo ina tabia moja: inakuja ili kufafanua, kuelekeza au kukemea hali mbaya inayojitokeza.

  Mojawapo ya malengo ya maamuzi ya Zanzibar ni kutoa tafsiri sahihi ili kupunguza kebehi inayofanywa dhini ya siasa yetu ya Ujamaa na Kujitegemea na pia kwenda na wakati.

  Mwaka 1967 lilitangazwa Azimio la Arusha. Mwaka 1971 ulifuatiwa na tamko la Iringa la "Siasa ni Kilimo". Tamko hili lilikuwa ni mbinu na msisitizo wa Siasa yetu ya Kujitegemea. Zlilipanua tafsiri ya Azimio la Arusha. Katika mwaka 1981 ilionekana kuna haja ya kutolewa mwongozo mwingine kulingana na wakati ule ambao nao ni upanuzi wa tafsiri ya Azimio. Ulitangazwa ili kukidhi haja ya wakati ule.

  Aidha, kabla ya hapo, katika mwaka 1974, Chama kilipitisha Agizo la Musoma kuhusu Elimu ya Kujitegemea ambalo madhumuni yake yalikuwa kutazama upya suala la uingizaji wanafunzi Chuo Kikuu na kupanua Elimu ya Msingi ili kutoa fursa kwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule kufanya hivyo.

  Maandiko yote hayo hayakupingana na Azimio la Arusha ila yakiongeza mwangaza kwa mambo ambayo yalihitaji yafanane na wakati wake. Na lazima iwe hivyo, kwani bila ya kwenda na wakati tungechekesha.

  Kwa mfano wakati wa Azimio la Arusha, mtakumbuka kuwa tafsiri ya neno Kiongozi ni pamoja na yule mwenye mshahra uliofikia shilingi 1,066/= kwa mwezi. Tungeng'ang'ania tafsiri hii tu, basi leo pasingekuwapo wafuasi. Wafanyakazi wote wangetafsirika kuwa ni viongozi wa CCM. Kwani ukiacha wakulima wafanyakazi wote sasa kwa tafasiri ya 1987 ni viongozi tena maradufu. Maana kima cha chini sasa ni Sh.2,500/=, ambazo ni zaidi ya mara mbili ya Sh.1,066/=. Ndiyo maana tukasema jamii yetu italazika Kufanya marekebisho kila inapokuwa lazima kufuatana na wakati. Tutafanya hivyo bila ya kuachana na misingi ya siasa yetu.

  Kwa hivyo, tulichokifanya kule Zanzibar ni kupanua tafsiri za Azimio ili ilingane na wakati tulionao. Kufanya hivyo si kuua Azimio bali ni kuliimarisha.

  CHIMBUKO LA AZIMIO LA ARUSHA

  Historia ya Azimio la Arusha tunaijua sote. TANU ilipigania kwa maneno mpaka nchi ikapata UHURU wake. Tanganyika ilipopata Uhuru na tukaanza kujitawala ishara potofu zilianza kuchomoza. Baadhi ya Viongozi walianza kuutumia uongozi wao kama mradi wa kujineemesha. Kwa kutumia nyadhifa zao, wakikopa fedha benki na kuanza kujijengea mashamba - si ya miti - bali ya majumba; si nyumba za kuishi tu bali majumba mengi ya kupangisha.

  Tabia hiyo ilizusha manung'uniko ya watu. Jamii ilianza kugawanyika makundi mawili; manaizi na makabwela. Kitendo hicho ndio chimbuko la kutangazwa kwa Azimio la Arusha. Azimio lilikuja kutoa mwongozo wa maadili ya wanachama na viongozi wa TANU. Kwa hivyo nia ya Azimio la Arusha, miongoni mwa mambo mengine, ilikuwa ni kuwazuia viongozi kutumia uongozi wao kujitajirisha. Hilo ndilo lililokuwa tatizo la hatari miongoni mwa matatizo wakati ule. Azimio lilikuja kuokoa jahazi - kukemea tabia potofu.

  MATATIZO LA SASA NI UCHUMI TEGEMEZI

  Mtu anaweza kuuliza je sasa kuna tatizo gani? Tatizo letu katika miaka ya tisini na kuendelea ni lile la uchumi tegemezi. Tatizo letu sasa ni kwamba uchumi wetu ni duni mno. Wakati idadi yetu inaongezeka, mapato ya Taifa, hasa ya fedha za kigeni, hayaongezeki. Wakati wa Uhuru idadi yetu ilikuwa ni watu milioni tisa. Lakini leo, tuko milioni tisa na tisa tena na nusu ya tisa. Lakini mapato yetu ya pesa za kigeni yapo pale pale, $ milioni 400. Wakati Azimio la Arusha lilitutaka tujitegemee, hali halisi ni kuwa tumekuwa wategemezi wakubwa. Maana Taifa letu hizi sasa, kwa pato lake lenyewe la fedha za ndani, linaweza kujitegemea kwa kipindi cha miezi saba tu katika mwaka. Tunategemea watu wengine, kwa njia ya ruzuku na mikopo, kumalizia miezi mitano inayosalia katika mwaka. Hii ni hatari. Lazima tunendelee kubuni mbinu za kuondokana na hali hiyo.

  MBINU ZA KUJITEGEMEA

  Ilani ya Uchaguzi inasema hivi:

  "Makusudi ya Chama katika kipindi cha miaka mitano ijayo ni kwa Taifa kukusanya nguvu zote za wananchi kwa kusaidiana na Serikali zao (Mbili), na kuzitumia katika kila eneo la maendeleo ili kutoa msukumo mpya wa utekelezaji wa siasa ya Ujamaa na Kujitegmea".

