Ngekewa tuko pamoja
Licha ya mashirika kuwa mengi na karibuni yote kundeshwa kwa kodi za wananchi na uchapishwaji wa noti mpya kila kukicha (refer Nyirabu-Nyerere relationship), serikali ilikuwa inafanya kazi ambayo haiihusu kabisa. Hebu angalia utitiri wa kazi au biashara ambazo serikali ilikuwa inahodhi:
Kampuni ya Kuku
Kampuni ya Maziwa
Kampuni ya Ng'ombe
Kampuni ya Usagishaji
Kampuni ya Usafirishaji ( UDA, KAMATA, KAU...RU, MA, etc.)
Kampuni ya Uvuvi
Kampumi ya Kilimo na Chakula
Kampuni ya Viatu
Kampuni ya Chai
Kampuni ya Chumvi
Kampuni ya Sukari (SUDECO)
Kampuni ya Magari
Na mengine mengi (orodha ni ndefu) ambayo serikali haikuwa na ulazima wa kuyaanzisha kuyahodhi huku yote yakiendeshwa kwa urasimu wa serikali. Watendaji wake wakuu wakilipwa mishahara na marupurupu yasiyolingana kamwe na uzalishaji wake. Namba ya ajira katika makampuni yote hayo haikujali uwezo halisi wa mahitaji ya biashara.
Tungeendelea kuchekesha na tusingekuwepo hapa tulipo kamamaamuzi sahihi ya kurekebisha uchumi yasingechukuliwa.
Azimio la Arusha halikuwa ni msahafu au biblia kana kwamba haliwezi kurekebishwa.
Azimio la Arusha msingi wake pia uliegemea katika mawazo ya mtu mmoja au kikundi kidogo cha watu.
Azimio la Arusha ndiyo lililoweka misingi mibovu ya uchumi wa nchi yetu kwa kuwanyang'anya uwezo wa kufikiri watanzania wazawa katika kuchemsha bongo zao na kuibuka kuwa wafanyibiashara wakubwa, badala yake walitakiwa wafanye kazi zaidi kwenye serikali au mashirika yake kwa ajili ya kujenga uchumi wa nchi yetu changa na huku ikwaachia uwanja mpana usiokuwa na upinzani watanzania wenye asili ya kiasia wakitawala fursa ya kufanya biashara kwani wao Azimio la Ausha halikuwagusa kabisa. Walipewa haki zote za kufanya biashara bila ya kuulizwa kama wana maduka mawili au zaidi, biashara zaidi ya moja, nk.
Turudi nyuma katika ukweli, kipndi ambacho Mwiny yuko madarakani ilikuwa ni kipindi ambacho mabadiliko mengi na makubwa ya kiuchumi na kisiasa yalikuwa yana fanyika duniani. Kwa mfano, mabadiliko ya mfumo wa siasa ya vyama vingi, kuanguka kwa Soviet, urekebishaji wa uchumi kwa nchi masikini nk. Wote tunakumbuka jinsi IMF na WB walivyokuwa wanatuasa tubadilishe sera zetu ili kuvutia mabadiliko ya kiuchumi. Ili kuyakubali yote hayo kama kiongozi wa nchi kunahitaji ujasiri na busara tele la sivyo ukigoopa kugeuka jiwe basi itabidi ung'atuke tu.
Hata hivyo ni lazima tuangalie ni kwani nini tunakuwa na Kiongozi wa nchi anayechaguliwa na wananchi kila baada ya muda fulani na kumwekea ukomo?
Hii ni wazi kuwa tunahitaji mawazo mbadala ndiyo maana kwa kila nchi yenye busara imeweza kuona mbali na kuhakikisha kuwa kuna kuwa na uongozi mpya kabisa kila baada ya miaka fulani. Kwa mantiki hiyo basi ni vema kila kiongozi aingiaye madarakani afanye jambo ambalo litaweza kusahihisha ukomo wa kufikiri wa kiongozi aliyepita. Kwa mfano kabla ya uongozi wa Mwinyi, kiongozi aliyekuwepo
aliamini kuwa wananchi kupiga mswaki wa mti na mkaa ilikuwa ni 'sawa tu', kuogea sabuni ya kufulia iliyo katika kiwango cha chini kabisa ni 'sawa tu',
kupangia wananchi kiwango cha manunuzi ya bidhaa muhimu kwa wiki au mwezi kama vile sukari nusu kilo kwa mwezi mzima kwa familia ni 'sawa tu'
kuogea sabuni ya Lux na kutumia Colgate ni kuhujumu uchumi.
kutopatia nafasi watoto wanaomaliza darasa la saba nafasi ya kuendelea na elimu ni 'sawa tu'
Sasa unapofikia mahali unapewa nchi ipo katika hali kama hiyo wewe kama kiongozi mpya wa nchi utaendelea kutumikia mawazo ya kiongozi aliyepita? ni wazi kuna limitations, ni vema kiongozi akaja na mikakati ya kubadilisha hali hiyo na hasa anapoona kuwa 'si sawa'.