  Hivyo, Chama na Serikali zake zinawajibika kuwarahisishia wananchi wao kujitegemea kwa chakula, kujitegemea kwa mavazi na kujitegemea kwa malazi. Ili kutimiza lengo hilo Taifa lazima liwawezeshe wananchi wake kuzalisha mazao ya biashara na chakula kwa wingi. Pia ni wajibu wa Chama na Serikali kuandaa mbinu za kuwasaidia wananchi kujijengea nyumba zao za kuishi ili ziwasitiri wanapostaafu au kuwa wazee.

  Je wananchi wakituuliza: hivi ni mbinu gani mlizofanya kumshirikisha kila mmoja wetu kutumia nguvu zake zote katika kuzalisha kama Ilani inavyosema? Tungejibu nini? Lakini sasa kila mwananchi, pamoja na mwana CCM, hataweza kutoa kisingizio kwa kusema:-

  "Mimi sikuweza kutumia nguvu zangu zote katika kufanya kazi ya kuzalisha kwa sababu nimezuiwa na Azimio la Arusha."

  MWANACHAMA KUCHANGIA UCHUMI KIKAMILIFU

  Azimio la Arusha lipo. Narudia tena kusema kuwa wanaohusika na tafsiri hii ni wanachama. Sisemi Viongozi, bali wanachama wa CCM. Tunataka kumpa Mwanchama wa CCM, kama mwanachama mwingine yeyote, uhuru zaidi wa kuzalisha ili kuchangia kadiri ya uwezo wake katika pato lake yeye mwenyewe na pato la Taifa Kwa jumla.

  Ili tujitoe, kitaifa, kwenye shimo la utegemezi tulimo hivi sasa, mbinu bora ni kutoa uhuru kwa kila mwananchi wa kila Kaya, wa kila Kata, wa kila Tarafa, wa kila Wilaya na wa kila Mkoa kutumia nguvu zake zote katika kuzalisha. Matokeo ya hatua hii ni kumwezesha kila mtu katika Kaya, Kata, Tarafa, Wilaya na Mkoa kujigemea. Tukifika hapo ndipo Taifa litapokuwa limeondokana na hali ya sasa ya uchumi tegemezi.

  KUPANGISHA NYUMBA

  Jambo la kupangisha nyumba nalitaja tu, kwani si lazima kwa sababu si jipya; hata hivyo ni vyema nalo litajwe. Mwenyekiti Mstaafu alilisemea jambo hili mahali pengi sana, tena alianza zamani kulisemea, sijui. Kwa mfano, hivi karibuni alilitaja tena katika hotuba yake ya kuadhimisha miaka ishirini ya Azimio aliposema hivi:

  "Nasharti hayo yanamkataza kiongozi wetu kuishi kikabaila kwa mbinu za kupangisha majumba.

  Lakini sharti hili halimkatazi mtu mwenye vyumba vya ziada katika nyumba yake anamoishi kuvipangisha kwa watu wengine kwa kodi nafuu, Hili ni jambo la kawaida kabisa katika nyumba zetu za "Waswahili"' na upangishaji huu mimi nimekuwa nikiutetea tangu zamani. Utaratibu huu unawasaidia sana watu wenye mapato madogo, wanafunzi, au wafanyakazi ambao bado hawajaoa au kuolewa kupata vyumba vya kupanga kwa kodi nafuu.

  Ni kweli kwamba huko nyuma tumekuwa wakali mno
  katika kutafsiri msharti haya.

  Azimio la Arusha linachokataa ni unyonyaji. Hivyo maskini ya Mungu mwenye kijumba chake cha mbavu za mbwa akimwona maskini mwenziwe anapata taabu, hana pakukaa, asimpangishe? Je akimpangisha atakuwa anamnyonya? Au anamstiri? Kwa hiyo tangu zamani kustiriana ni ruhusa (Makofi).

  Hatukuishia hapo kule Zanzibar, tulikwenda zaidi, tulisema pia kwamba wapo viongozi miongoni mwetu ambao baadhi yao wamefanya kazi za Chama au za Serikali kwa miaka 30 au zaidi. Lakini hawana nyumba; ukifika wakati wao wa kustaafu viongozi hao huwa wanababaika kwa kutojua wataishi wapi. Ndipo wanapoanza kutafuta mbinu - ndiyo maana siku hizi utakuta misururu mirefu katika Ofisi ya Vyeti vya kuzaliwa. Watu wanakwenda kubadilisha tarehe zao za kuzaliwa, kujifanya bado wangali vijana ili wachelewe kustaafu. (Makofi).

  Sisi tunaamini kwamba baada ya kipindi kirefu cha utumishi, mtu aweze kuwa na nyumba ili, hata akiwa kipofu angalau aweze kupapasa kuta zake na kusema: Hii ni nyumba yangu niliyoipata kwa jasho langu la kazi ya miaka 30. Tunataka awe na kitu. Lakini, Ndugu Wazee, bahati nzuri wanachama wa CCM, kama wananchi wengine, wanaruhusiwa kukopa. Wanaweza kukopa kwenye benki zetu wakajenga nyumba za kukaa. Sasa jamani tukisema kwamba hata mtu aliyekopa asiipangishe nyumba hiyo atalipia nini huo mkopo?

  Vinginevyo tutakuwa tunamfanyia mzaha mtu huyo. Maana atachukua mkopo, ajenge nyumba, kisha ashindwe kulipa huo mkopo. Waliomkopesha wataikama hiyo nyumba na kuiuza ili kurudisha fedha yao. Katika hali hiyo mwana-CCM gani atakayekuwa na nyumba iwapo mwisho wake ni kuchukuliwa na kile chombo kilichomkopesha? Kwa hivyo nasema mtu kama huyu ana dharura; ana dharura ya deni. Amejenga nyumba kwa nia ya kukaa mwenyewe lakini ana deni la mkopo. Kama anaweza kukaa nyumbani mwake, akae. Lakini pia awe na ruhusa ya kupangisha nyumba yake, akitaka, ili imsaidie kulipa mkopo. Anapostaafu awe anayo nyumba ya kumstiri uzeeni. Kitendo hicho kisimpotezee uanachama wake wa CCM.

  Kwa hivyo Ndugu Wanachama, huko ndiko kwenda na wakati, vinginevyo tutapwelewa. Mtu kama huyu aruhusiwe kupangisha nyumba yake, iwe nusu ya nyumba, ama robo ya nyumba au yote: (makofi).

  BIASHARA YA KUPANGISHA MAJUMBA BADO NI MWIKO

  Lakini kikao cha Zanzibar hakikutengua miiko ya kiongozi wala ya mwanachama wa CCM. Bado ni mwiko kwao kuwa na biashara ya kupangisha majumba.
  Kwa mfano, kama kuna mwanachama anayeomba mkopo, akipata anajenga nyumba, halafu anaikodisha, akipata fedha za kodi anajenga nyingine mpya, ambayo nayo anaikodisha na kuendelea kujenga nyingine. Huyo ni mfanyabiashara. Kazi yake ni kujenga na kupangisha majumba. Kikao cha Zanzibar hakikusudii mwanachama wa aina hii. Huyu siye (Makofi).

  Vile vile, Mwanachama wa CCM, hata akiwa kiongozi katika mazingira maalum, aruhusiwe kukodisha nyumba yake, ikiwa haihitaji kuikaa wakati ule. Inawezekana haihitaji kuishi katika nyumba yake kwa kuwa kapata uhamisho. Mfano, mtu kahamishiwa Iringa kwa kazi wakati nyumba yake iko Dar es Salaam. Je ikae bure watu waitumie bure tu kweli? (Makofi).

  Ni mwanachama wa aina hii ndiyo tulisema huko Zanzibar kuwa aruhusiwe kupangisha nusu ya nyumba ama robo ya nyumba au yote, maadam mtu huyo anapo pengine pa kukaa. Lakini tunasisitiza kuwa bado si ruhusa kwa mwana CCM wala kiongozi wa CCM kuendesha biashara ya kupangisha majumba.

  HISA KATIKA MAKAMPUNI YA UMMA, KUPUNGUZA UKWASI!

  La pili lililoamuliwa huko Zanzibar ni kuwaruhusu wanachama wa CCM, kwa kufuatana na hali ya wakati ulivyo, sasa aruhusiwe kuwa na hisa katika kampuni ya Umma. Hii leo tunayo Mashirika ya Umma zaidi ya 400, lakini mengine yao hayana fedha za kuendeshea kazi zao.

  Mfano kuna mwananchi mmoja alikwenda kwenye kiwanda cha Umma kutaka huduma ya kusafishiwa ngozi zake. Alipofika hapo alikuta "pamelala paka" Yaani palikuwa kimya, hapakuwa na kazi yoyote inayofanyika. Kumbe kile kiwanda kilikuwa kimefungwa kwa kukosekana fedha za kukiendeshea ........... umeme ulikatwa na wafanyakazi walipewa likizo.

  Meneja alimfahamisha huyo mteja kuwa kiwanda kimefungwa kwa sababu ya deni la maji na umeme pamoja na pesa za mishahara ya wafanyakazi. Huyo mteja alikubali kulipa arubuni (advance ) ya milioni saba ili kukikwamua kiwanda. Wiki ya pili yake kiwanda kilianza kufanya kazi zake za kuzalisha kama kawaida.

  Kisa cha kiwanda hicho kusimama kazi ni kukosa fedha za kuendeshea. Kiswahili cha siku hizi huitwa ukwasi. Kwa hiyo kazi ilisimama.

  Katika hali kama hii, tumeona ni vyema kuwaruhusu wananchi wote pamoja na wakulima, na wafanyakazi wa shirika lenyewe wakiwemo wanachama wa CCM kununua hisa chache kwa kila atakaetaka

  UBIA WA UMMA NA DOLA KATIKA SHIRIKA

  Narudia, watakaoruhusiwa kununua hisa ni wananchi wowote watakaopenda pamoja na wakulima wa pamba, korosho, kahawa, tumbaku na wafanyakazi wa hilo shirika lenyewe. Kwa njia hiyo, Shirika hilo sasa litapata sura mpya, litakuwa ni la ubia kati ya Serikali, wafanyakazi na wananchi. Fedha tunazozizungumzia hivi sasa, za kulipia taa na mahitaji mengine zingetokana na ununuzi wa hisa ili uzalishaji uendelee. Katika hali kama hiyo kiwanda kitakuwa ni mali ya umma kweli. Maana kuna tofauti ya Shirika la Dola na Shirika la Umma kwa maana ya wananchi wenyewe.

  Endapo shirika la umma litataka kuwashirikisha wananchi na wafanyakazi wake kwa kulichangia ili kuondoa tatizo la Ukwasi, jambo hilo liwe ni halali, na Mwana CCM naye aruhusiwe kuwa miongoni mwao. (Makofi)..Kilichofanywa na maamuzi ya Zanzibar ni kumruhusu mwanachama wa CCM naye kushiriki kikamilifu katika sera ya Taifa ya uwekezaji wa rasilimali nchini.

  Katika sera ya uwekezaji rasilimali tunaruhusu ubia katika uchumi wetu. Ubia huo unaweza kuwa baina ya watu wa ndani ya nchi peke yao, au kati ya wawekezaji wa nje na wa ndani. Baada ya kuikubali misingi hiyo hatuoni kwa nini tusianzie kwa kuwaruhusu wananchi, wakulima na wafanyakazi kuwa na hisa katika Mashirika wanayofanyia kazi (Makofi).