Pamoja na mambo mengi, siasa zote za nchi yeyote zisifike mahali masuala muhimu ya ustawi wa wananchi yakataifishwa kwa kisingizio cha kulinda madili ya viongozi, ni vema wakati hao viongozi walipoweka namna ya kudhibitiana basi hayakupaswa kutuathiri sisi wananchi wa kawaida ambao si sehemu yao.
Ninadiriki kusema kuwa Azimio la Arusha ndiyo chanzo cha kuona wanazuoni wetu wazuri tu wanaacha kazi zao nzuri na kukimbilia siasa kwani tayari walishajengwa mawazoni mwao kuwa kwenye siasa ndiyo kila kitu. Kila mtu anafikiria ubunge na si kufanya biashara kwani kila mtendaji mkuu katika mashirika ya serikali alipewa nyumba bure, usafiri wa kumwaga yeye na mkewe na watoto na mjomba na shangazi. Hakukuwa na ufuatiliji wa mtendaji huyo, sana sana akiharibu basi atahamishwa kwenda kuharibu pengine
Ngekewa, Pundamilia, Makoko, August n.k
Nadhani tatizo linalotokea hapa na ambalo inabidi tulikwepe au tusema wazi ni kuwa;
1. Nyerere anayo aliyofanikiwa na anayo aliyofeli
2. Mwinyi anayo aliyofanikiwa na anayo aliyofeli
Never mention Mkapa na Kikwete.
Kosa ni pale kumlaumu mwinyi pasi kusema ukweli na aliyofanikisha, na kosa pia kumlaumu Nyerere pasi kusema uzuri wake.
Sehemu walizofeli hawa wakuu hatusemi wao , tunasema tulishindwa hapa, hiyo inakuwa lugha ya kifamilia zaidi kama taifa ni moja.
Tumethibitishiwa na kuhakikishiwa mara nyingi kuwa AD lilikuwa ni wazo, wazo lile lilikuwa zuri, ulikuwa mwongozo, chombo cha kuleta ari, umoja na hamasa!
Tamko lile au wazo lile hata kama lilishindwa halimfanyi ,mtoa wazo kuwa mshindwa, wala halimlazimishi mpokea wazo kulazimishwa kulikubali wazo.
Ila wazo hili kama tunaona linapositive ideas why bother? kwa nini tusiseme Ok, it was good Idea let amend and move on with it!
Tukiendela na mchezo wa kumsema Mwinyi vibaya na Nyerere vibaya hatutakaa tujue , tuna matatizo gani, tulianguka wapi, na tuamke vipi!
Ukikosea ukasema mazuri ya Mwinyi basi unaweza ukashangaa watanzania asilimia 90 wanasema afadhali mwinyi kuliko Nyerere aliyefanya tusugue meno kwa mkaa! But even Nyerere that was a process, tena naweza kusema tungekaa zaidi pale tujifunze zaidi shida zilivyo, pengine viongozi leo wangekuwa na utu! we can never by any means kumlaumu mto wazo na mwenye nia nzuri na taifa! kushindwa ni alama tosha ya kutokuwa na watu wa kusaidia,
Mbio za kijiti hizi ,ni teamwork, kulaumiwa Mwinyi wakati JKN alikuwa yupo pembeni ni sawa na kusema JKN alitusaliti baadae! mbaya zaidi watu walilipiga chini waliokuwa wanafunzi wa JKN, Mkapa leo hatuwezi tukampachika jina ulikuwa mbaya kwa kukataa Azimio wakati kafundishwa kabisa na JKN! what went wrong? tukasema pia tusikosee na kufana azimio kama dini!
AD ni wazo, haukuwa mfumo, tatizo ni kuwa ngau JKN tulijua anaamini nini, akina marais wengine wote hawana wanachoamini, kama ni dini basi siasa ya nchi ytu ni ya kipagani.
However, still we can move on, kama Sheria na Katiba zitafuatwa vyema, still tumeona Katiba na sheria vinahitaji mabadiliko mengi tu.
AD kama anatokea leo mtu analifufua basi lipate nguvu ya kisheria, bila hivyo tutakuwa tunacheza
Enyi wana wa nchi hii, stop pointing fingers to JKN and Mwinyi, simameni kwa miguu yenu na kuamka leo!