  WAFANYAKAZI KUSIMAIA UWAJIBIKAJI

  Nia nyingine ya kufanya hivyo inatokana na kutambua kuwa wafanyakazi wenye hisa katika kiwanda watakuwa wasimamizi wakereketwa wa uwajibikaji katika viwanda hivyo. Watakereketwa zaidi pakiwa na ubadhirifu au kutowajibika.

  Hivi leo baadhi ya mashirika ya Umma ni mashirika ya umma kwa jina tu. Watu wanayaibia wakidai wanachukua chao. Pengine wanashindana kufanya hivyo ili wasipunjwe. Baadhi ya mashirika ya Umma yanahujumiwa kana kwamba hayana wenyewe. Baada ya maamuzi ya Zanzibar kuanza kutekelezwa, Mashirika hayo yatakuwa na wenyewe.

  MWONGOZO WA 1981 KUHUSU UWAJIBIKAJI

  Maamuzi ya Zanzibar si mapya. Mwongozo wa chama wa 1981 umetoa ilani juu ya kupungua kwa uwajibikaji katika Mashirika ya Umma, jambo ambalo hivi sasa tunalitafutia ufumbuzi. Mwongozo wa 1981 unasema hivi:

  "Imezuka tabia ya aibu nchini ambayo imekuwa ikiongezeka ya vitendo vya kuharibu na kuvitumia vibaya vyombo muhimu vya kazi na mali ya umma kwa jumla. Magari, matrekta, zana nyingine muhimu z chama, serikali, mashirika ya umma mara nyingi hayadumu muda mrefu kama ambavyo ingetazamiwa kutokana na matumzi mabaya."

  Lakini ikiwa watu pale pale wenyewe wana hisa katika kampuni au shirika - mfano - TANESCO kuwa Mkurugenzi katika kampuni ya Kibepari. Napenda suala hili lieleweke vizuri ili kujibu fikra zilizojengeka kuwa uamuzi huo umevunja Azimio la Arusha.

  Kwanza inafaa tufafanue maana ya Mkurugenzi. Tafsiri ya Mkurugenzi inayojulikana sana ni ile ya mjumbe wa bodi ya wenye hisa katika Kampuni fulan. Kwa hiyo wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi katika Kampuni ya Kibepari huwa ni miongoni mwa wale wenye hisa zao katika kampuni inayohusika Watu hao huchanguliwa na wenzao wenye hisa kama wa kuongoza shughuli za Kampuni yao kwa faida ya pamoja. Mkurugenzi wa aina hii hawezi kuwa mwanachama wa CCM.

  Lakini kuna Mkurugenzi wa aina nyingine ambaye ni tofauti kabisa na Mkurugenzi mwenye mali. Mkurugenzi huyu ni yule ambaye ameajiriwa tu na wenye mali yao, kutokana na sifa zake za utaalam, kuendesha kampeni. Mtu huyu huwa ni mwajiri tu, anayefanya kazi. Huyu ni mtumishi tu kama watumishi wengine, hana chake katika kampuni inayohusika. Anachotegemea ni mshahara wake na marupurupu mengine kama yapo. Huyu ndiye Mkurugenzi anayeruhusiwa kuwa mwanachama wa CCM.

  Azimio la Arusha bado lilo pale pale kwa wale wakurugenzi wa aina ya kwanza. Wao Azimio linawabana, hawawezi kuwa wanachama wa CCM. Lakini huyu wa aina ya pili aliyeajiriwa tu, akija kuomba uwanachama tunamkubali. Azimio la Arusha kamwe halijamkataa mfanyakazi mwenziwao kwa "koa" la kutumikia Kampuni ya Kibepari, hivyo ndivyo tulivyoamua Zanzibar


  MWANA - CCM KUWA NA HISA KATIKA KAMPUNI YA KIBEPARI

  Jambo jingine ambalo halikueleweka vizuri na linahitaji ufafanuzi ni lile la kumruhusu mwanachama wa CCM kuwa na hisa katika kampuni ya Kibepari. Hili nalo tumeliruhusu huko Zanzibar, lakini sharti iwe katika mazingira maalum.

  Ni vyema kukumbushana kuwa yapo makampuni ya kibepari ambayo tumekuwa nayo hata kabla ya Azimio la Arusha. Kampuni hizo zimekuwa zikidhi kiasi fulani cha ajira ya Watanzania, pamoja na Wanachama wa CCM.

  Ni jambo hili lieleweke vizuri, nitatoa mfano tu wa Kampuni ya mtu binafsi. Mwenye Kampuni ya binafsi anaweza kabisa akaamua kwa hiari yake kuuza baadhi ya hisa kwa wafanyakazi wake ili kuwapa motisha ya kazi Tajiri yeyote akiamua kufanya hivyo, Chama na Serikali vitamwona kuwa amechukua hatua ya kimaendeleo. Kitendo chake hicho ni halali. Kwa sababu itakuwa ameuzimua ubepari kwa kuifanya kampuni yake ni ya ubia kati yake na wananchi aliowaajiri. Kwa kweli kampuni hiyo itakuwa kama chama cha ushirika.

  Katika hali hiyo, hata Mwanachama wa CCM anaruhusiwa kupokea/kununua hisa alingane na wafanyakazi wenzie.

  Ni mazingira maalum ya namna hii tu ndiyo yanayoruhusu Mwanachama wa CCM, kama mfanyakazi mwingine, kuchukua hisa katika Kampuni anayofanyia kazi. Atakapostaafu ataweza kuendelea kupokea faida ya hisa yake au kuiuza.

  MISHAHARA MIWILI KWA MWANA-CCM

  Kuhusu mishahara miwili, Azimio la Arusha linasema hivi:

  "Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata malipo ya haki kutokana na kazi yake".

  Kufuatana na ukweli huo, anayefanya kazi mbili za halali anastahiki kupata malipo ya kazi ya pili. Tuchukue mfano wa Profesa ambaye mchana kutwa anasomesha Chuo Kikuu. Baada ya saa za kazi anaweza kuamua kufanya azi ya akili, kwa mfano kutoa ushauri au kuandika mradi kwa aliyemwomba huduma hiyo.

  Mwanachama huyo atastahiki kupata malipo ya kazi hiyo. Hili si geni, katika sherehe za kuadhimisha miaka 20 ya Azimio la Arusha, baba wa taifa alisema hivi:

  "Lile sharti la kutopokea mishahara miwili kwa kweli ni sharti la tahadhari tu. Ni vigumu sana kufanya kazi mbili za kuajiriwa na zote mbili ukazifanya vizuri. Huwezi kuwatumikia mabwana wawili! Lakini sharti hili halimkatazi kiongozi wetu kujiongezea pato kwa kutumia muda wake wa kupumzika kwa kufanya shughuli nyingine: kama kulima au kufuga, ikiwa yeye si mkulima au mfugaji, kuandika, kufanya kazi ya useremala, au kufanya shughuli nyingine yoyote kwa mikono yake au kwa ajili zake".

  Jambo la msingi ni kwamba lazima twende na wakati. Mwaka 1987 lilipotungwa Azimio la Arusha ilikuwa hakuna haja ya kuwa na mishahra au malipo ya kazi zaidi ya moja kwa sababu wakati ule mshahara mmoja ulikuwa unatosha kukidhi mahitaji yote muhimu. Kwa mfano, mimi, mwenyewe, mshahara wangu wakati ule ulikuwa shilingi 2,200/= kwa mwezi. Mshahara huo, hasa kwa Zanzibar, ulikuwa ukinitosha kukidhi mahitaji yangu yote ya lazima.

  Wazee wangu watakumbuka kwamba wakai ule kule kitunguu, pilipili na bizari -yote hivyo kwa senti tano tu. Ilikuwa inawezekana pia kununua samaki mkubwa kiasi kwa senti ishirini mpaka 50 tu; au kununua kuni za kuweza kupikia mlo mzima kwa senti kumi tu.

  Siku hizo iliwezekana mnunuzi kujaziwa mafuta ya kupikia au samli kikombe kizima kwa senti ishirini hasitini tu. Halikadhalika kwa senti ishirini tu mtu aliweza kununua matunda, kama vile fungu la ndizi mbivu au machungwa au papai. Kwa ufupi, kwa mahitaji ya siku nzima, tangu asubuhi hadi jioni, iliwezekana mtu kutumia pesa kidogo sana.

  Katika hali hiyo, kulikuwa hakuna ulazima wa kufanya kazi ya pili. Afanyae kazi zaidi ya moja huonekana ni mlafi au ana tamaa. Kwa mshahara huo huo niliweza kudunduliza pesa na mwishowe kununua gari mpya kabisa. Gari hilo lilinigharimu pesa nyingi kwa wakati huo - shilingi 13,000/=!! Wakati huo bei ya mafuta nayo ilikuwa shilingi tatu tu kwa galoni zima. Katika mazingira ya aina hii mshahara mmoja ulimudu kukidhi mahitaji ya wafanyakazi wengi ukiacha walevi.

  HALI IMEBADILIKA

  Lakini leo mambo yamebadilika. Gharama ya maisha imepanda san. Serikali yenyewe imeungama waziwazi kuwa haina uwezo wa kumlipa mfanyakazi wake mshahara unaomwezesha kumudu gharama za maisha. Kutokana na hali hiyo, wafanyakazi wengi, wanashindwa kukidhai mahitaji yao muhimu. Ndio maana Chama na Serikali yake vimekuwa vikiwahimiza wafanyakazi kufanya shughuli nyingine za halali, baada ya saa za kazi, ili kujiongezea mapato. Mfano wa kazi hizo ni kama vile: kutibu, kuandika vitabu, kuandikamradi, kutoa ushauri wa kitaalamu, kufundisha, overtime, useremala, ufundi bomba, ufundi umeme, ufundi cherahani, kilimo, ufugaji, kuziba mipira ya magari, kuteka maji ya kuuza, kupiga matofali, kutengeneza baiskeli na kadhalika.

  KOFIA MBILI MSHAHARA MMOJA

  Lakini lazima tuelewane kuwa hii mishahara miwili tunayozungumzia haimhusu kiongozi mwenye kofia mbili. Kwa mfano, Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya, ambao vile vile ni Katibu wa Chama wa Mkoa au Wilaya, hawaruhusiwi kupokea mishahara miwili. Hawa watalipwa mshahara mmoja tu, maana hii kazi ya pili ni sehemu tu ya ile ya kwanza. Lakini wanaruhudiwa kufanya kazi za ziada kama vile kilimo, ufugaji na kadhalika, baada ya saa za kazi, kama walivyoruhusiwa wafanyakazi wengine. Hapa nitapenda kusisitiza kuwa wale watu wanaoeneza maneno ya kejeli kuwa ati Maamuzi ya Zanzibar ni mbinu tu za "wakubwa" kujifufanisha wenyewe, ijulikane kuwa si kweli. Kazi zilizoorodheshwa hapa si za wakubwa bali ni kazi zinazoweza kufanywa na kila mtu kufuatana na ujuzi alionao na mazingira ya mahali anapofanyika kazi.

  MWANA-CCM MKULIMA NA MFUGAJI

  Watanzania wengi ni wakulima, wakulima ndio wengi zaidi. Mkulima kwa maana pana ni pamoja na mfugaji. Katika siku za nyuma, baadhi ya wanachama waliwahi kutiwa msukosuko kwa kuwa na mashamba makubwa au kufuga kuku 500. Lakini baadaye Chama kilijisahihisha kama inavyosema Programu ya Chama:

  "Chama Cha Mapinduzi ni Chama kinachokua (haikudumaa). Kinakaa katika nadharia na falsafa yake, (ili kwenda na wakati)".

  Hii ndio ilivyokifanya Chama kijisahihishe kila kinapokosea.

  Kwa hiyo kama siku moja tulimtia mwenzetu msukosuko kwa kuwa na shamba kubwa, mbuzi 18 au kuku 500, sasa Chama kimekua katika falsafa yake. Falsafa ya sasa inatia maanani hali halisi ya wakati wa sasa. Ndio maana kule Zanzibar tukaruhusu kiongozi awe na shamba lisilozidi hekta 20, hasa kama shamba hilo limo katika eneo la kijiji.

  Kuhusu ufugaji, kuna baadhi ya wenzetu katika makabila ya Tanzania ambao kwao ni utamaduni wao kuwa na ng'ombe wengi. Mfano mzuri ni wenzetu wa makabila ya wamasai, Wasukuma na Wagogo. Je, mwenye utamaduni wa kumiliki ng'ombe wengi akataliwe katika Chama kwa sababu ya kumiliki ng'ombe wengi? Tunasema hapana. Akiomba uanachama wa CCM akubaliwe. Chama Cha Mapinduzi hakimkatai tajiri aliyepata utajiri wake kwa njia ya halali na kulipa kodi ya Serikali analipa. Anayekataliwa na CCM ni yule aliyepata utajiri kwa wizi, kwa rushwa, dhuluma na kwa kwa njia nyingine za haramu.

  Huko Zanzibar tulifikria labda tuweke kiwango maalum cha mifugo, kama vile iwe mwisho ng'ombe 200 peke yake. Lakini tulijiuliza kama ng'ombe mmoja akizaa na jumla kufikai 201, je huyo ndama amnyonge shingo?

  Hiyo ndio hali halisi iliyotufanya tukubaliane kuwa mfugaji yeyote anaetaka kuwa mwanachama bila ya kujali idadi ya mifugo yake. Mwenye mshahara mkubwa, vile cvile hata wa malaki, maadam ni mshahara wa kazi halali, naye pia aruhusiwe kuwa mwanachama wa CCM.

  MAFUNZO YA MIEZI MITATU

  Ili kukiimarisha zaidi Chama, tumewaruhusu wananchi kuwa wanachama wa CCM bila ya kuhdhuria yale mafunzo ya miezi mitatu.

  BIASHARA NDOGO NDOGO

  Huko Unguja hatukuishia hapo. Tuliamua kuwa Mwanachama wa CCM wa kawaida naye pia aruhusiwe kuwa na biashara ndogo ndogo ili kumwongezea kipato. Biashara hizo, ambazo sharti zifanywe baada ya saa za kazi, ni pamoja na uvuvi, kuwa na gari ndogo au pick-up ya kukodisha kwa kuchukulia abiria au mizigo, kushona, kusindika matunda, mafuta na mashine ya kukoboa au kusaga unga.

  Mwanachama mwenye mashine ya kusaga unga hanyonyi bali anatoa huduma kwa jirani zake kijijini. Chama na Serikali vimo mbioni kuhimiza na kutafuta teknolojia ya kumrahisishia kazi Mtanzania, hasa wanawake. Ni vyema kukaribisha teknolojia ya kuwasaidia wanawake waondokane na kufanya kazi ngumu ngumu zinazoweza kuwapotezea wakati na kuathiri afya zao, kama vile kutwanga au kusaga nafaka, kubeba mizigo ya kuni, maji na mtoto mgongoni. Si vyema kwa jamii yetu kuingia katika karne ya ishirini na moja katika hali hiyo. Ndio maana kule Zanzibar tulamua kuruhusu biashara ndogo ndogo kuendeshwa na mwanachama wa CCM kwa manufaa yao na ya jamii.

  Ndugu Wazee, haya kwa muhtasari ndio yaliyoamuliwa Zanzibar. Haya kamwe hayabomoi Azimio la Arusha, badala yake yanaliimarisha. Azimio la Arusha ni msingi wa siasa yatu ya ujamaa na Kujitegemea. Ili tuweze kujitegemea lazima tuandae mbinu na mikakati ya kuzalisha maji, huduma na chakula. Hili ndio lengo la maamuzi ya Zanzibar.

  Mshairi mmoja amesema:-

  "Kutaraji uongofu bila kupitia njia zake ni kama kulitaka
  jahazi kutembea nchi kavu"

  Ndugu Wazee Ahsanteni sana. (Makofi).
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Wanasiasa hawawezekani kabisa! Ni magwiji wa kukwepa lawama, tena kimachomacho.
   
 3. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2010
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hebu tupatieni taarifa kamili ni nini alichokisema Mzee Ruksa kwanza.Mmetpa in short tunataka context.
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Magazeti bana:

  Habari Leo-Mwinyi:wasiomcha mungu walizima Azimio la Arusha
  Mwananchi-Mwinyi akumbuka Azimio la Arusha
  Nipashe-Sikulifuta Azimio la Arusha
  Guardian-Mwinyi:Arusha Declaration alive
  Daily News-Coherent mechanism failed Arusha accord,says Mwinyi
   
 5. Madabwada

  Madabwada JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2010
  Joined: May 8, 2009
  Messages: 537
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mzee Kifimbo alishaliweka wazi hilo ... nahisi alijua watakuja kuruka tu baadae ..... nahisi kama yanatimia vile ... ??

  Mzee ruksa anasepa kivuli chake mwenyewe??
   
 6. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Ukweli huna mwenyewe, na hakuna awezaye kuuhodhi na kuupindisha kwa faida yake.
  JK amefanya vema kumpa zigo la kutatua misuguano ndani ya chama tawala Mzee Ruksa.
  Walipoketi na kuua misingi ya ukweli ,haki na utu wa kila Mtanzania nafikiri hawakutegemea haya yanayoonekana leo.
  Wenye kitu ndo wana haki zaidi ndani ya chama tawala na inakuwa vigumu hata viongozi waadilifu kusema hilo kwa kuhofia usalama wao kisiasa.
  Leo tunaanza kulikumbuka Azimio la Arusha kwa misingi yake ya kuleta usawa na haki.
  Mimi nafikiri "we ain't seen nothing yet"
   
 7. C

  Chongowela Member

  #7
  Mar 19, 2010
  Joined: Sep 5, 2008
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijaipata sawasawa.Tupeni hotuba yake tusim"quote" out of context. Vinginevyo hatujamwelewa anataka kusema nini....
  Au kulikuwa mvinyo pale???

  Ni sawa na mwizi anayasema yake kamba tu, mbuzi aliye mwisho wa kamba kanasa mwenyewe!!!!
   
 8. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kwanini hakusema/kujibu hizi tuhuma wakati Kambarage yuko hai, kwa nini anaanza kuongea hivi baada ya Kambarage kuaga dunia?.

  "Walivyorudi kutoka Znz walirudi vichwa chini, wenye akili tukagundua kuwa azimio la Arusha halipo tena, limefutwa" - Kambarage
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  ...........wangeacha hata ile miiko ya uongozi....duh hivi ile tume ya maadili ya viongozi pale Ohio netx to Holland house inafanya kazi bado?....
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  ...........wangeacha hata ile miiko ya uongozi....duh hivi ile tume ya maadili ya viongozi pale Ohio next to Holland house inafanya kazi bado?....
   
 11. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Chongowela, labda kwa ufipi, extracts kutoka Nipashe;

  Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, amesema Azimio la Arusha halijafutwa kama watu wengi wanavyodhani.

  Alisema hivi karibuni kupitia kwenye vyombo vya habari, alisikia aliwasikia baadhi ya watu wakililia Azimio la Arusha kwa madai kuwa limefutwa na kueleza kwamba kimsingi, azimio hilo halija wahi kufutwa.

  Alisema hata azimio la Zanzibar ambalo lilidaiwa kuwa ndilo lililofuta azimio la Arusha halikufutwa bali lilizimwa na baadhi ya mambo yaliyotokea kipindi hicho."Hakuna siasa nzuri na bora kwa Watanzania kama ujamaa ulioletwa na Mwalimu Julius Nyerere, lakini nia ile ilitanguliwa na uwezo wa Watanzania kwa sababu kulikuwa na sera nzuri lakini matokeo yake sera hiyo ilihitaji makanisa na misikiti iwafinyange watu ili itekelezwe,” alisema na kuongeza:

  “Awali kulikuwa na mashirika ya umma 400 lakini yalikuwa ganda tu, yamegunguliwa kama mchwa anavyogungua msonobari, nje unaona kitu ni kizuri lakini ndani hamna kitu.”

  Alieleza kuwa changamoto hiyo ndio iliyozaa azimio la Zanzibar ambalo alisisitiza kuwa halikufuta na azimio la Arusha.

  Alisema mashirika yaliuzwa kwa sababu yalionekana mzigo kwa taifa. Alisema wengi walioyaendesha mashirika hayo hawakumuogopa Mungu ndio maana yalifikia hapo.

  Nadhani Mwinyi anazeeka vibaya, maana ukiangalia hiyo habari anajaribu kuwaeleza Watanzania kwamba walichofanya Zanzibar ni kuweka mkakati wa kuokoa mashirika ya umma, basi.

  Ndio maana binafsi nasikia kichefuchefu. Hakuna kitu nachukia kama kiongozi yeyote kutufanya Watanzania wengine wote ni mbumbumbu wazungu wa reli na tuko "gullible"! I say hii kitu naichukia SANA, iwe ni raisi anaongea au balozi wa nyumba kumi.
   
 12. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Sasa yeye anamuogopa Mungu?
  1.Si ndiye aliyetuletea shida ya umeme na IPTL yake?
  2.Tunaambiwa humu JF mwanawe Hussein anajenga apartment blocks hapo Seaview..kapatawapi hiyo plot na hizo pesa?
  3.Alimtoaje Capt.Aziz jela na kuwaacha watoto wa walala hoi jela eti kwa kuwa mama yake alienda kumlilia...mama wangapi wana watoto jela wengine bila hatia?
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hapa utaona kwamba kusema kweli viongozi wengine akili zao ni kama mchwa...Yaani ni ajabu sana kwa Mwinyi ambaye ni mchwa kuweza kuzungumzia ubovu ama uimara wa msonobari alokula ukaisha na kubakia ganda tupu.
  .
  Ni hawa hawa akina Mwinyi na viongozi wengine walioua mashirika ya Umma.. wao kama mchwa waliyafilisi mashirika kisha wakaamua kuyauza kama vile mapungufu yapo ktk mashirika..tatizo ni mchwa kwa nini wakayauza mashirika na sio kuthibiti hao mchwa? sii ndio yale yale ya kugawa vyandarua kuzuia malaria hali wakiacha mbu wakizaana!.

  kwa akili zake za ajabu, Mwinyi anakiri kwamba kwamba haya mashirika yaligunguliwa na mchwa, ambao ndio wao...cha ajabu wameuza mashirika ambayo tayari yamekwisha liwa na mchwa, kisha Hilo Azimio la Zanzibar likawapa RUKSA hao mchwa walio yaharibu mashirka ya Umma wahamie miti mingine..

  Mimi nadhani huyu Mwinyi anazeeka vibaya, anakosa hekima na busara zake za awali kwani hakuwa na sifa yoyote ya Uongozi zaidi ya hekima zake!
   
 14. Companero

  Companero Platinum Member

  #14
  Mar 19, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Jamani rejeeni hotuba ya Mwinyi ya kuleta Azimio la Zanzibar - ipo humu humu JF kwenye mjadala wa Azimio la Zanzibar, kwa kiasi fulani yuko sahihi hawakulifuta kabisa Azimio!
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Companero,
  Mkuu wangu ktk hotuba ile alisema hawakulifuta Azimio la Arusha ila wameliboresha kwa kufuta baadhi ya sheria ili kutuwezesha kitaifa kwenda na wakati! akilenga soko huria na Utandawazi.

  Lakini kama kweli walitaka kulenga Soko Huria na Utandawazi, hapakuwepo na sababu ya kuuza mashirika ya Umma ikiwa makosa ni WATU walioharibu mashirika hayo. kifupi hawkuuza nyumba ama gofu ila waliuza viwanja..Sisi wananchi tunatazama thamani ya viwanja vile, wakati wao wanatupa hadithi za magofu...Ni hadithi hii hii wnaitumia kuuza pia nyumba za National housingi na Msajili.
  Pili, hapakuwepo na sababu ya kuondoa miiko na maadili ya Uongozi ikiwa soko huria halihusianai na viongozi kufanya Biashara...kuepuka conflict of interest ni moja ya Maazimio makubwa ya Arusha.

  Ndani ya roho zetu sisi sote tunajua fika kwamba - Siasa ya Ujama na Kujitegemea ilikufa na hakuna kitu wala mfano hata mmoja kiutawala unaolenga siasa ya Ujamaa na Kujitegemea hii leo, sasa nambie wewe mkuu wangu, ikiwa Ujamaa na Kujitegemea umekufa hilo Azimio la Arusha ni lipi analozingimzia Mwinyi?....
   
 16. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  NINAMUHESHIMU MZEE MWINYI ZAIDI YA MAELEZO ! UJAMAA(azimio la arusha) LINABAKI KUWA PEKEE MPAKA SASA LENYE NIA YA KWELI NA YA DHATI KUMSAIDIA MTANZANIA....! HUENDA BABA YETU MWINYI AMEGUNDUA HILO NDO HATA SASA AMEKUJA NA HOJA HII....MZEE HAJAKOSEA INABIDI TUMPONGEZE KWA KUNG'AMUA HILO.......AMELETA UBEPARI LAKINI AMEONA YOTE SI MAJIBU KWA MTANZANIA BALI UJAMAA....(azimio la arusha)HONGERA NA PONGEZI MZEE WETU KWA KUJIREKEBISHA....WENGINE NAO WAUNGE MSTARIIIIII....!
   
 17. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Hapo sasa.....mimi naona ni namna yalivouzwa mashirika haya...ilitakiwa kufanyika IPO na zaidi walitakiwa ku fast track stock markets lakini kwa ujanja wao wakauza mashirika kwa wanaowataka kupitia PSRC matokeo yake mtanzania wa kwaida anawekeza viakiba vyake kWenye HIACE...lankini angepewa nafasi angenunua sehemu ya hayo mashirika 400
   
 18. K

  Keil JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mahesabu,

  Kama amegundua hivyo, hakutakiwa kusema kwamba waliboresha, bali alitakiwa asikitike kwamba alishiriki kuliua Azimio la Arusha jambo ambalo limepelekea kuongeza matabaka (classes) na mbaya zaidi most of the politicians ndio wamekuwa matajiri wakubwa kuliko hata wafanyabiashara. Sasa hivi wafanya biashara wengi wanakimbilia kwenye siasa kwa kuwa wanajua wakiingia huko ndo wanaongeza utajiri wao na kuulinda ule walio nao.
   
 19. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #19
  Mar 19, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Na kibaya kuliko vyote ni kuwa hawa jamaa walikaa zanzibar na kuamua kuua azimio la arusha bila kutoa vision ya Tanzania mpya waliotaka kuunda. hatima yake kila mjanja akajiundia yale anayoyaona yanamfaa kwa wakati wake. Sasa hivi sisi sio wajamaa wala mabepari. Tumekuwa watu wa deal deal tu
   
 20. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wanajuta kwani walikuwa wanalipinga wamo bado kwa uongozi uliopo sasa yaaani nawasikitikia sana,

  " .....Basi tulipofika pele nkaona watu wanapinga tu wanalikataa azimio la arusha nikashangaa kweli ila mie sijaona tatizo kabisa, basi na ikawa ivyo, by Mwl JKN"

  ndivyo mambo sasa yana warudi, haya mambo ya hawa viongozi kupinga vitu na mwataka mfumo fulani huku na mwashindwa kuutetea na kuujengea hoja ndio matunda yake haya sasa, nchi yajiendea tuuu

  Sasa kumbe Azimio la Arusha hamkufuta mlitaka nini?

  hao wawekezaji wakigundu kuwa sie bado tuna siasa ya ujamaaa wata sepa any time na tulivyo mazoba bado hatuja jiwekea mikakati endapo hawa wawekezaji wakisepa je sisi tutaweza songa mbelee??
   
Loading...